Thursday, 30 January 2020

AFISA USALAMA WA TAIFA FEKI AKAMATWA AKITAPELI WATUMISHI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SHINYANGA

                                      Sheliku Sweya
                      Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga Dk. Rose Malisa amenusurika kutapeliwa na mwanaume aitwaye Sheliku Sweya (45)ambaye alijifanya kuwa ni ofisa usalama wa taifa akimtaka ampe rushwa ya ngono ili amsaidie kutatua changamoto zilizopo hospitalini huku Dk. Geofrey Mboye akitapeliwa Sh 300,000 ili asaidiwe kupata uhamisho wa kwenda mkoani Dodoma.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juzi,Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba alisema baada ya kupata taarifa hizo waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata Januari 23,2020, ambapo katika uchunguzi wa awali wamebaini mtuhumiwa siyo ofisa usalama wa taifa bali amekuwa akitumia cheo hicho kujipatia kipato au rushwa ya ngono ili kufanikisha malengo yake.

Alisema madaktari wote ni watumishi katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambapo Dk .Malisa ambapo alielezwa kuwa iwapo atatoa rushwa ya ngono atapatiwa vifaa tiba na kuongezewa watumishi wa afya ikiwa ni pamoja na kumuahidi kumfutia deni kiasi cha Shilingi milioni 40  anazodaiwa na taasisi ya afya alikopatia masomo yake ya udaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama.

"Kutokana na ushirikiano mkubwa uliofanyika na Dk.Malisa tuliweka mtego na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa kabla hajafanikiwa kupata rushwa ya ngono,anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika",alisema kamanda Magiligimba.

Katika maelezo yake polisi Dk. Rose Malisa alieleza kuwa alimtilia mashaka mtuhumiwa na kutoa taarifa polisi ambao walishirikiana ikiwa ni pamoja na kuweka mtego ambao ulisaidia kufanikiwa kumkamata mtu huyo aliyejifanya ofisa usalama wa taifa ili kufanikisha malengo yake.
Share:

Kagame: Sitashurutishwa kufungua mpaka na Uganda


Rais wa Rwanda Paul Kagame, alisema Jumatano kwamba serikali yake itafungua mpaka na Uganda wakati itajihisi kufanya hivyo akisisitiza kwamba hakuna mtu wala nchi yoyote itamshurutisha kufanya hivyo.

Akihutubia mabalozi katika mkutano wa kila mwaka na waakilishi wa nchi za nje pamoja na mashirika ya kimataifa katika ikulu ya raia mjini Kigali, Kagame alizungumzia swala la Uganda na Rwanda, akigusia kwamba maafisa wake wanajitayarisha kwa mkutano wa Angola kuzungumzia uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Hata hivyo, rais huyo alisisitiza kwamba hakuna litakalobadilika iwapo matakwa ya Rwanda hayatazingatiwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya rais mjini Kigali, iliyowekwa kwenye ukurasa wa twitter wa serikali ya Rwanda, rais Kagame amesema mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, ni jirani wake Uganda akielezea kwamba tatizo lililopo ni kubwa kuliko kufungwa kwa mpaka kama inavyoripotiwa.

“Hata iwapo tunafungua mpaka wa Rwanda na Uganda, swala kuu ni kukamatwa na kuzuiliwa kwa raia wetu nchini Uganda”, amesema rais Kagame.

Mwezi Desemba mwaka uliopita 2019, Uganda iliachilia huru raia kadhaa wa Rwanda, waliokuwa wanazuiliwa kwa maadai ya kuifanyia Rwanda ujasusi.

“Swala hili sio la kufunga wala kufungua mpaka. Ni swala la raia wetu kukamatwa wakiwa Uganda. Tumefunga mpaka kwa sababu hatutaki raia wetu kuingia Uganda kwa sababu watakamatwa. Lakini raia wa Uganda wapo huru kuingia Rwanda”, aliendelea kusema rais Kagame.

Uganda imekuwa ikikanusha madai ya kuakamata raia wa Rwanda wanaotii sheria, ikisisitiza kwamba wanaokamatwa wanashukiwa kufanya uhalifu.

Kagame alitaja hatua ya Uganda ya kuachilia huru raia wa Rwanda kuwa nzuri lakini akawa mwepesi wa kuongezea kwamba haitoshi na kwamba ni idadi ndogo sana ya raia wa Rwanda waliachiliwa huru, akidai kwamba raia wawili wa Rwanda walikufa wakiwa kizuizini Uganda kutokana na mateso.

Kagame pia alisema kuongoza jumuiya ya Afrika mashariki ni kazi ngumu sana kuliko kuongoza umoja wa Afrika – AU.

“Na wakati haya yote yanaendelea, tunazungumza sana kuhusu ushirikiano katika jumuiya ya Afrika mashariki. Tutaendelea tu kuzungumza kuhusu ushirikiano huo bila mafanikio kama tunayofanya ni tofauti na tunayosema. Tunastahili kufanya yaliyo sawa”, aliendelea kusema Kagame.

Rwanda inaishutumu Uganda kwa kuunga mkono makundi ya wapiganaji yenye lengo la kupindua serikali ya Kagame, kuwakamata raia wa Rwanda, na kuhujumu uchumi wake.

Rwanda imeweka marufuku ya biashara na kufunga mpaka wake na Uganda tangu Februari mwaka uliopita 2019 na kuwaonya raia wake kutoingia Uganda.

Uganda nayo inaishutumu Rwanda kwa kuiwekea marufuku ya kibiashara, kufanya upelelezi dhidi ya serikali ya rais Yoweri Museveni kwa lengo la kutatiza usalama wake, kuwafuta kazi maafisa wa ngazi ya juu raia wa Uganda waliokuwa wakifanya kazi Rwanda na kueneza habari za chuki dhidi ya Uganda na maafisa wake serikalini.

Rwanda imekuwa na uhusiano mbaya na majirani wake Burundi na Uganda, huku Burundi ikiishutumu kwa kuyapatia silaha makundi yanayopinga utawala wa rais Piere Nkurunziza na kupanga njama za kuangusha utawala wake katika mapinduzi yaliyofeli ya mwaka 2015.

Uganda imekataa kuzungumzia mgogoro wake na Rwanda katika vyombo vya habari.


VOA





Share:

Eneo kubwa linauzwa: Mapinga(Bagamoyo) ......Bei ni Nzuri Kabisa

Eneo kubwa linauzwa: Mapinga(Bagamoyo)

 Eneo kubwa la ekari 5 linauzwa bei nafuu sana. Eneo linafaa kwa uwekezaji wa shule, hospitali, chuo, yard, kiwanda n.k
Eneo liko sehem nzuri, yenye view nzuri na barabara ya uhakika.


Umbali kutoka Bunju  ni 5km

Bei ya kila ekari moja ni tsh 20 mil fixed.

Call 0758603077


Share:

Waziri Ummy: Tanzania Haina Mgonjwa Wa Corona

Na. WAMJW-Dodoma
Mpaka sasa Tanzania haina Mgonjwa wala muhisiwa wa ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha Coromna (Hona kali ya mafua) hata hivyo kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo hasa kibiashara na kijamii kati ya Tanzania na nchi za bara la Asia ikiwemo nchi ya China nchi inakuwa katika hatari pia ya ugonjwa huo.

Haya yamesemwa jana na Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa tarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugponjwa huo jijini hapa.

“Ugonjwa huu unasababiswa na kirusi jamii ya Corona na ni kipya “Novel (New) Corona virus 2019” (2019-nCOV) ambacho ni tofauti na virusi vingine vya jamii hiyo ambavyo viliwahi kusababisha milipuko ya ugonjwa uliojulikana kama ‘SARS-CoV’ mwaka 2003 na MERS-CoV Corona Virus mwaka 2013”.Amesema Waziri Ummy.

Aidha, waziri Ummy amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya hewa kwa kuingiwa na majimaji yenye virusi kutoka mtu mmoja kwa njia ya kukohoa au kupiga chafya au kwa kugusa majimaji au makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na dalili za ugonjwa huo na dalili huanza kuonekana kati ya siku moja hadi kumi na nne tangu kupata maambukizo.

Hata hivyo ametaja dalili za ugonjwa huu ni pamoja na Homa, mafua, kuumwa kichwa, mwili kuchoka, kikohozi, kubanwa mbavu, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, mapafu kuathirika, kupumua kwa shida na hata kifo.

“Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja, hivyo kama yalivyo magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi, matibabu hufanyika kwa kuzingatia dalili zilizopo na ufuatiliaji wa karibu” Amesisitiza Waziri Ummy.

Wakati huo huo waziri huyo amewashauri wananchi kuchukua hatua ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuzingatia kanuni za afya na usafi ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na mtu mwenye dalili za mafua mwenye historia ya kusafiri katika nchi zilizokumbwa na mlipuko na kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kitambaa safi au nguo uliyovaa sehemu za mikono

“Kutokana na mwenendo na kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huo kipindi hiki cha mlipuko, Wizara inashauri kusubiri na kuepuka safari zisizo za lazima kwenda kwenye maeneo yaliyoathirika na inapolazimu kusafiri basi


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi January 30



















Share:

Wednesday, 29 January 2020

Global Health & Social Medicine International Postgraduate Scholarship At King’s College London, UK

Scholarship Description: Global Health & Social Medicine International Postgraduate Scholarship at King’s College London, UK is open for International Students The scholarship allows Postgraduate level programm(s) in the field of All Subjects, Global Health taught at King’s College London The deadline of the scholarhip is 31 Mar 2020. Degree Level: Global Health & Social Medicine International Postgraduate Scholarship… Read More »

The post Global Health & Social Medicine International Postgraduate Scholarship At King’s College London, UK appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Australia Awards Scholarships

Scholarship Description: Australia Awards Scholarships, formerly known as Australian Development Scholarships (ADS), provide opportunities for people from developing countries, particularly those countries located in the Indo-Pacific region, to undertake full time undergraduate or postgraduate study at participating Australian universities and Technical and Further Education (TAFE) institutions. Universities Participating:  Many universities from Australia participate in this program you can… Read More »

The post Australia Awards Scholarships appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

DC MACHA ABAINI DANGURO LA BIASHARA YA NGONO LINALOMILIKIWA NA KIGOGO WA CCM KAHAMA MJINI

Jengo la  Bijampola lililoungana na vyumba vya kulala wageni


Na Mwandishi wa Malunde 1 blog Kahama
Imebainika kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Wilaya ya Kahama Sipilaus Bijampola anamiliki nyumba bubu ya kulala wageni maarufu kama Danguro huku nyumba hiyo ikitumiwa na wanawake kwa biashara haramu ya ngono. 

Uwepo wa jengo hilo umebainika jana Januari 28,2020 wakati na mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, Anamringi Macha alipofanya ziara ya kushtukiza ili kuhimiza suala la usafi katika nyumba mbalimbali za kulala wageni pamoja na kumbi za starehe. 

Ziara hiyo ililenga kufanya ukaguzi katika vyumba mbalimbali wanakolala wanawake hao pamoja na kuzungumza nao ili kujua zaidi shughuli walizonazo ikiwa ni pamoja na kuwasisitiza kufanya usafi vyumbani mwao.

Akiendelea na zoezi la ukaguzi, Macha alishangazwa na kitendo cha vyumba katika nyumba ya kulala wageni inayomilikiwa na Sipilaus Bijampola iliyopo Kata ya Nyihogo Mjini Kahama kukithiri kwa uchafu huku vikitoa harufu mbaya.

"Mazingira niliyokuta hayakuwa rafiki na yanatia mashaka kuwa hilo ni Danguro,vyumba vinadaiwa kuwa ni Guest house ni vichafu,ukaaji wa mule ndani ya vyumba,haukuturidhisha, ulitutia mashaka kuwa ni sehemu panapofanyika biashara haramu,biashara za kihuni",amesema Macha. 

DC Macha alieleza kukerwa na kitendo cha biashara haramu kama hiyo pamoja na uchafuzi wa mazingira kuendeshwa na kiongozi ngazi ya chama kinachoongoza Serikali, na kutumia fursa hiyo kuziagiza Mamlaka zinazohusika kutembelea nyumba hiyo ili kujiridhisha na uhalali wa Biashara hiyo pamoja na uchafu huo iwapo itabainika kuendeshwa kinyume na utaratibu wa serikali hatua za kisheria zichukuliwe.

“Kwa kweli ni kitendo cha ajabu sana kama biashara hii inafanyika na mamlaka zinazohusika zipo vyumba ni vichafu, Vinatoa harufu mbaya na binadamu wanaishi katika nyumba hii naagiza mamlaka zinazohusika wafike hapa kuchunguza ili kubaini ukweli lakini suala la usafi maafisa wapo, kama kuna ukiukwaji wa sheria hatua zichukuliwe,” amesema Macha.

"Nilimpigia simu mmiliki Sipilaus Bijampola na kumuonya nikimtaka azingatie sana suala la usafi ndani na nje ya nyumba hiyo inayosemekana kuwa ni Gesti bubu ili kuepuka maradhi yatokanayo na uchafu. na pia nilimuagiza Bwana Afya wa halmashauri ya Mji Kahama amwelekeze mmiliki wa nyumba hiyo afanye marekebisho",ameongeza.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba akizungumza jana na waandishi wa habari ofisini kwake alikiri Bijampola kubainika na makosa mbalimbali ya ukwepaji wa kodi ya Serikali likiwemo la uchafu na kuongeza kuwa hivi karibuni alipigwa faini na kulipa kiasi cha shilingi 800,000 kwaajili ya uchafuzi wa mazingira.

“Kumbukumbu zangu zinaonyesha tulienda Umbwe gest house tulimpa leseni lakini tulipofanya ukaguzi baadaye tulikuta Danguro tukamfungia, tulipoendelea na ukaguzi huo tulienda Bijampola tukakuta naye anamiliki Dangulo pia tukamfungia na kila ukaguzi tukibaini hayo tunachukua hatua ya kuwafungia,” alisema Anderson Msumba na kuongeza.

“Licha ya agizo la mkuu wa Wilaya kuzitaka mamlaka kufika katika maeneo hayo sisi kama Halmashauri tunaendelea na ukaguzi na kubaini wanaokiuka sheria, Bijampola anapaswa kufanya biashara zake kwa kufuata misingi ya sheria zilizopo na sisi Halmashauri tunaendelea kuzisimamia, Tulienda tukakuta pachafu na kukiuka sheria kwa mujibu wa leseni tukamsitisha na kumtoza faini na tuendelea kufungia madanguro,”

Hata hivyo Mkurugenzi wa baa ya Bijampola na nyumba hiyo ya kulala wageni Sipilaus Bijampola akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu   yake ya kiganjani akiwa mjini Shinyanga akiendelea na vikao alikili mkuu wa Wilaya kufika katika eneo la biashara zake.

“Hayo ni mambo madogo madogo suala la Dangulo haliwezi kufuta biashara zangu na wala sibabaishwi na Waandishi wa Habari kama Benki ya NMB walipiga mnada lakini na bado mmiliki ni mimi, mimi sina cha kusema zaidi mwandishi wa Habari”.

Licha ya nyumba hiyo ya kulala wageni  kudaiwa kuwa inatumika kuendesha biashara haramu ya ngono, biashara hiyo imezidi kushamiri na kufanyika wazi wazi katika maeneo mengi ya wazi na yale yenye mkusanyiko mkubwa wa watu katika Halmashauri ya Mji wa Kahama licha ya mamlaka husika kukemea vitendo hivyo mara kwa mara.
Share:

CLINIC NURSE/COUNSELORS – 6 posts at Management and Development for Health (MDH)

Management and Development for Health (MDH) is a non-profit organization in Tanzania contributing to address public health priorities. MDH works with the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children (MOHCDGEC); President’s Office Regional Authorities and Local Government (PORALG); as well as academic and nonacademic institutions to address the problems of Tuberculosis, Malaria, HIV/AIDS, Nutrition, Maternal and… Read More »

The post CLINIC NURSE/COUNSELORS – 6 posts at Management and Development for Health (MDH) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Medical Officers (3) and Clinical Officer (3) at Management and Development for Health (MDH)

Management and Development for Health (MDH) is a non-profit organization in Tanzania contributing to address public health priorities. MDH works with the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children (MOHCDGEC); President’s Office Regional Authorities and Local Government (PORALG); as well as academic and nonacademic institutions to address the problems of Tuberculosis, Malaria, HIV/AIDS, Nutrition, Maternal and… Read More »

The post Medical Officers (3) and Clinical Officer (3) at Management and Development for Health (MDH) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Beverage Manager at Serengeti

Beverage Manager (Tanzanian Only) Serengeti This position is for a Tanzanian and we can not accept any other applicants. Please only apply of you are Tanzanian.Based at the Lodge in Serengeti National Park, you should be comfortable with remote living.We can not accommodate families however you will have leave every 11 weeks to go home. This job entails;… Read More »

The post Beverage Manager at Serengeti appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Vcancies at BAGAMOYO District Council

Job Descriptions Job Vcancies at BAGAMOYO District Council. Read carefully all currently available jobs descriptions by downloading PDF File attached. DOWNLOAD PDF FILE)

The post Job Vcancies at BAGAMOYO District Council appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HUYU NDIYO SIRI YASINI KIONGOZI MAHIRI MWANAMKE ALIYETUMIKIA VYAMA VYA SIASA MIAKA 25 SASA…KATANGAZA KUNYAKUA JIMBO LA SHINYANGA MJINI 2020

Bi. Siri Yasini Swedi

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 
Kujiamini ndiyo silaha kubwa kwa mwanamke kufanikiwa katika masuala ya uongozi!!! Hii ni kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha ACT Walazendo mkoa wa Shinyanga Bi. Siri Yasini Swedi aliyetumikia uongozi katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo mkoani Shinyanga kwa kipindi cha miaka 17 na sasa ni Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo mkoa wa Shinyanga tangu mwaka 2015. 

SIRI YASINI SWEDI NI NANI? 

Siri Yasini Swedi ni mama mwenye watoto wanne,ameolewa alizaliwa mwaka 1974 katika kata ya Kambarage halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. 

Siri Yasini alianza kujihusisha na masuala ya siasa mwaka 1998 akiwa binti wa miaka 24. 

Anasema mwaka 1998 akiwa mfanyabiashara wa mihogo na nafaka katika soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiwa katika harakati za kutafuta wanachama,alishawishiwa kuwa mwanachama wa CHADEMA akakubali na ndiyo safari yake katika masuala ya siasa ilipoanzia. 

Siri Yasini anasema baada ya kuwa mwanachama,mwaka huo huo 1998 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA)wilaya ya Shinyanga hadi mwaka 2000. 

“Ukishakuwa Mwenyekiti wa wilaya unakuwa Mjumbe wa Baraza Kuu CHADEMA na Mjumbe wa Mkutano Mkuu CHADEMA taifa”,anaeleza Siri Yasini. 

“Nikiwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga, Mwaka 1999 wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa nilichaguliwa kuwa Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Tanesco kata ya Chamaguha katika Manispaa ya Shinyanga kupitia CHADEMA. Wakati huo kulikuwa na shida kidogo kwani chama kilikuwa bado kidogo na watu walikuwa hawakielewi elewi. 

Nilitumikia nafasi ya ujumbe wa serikali ya mtaa hadi mwaka 2004”,anasimulia Siri Yasini. 

“Mwaka 2000 kwenye uchaguzi Mkuu wa CHADEMA,nilifanikiwa tena kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga.Tuligombea wanne ambapo wanaume walikuwa watatu,mwanamke nilikuwa peke yangu,nikashinda.Nimeitumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2005”,anasema Siri Yasini. 

Anabainisha kuwa hata kwenye uchaguzi mkuu wa CHADEMA mwaka 2005 aligombea tena nafasi hiyo akichuana na wanaume wawili kutokana na uimara wake katika masuala ya siasa akachaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga kwa miaka mitano mingine hadi mwaka 2010. 

Mnamo mwaka 2010 Siri Yasini aliingia kwenye Kinyang’anyiro cha Udiwani kwenye kura za kuchaguliwa ndani ya chama kata ya Chamaguha akapata nafasi ya pili akigombea na wanaume wawili na baada ya kushindwa akateuliwa kuwa Diwani wa Viti Maalumu kata ya Chamaguha mpaka mwaka 2015. 

Hata hivyo baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga Philip Shelembi mwaka 2011 Siri Yasini aliteuliwa kushikilia nafasi ya Mwenyekiti mkoa kwa muda hadi muda wa uchaguzi alipochaguliwa mwenyekiti mwingine. 

Mwaka 2015 Siri Yasini alihama CHADEMA na kwenda Chama Cha ACT Wazalendo na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho cha ACT Wazalendo nafasi ambayo anaitumikia mpaka sasa. 

NINI SIRI YA SIRI YASINI KUFANIKIWA KUWA KIONGOZI WA KISIASA MWANAMKE KWA MUDA WA MIAKA 25 MFULULIZO? 

Siri Yasini anasema licha ya kubezwa kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi,kitu cha msingi alichokisimamia yeye kama mwanamke na hatimaye kufanikiwa katika uongozi wa kisiasa ni kujiamini na kutofanya kazi kinadharia. 

“Siasa inaongozwa na katiba.Kwa hiyo ni vizuri sana ukaielewa Katiba na Ilani ya Uchaguzi ya Chama chako cha siasa. Unapoenda kwenye majukwaa yako ni vyema pia ukapitia katiba ya Nchi, na kupitia vitu vinayoleta shida ndani ya nchi ama kwenye eneo unalotaka kugombea uongozi. Lazima ujue vitu vya kila siku ambavyo unaishi navyo ndipo utajiamini. 

“Unapoenda kusema kitu usiseme kwa kufikiri,jaribu kukifanyia utafiti kwanza uone kama kina ukweli ndani yake au la! Halafu ndiyo nenda ukaseme. Ukweli ndiyo utakufanya ujiamini. Usipojiamini anaweza kutokea mtu akakuuliza kitu kidogo tu ukababaika. 

Usikae sehemu moja ukajifungia maana yake hautajua changamoto kwani chama cha siasa hususani cha upinzani kinaangalia changamoto ambazo zipo ndani ya serikali inayoongoza.Ni vizuri ukafuatilia hizo changamoto ukaujua ukweli. Fanya utafiti, ujiridhishe vinginevyo wananchi watakushangaa kuzungumzia vitu ambavyo havipo kwenye eneo lako”,anafafanua Siri Yasini. 

Kuhusu Matumizi ya pesa nyingi ili kufanikiwa katika siasa, Siri Yasini anasema: 

“Kwa kweli katika nafasi za uongozi nilizopitia sijatoa pesa kabisa. Nilikuwa nasimama na kunadi sera zangu na nikapewa kura licha ya maneno mengi mtaani ‘Mwanamke hana hela atakuwa malaya,wakubwa hawatamuacha’. Siasa ina maneno mengi sana ya kukatisha tamaa,Huwezi kumzuia mtu kusema. Mimi nilikuwa naujua ukweli wangu ni nini,nilisimamia ukweli wangu ndiyo maana nilifanikiwa kusimama mpaka hapa nilipo leo”,amesema Siri Yasini. 

CHANGAMOTO GANI KAPITIA? 

Siri Yasini anasema changamoto kubwa aliyopitia ni kubezwa ambapo jamii ilimbeza sana ambapo wengine walibeza umri wake mdogo (umri miaka 24) kupewa dhamana ya kuongoza chama. 

“Changamoto zingine zinakuwa ndani ya chama,wapinzani unaogombea nao nafasi za uongozi.Kuna wengine wanaamua kukuchafua tu na kipindi hicho nilianza uongozi nikiwa binti mdogo umri wa miaka 24.Kipindi hicho vijana wachache walikuwa wanapata nafasi za uongozi. 

Wengine walikuwa wanasema ‘mmempa huyu binti uongozi atakiharibu chama’ lakini mwisho wa siku wakiangalia utendaji kazi wako inabidi tu wakubaliane na wewe. Kuna maneno mabaya kabisa ambayo kwa kweli hayaleti picha nzuri”,amesema Siri Yasini. 

RAI YA SIRI YASINI KWA WANAWAKE 

Siri Yasini anawasisitiza wanawake wanaotaka kugombea nafasi za uongozi kuacha kuoga,wajiamini na kupuuza wanaowabeza kwani Uongozi ni Busara, Akili wala siyo Misuli akibainisha kuwa wanaume sasa wanawafurahia wanawake wachapakazi na wanaojiamini ndiyo maana yeye amekuwa kiongozi Mwanamke ndani ya CHADEMA na ACT Wazalendo na wanaume na wanawake wanapenda utendaji kazi wake ndiyo maana hadi sasa ni kiongozi. 

“Kutokujiamini kuna mambo mengi ikiwemo kuwaza kuwa mimi nikienda nani ataniunga mkono ‘nani atani sapoti’ sina hela mkononi,nitasimamaje jukwaani na mambo mengine mengi ambayo yanamsababisha hata hamu ya kugombea inafifia.Hutakiwi kuwaza hayo unachotakiwa kuwaza ni kuona unaweza kufanya nini kwa sababu unajiamini”,amesema. 

Hata hivyo anasema mila na desturi za kwamba mwanamke hawezi kuongoza zimepitwa na wakati kwani sasa jamii ina uelewa na wanawake viongozi wanapewa heshima kama wanavyopewa wanaume na wanawake viongozi wamekuwa na mashabiki wa kike na wa kiume. 

“Uoga ni tatizo kubwa sana kwa wanawake kutothubutu kugombea nafasi za uongozi. Uoga mwingine unatokana na kubezwa kuanzia ndani ya familia,wanawake wengi wanakatishwa tamaa ndani ya familia zao. 

Hata mme wako anaweza kukubeza lakini ukisimama vizuri huyo atakuwa shabiki wako namba moja na atakusaidia kushawishi na kukutafutia kura kwa wanaume wenzake na jamii kwa ujumla. Hakuna mtu anamuunga mkono mtu muoga, hivyo wanaotaka uongozi wasiwe waoga wajiamini”,anasema Siri Yasini. 

NINI USHAURI WA SIRI YASINI KWA JAMII? 

Siri Yasini anaiomba jamii kuwapa ushirikiano ‘sapoti’ wanawake kwa sababu kwanza wanawake wanaweza kufanya mambo makubwa. 

“Kupitia mimi nimeona wanawake wanafanya mambo makubwa.Nikiwa Mwenyekiti wa CHADEMA hapa wilaya ya Shinyanga Mjini nilikuta wenyeviti wa vitongozi wawili mmoja alikuwa Negezi Mwawaza na mwingine Mpera A Ibadakuli,lakini baada ya kuwa kiongozi ndani ya miaka mitano nikapata viongozi wanawake zaidi ya 20 na katika uongozi wangu hatujawahi kushuka,wanawake wameendelea kujitokeza kugombea nafasi za uongozi hadi ngazi ya Udiwani na Majimbo na mimi nikiwa mfano wao”,amesema Siri Yasini. 

Siri Yasini anaishukuru jamii sasa kwa kuendelea kuwaamini na kuwapa nafasi za uongozi wanawake tofauti na siku za nyuma ambapo wanawake walikuwa hawapewi nafasi za uongozi akidai kuwa hata yeye wakati alipopewa nafasi kuongoza CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini jamii ilikuwa inamshangaa na kuona kama jambo la ajabu mwanamke kuongoza jamii. 

“Siku za nyuma ilikuwa changamoto,wanaume walikuwa wanashangaa sana kuniona mwanamke napanda jukwaani,walikuwa wanashtuka sana kusikia sauti ya mwanamke kwenye majukwaa ya siasa.Wengine walikuwa wanakuja kwenye mikutano kunishangaa tu nikiwa jukwaani. Mwanamke anasimamaje Jukwaani? Walikuwa wanawaza kuwa mwanamke hawezi. Walivyonisikiliza na kunielewa wakanikubali na wakawa mashabiki zangu”,anasimulia Siri Yasini. 

WITO WA SIRI YASINI KWA WANAWAKE WANAOTAKA UONGOZI. 

Siri Yasini anawaomba wanawake wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi za uongozi (Udiwani,Ubunge na Urais) katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka huu 2020. 

“Mwanamke anaweza kuwa diwani mzuri kabisa,anaweza kuwa Mbunge mzuri na akaongoza Jimbo lake vizuri kabisa.Tunaona kuna wabunge wengine majimbo yao yamewashinda lakini nafasi hiyo akipewa mwanamke mabadiliko makubwa lazima yaonekane”,amesema Siri Yasini. 

“Nawasihi wanawake wajitokeze kuchukua fomu kugombea nafasi za uongozi katika Jimbo la Shinyanga Mjini. Natamani angetokea mwanamke mwenye uwezo,anayejitambua,mwenye kuweza kutetea na kujenga hoja vizuri.

Naomba wananchi wa Shinyanga wafanye hivyo kwani haijawahi kutokea Mwanamke kuwa kiongozi wa jimbo ni vizuri safari hii tukaamua kubadilisha tuweke mwanamke ili tuweze kutoka hatua moja kwenda nyingine.Wachukue fomu na watafanikiwa. 

Mwanamke akishika nafasi huwa panaonekana kweli pameshikwa .Mwanamke ni mtu anayejituma,mwanamke ni mtu mwenye misimamo,ni mtu mwenye nidhamu siyo nidhamu ya uoga,ana nidhamu ya kitu anachokifanyia kazi”,anaeleza Siri Yasini. 

Amesema Chama Cha ACT Wazalendo kimejipanga vizuri katika chaguzi zake za ndani na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 na kwamba agizo kubwa la Chama ni kuhakikisha wanawake wengi wanachukua fomu za kugombea za uongozi na tunaendelea kufanya mikakati ya kuwafikia wapiga kura na kuwaeleza kuwa mwanamke anao uwezo wa kuongoza vizuri. 

“Katika chama chetu cha ACT Wazalendo tunaendelea na mkakati mkubwa wa kuhamasisha wanawake kugombea nafasi za uongozi na nyinyi vyombo vya habari ni sehemu ya sauti yetu kutushika mkono ili tufikie malengo yetu tunayoyafikiria”,amesema. 

NDOTO YAKE NI NINI 2020? 

Siri Yasini ambaye amekuwa kiongozi wa vyama vya siasa kwa takribani miaka 25 sasa, anasema ndoto yake kubwa mwaka 2020 ni kugombea Ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini na anawaomba Watanzania kumuunga mkono pindi muda utakapowadia kwani uwezo wa kuongoza anao na anajiamini. 

Septemba 27,2019, TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Taasisi ya Women Fund Tanzania na Mtandao wa Wanawake na Katiba,Uchaguzi na Uongozi ulizindua Ilani ya Uchaguzi ya Wanawake ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020. 

Ilani ya uchaguzi ya wanawake ya mwaka 2019/2020 imeweka masuala muhimu ya jinsia katika uchaguzi na inazitaka mamlaka zote kuzingatia masuala ya jinsia katika uchaguzi. 

Ilani hiyo pia inataka wadau wote wa uchaguzi kuzingatia misingi ya ushindani wa haki na huru na usawa wa jinsia kama ilivyoainishwa kwenye katiba,sheria,sera,mipango ya nchi na kubainishwa kwenye mikataba ya kimataifa na kikanda ambayo serikali yetu imeridhia. 

Share:

Head; Channels Services & Systems Support at NMB Bank

Head; Channels Services & Systems Support   Job Purpose Driving technology alternative channels roadmap and strategy for all digital self-services, agency network, cards settlement, remittance and payments systems to ensure high and sustainable channels systems performance, SLAs and integration of channels systems with internal and third parties systems. Main Responsibilities Responsible for managing NMB second level support teams for… Read More »

The post Head; Channels Services & Systems Support at NMB Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Quality Assurance Engineers at Vodacom

Quality Assurance Engineer 2 Posting Country:  Tanzania, United Republic of Date Posted:  28-Jan-2020 Full Time / Part Time:  Full Time Contract Type:  Permanent Joining Vodacom is more than a job, what we do matters. We don’t just carry minutes, texts and data – we carry people’s lives. And that’s a huge responsibility. If you think for a minute about… Read More »

The post Quality Assurance Engineers at Vodacom appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Kamati Za Usimamizi Wa Maafa Mikoa Ya Mradi Bomba La Mafuta Zashauriwa Kuuweka Mradi Kwenye Mpango Wa Kujiandaa Na Kukabiliana Na Maafa.

Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, imezishauri Kamati za Usimamizi wa Maafa katika  mikoa 8 na vijiji 184  vinavyopatikana   katika wilaya 24 zilizopo katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, ambapo Mradi wa Bomba la Mafuta utatekelezwa kuuweka Mradi huo katika Mipango yao ya kujiandaa na kukabiliana na Maafa ili kuhakikisha mradi huo hauthiriwi na majanga yanayoweza kutokea.

Kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha majukumu ya  kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutoa taarifa za tahadhari ndani ya eneo husika, Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji  wilaya au mkoa, pamoja na kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika.

Akiongea mara baada ya kutembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa, Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amefafanua kuwa Kamati za maafa zinalo jukumu la kuchukua tahadhari ya namna ya kuhakikisha majanga yanayoweza kuuathiri mradi huo yanakuwa katika mipango yao ya menejimenti ya maafa ili faida zitakazotokana na utelelezaji wa mradi huo zinakuwa endelevu.

Kwa upande wake,  Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Noel Kazimoto ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo utafungua fursa za kiuchumi kwa watanzania hivyo ni dhahiri kuwa eneo la Chongoleani litakuwa na mwingiliano mkubwa wa watu na shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii zitakuwa zikiendeshwa, kwa kuwa wananchi ni wadau wa menejimeti ya maafa kupitia kamati za menejimenti  za maafa kuanzia ngazi ya vijiji, wataendelea kuelimishwa juu ya majanga  yanayoweza kuuathiri mradi huo ili waweze kuhakikisha mradi unakuwa endelevu.

Kwa mujibu wa Tovuti rasmi ya Kampuni inayojenga mradi huo, East African Crude Oil Pipeline www.eacop.com. Kampuni hiyo inabainisha kuwa wanao mpango unaohakikisha utelezaji wa mradi huo unazingatia majanga na maafa wakati wa kupanga, kujenga na kuendesha Bomba, ambapo Mpango huo unahakikisha kwamba, katika tukio la dharura linaloweza kutokea, hatua za haraka, zinachukuliwa.

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi unatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikisha kampuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikali za Tanzania na Uganda. Mafuta ghafi yatasafirshwa kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. Mradi wa Bomba hilo una umbali wa kilometa 1,445 ambapo kilometa 298 zitakuwa nchini Uganda, na kilometa 1,147 zitakuwa nchini Tanzania.

MWISHO.


Share:

Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya Sheria Ndogo Kusikiliza Maoni Ya Wadau Jan, 31 ,2020.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo imepanga  kufanya mkutano  wa kusikiliza Maoni ya wadau [Public Hearing ]kuhusu Muswada wa sheria wa usuluhishi ya Mwaka  2020[The Arbitration Bill 2020] kwa mujibu ya kanuni  ya 84[2] ya kanuni za kudumu za Bunge,Toleo la Januari ,2016,ambapo Muswaada huo umesomwa  kwa mara ya kwanza   Bungeni tarehe 28,Januari,2020.

Katika taarifa iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano  na Uhusiano wa kimataifa  ofisi ya Bunge Januari 28,2020  jijini Dodoma imefafanua kuwa mkutano huo wa kusikiliza maoni ya wadau[Public Hearing ]utafanyika siku ya Ijumaa  tarehe 31,Januari,2020 saa saba mchana  katika ukumbi Na. 229 jengo la Utawala Bungeni jijini Dodoma.

Aidha,katika taarifa ya kitengo hicho cha Mawasiliano na Uhusiano wa kimataifa Ofisi ya Bunge imeendelea kufafanua kuwa ,kwa kuzingatia umuhimu wa muswada huo ,kamati inawaalika wadau wote  kufika na kuwasilisha maoni  ya wadau ambapo pia Maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa   kwa barua pepe cna@bunge.go.tz  na muswada  unaweza kupakuliwa kupitia   www.parliament.go.tz.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger