Sunday 28 August 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI TAREHE 28.8.2016






Share:

Saturday 27 August 2016

Angalia Picha 30: ASKARI WA JESHI LA POLISI SHINYANGA WAKIFANYA MAZOEZI KUJIANDAA KUKABILIANA NA UHALIFU



Leo Jumamosi,Agosti 27,2016 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeendelea kufanya ya mazoezi ya utayari wa kukabiliana na vitendo vya kihalifu.
Akiongoza mazoezi hayo,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amesema mazoezi hayo aliyoyataja kwa jina la Kiingereza ““Route Match” ni ya kawaida kwa ajili ya kujiweka tayari kukabiliana na uhalifu unaoweza kujitokeza. 
Kamanda Muliro amesema wamekuwa wakifanya mazoezi mara kwa mara lakini kilichofanyikani kubadilisha muda wa kufanya mazoezi na wataendelea kufanya kila siku za Jumamosi. 
“Huu ni mfumo huu ni wa kawaida kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazolisimamia jeshi la polisi..tumefanya matembezi yanayohusiana na ukakamavu,yanayojenga ujasiri kwa askari kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake,kwa hiyo kwa wananchi wanaoishi karibu na kambi ya jeshi siyo wageni wa mambo haya ambayo huwa tunayafanya siku za Jumamosi ”,alieleza Muliro. 
“Kilichofanyika leo tumepita mtaani asubuhi/mchana badala ya usiku/alfajiri (saa 11 hadi saa 1.30) kama vile tumekuwa tukifanya lakini lengo ni moja tu,watambue kuwa jeshi lao la polisi liko imara katika kuwalinda raia na mali zao,kusimamia sheria za nchi na askari mzuri ni yule mkakamavu,mwepesi ana uwezo wa kufikiri haraka kujua kile anachokitekeleza kimesimamia sheria gani”,aliongeza Muliro. 
Alisema mazoezi hayo ni ya kawaida na kusisitiza kuwa kwa wananchi ambao siyo wahalifu na walio wema wamefurahia mazoezi hayo. 
Askari polisi wakiongozwa na kamanda Muliro walipita katika maeneo mbalimbali mjini Shinyanga na maeneo huku wakiwa na vifaa mbalimbali vya jeshi hilo ikiwemo magari,silaha na magari ya maji ya kuwasha. 
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo maeneo mbalimbali walikopita askari polisi mjini Shinyanga,ametuletea picha 31…Shuhudia hapa chini 
Hapa ni katika kambi ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga-Kulia ni Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akitoa maelekezo kwa askari wa jeshi hilo kabla ya kuanza mazoezi mtaani leo majira ya saa tatu asubuhi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akieleza kuhusu mazoezi ya "Route Match"
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akisisitiza jambo kabla ya kuanza kufanya mazoezi
Askari polisi wakiwa kambini kabla ya kuanza kufanya mazoezi mtaani
Askari polisi wakijiandaa kuanza kufanya mazoezi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akifanya mazoezi na askari polisi wa jeshi hilo mjini Shinyanga
Askari polisi wakiendelea na mazoezi mtaani
Askari polisi wakiwa katika gari la maji ya kuwasha
Mazoezi yanaendelea katika eneo la Phatom mjini Shinyanga
Gari la maji ya kuwasha likiwa barabarani
Magari ya polisi yakiwa barabarani
Mazoezi yanaendelea
Askari polisi wakiwa ndani ya gari 
Wananchi wakiendelea na shughuli zao huku askari polisi wakiendelea na mazoezi yao
Wananchi wakiendelea na safari zao
Askari polisi wakiendelea na mazoezi yao
Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi 
Askari polisi wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi mtaani
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza kambini ambapo aliwaambia askari polisi kuwa watakuwa wanafanya mazoezi ya namna hiyo kila siku za Jumamosi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akisisitiza jambo
Maafisa wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi
Askari polisi wakiwa kambini
Askari polisi wakimsikiliza kamanda Muliro
Kamanda Muliro akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kufanya mazoezi
Waandishi wa habari wakiwa kambini
Askari polisi wakijiandaa kutawanyika baada ya kumaliza kufanya mazoezi.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Share:

Picha: JESHI LA POLISI LAONGEZA ASKARI WENGINE 80 KUSAKA MAJAMBAZI VIKINDU MKOANI PWANI


  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeongeza nguvu kwa kutuma askari wengine 80 katika oparesheni ya kusaka majambazi inayoendelea katika maeneo ya Vikindu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
 Akizungumza na vyombo vya habari leo katika kituo kikuu cha  Polisi Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Kamishna Simon Sirro, amesema Jeshi hilo limeanza rasmi oparesheni hiyo usiku wa kuamkia jana, ikiwa na lengo la kusaka watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wanaodaiwa kufanya matukio kadhaa ya ujambazi likiwemo lile la kuuawa kwa askari wanne waliokuwa wakienda lindoni, katika benk ya CRDB, Mbade jiji Dar es Salaam. 
 Amesema kuwa katika oparesheni hiyo kuna watu waliouawa na wengine wanashikiliwa na jeshi hilo, lakini amekataa kutaja idadi yoyote ile ya waliouawa au waliokamatwa kwa sababu za kiusalama kwa kuwa oparesheni hiyo bado inaendelea.
“Itakuwa ni kinyume cha utaratibu nikieleza kinachoendelea kwenye operesheni, niwahakikishie silaha zilizochukuliwa zinarudi,kinachoendelea nitawajulisha jumanne ili wananchi wajue kitu gani kinaendelea,” amesema.
Ameongeza kuwa; “Mapambano ni ya kawaida sana, na ndio maana askari polisi akifa kwa silaha ni jambo la kawaida sana. Operesheni tutaifanya maeneo ya Vikindu, Pwani Dar es Salaam, sababu hii network (mtandao) ipo na lazima tutaisafisha.Kama walidhani wataitawala DSM wamejidanyanya lazima tutarudisha heshima ya jiji.”
Katika hatua nyingine, Sirro amesema amepata taarifa kuwa wapo baadhi ya watu wanapewa fedha kwa ajili ya kufanya maandamano Septemba Mosi mwaka huu ambapo ametoa onyo kwa watakaoshiriki kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kuwa maandamano hayo hayajaruhusiwa.
“Wote tunajua madhara ya fujo, wazalendo naomba msishiriki, Wanaotaka kujionesha wanapambana na polisi waje barabarani, ” amesema.
Usiku wa kuamkia jana, hali ya taharuki iliwakumba wakazi wa Vikindu baada ya kikosi maalum cha askari kuvamia nyumba moja iliyoko eneo hilo, na kisha kuzuka kwa majibizano ya risasi kati ya polisi na wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa katika nyumba hiyo.
Baadhi ya askari wakiwa tayari kwenye magari yao wakati wa kujiandaa kuelekea Vikindu kwenye mapambano 
Vikosi hivyo vikitoka makao makuu ya kanda maalum ya Dar kuelekea kwenye mapamban 
Share:

LOWASSA AKUTANA USO KWA USO NA RAIS MAGUFULI KANISA LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM


Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa leo tarehe 27 Agosti, 2016 ameadhimisha Jubilei ya Dhahabu ya Miaka 50 ya Ndoa yake na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Hafla ya Jubilei hiyo imefanyika nyakati za mchana katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa uliopo kando ya kanisa la Mtakatifu Petro-Oysterbay na imetanguliwa na Misa ya shukrani iliyofanyika katika kanisa hilo majira ya asubuhi.
Jubilei hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Cleopa Msuya, Dkt. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba na Mhe. Edward Lowassa.
Misa Takatifu ya Shukrani imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Askofu Josephat Lebulu na kuhudhuriwa na Maaskofu na Maaskofu Wakuu saba akiwemo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa Misa Takatifu Rais Magufuli amempongeza Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa kwa kutimiza miaka 50 ya ndoa na ameeleza kuwa ndoa hiyo iliyowaunganisha wanandoa wanaotoka katika madhehebu tofauti ya Kikristo imetoa fundisho kubwa kuwa binadamu wanapaswa kuwa wamoja hata kama wana tofauti mbalimbali zikiwemo za kimadhehebu ya dini, siasa na kanda.
Rais Magufuli amesema miaka 50 ya ndoa ya Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa Katoliki na Mkewe Mama Anna Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa la Kilutheri inawafundisha watanzania wote hususani wanasiasa kuishi kwa upendo na kuilinda amani waliyonayo na ametoa wito kwa viongozi dini kuendeleza juhudi zao za kuliombea taifa na kuwaunganisha wananchi licha ya tofauti walizo nazo.
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa pamoja na kuwashukuru Viongozi wote, ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria Misa ya Shukrani na Jubilei hiyo ya miaka 50 ya ndoa yake amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijaalia ndoa yake umri mrefu.
Rais Mstaafu Mkapa pia ametoa wito kwa watanzania kupenda na kushirikiana huku akibainisha mafunzo aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa dini kuwa "Kila mmoja ni zawadi kwa mwenzake"
Nae Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amempongeza Rais Mstaafu Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa kwa kuadhimisha miaka 50 ya ndoa na amewasihi watanzania kuiga mfano mwema uliooneshwa na wana ndoa hao ambao wamedumu katika imani bila kuyumba.
Kardinali Pengo amesema ndoa ya Rais Mstaafu Mkapa anaifundisha jamii kuwa tunaweza kuishi kwa imani zetu bila kubadili dini
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
27 Agosti, 2016
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SAUT-ARUSHA 2016/2017

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger