Tuesday, 15 April 2025

NELSON MANDELA NA WIZARA YA KILIMO KUSHIRIKIANA KUPITIA TEKNOLOJIA ZA KIDIGITALI KUIMARISHA KILIMO




Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ( kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli ( kushoto) wakionyesha hati ya makubaliano ya ushirikiano mara baada kusaini Jijini Dodoma.

Na Alex Sonna-DODOMA

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) na Wizara ya Kilimo wamesaini makubaliano ya mashirikiano katika tafiti na ubunifu ili kuimarisha matumizi ya teknolojia za kidijitali katika sekta kilimo.

Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kusaini makubaliano hayo, Makamu Mkuu wa taasisi hiyo, Prof.Maulilio Kipanyula amesema kuwa, makubaliano hayo ni mwendelezo wa hatua za kimkakati za kuimarisha mahusiano kati ya Wizara ya Kilimo na taasisi za Elimu ya Juu na Utafiti ikiwemo Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.

“Hatua hii inaipa fursa taasisi yetu kuwa sehemu ya mageuzi makubwa na ya kihistoria yanayofanywa na Wizara ya kilimo katika sekta ya kilimo nchini ” amesema Prof. Maulilio Kipanyula.

Aidha ameongeza kuwa mifumo hiyo kuwa ni pamoja na ile itakayorahisisha ukusanyaji, utunzaji na uchakataji wa takwimu mbalimbali katika sekta ya kilimo katika kuzalisha teknolojia za kibiolojia za kupambana na magonjwa na wadudu waharibifu kwenye mazao ya kilimo cha biashara na chakula kwa uboreshaji wa mbegu, afya ya udongo, teknolojia za umwagiliaji na teknolojia za kisasa za uvunaji na uhifadhi wa mazao ya kilimo.

Anazidi kufafanua kuwa makubalianao hayo yatahusisha kufanya tafiti, na bunifu za kisayansi katika sekta ya kilimo hususan katika maeneo ya teknolojia za kidijitali zinazo chipukia na matumizi yake , maabara za kisasa na wanasayansi wabobezi wa taasisi, wataiongezea nguvu wizara ya kilimo katika eneo la utambuzi wa vihatarishi "risks assessment" katika mazao na bidhaa za kilimo zinazo kwenda nje ya nchi, ambapo hatua hiyo itaongeza mchango wa wizara katika kuzalisha fedha za kigeni nchini.



Vilevile Taasisi ya Nelson Mandela itashirikiana na Wizara ya Kilimo katika kujenga uwezo wa watumishi na wadau wengine wa sekta ya kilimo kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi kupitia warsha, semina, mafunzo, na ushauri wa kitaalamu kwa wataalamu kutoka pande zote mbili pia kuhakikisha tunaongeza maarifa na ujuzi unaohitajika katika mzingira ya sasa ya kilimo yanayobadilika kwa kasi.



Prof. Kipanyula ameupongeza uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hususani katika sekta ya ya Kilimo kwa mageuzi makubwa yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika na hivyo kupelekea jamii na hasa vijana kujenga imani kuwa kilimo ni shughuli ya biashara kama zilivyo biashara nyingine.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw Gerald Mweli, ameeleza kuwa ushirikiano huo hauna kikomo na utawezesha wataalam mbalimbali wa Wizara ya Kilimo kupata maarifa kutoka Taasisi ya NM-AIST katika utafiti wa kilimo ili kuongeza tija kwa wakulima.

Ameongeza kuwa Taasisi ya Nelson Mandela itasaidia katika sekta ya kilimo katika upatikanaji wa teknolojia bora za kisasa katika kupambana na visufumbufu vya magonjwa yanayoadhiri mazao ya kilimo ambapo itaongeza tija katika uzalishaji wa mazao kwa wakulima.





Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ( kulia) akibadalishana hati ya makubaliano ya ushirikiano na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli ( kushoto) mara ya hafla ya kusaini makubaliano hayo Aprili 14, 2025 Jijini Dodoma.


Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ( kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli ( kushoto) wakionyesha hati ya makubaliano ya ushirikiano mara baada kusaini Aprili 14, 2025 Jijini Dodoma.


Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ( wa pili kulia) akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli ( wa pili kushoto) alipomtembelea ofisini kwake Aprili 14, 2025 Jijini Dodoma.


Wajumbe kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela na Wizara ya Kilimo wakifuatilia mawasilisho wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya mashirikiano Aprili 14,2025 jijini Dodoma.


Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli ( katikati) wakiwa katika picha na washiriki wa hafla ya makubaliano ya ushirikiano iliyofanyika Aprili 14, 2025 Jijini Dodoma.
Share:

KATAMBI AMEKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAJUMBE WA CCM SHINYANGA MJINI


Na; Mwandishi Wetu - DODOMA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi (Mb) amekutana na kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga Mjini walipokutana nao (Siku ya Jumatatu Aprili 14, 2025) jijini Dodoma.

Aidha, Mhe. Katambi amewashukuru wajumbe hao na wananchi wa shinyanga kwa kumuamini na kumpatia fursa hiyo muhimu ya kuwakilisha hivyo ameahidi kuendelea kujitolea kwa ajili ya kukuza Maendeleo ya wananchi wa mkoa huo.

Wageni hao wa Naibu Waziri Katambi watatembelea ukumbi wa bunge tarehe 15 Aprili, 2025 kwa lengo la kushuhudia zoezi la kuhitimisha uwasilishaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wanaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Anold Makombe na Katibu wa CCM Wilaya, Halima Chacha.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 15,2025



Magazeti ya leo
Share:

Monday, 14 April 2025

ALINIITA MSALITI NA KUIKATAA MIMBA


Naitwa Pili kutokea Zanzibar, miaka kama sita iliyopita nilikutana na kijana mmoja anayetokea familia ya kutajiri, tulipendana sana na tulifanya kila kitu, baada ya muda nilibeba ujauzito wake. 

Kwa bahati mbaya, kumbe mwenzangu alikuwa na matatizo tangu kuzaliwa bila mimi kujua na hakuwahi kuniambia, sina hakika ni matatizo gani, ila alikuwa hawezi  kumtungisha mwanamke mimba.

Hivyo nilipomwambia nina ujauzito wake, alikataa kabisa mimba, mimi nilidhani labda uoga tu ila aliendelea kunisisitiza nimtafute mwenye mimba maana sio yake. Huo ndio ulikuwa msimamo wake wa siku zote. 

Kwa kiasi kikubwa nilishangaa sana, nikikumbuka mbona mimi sio mchepukaji kabisa na sijawahi kutembea na mwanaume mwingine zaidi yake na sina kumbukumbu ya kufanya usaliti? imekuaje tena?.

Siwezi kusahau, alinipiga sana yaani akinishtumu kuwa mimi ni msaliti na nimtafute mwenye mimba, alinikataa katu katu kwa asilimia 100, hakunitaka tena kuniona katika maisha yake. 

Wakati sielewi mwelekeo wa maisha, alitokea kijana ambaye ni mwalimu, nashukuru kweli alitokea kunipenda na alinitolea mpaka posa nyumbani kwetu hivyo nikawa nasubiria tu ndoa. 

Siku moja uliingia ugeni mzito pale nyumbani walituweka mtu kati na wazee wao wakisisitiza mimba sio yao na nimtaje mwenye mimba, walisisitiza kuwa mtoto wao ana matatizo na hawezi kumpa mtu mimba hivyo nipambane hali yangu na nisimjue tena.

Acha tu, niliumia sana, mbaya zaidi nilikuwa na uhakika kuwa ni yake na hakuna mtu anayenielewa, sitakaa kusahau nilijifungua kwa tabu kidogo sababu ya stress japo. Yule mwalimu alisema atalea mtoto na hana shida.

 Cha ajabu kujifungua mtoto amefanana sana yule kaka, tena kafanana na baba yake kila kitu, sasa ndugu wakaajua yule ni mtoto wao, hivyo wakataka kumgharamia matuzo kila kitu. 

Yule mpenzi wangu alikuja nyumbani pekee yake na kunieleza kweli alikuwa na tatizo hilo na alienda Hospitali mbalimbali bila kupona, ila aliamua kutumia dawa za mitishamba kwa siri kutoka kwa Kiwanga Doctors bila kuwaambia ndugu zake. Na sasa ameamini kweli dawa za Kiwanga zinafanya kazi vizuri.

Tulikuja kukaa kama familia na kuzungumza kuhusu jambo hilo na mambo yakakaa sawa na sasa tunaishi pamoja na mtoto wetu na siku sio nyingi naweza kusema tunatarajia mtoto mwingine. 

Kutokana na kile alichonieleza mpenzi wangu hapo awali kuwa Kiwanga Doctors kutokea Migori, Kenya ndiye alimpa tiba, nilitaka sana kumfahamu mtu huyo, nilikiingia kwenye tovuti yake na kubaini mambo kadhaa. 

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao, https://ift.tt/MRn5HYm kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 

Share:

Sunday, 13 April 2025

MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU WA WAAMUZI WA MPIRA WA MIGUU TANZANIA 'FRAT' WAANZA

 
Na Hadija Bagasha - Tanga

Mchakato wa  Uchaguzi mkuu wa chama cha waamuzi wa mpira wa miguu Tanzania (FRAT) umeanza rasmi leo April 12 ambapo wanachama wenye sifa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Mwenyekiti ngazi ya Taifa, mjumbe wa mkutano mkuu wa chama cha mpira wa miguu (TFF) , pamoja na nafasi tatu za wajumbe wa kamati ya utendaji wa chama hicho Taifa. 

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya chama cha waamuzi wa mpira wa miguu Tanzania (FRAT) Wakili George Banoba  amewatangazia wananchama wote ambao ni waamuzi wa mpira wa miguu kwamba mchakato wa uchaguzi mkuu umeanza rasmi mapema leo ambapo fomu zitaanza kutolewa hapo kesho April 13 na kwamba zoezi hili litasitishwa April 19 mwaka huu. 

"Taratibu na kanuni za kuzingatia ni kama zilivyo kwenye kanuni za chama niwaombe wananchama wote ambao wanajua wana sifa za kugombea wajitokeze na kugombea, "alisisitiza Wakili Banoba.

Wakili msomi George Banoba amesema kwamba amesema kwamba kama kuna mapingamizi taratibu nyingine zitaendelea lakini pia watafanya usaili tarehe 27 mpaka 29 April mwaka huu ambapo baadae zitaendelea taratibu nyingine za kikanuni. 

"Baada ya hapo tarehe 29 tunategemea kuhitimisha zoezi la kampeni za wagombea baada ya kuwa wametangazwa kwa mchujo utakaokuwa umefanyika kwenye usaili,  tunatarajia uchaguzi uhitimishwe tarehe 30 mwezi Mei mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa chama utakaofanyika pale jijini Tanga, "alisisitiza Wakili Banoba. 

Aidha amebainisha mikakati yao kwamba kama ilivyo kwenye Katiba na kanuni ya chama ni kwamba kazi waliyopewa ni kusimamia mchakato huo wa uchaguzi na mara baada ya uchaguzi kukamilika kitakachofuata ni viongozi wapya kukabidhiwa majukumu yao na baadae kuanza kupitia mpango wa chama uliopo ambao kama wataona unafaa uendelee kutumika na iwapo utaonekana haukidhi basi utahuishwa bila kuathiri malengo ya chama. 


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger