Saturday, 8 November 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 8,2025


Magazeti

Share:

Friday, 7 November 2025

VIJANA WASHAURIWA KUACHA MIHEMKO NA KUILINDA AMANI



Wananchi wa Mkoa wa Dar Es salaam wameeleza kuwa mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali nchini pamoja na ukosefu wa huduma na bidhaa muhimu kulikotokana na ghasia na vurugu za Oktoba 29, 2025 kumewaathiri kiuchumi, wakiwataka Vijana kuacha mihemko na kutokubali kurubuniwa katika kuharibu amani na utulivu uliopo nchini.

Wananchi hao kwa nyakati tofauti wakizungumza na waandishi wa habari akiwemo Bw. Rahim Hassan Bakari, Mfanyabiashara wa soko la Kariakoo amesema kwa siku sita za ghasia hizo na zuio la kutofanya biashara kwa saa 24 kama walivyozoea limesababisha mfumuko huo ikiwemo katika bidhaa za vyakula ambapo nyanya moja kwasasa inauzwa shilingi 1, 000 kutoka Shilingi 100 huku Mchele ukiuzwa Kilo moja Shilingi 4,000 badala ya 2500.

"Vijana wenzangu nawashauri tuache mihemko, kilichotokea juzi kilikuwa mihemko tu kwasababu leo ukimuuliza aliyeandamana kwamba kwanini aliandamana atakuambia hana majibu. Mimi niombe tu kuwa tuache mihemko na kama tuna madai mbalimbali tufuate njia sahihi za kushughulikia changamoto zetu." Amesisitiza Bw. Bakari.

Kwa upande wake Bi. Faizat Peter, Mkazi wa Mbagala Jijini Dar Es Salaam ameeleza namna ambavyo maandamano hayo yamemuathiri kiuchumi na kijamii, akitoa wito wa amani nchini Tanzania na Watanzania wote kufanya tafakuri na kujifunza kutokana na athari zilizojitokeza Oktoba 29 kutokana na vurugu na ghasia zilizotokea Mkoani Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha, Songwe na Mbeya.


Share:

Thursday, 6 November 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 7, 2025

Share:

MRADI WA SHULE BORA KUKAMILISHA UJENZI WA DARASA SHULE YA MSINGI BIRIKANI – HANDENI MJI




Na Mwandishi Wetu, Handeni TC 

MRADI wa Shule Bora upo hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa darasa jipya katika Shule ya Msingi Birikani, Halmashauri ya Mji Handeni, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elieskia Mmbuji, ametoa taarifa hiyo kwa Timu ya Usimamizi ya Halmashauri iliyoongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri, Maryam Ukwaju, wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo.

Mmbuji amesema kuwa hadi sasa jumla ya Sh.11,774,310 zimetumika katika hatua mbalimbali za ujenzi, kati ya Sh. milioni 15 zilizopokelewa kutoka Mradi ya Shule Bora mnamo Mei 27, 2025.

Ameeleza kuwa ujenzi huo umeanzishwa kwa lengo la kupunguza changamoto ya mrundikano wa wanafunzi na kuimarisha mazingira ya kujifunzia, jambo litakalosaidia walimu kutoa elimu bora zaidi.

“Ukamilishaji wa darasa hili utapunguza msongamano wa wanafunzi madarasani na kuboresha mazingira ya kujifunza, hivyo kuongeza ubora wa elimu katika shule yetu,” amesema Mmbuji.
Share:

SAMUU PRIMARY SCHOOL YANG’ARA KITAIFA, YAPATA DARAJA A KWA WOTE MATOKEO DARASA LA SABA 2025!



SAMUU PRIMARY SCHOOL YANG’ARA KITAIFA, YAPATA DARAJA A KWA WOTE MATOKEO DARASA LA SABA 2025!

Shule ya Msingi Samuu Primary School iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga imefanya vizuri kwa kiwango cha juu katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba (PSLE) mwaka 2025, baada ya wanafunzi wake kufaulu kwa asilimia 100 na shule hiyo kupata Daraja A (Bora).

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), jumla ya wanafunzi 63 walifanya mtihani huo na wote wamefaulu kwa mafanikio makubwa, huku shule ikipata wastani wa alama 272.3968.

Kati ya wanafunzi hao, wasichana 28 na wavulana 35 walishiriki mtihani, ambapo wanafunzi 59 wamepata daraja A, na wanafunzi 4 wakipata daraja B. Hakuna mwanafunzi aliyepata daraja C, D au E – ishara kwamba shule hiyo imejipambanua kuwa miongoni mwa shule bora zaidi katika Mkoa wa Shinyanga na hata kitaifa.

Mafanikio hayo yanatajwa kuwa matokeo ya juhudi kubwa za walimu, ushirikiano mzuri wa wazazi pamoja na nidhamu na bidii ya wanafunzi, chini ya uongozi makini wa walimu wakuu wa shule hiyo.

Wazazi na wananchi wameipongeza shule hiyo kwa kuendelea kuwa kielelezo cha ubora wa elimu, huku wakihamasisha shule nyingine kuiga mfano wake wa mafanikio.

Wasiliana na Samuu Primary School 
kwa simu : 0765018834/0754765336
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 6,2025



Magazeti







Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger