Sunday, 31 August 2025

BARRICK BULYANHULU YAFANIKISHA UJENZI WA STENDI YA MABASI YA KISASA IKANGALA - NYANG’HWALE

Mkuu wa Wilaya ya Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale ,Grace Kingalame akiongea katika hafla ya uzinduzi wa stendi ya mabasi ya Ikangala ambayo imejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Barrick Bulyanhulu

***
Nyang’hwale: Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umefanikisha kuondoa kero ya muda mrefu ya kutokuwepo stendi ya mabasi kwenye Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, ambapo kupitia fedha za uwajibikaji wa jamii (CSR) kwa kushirikiana na Halmashauri hiyo umejenga stendi ya kisasa ya Ikangala kwa gharama ya shilingi milioni 299.9.

Hafla ya uzinduzi wa stendi hiyo imefanyika wilayani humo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wananchi, wafanyakazi wa Barrick ambapo mgeni alikuwa ni Mkuu wa wilaya hiyo, Grace Kingalame.

Akifungua stendi hiyo, Grace Kingalame amesema miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na wawekezaji ni matunda ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki kwa uwekezaji nchini.

Kingalame amewataka wananchi , wafanyabiashara pamoja na wadau wote wa usafirishaji kutumia fursa ya stendi katika kujikwamua kiuchumi.

“Natoa rai kwa wananchi na wadau wote wa usafirishaji waweze kutumia fursa ya uwepo wa stendi hii kujikwamua kichumi kupitia biashara mbalimbali zinazotokana na mahitaji ya utoaji wa huduma kwa wasafiri," amesema.

Awali Akisoma Taarifa ya ujenzi, Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Bruno Marco amesema ujenzi huo unatekelezwa kwa awamu kwa kutumia mfumo wa mkandarasi kwa baadhi ya kazi na wataalamu wa ndani (Force Akaunti), na hadi sasa mradi umefikia asilimia 85.

“Ujenzi wa Stendi ya Ikangala unajumuisha miundombinu mbalimbali ikiwemo choo cha stendi, eneo la kuegesha magari ya abiria, jengo la abiria, jengo la huduma ya chakula, jengo la mkusanya mapato, kizimba cha kuhifadhia taka, fremu za maduka, jengo la polisi, na Mgahawa”, amefafanua.

Mwakilishi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika hafla hiyo, David Magege ambaye ni Afisa Uhusiano wa Jamii katika mgodi huo ameipongeza Halmashauri ya Nyang’hwale kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa mradi huo na miradi mingine inayoendelea kutekelezwa na fedha za CSR na kutoa wito kwa kamati ya maendeleo ya jamii (CDC) kuendelea kuibua miradi yenye tija inayolenga kuleta maendeleo na kunufaisha wananchi.

Mwenyekiti wa Wafanyabishara Wadogo yaani Machinga wa wilaya hiyo Bi. Dorcas Hussein akiongea kwa niaba ya wafanyabiashara na wananchi amesema wamefurahishwa kufunguliwa na kuanza kutumika kwa stendi ya mabasi Ikangala kwa kuwa utawapatia fura ya kujiendeleza kibiashara sambamba na kujikwamua kiuchumi,"Tunashukuru Serikali na Barrick Bulyanhulu kwa kuendelea kutuletea miradi ya maendeleo", amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale ,Grace Kingalame akiongea katika hafla ya uzinduzi wa stendi ya mabasi ya Ikangala ambayo imejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Barrick Bulyanhulu
Mkuu wa Wilaya ya Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale ,Grace Kingalame akiongea katika hafla ya uzinduzi wa stendi ya mabasi ya Ikangala ambayo imejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Barrick Bulyanhulu
Mwakilishi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu, David Magege akiongea katika hafla ya uzinduzi wa stendi ya mabasi ya Ikangala ambayo imejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Barrick Bulyanhulu
Mwakilishi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu , David Magege akiongea katika hafla ya uzinduzi wa stendi ya mabasi ya Ikangala ambayo imejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Barrick Bulyanhulu
Sehemu ya miundombunu katika stendi ya Ikangala
Sehemu ya wananchi wakiwa katika hafla hiyo
Sehemu ya wananchi wakiwa katika hafla hiyo
Sehemu ya wananchi wakiwa katika hafla hiyo
Sehemu ya  wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakiwa katika hafla hiyo
Sehemu ya  wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakiwa katika hafla hiyo
Share:

UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU 2025 GEITA SEPTEMBA 2

 


#MchagueSamia
#MchagueBiteko
#KusemaNaKutenda
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#OktobaTunatiki
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI 31,2025

 

magazeti    

  
Share:

Saturday, 30 August 2025

CHUO KIKUU HURIA NA JESHI LA POLISI RUVUMA WATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHIPOLE



Na Regina Ndumbaro, Songea – Ruvuma

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kimetoa msaada kwa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Chipole kilichopo Kata ya Magagura, Halmashauri ya Songea Vijijini. Msaada huo ulihusisha fedha taslimu shilingi milioni moja na laki mbili (1,200,000) pamoja na mahitaji muhimu kama vyakula, nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya kila siku.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Huria, Vincent Mpepo, alisema kuwa waliguswa na hali ya watoto hao baada ya kuona picha na video zilizosambazwa na Inspekta Dominic Msangi, Polisi Kata wa Magagura, ambazo zilionesha mazingira ya kituo hicho na kuhamasisha wadau kujitokeza kusaidia.

Mpepo ameeleza kuwa msaada huo ni mwanzo wa safari ya ushirikiano kati ya chuo hicho na kituo hicho, na kuahidi kuwa wataendelea kujitokeza kadri watakavyoweza ili kusaidia watoto hao kupata maisha bora.

 Pia amesema wana mpango wa kufadhili bima za afya kwa watoto 50, jambo litakalosaidia sana katika kukabiliana na changamoto za matibabu.

Kwa upande wake, Inspekta Msangi alieleza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa mkakati wa Kamishna wa Polisi Jamii wa kushirikiana na wadau kusaidia jamii, hasa makundi maalum kama watoto yatima, kwa lengo la kuimarisha mshikamano na huruma miongoni mwa Watanzania.

Akizungumza kwa niaba ya kituo, Mtawa Maria Akwinata kutoka Shirika la Watawa wa Chipole alishukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa kituo hicho kinalea watoto wa rika mbalimbali kuanzia wanaozaliwa hadi kufikia elimu ya sekondari, hivyo mahitaji yao ni makubwa na yanahitaji msaada wa mara kwa mara kutoka kwa jamii.

Mmoja wa watoto wa kituo hicho, Richard Haule, ameeleza kufarijika kwao kwa kutembelewa na kusaidiwa, akisema kuwa msaada huo umeonyesha kuwa bado wanakumbukwa na jamii.

 Ametoa wito kwa taasisi na watu binafsi kuendelea kujitokeza kusaidia ili kuwajengea watoto hao matumaini na mustakabali mzuri wa maisha.





Share:

WADAU WA UTALII WAZIDI KUITIKIA WITO WA SERIKALI.


-Hoteli ya Kifahari ya Mapito Safari Camp yazinduliwa rasmi Serengeti

Matokeo ya jitihada kubwa za Serikali ya Tanzania kutangaza vivutio pamoja na kuvutia wawekezaji wa kimataifa kuja kuwekeza nchini zinazidi kuzaa matunda kwani alhamisi, Agosti 29, 2025 imezinduliwa hoteli ya Mapito Safari Camp katika kijiji cha Robanda, Serengeti iliyojengwa na kampuni kubwa na maarufu ya hoteli duniani kutoka nchini Marekani ya Marriott.

Dkt. Thereza Mugoba, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii ameshiriki uzinduzi huo akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, hafla hiyo pia pamoja na wageni wengine imehudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Andrew Lentz.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger