Wednesday 25 January 2017

NACTE:ORODHA YA VYUO VILIVYO RUHUSIWA KUDAHIRI WANAFUNZI KWA KIPINDI CHA MARCH / APRIL, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016 / 2017


 
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)


ORODHA YA VYUO VILIVYO RUHUSIWA KUDAHILI WANAFUNZI KWA
KIPINDI CHA MARCH/APRIL, 2017 KWA MWAKA WA
MASOMO 2016/2017




Share:

NACTE YAANZA KUPOKEA MAOMBI YA WANAFUNZI WANAOTAKA KUJIUNGA NA VYUO VYA AFYA,UALIMU,MIFUGO,KILIMO ETC NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 -MARCH /APRIL INTAKE

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)

TAARIFA KWA UMMA

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yaani “Online Central Admission System (CAS)”, umefunguliwa rasmi tarehe 23 Januari, 2017, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada na Stashahada kwa Kipindi cha Machi/April, 2017 kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Namna ya Kufanya Maombi
Maombi yote yafanyike kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) au kupitia chuoni ambapo mwombaji anapendelea kwenda kusoma, ambapo chuo kitamdahili mwanafunzi husika kwenye mfumo wa udahili kupitia “Institutional Panel”.

Tanbihi: Waombaji wa kozi za Afya waliohitimu Astashahada (NTA Level 5), pia wataomba kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.
Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo:
  1. Biashara, Utalii na Mipango, mfano; Uhasibu, Meneja Rasilimali Watu, Wanyama Pori, Mipango.
  2. Sayansi na Teknolojia Shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya Mawasiliano, Usanifu Majengo, Mifugo.
  3. Afya na Sayansi Shirikishi, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi.
Sifa za muombaji
  1. Awe amehitimu kidato cha nne mwaka 2015 au kabla ya hapo.
  2. Awe na Astashahada ya mwaka 2016 au kabla ya hapo kwa wanaojiendeleza.
  3. Sifa kwa kozi mahsusi ziko kwenye mwongozo wa kozi (Guidebook) ulioko kwenye mfumo (CAS).
Ada ya maombi ni kama ifuatavyo:
  1. Kwa eneo la Afya na Sayansi Shirikishi ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
  2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=.
  3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Biashara, ada ni Tshs 30,000/=, ambapo muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 06/03/2017.

Muhimu: Hakutakuwa na muda wa nyongeza wa kufanya maombi. Hivyo waombaji wanashauriwa kuwa makini wakati wa kufanya maombi yao.

Angalizo: Kwa eneo la Mafunzo ya Ualimu na kozi ya Muhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (Community Health Workers) hayatakuwepo kwenye udahili wa awamu hii.







Imetolewa na: 
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
23 Januari, 2017
Share:

Tuesday 24 January 2017

MSHINDI WA UBUNGE DIMANI AHAIDI KUWA DARAJA

Share:

TCRA YATAHADHARISHA MATAPELI WA NJIA YA SIMU

Share:

WANASIASA WANAOENEZA TAARIFA ZA UONGO KUHUSU NJAA KUKAMATWA

Naibu  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ameonya kuwa watu wakiwemo wanasiasa wanaoeneza taarifa za uongo za kuwepo kwa baa la njaa, ni kosa na wachukuliwe hatua ikiwemo kukamatwa.

Masauni amesema bado kuna watu wanajichukulia mamlaka ambayo sio yao na kueneza uongo kuwa kuna njaa nchini, hilo ni kosa kwa kuwa kwa kueneza propaganda hiyo kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

“Hizo ni propaganda za watu wasioitakia mema nchi hii ….. mtu anapofanya kosa lazima achukuliwe hatua …… Jeshi la Polisi liangalieni hili,” alisisitiza.

Masauni alitoa onyo hilo wakati wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya jana mkoani Rukwa ambako Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven alimhakikishia kuwa mkoa huo hauna njaa, bali una ziada ya kutosha.

“Nyie wenyewe mmemsikia mkuu wa mkoa (Zelothe) amethibitisha kuwa hakuna njaa mkoani hapa lakini sio hapa tu, pia mikoa ya Mbeya na Songwe wamenithibitishia kuwa hawana njaa,” alisema Naibu Waziri Masauni na kuongeza: 
“Sasa wapo wanasiasa uchwara wanaeneza propaganda kuna njaa, sio mamlaka yao kutangaza kuwa kuna njaa, kueneza uongo kama huo ni si sawa kwa kuwa kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini, wanastahili kuchukuliwa hatua ikiwemo kukamatwa,” alisisitiza.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe alimweleza Naibu Waziri Masauni kuwa hali ya kiusalama katika mkoa huo ni shwari ambapo amani na utulivu umeshamiri kwa kuwa una chakula cha kutosha.
Share:

WALIMU WATATU WAKAMATWA KWA KUPIGA DILI LA KUPOKEA MISHAHARA PRIVATE NA SERKALINI

Walimu watatu mkoani Mwanza wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la  kukimbia vituo vyao vya kazi na kufanya kazi shule binafsi huku wakiendelea kupokea mishahara ya serikali

Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Mwanza imewataja walimu hao waliokamatwa jana asubuhi katika mtaa wa Buhongwa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,kuwa ni pamoja na Richard Mgendi (30), Rwiza Ntare (27) na Gilbert Makwaya (33).

Walimu hao kila mmoja ana story yake kama ifuatavyo:-

Mwalimu Richard Mgendi alikuwa akifundisha shule ya sekondari ya Misasi wilayani Misungwi, mwaka 2012 alimuaga mkurugenzi wa wilaya hiyo kuwa anakwenda kusoma Masters ya lugha (Linguistic) katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino, kwa kipindi chote hicho inadaiwa mwalimu huyo alikwenda kusoma na alipomaliza hakurudi katika shule yake ya awali bali alikuwa akifundisha shule binafsi ya sekondari iitwayo Musabe iliyopo Buhongwa huku akiendelea kulipwa mshahara kutoka serikalini.

Mwalimu Rwiza Ntare alikuwa akifundisha shule ya sekondari iitwayo Kigongo sekondari iliyopo wilaya ya Chato mkoani Geita ambapo mwaka 2015, alimuaga mkurugenzi wake kuwa anakwenda hospitali ya rufaa ya Bugando kupatiwa matibabu ya macho na vidonda vya tumbo lakini hakurudi tena bali inadaiwa alikuwa akifundisha shule binafsi ya sekondari iitwayo Musabe iliyopo mtaa wa Buhongwa huku akiendelea kulipwa mshahara na serikali.

Mwalimu Gilbert Makwaya alikuwa akifundisha Runima sekondari iliyopo maeneo ya Buhongwa na alimuaga mkurugenzi wa wilaya ya Nyamagana tarehe 27/09/2015 kuwa anakwenda kusoma Masters ya Hesabu katika chuo kikuu cha Mwenge kilichpo mjini Moshi lakini hakwenda bali alikuwa akifundisha shule binafsi ya Musabe iliyopo mtaa wa Buhongwa huku akiendelea kupokea mshahara kutoka serikalini.

Walimu wote watatu wapo katika mahojiano na jeshi la polisi na pindi uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Jeshi la polisi linaendelea kuwatafuta baadhi ya walimu ambao wametoroka lakini inadaiwa wapo katika shule hiyo binafsi ya Musabe huku wakiendelea kulipwa mshahara na serikali pamoja na mkurugenzi wa shule hiyo.
Share:

MAJAMBAZI WAWILI 2 WAUAWA JIJINI MWANZA

Watu wawili waliokuwa wakituhumiwa kwa ujambazi wameuawa wakati wakitaka kujaribu kuwatoroka askari polisi wilayani Ilemela mkoani Mwanza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza amesema kwamba tukio hilo lilitokea  tarehe 20.01.2016 majira ya saa 2:30  usiku, katika mtaa wa kiloleli “A” kata ya Nyasaka mkoa wa Mwanza na kuwataja majambazi waliouawa kuwa ni Eric Magese miaka 22, na aliyejulikana kwa jina moja la Peter miaka kati 25 hadi 27 wote wakazi wa Mecco jijini Mwanza.

Amesema majambazi hao waliuawa wakati wakijaribu kutoroka askari polisi pindi wakiwapeleka mahali ambapo wenzao wamejificha ili waweze kufanya uvamizi.

Amesema kuwa katika tukio hilo pia ilipatikana silaha moja aina ya short gun yenye namba TZ CAR 103283 ikiwa na risasi tatu ambayo inadaiwa walipora kwenye kampuni ya ulinzi iitwayo Malika Security Service Limited

Msangi amesema majambazi hao walikuwa wakitafutwa na polisi baada ya kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza ilikiwemo tukio la Kitangiri mnamo tarehe 19.12.2016 na tukio la tarehe 02.01.2016 katika mtaa wa Nyasaka.

Jinsi walivyouawa
Msangi amesema baada ya upelelezi uliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao, walikubali kuwapeleka askari katika eneo ambalo walikuwa wamepanga pamoja na wenzao wawili kwa ajili ya kufanya matukio zaidi ya ujambazi.

Amesema walipofika katika eneo hilo, watuhumiwa hao walipiga kelele kama ishara ya kuwatorosha wenzao na kuanza kuwakimbia askari.

Askari walifyatua risasi kadhaa hewani wakiwaamuru wasimame lakini waligoma ndipo waliwafyatulia risasi za mguuni kwa bahati mbaya ziliwalenga maeneo ya juu ambapo walifariki dunia wakati wakipelekwa hospitali.
Share:

WARAKA WA ZITTO KABWE KUHUSU UCHAGUZI WA MARUDIO

Share:

TUNDU LISSU AFUNGUKA KUHUSU UPINZANI KUBURUZWA NA CCM UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO

Share:

KAULI YA MTATAIRO BAADA YA UPINZANI KUANGUKIA PUA UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO

Share:

KAULI YA RAIS MAGUFULI BAADA YA CCM KUSHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO

Share:

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARY TAREHE 24.1.2017

Share:

Monday 23 January 2017

Bulembo amtaka Lowassa Aachane na Siasa

Share:

Hatimaye Jecha Afunguka Kuhusu Kufuta Uchaguzi Zanzibar...

Share:

Bibi Akutwa amekufa Huku akiwa na vibuyu 5 na kuku mweupe

Bibi  mwenye umri wa miaka 60 amekutwa amekufa mkoani Tabora huku amevaa nguo nyeusi aina ya kaniki, akiwa na vibuyu vitano na kuku mweupe, katika mazingira yanayoashiria kushiriki vitendo vya kishirikina.

Aidha, mwili wa mtu mwingine umekutwa pembeni ya mti aliokuwa akichimba dawa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Selemani iliwataja waliokutwa wamekufa kuwa ni Nsoma Dotto (60) mkazi wa Kijiji cha Zugimlole Wilaya ya Kaliua na Mayara Marashi (50) ambaye ni mkazi wa Igunga.

Kamanda Selemani alisema Nsoma alikutwa akiwa amekufa umbali wa mita 200 kutoka nyumbani kwake juzi.

Alisema bibi huyo alikutwa amevaa nguo nyeusi aina ya kaniki akiwa na vibuyu vitano huku pembeni yake kukiwa na kuku mweupe. Uchunguzi wa awali wa jeshi hilo, unaonesha kuwa huenda ni imani za kishirikina.

Aidha, alisema Marashi ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mwakapinga, Kata ya Nanga, aliyekuwa mganga wa kienyeji, mwili wake uliokotwa Januari 16, mwaka huu ukiwa umeanza kuharibika.

Kwa mujibu wa Kamanda Selemani, mganga huyo wa kienyeji aliondoka nyumbani kwake Januari 8, mwaka huu kwenda porini kuchimba dawa, lakini hakurudi kijijini hadi maiti yake ilipookotwa akiwa amekufa.

Alisema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho. Aliwaomba wananchi wanaoenda porini kwa ajili ya shughuli zozote zile, wawe wanatoa taarifa kwa ndugu zao ili iwe rahisi tatizo linapotokea.
Share:

Rais wa Uturuki Awasili Nchini Kwa Ziara ya Kikazi

RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini jana jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.

Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt ÇavuÅŸoÄŸlu, Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat  Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak

Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   na Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan  aliyefuatana na  mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia) wakifuhia ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage jijini Dar es salaam baada ya Rais huyo  kuwasili kwa ziara rasmi nchini Januari 22, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Share:

Zitto Kabwe Asakwa na Jeshi la Polisi kwa Uchochezi,ACT Wazalendo Wadai Yuko Salama, Wataka Polisi Wafuate Utaratibu

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger