

Nabii Rabiel Akyoo wa Kanisa la Ukombozi akiongea na waandishi wa habari
Nabii Rabiel Akyoo wa Kanisa la Ukombozi anatarajiwa kuongoza maombi ya kitaifa kesho jijini Arusha kwa lengo la kuliombea taifa kudumisha amani na mshikamano wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.
Akizungumza na waandishi wa habari Nabii Akyoo alisema maombi hayo yatakusanya waumini kutoka maeneo mbalimbali nchini na yatakuwa na ajenda kuu ya kuombea utulivu na mshikikano wa taifa.
“Ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda amani Ikitoweka, hakuna kazi, hakuna kipato, na maisha yatakuwa magumu kwa kila mmoja wetu,” alisema.
Sambamba na maombi hayo, kutafanyika harambee ya kuchangia kituo kipya cha habari cha kanisa hicho, kitakachojumuisha televisheni na redio, huku sera yake ikizinduliwa rasmi.
Katika siku hiyo pia kutakuwa na burudani ya nyimbo za injili kutoka kwa waimbaji mbalimbali maarufu akiwemo Upendo Nkone, anayetarajiwa kupamba maombi kwa nyimbo zake za kumsifu Mungu.
Waumini na wananchi wataungana kushiriki ibada ya Meza ya Bwana, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano wa kiroho na taifa kwa ujumla.
Nabii Akyoo aliwaasa Watanzania kujitokeza siku ya kupiga kura kwa amani na utulivu, akisisitiza kuwa kura ni sauti ya kila raia, lakini amani ya taifa ni urithi wa kudumu.
“Kura yako ni sauti yako, lakini zaidi ya yote, amani ya taifa letu ndiyo urithi mkubwa tunaopaswa kuudumisha,” alisema Nabii huyo.
Maombi hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na waumini wa madhehebu mbalimbali, viongozi wa dini na wananchi kutoka mikoa tofauti, huku Arusha ikitarajiwa kuwa kitovu cha ibada kubwa ya taifa
Na Oscar Assenga,TANGA
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bandari ya Tanga imesema kwamba wanatumia umakini mkubwa na ufanisi katika kuhudumia shehena mbalimbali zinazopita kwenye Bandari hiyo ikiwemo ya magari ambayo imekuwa ikiongezeka kila mara
Hayo yalisemwa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Bw. Peter Millanzi alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya taarifa zilizosambaa kwa baadhi ya mitandao kuwa uwepo wa wizi wa baadhi ya vifaa kwenye magari ambayo yanapitia katika Bandari hiyo jambo ambalo limewashangaza kutokana na umakini wao katika kuhudumia shehena hiyo.
Millanzi alisema kwamba , shehena ya mzigo unaopita wanaouchukulia kwa umakini zaidi ambayo watu wengi wana masilahi yao binafsi ambapo wametengeneza utaratibu wa kuhakikisha mizigo yote inayoingia na kutoka bandarini hapo ipo salama na inafika kwa wateja ikiwa salama.
“Kwa hiyo katika kuhudumia shehena hizo ikiwemo magari kwa tunatengeneza utaratibu ambapo meli inapotia nanga bandarini lazima kuwepo na taasisi mbalimbali ikiwemo Wakala wa Meli (TASAC),Survey, na TPA kwa hiyo magari yanapoteremka yanakaguliwa na kurekodiwa taarifa zake kwenye fomu maalumu inayoitwa “VDITT”inaonyesha hali halisi ya gari lilivyopokelewa bandari hapo na kuna maeneo mbalimbali yanawekwa alama ya vema kuonyesha vifaa ambavyo vilivyoanishwa havijanyofolewa” Aliongeza Millanzi
“Lakini pia yapo magari tunayapokea yakiwa yamenyofolewa na yenyewe tunaonyeshwa kwenye ile fomu na hao wote waliotajwa wanashuhudia kile kilichojazwa na yapo makubaliano baada ya kujaza jinsi hali halisi gari lilivyopokelewa kwenye bandari na kutiliana saini ya makubaliano na hilo gari linapelekwa eneo la kuhifadhi” Alisema Millanzi
Aidha alisema kwamba katika eneo la kuhifadhi kuna watu wanapokea wa ulinzi na makarani kisha kusaini ili kuonyesha kwamba magari waliopokea ni sawa na vile walivyojaza na magari yanapokuja kuchukuliwa na mteja anasaini baada ya kulikagua gari lake na wakijiridhisha wanatoa ushuhuda gari lake amelipokea kama lilivyopokelewa bandarini hapo.
“Baada ya hapo anasaini na kulichukua kwenda zake kiujumla kipindi chote hatujawahi kupokea tukio lolote la malalamiko kwamba gari limenyofolewa au kuharibiwa likiwa mikononi mwa bandari.”Alisema Kaimu Meneja huyo wa Bandari ya Tanga.
katika hatua nyingine Milanzi alisema kwamba hivi sasa wameongeza ufanisi mkubwa katika kuhudumia shehena hususani Magari kutokana na uwepo wa maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali kwa kutumia kiasi cha Sh.Bilioni 429.1 na hivyo tokea walipoanza kuhudumia magari imepita mwaka mmoja
Millanzi alisema kwamba, kutokana na uwekezaji huo shehena ya Magari imekuwa ikiongezeka mwezi hadi mwezi kutokana kuongezeka kwa ufanisi katika kuhudumia shehena mbalimbali na hivyo wenye meli na wateja wameamua kupitisha mizigo yao katika Bandari ya Tanga na magari yalianza kupitia bandari hiyo mwezi Agosti mwaka 2024 .
Alisema kwamba na takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa kuanzia mwezi Agosti, 2024 hadi mwezi Julai , 2025 wameweza kuhudumia meli 45 zilizokuwa zimebeba shehena ya magari na magari yaliyohudumiwa ni magari 9,665 na wamepata bahati ya kupata wateja na mawakala mbalimbali ambao wameamua kupitisha shehena ya magari katika bandari hiyo.
“Shehena hizo za magari yanapita hapa nchini na mengine nje ya nchi kama unavyojua Tanzania imepakana na nchi nyingi ambazo hazipakani na bahari kama vile Rwanda,Burundi,Kongo,Uganda ,Malawi,Zambia na nchi nyengine iliyopo mbali zaidi lakini kutokana na kuwepo huduma bora imeamua kupitisha mizigo yake ni Zimbambwe “ Alisema Millanzi
Alieleza pia wamekuwa na vikao mbalimbali na wadau ili kuweza kuona kama kuna changamoto wanakutana nazo ili kuzipatia ufumbuzi kwa kufikia viwango vya juu na meli zinapofika Bandarini kupeleka shehena ya mbalimbali ikiwemo magari zinahudumiwa kwa muda wa saa 72 iwapo mteja amekamilisha taratibu zote za kiforodha mara gari linapopokelewa anayofursa ya kuchukua gari lake.
-