Monday, 28 April 2014

ROSE NDAUKA "NDOA YANGU SOON!"




MSANII maarufu wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka amesema kuwa watu wasiwe na wasiwasi kwani kwa mipango ya Mungu atafunga ndoa na mzazi mwenzake Maliki Bandawe hivi karibuni.

“Si muda mrefu mambo yatakuwa mazuri tulikuwa tunaendelea kujuana, nadhani sasa tunafahamiana vizuri hivyo watu wasiwe na shaka, tutafunga ndoa soon,” alisema.

Rose ambaye hivi karibuni alihamasisha zoezi la usafi na kuungwa mkono na wasanii mbalimbali akiwamo Meya wa Ilala Jerry Slaa, alisema watu wasihofu kuhusu ndoa hiyo kwani ipo njiani.

“Hatujui labda kuchelewa kwetu kuna kitu Mungu amekiepusha, siku zote haraka haraka haina Baraka,” alisisitiza Ndauka ambaye amepanga kutembea Tanzania nzima kuwahamasisha wananchi kuzingatia usafi.
Share:

DIAMOND ANATAFUTWA CHINA,KISA MADAWA YA KULEVYA


 
STAA  wa  muziki  wa  bongo  fleva  nchini, Abdul  Nassib  "Diamond"  ametakiwa  kutokanyaga  kabisa  nchini  China  na  kwamba  akitokeza  pua  yake  nchini  humo  asahau  kabisa  kurudi  uraiani... 

Hiyo  inafuatia  kijana  mmoja  mtanzania  kukamatwa  wiki  iliyopita  uwanja  wa  ndege  wa   Macau   China  na  kudai  kuwa  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania....

Habari  kutoka  Macau  China  zinadai  kuwa  kijana  huyo  aliyejulikana  kwa  jina  moja  la  Manyota  alikamatwa  akiwa  kwenye  harakati  za  kuingiza   mzigo  huo  wa  dawa  za  kulevya  kwa  kupitia  uwanja  wa  ndege  wa  Macau....

Kwa  mujibu  wa  vyanzo  vyetu  vya  habari, inaarifiwa  kuwa  Manyota  alikamatwa  Alhamisi  ya  wiki  iliyopita  katika  uwanja  uleule  aliokamatwa  mtanzania  mwingine  Jackline  Patrick, anayesotea  rumande  mpaka  hii  leo  huko  huko  Macau  China.....

Kijana  mmoja  wa  kitanzania  anayefanya  shughuli  zake  huko  China  amedai  kuwa  Manyota  alikamatwa  na  maofisa  wa  usalama  wa  uwanja  wa  ndege  na  katika  utetezi  wake  alidai  kuwa  yeye  ni  mwanamuziki  toka  Afrika  Mashariki...

Mtanzania  huyo  aliendelea  kudai  kuwa, Manyota  baada  ya  kukamatwa  alianza  kubabaika  kwa  kujifanya  mwanamuziki  na  baadae  akadai  kuwa  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania....

"Alijifanya  yeye  ni  mwanamuziki, baadae  akabadilika  na  kudai  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania  na  kwamba  ndani  ya  ule  mzigo  alikuwa  hajui  kuna nini  zaidi  ya  kuombwa  na  jamaa  zake  wa  Dar  awapelekee  nchini  China"...Alisema  mtanzania  huyo

Inasemekana  kuwa, ili  kujiridhisha, maofisa  hao  wa  usalama  wa  uwanja wa  ndege    walimtaka  kijana  huyo  aoneshe  moja  ya  kazi  zake  na  yeye  akaishia  kuwaonesha  moja  ya  video  za  Diamond  kupitia  mtandaoni  na  kumuonesha  mmoja  wa  wacheza  shoo  wa  mwanamuziki  huyo  kuwa  ndo  yeye  Manyota...

Inasemekana  kuwa, pamoja  na  utetezi  wake  huo  ambao  unaweza  kumuingiza  matatani  Diamond,maofisa  hao  wa  usalama  walishndwa  kumuelewa  na  kumtupa  ndani.....


Mtanzania  huyo  alihitimisha  kwa  kudai  kuwa, kutokana  na  mazingira  yalivyo,ni  vyema  mwanamuzi  Diamond  akawa  makini   sana  kama  atakuwa  na  safari  za  kwenda  China  kwani  kwa  namna  moja  ama  nyingine  jina  lake  limewekwa  kwenye  orodha  ya  majina  machafu   na  wanaweza  kumkamata  kwa  lengo  la  kuujua  ukweli....
Share:

BASI LA RATCO LAPATA AJALI KIBAHA, PWANI


 Wananchi wakitoka kwenye gari kupitia madirishani.
 Aha! kila mmoja akichomoka kujiokoa bila kusahau kipimajoto mkononi...
Basi la RATCO linalofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Tanga limepata ajali eneo la Kibaha, Pwani leo jioni Aprili 27, 2014.

Kwa mujibu wa shuhuda aliyefika eneo la tukio alisema gari hilo lilipinduka ubavu baada ya kuacha njia.

Endelea kuungana paparazihuru... 
Tunaendelea na uchunguzi, utapata habari zaidi badaae. 
Share:

BATULI AKUBALI KUIGIZA NUSU UTUPU

MWANADAFADA mkali wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa kwa sasa yupo tayari kuigiza nusu utupu kwa sinema za nje ya nchi.
Mwanadafada mkali wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Akipiga stori mbili-tatu na kona hii, Batuli alisema kuwa muvi nyingi Bongo huwa zinafungiwa kwa kukosa maadili na kwamba kama ikitokea nafasi akaitwa nje ya nchi kuigiza sini hizo, atakuwa tayari.
“Zamani nilikuwa nikiogopa kuigiza nusu utupu. Wenzetu Nigeria wameendelea na ndiyo maana wanaigiza hata nusu utupu, kama itatokea nafasi ya kuigiza huko (nje ya Bongo) nusu utupu, nipo tayari,” alisema Batuli.
Share:

NAY WA MITEGO ASAKWA KWA KUTISHIA KUUA

KIMENUKA! RB namba KT/RB/1178/2014-KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA MTANDAO inamsaka staa wa Ngoma ya Nakula Ujana, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa tuhuma ya kutishia kumuua mdogo wake aliyetajwa kwa jina la Amani Shija, Ijumaa Wikienda limeinyaka.
Staa wa Ngoma ya Nakula Ujana, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Nay alikuwa akiishi na Shija kwa zaidi ya miaka mitano nyumbani kwake, Manzese jijini Dar.
Habari zilitonya kuwa ugomvi wa Nay na Shija ulianza zaidi ya miezi mitatu iliyopita ambapo hivi karibuni walikuwa maeneo ya Kijitonyama, Dar, wakipata chakula cha usiku na marafiki zao wengine ndipo ghafla dogo akajichanganya na kujikuta akiropoka neno lililomuudhi Nay, akapaniki.
Ilisemekana kwamba baada ya kupaniki, Nay alianza kumfokea Shija na kutishia kumuua, ambaye alishindwa kujizuia na kujikuta akimwaga chozi.
Akaendelea kueleza kuwa hata baada ya siku hiyo, Nay aliendelea kumtumia SMS za kutishia kumuua ambazo bado anazo kama ushahidi Baada ya kudaka mchongo huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shija ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva na kumuuliza juu ya malalamiko hayo, akakiri kugombana na kaka yake huyo.
Alikwenda mbele zaidi na kudai kuwa Nay amekuwa akiendelea kumtishia kumuua jambo linalomfanya aishi kwa shaka mjini.
Alisema ili kujilinda ndipo alipoamua kulifikisha suala hilo kwenye Kituo cha Polisi Kitunda, Dar anakoishi kwa sasa kisha kufunguliwa jalada la kesi namba KT/RB/1178/2014 KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA MTANDAO.
Gazeti hili lilimtafuta Nay bila mafanikio lakini kwa mujibu wa mtu wake wa karibu, baada ya kujua msala huo ametorokea nchini China.
-GPL
Share:

MKE NUSURA APEWE TARAKA BAADA YA MUME KUTUMIWA PICHA ZA MKEWE BBM NA RAFIKI YAKE,...



Share:

JOKATE, NATURE NDANI YA BIFU KUBWA

PASUA jipu!  awili wenye majina makubwa Bongo, mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Juma Kasim ‘Juma Nature’ wanadaiwa kuacha mshangao kwa wasanii wenzao baada ya kutifuana, Ijumaa Wikienda limeng’atwa sikio.
Mkali wa Bongo Fleva, Juma Kasim ‘Juma Nature’.
Pamoja na kwamba Nature amekuwa akizuga kutomaindi lakini habari za kushangaza zilidai kwamba mkali huyo wa Temeke amekuwa akimtuhumu mwanadada huyo kuwa amemuibia wazo lake la biashara ya ndala au kandambili.
Kabla ya madai haya mapya, Nature aliwahi kunukuliwa redioni wakati akitambulisha wimbo wake mpya wa Chuma Ulete kuwa yupo mbioni kuingiza bidhaa hiyo sokoni.
Madai ya sasa yanaeleza kwamba Nature amekuwa akilalamika kuwa Jokate ‘amekopi’ na ‘kupesti’ wazo lake la biashara.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Pia ilisemekana kwamba Nature amekuwa akimtafuta Jokate ili kuweka suala hilo sawa bila mafanikio.
“Nature amekuwa akimpigia simu Jokate lakini haipokelewi,” kilidai chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa popote hata kwa mtutu wa bastola.
Kwa mujibu wa Nature bado hajabahatika kuziona kandambili za Jokate lakini amekuwa akiambiwa na watu wake kuwa mrembo huyo kamuibia.
NATURE AFUNGUKA
Alifunguka: “Hadi sasa hivi sijabahatika kuziona hizo ndala ila nishaambiwa na watu wangu wengi tu kuwa Jokate ameniibia wazo langu.
“Mimi nasema ni wizi wa ajabu ambao sikutegemea kama Jokate angenifanyia kitu mbaya.
“Kweli sikutegemea kama ishu kama hiyo ingefanywa na mtu kama yeye (Jokate) ila hata kama ametoa mimi wazo langu liko palepale.“Nitakuja kuzitoa tu hizo kandambili zenye picha na jina langu.”
Kandambili zilizosababisha mtifuano.
BOFYA HAPA KUMSIKIA JOKATE
Baada ya kusikia upande mmoja wa Juma Nature, kama ilivyo ada kupata mzani wa habari, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Jokate na kumsomea mashitaka yake hayo ya kuiba wazo la biashara la Juma Nature.
Bila kupepesa macho wala kuchezesha masikio, Jokate alifunguka kwamba kwa upande wake anasikitishwa na mtu kama Nature kumtuhumu kwani ni kati ya watu anaowaheshimu.
Jokate alikwenda mbele zaidi na kueleza kuwa mbali na kumheshimu pia ni kaka yake.
“Wewe siyo wa kwanza kusikia tuhuma hizo kutoka kwa Nature, niliamini baada ya mimi kutoa hizo ndala, atanisapoti kwani mimi niko katika kuendeleza na kutoa ajira kwa vijana wenzangu ili kulisukuma gurudumu letu la maisha.
MASIKITIKO
“Kweli Nature amenisikitisha sana kwa kitendo chake cha kunitangazia ubaya.
“Hata hivyo, siwezi nikaacha kutoa bidhaa zangu, nitaendelea kutoa ‘so’ itabidi tu anisamehe. Kama vipi na yeye atoe za kwake,” alisema Jokate, mmiliki wa lebo ya mavazi ya Kidoti.
MASTAA WANASEMAJE KUHUSU SAKATA HILO?
Wanahabari wetu walizungumza na baadhi ya mastaa ambao walionesha kushangazwa na sakata hilo huku wakihoji kulikoni Jokate na Nature kuhitilafiana wakati kazi zao zinategemeana.
“Unajua msanii kwa msanii kutofautiana kupo tu lakini kwa Nature na Jokate unajua ni watu ambao muda wowote wanaweza kukutana kwa ajili ya kufanya kazi,” alisema mmoja wa wanamuziki wakubwa wa Bongo Fleva.
NATURE KAMGEUKA JOKATE?
Kwa mujibu wa mastaa hao, awali Nature aliposikia Jokate ana ‘aidia’ kama hiyo alinukuliwa akisema freshi tu kwani ni msanii mwenzake hivyo kipato atakachopata kitamsaidia maishani lakini kumbe inawezekana kimoyomoyo ilimuuma ndiyo maana ameendelea kumtuhumu Jokate.
KUTOKA IJUMAA WIKIENDA
Ni vyema Jokate na Nature wakakaa na kukubaliana waifanye biashara hiyo kwa pamoja kwani itawaingizia kipato kikubwa zaidi, ni kiasi cha kuona
Share:

Sunday, 27 April 2014

Some Useful Nokia Codes & How To Format/Reset Ur Phone


SOME OF THESE CODES MIGHT NOT WORK FOR YOUR PHONE CUZ SOME WORK WITH S60 PHONES ONLY AND SOME FOR S60V3.

On the main screen type in
*#06# for checking the IMEI (International Mobile Equipment Identity).
*#7780# reset to factory settings.
*#67705646# This will clear the LCD display(operator logo).
*#0000# To view software version.
*#2820# Bluetooth device address.
*#746025625# Sim clock allowed status.
#pw+1234567890+1# Shows if sim have restrictions.
*#92702689# - takes you to a secret menu where you may find some of the information below:
1. Displays Serial Number.
2. Displays the Month and Year of Manufacture
3. Displays (if there) the date where the phone was purchased (MMYY)
4. Displays the date of the last repair - if found (0000)
5. Shows life timer of phone (time passes since last start)


*#3370# - Enhanced Full Rate Codec (EFR) activation. Increase signal strength, better signal reception. It also help if u want to use GPRS and the service is not responding or too slow. Phone battery will drain faster though.
*#3370* - (EFR) deactivation. Phone will automatically restart. Increase battery life by 30% because phone receives less signal from network.
*#4720# - Half Rate Codec activation.
*#4720* - Half Rate Codec deactivation. The phone will automatically restart
If you forgot wallet code for Nokia S60 phone, use this code reset: *#7370925538#
Note, your data in the wallet will be erased. Phone will ask you the lock code. Default lock code is: 12345
Press *#3925538# to delete the contents and code of wallet.
Share:

All Samsung Hard Reset Codes


[Q]What does a Samsung Hard reset really means?

[Answer] What does a hard reset really means? it means to reset your phone to the settings and features
which were accompanied from the company or at firmware update instant.




There are actually two codes you can use to reset the password and phone setting.
Below are these codes. Type them in the phone and this should solve your problem.

*2767*3855#

and

*2767*2878#

The security code will be reset to 0000.
This will allow you to format the phone easily.

================================================

Here some tutotial how unlock phone, this work on many models:
Follow those steps:

1.)*2767*3855#
2.)*7465625*638*00000000*00000000#
3.)#7465625*638*00000000#


Now your phone is unlock forever Permanent
Share:

Samsung Galaxy Pocket S5300 hard reset



Warning :  by performing the hard reset will erase all fo personal data in internal storage, e.g. contact, message, reminder etc. Please do full backup first.
To perform the hard reset on Samsung Galaxy Pocket GT-S5300, there's two methodes :
- First, input secret code methode : Go to dial pad and type *2767*3855#

- Use recovery mode methode :

  • Turn off the phone
  • Press & hold volume up + home button simultaneously, then power on the phone
  • Release volume up + home button if recovery menu appear
  • Scroll down to factory data reset menu, use volume down to navigate and home button to confirm.
  • Phone will automatically restart and now the phone is on factory state.

 or

 

our device freezes or has fatal errors

If your device freezes or hangs, you may need to close programs or reset the device to regain functionality. If your
device is frozen and unresponsive, press and hold [POWER] for 8-10 seconds, the device will reboot automatically or pull out the battery and then reinsert it. Replace the back cover and power on the device.
Samsung Galaxy Pocket S5300 battery reset


If this does not solve the problem, perform a factory data reset. In Idle mode, open the application list and select
Settings → Privacy → Factory data reset → Reset phone → Erase everything.

or Factory Format by entering S5300 RESET CODE

Use this method to hard reset your Samsung Galaxy Pocket S5300 phone: Enter *2767*3855#. Warning! All your data including contacts, messages etc. will be lost! Copy all your necessary data/Contacts/Messages etc. to SIM or make backup to your PC before full reset! Take out SIM card before full reset.
When disposing of your device, back up all data and then reset your device to prevent misuse of your personal information.





Share:

UKAWA wamjibu Kikwete


ukawa5 eeb08
Na Hudugu Ng'amilo
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) warudi bungeni akidai hawana sababu ya kwenda kushitaki kwa wananchi kwa sababu watawacheka na kuwasikitikia, umoja huo umemjibu wakisema wapo tayari kuchekwa.
Akihutubia vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi, siku moja kabla ya sherehe za miaka 50 ya muungano, Rais Kikwete alisema kuwa huko nje wanakotaka kwenda UKAWA siko na siku yake sio sasa, hivyo akawaomba wasipoteze fursa hiyo muhimu ya kutoa mawazo yao bungeni ili yafanyiwe kazi.
Alisema wananchi hawahusiki wala hawana namna ya kuwasaidia kwani mengi ya hayo yanayowakasirisha ni matatizo waliyoyazusha wao.
Mwenyekiti wa UKAWA, Freeman Mbowe, aliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa
kama Kikwete anafikiri kwamba watarudi bungeni kwenye mijadala ya dharau, ubaguzi na matusi inayofanywa na wajumbe wa CCM, basi hajui chimbuko la tatizo.
"Kadiri anavyoendelea kuliacha Bunge liendelee na mijadala ya kibaguzi na matusi, taifa linazidi kupasuka na washauri wake hawamwelezi tatizo hilo," alisema.
Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema kuwa Rais Kikwete asipokuwa makini atalitumbukiza taifa kwenye machafuko ingawa yeye anafanya utani kwa kuipasua nchi na kushangilia kauli za kibaguzi, kejeli na matusi zinazotolewa na baadhi ya wajumbe wa CCM.
"Rais na wasaidizi wake inaelekea hawajasikiliza hata kauli zinazotolewa na viongozi wa dini kuhusu rasimu ya Warioba, atuache twende kwa wananchi, wao ndio wataamua. Tumevumilia kwa kiwango fulani, lakini itafika mahali uvumilivu utaisha, kwani hatuwezi kuendelea kuzuiliwa kufanya mikutano na jeshi la polisi wakati mikutano ya CCM inafanyika kote nchini kutuchafua," alisema Mbowe.
CHANZO: TANZANIA DAIMA
Share:

Wastaafu wamteka JK

wastaafu 13cf0
Na Hudugu Ng'amilo
RAIS Jakaya Kikwete amehujumiwa na viongozi wakuu wastaafu waliomlazimisha kuachana na msimamo wa muundo wa muungano wa serikali tatu na kukumbatia serikali mbili zilizopendekezwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa kutoka kwa baadhi ya vyanzo vya habari vilivyo karibu na rais, Ikulu na makao makuu ya CCM, zimelithibitishia  kwamba hadi Bunge Maalumu la Katiba linaanza, Rais Kikwete alikuwa na msimamo ule ule wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Baadhi ya viongozi wastaafu, wakiwamo marais na viongozi waandamizi wa CCM, walishinikiza rais aachane na serikali tatu, kwa vitisho kwamba zitaua muungano.
Baadhi ya wastaafu hao walimficha Rais Kikwete kwamba kwa kuwa yeye aliingia madarakani akiwa rais wa muungano wa serikali mbili, halikuwa jambo la busara kwake kujiingiza kwenye historia ya kuwa rais aliyevunja muungano.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, shinikizo hilo liliambatana na jingine la kumtaka asizindue Bunge kabla ya rasimu ya pili ya katiba mpya kuwasilishwa bungeni, ili apate fursa ya kudhoofisha hoja ya serikali tatu.
Mara baada ya Rais Kikwete kukubaliana na "washauri wake", serikali ililazimika kuingilia kati ili Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta atengue kanuni, Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba awasilishe rasimu kabla ya rais kuzindua Bunge, jambo ambalo limesababisha mvurugano unaotishia kuvuruga kabisa mchakato wa katiba mpya.
Hata hivyo, hali hiyo inasemekana kumnyima amani Rais Kikwete ambaye ndiye aliyepokea na kusaini rasimu hiyo, kwa maana kwamba aliridhia.
Uamuzi huo umefanya rais aonekane kiongozi asiye na msimamo thabiti katika masuala muhimu.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanadai hatua hii imemfanya ashindwe kuacha urithi makini na muhimu katika utawala wake wa miaka 10, kama ambavyo alikuwa amedhamiria.
Wadadisi wanasema wastaafu walimzuia rais kutekeleza azima yake kwa sababu ya hofu tu, wakidhani kwamba katiba mpya yenye mfumo mpya inaweza kufumua mambo yaliyofichika na kuwaingiza matatani.
Wanadai kwamba muungano wenye mfumo mpya una kila dalili za kuiondoa CCM madarakani, na kuhatarisha maslahi ya watawala waliopo na waliopita.
Hoja hii, kwa mujibu wa vyanzo vyetu, ndiyo ilimkuna Rais Kikwete hata akabadili msimamo.
Kwa hali halisi ilivyo, na mchakato unavyoendelea, ahadi ya Rais Kikwete kuwapa Watanzania katiba mpya mwezi huu imeshindikana.
Alipohutubia taifa na kutangaza kuanzisha mchakato wa katiba mpya miaka mitatu iliyopita, alisema kwamba lengo lake lilikuwa kuzindua katiba mpya katika maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya muungano iliyofanyika jana.
Hadi Bunge Maalumu la Katiba linaahirishwa juzi, zilikuwa zimepita siku 68 kati ya 70 zilizotengwa kwa ajili ya Bunge hilo, huku kukiwapo mgawanyiko mkubwa wa wajumbe na kutishia uhai wa muungano, hasa baada ya wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kususia Bunge baada ya kukerwa na hujuma na matusi kutoka kwa wajumbe wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hadi sasa Bunge la Katiba limefanikiwa kujadili sura mbili za rasimu bila ya kuzipigia kura. CCM imekataa maoni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba yanayopendekeza mfumo wa muungano wa serikali tatu, wakatetea mfumo wa serikali mbili.
Mapendekezo hayo ni kinyume kabisa cha yaliyomo kwenye rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyowasilishwa ili ijadiliwe na wajumbe hao na kisha kutunga katiba mpya.
UKAWA wanadai kuchoshwa na vitisho na matusi kutoka kwa wajumbe wa CCM na viongozi wa serikali, wakisema kuwa kwa hali ilivyo katiba bora ya wananchi haiwezi kupatikana kwa shinikizo la muundo wa serikali mbili.
Katika hili, Rais Kikwete analalamikiwa kuwa ndiye mvurugaji wa kwanza wa mchakato ambao aliuasisi na kuahidi kuwapatia wananchi katiba bora kabla ya kuondoka madarakani.
Wakati akilihutubia Bunge la Katiba na kulizindua rasmi Machi mwaka huu, Rais Kikwete aliibeza rasimu ya Tume ya Jaji Warioba, akisema takwimu zao kuhusu watu waliotoa maoni ya muundo wa muungano zinatiliwa shaka.
Alisema kuwa muundo wa serikali tatu unaopendekezwa hautekelezeki kwani rais wa dola hiyo hatakuwa na mamlaka kwa vile hana ardhi, rasilimali na hivyo hataweza kukopa.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, katika hali kama hiyo, jeshi linaweza kupindua serikali na hivyo ukawa mwanzo wa kuvunjika kwa muungano, huku akisisitiza kwamba wao kama CCM muundo ambao unaweza kutatua kero zilizopo ni ule wa sasa wa serikali mbili.
Kauli hiyo ya rais iliibua mjadala mkubwa, na hivyo kufifisha ndoto za kupatikana kwa katiba bora kwani ilionyesha wazi kwamba mapendekezo ya wananchi ya serikali tatu yaliyomo kwenye rasimu hayatazingatiwa.
Hali hiyo imeendelea kujitokeza kwenye Bunge Maalumu la Katiba baada ya wajumbe wote wa CCM kuendeleza msimamo wa rais wa serikali mbili na kumshambulia Jaji Warioba binafsi kwa matusi mazito wakidai ana ajenda ya kuvunja muungano kwa kupendekeza serikali tatu.
Hatua ya Rais Kikwete kubadilika na kuvuruga mchakato aliyouasisi na kuusimamia kwa mafanikio makubwa, imeelezwa kusababishwa na mambo makubwa mawili, likiwemo hilo la kuburuzwa na viongozi wastaafu.
Duru nyingine za kisiasa katika suala hilo la kukwama kwa mchakato wa katiba, zinahusisha na rasilimali ya gesi na mafuta zilizopatikana nchini, ambapo inadaiwa mataifa makubwa yanayotaka kuwekeza ndiyo yanaishinikiza serikali isibadili muundo wa muungano uliopo.
Vyanzo vyetu vya habari vinaeleza kwamba mataifa hayo tayari yameweka msimamo wa kuisaidia CCM kifedha ili kuhakikisha inapigana kufa au kupona kutobadili muundo wa muungano katika katiba mpya.
Inaelezwa kuwa muundo wa shirikisho la serikali tatu unaopendekezwa kwenye rasimu ya katiba mpya, unatoa fursa ya wazi kwa wananchi wa serikali washirika kusimamia rasilimali zao tofauti na ilivyo katika muundo wa sasa ambapo mambo mengi yamefanywa siri na serikali.
Hadi sasa majaliwa ya kupatikana kwa katiba mpya yametoweka baada ya UKAWA kujiondoa, na hivyo kulifanya Bunge la Katiba kushindwa kufanya maamuzi ya kupitisha ibara na sura za rasimu kutokana na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar kushindikana.
Chanzo Tanzania Daima.
Share:

(CCM) kimepanga mkakati wa kuengua wataka urais wanaume

(CCM) kimepanga mkakati wa kuengua wataka urais wanaume.

migiro ec14d
Na Hudugu Ng'amilo
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga mkakati mpya wa kuengua wataka urais wanaume kwa kuingiza hisia za kijinsia kama walivyofanya kumdhibiti aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta, alipotaka kugombea tena nafasi hiyo mwaka 2010.
Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wameliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa mkakati huo unalenga zaidi kumng'oa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ambaye anaonekana tishio kwa wenzake wanaotajwa kutaka urais.
Kwa mkakati huo, kundi la wana CCM walio karibu na Rais Jakaya Kikwete, wameanza kuzungumzia jinsi ya kumpitisha Dk. Asha-Rose Migiro agombee urais katika uchaguzi mkuu ujao 2015.
Kisingizio wanachotumia katika kampeni yao ya siri, ni kusaka kura za wanawake.
Katika mkakati huo, wanamwandaa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kuwa Waziri Mkuu. Tayari Membe ameshatangaza kuwa hatagombea ubunge mwaka 2015.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Membe ndiye alikuwa akipigiwa chapuo zaidi miongoni mwa makada wa CCM ili kurithi mikoba ya Rais Kikwete, lakini kutokana na uhusiano wa kifamilia uliopo baina ya wawili hao, sasa ameshawishiwa kuwa atakuwa waziri mkuu endapo Dk. Migiro atashinda.
Wiki hii, gazeti dada la Tanzania Daima Jumatano liliripoti mkakati wa kumzima Lowassa asigombee urais, ambao unaendeshwa na mtoto wa kigogo akishirikiana na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Dk. Migiro ambaye kwa sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria, na pia Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Nje wa CCM, tayari ameanza kuzungushwa mikoani ili kumjengea uwezo na uzoefu wa kisiasa.
Miongoni mwa wana CCM wanaotajwa kuutaka urais 2015 mbali na Lowassa na Membe, ni Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano), Stephen Wasira, William Ngeleja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
"Ukiwalinganisha Membe na Lowassa kwa nguvu na umaarufu ndani ya CCM, hata vigogo wengine wanaotajwa kuutaka urais, utaona hakuna wa kumshinda Lowassa, sasa ndani ya chama wameamua kumchezea rafu.
"Kwa vile ana mtandao mrefu ndani ya CCM, wanafahamu wakikata jina lake itakuwa balaa, hivyo wameona waibuke na hoja ya zamu ya wanawake kama walivyomzima Samuel Sitta asigombee uspika wakampa Anne Makinda," alisema mtoa habari wetu.
Chanzo hicho kinaongeza kuwa mlengwa ni mtoto wa kigogo ambaye anaendesha mkakati wa kumchafua Lowassa ili 2025 ndiye awe mgombea urais baada ya Dk. Migiro kumaliza uongozi wake endapo atachaguliwa kwa vipindi viwili.
Pamoja na mkakati huo, kundi la Membe limeshauriwa kuendelea na harakati za kujiimarisha ili kuhadaa makundi mengine ndani ya chama yaamini kwamba naye ni miongoni mwa watakaochukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais.
Hata hivyo, wakati CCM ikiendesha mkakati huo dhidi ya Dk. Migiro ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, baadhi ya wasomi wamemchambua mwanamama huyo wakisema hana uwezo huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, alisema kuwa Dk. Migiro haonekani kubadilika licha ya kuwa na elimu kubwa.
"Nilimtembelea ofisini kwake akiwa UN kama Naibu Katibu Mkuu, nilikuwa na kazi za kitaifa kabisa kwa masuala yaliyoshirikisha mabalozi wa Ulaya, lakini aliponiona aliniuliza kwanini sitaki kurejea CCM.
"Huyu hawezi hata kubaini hapa tunazungumzia masuala ya kitaifa au kimataifa, yeye akili yake inawaza CCM tu kila wakati, hajaonyesha kutofautisha u-CCM wake na taaluma ili aweze kusaidia katika nyanja za kitaifa na kimataifa," alisema.
Dk. Slaa aliongeza kuwa aliposikia kuwa Dk. Migiro ndiye aliyeandaa rasimu ya kwanza na ya pili ya katiba kwa upande CCM ambazo zinaleta shida kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba zikikinzana na rasimu ya Tume ya Jaji Warioba, amedhihirisha kabisa udhaifu wake.
"Ukiangalia rekodi zake akiwa UN, huwezi ukaona matokeo yoyote, ndiyo maana Ban Ki moon hakutaka tena asaini mkataba kwa awamu nyingine kwani hakuwa na msaada kwake," alisema Dk. Slaa.
Dk. Azavery Lwaitama ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bukoba ambaye alisema kuwa Dk. Migiro sio mtu mwenye umaarufu wowote ambao unaweza kumfanya amweke katika orodha ya watu wanaoweza kuwa viongozi wa nchi hii.
"Aliteuliwa kuwa Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, akafanya kazi kipindi kifupi na baadaye akafanywa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati wa awamu ya Rais Kikwete.
"Kutokana na kunong'onezana kati ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon na Rais Kikwete, Dk. Migiro aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na baadaye kwa utaratibu huo huo wa kunong'onezana akarejeshwa tena nchini," alisema.
Dk. Lwaitama aliongeza kuwa vyombo vya habari vya nje viliandika vizuri kuhusu uwezo wa Dk. Migiro wakati akiwa Umoja wa Mataifa, lakini Watanzania hawakujishughulisha kuangalia yaliyoandikwa.
"Nilitarajia kuwa yeye atakuwa na mawazo tofauti katika mjadala wa rasimu iliyopo bungeni, lakini amerudi kwa wana CCM wenzake, anafikiri kama wao, analeta ushabiki wa makundi ya kisiasa, kwa utaratibu huo hawezi kuwa kiongozi anayefaa," alisema.
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) ambaye ni mwanafunzi wa Dk. Migiro, alisema haoni dalili au uwezo wowote wa yeye kuwa kiongozi katika wadhifa huo mkubwa wa urais.
"Huyu hajawahi kushiriki uchaguzi wowote akashinda, ukiwemo hata ubunge, isipokuwa nafasi za kuteuliwa ambazo hupewa na marais.
"Angalia kwa mfano katika Bunge hili la katiba ametoa mchango gani wa kukumbukwa na wananchi licha ya kuchangia na kubaki katika Bunge linalotoa matusi na kuacha kujadili rasimu?" alisema Lissu.
Share:

Waziri mkuu nchini Korea Kusini ajiuzulu

Waziri mkuu nchini Korea Kusini ajiuzulu



Waziri mkuu nchini Korea Kusini amejiuzulu kutokana na vile serikali yake ilivyolichukulia swala lote la ferry iliozama siku kumi na moja zilizopita.
Chung Hong Won amesema kuwa kusalia afisini ni mzigo mkubwa kwake.
Bwana Chung alizomwa alipozitembelea familia za waathiriwa waliotoweka katika ferry hiyo ya Sewol,baada ya kuzama katika hali ya kutatanisha.
Takriban watu 200 wanadaiwa kufa maji katika tukio hilo huku zaidi ya mamia wengine wakiwa hawajulikani waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu waliokuwa wakielekea katika ziara ya shule.
Wapiga mbizi bado wanaendelea kuwasaka waathiriwa chini ya ferry hiyo iliozama.
Ripoti za awali zimedai kuwa watu wote wametolewa katika boti hiyo.
Share:

Viongozi wa Dini Mikoa ya Lindi na Mtwara kuhudhuria mafunzo ya gesi asilia na mafuta nchini Thailand

Viongozi wa Dini Mikoa ya Lindi na Mtwara kuhudhuria mafunzo ya gesi asilia

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Nishati, Bw.Mrimia Mchomvu (kushoto) akiongea na Viongozi wa Dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara waliofika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, kabla ya kuanza ziara ya mafunzo ya gesi asilia na Mafuta nchini Thailand.Kushoto kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Maseke Mabiki.  KUSOMA KWA KINA BOFYA HAPA...
Share:

HUYU NDIYE MBUNGE MDOGO KULIKO WOTE MWENYE MIAKA 21 TU AMBAYE YUPO BUNGE LA KATIBA??? MFAHAMU HAPA




Mbunge Teddy Ladislaus Patrick (21), ndiyo mbunge mdogo kulioko wote katika bunge maalum la katiba.


Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mh. Samuel Sitta akimuapisha Theddy L. Patrick kuwa mbune wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kati.

Share:

Saturday, 26 April 2014

SHEREHE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZAFANA JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
 Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya Muungano.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
 Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
 Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono.
 Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu.
 Kikosi cha Wanamaji
 Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika kwenye Kilele cha  Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.
 Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha mwamvuli .
 Maandamano ya Pikipiki.
 Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano .
Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya miaka 50 ya Muungano ambapo watu waliorusha njiwa hao nao wametimiza miaka 50.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger