Friday, 21 February 2025

MKATABA UJENZI WA MAABARA ZA SAYANSI OUT, WASAINIWA


Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), kimesaini mkataba na kampuni ya kandarasi ya Arm-Strong International Ltd ya jijini Mwanza kuanza ujenzi wa maabara tatu za sayansi katika kipindi cha miezi nane ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika chuo hiki.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo iliyofanyika Februari 20, 2024, makao makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo na mgeni rasmi katika hafla hiyo, Prof. Joseph Kuzilwa, amesema hii ni hatua kubwa kwani chuo hiki kinaungana moja kwa moja na serikali katika kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya elimu.

“Nchi zenye wanasayansi wengi waliojikita katika maeneo ya utafiti na maendeleo ndiyo nchi zilizopiga hatua kubwa katika maendeleo, kwa kutambua hilo nchi yetu inaelekea huko kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali hii kupitia mradi huu wa HEET ambao sehemu mojawapo ya utekelezaji wake katika chuo hiki ni ujenzi wa maabara za sayansi. Naamini katika utekelezaji wa zoezi hili tutashirikiana pande zote ili fedha za mradi huu zitumike vizuri na kwa wakati,” amesisitiza Prof. Kuzilwa.

Aidha, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Bisanda, amesema mkataba huu unasainiwa hadharani ikiwa ni kusisitiza weledi na uaminifu katika utekelezaji wa mkataba huo ili kufanya matokeo ya mradi huo kuwa na maana kubwa na kuleta maendeleo ya moja kwa moja katika jamii zetu.

“Haya ni matokeo makubwa ya uwekezaji wa serikali yetu, uwepo wa mradi huu wa ujenzi ni sehemu ya maeneo saba ya utekelezaji wa mradi wa HEET. Tunajenga maabara za sayansi sababu tunatambua nchi haiwezi kuendelea au kubadilika bila kuweka msisitizo kwenye sayansi,” amesema Prof. Bisanda.

Naibu Makamu Mkuu wa OUT katika Taaluma, Utafiti na Huduma za Ushauri wa Kataalamu. Prof. Alex Makulilo, amesema utekelezaji wa Mradi wa HEET katika chuo hiki umegawanyika katika vipengele mbalimbali, ambapo asilimia 75 ya mradi mzima zinaenda kwenye ujenzi wa maabara saba katika Kanda saba za nchi ambazo ni Arusha (Kaskazini), Mwanza (Kanda ya Ziwa), Kigoma (Magharibi), Morogoro (Kati), Njombe (Nyanda za Juu Kusini), Mtwara (Kusini) na Pwani (Ukanda wa Pwani).

Ameendelea kusema katika mkataba huu wa awali, Kampuni ya Arm-Strong International Ltd itajenga maabara tatu katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Kigoma. Maabara nyingine zinazosalia zitajengwa na wakandarasi tofauti tofauti ambao mikataba yao itaingiwa hivi karibuni.

Mwanasheria wa Chuo, Wakili Nelly Moshi, ameomba pande zote kuhakikisha zinatekeleza na kufuata sheria zilizowekwa katika mkataba huo ikiwamo umalizaji wa kazi husika ndani ya muda ili kuondoa mivutano isiyo na lazima wakati wa utekeleaji wake.

Naye Ndg. Pastory Masota, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Arm-Strong International Ltd, amesema wao kama watekelezaji wa mradi huo watahakikisha mradi unatekelezwa vyema kama waliyokubaliana katika mkataba na wanatarajia kupata ushirikiano kutoka katika pande zote za wahusika wa utekelezaji wa mradi huo ili fedha za mradi huu zitumike vyema na kwa wakati.

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, ni miongoni mwa vyuo vikuu nchini vinavyotekeleza mradi wa HEET chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia, ambapo chuo hiki kimepata tengeo la thamani ya dola milioni tisa ambalo sehemu mojawapo ya utekelezaji wake ni ujenzi wa maabara za sayansi ambazo mkataba wake umesainiwa na tayari kwa kuanza ujenzi.
Share:

MBUNGE WA MADABA ATEMBELEA KATA YA MKONGOTEMA, AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO


Mbunge Joseph Kizito Mhagama akicheza ngoma iliyoandaliwa na wananchi wa kijiji cha Lutukira na Ndelenyuma
Wananchi wakimshangilia  Mbunge Joseph Kizito Mhagama
Mbunge Joseph Kizito Mhagama akisalimiana na wananchi kata ya Mkongotema

Na Regina Ndumbaro -  Madaba

Mbunge wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Joseph Kizito Mhagama, ametembelea kata ya Mkongotema kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika eneo hilo. 

Ziara hiyo imewapa wananchi nafasi ya kueleza mafanikio yaliyopatikana kupitia utekelezaji wa miradi hiyo.

Katika hotuba yake, Mbunge Mhagama ameishukuru Serikali kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule, zahanati, miradi ya maji safi na salama, pamoja na usambazaji wa umeme katika vijiji mbalimbali.

Akitolea mfano wa mafanikio hayo, Mhagama amekitaja kijiji cha Lutukila kama moja ya maeneo yaliyopokea huduma hizo kwa ufanisi mkubwa. Pia, ameongeza kuwa kijiji cha Ndelenyuma hapo awali kilikuwa na changamoto kubwa, lakini kwa sasa huduma muhimu kama maji, elimu, umeme, ujenzi wa ofisi za kijiji, na miundombinu ya barabara zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa kwa bajeti kiasi cha shilingi bilion na milioni moja na ishirini .

Mwenyekiti wa kijiji cha Ndelenyuma Stanley Ngailo amepongeza juhudi za Mbunge Mhagama kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kijiji chao. 

Ameeleza kuwa wananchi wana imani kubwa naye na wanahitaji aendelee kuwaongoza kutokana na mchango wake mkubwa katika kuwaletea maendeleo.

Wananchi wa vijiji vya Lutukila na Ndelenyuma wameeleza kuridhishwa kwao na juhudi za Mbunge wao, wakisema kuwa kupitia uongozi wake, wamepata huduma bora za elimu, maji safi na miundombinu ya barabara inayorahisisha shughuli zao za kila siku.

Katika kata ya Mkongotema, wananchi wameonyesha furaha yao kwa maendeleo yaliyopatikana. 

Wamesema kuwa hawana deni lolote kwa Mbunge wao kwani ametekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.

Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa wanampenda sana Mhagama na wanatamani hata kumbeba kwa furaha ili kusherehekea mafanikio hayo pamoja naye. 

Hii ni ishara ya mapenzi yao kwa Mbunge wao na kuthamini kazi anayoifanya kwa ajili ya jamii.

Kwa ujumla, ziara hii imedhihirisha jinsi Ilani ya CCM inavyotekelezwa kwa vitendo katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zote za msingi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Share:

DAWA YA UHAKIKA YA HOMA YA UTI WA MGONGO HII HAPA!

Kutana na Hassan Omondi ambaye ni baba mwenye upendo na anayejali wa watoto wake wawili, anafanya kazi kama mwalimu katika shule ya msingi ya eneo la Kibera, kaunti ya Nairobi nchini Kenya. 

Hata hivyo, maisha yake yalibadilika wakati mwanawe, Brian, alipougua ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo ambayo inaweza kusababisha matatizo makubwa, kama vile uharibifu wa ubongo, kupoteza kusikia na hata kifo.

Omondi aligundua kwamba Brian alikuwa na homa kali, maumivu ya kichwa, shingo, kutapika na kuchanganyikiwa, mara moja alimkimbiza hospitali ya karibu ambako aligunduliwa na ugonjwa huo.

Madaktari walimwambia kwamba Brian alihitaji matibabu ya haraka, pia walimwambia kwamba matibabu yalikuwa ya gharama kubwa na kwamba alipaswa kulipa mapema kabla ya kumlaza.

Omondi alihuzunika sana maana hakuwa na pesa za kutosha kulipia matibabu, tayari alikuwa ametumia kiasi kikubwa cha akiba yake kulipa karo ya shule ya bintiye na bili za matibabu za mke wake. 

Alijaribu kukopa pesa kutoka kwa marafiki na jamaa zake, lakini pia nao walikuwa wakihangaika kuhusu ukosefu wa kifedha. Alijihisi mnyonge na asiye na tumaini lolote katika maisha yake. 

Alikaribia kukata tamaa ila alikumbuka kuhusu uwepo wa Kiwanga Doctors, kundi la waganga wa kienyeji ambao wana suluhisho la kila aina ya matatizo yanayoikabili jamii kila wakati, wao huyatolea ufumbuzi ndani ya muda mfupi. 

Omondi alikuwa amesikia habari zao kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake, ambaye alitumia huduma zao kutatua tatizo la ndoa yake, hivyo akamshauri kuwajaribu, na mara moja alichukua hatua ya kuwasiliana nao. 

Kiwanga Doctors walikuwa na huruma kwake na wenye kuelewa mazito aliyokuwa akiyapitia, walimuuliza baadhi ya maswali kuhusu historia ya afya ya mtoto wake, dalili na hali yake ilivyokuwa ikiendelea. 

Kisha wakamwambia kwamba watamsaidia ili kupona ugonjwa huo kwa kutumia mitishamba maalum. Walimhakikishia kwamba huduma zao zilikuwa za ufanisi na za bei nafuu. Na kweli ndani ya muda mfupi mtoto yule aliweza kupona na sasa anaendelea vizuri na masoko yake. 

Kiwanga Doctors wana uzoefu wa miongo kadhaa ya kutibu kwa kutumia dawa kali za mitishamba kuponya magonjwa kama shinikizo la damu, kisukari, vidonda vya tumbo, kisonono, kaswende, TB, miguu kuvimba au kuwaka moto n.k. 

Vilevile hushughulikia matatizo ya jumla kuanzia kushinda kesi za mahakama, kushinda bahati nasibu, ulinzi wa familia na mali na hutabiri kwa usahihi nyota.

Ukiona mambo hayaendi kama unavyotaka, basi usisite kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba +254 769 404965, wataalamu hawa wamesaidia watu wengi ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. 

Mwisho. 

Share:

Thursday, 20 February 2025

TANESCO SHINYANGA YATOA WIKI MOJA KWA WAKULIMA KUONDOA MAZAO KWENYE NJIA KUU YA UMEME


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

TANESCO Shinyanga imetoa onyo kwa wakulima na wananchi wilayani Kahama kuacha kulima mazao kwenye njia kuu ya umeme huku ikiwapa wiki moja wale waliolima kuondoa mazao yao kwenye njia kuu ya umeme ili kuepuka madhara ya umeme.

Hii ni sehemu ya juhudi za TANESCO kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda na kutunza miundombinu ya umeme, ili kuepusha madhara na kuongeza usalama.

Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Bw. Paul Maisori, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wananchi katika kutoa taarifa za watu wanaohujumu miundombinu ya umeme, hususan wale wanaoharibu kwa kuiba vyuma na nati kutoka kwenye nguzo za umeme. 

Amewahimiza pia wakulima kuondoa mazao yao haraka, akieleza kuwa maagizo ya awali yalishatolewa, lakini bado baadhi ya wananchi wamekuwa wakikaidi.

“Watakaobainika kuwa bado na mazao yao kwenye maeneo hayo, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani,” amesema Bw. Maisori.

Kwa upande mwingine, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Victory Senge, amesisitiza kuwa miundombinu ya umeme ni muhimu na inahitaji uangalizi wa pamoja. 
Amefafanua kuwa wananchi walishalipwa fidia kwa maeneo yao, hivyo wanapaswa kuzingatia maagizo ya serikali na kuacha kulima kwenye njia kuu ya umeme ili kuepusha madhara.

TANESCO inasisitiza ushirikiano wa wananchi katika kutunza miundombinu ya umeme, na wale watakaokiuka maagizo watachukuliwa hatua kali za kisheria.


Share:

MBUNGE MSHASHU AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UTENDAJI ULIOTUKUKA



Na Lydia Lugakila- Bukoba

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kagera Bernadeta Kasabago Mshashu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu hassan kwa jinsi alivyoupendelea Mkoa huo na kuupatia Mabilioni ya pesa ambayo yameuwezesha Mkoa huo kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi  pamoja na kuiongoza Nchi kwa umakini mkubwa.

Mshashu ametoa kauli hiyo katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa -RCC kilichofanyika Februari 19,2025 katika ukumbi wa Mkoa huo.

"Tumeona kazi kubwa aliyoifanya Rais wetu tumeona miradi mingi ya kimkakati   tunampongeza Rais Samia hakika ametuheshimisha Kagera"alisema mbunge huyo.

Mshashu Amempongeza pia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajat Fatma Mwassa kwa usimamizi imara katika miradi mbali mbali ya maendeleo Mkoani humo huku akiwapongeza pia  wakuu wa Wilaya pamoja na watendaji mbali mbali ambao wemeweka juhudi zao katika kuuinua Mkoa huo ki uchumi.

Hata hivyo kiongozi huyo amewaomba Wanakagera na Watanzania kumuombea Afya njema Rais Samia ikiwa ni pamoja na kumpigia kura za Kishindo kwa uchaguzi mkuu ujao Mwaka huu.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 20,2025



Magazeti

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger