Wednesday, 18 September 2024

WAZIRI JAFO ATAKA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KILWA KUKAMILIKA KWA WAKATI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

Na.Mwandisi Wetu.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Selemani Jafo amewashauri wananchi wa wilaya ya Kilwa kushikamana na kusimamia Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa wilayani humo ikamilike kwa wakati na iendane na gharama halisi ili kutimiza Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha wananchi hao wananufaika na miradi hiyo.


Dkt.Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara Maalum Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na kuongea na Wananchi wa Maeneo hayo ikiongozwa na Kauli Mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

Waziri Jafo ameliagiza Shirika la Umeme (TANESCO ) kuhakikisha mradi wa nyumba za walimu (Two in One) zilizopo Kata ya Somanga zinapata umeme na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanajenga barabara nzuri ndani ya miezi miwili ili kuweka mazingira bora ya kuishi na kufanya kazi kwa ufanisi kwa Walimu hao.


"Naielekeza Mamlaka ya Maji Kilwa Masoko (KIMUWASA) inayosimamia Mradi wa maji katika vijiji vya Mavuji, Nangurukuru, Singino, Kivinje, Mpara na Masoko uliopo Wilayani Kilwa kusimamia Mradi huo kukamilifu na kuandaa Mpango unaonesha Mradi huo utakamilika lini na kuwasilisha katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi ndani ya Wiki mbili (2) ili kuhakikisha Mradi huo unaleta manufaa yanayotarajiwa kwa Wananchi wa Kilwa."amesisitiza Dkt.Jafo

Aidha, Dkt Jafo amebainisha kuwa ujenzi wa Mradi wa Bandari ya Uvuvi unaolenga kurahisisha upatikanaji wa Samaki, Soko na kukuza biashara uchumi kwa ujumla pamoja ujenzi wa Kituo cha Afya cha Njinjo, Kipimimbi unaendelea kwa kasi , unaendana na gharama iliyopangwa na hivyo kufikia malengo yanayotarajiwa na Wananchi wa Kilwa.

Akiongea na Wananchi wa Kipimindi Wilayani Kilwa Dkt Jafo amewapongeza wananchi wa Wilaya hiyo kwa kutumia Mfumo wa stakabadhi gharani hususani katika mazao ya ufuta na mbaazi na kupata mafanikio makubwa katika kuuza mazao hayo ndani na nje ya nchi kwa bei inayoridhisha na kuchangia katika kukuza biashara na kuongeza pato la Taifa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani humo inayolenga kuleta manufaa makubwa kwa Wananchi wa Mkoa huo na kuwaomba kutumia fursa za miradi hiyo ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili mkoani Lindi kwa jaili ya kufanya ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Kilwa, Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Somanga iliyopo Kata ya Somanga, alipotembelea Shule hiyo kujionea Mradi wa ujenzi wa nyumba za Walimu (two in one) wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".





Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakikagua ujenzi wa Mradi wa Maji mavuji,Nangurukuru,Singino,Kivinje,Mpara ,Masoko uliopo wilayani Kilwa wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".




Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi wa Kipimindi wilayani Kilwa baada ya kutembelea ujenzi wa Kituo cha Afya cha Njinjo Mkoani humo wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

Share:

MKOA WA TABORA TUMEPIGA VITA MAFUNDI UMEME VISHOKA”-RAS TABORA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt John Mboya, akizungumza wakati akifungua semina ya siku moja kwa mafundi umeme wa mkoa huo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Paul Matiko Chacha, leo Septemba 17,2024.
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Walter Christopher akizungumza na wadau wa sekta ndogo ya umeme wakiwamo mafundi, wakandarasi na wawakilishi wa taasisi mbalimbali wakati wa semina ya kuwajengea uwezo mafundi umeme wa mkoa wa Tabora.



MAFUNDI umeme wakimsikiliza Katibu Tawala wa Tabora, Dkt John Mboya wakati wa semina kuhusu utekelezaji wa sheria na kanuni za ufungaji umeme za mwaka 2022 iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) mkoani Tabora.

Na.Mwandishi Wetu

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt John Mboya, akifungua semina ya siku moja kwa mafundi umeme wa mkoa huo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Paul Matiko Chacha, leo 17 Septemba 2024,amewasihi mafundi umeme wote mkoani humo kuhakikisha wanakuwa na leseni za ufungaji mifumo ya umeme zinazotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa mujibu wa Kifungu cha. 8 (h) cha Sheria ya Umeme,Sura Na. 131.

“Kuanzia leo, mkoa wa Tabora tumepiga vita mafundi vishoka, na ni imani yangu kwamba baada ya semina hii kila asiye na leseni ataomba leseni ili afanye kazi kwa uhalali, ninawasihi sana tusipoteze fursa hii kwani mkoa wetu una miradi mingi ambayo ni fursa kwa mafundi umeme na kuanzia sasa vishoka wote hawatapewa kazi mpaka pale watakapokuwa na leseni ya EWURA,” alisema.

Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi Walter Christopher, alisema semina hiyo iliyowashirikisha mafundi umeme na wadau zaidi ya 150, ililenga kuwajengea uwezo wataalam na wadau hao kuhusu sheria, kanuni, miongozo na utaratibu wa utendaji kwenye shughuli za ufungaji wa mifumo ya umeme.

Wadau wengine walioshiriki semina hiyo ni Wakala wa Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Wakala wa Majengo (TBA) na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

Mafundi umeme wanaweza kuomba leseni kupitia mfumo wa LOIS unaopatikana kwenye tovuti ya EWURA www.ewura. go.tz na kupakua fomu ya kukamilisha ufungaji mifumo ya umeme katika tovuti hiyo hiyo au kuwasiliana na EWURA kwa simu 0800110030, mitandao ya kijamii au barua pepe; info@ewura.go.tz.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 18,2024

 
 
Share:

Tuesday, 17 September 2024

RC TANGA AONYA WATAKAOFANYA MAKOSA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA




Na Hamida Kamchalla, TANGA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt. Batilda Buriani ametoa onyo kwa wananchi watakaokwenda kinyume na taratibu za uchaguzi na kufanya makosa ambayo yatawatia hatiani katika uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba, 27 mwaka huu.

Dkt Buriani ametoa onyo hilo Jana ofisini kwake akizungumza na waandishi wa habari na kuainisha makosa kadhaa yatakayomtia hatiani mwananchi  au mjumbe yeyote anayegombea katika uchaguzi huo.

Amesema ni endapo ataharibu orodha ya wapiga kura au nyaraka zozote zinazohusiana na uchaguzi, pili endapo atatoa taarifa za uongo kuhusu Uraia wake, lakini pia kama atajiandikisha zaidi ya mara moja ikiwa ni pamoja na kupiga kura zaidi ya mara moja kwa wagombea wa nafasi moja.

Kosa jingine ni kutishia wapiga kura au wagombea ili kuvuruga uchaguzi, lakini pia kufanya kampeni siku ya uchaguzi, kuonesha ishara au kuvaa mavazi yanayoonesha yanayomtambulisha mgombea au chama cha siasa mita 200 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.

Amesema kosa jingine ni kumzuia msimamizi wa uchaguzi au msimamizi wa kituo atakayeteuliwa kutekeleza majukumu yake, kukiuka masharti ya kiapo chake, kupatikana Kwa karatasi ya kupigia kura zaidi ya moja kwa nafasi moja aliyogombea.

"Makosa yapo kadhaa ikiwamo na mjumbe au mwananchi yeyote atabainika kuvuruga au kuvunja ratiba ya mikutano ya kampeni ya uchaguzi, kukutwa na silaha kwenye eneo la uteuzi wa wagombea" ,amesema.

Lakini pia endapo atatangaza matokeo ya uchaguzi kabla hayajatangazwa rasmi na msimamizi wa uchaguzi lakini pia kufanya jambo lolote kinyume cha kanuni za uchaguzi pamoja na sheria nyingine za nchi zinazohusiana na uchaguzi.

"Makosa haya yanapotokea na mtu yeyote atakayepatikana na hatia za kosa lolote la uchaguzi atahukumiwa adhabu ya faini isiyozidi sh laki tatu au kifungo kisichozidi miezi 12 au vyote kwa pamoja,

"Hivyo ni vizuri wananchi wakajua makosa haya ili wasije kujikuta kwenye matatizo bila kujua,  wito wangu kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga, ninawasihi sana, wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 au wale watakaofikisha umri huo siku ya kupiga kura" amesisitiza.

Sambamba na hayo amewataka wananchi kujiandikisha tena kwenye daftari la mpiga kura ifikapo Octoba 11, ili wasipoteze haki ya kuchagua viongozi wanahitajika kwa maendeleo ya Mkoa pamoja na kwenye maeneo yao na pia wasipoteze haki yao ya kikatiba.

Baadhi ya wananchi wameiomba serikali kuboresha huduma kwenye vituo vya kujiandikisha na kupigia kura, ikiwa ni pamoja na muda wa kujiandikisha uongezwe kwakuwa siku 10 pekee hazitatosha kwani wengi wanabanwa na muda wa kutekeleza majukumu yao.

"Tunaona wakati mwengine kunatokea matatizo mbalimbali, suala la huduma ya kwanza ni muhimu sana kwani kwenye maeneo ya kupigia kwakuwa wengine ni wazee lakini pia kuna wagonjwa" amesema Mohamedi Dondo, Karibu wa Wazee Asili, Wilaya ya Tanga.

"Kama wazee, tunawashawishi vijana wetu waweze kujiandikisha na kwenda kupiga kura, lakini pia tunaiomba serikali kuongeza muda wa kujiandikisha katika daftari la mpiga kura, siku walizoweka ni kidogo sana ikilinganishwa na shughuli zetu za kujitafutia kipato" amesema.

Naye Majid Shali amesema, "nikiwa kijana nimejiandaa vizuri na uchaguzi, ni haki ya kila Mtanzania, kumekuwa na tabia ya vijana wengi kukataa kwenda kupiga kura kisha tunalalamikia viongozi hawafai,

"Ili kupata viongozi bora ni lazima tujitokeze na kujua kura ni haki zetu na tunapaswa kujumuika ili kuchagua viongozi bora ambao tutawachagua sisi na siyo kusubiria kuchaguliwa na watu wengine" amefafanya.



Share:

BOSI WA MATI AZINDUA TAWI LA FOUNTAIN GATE ROYAL FANS BABATI


Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mati super brands LTD David Mulokozi  amezindua tawi la mashabiki wa timu ya Soka ya fountain gate FC tawi la Babati mkoani Manyara  ikiwa na lengo la kuhamasisha Vijana kupenda michezo na kuiunga mkono timu hiyo iliyohamia Mjini Babati katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa kutoka mkoani Mwanza.

Akizungumza mara baada ya kuzindua tawi hilo Septemba 16, 2024 katika mtaa wa Oster bay  amepongeza ubunifu huo wa Vijana walioamua kuwaza jambo hilo ambalo ni kubwa na kwamba Kampuni ya Mati ipo tayari kulisaidia tawi hilo kwa kila namna.

Amesema Mati super brands sio matajiri Sana wala sio masikini Sana kwa sababu wana moyo wa kutoa hivyo kila walichoomba Mashabiki hao katika risala yao wamekipata.

"kupitia Mashabiki hawa itakuwa chachu na hamasa kwa kila Mahali ambapo timu itakwenda nao kufungua matawi kama haya"

"Na Sisi kama wadhamini wakuu tutajitahidi kwa namna Moja ama nyingine kusapoti yale matawi kuyatambua"

Amesema Fountain Gate FC walivyofika kuomba udhamini Mati super brands waliwapokea kwa mikono miwili kwa sababu ni fursa ya kibiashara kwa mji wa Babati na kwa Kampuni kuutangaza bidhaa zao.

Katika risala yao fountain gate Royal fans waliomba kupatiwa Tv kubwa inchi 75 na usafiri kwa ajili ya kusafiri na timu maeneo mbalimbali Nchini.

Hata hivyo uongozi wa Fountain Gate FC umeridhia kufunguliwa kwa tawi hilo ambalo ndo la kwanza nchi nzima na kwamba wapo tayari kutoa Magari matano (Coaster) kusafirisha Mashabiki hao kwenye mechi zao za nje ya Babati.

Nao uongozi wa tawi la Fountain Gate royal fans chini ya mwenyekiti Emmanuel Hondi  wamemshukuru David Mulokozi kwa kuwapatia mahitaji hayo pamoja na kuendelea kuiunga mkono Fountain Gate FC kwa kuipa udhamini wa mwaka mmoja.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger