Tuesday, 8 July 2025
Monday, 7 July 2025
EXPLORE THE WILD WONDERS OF SERENGETI – UNFORGETTABLE DAY TRIP FROM BUNDA!
TECTO COMMUNITY COMPANY LTD (TECTO TOUR & TRAVEL)
Your Gateway to Wildlife, Culture & Conservation in Tanzania
🌍 SERENGETI NATIONAL PARK TOUR – WESTERN SERENGETI (Day Trip)
Date: 08/08/2025 (Friday)
Route: Via Ndabaka Gate (Only 20km from Bunda)
Group Offer: Tsh 880,000 for 5 Adults & 2 Children
Package Includes:
✔️ Lunch Box
✔️ Soft Drinks
✔️ T-shirt
✔️ Park Entry Fees
✔️ Guide Fees
✔️ Wildlife Photography Opportunities
Welcome / Karibu Sana!
🚌 STAFF & GROUP TOUR OPTION (30 Tourists)
Travel by Bus (TATA or Coaster)
Cost per Person: Tsh 85,000
Includes:
✔️ Transport
✔️ Lunch Box
✔️ Soft Drinks
✔️ T-shirt
✔️ Park Entry Fees
✔️ Guide Fees
📍Visit Our Lake Victoria Zone Office:
Sarakwa Road, Opposite Diamond, Bunda - Mara, Tanzania
📞 Contact Us Today:
WhatsApp/Call: +255 746 988 397
Call: +255 785 064 024
📧 Email: tectocampany2020@gmail.com
WAHITIMU WA DARASA LA SABA 2002 MITWERO WAKABIDHI MADAWATI, WAMEOMBA WADAU KUJITOKEZA KUSAIDIA
Na Regina Ndumbaro-Lindi
Baadhi ya wahitimu wa darasa la saba mwaka 2002 kutoka Shule ya Msingi Mitwero, iliyopo Kata ya Rasibula, Manispaa ya Lindi, wamekabidhi msaada wa madawati 8 yenye thamani ya Shilingi 780,000 kwa shule yao ya zamani.
Wahitimu hao walikabidhi madawati hayo kama njia ya kurudisha shukrani kwa jamii na kusaidia kutatua changamoto ya uhaba wa madawati shuleni hapo.
Mwenyekiti wa umoja huo, Mosses Verisi, amesema wameanza na kidogo lakini wana dhamira ya kuendelea kusaidia zaidi kila mwaka.
Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Mitwero, Amina Mohamedi, amesema shule hiyo ilikuwa na uhaba wa madawati 45 na msaada huo wa madawati 8 umepunguza pengo hilo hadi 37.
Amewataka wahitimu wengine pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia ukarabati wa madarasa chakavu ambayo yanavuja, akisisitiza kuwa shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi za miundombinu.
Kwa upande wa wanafunzi wa sasa, akiwemo Yasini Steven na Agnes Raymond, wameeleza furaha yao kwa kupokea madawati hayo, wakisema yatasaidia kupunguza msongamano darasani na kuongeza hamasa ya kuhudhuria masomo.
Wametoa wito wa kupatiwa msaada zaidi kama vitabu na vifaa vingine vya kufundishia
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva, amewapongeza wahitimu hao kwa moyo wao wa kujitolea na kuwasihi wahitimu wengine wa shule za serikali kufuata mfano huo.
Pia Kaimu Afisa Elimu Msingi na Awali, Selemani Mgeleka, ameahidi kushirikiana na wadau hao na kuwataarifu pindi shughuli za ukarabati zitakapoanza ili waweze kushiriki kikamilifu.
Sunday, 6 July 2025
NILISHINDWA KUJIFUNGA VIATU KWA TUMBO KUBWA LAKINI BAADA YA DAWA HII YA ASILI, WATU HUNIPITA WAKIDHANI MIMI NI MWANAFUNZI WA SEKONDARI

KATIBU TAWALA WILAYA YA KAHAMA AWAPONGEZA WASHIRIKI WA MAONESHO YA SABASABA 2025 KUTOKA MKOA WA SHINYANGA
DIB YAENDELEA KUTOA ELIMU KATIKA MAONESHO YA 49 YA SABASABA




























