Tuesday 31 January 2017

Tathmini ya Matokeo ya Kidato cha nne 2016 -Tazama matokeo Hapa


  
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.

Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

Share:

Wanafunzi 10 Waliofanya Vizuri Zaidi Kitaifa Katika Matokeo Ya Kidato cha Nne 2016

Share:

Shule 10 Bora na 10 za Mwisho katika Matokeo Kidato cha Nne 2016


Leo January 31 2017 Baraza la mitihani Tanzania NECTA limetangaza matokeo ya kidato cha nne ‘CSEE 2016’.
Hapo chini kuna orodha ya shule 10  bora kitaifa na shule 10 zilizoshika mkia
Share:

Monday 30 January 2017

TANGAZO JIPYA LA KAZI MASWAYETU BLOG

Habari zenu,

Maswayetu blog inatafuta vijana 10 ambao watafanya kazi na blog hii kwa kupost habari mbalimbali kila zinapotokea na kushare sehemu mbalimbali.
Share:

MAALIM SEIF:NITAKUWA RAIS WA ZANZBAR

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema mgogoro wa Zanzibarna anaamkni atakuwa Rais Zanzibar.

Amesema, mgogoro visiwani humo utamalizika endapo viongozi wa vyama vyote va siasa watakaa chini kufanya mazungumzo.

Akizungumza katika mahojiano katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Azam, Maalim Seif alisema jambo la muhimu ni viongozi kukubali Zanzibar kuna tatizo.

Alisema anaamini kama kuna nia njema, maridhiano yanaweza kupatikana Zanzibar na migogoro yote ya kisiasa kumalizika.

“Hii naamini kabisa, kama kuna nia njema, kila upande ukubali Zanzibar kuna tatizo, ukubali kuna haja ya viongozi kupata ufumbuzi wa tatizo na watapata vipi, ni kwa kushirikiana pamoja,” alisema Maalim Seif aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Alisema Serikali iliyopita ya Umoja wa Kitaifa, ilikuwa na mafanikio makubwa na kwamba anavyoona hakuna kitakachorudisha hali ile, kama si kwa vyama kushirikiana.

“Kila upande ukiona unawakilishwa itasaidia kuleta Wazanzibari pamoja,” aliongeza Maalim Seif.
Aidha, Maalim Seif alisema anajua kuna majaribio makubwa yanafanywa kutafuta ufumbuzi, hivyo ufumbuzi ni vema upatikane ili kuridhisha pande zote, na kwamba kuna njia nyingi ya kupata muafaka na hiyo ni pamoja na kufanyika mazungumzo, lakini ni baada ya kila upande kukubali kuwa Zanzibar kuna tatizo.

Akizungumzia kugombea tena nafasi ya urais mwaka 2020, Maalim Seif alisema ni vema kusubiri ili kuona hali ya kisiasa itakapofika wakati huo.

“Tusubiri kwanza wakati wake tuone kama tunafanikiwa au hatufanikiwi kwenye hili, halafu tutafanya maamuzi,” alisema Maalim Seif ingawa baadaye alisema kuwa karibuni anatarajia atakuwa Rais wa Zanzibar.

“Natarajia muda mfupi ujao, Inshaallah nitakuwa Rais wa Zanzibar,” alisema bila kufafanua anawezaje kuwa rais wakati hakushiriki uchaguzi mkuu wa Machi, 2016.

Akizungumzia mgogoro ndani ya CUF, Hamad alisema Msajili wa Vyama vya Siasa aliruhusu upande wa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuchukua Sh milioni 369 ambazo ni fedha za ruzuku na kwamba baadaye chama kitashindwa kuzijibia matumizi yake.

Kuhusu hilo, alisema wamemwandikia Msajili, Gavana wa Benki Kuu (BoT) na pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), waangalie hatua ya kuchukua.

Akizungumzia afya yake, alisema anamshukuru Mungu kwamba afya yake ni njema. Hata hivyo alisema tangu aondoke madarakani, amekuwa akijihudumia mwenyewe katika matibabu na si fedha za serikali ikiwa ni pamoja na matibabu nchini India.
Share:

MTUMISHI ASIEWASILISHA CHETI CHAKE IFIKAPO MACHI MOSI MWAKA HUU KAJIFUKUZISHA KAZI

MTUMISHI wa umma atakayeshindwa kuwasilisha cheti cha elimu na taaluma au “Index number” ya mtihani ili zihakikiwe na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), itakapofika Machi mosi mwaka huu, atakuwa kajiondoa kazini mwenyewe, imeelezwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Angellah Kairuki alibainisha hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua Mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
“Watendaji wakuu ninawaomba msimamie uhakiki wa vyeti ili watumishi wenu wafanye kazi kwa sifa stahiki,” alisisitiza Kairuki, katika taarifa iliyotolewa na wizara yake.
Aliongeza kwamba serikali ilisitisha ajira mpya ili kupisha kazi ya kuondoa watumishi hewa, ambayo imefika ukingoni na siku za karibuni, ajira zitarudishwa.
Akiwa mjini Dodoma, Septemba mwaka jana, wakati wa kuapishwa kwa wakurugenzi watendaji wapya 13 walioteuliwa Septemba 10, mwaka huu, Kairuki alisema kuanzia serikali imewaondoa watumishi hewa 17,201 kwenye utumishi wa umma na kazi hiyo inaendelea.
Kairuki aliwataka watendaji wakuu kuweka mikakati ya kuepuka watumishi hewa na kusimamia kwa dhati kwa sababu jambo hilo, limeumiza na kupoteza rasilimalifedha nyingi za serikali.
Alisema anatambua kuna wakala zenye upungufu wa watumishi, hivyo zinaingia gharama kubwa za kuajiri wafanyakazi wa mikataba, hata hivyo alielekeza kila Mtendaji Mkuu ajiridhishe kwa kuandaa taarifa ya mahitaji halisi ya watumishi.
Pamoja na hilo, Kairuki alielekeza wakala zenye watumishi wa mikataba zifanye tathmini na kuhakiki kama kweli watumishi hao wanahitajika kwa kuwa eneo hilo ni moja ya maeneo yenye ajira za mashaka kwa baadhi ya taasisi.
Aliongeza kuwa yapo malalamiko kuhusu suala la maadili na uwajibikaji yanayozigusa Wakala za Serikali.
Aliainisha masuala hayo ni pamoja na watumishi hewa, taarifa chafu za watumishi, matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za umma, kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa mifumo ya utendaji kazi na wakati mwingine kutotekeleza majukumu ya msingi ya wakala.
Alifafanua kuwa amegundua kupitia taarifa mbalimbali kuwepo kwa changamoto ya mawasiliano hafifu kati ya wizara mama na wakala zilizo chini yao ambapo taarifa kutoka katika wakala hazichambuliwi inavyostahili na hata zinapochambuliwa na wizara mama, hazitoa mrejesho kwenda katika wakala.
Awali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Utumishi), Dk Laurean Ndumbaro alizitaka wakala za serikali kuimarisha eneo la ufuatiliaji na tathmini ili kuimarisha utendaji kazi na kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na Watanzania
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARY TAREHE 30.1.2017

Share:

Mahakama Yapiga marufuku amri ya Rais Trump kuzuia Watu Kuingia Marekani

Mahakama moja ya New York Marekani imeridhia ombi la wanaharakati waliokwenda Mahakamani kupinga amri ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo, kupiga marufuku Wakimbizi wa Syria na raia wengine wa nchi sita za kiislamu kama Iran, Iraq, Somalia, Sudan, Libya na Yemen wasiingie Marekani.

Mahakama hiyo imeamuru wote waliozuiliwa kupitia amri hizo waachiwe ikiwa ni agizo la lililotolewa saa kadhaa baada ya kuwepo Ripoti kutoka uwanja wa ndege wa John F Kennedy New York kwamba watu kadhaa wamezuiwa kuingia Marekani wakiwemo wale ambao walikuwa wamepewa ruhusa kwenda kuishi Marekani kupitia mpango maarufu wa Green Card.

Tayari pia Raia wawili wa Iraq wameishitaki Mahakamani serikali ya Marekani baada ya kushikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa John F. Kennedy New York na kuzuiwa kuingia Marekani ambapo inaripotiwa wakati huo kuna raia wengine 10 walikua wamezuiwa kuingia Marekani muda mfupi tu baada ya ndege kutua.
Share:

Picha: Treni ya abiria yapata ajali ikitokea Kigoma kwenda Dar

Treni ya abiria ya EXPRESS ikitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam leo January 29 2017 imepata ajali maeneo ya Ruvu ndani ya mkoa wa Pwani ikiwa ni kilometa kadhaa kabla ya kufika kwenye jiji la Dar es salaam.
Shuhuda ambaye alikua ndani ya Treni hiyo amesema Behewa zaidi ya 10 zimepinduka na watu wanaendelea kuokolewa kwa kupitia Madirishani.

Share:

Friday 27 January 2017

Wazee 2 mbaroni kwa ubakaji, ulawiti watoto 11


WAKAZI wawili akiwemo Mustafa Kassimu (75) ambaye ni mganga wa tiba za asili katika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga na fundi wa kushona nguo, Rashidi Singano (70) wa wilayani Lushoto, wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kubaka na kulawiti wanafunzi 11 wa shule za msingi.
Katika tukio la kwanza la Januari 24, mwaka huu, Polisi inamshikilia fundi cherehani huyo ambaye anaishi Kijiji cha Mshwamba Kata ya Lunguza wilayani Lushoto kwa tuhuma za kubaka na kulawiti kwa nyakati tofauti watoto 10 (majina yamehifadhiwa).
Mtuhumiwa huyo inadaiwa alitumia ushawishi wa kuwapa fedha kati ya Sh 300, Sh 600 hadi Sh 1,000 na kuwavizia njiani, kama mbinu ya kuwanasa watoto hao, ambao wote ni wanafunzi katika moja ya shule ya msingi iliyopo Kata ya Lunguza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alithibitisha tukio hilo kwa kuwaeleza waandishi wa habari kwamba walipata taarifa za ukatili dhidi ya watoto hao kutoka kwa mwalimu wa watoto hao, ambaye jina lake limehifadhiwa.
“Tulipokea taarifa kuhusu tukio hilo kutoka kwa mwalimu wa shule wanayosoma watoto hao, akidai kwamba siku hiyo akiwa shuleni, aligundua kuwa wanafunzi kumi wa kike kati yao sita wote wakiwa wamebakwa, huku wengine wanne wakiwa wamelawitiwa kwa nyakati tofauti na fundi cherehani huyo,” alieleza.
Aliongeza, “Mwalimu huyo alitaja wanafunzi wengine watano na kudai kwamba hao wamenusurika kunaswa kwenye mtego wa kutendewa ukatili huo na Mzee Singano ambaye anaishi maeneo ya jirani na shule hiyo,” alieleza Kamanda Wakulyamba.
Alisema katika uchunguzi, imebainika kwamba mtuhumiwa alikuwa akifanya vitendo hivyo vya kubaka na kulawiti watoto hao ndani ya nyumba anayoishi pamoja na kufanyia shughuli hizo za ushonaji, na aliwapata wakati walipokuwa wakienda kupeleka nguo na wakati wa mchana wanapotoka shuleni kurejea nyumbani.
“Chanzo cha tukio hili kwa kweli ni tamaa mbaya za kimwili alizokuwa nazo mtuhumiwa ambapo alikuwa akiwalaghai wanafunzi hao kwa kuwapa fedha kati ya shilingi mia tatu hadi mia sita wakati wanapopeleka nguo zao kushonwa,” alifafanua.
Tukio la pili linamhusisha mtoto mwingine mwenye umri wa miaka 12, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu (jina limehifadhiwa) wa Kijiji cha Fune wilayani Korogwe aliyelawitiwa na Kassimu (75) wakati alipokuwa akimpatia matibabu ya asili, yaliyolenga kumwongezea nguvu za kiume.
Share:

MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE JAN 27.


Share:

Watu 14 akiwamo Mchina wafukiwa mgodini Geita

Watu 14 akiwemo Mchina, wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa katika mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga jana alisema watu hao wamefukiwa chini ya mgodi baada ya mlango wa kuingilia kwenye shimo la mgodi kumeguka udongo na kujiziba.

“Usiku wa kuamkia leo (jana) saa tisa kwenye mgodi huo unaoendeshwa na Wachina, mlango wa kuingilia mgodini mmoja ulimeguka na kujifunga watu 14 wakiwa ndani,” alisema Kyunga.

Kyunga alisema kwa mujibu wa kitabu cha orodha ya watu wanaojiandikisha kuingia mgodini, kuna majina ya Watanzania 12 na Mchina.

Aidha, alisema mbali na watu hao 13, pia kuna Mtanzania mmoja ambaye aliingia bila kujiandikisha na hiyo ni kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo hivyo kufanya idadi ya watu waliofukiwa kuwa 14. 
Kyunga alisema tangu jana asubuhi jitihada mbalimbali za kuondoa udongo kuwaokoa watu hao zinaendelea wakitumia mitambo na wataalamu.

“Kwa kusaidiana na Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) na wataalamu wengine, jitihada zinaendelea ili kuhakikisha tunawaokoa watu hao,” alisema Kyunga. 
Alisema wakati huo huo wamefanikiwa kutoboa eneo jingine na kupitisha mabomba ya hewa ya oksijeni ili kuwafanya watu hao wasikose hewa.
Share:

Tanzania na Malawi Kukutana Kujadili Sakata la Watanzania 8 Waliokamatwa

Tume  ya Ushirikiano wa Pamoja ya Kudumu (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi, inatarajia kukutana nchini humo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali, ikiwemo la Watanzania nane kukamatwa nchini humo kwa tuhuma za kuingia eneo la migodini bila kuwa na kibali.

Mbali na kujadili suala la Watanzania hao, lakini pia tume hiyo itajidili mgogoro wa mpaka uliopo baina ya nchi hizo mbili katika Ziwa Nyasa.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza Februari 3 hadi 5 mwaka huu nchini Malawi.

Akizungumza Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga alisema tume hiyo ilikuwa haijakutana kwa muda mrefu, jambo ambalo limesababisha watu kuwa na sintofahamu kati ya ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Kasiga alisema mkutano wa tume hiyo, mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2003 jijini Dar es Salaam, hivyo kuwa kimya kwa muda mrefu kuna baadhi ya watu walidhani kuwa ushirikiano wa nchi hizo mbili si mzuri.

“Kikao kama hiki kilikaa miaka mingi kidogo… kuna masuala yaliyochelewa kutekelezwa kutokana na kukaa kwa kikao hiki, lakini kwa sasa yatatekelezwa kupitia vikao hivyo,” alisema Kasiga.

Aliongeza kuwa kwa mara ya kwanza, vikao hivyo vitashirikisha wafanyabiashara kutoka mikoa ya Njombe na Ruvuma, pia wavuvi kutoka katika mikoa hiyo ambao wataeleza namna wanavyofanya shughuli zao kwa kushirikiana na wenzao wa Malawi bila kuingilia.

Mindi alisema katika kikao hicho, ujumbe wa Tanzania utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga; na mbali na kujadili mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na Watanzania waliokamatwa, pia utajadili masuala mbalimbali katika sekta za biashara, elimu, kilimo pamoja na sekta zingine.

Kasiga pia alikabidhi tuzo za Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walizoshinda kutoka Umoja wa Afrika (AU). SSRA ambayo imekuwa wa kwanza katika Tuzo za Ubunifu Katika Sekta za Umma Afrika (AAPSIA), ilikabidhiwa kikombe pamoja na cheti cha ushindi.

Ushindi huo wameupata kupitia mradi wao wa Mradi wa Kanzidata ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Bi Mindi akimkabidhi Bi. Sarah kombe la ushindi kwa niaba ya Wizara. Bi. Kibonde aliipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Meneja wa Mradi wa Mfumo wa Forodha wa TANCIS kutoka TRA akipokea zawadi ya cheti cha ushindi kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga.
Share:

Mkuu wa Wilaya ajiuzulu, amwandikia barua Rais Dkt Magufuli

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Uyui Bw.Gabriel Mnyele akizungumza na Mwandishi wa habari wa Azam tv Juma Kapipi wakati akiwa ofisi za CCM Wilaya ya Uyui ikielezwa kuwa alikuwa ameitwa na Uongozi wa chama hicho kufuatia kuwepo kwa taarifa kwamba ameamua kuachia ngazi nafasi ya Ukuu wa wilaya hiyo ya Uyui jambo ambalo alilithibitisha kwa Katibu wa CCM wilaya ya Uyui kwamba ni kweli amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli. 

 *****
Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gabriel Simon Mnyele amejiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi Januari 26, 2017 na kuwaaga madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano alioufanya wilayani humo.

Akieleza sababu ya kufanya uamuzi huo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa alimwandikia Rais Dkt Magufuli barua ya kujiuzulu nafasi hiyo akielezea kusongwa na majukumu binafsi.

Mkuu wa Wilaya, Gabriel Simon Mnyele alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 26 Juni, 2016.
Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka Waandishi waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu."Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe,kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?Aliwahoji waandishi.
Share:

Thursday 26 January 2017

AUDIO | Linex Sunday Mjeda - Kiherehere | Download

Share:

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARY 26 2017


Share:

Wednesday 25 January 2017

Magazeti ya Leo Jumatano ya January 25 2017

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger