Thursday, 17 October 2024

TUME YAWAPIGA MSASA MAOFISA WA POLISI KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI




Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya siku moja kuhusu sharia za uchaguzi kwa Maafisa Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya nchini. Mafunzo hayo yamefanyika leo Oktoba 17, 2024 jijini Dodoma. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Ramadhani Kingai.
***********
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Maafisa wa Polisi nchini wametakiwa kujenga tabia ya kujikumbusha sheria mbalimbali ikiwemo zinazohusu masuala ya uchaguzi ili kuepuka kuyumbishwa na wanasiasa wanaoamua kupotosha yaliyomo katika sheria hizo kwa maslahi yao binafsi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani wakati akifungua mafunzo ya Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya nchini yaliyofanyika leo Oktoba 17, 2024 mkoani Dodoma.

Kailima amesema, mafunzo ya aina hii ni muhimu kwa kipindi hiki ambacho kuna Sheria Mpya mbili zinazosimamia masuala ya Uchaguzi. Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024 na Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya mwaka 2024.

“Katika sheria zote mbili yapo mabadiliko makubwa katika maeneo mbalimbali ambayo ni muhimu sana kwenu kuyafahamu kipindi hiki ambacho uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga unaendelea na mwakani itakuwa ni uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani,” alisema Kailima.

Aliongeza, mafunzo hayo kuhusu sheria za uchaguzi yana umuhimu na maana kubwa katika maandalizi ya zoezi zima na mchakato wa kuelekea chaguzi zilizopo mbele yetu kama Taifa.

“Uelewa wenu kuhusu sheria hizi, utasaidia sana usimamiaji wa sheria na kuchukua hatua za udhibiti wa uvunjifu wa sheria hizo pamoja na sheria zingine ili watakaokiuka sheria hizo waweze kufunguliwa mashtaka ipasavyo na kuwatendea haki kwa kitakachoamuliwa na Mahakama,” alisisitiza Kailima.

Aliendelea kwa kusema kuwa, anaamini kuwa baada ya mada inayohusu sheria za uchaguzi kuwasilishwa wakuu hao wa upepelezi watakuwa mabalozi wa kuhamasisha wananchi kwenda kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura pindi zoezi linapofanyika katika maeneo yao.

Lengo la mafunzo kwa maafisa hayo ni kuwajengea uelewa kuhusu haki za vyama, wananchi na makundi mengine katika vipindi vyote vya uchaguzi, kwa maana kabla ya uchaguzi Mkuu, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Pamoja na masuala ya Sheria za uchaguzi, washiriki hao ambao ni Wakuu wa Upelelezi walipata kujua wajibu wa Jeshi la Polisi wakati wa uchaguzi, Bank Note Security features, utambuzi wa bidhaa bandia na hatimiliki, upelelezi sambamba na utafiti katika mapungufu ya kisheria.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Ramadhani Kingai (kulia) akifafanua jambo akati wa mafunzo ya siku moja kuhusu sharia za uchaguzi kwa Maafisa Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya nchini. Mafunzo hayo yamefanyika leo Oktoba 17, 2024 jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani.

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bw. Selemani Mtibora akiwapitisha katika maeneo muhimu yaliyomo kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024 na Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya mwaka 2024.
Mkurugenzi wa Daftari na Tehama wa INEC, Stanslaus Mwita akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Ramadhani Kingai wakati wa mafunzo ya siku moja kuhusu sheria za uchaguzi kwa Maafisa Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya nchini. Mafunzo hayo yamefanyika leo Oktoba 17, 2024 jijini Dodoma.

Washiriki wakifuatilia mada


Washiriki mbalimbali ambao ni Wakuu wa Upelelezi Wilaya na Maofisa wengine mbalimbali wakishiriki katika mijadala kuhusu sheria za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.





Share:

TCRA YATOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA MTANDAO KWA WATU WENYE ULEMAVU MKOA WA SHINYANGA


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya Mtandao kwa watu wenye mahitaji maalum Mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea uelewa wa pamoja namna ya kujilinda dhidi ya uhalifu mtandaoni.

Mafunzo hayo yametolewa leo Alhamisi Oktoba 17,2024 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum amesemaTCRA inatekeleza majukumu yake ya kuhakikisha watumiaji wote wa mitandao wakiwemo watu wenye ulemavu wanapata huduma salama na sahihi mtandaoni ikiwa ni utekelezaji wa  Kampeni Kabambe ya 'Ni Rahisi Sana' yenye lengo la kuwahimiza watanzania wote wajilinde dhidi ya uhalifu mtandaoni.

Amesema Kampeni ya Ni Rahisi Sana imelenga kuwahimiza watanzania wote wajilinde dhidi ya uhalifu mtandaoni akieleza kuwa uwepo wa mazingira salama mtandaoni yatawezesha kufikia malengo ya uchumi wa Kidijiti.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum

“TCRA inatoa elimu kuhusu usalama wa mtandaoni kupitia kampeni za uhamasishaji kwa umma ikiwemo hii Kampeni ya Ni Rahisi Sana. Kampeni hii inahusisha jinsi ya kutambua uhalifu mtandaoni, uonevu wa mtandaoni na matapeli. Tunatoa mafunzo juu ya kutumia nywila salama, kujilinda dhidi ya utapeli wa kifedha mtandaoni na jinsi ya kuweka mipangilio ya faragha kwenye mitandao ya kijamii”,amesema Mhandisi Imelda.

Amefafanua kuwa TCRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wanaendelea kudhibiti vitendo vya uhalifu na wanaendelea kutoa elimu ili watumiaji wote wa mtandao wanakuwa salama bila kuwaacha nyuma watu wenye ulemavu ili kuhakikisha wanapata haki sawa za usalama wa taarifa binafsi.

Ameongeza kuwa, TCRA ina wajibu wa kuwalinda watumiaji wote wa mtandao na kupitia juhudi hizi, tunahakikisha watu wenye ulemavu wanaweza kutumia mtandao kwa usalama na bila wasiwasi wa kukumbana na uhalifu au ukiukwaji wa haki zao na imeendelea kutoa njia za kuripoti uhalifu na matukio ya hatari mtandaoni kama vile uonevu, udanganyifu au utapeli. 
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum (kulia) akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni.

Akielezea njia za kuwa salama mtandaoni amesema ni pamoja na kuepuka kutoa taarifa za kibinafsi kwa watu usiofahamu na kutumia njia salama za malipo mtandaoni.

“Usiruhusu kitambulisho chako cha NIDA kumsajilia mtu mwingine laini ya simu na usimpatie mtu yoyote namba ya siri (PIN) ya pesa. Kwenye masuala ya mtandao hakuna mambo ya mwili mmoja ndiyo maana kila mtu anasajili kwa kutumia namba yake ya NIDA.  Hakiki namba zako kupitia *106# ”,ameeleza Mhandisi Imelda.

 Aidha amewashauri watumiaji wa mtandao kulinda taarifa zao kwa kutumia nywila (neno la siri) thabiti akisisitiza kutumia neno la siri tofauti kwa kila akaunti

 “Pia tuwaelimishe watoto juu ya hatari zilizomo kwenye mtandao na jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kwa usalama. Tunza faragha yako binafsi pamoja na ile ya familia yako, epuka kuweka  kwenye mtandao wa kijamii taarifa binafsi kwa kina. Achana na mambo ya kuweka kila kitu chako mtandaoni, kuweka taarifa zako nyingi mtandaoni ni hatari”,ameongeza Mhandisi Imelda.

Wadau wakifuatilia elimu ya Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 

“Usitekeleze maelekezo yoyote kutoka kwa mtu anayejitambulisha kuwa mtoa huduma ikiwa amekupigia kwa namba ya kawaida kwani Mtoa huduma wako wa mtandao wa simu atawasiliana na wewe kwa namba 100 pekee”,ameeleza.

“Ni rahisi sana kumtambua tapeli kwani atakupigia namba ya kawaida badala ya namba 100, Ni rahisi sana kutoa taarifa kwa mtu anayetaka kukutapeli tuma namba yake kwenye namba 15040. Ni rahisi sana kuwasiliana na TCRA endapo una malalamiko yanayomhusu mtoa huduma wako au ukitaka kupata elimu au ushauri wa kutaka kuanzisha biashara ya mawasiliano piga namba ya bure 0800008272”,amesisitiza Mhandisi Imelda.

Aidha ameshauri wahakikishe program za kifaa cha mawasiliano zimeboreshwa (Updated) zimesasishwa.

“Punguza uharaka unapotuma pesa, hakiki namba unayotaka kuitumia pesa. Kabla ya kufanya malipo au kununua bidhaa mtandaoni, hakikisha taarifa za mtu unayemlipa au tumia huduma ya wakala aliyesajiliwa. Usitume pesa kabla ya kupokea mzigo au kuwa na mawasiliano ya uhakika ili kulinda usalama wa pesa zako, usiwe na haraka”,amesema.

“Epuka kufungua fungua, kubofya viunganishi (links)  usivyovifahamu mtandaoni, jiepushe ili kulinda taarifa zako na ukihisi akaunti yako imeingiliwa au kudukuliwa (Hacked) toa taarifa kwa jeshi la polisi”,amesema Mhandisi Imelda.
 Aidha amewataka watumiaji wa mtandao kuepuka kusambaza mtandaoni maudhui yaliyokatazwa kama vile udhalilishaji, uongo, uchochezi au upotoshaji lakini pia wahakikishe kabla ya kusambaza taarifa, wajiridhishe kama ni za kweli na zimethibitishwa kutoka chanzo rasmi kama vile chombo cha habari rasmi au ukurasa rasmi wa taasisi.

“Epuka kusambaza maudhui ya ngono mtandaoni kwa sababu inaweza kusababisha madhara kwa watoto na kuharibu mahusiano. Usikubali kutuma picha za utupu hata kama unampenda kiasi gani. Lile wazo la kupiga picha za utupu, unapiga ili iweje, unazipakua, unazitunza za kazi gani? Huu ni ushetani. Tuwe makini haya mambo ni hatari usiombe yakukute mtu kasambaza picha zako za utupu”,ameongeza.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru TCRA kwa kuwapatia elimu hiyo na kuomba kuendelea kutoa elimu zaidi ili watumiaji wa mitandao wawe salama zaidi.


Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Oktoba 17,2024 Mjini Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum (katikati) akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum (katikati) akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salum (katikati) akitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Ansila Joackim Materu akizungumza wakati TCRA ikitoa elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao kwa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 
Wadau wakifuatilia elimu ya Usalama Mtandaoni : Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao 
Wadau wakipiga picha ya kumbukumbu
Wadau wakipiga picha ya kumbukumbu.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

UZUSHI WA WANAHARAKATI DHIDI YA RAIS SAMIA WAFICHUKA



Katika mazingira ya kisiasa yanayozidi kujaa maneno ya uzushi na habari za kughushi, kundi moja la wanaharakati wanaojificha jijini Nairobi limejikuta katika fedheha kubwa baada ya kujaribu kumchafulia jina Rais Samia Suluhu Hassan na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutumia taarifa za uongo.

Kundi hili linadai kuwa CCM imenunua magari aina ya Toyota Land Cruiser kwa bei ya dola za Kimarekani 200,000 (sawa na shilingi milioni 540 za Kitanzania). Hata hivyo, taarifa hizo zilihusishwa na picha zinazodaiwa kuonyesha magari hayo yakipakiwa katika eneo la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Lumumba, Dar es Salaam.

UKWELI ULIVYO

Baada ya uchunguzi wa haraka kupitia mtandao wa Google, ukweli ulibainika kuwa picha zilizotumiwa na wanaharakati hao si za magari yaliyonunuliwa na CCM, wala hayakuhusiana na Tanzania. Picha hizo zinatokana na makala ya BBC Top Gear yenye kichwa cha habari “This Secret Dealer Is Selling New Old Toyota Land Cruisers That Are Supposed To Save The World.” Magari hayo yameonekana yakiwa yamepakiwa kwenye stoo moja nchini Uholanzi, yakisubiria wateja.

Tukio hili linaonyesha wazi jinsi wanaharakati hao walivyojaribu kutumia mbinu za udanganyifu kueneza habari potofu kwa lengo la kuipaka matope serikali ya Rais Samia. Picha hizo zilikuwa ni za magari ya Toyota 650 ambayo hayahusiani kabisa na Tanzania, achilia mbali UVCCM.

MBINU ZA KUPOTOSHA NA AJENDA BINAFSI

Wanaharakati hawa wamekuwa wakijaribu kwa muda mrefu kumchafua Rais Samia na uongozi wake kwa kueneza taarifa za kughushi. Inaonekana wameishiwa hoja za msingi, na sasa wanatumia mbinu za kutunga hadithi za uongo, huku wakilenga kuendeleza ajenda zao zisizokuwa na msingi wa kweli.

Kile kinachowasukuma wanaharakati hawa ni uhitaji wa fedha kutoka kwa wafadhili wa nje, ambao wanasubiri kuona ajenda inayoendeshwa dhidi ya serikali ya Tanzania. Katika jitihada za kujihakikishia fedha hizi, wanaharakati hawa wamekuwa wakiwalipa vijana wa mitandao ya kijamii ili kusambaza uzushi unaolenga kupotosha umma kuhusu uongozi wa Rais Samia.

KIPAJI CHA UONGO KIMEFIKIA KIWANGO CHA JUU

Mbali na kuwa na ajenda za kisiasa, wanaharakati hawa wanaonekana kuwa na kipaji cha hali ya juu cha kuunda hadithi za uongo. Walakini, badala ya kutumia kipaji hicho kwa manufaa ya jamii, wanakitumia kutunga simulizi za kupotosha ili kuwadanganya wananchi na ulimwengu mzima.

Pengine sasa ni wakati mwafaka kwa wanaharakati hawa kufikiria njia nyingine ya kutumia kipaji chao cha kutunga hadithi. Badala ya kuzusha na kueneza uongo kwa lengo la kupata fedha, wanaweza kutumia uwezo wao huo wa ubunifu kutunga script za tamthilia au filamu, ambazo zinaweza kupata nafasi kwenye runinga au majukwaa ya burudani. Bila shaka, wanaharakati hawa wana uwezo wa kuwa "director" wa uongo, na "Mariawood" inaweza kuwa kiwanda sahihi cha kuzalisha hadithi zao za kufikirika.

HITIMISHO

Kisa hiki cha udanganyifu kinathibitisha jinsi baadhi ya wanaharakati wamepoteza uhalali wa hoja zao na kuamua kuingia kwenye njia ya uongo na uzushi. Taarifa zisizo na msingi kama hizi zinaharibu hadhi ya siasa za Afrika na kuchochea migogoro isiyo na sababu. Ni muhimu kwa jamii kuwa na uwezo wa kuchuja na kuhoji taarifa zinazotolewa na vyanzo visivyo na uhakika, kwani ukweli hauwezi kusimama na uzushi.

Katika nyakati hizi ambapo ukweli na uongo vimechanganyika, tukio hili linatufundisha kwamba uchunguzi wa kina na uhakiki wa taarifa ni muhimu zaidi kuliko wakati wowote. Wananchi wanapaswa kuwa macho dhidi ya propaganda zinazolenga kupotosha ukweli, ili kulinda amani na utulivu wa taifa.

Share:

MRADI WA MAJI NGARA KUNUFAISHA MAELFU YA WANANCHI, HISTORIA NYINGINE KUANDIKWA

 

 Na, Mwandishi wetu - Fichuzi Blog.

Changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama inatajwa kuwa historia kwa siku za usoni kwa wananchi wa Kijiji cha Katerere Kata ya kanazi Wilayani Ngara Mkoani Kagera baada ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ndaisaba Ruhoro kukabidhi mradi wenye thamani ya shilingi Bilion 1.1 kwa Mkandarasi unaotekelezwa na serikali ya awamu ya sita Chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Makabidhiano hayo yamefanyika Oktoba 16, 2024 ambapo Mkandarasi anatarajiwa kuanza utekelezaji huo ndani ya siku saba ambao utatekelezwa kwa kipindi kisichozidi miezi nane ukiwa na lengo la Kumtua mama ndoo kichwani ambapo mara baada ya kukamilika wanatarajia kuingiza maji kwa kaya 100.


Mradi huo ambao ni neema kwa wananchi hao ni baada ya Serikali kufanya juhudi za muda mrefu za kuchimba visima ambavyo juhudi ziligonga mwamba kwa kukosa maji na hatimaye suluhisho limepatikana.


Ndaisaba amewataka wananchi kutunza mradi huo ili uweze kuwahudumia kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kumtaka mkandarasi huyo kufanya kazi nzuri ili kutimiza mkakati wa Serikali ya kuhakikisha mwananchi anapata huduma zote muhimu kwa wakati.


Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata hiyo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Ngara kwa kufanikisha mpango wa wananchi kupata maji safi.














Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger