Thursday, 26 September 2024

SERIKALI INAENDELEA KUBORESHA BARABARA ZA KAVUU


Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameshiriki kikao cha halmashauri ya CCM kata ya Mamba wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

Katika kikao chake Mhe. Pinda aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo, namna serikali ya Awamu ya Sita inavyotekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya jimbo la Kavuu.

Ametolea mfano wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya barabara ambapo amesema barabara ya urefu wa Km 1 kutoka Mamba kuelekea Kasansa hadi Majimoto inakwenda kutengenezwa katika kiwango cha lami.

Mhe. Pinda ameweka wazi kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza kasi ya ukuaji maeneo mbalimbali sambamba ufikiaji eneo moja kwenda lingine ikiwa pamoja na urahisi wa kusafirisha mazao na kurahisisha utoaji wa huduma za jamii katika jimbo hilo.

"Lakini pale majimoto upande wa viwandani kwa sababu ndio uchumi wetu uko pale tupitishe barabara ikaguse upande wa pili wale wafanyabishara wetu wawe na amani na hata nyie mnapotoa mazao kule sehemu ya lunguya ukifika pale pawe na ulaini wa kupitisha mazao yetu" amesema mhe. Pinda.

Naye, Katibu wa Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama hicho ndugu Renatus Kamaneja amewahimiza Madiwani wote ni jukumu nlao la kwanza kuendelea kuisemea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zao.

Mhe. Geophrey Pinda yupo katika muendelezo wa ziara yake iliyoanza tarehe 25 Sept 2024 na kukamilika Oktoba 4, 2024 ambapo atatembelea kata zote ndani ya jimbo la Kavuu.

Share:

DR. MLACHA : WANANCHI TEMBELEENI VITUO VYA AFYA MPIME HOMA YA INI

Na George Mganga, SHINYANGA RRH

WANANCHI wa Mkoa wa Shinyanga pamoja na maeneo jirani wametakiwa kutembelea vituo vya afya kwa ajili ya kupima afya zao hususani Homa ya Ini, ili kuepukana na changamoto za kiafya ikiwemo kansa ya ini na kifo.

Hayo yamesemwa Septemba 25, 2024 na Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Peter Mlacha, wakati akitoa elimu ya ugonjwa huo kwa watumishi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga.

Mlacha ameeleza maambukizi ya ugonjwa huo yanasababishwa na virusi ya Homa ya Ini, ikichagizwa zaidi na ngono zembe, kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto pia kwa mfumo wa majimaji (kukumbatiana na mtu mwenye jasho).

“Tujitahidi kufanya vipimo ili kujua hali ya afya zetu, huu ugonjwa namna unavyoambukiza ni sawa na virusi vya UKIMWI.

“Ukishapima na ukagundulika uko salama utapata chanjo na utaishi salama”, amesema Dkt. Mlacha.

Aidha, Mlacha amesema takwimu zinaeleza kuwa utafiti uliofanyika, zaidi ya asilimia 95 ya waliopata chanjo ya Homa ya Ini hawajafanikiwa kupata maambukizi ya ugonjwa huo ambao umekuwa na athari kubwa ikiwemo Kansa ya Homa ya Ini.

Ameainisha baadhi ya athari ambazo zinaweza kumpata mtu mwenye ugonjwa huo ukiachilia Kansa ya Ini, ni ini kutofanya kazi yake, lakini vilevile inaweza pelekea mtu akapoteza uhai.

Ili kujikinga, Mlacha amewasihi wananchi waepukane na ngono zembe, kuwa na wapenzi wengi, kufanya ngono salama na muhimu zaidi kupata chanjo mapema kwa ajili ya kuepukana na homa hiyo.

Mlacha pi ameeleza rika ambalo linapaswa kupata chanjo mapema zaidi, na ambalo lina hatari kubwa ya kupata maambukizi, ni kundi la vijana kuanzia umri wa miaka 14 na kuendelea.

Halikadhalika, ili kutokomeza na kuzuia maambukizi ya Homa ya Ini, Mlacha anawapa wito wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga na maeneo mengine kuhakikisha wanafika kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kupima.

Amehitimisha kwa kueleza ugonjwa wa Homa ya Ini hauna TIBA, bali una dawa zinazosaidia kufubaza makali ya virusi hivyo ili visisababishe athari zaidi kiafya.

Share:

RC SINGIDA ABORESHA TAARIFA ZAKE KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA


Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Halima Dendego akionesha Kadi yake ya Mpiga Kura baada ya kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linaloanza Uboreshaji Septemba 25,2024 na litadumu kwa siku saba mkoani Singida hadi Oktoba mosi mwaka huu.


Mkuu wa Mkoa aliboresha taarifa zake katika Kituo cha Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye ulemavu Sabasaba leo Septemba 25,2024.


Akixungumza baada ya kumaliza uboreshaji, Mhe.Dendego aliwahimiza wananchi wa mooa wa Singida kujitokeza kwa wingi kujiandikisha lakini pia kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati huu ambao Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeweka kambi mkoani humo.


Amesema ni muhimu kila mwanasingida mwenye Sifa kujitokeza na kujiandikisha ili apate fursa ya kujiandikisha katika Daftari hilo ili apate fursa ya kuchagua viongozi anaowataka wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar (kushoto) akiangalia kadi ya Mpiga Kura aliyokabidhiwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego mara baada ya kuboresha taarifa zake katika Daftari la Wapiga Kura katika uboreshaji ulioanza jana mkoani Singida.Wananchi wa Mkoa wa Singida wameanza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Septemba 25, 2024 hadi Oktoba 1, 2024.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar (katikati) akishudia Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akichukuliwa taarifa zake na Mwandishi Msaidizi Failuna Bira wakati mkuu huyo wa mkoa alipofika katika Kituo cha Chuo cha ufundi na Marekebisho kwa watu wenye ulemavu Sabasaba,Kata ya Utemini, Manispaa ya Singida. Wananchi wa Mkoa wa Singida wameanza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Septemba 25, 2024 hadi Oktoba 1, 2024.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego (kulia) akichukuliwa picha na Mwendesha Vifaa vya Biyometriki (BVR), Christina Isaya aliyepo Kituo cha Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye ulemavu Sabasaba leo Septemba 25,2024 katika siku ya kwanza ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoa wa Singida. Katikati ni Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akishuhudia.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego (kushoto) akiweka saini katika kadi yake ya Mpiga Kura kupitia kishkwambi cha BVR. Mkuu wa Mkoa aliboresha taarifa zake katika Kituo cha Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye ulemavu Sabasaba leo Septemba 25, 2024.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar leo ametembelea vituo kadhaa na kushuhudia wananchi mbalimbali wakijiandikisha na kuboresha tarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.


Uboreshaji wa Dafrati la Kudumu la Wapiga Kura umeanza leo Septemba 25, 2024 na utadumu kwa siku sana hadi Oktoba 1 mwaka huu.


Wananchi wakiwa katika vituo vya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuboresha taarifa zao na kujiandikisha katika Daftari hilo mkoani Singida.


Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar leo ametembelea vituo kadhaa na kushuhudia wananchi mbalimbali wakijiandikisha na kuboresha tarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Share:

Wednesday, 25 September 2024

WANANCHI WASEMA MAANDAMANO HAYANA TIJA




Kufuatia kutofanikiwa kwa maandamano yaliyokuwa yamepangwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wananchi wameendelea kulaani vikali mipango hiyo ambapo wamesema kuwa suala la maandamano halina tija katika maendeleo ya taifa hivyo wananchi wajitume ili kukuza uchumi wa nchi.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa wananchi waache tabia ya kufuata mikumbo kutoka kwa baadhi yao wasio na nia njema kwani maandamano yamekuwa yakileta hasara kubwa ambapo wametolea mfano maandamano yaliyofanyika nchi jirani ya Kenya.


"Mwananchi usiongozwe na mwenzako, ukafuata akili ya mwenzako kwenda kuandamana sote tumeona nafkiri tumeangalia habari kutoka nchi ya jirani kenya wananchi vile wamepoteza maisha na hakuna kitu walichoambulia usifuate ushauri wa mwenzako akakupa ushauri mbaya mkaandamana".

Vilevile wameeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa chadema hawakufuata sheria katika maandamano hayo na vilevile vijana wamekuwa wakiliowpwa kwa ajili ya kuandamana kutokana na ukukosa kipato hivyo ni vyema kwa vijana nchini kufanya kazi kwa bidii ili kuepuka kushawishiwa.

"Inaonekana kabisa CHADEMA hawakufuata sheria mbnona mikutano ilikuwa ninafanyika enzi na enzi, nchi yetu ni ya amani sasa vichocezi vidogovidogo visije vikatuweka kwenye sehemu mbaya, vijana wajitume wafanye kazi, ukitaka upate kirahisi ndio mwisho wa siku mnachukuliwa vijana 1000 mnalipwa kiasi fulani twendeni tukaandamane, mnaanzisha fujo"


Itakumbukwa kuwa Septemba 11, 2024 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa na mauaji, yakiwemo ya makada wake, lakini Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku maandamano hayo yaliyotarajiwa kufanyika Septemba 23
Share:

RAIS SAMIA AZINDUA JENGO LA OFISI YA MKURUGENZI MBINGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga mkoani Ruvuma tarehe 25 Septemba, 2024.
Share:

POLISI SHINYANGA WADAKA WATUHUMIWA 55, MALI MBALIMBALI ZA WIZI


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Kennedy Mgani akizungumza na waandishi wa habari - Picha na MALUNDE
Katika kuhakikisha Usalama waa raia na mali zao, Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa kushirikiana na Jamii pamoja na vyombo vingine vya ulinzi katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu kwa kufanya doria, misako, operesheni na kutoa elimu kwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Septemba 25,2024 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Kennedy Mgani amesema  kuanzia Agosti 22, 2024 mpaka Septemba 24, 2024 Jeshi la Polisi Mkoa wa  Shinyanga  limefanikiwa kukamata watuhumiwa 55 pamoja na vielelezo mbalimbali.

Amevitaja vielelezo hivyo kuwa ni mafuta ya petroli lita 55, mitungi 05 ya gesi, tairi 02 za gari, Pikipiki 05, simu 09, Redio 02, Boksi 10 za pombe aina ya roboti, Seti ya CCTV CAMERA, TV 03, Jenereta 01, pombe ya moshi lita 10, mtambo 01 wa kutengeneza pombe ya moshi, Laptop 01 na vifaa mbalimbali vya kupiga ramli chonganishi.


Kwa upande wa mafanikio ya kesi mahakamani, amesema jumla ya kesi 19 zimepata mafanikio ambapo kesi 01 ya kulawiti mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha maisha jela, kesi 02 kubaka washtakiwa 02 walihukumiwa miaka 30 jela, kesi 02 unyang'anyi wa kutumia silaha washtakiwa 02 walihukumiwa miaka 29 na miezi 05 jela, kesi 02 za kula njama washtakiwa 07 walihukumiwa miaka 13 jela kesi 01 kupatikana na madawa ya kulevya aina ya bhangi mshtakiwa alihukumiwa miaka 02 jela.


Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni kesi 01 ya gari kumgonga mpanda baskeli na kusababisha kifo mshtakiwa amefungiwa leseni kwa kipindi cha miaka mitatu, kesi 05 za kuingia kwa jinai washtakiwa 06 walihukumiwa miaka 03 jela, kesi 01 wizi wa mtoto mshtakiwa alihukumiwa mwaka mmoja na nusu jela, kesi 01 kupatikana na noti bandia mshtakiwa alihukumiwa mwaka 01 jela na kesi 03 za wizi washtakiwa 03 walihukumiwa miezi miwili mpaka sita jela. 

"Lakini pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kupitia kikosi cha Usalama barabarani limefanikiwa kukamata jumla ya makosa 5,048 kwa mchanganuo ufuatao;- makosa ya magari ni 3,460 na makosa ya bajaji na pikipiki ni 1,588 wahusika waliwajibishwa kwa kulipa faini za papo kwa hapo",amesema Kamanda Mgani.

Akizungumzia kuhusu utoaji wa elimu, amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kufanya jumla ya mikutano 41 ya uelimishaji kwa jamii ikiwemo shuleni, mikutano ya hadhara na vikundi 34 vya ulinzi shirikishi vimepatiwa elimu ya ukamataji salama wa wahalifu kwa kuzingatia haki za binadamu pia waendesha pikipiki maarufu bodaboda wameelimishwa kuzingatia taaluma yao waliyoipata pindi wawapo vyuoni katika uendeshaji salama na kuzingatia Sheria za Usalama barabarani wakati wanapotumia vyombo vya moto.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaishukuru jamii kwa kuendelea kupokea elimu inayotolewa kwa ushirikiano madhubuti katika kuhakikisha Usalama wa Mkoa wa Shinyanga unakuwa shwari sambamba na kupokea elimu inayotolewa, pia linatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutii na kufuata Sheria, taratibu na kanuni za nchi',ameongeza.



Share:

CHALINZE KUONGEZA ZAIDI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Mwalimu mkuu, Gema Kinyange akitambulisha walimu wake
Mgeni rasmi, meneja wa CRDB Tawi la Chalinze, Bw. Boniphace Shija
Diwani wa kata ya Bwilingu, Bw. Nasser Karama
Mwenyekiti wa kamati ya shule , Bw. Abraham Dauson


NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE.
KATA ya Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze mkoa wa Pwani imepania kuongeza shule kutokana na mahitaji ya jamii husika.

Hayo yamesemwa na Diwani wa Kata ya Bwilingu, Mh. Nasser Karama alipokuwa akihutubia katika mahafali ya kwanza ya darasa la saba katika shule ya msingi Ridhiwani Kikwete mjini hapa jana. 

Mh. Nasser amesema bado jamii ya kata yake inahitaji huduma zaidi katika elimu, ila katika hatua inayofuata watajenga shule ya sekondari eneo la Chalinze Mzee na shule nyingine ya msingi eneo la Koo  katika kata ya Bwilingu.

Diwani Nasser amesema kwa kufikia hatua hiyo kata ya Bwilingu itakuwa na shule 13 za msingi na shule 5 za sekondari.

Akijibu risala ya shule hiyo ,mgeni rasmi meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Chalinze Bw. Boniphace Shija amesema benki inakwenda kujenga jiko kwaajili ya huduma shuleni huku mahitaji mengine ikiwa pamoja na  mashine ya fotokopi na ujenzi wa nyumba za walimu utasubiri hadi taasisi yake itakapopata uwezo.

"Ombi la ujenzi wa jiko la shule tunakwenda kushughulika nalo, ila huduma zingine zinahitaji muda na bajeti zaidi",alisema mgeni rasmi huyo.

Akimkaribisha mgeni rasmi kuzumgumza, Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Bw. Abraham Dauson aliipongeza benki hiyo kwa kuipa shule meza na viti 50 bila kusahau kuwasaidia mfumo wa umeme shuleni hapo kwa siku za hivi karibuni.

Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi. Gema Kinyange amewaambia wazazi kuwa wajiandae kupeleka watoto wao kidato cha kwanza mwakani, kwani ana imani kubwa na kazi iliyofanywa na walimu wake katika ufundishaji.

Jumla ya wanafunzi 96 wamehitimu elimu ya msingi katika shule hiyo kwa mwaka 2024.

Share:

Tuesday, 24 September 2024

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA MAJI MKOANI RUVUMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024. 
Muonekano wa ujenzi wa Mradi wa maji Mtyangimbole uliopo katika eneo la Kibilang’ombe, Madaba mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya mradi wa maji wa Mtyangimbole uliopo katika eneo la Kibilang’ombe, Madaba mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la Msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma leo Septemba,24 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma leo Septemba, 24 2024.
Share:

KAFULILA ATANGAZA MAGEUZI MAKUBWA VIVUKO, KARAKANA ZA SERIKALI

* TEMESA kushirikiana na sekta binafsi kwenye uendeshaji wa karakana, vivuko na ukodishaji wa mitambo

Septemba 24, 2024

Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam

Wakala wa Ufundi na Umeme wa Tanzania (TEMESA) imepanga kuendesha vivuko, karakana na mitambo ya kukodishwa kwa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuongeza ufanisi, ubunifu, ujuzi na teknolojia mpya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP Centre), David Kafulila, amesema kuwa utekelezaji wa miradi ya taasisi za umma kwa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi umeibuka kuwa njia sahihi na muhimu inayosaidia uanzishaji au utekelekezaji wa miradi ya taasisi za umma. 

"Kwa siku za hivi karibuni, idadi ya taasisi za Umma zinanzovutiwa kutekeleza miradi yake ya maendeleo kwa njia ya ubia kati ya setka ya umma na binafsi, imekuwa ikiongezeka jinsi muda unavyozidi kwenda," Kafulila amesema.

Sasa ni zamu ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA). 

Wakala huu umetangaza fursa adhimu kwa wawekezaji binafsi wa ndani nan je ya nchi kuonyesha nia ya kuwekeza, kuboresha na kuendesha karakana zake kupitia njia ya Ubia. 

Kama invyofahamika na kwa mujibu wa sheria iliyoianzisha wakala huu, TEMESA ina jukumu la kufanya matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo ya Serikali katika karakana ambazo zipo kila mkoa. 

Vile vile, inafanya shughuli za uendeshaji wa vivuko vya Serikali na kukodisha mitambo kwa wadau wanaofanya shughuli za ujenzi wa miundombinu. 

TEMESA inasimamia mtandao wa karakana 30 katika mikoa 26 nchini, ambazo kwa wastani zinahudumia magari takriban 29,263 kwa mwaka. 

Pia, TEMESA inakarabati na kuhudumia magari ya serikali yapatayo 9,183, pikipiki 12,778 na vifaa au mitambo 433. Aidha, TEMESA inaendesha vivuko 32 katika mikoa 12 na maeneo ya kuvuka 22 kote nchini. 

Takriban abiria 79,863 na magari 3,696 hupita katika vivuko hivi kila siku. Serikali inajenga vivuko vipya nane ambapo vitano vitafanya kazi katika Ziwa Victoria na vitatu katika Bahari ya Hindi. 

"Fursa nyingine za uwekezaji zilizopo kwenye vivuko hivi ni pamoja na ardhi, majengo na miundombinu muhimu kama sehemu za kusubiria abiria, migahawa, ofisi na mifumo mbalimbali," amesema Kafulila.

Pia, Wakala unamiliki mitambo ya aina mbalimbali 41 kwa ajili ya kukodisha kwa wateja kwenye sekta za umma na binafsi. 

Katika nia za kuimarisha ufanisi na ubora, TEMESA imedhamiria kuendesha karakana zake kumi na tatu (13) kwa njia ya ubia. Karakana hizi ziko katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Shinyanga, Kagera, Singida, Iringa, na Mara. Nyingine zipo katika mikoa ya Manyara, Pwani, Lindi, Ruvuma, Njombe, na Simiyu. 

Vile vile, wakala unakusudia kuendesha huduma zote za vivuko nchini kupitia kwa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP). 

Mwekezaji ataruhusiwa kukodisha huduma za kivuko chote, kuunda kampuni ya ubia na TEMESA, au kuendesha vivuko vyake sambamba na vivuko vya TEMESA. 

Aidha, wakala unakusudia kumshirikisha mwekezaji binafsi katika kutoa huduma za ukodishaji wa vifaa kwa njia ya ubia kati ya TEMESA na mwekezaji. 

Hatua hii ya kimapinduzi ya TEMESA inaungwa mkono kikamilifu na mfumo wa kisheria wa utekelezaji wa miradi kwa njia ya ubia, ambapo Kanuni za 36 (b) & (d) za Kanuni za Ubia kati ya sekta ya umma na binafsi za mwaka 2020 kama zilivyorekebishwa mwaka 2023, zinairuhusu TEMESA kuwaalika wawekezaji katika utekelezaji wa miradi yake kwa njia ya ubia. 

"Mpango wa TEMESA wa kuboresha karakana zake, vivuko na kutoa huduma ya ukodishaji mitambo kwa njia ya Ubia unatoa matumaini ya kukidhi mahitaji makubwa ya huduma hizi yaliyopo kwenye soko," amesema.

Ushirikishwaji wa wawekezaji utaleta manufaa mengi ikiwepo kuvutia teknolojia za kisasa, kuchochea ufanisi wa uendeshaji wa karakana na vivuko pamoja na kuboresha ubora wa huduma za Wakala kwa ujumla wake. 

Kituo cha Ubia kati ya sekta ya umma na binafsi, chini ya uongozi mahiri wa Mkurugenzi Mtendaji wake, David Kafulila, kimekuwa ni kiungo muhimu katika kusaidia taasisi za Umma kubuni miradi inayofaa kutekelezwa kwa njia ya ubia. 

Tangu Kituo cha Ubia kilipoanzishwa rasmi mapema mwaka huu, nchi imeshuhudia mabadiliko makubwa kwenye uratibu wa miradi kwa njia ya Ubia. 

"Mageuzi makubwa yatazidi kutokea katika miradi ya ubia baada tu ya Kituo kufikia adhma yake ya kutoa huduma zote za ubia ndani ya Kituo (one-stop centre)," amesema Kafulila.

Share:

JAJI MSTAAFU MWANGESI : HAUWEZI KUWA MWANGALIZI WA MAADILI YA WATU WENGINE KAMA WEWE HUNA MAADILI




Kamshina wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi ,akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Cate mjini Morogoro.

......

Rai imetolewa kwa Watumishi wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na weledi wa hali ya juu wanapotekeleza majukumu yao.

Rai hiyo imetolewa na Kamshina wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Cate mjini Morogoro.

‘’Hauwezi kuwa mwangalizi wa maadili ya wengine wakati wewe mwenyewe hauna maadili, hivyo kama mfanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma unatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na watumishi wengine wa Umma katika nyanja ya uadilifu,’’alisema Mhe. Mwangesi.

Jaji (Mst.) Mwangesi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wafanyakazi wa ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ameongeza kuwa uadilifu unajengwa kwa nguzo kuu tatu.

Alizitaja nguzo hizo kuwa ni utaalamu, uaminifu na uwajibikaji na kuongeza kuwa ni wajibu kwa kila mtumishi wa Sekretarieti kuzingatia nguzo hizo.

‘’Ninawaasa kuzingatia nidhamu na kujituma katika kutekeleza majukumu yenu na yeyote atakayeenda kinyume na hayo, atakua si miongoni mwetu na hatutasita kumchukulia hatua kutokana na mwenendo wake,’’alisema.

Katika hatua nyingine, Kamishna huyo wa Maadili, amezungumzia umuhimu wa watumishi kutunza na kulinda rasilimali za Taasisi na kuacha uzembe katika matumizi ya mali na vitendea kazi vya ofisi kutokana na upatikanaji wake kuwa wa gharama.

‘’Niwaombe kuacha uzembe na kuwa makini katika matumizi ya vitendea kazi na kuvitunza kwa hali na mali kwani vitendea kazi tulivyonavyo ni vichache na upatikanaji wake ni washida sana,’’amesisitiza.

Kuhusu kuufanyaji kazi kwa ushirikaiano, Mwenyekiti huyo wa Baraza la Wafanya kazi, aliwapongeza watumishi wa Sekretarieti ya Maadili kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kuomba hali hiyo iwe endelevu na amesisitiza kuwa kwake milango ipo wazi kwa yeyote mwenye jambo kumuona na kujadili kwa pamoja.

‘’Niwapongeza kwa ushirikiano wenu katika utendaji kazi na ninawaomba ushirikiano huo mnaonionyesha mimi pia uwe endelevu miongoni mwenu ili tuweze kuifikisha mbali Taasisi yetu,’’ alisisitiza.
Share:

Monday, 23 September 2024

ASINGIZIWA AMEBAKA BAADA YA KUMNYIMA FEDHA MSICHANA WAKE

Ilikuwa afueni kwa mwanaume moja aitwaye Isaac kutoka katika kaunti ya Busia baada ya kuachiliwa na mahakama moja huko Kisumu, alikuwa akihutumiwa kumbaka msichana mmoja wa shule mwaka wa 2016.

Kulingana na jamaa zake, msichana huyo alikuwa na uhusiano na ndugu yao ila mambo yakabadilika kwani alikata matakwa ya kidosho huyo ya kumpa fedha fulani, ndipo wakaamua kumsingizia kesi ya uongo.

Kesi yake ilikuwa ikiahirishwa kila mara, jamaa alibaki kuhangaika rumande, familia yake vile vile ilikuwa na mshangao ni vipi jamaa wao anatuhumiwa kufanya ubakaji ilhali msichana huyu alikuwa amekubali kushiriki naye mapenzi. 

Mwisho wa siku Jamaa huyp alitoka rumande akiwa myonge sana na ilikuwa shangwe na nderemo kwa ndugu zake ambao walikuwa wamekaa muda mrefu bila kumuona kijana wao.

Kwa mujibu wa Baba ya Jamaa huyo, alienda kutafuta usaidizi kwa mtaalam wa tiba asilia, Dr Bokko ambaye alifanya mshukiwa kishinda kesi.

Siku hiyo kwenye uamuzi wa kesi, Jaji alisema kwamba jama yule aachiliwe huru kwani kesi ile haikuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani. 

Pia Dr Bokko hutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, msukomo wa damu, kifafa n.k, husuluhisha shida za kifamilia kama kutokuwa na uwezo wa kupata mtoto, kutopata mchumba au mwenza wa maisha n.k. Piga simu +255618536050.

Mwisho.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger