Sunday 15 January 2017

HAYA HAPA MATOKEO YA DARASA LA NNE 2016

Share:

HAYA HAPA MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2016

Share:

HAKUTAKUWA NA FIELD KWA WANAFUNZI WA VYUO WA MWAKA WA KWANZA


Leo kumuibuka taharuki kwenye mitandao ya kijamii baada ya taarifa kutolewa na kituo cha habari cha Chennel Ten kuwa hakutakuwa na Mafunzo kwa Vitendo yaani BTP ama Field kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kuanzia mwaka huu. Taarifa ambayo imetolewa na Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako.
Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 14 katika kipindi cha habari za saa kinachopeperushwa na Channel Ten. Sababu za kutokuwaruhusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwenda field ni kile kinachosemwa kuwa ni kutokuwa na ukomavu katika taaluma yao.
Share:

AJIRA KWA WALISOMA CHUO CHA MAJI, SERIKALI YAONESHA DALILI

IMG_1377
Uongozi na wanafunzi wanaosoma kwenye Chuo cha Maji, wameiomba serikali kusaidia kuwa na mpango bora wa upatikanaji wa ajira kwenye halmashauri na mamlaka za miji kwa wahitimu wa chuo hicho, ambacho kimekuwa wakala wa serikali tangu mwaka 2008.
Chuo cha Maji ambacho ni chuo pekee kikiwa na jukumu la kutoa mafunzo katika kiwango chenye ubora kwa ajili ya kupata mafundi sanifu wa maji nchini pamoja na ushuri wa kitaalam kwenye sekta ya maji, kinakabiliwa na changamoto ya wahitimu wake kukosa ajira kwa kiwango kikubwa hivyo kushindwa kutimiza malengo yake tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974.
Kwa sasa wahitimu wengi wanaopitia kwenye chuo cha Maji kilichopo jijini Dar es salaam wanakabiliwa na ukosefu wa ajira licha ya uhaba mkubwa uliopo nchini wa wataalamu wa sekta ya maji kwa ngazi za stashahada kwenye halmashauri na mamlaka mbalimbali za miji hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na uongozi wa Chuo cha Maji pamoja na wahitimu 313 wa stashahada mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho wakati wa mahafali ya nane yaliyofanyika jijini Dar es salaam, ambapo serikali iliwakilishwa na naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi  ISACK KAMWELWE.
Kwa upande wake Serikali imewataka wahitimu wanaomaliza kwenye chuo hicho kuwa licha ya kwamba inakusudia kutangaza nafasi za mafundi sanifu wa maji nchi nzima lakini pia wawe na ujasiri wa kujiajiri kwa kujiunga pamoja katika vikundi na kutumia ujuzi wao waliopata chuoni.
Katika mahafali ya nane ya Chuo cha Maji, jumla ya wahitimu 313 walitunukiwa stashahada za uhandisi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira, Hadrojiolojia na Uchimbaji wa Visima, Haidrolojia na hali ya Hewa, Teknolojia  ya maabara ya Ubora wa Maji na Uhandisi wa Umwagiliaji.
Share:

MWANAFUNZI MTANZANIA ALIYEKUWA AKISOMA NCHINI CHINA AFARIKI DUNIA NA KIFO CHAKE BADO KINA UTATA

tumepata taarifa za kuhuzunisha ambazo zinamhusu binti mtanzani aliyekuwa anasoma nchini China katika Chuo Kikuu cha Nanchang aliyekuwa akitambuliaka kwa jina la Safina John kuwa amefariki dunia. Marehemu alikutwa amefariki usiku wa kuamkia tarehe 13 Januari 2016 chumbani kwake.
Bado kuna utata mkubwa juu ya chanzo cha kifo cha marehemu kutokana na kuwa na taarifa tofauti zinazokinzana. Taarifa kutoka kwa watu wa karibu yake zinasema  marehemu alikuwa anaumwa kwa takribani wiki mbili zilizopita na alikuwa haonekani darasani wakati wakala wa marehemu huyo (Global Education Link) ametoa taarifa na kusema kifo ni cha ghafla. Bado uchunguzi wa chanzo chakifo hicho unaendelea. Taratibu zakusafirisha mwili wa marehemu zinafanyika.
Chuo alichokuwa akisoma marehemu
KUHUSU KUSAFIRISHA MWILI
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa TASAFIC (Umoja wa wanafunzi wanaosoma China)  ni kwamba, gharama za kusafirisha mwili  ni Dola 10000 ambayo ni sawa na 63,000RNM yaani takribani Tsh Millioni 20. Gharama hizi zinatakiwa kulipwa na familia ya marehemu  na siyo wakala wake “Agent”  japo wakala amesema atalipa halafu familia itazirudusha.
Share:

Barua ya TEC Kwenda Kwa Maaskofu wa Makanisa Yote Kuombea Mvua Inyeshe

Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 15 2017

Share:

Saturday 14 January 2017

Magazeti Ya Leo Jumamosi ya January 14


Share:

Wizara ya Elimu Yatoa ONYO Kali,Ni Kuhusu Kuwatimua Wanafunzi Vilaza

Serikali imezionya shule zote za sekondari na msingi nchini hususani za mashirika ya dini ambazo bado zinakaririsha wanafunzi darasa kwa kigezo cha kutofikia alama za ufaulu zilizowekwa na shule, kuacha kufanya hivyo kwa kuwa ni kinyume na sheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamishna wa Elimu nchini Nicolas Burreta imesema kuwa serikali kupitia wizara ya elimu imebaini kuwa bado kuna shule ambazo mbali na kukaririsha wanafunzi darasa, zimekuwa pia zikiwafukuza wanafunzi shule, na nyingine zikiwahamishia katika shule nyingine.

Kamishna Burreta katika taarifa hiyo ameziagiza shule hizo kufuta maagizo yao ya ama kuwakaririsha darasa, kuwafukuza wanafunzi hao, au kuwahamisha huku akiwataka wazazi ambao watoto wao wamefukuzwa au kuhamishwa, wawarudishe watoto wao katika shule hizo waendelee na masomo.

Pia amewataka wathibiti ubora wa shule, kanda wilaya na maafisa elimu wa wilaya na mikoa kusimamia agizo hilo na kwamba shule yoyote itakayokiuka maagizo hayo itachukuliwa hatua kali za kisheria.

Share:

Ufafanuzi wa Wizara ya Nishati Kuhusu Tuhuma za Profesa Muhongo Kushiriki Kupandisha Bei ya Umeme


Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kikao cha Waziri wa Nishati na Madini na Ujumbe wa Benki ya Dunia kilichofanyika tar
Share:

Tangazo Kwa Umma Kuhusu Wahitimu Wa Shahada Na Stashahada Za Ualimu (Sayansi) Waliotakiwa Kuwasilisha Vyeti

Share:

Mhadhiri Chuo Kikuu Akamatwa na TAKUKURU Kwa Kuomba Rushwa ya Ngono ili Ampatie matokeo mazuri ya mtihani wake wa Supplementary

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Taifa cha Usifirishaji (NIT) amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Konondoni baada ya kunaswa katika mtego wa rushwa ya ngono.

Mhadhiri huyo anayefahamika kwa jina la Samson Jovin Mahimbo (66) mkazi wa Makongo Juu, Dar es Salaam alikamatwa  Januari 12, 2017 katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kama Camp David iliyopo eneo la Mlalakua, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Samson Mahimbo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego kufuatia taarifa iliyotolewa na mwanafunzi huyo aliyeombwa rushwa ili aweze kumpatia alama (marks) nzuri  katika mtihani wake wa marudio (supplementary examination) alioufanya tarehe 5 Januari 2017.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa tuhuma za kufanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2017.
Share:

Azam Fc Yatwaa Ubingwa wa Mapinduzi Cup 2017 Kwa Kuitandika Simba 1-0

Shuti la ‘mwendokasi’ la umbali usiopungua mita 25 la kiungo Himid Mao limetosha kuamua matokeo ya mchezo wa Fainali ya Mapinduzi uliofanyika mjni Zanzibar.

Miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliichapa Simba bao 1-0 na kutosha kutangazwa mabingwa wapya wa Kombe la Mapinduzi.

Wakinolewa na kocha wa vijana wa Azam, Idd Cheche aliyechukua kwa muda mikoba ya Zeben Hernandez aliyetimuliwa kwa matokeo mabaya, Azam FC iliibuka na ushindi wa bao la dakika ya 13 lililofungwa na kiungo huyo wa Taifa Stars, Himid.

Ushindi huo pia umeifanya Azam FC kutwaa taji la tatu la Kombe la Mapinduzi baada ya awali kulitwaa miaka ya 2011 na 2012.

Katika mashindano hayo, beki wa Simba, Method Mwanjali amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Mapinduzi Cup, tuzo ya kipa bora imekwenda kwa Aishi Manula wa Azam FC, timu bora ya vijana ni Taifa Jang’ombe.

Mfungaji bora ni kiungo wa Yanga, Saimon Msuva, aliyeweka kimiani mabao manne, wakati mwamuzi bora wa mashindano hayo akichaguliwa kuwa Mfaume Ali.
Share:

Friday 13 January 2017

TANGAZO KWA UMMA: KUHUSU WAHITIMU WA SHAHADA NA STASHAHADA ZA UALIMU (SAYANSI) WALIOTAKIWA KUWASILISHA VYETI

Image result for serikali ya tanzania 


TAREHE 12/12/2016 WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA ILITANGAZA KUWA WAHITIMU WA STASHAHADA NA SHAHADA ZA UALIMU KATIKA MASOMO YA SAYANSI (FIZIKIA, KEMIA, BIOLOJIA) NA HISABATI WA MWAKA 2015 WAWASILISHE VYETI VYAO KWA
AJILI YA UCHAMBUZI WA WAHITIMU WENYE SIFA.

WAHITIMU WALIOKUWA NA MAPUNGUFU KATIKA NYARAKA ZAO WANATAKIWA WAWASILISHE TENA. WAHITIMU HAO NI KAMA IFUATAVYO:-
     (1) WALIOTUMA NAKALA ZA “RESULTS SLIPS” AU “ACADEMIC TRANSCRIPTS” BILA NAKALA ZA VYETI HALISI VYA KIDATO CHA 4, 6, STASHAHADA AU SHAHADA
     (2) WALIOTUMA NAKALA ZA VYETI VYA STASHAHADA ZA UZAMILI (POSTGRADUATE DIPLOMA IN EDUCATION – PGDE) BILA NAKALA ZA “VYETI VYA SHAHADA YA KWANZA PAMOJA NA “ACADEMIC TRANSCRIPTS” ZAKE;
WAHITIMU AMBAO HAWAKUTUMA KABISA NAKALA ZA VYETI VYAO WANAPEWA FURSA YA MWISHO KUTUMA.
WAHITIMU AMBAO NYARAKA ZAO ZILIWASILISHWA MAJINA YAO YANAPATIKANA KATIKA LINK HIZI .
WAHITIMU WALIOPO KWENYE ORODHA HAPO JUU WASIWASILISHE NYARAKA HIZO TENA.
UTARATIBU WA KUTUMA VYETI NI KAMA IFUATAVYO:-
  1. WAOMBAJI LAZIMA ‘WA-SCAN’ VYETI HALISI (ORIGINAL CERTIFICATES - KIDATO CHA 4, 6, STASHAHADA, STASHAHADA YA UZAMILI AU SHAHADA) NA SIYO KIVULI CHA CHETI (PHOTOCOPY) ;
  2. WAOMBAJI WA STASHAHADA YA UZAMILI (PGDE) NA SHAHADA LAZIMA ‘WA-SCAN’ NA KUTUMA NAKALA ZA “ACADEMIC TRANSCRIPTS” ZA SHAHADA YA KWANZA.
  3. WAOMBAJI LAZIMA WAWEKE NAKALA ZA VYETI VYAO VYOTE KWENYE ‘FILE’ MOJA LIKIWA KATIKA ‘PDF’ NA LIPEWE JINA LA MWOMBAJI HUSIKA KABLA YA KUTUMA. NYARAKA ZITUMWE KUPITIA ‘BARUA PEPE’ ZAO WENYEWE NA SIYO ZA WATU WENGINE.
TANBIHI:
  1. WAOMBAJI WATUME TAARIFA ZAO KUPITIA BARUA PEPE YA WIZARA info@moe.go.tz
  2. TAREHE YA MWISHO KUPOKEA NYARAKA NI 17 JANUARI,2017.
  3. BARUA PEPE ZA KUWASILISHA NYARAKA ZA WAOMBAJI ZITUMWE MARA MOJA TU NA SI KWA KURUDIA RUDIA ILI KUEPUKA USUMBUFU WA KUTAFUTA ZILIZO SAHIHI.

IMETOLEWA NA
PROF. SIMON S. MSANJILA
KAIMU KATIBU MKUU
12/01/2017

Share:

AUDIO | Darassa Ft. Lameck Ditto - Weka Ngoma | Download #TBT


Share:

TUNDU LISSU ATOA UFAFANUZI KUHUSU KUFUNGWA JELA KWA MBUNGE WA CHADEMA KILOMBERO-LIJUAKALI

HATUA ya Mahakama ya Wilaya ya Kilombero, Morogoro kumfunga Peter Lijualikali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero miezi sita jela, inatokana na visa vya kisiasa

Ni kauli ya Tundu Lissu, Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo mbele ya waandishi wa habari aliokutana nao kwenye Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki amesema kuwa, vita kati ya upinzani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimesababisha Lijuakali (Chadema) kupata hukumu hiyo ya kisiasa.

Mbele ya waandishi wa habari Lissu amesema kuwa, “hiyo ni hukumu ya kisiasa” na kwamba, Jeshi la Polisi nalo limeingizwa kwenye vita hivyo.

Lissu amesema, chanzo cha hukumu hiyo kinatokana na mgogoro wa uongozi ndani ya Halmashauri ya Kiliombero ambapo Chadema na washirika wake wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) walishinda madiwani wengi.

Hivyo, kwa mujibu wa Lissu, Halmashauri ya Kilombero ilipaswa kuongozwa na mwenyekiti anayetoka na Ukawa na awe Chadema.

“Ili hilo lisiwezekane, na ili CCM wachukue Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero licha ya kushidwa kwenye udiwani, ilibidi wamfanyie Lijualikali mambo ya ajabu,” amesema Lissu.

Lijualikali (30) amehukumiwa jana kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki. Huku Stephano Mgata (35), Dereva wake ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo akifungwa kifungo cha miezi sita nje.

“Kifungo cha Mh. Lijualikali ni adhabu ya kisiasa. Mh Lijualikali ni mfugwa wa kisiasa. Amefugwa kwa sababu ya siasa.

“Adhabu ya kisisa ni vita ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya Chadema na wanatumia Jeshi la Polisi, wanatumia mahakama na kwingineko. Vita hii hii wanawatumia akina Lipumba (Profesa Ibrahim Lipumba,” amesema Lissu na kuongeza;

“Kwingine wamemweka Lema (Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini) mahabusu kwa miezi mitatu. Hakuna jinai yoyote. Tuliwashinda kwenye uchaguzi.

“Sasa baada ya uchaguzi walimfungulia Lijualikali kesi ya kupinga matokeo mahakama kuu, tukawapiga chini. Wamefungua rufaa na tunawatandika.”

Mwanasheria huyo amesema kuwa, nchi hii ina wafungwa wa kisiasa na kwamba, pamoja na CCM kudhani kwamba, kumfungulia kesi Lijuakali kutawapa afueni. Wasahau.

“Tuna wafungwa wa kisiasa nchi hii. Wale wanaofikiria kwamba kumfunga Lijualikali CCM itapendwa na wananchi wa kilombelo wasahau hilo.

“Huwezi kuwatesa wananchi, ukatesa viongozi waliowachagua kwa mapenzi yao halafu ukategemea wakupende. Wasahau,” amesema Lissu.

Aidha, Lissu ametoa ufafanuzi kuwa Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamlinda Lijualikali hivyo hawezi kupoteza ubunge wake kutokana na hukumu hiyo.

Amesema Chadema hakijaridhika na hukumu hiyo, hivyo kwa sasa wanaandaa utaratibu wa kisheria ili kukata rufaa kuipinga ambapo hatua hiyo inaweza kuchukua siku mbili kukamilika.

Timothy Lyon, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo alisema, amemhukumu Lijualikali baada ya kumtia hatiani kwa kosa yeye na dereva wake na kwa kuwa, mbunge huyo alipatikana na hatia katika kesi tatu huko nyuma na kuhukumiwa kulipa faini hivyo alistahili kutumikia adhabu hiyo.

Kesi zilkizotajwa na Lyon zinazomuhusu Lijualikali ni namba 338, namba 220 na namba 340 zote za mwaka 2014.

Katika kesi hiyo, Dotto Ngimbwa, Inspekta wa Polisi aliiambia mahakama kuwa, Lijuakali akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na Mgata walitenda kosa hilo Machi Mosi mwaka 2016 eneo la Kibaoni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kialombero na kwamba, walifanya fujo kinyume cha sheria.

Alisema tukio hilo lilitokea Machi Mosi mwaka huo saa 4 asubuhi ambapo washtakiwa walikana mashtaka lakini upande wa mashtaka ukathibitisha bila kuacha shaka kwamba, walitenda kosa.
Share:

RAIS MAGUFULI ASEMA MARUFUKU KUMPANGIA MKULIMA BEI YA MAZAO

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepiga marufuku viongozi wa serikali wenye tabia ya kuwapangia bei ya mazao wakulima na kuwataka wawaache wakulima wauze mazao yao kwa bei itakayowanufaisha wakulima kutokana na mazao yao

Ameonya juu ya tabia hali ilivyo sasa ambapo mkulima amekuwa akipunjwa kutokana na bei ndogo anayolipwa pindi anapouza mazao yake.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati ambapo amemaliza ziara ya siku mbili mkoani Simiyu na kuanza rasmi ziara ya siku mbili mkoani Shinyanga na kuahidi kuendelea kuulinda Muungano wa Tanzania Bara na  Zanzibar kwa nguvu zake zote

Rais Magufuli amesema Mapinduzi matukufu ya Januari 12,1964 ndio yaliyosababisha kuwepo kwa Muungano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar na hivyo kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa  Watanzania kuuenzi na kuulinda kwa manufaa ya wananchi wote.

'' leo ni siku muhimu sana kwetu Watanzania kwa kuwa siku hii ya Januari 12,1964  miaka 53 iliyopita  ndio siku yalipofanyika Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliyopelekea kuondolewa kwa utawala dhalimu wa kikoloni na kupelekea kuzaliwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Tanzania Bara na  Zanzibara kuungana,hivyo tuna kila sababu ya kuienzi siku hii muhimu'' amesema Rais Magufuli.

Akiwa Wilayani Maswa mkoani Simiyu mara baada ya kutembelea kiwanda cha kutengenezea chaki na kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa barabara ya Mwigumbi hadi Maswa yenye urefu wa kilomita 50.3 kwa kiwango cha lami, Rais Magufuli amewataka wananchi wa mkoa wa Simiyu kutumia barabara hiyo kujiletea maendeleo.

Rais Magufuli ameupongeza mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza kwa vitendo Sera ya Serikali ya awamu ya Tano ya Tanzania ya viwanda kwa ujenzi wa kiwanda cha Chaki na  kutoa wito kwa uongozi wa kiwanda hicho kuongeza uzalishaji wa chaki ili ziweze kukidhi soko la nchi nzima badala ya mikoa kumi ya sasa inayotumia chaki zinazozalishwa na kiwanda hicho.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger