Monday, 20 January 2025

WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUFANYA UTAFITI WA HALI YA UPATIKANAJI NA MATUMIZI YA NISHATI

Wananchi wa Kitongoji cha Mpazu Wilaya ya Iramba Mkoani Singida wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kufanya utafiti wa hali ya upatikanaji na matumizi ya nishati. ya wilayani humo.

Wametoa pongezi hizo Januari 19, 2025 kwa nyakati tofauti baada ya kufanyiwa mahojiano ikiwa ni moja ya hatua muhimu katika utekelezaji wa tafiti hiyo.

Walisema kuwa hatua hiyo ya utafiti inaonyesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kuweka mipango thabiti ya kuwasogezea huduma muhimu za nishati wananchi wake.

"Tunaipongeza Serikali kwa kufanya utafiti huu, tunaamini matokeo ya utafiti huu yatazalisha miradi itakayotuondolea adha mbalimbali tulizonazo," alisema Gabriel Ndabo.

Alisema kumekuwepo na changamoto ya ukataji ovyo wa miti kwa ajili ya kuni na kwamba kupitia utafiti huo, Serikali itaweka mkakati imara wa kulinda misitu.

Naye Juliana Mtuwa alisema kwa sasa wanatumia zaidi kuni kupikia na kwamba madhara yatokanayo na matumizi ya kuni ni mengi ikiwemo kusababisha madhara ya kiafya.

"Tunachangamoto, tunahitaji maendeleo na utafiti huu ni hatua muhimu ya maendeleo," alisema Bi Mtuwa.

Aliongeza kuwa tarafa hiyo haijafikishiwa umeme na kwamba wanafunzi wanapata tabu kujisomea hivyo kupitia tafiti hiyo Serikali itapata mwanga wa hali halisi ilivyo.

Akizungumzia utekelezaji wa utafiti huo, Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bi Gloria Nkungu alisema huo ni utafiti wa tatu anashiriki na kwamba akilinganisha utafiti uliyopita na huu kuna hatua imepigwa.

"Huu ni utafiti wa tatu wa Nishati ninashiriki, tunaendelea vizuri wananchi wanatupa ushirikiano na kwa baadhi ya maeneo tumeshuhudia mabadiliko makubwa," alisema Bi Nkungu.

Serikali inafanya utafiti wa upatikanaji na matumizi ya nishati katika mikoa yote Tanzania Bara kwa lengo la kubaini hali ya usambazaji na matumizi ya nishati ili kuboresha maisha ya wananchi wake kupitia sekta ya nishati.

Zoezi hili la ukusanyaji wa takwimu kwa ajili ya tafiti ya upatikanaji na matumizi ya nishati lilianza tangu mwezi Desemba 2024 na linatarajia kuhitimishwa mwezi Januari 2025 ili kuendelea na uchakataji wa takwimu zilizokusanywa na Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kutoka mwezi Machi 2025.

Share:

Sunday, 19 January 2025

RASMI MITANO TENA KWA SAMIA!!! KUGOMBEA URAIS 2025, MGOMBEA MWENZA DKT. EMMANUEL NCHIMBI!




Share:

DEREVA ALIYEPOTEA AKUTWA AMEUAWA MWILI UMETUPWA SHIMO LA MAJI MACHAFU, WATUHUMIWA WADAKWA WAKITOROSHA HIACE

Share:

NI WAZI! DR. SAMIA, DR. HUSSEIN MWINYI KUGOMBEA URAIS 2025




Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) leo tarehe 19 Januari 2025 wamepitisha kwa kauli moja Azimio la kuwaridhia Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, kugombea tena nafasi zao katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambapo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ametoa ushauri muhimu kuhusu umoja na uwazi ndani ya chama.

Kikwete amesisitiza umuhimu wa kufuata utaratibu rasmi wa chama kwa kupitisha azimio la kuidhinisha majina ya viongozi hao kama wagombea wa urais.

 Ameweka wazi kuwa ushindi wa CCM katika uchaguzi ujao hauwezi kutiliwa shaka kutokana na mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia na Rais Mwinyi.


“Kama tumekubaliana katika mkutano huu, basi Rais Samia na Rais Mwinyi wanaelekea kuendelea kushika madaraka kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Hata hivyo, ni muhimu tupitishe azimio hili ili tuzingatie kanuni za chama na kuonyesha mshikamano kwa wanachama wetu wote,” amesema Kikwete.


Azimio hilo limezingatia Ibara ya 100(2) ya Katiba ya CCM, inayotaja kwamba Mkutano Mkuu wa CCM ndio chombo cha juu chenye mamlaka ya mwisho katika maamuzi makubwa ya chama.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu walijadili utekelezaji wa Ilani ya CCM, wakionesha kuridhishwa na mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Dkt. Samia na Dkt. Mwinyi. Kufuatia hoja zilizowasilishwa, Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilichukua jukumu la kuandaa Azimio hilo na kulipeleka kwa Mkutano Mkuu ulioketi katika Ukumbi wa JKCC, Dodoma, ambapo wajumbe wote waliridhia kwa asilimia 100.

Kwa kauli moja, wajumbe wameonesha mshikamano na imani kubwa kwa viongozi hawa, wakisifu juhudi zao za kuboresha maendeleo ya wananchi na kukuza uchumi wa taifa.

Share:

WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA UJENZI WA BARABARA ZA LAMI MBAMBABAY


Baadhi ya wakazi wa Mbambabay wakipita barabarani
Barabara ya lami Mbambabay

Na Regina Ndumbaro Ruvuma

Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa juhudi za kuboresha miundombinu ya barabara katika mji mdogo wa Mbambabay kwa kiwango cha lami. 

Wakazi hao wamesema kuwa ujenzi wa barabara hizo umeboresha huduma za usafiri na usafirishaji, kuondoa changamoto za vumbi na matope, na kuongeza thamani ya maeneo yao.

Petro Zambala  ni  mkazi wa Mbambabay amepongeza juhudi za Serikali ya awamu ya sita, akibainisha kuwa ujenzi wa barabara hizo umeongeza kasi ya maendeleo na kuchochea uchumi wa wananchi mmoja mmoja na wilaya kwa ujumla. 

Ameongeza kuwa, kabla ya ujenzi huo, wananchi walipata changamoto kubwa kufika kwenye huduma za kijamii kwa wakati.

Nikaya Mbalale, mkazi mwingine wa mji huo, amesema kuwa fedha zilizotolewa na Serikali zimebadilisha kwa kiasi kikubwa miundombinu ya mji huo. Amesema barabara nyingi za mitaa zilikuwa za vumbi lakini sasa zimejengwa kwa kiwango cha lami, jambo ambalo limevutia wawekezaji wengi na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo.

Mbalale ameeleza kuwa kukamilika kwa barabara ya Mbambabay-Mbinga yenye urefu wa kilometa 66 kwa kiwango cha lami kumeleta unafuu mkubwa kwa wananchi. Nauli ya kutoka Mbambabay hadi Mbinga imeshuka kutoka Shilingi 15,000 hadi kati ya Shilingi 9,000 na 10,000. Hii ni hatua kubwa katika kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji wa bidhaa.

Jackob Madondola amebainisha kuwa, miaka ya nyuma, wananchi walikabiliwa na mateso makubwa kutokana na ubovu wa miundombinu, hususan katika kipindi cha masika. Amesema ujenzi wa mifereji ya kutiririsha maji sambamba na barabara za lami umesaidia kuondoa tatizo la mafuriko na kuwapa wananchi fursa ya kuendelea na shughuli zao za kiuchumi kwa amani.

Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Nyasa, Derick Theonest, amesema kuwa wamebakisha kilometa moja tu ili kukamilisha mtandao wa barabara za lami katika mji wa Mbambabay. Ameshukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha ambazo zimewezesha kuboresha miundombinu, akisisitiza kuwa barabara hizo ni muhimu katika kuchochea maendeleo.

Wananchi wamehimizwa kuhakikisha wanatunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu, kwani imegharimu fedha nyingi. 

Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kuimarisha miundombinu ya barabara kwa manufaa ya wananchi na kukuza uchumi wa maeneo ya vijijini na mijini.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 19,2025




Magazetini



Share:

Saturday, 18 January 2025

STEPHEN WASIRA APENYA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI CCM KUBEBA MIKOBA YA KINANA

Kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, ameteuliwa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa unaoendelea jijini Dodoma leo, Januari 18, 2025.

Jina la Wasira limewasilishwa mbele ya Mkutano Mkuu na limepata baraka za Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana, ambaye alitangaza kupumzika miezi mitano iliyopita.

Wasira, ambaye ni miongoni mwa viongozi wazoefu na wenye ushawishi mkubwa ndani ya chama, anapigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa. 

Uteuzi huu unalenga kuimarisha uongozi wa chama na kuendeleza mipango ya chama hicho katika kipindi kijacho.

Stephen Wasira alizaliwa mwaka 1945
Share:

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO KWA MWAKA WA MASOMO 2025 – BECO PRE & PRIMARY SCHOOL

  

🚨 Beco Pre and Primary School inatangaza rasmi nafasi za masomo kwa mwaka wa masomo 2025! 

BECO ni miongoni mwa shule bora nchini Tanzania na inajivunia mafanikio makubwa katika elimu!

Ufanisi katika Mitihani ya Taifa

  • Mwaka 2021, BECO ilishika nafasi ya 10 kitaifa.
  • Mwaka 2022, 2023 na 2024, BECO imekuwa miongoni mwa shule bora zaidi nchini na imefanikiwa kupata Daraja 'A' bora katika mtihani wa darasa la saba kwa wanafunzi wote.

Faida za Kusoma BECO Pre & Primary School:

👉 Mazingira Bora ya Kielimu

  • Shule yetu ina mazingira bora yanayochangia maendeleo ya mwanafunzi.
    👉 Walimu Bora
  • Tunao walimu wenye ufanisi na weledi katika taaluma zao.
    👉 Mafunzo ya Maadili
  • Tunatoa mafunzo ya maadili mema kwa watoto wa dini zote.
    👉 Usafiri wa Uhakika
  • Tunatoa usafiri wa uhakika kwa wanafunzi wetu.
    👉 Ada Nafuu
  • Ada ni rafiki kwa wazazi, kuhakikisha elimu bora inapatikana kwa gharama nafuu.

Nafasi Zinazopatikana:

  • Chekechea
  • Darasa la Kwanza
  • Wanaohamia madarasa mengine

Shule yetu inapatikana Shinyanga Mjini, nyuma ya Kom Sekondari.

Wasiliana nasi:

📞 0763 157 400
📞 0624 293 323

BECO – The Home of Bright Children!

Share:

WADAU WASHAURI BAJETI YENYE MTAZAMO WA KIJINSIA KUSAIDIA WATOTO NJITI





Mjumbe wa kamati ya Ufundi ya Mtandao wa Afya ya Uzazi, Dkt. Dinner Mbaga, akizungumza

Mkurugenzi Mtendaji wa WFT-T, Bi. Rose Marandu, akizungumza wakati wa mjadala

Na Deogratius Temba, Dar es salaam

Mtandao wa Haki ya afya ya uzazi umeshauri Serikali kutenga bajeti yenye mtazamo wa Kijinsia katika sekta ya afya ili kupunguza mzigo wa gharama za matibabu na utunzaji wa watoto njiti wanapozaliwa.
 
Hayo yamesemwa na wanachama wa Mtandao wa haki ya Afya ya uzazi (SRHR) wakati wa mjadala wa pamoja kuhusu marekebisho ya sheria ya ajira, ambapo mswada wake unatarajiwa kuwasilishwa Bungeni hivi karibuni.
 
Akizungumza mjumbe wa Kamati ya kushughulikia ushawishi na utetezi kwenye mabadiliko ya sheria hiyo, ili kuwapa nafasi wanawake kupata likizo ya uzazi ya kutosha pindi wanapojifungua watoto Njiti, Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Moleli Foundation, Doris Moleli, alisema kwamba suala la uzazi wa mtoto njiiti ni lazima lijadiliwe na jamii kubadilisha mitazamo hasi, lakini kutenga bajeti katika ngazi za kijiji na kata ili zahanati na vituo vya afya viweze kuweka miundombinu na vifaa vya kusaidia kuhudumia watoto njiti katika ngazi hiyo.

“ ….Zanahati zetu na Vituo vya afya huko vijijini zikipewa rasilimali fedha na vifaa vya kuhudumia watoto njiti, itasaidia sana kuondoa tatizo. Wanawake wanaojifungua watoto njiti wanasafiri umbali kutoka vijijini , kutumia muda mrefu kufuata huduma hospitali kubwa na kusababisha umasikini miongoni mwa jamii kutokana na mzigo wa gharama”, alisema Doris.

Doris aliongeza kwamba, endapo serikali itatenga fedha za kutosha kwenye bajeti ya wizara ya afya, hususani katika kuwekeza kwenye kuhudumia mama wanaojifungua watoto njiti, sambamba na ununuzi za vifaa vya kuhudumia watoto hao, itapunguza mzigo wa kazi na kuondoa usumbufu na mzigo wa gharama za matibabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake (WFT-T), Rose Marandu alisema kwamba suala la kutenga rasilimali fedha kwenye bajeti za serikali ngazi zote ni la msingi na litaweza kuondoa kwa kiasi kikubwa umaskini, udhalilishaji na ukatili wa Kijinsia kwa wanawake wanaojifungua watoto njiti.
 
“Mtoto wa haki ya afya ya uzazi una kazi kubwa kuhakikisha kuwa elimu inatolewa kwa jamii, Jamii hasa wanaume ambao ni wadau wakubwa kwenye suala la uzazi washirikishwe kikamilifu na kuelewa wajibu wao ili mwanamke anapojifungua mtoto njiti, asinyanyasike, kudhalilishwa na kufanyiwa ukatili, lakini wanaume wanapaswa kutenga bajeti kwenye ngazi ya familia na kutoa muda wao kumsaidia mwenza kwenye kulea mtoto njiti”, alisema Marandu.

Mapendekezo ya Mtandao wa SHRSR kwenye muswada wa sheria ni kwamba kifungu cha 33 kilichopendekezwa kwamba likizo ya uzazi kwa mama aliyejifungua mtoto njiti, iongezwe na kuanzia wiki ya 36 ya ujauzito ambapo mtoto angepaswa kuzaliwa kawaida, ndipo ianze likizo ya kawaida, iongezwe hadi wiki ya 40 kwasababu wapo wanawake wanojifungua kawaida ambao hufikia wiki ya 40.

“Kifungu kina tija kwa wafanyakazi waliojifungua kabla ya muda ili kuruhusu mzazi kuhudumia mtoto kwa ukaribu ili atengemae ispokua siku zilizotajwa hapo ziongezeke kutoka wiki 36 mpaka wiki 40 kwa sababu za Kiafya hasa makuzi ya mtoto” ,alisema Dkt. Dinna Mbaga, ambaye ni Mjumbe katika kamati ya kiufundi ya Mtandao wa haki ya Afya ya Uzazi.


Share:

Friday, 17 January 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 18, 2025

Share:

Wimbo Mpya : SLYVEPO Ft.SHEDDY THE MIX - ZIMA


Huu hapa wimbo mpya wa Slyvepo akimshirikisha Sheddy The Mix unaitwa Zima
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger