Thursday, 7 August 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA AGOSTI 8,2025


Magazeti






Share:

EWURA  YATOA ELIMU KWA UMMA KATIKA MAONESHO YA NANENANE



MENEJA wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kati Hawa Lweno,akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la EWURA katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika kiwanja cha Nzuguni jijini Dodoma.

Na Alex Sonna-DODOMA

MENEJA wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kati Hawa Lweno, amesema Mamlaka hiyo imeshirikiana kikamilifu na wadau mbalimbali katika maonesho ya Nanenane kwa lengo la kutoa elimu kuhusu huduma zinazodhibitiwa na EWURA.

Timu ya wataalamu kutoka sekta za umeme, petroli,gesi asilia, maji na usafi wa mazingira , gesi pamoja na huduma kwa wateja wapo katika banda la EWURA ikitoa elimu kuhusu kazi na huduma zinazofanywa na mamlaka hiyo, ikiwemo kutoa leseni, kudhibiti ubora wa huduma na kuhakikisha upatikanaji na matumizi sahihi na salama ya huduma za nishati na maji.

Lweno amesema wadau wengi wamefika kupata elimu na kutoa maoni yao, wakiwemo wakulima, wadau wa nishati na maji, wamiliki wa vituo vya mafuta na wananchi wanaopata huduma za umeme na gesi.

Ameeleza kuwa changamoto kubwa ni upatikanaji wa mafuta vijijini, ambapo EWURA imekuwa imeweka masharti nafuu na kuendelea kutoa elimu kwa wakulima na wadau kuhusu namna ya kusogeza huduma hizo maeneo ya pembezoni jambo ambalo ameeleza kuwa limepata mwitikio mkubwa.

“Kwa mjini kituo kinaweza kuwa na mauzo ya hadi milioni 100 kwa siku na pampu nyingi, wakati vijijini kinaweza kufikia milioni 20 pekee na pampu moja tu, hivyo nitoe wito kwa watanzania hususani wakulima kuiona fursa hii” amesema.

Aidha, amesema EWURA imeendelea kuelimisha wananchi kuhusu taratibu za kupata leseni za kutoa huduma za nishati na maji, jambo ambalo limeongeza uelewa na hamasa ya wananchi wengi kutaka kufahamu zaidi.

Lweno pia amebainisha kuwa masuala ya maji yamekuwa miongoni mwa hoja zinazojitokeza zaidi katika maonesho hayo, ambapo baadhi ya wateja wameonesha wasiwasi kuhusu ubora wa maji wanayoyapata na EWURA imewahakikishia kuwa ubora wa maji ni eneo ambalo imekuwa ikilifuatilia kwa umakini.

Aidha amesema EWURA, imekuwa ikiwapa wananchi elimu kuhusu vigezo vya ubora na usalama wa maji.

Ametumia nafasi hiyo kutaka wananchi wote wanaotembelea maonesho ya Nanenane kufika katika banda la EWURA ili kupata elimu zaidi ya masuala ya udhibiti wa huduma za nishati na maji.
Share:

DKT. SERERA ATEMBELEA BANDA LA WHI KATIKA MAONESHO YA NANENANE


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera atembelea banda la WHI katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja Nanenane Nzuguni. Tembelea banda letu lililopo katiba banda kubwa la taasisi za serikali namba 4 upate elimu ya uwekezaji na nyumba.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera atembelea banda la WHI katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja Nanenane Nzuguni. Tembelea banda letu lililopo katiba banda kubwa la taasisi za serikali namba 4 upate elimu ya uwekezaji na nyumba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Abdul Athumani Mombokaleo atembelea banda la WHI katika maonesho ya Nanenane jijini Dodoma na kupata maelezo ya miradi inayotekelezwa pamoja na uwekezaji katika Faida Fund. Bw. Mombokaleo amewapongeza WHI kwa ubunifu wa e-Wekeza ambao umerahisishwa makato ya moja kwa moja kutoka kwenye mshahara na kuwekeza katika faida fund ambayo sasa itasaidia watumishi kujiongezea vipato kupitia uwekezaji
Share:

Wednesday, 6 August 2025

SENYAMULE AIPONGEZA EWURA CCC, ATOA MAELEKEZO YA KUPELEKA HUDUMA VIJIJINI




Na Dosca Kusenha, Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amelielekeza Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC) kuongeza nguvu ya utoaji elimu na kusogeza huduma karibu zaidi kwa watumiaji ili kuboresha uelewa wa haki na wajibu wao kuhusu huduma za mafuta, gesi, umeme na maji.

Akizungumza leo Agosti 5, 2025 baada ya kutembelea banda la EWURA CCC katika Maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, Senyamule amesema wananchi wengi wa pembezoni hukosa taarifa muhimu za namna ya kushughulikia changamoto na malalamiko kuhusu huduma za nishati na maji, jambo linalozuia maendeleo yao ya kiuchumi.

"Ili kuongeza uelewa wa haki na wajibu wao katika matumizi ya huduma za mafuta, gesi, umeme na maji, ni lazima wananchi wapate elimu endelevu itakayowawezesha kufahamu taratibu za kudai huduma bora, " amesema

Licha ya hayo Senyamule ameipongeza EWURA CCC kwa hatua yake ya kutumia maonesho ya Nanenane kutoa elimu ya moja kwa moja kwa wananchi na kueleza kuwa ni njia bora ya kuwajengea uwezo wa kutambua haki na wajibu wao.

Amesisitiza kuwa elimu hiyo itasaidia wakulima kupunguza gharama za uzalishaji kupitia matumizi sahihi na endelevu ya nishati na maji.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma amesisitiza umuhimu wa EWURA CCC kuongeza kasi ya kutoa elimu kuhusu utaratibu sahihi wa kushughulikia na kuwasilisha malalamiko, ili watumiaji wawe na uelewa mpana na waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo na biashara kwa tija na ufanisi zaidi.

Aidha Senyamule ameshauri EWURA CCC kuendelea kutumia majukwaa ya maonesho kama Nanenane sio tu kwa kutoa elimu, bali pia kukusanya maoni na changamoto za wananchi ili kusaidia Serikali kuboresha sera na mikakati ya kudhibiti huduma hizo.

Amesema ;“Tukiwaelimisha wananchi namna bora ya kutumia huduma za nishati na maji, tutakuwa tunawawezesha kuongeza tija katika kilimo na uzalishaji, "ameeleza

Kwa upande wake Afisa Uelimishaji na Uhamasishaji wa EWURA CCC, Lugiko L. Lugiko, ameeleza kuwa ushiriki wa Baraza hilo katika maonesho ya mwaka huu ni sehemu ya mkakati wa kusogeza huduma kwa wananchi na kuwaelimisha kuhusu haki zao na taratibu sahihi za kushughulikia changamoto wanazokutana nazo.

Lugiko amesema kupitia maonesho hayo, EWURA CCC inatoa mafunzo ya moja kwa moja kwa wakulima na wananchi kwa ujumla kuhusu namna ya kutambua bei halali za mafuta, kushughulikia bili zisizoeleweka na kushirikiana na watoa huduma ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Aidha, Lugiko amebainisha kuwa banda la EWURA CCC limekuwa likitoa elimu kwa vikundi vya wanawake, vijana na wakulima wadogo,kuhusu namna huduma bora za nishati na maji zinavyoweza kuongeza thamani ya mazao .

Kutokana na hayo baadhi ya Wananchi waliotembelea banda hilo wamepongeza jitihada hizo, akiwemo Lucy Joseph mkulima kutoka Singida ambaye amesema: “Kupitia EWURA CCC tunajua sasa njia sahihi ya kushughulikia changamoto za maji na umeme ,mwanzoni hatukijua namna ya kutatua kero zetu.”

EWURA CCC imeahidi kuendeleza ushirikiano na wadau mbalimbali ili kuhakikisha elimu na ushawishi wa watumiaji wa huduma za nishati na maji unawafikia Watanzania wote, hatua inayotarajiwa kuchochea uwajibikaji na uboreshaji wa huduma kwa manufaa ya taifa.


Share:

Tuesday, 5 August 2025

ALIYEKUWA MENEJA WA KANDA YA MASHARIKI TMDA DAR ES SALAAM AMWANGUSHA MWIJAGE KURA ZA MAONI MULEBA KASKAZINI


Na Mariam Kaagenda _Kagera 

 Aliyekuwa Meneja  wa  TMDA  Kanda ya Mashariki Adonis Bitegeko ameshinda Uchaguzi wa Kura za maoni Jimbo la Muleba Kasikazini katika Uchaguzi wa ndani wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Ubunge  kwa kupata Kura 4392 na kumshinda aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo  Charles Mwijage ambaye amepata Kura 2320 



Wakati akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo mkurugenzi wa Uchaguzi wilaya ya Muleba Agnes Kasera amesema kuwa Kura zilizotarajiwa kupigwa ni 8637,Kura zilizopigwa ni 7252,zilizoharibika ni 92 na Kura halali ni 7160 


Ambapo Adonis Bitegeko ameibuka kidedea kwa kupata Kura 4392 ambapo wengine waliogombea katika Uchaguzi huo Jimbo la Muleba Kasikazini ni Fortunatus Muhalila aliyepata Kura 248 ,Edward Mujungi Kura 157,Danstan Mutagaywa Kura 53 


Adonis amewashukuru Wajumbe kwa kumuamini na kumpatia Kura nyingi ambapo amesema kuwa Chama chake cha Mapinduzi kikimteua hatowaangusha Wajumbe waliomchagua   kwani atawalipa uwajibikaji katika swala la Maendeleo ya Jimbo la Muleba Kasikazini .

Share:

NILIWAFUMANIA MPENZI WANGU NA DADA YANGU MIAKA MITATU BAADAYE NINA HARUSI NA WAO BADO HAWANA WAPENZI


Nilikuwa na miaka 24 tu wakati moyo wangu ulipasuliwa vipande vipande na watu wawili ambao niliwategemea zaidi duniani mpenzi wangu wa miaka miwili na dada yangu wa damu. 

Ilikuwa ni siku ya Jumamosi jioni niliporudi nyumbani mapema kutoka kazini baada ya mkutano wetu kuahirishwa ghafla. Sikuwa nimewapa taarifa, na nadhani hiyo ndiyo iliyofanikisha kile kilichofuata.

Share:

ALISHINDA BAHATI NASIBU YA KIMATAIFA KWA TIKETI YA MTANDAONI NA SASA ANASAFIRI DUNIANI KWA STAREHE


Jina langu ni Saidi kutoka Tanga, na hadi leo bado siamini maisha niliyonayo sasa. Kuna wakati nilikuwa napambana tu kupata hela ya nauli, sasa hivi nasafiri duniani kama mtu wa hadhi, nikilala hoteli za nyota tano, nikila chakula cha kifahari, na hata kupewa heshima ya mgeni mashuhuri kwenye baadhi ya mataifa. Yote haya yalianza kwa kubonyeza tu linki ya tiketi ya bahati nasibu mtandaoni.

Nilikuwa tu kwenye simu yangu jioni moja baada ya kazi ya mchana ya kubeba mizigo bandarini. Niliona tangazo kwenye mtandao kuhusu bahati nasibu ya kimataifa, tiketi ilikuwa dola 5 tu. Kwa kawaida siamini mambo kama hayo, lakini kuna kitu ndani yangu kilinisukuma nijaribu.
Share:

UMMY MWALIMU AIBUKA KIDEDEA UBUNGE TANGA MJINI! WAJUMBE WATIKI



Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tanga Mjini wamemchagua ndugu. Ummy Ali Mwalimu kuwa mgombea ubunge wa Jimbo hilo kwa kura 5,750 kati ya kura 10,293 zilizopigwa.

Akitangaza matokeo hayo August 04, 2025 Msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Jimbo la Tanga Mjini lina jumla ya wajumbe 12,620 na waliopiga kura ni 10,293 ambapo kura zilizoharibika ni 117, kura halali zilizopigwa ni 10,176 sawa na Wastani wa asilimia 56.5

Ummy Ali Mwalimu amepata kura 5,750 ambayo ni sawa na 56.5%, Omary Ayoub akipata 4,146 sawa na 40%, Kassim Mbaraka 80 sawa na 1%, Rajabu Abasi 130 sawa na 1% huku Arif Fazel akipata kura 70 sawa na 0%.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger