Wednesday, 29 October 2025

DKT. SAMIA APIGA KURA CHAMWINO



Na Dotto Kwilasa, Dodoma


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatano Oktoba 29, 2025, amejitokeza kupiga kura katika kituo cha Kijiji cha Chamwino, mkoani Dodoma, wakati wa zoezi la Uchaguzi Mkuu linaloendelea kote nchini.

Dkt. Samia alipowasili kituoni hapo mapema asubuhi, alijiunga na wananchi wengine kwenye mstari wa foleni akisubiri zamu yake kupiga kura  tukio lililopokelewa kwa hisia kubwa za furaha na hamasa kutoka kwa wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Baada ya kupiga kura, Dkt. Samia amewataka Watanzania wote kujitokeza kwa wingi kutekeleza haki yao ya Kikatiba kwa utulivu, akisisitiza kuwa amani na mshikamano ni msingi wa maendeleo ya taifa.


Share:

WANANCHI WAJITOKEZA KWA UTULIVU KUPIGA KURA BUYUNI, DAR ES SALAAM





Na Mwandishi wetu, Dar

Zoezi la kupiga kura linaendelea kwa utulivu katika kituo cha Buyuni, kilichopo Changanyikeni, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, likianza mapema saa 1.00 asubuhi. Wananchi wameendelea kujitokeza kwa utaratibu kutekeleza haki yao ya kikatiba katika mazingira ya amani na usalama.

Maafisa wa tume ya uchaguzi wanaendelea kusimamia mchakato huo kwa weledi, wakitoa huduma kwa wapiga kura kwa namna inayoonesha maandalizi mazuri ya uchaguzi huu.

Wananchi wametakiwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani, wakizingatia maelekezo yanayotolewa na wasimamizi wa vituo, ili zoezi hilo muhimu kwa demokrasia ya nchi liwe na mafanikio makubwa.
Share:

WAZIRI NDUMBARO APIGA KURA APONGEZA UTULIVU NA UHAMASISHAJI WA WANANCHI SONGEA

Waziri wa Katiba na Sheria daktari Damasi Ndumbaro akiwa anapiga kura katika kituo alichojiandikisha leo mapema katika mtaa wa Mjimwema A Songea Mjini 

 Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma 

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, ameambatana na familia yake kupiga kura katika kituo namba moja cha Mjimwema A, eneo ambalo amekuwa akipigia kura kwa miaka mingi. 

Akizungumza mara baada ya kupiga kura, Dkt. Ndumbaro amesema amefika kutimiza haki yake ya kikatiba ya kuwachagua viongozi, na amepongeza muitikio mzuri wa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo muhimu la kidemokrasia.

Ameeleza kuwa katika eneo la Mjimwema A kuna jumla ya vituo tisa vya kupigia kura na wananchi wamejitokeza kwa wingi, huku mchakato ukiendelea kwa amani na utulivu.

 Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa mji wa Songea una jumla ya vituo 500 vya kupigia kura, na baada ya kupiga kura wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku za kujiletea maendeleo katika hali ya usalama na utulivu.

Aidha, Waziri Ndumbaro amewahimiza wananchi ambao bado hawajapiga kura kujitokeza kutimiza wajibu wao wa kikatiba, huku akiwataka waliomaliza kupiga kura kuendelea na shughuli zao kwa amani. 

Kwa upande wake, Zakaria Ngonyani, mkazi wa Mtaa wa Mjimwema A, amesema ameridhishwa na maandalizi na mwenendo mzima wa zoezi la upigaji kura, na amepongeza hatua ya kuongeza vituo vingi vya kupigia kura, jambo lililorahisisha ushiriki wa wananchi wengi zaidi.


Share:

Tuesday, 28 October 2025

MCHENGERWA AFUNGA KAMPENI KWA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUZINGATIA AMANI


Na Yohana Kidaga- Utete, Rufiji

Mgombea wa Ubunge jimbo la Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa amefunga kampeni yake huku akitoa wito wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa kesho kwa amani na kurejea majumbani huku akimwombea kura Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni jana kwa jimbo la Rufiji kukiombea kura Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika kesho Oktoba 29, 2025 kwa ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani katika eneo la Utete Mhe. Mchengerwa ambaye pia ni Waziri wa TAMISEMI ametoa wito kwa wananchi wote nchini kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura wakizingatia amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi.
Aidha, amefafanua kuwa wananchi wawaepuke baadhi ya watu wenye nia mbaya ya kuleta fujo kwa kuwa amani ikitoweka watakaopata shida ni watoto, wazee na akina mama ambao hawana hatia.

"Ndugu zangu naomba ieleweke kuwa watanzania hatuna Tanzania nyingine hivyo ni muhimu kuelewa kuwa nchi yetu imejengwa katika misingi ya amani aliyotuachia baba wa taifa Mwalimu Nyerere hivyo hatuna budi kuendelea kutunza amani yetu katika kipindi hiki cha uchaguzi". Amesisitiza Mhe Mchengerwa 
Aidha, ameeleza kuwa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeleta mapinduzi makubwa nchini ambapo Jimbo la Rufiji limekuwa ni miongoni mwa wanufaika wakubwa.

Ametaja baadhi ya maeneo ambayo Serikali imeboresha kwa jimbo la Rufiji ni kwenye kuleta huduma ya umeme kwenye vijiji vyote na ujenzi madaraja na barabara za kiwango cha lami, huduma ya maji safi na salama, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya pia madarasa ya shule za msingi na Sekondari.
Amesema endapo wananchi watampa ridhaa tena ya kuliongoza jimbo hilo atahakikisha anaiomba Serikali kukamilisha kazi kubwa iliyofanyika hususan ya ujenzi wa barabara ya Utete- Nyamwage na ahadi zote zilizo ndani ya Ilani ya CCM.

Mkutano wa kufunga kampeni ulikuwa na vibe Babkubwa kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki wakiongozwa na msanii anayetamba nchini Mboso, na msanii chipukizi Dogo Pattern aliyechana mistari na kuwaacha wapenzi wa Singeli kuserebuka vilivyo.
Mhe. Mchengerwa ni Mbunge wa tisa wa kuchaguliwa katika jimbo hilo la Rufiji toka lianzishwe na kuongozwa na wabunge kadhaa kuanzia Mhe. Bibi Titi Mohamed ambapo anaelezewa kuwa ni miongoni mwa wabunge walioliletea maendeleo makubwa Jimbo hilo ukilinganisha na wabunge waliotangulia.

Licha ya kuwa Mbunge wa tisa wa Jimbo hilo, Mhe. Mchengerwa ni miongoni mwa wanasiasa wachache nchini ambao wamehudumu kwenye mihimili yote katika nafasi za juu za uandamizi.


Akiwa kwenye mkutano wa kampeni zake alioufanya Ikwiriri, Mgombea wa Urais, mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alimwelezea Mhe Mchengerwa kuwa amefanya kazi nzuri katika Wizara zote nne alizomteua kuhudumu kwenye kipindi chake cha uongozi.

Share:

WAPIGA KURA 37,647,235 KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na wananchi wakati akisoma risala yake kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotaraji kufanyika Oktoba 29, 2025.

Share:

Monday, 27 October 2025

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA SHINYANGA WATOA TAMKOA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29

Share:

Ngoma Mpya : KALICHO _ MASAMVA GATWAMBELEJE

 



Share:

Sunday, 26 October 2025

POLISI JAMII FITNESS CENTER SHINYANGA YAZINDUA MARATHON KUKUSANYA MILIONI 520 KWA AJILI YA PIKIPIKI ZA KUIMARISHA USALAMA


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Kikundi cha mazoezi cha Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) kilichopo Manispaa ya Shinyanga kimezindua rasmi kampeni ya mbio za marathon zenye umbali wa kilomita 5, 10 na 21 pamoja na vifaa mbalimbali vitakavyotumika, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukusanya Shilingi milioni 520 kwa ajili ya ununuzi wa pikipiki zitakazotumiwa na maafisa wa Polisi Jamii katika kuimarisha utendaji wao wa kazi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Oktoba 25,2025, Mwenyekiti wa mbio hizo, Ignas Banyema, ameupongeza uongozi wa serikali ya mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kushirikiana nao katika kufanikisha malengo ya kikundi hicho, huku akiomba msaada wa kupata wadhamini zaidi ili kufikia lengo lililowekwa.

“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya tunakushukuru sana kwa kufika hapa leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wetu wa Shinyanga Mheshimiwa Mboni Mhita. Umezindua rasmi mpango wa Shinyanga Marathon pamoja na vifaa vitakavyotumika. Tunaomba serikali ya mkoa iendelee kutushika mkono katika hatua zote za kupata wadhamini, kwani lengo letu ni kukusanya Shilingi milioni 520 ili kufanikisha ununuzi wa pikipiki kwa askari wetu wa Polisi Jamii,” amesema Banyema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, ameipongeza PJFCS kwa ubunifu na dhamira njema waliyoionesha kupitia kampeni hiyo, huku akiahidi kuwa serikali ya mkoa itaendelea kuwaunga mkono.

“Serikali ya mkoa itaendelea kuwa bega kwa bega nanyi, kwani malengo yenu ni mazuri na yenye manufaa makubwa kwa Polisi Jamii na jamii kwa ujumla. Endeleeni na jitihada hizi, kwani mazoezi ni afya na pia yanaunganisha watu. Hata hivyo, niwakumbushe kuendelea kushiriki ipasavyo katika zoezi la uchaguzi mkuu,” amesema Wakili Mtatiro.

Kikundi cha Polisi Jamii Fitness Center kimekuwepo kwa zaidi ya miaka 10, kikiwa na washiriki zaidi ya 200, kikijikita katika kuhamasisha mazoezi, afya, na ushirikiano baina ya wananchi na Jeshi la Polisi.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni:“Kimbia kwa Afya, Imarisha Usalama wa Raia na Mali Zao.”





























Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger