Wednesday 18 September 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 18,2024

 
 
Share:

Tuesday 17 September 2024

RC TANGA AONYA WATAKAOFANYA MAKOSA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA




Na Hamida Kamchalla, TANGA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt. Batilda Buriani ametoa onyo kwa wananchi watakaokwenda kinyume na taratibu za uchaguzi na kufanya makosa ambayo yatawatia hatiani katika uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba, 27 mwaka huu.

Dkt Buriani ametoa onyo hilo Jana ofisini kwake akizungumza na waandishi wa habari na kuainisha makosa kadhaa yatakayomtia hatiani mwananchi  au mjumbe yeyote anayegombea katika uchaguzi huo.

Amesema ni endapo ataharibu orodha ya wapiga kura au nyaraka zozote zinazohusiana na uchaguzi, pili endapo atatoa taarifa za uongo kuhusu Uraia wake, lakini pia kama atajiandikisha zaidi ya mara moja ikiwa ni pamoja na kupiga kura zaidi ya mara moja kwa wagombea wa nafasi moja.

Kosa jingine ni kutishia wapiga kura au wagombea ili kuvuruga uchaguzi, lakini pia kufanya kampeni siku ya uchaguzi, kuonesha ishara au kuvaa mavazi yanayoonesha yanayomtambulisha mgombea au chama cha siasa mita 200 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.

Amesema kosa jingine ni kumzuia msimamizi wa uchaguzi au msimamizi wa kituo atakayeteuliwa kutekeleza majukumu yake, kukiuka masharti ya kiapo chake, kupatikana Kwa karatasi ya kupigia kura zaidi ya moja kwa nafasi moja aliyogombea.

"Makosa yapo kadhaa ikiwamo na mjumbe au mwananchi yeyote atabainika kuvuruga au kuvunja ratiba ya mikutano ya kampeni ya uchaguzi, kukutwa na silaha kwenye eneo la uteuzi wa wagombea" ,amesema.

Lakini pia endapo atatangaza matokeo ya uchaguzi kabla hayajatangazwa rasmi na msimamizi wa uchaguzi lakini pia kufanya jambo lolote kinyume cha kanuni za uchaguzi pamoja na sheria nyingine za nchi zinazohusiana na uchaguzi.

"Makosa haya yanapotokea na mtu yeyote atakayepatikana na hatia za kosa lolote la uchaguzi atahukumiwa adhabu ya faini isiyozidi sh laki tatu au kifungo kisichozidi miezi 12 au vyote kwa pamoja,

"Hivyo ni vizuri wananchi wakajua makosa haya ili wasije kujikuta kwenye matatizo bila kujua,  wito wangu kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga, ninawasihi sana, wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 au wale watakaofikisha umri huo siku ya kupiga kura" amesisitiza.

Sambamba na hayo amewataka wananchi kujiandikisha tena kwenye daftari la mpiga kura ifikapo Octoba 11, ili wasipoteze haki ya kuchagua viongozi wanahitajika kwa maendeleo ya Mkoa pamoja na kwenye maeneo yao na pia wasipoteze haki yao ya kikatiba.

Baadhi ya wananchi wameiomba serikali kuboresha huduma kwenye vituo vya kujiandikisha na kupigia kura, ikiwa ni pamoja na muda wa kujiandikisha uongezwe kwakuwa siku 10 pekee hazitatosha kwani wengi wanabanwa na muda wa kutekeleza majukumu yao.

"Tunaona wakati mwengine kunatokea matatizo mbalimbali, suala la huduma ya kwanza ni muhimu sana kwani kwenye maeneo ya kupigia kwakuwa wengine ni wazee lakini pia kuna wagonjwa" amesema Mohamedi Dondo, Karibu wa Wazee Asili, Wilaya ya Tanga.

"Kama wazee, tunawashawishi vijana wetu waweze kujiandikisha na kwenda kupiga kura, lakini pia tunaiomba serikali kuongeza muda wa kujiandikisha katika daftari la mpiga kura, siku walizoweka ni kidogo sana ikilinganishwa na shughuli zetu za kujitafutia kipato" amesema.

Naye Majid Shali amesema, "nikiwa kijana nimejiandaa vizuri na uchaguzi, ni haki ya kila Mtanzania, kumekuwa na tabia ya vijana wengi kukataa kwenda kupiga kura kisha tunalalamikia viongozi hawafai,

"Ili kupata viongozi bora ni lazima tujitokeze na kujua kura ni haki zetu na tunapaswa kujumuika ili kuchagua viongozi bora ambao tutawachagua sisi na siyo kusubiria kuchaguliwa na watu wengine" amefafanya.



Share:

BOSI WA MATI AZINDUA TAWI LA FOUNTAIN GATE ROYAL FANS BABATI


Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mati super brands LTD David Mulokozi  amezindua tawi la mashabiki wa timu ya Soka ya fountain gate FC tawi la Babati mkoani Manyara  ikiwa na lengo la kuhamasisha Vijana kupenda michezo na kuiunga mkono timu hiyo iliyohamia Mjini Babati katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa kutoka mkoani Mwanza.

Akizungumza mara baada ya kuzindua tawi hilo Septemba 16, 2024 katika mtaa wa Oster bay  amepongeza ubunifu huo wa Vijana walioamua kuwaza jambo hilo ambalo ni kubwa na kwamba Kampuni ya Mati ipo tayari kulisaidia tawi hilo kwa kila namna.

Amesema Mati super brands sio matajiri Sana wala sio masikini Sana kwa sababu wana moyo wa kutoa hivyo kila walichoomba Mashabiki hao katika risala yao wamekipata.

"kupitia Mashabiki hawa itakuwa chachu na hamasa kwa kila Mahali ambapo timu itakwenda nao kufungua matawi kama haya"

"Na Sisi kama wadhamini wakuu tutajitahidi kwa namna Moja ama nyingine kusapoti yale matawi kuyatambua"

Amesema Fountain Gate FC walivyofika kuomba udhamini Mati super brands waliwapokea kwa mikono miwili kwa sababu ni fursa ya kibiashara kwa mji wa Babati na kwa Kampuni kuutangaza bidhaa zao.

Katika risala yao fountain gate Royal fans waliomba kupatiwa Tv kubwa inchi 75 na usafiri kwa ajili ya kusafiri na timu maeneo mbalimbali Nchini.

Hata hivyo uongozi wa Fountain Gate FC umeridhia kufunguliwa kwa tawi hilo ambalo ndo la kwanza nchi nzima na kwamba wapo tayari kutoa Magari matano (Coaster) kusafirisha Mashabiki hao kwenye mechi zao za nje ya Babati.

Nao uongozi wa tawi la Fountain Gate royal fans chini ya mwenyekiti Emmanuel Hondi  wamemshukuru David Mulokozi kwa kuwapatia mahitaji hayo pamoja na kuendelea kuiunga mkono Fountain Gate FC kwa kuipa udhamini wa mwaka mmoja.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 17,2024

 

Magazeti ya leo
   
     
Share:

Monday 16 September 2024

NAMNA NILIVYOJENGA NYUMBA MBILI KWA KUSHINDA BAHATI NASIBU

Katika maisha yangu sikuwahi kuwaza kuwa nitakuja kujenga nyumba nikiwa na umri wa miaka 26, na sio nyumba tu nyumba mbili, hii imekuwa ni kama ndoto kwangu.

Hata wazazi wangu na ndugu zangu hawaamini jinsi ambavyo niliweza kutoka kimaisha kwa maana sikwenda shule, hivyo nilikuwa nafanya kazi ambazo nilikuwa nalipwa tu fedha za kawaida za kuweza kusukuma maisha.

Jina langu ni Alex kutokea Nairobi, nimetokea katika familia masikini sana lakini sasa mimi ni mmiliki wa nyumba mbili hapa hapa jijini Nairobi. Je, nilifanikiwa vipi?, ngoja nikueleze ilivyokuwa!.

Baada ya kufanya kazi kwa muda na kuona napata tu fedha za kawaida, niliamua kuanza kushiriki michezo mbalimbali ya bahati nasibu hasa kubashiri matokeo ya soka.

Kipindi cha mwanzo naanza kazi hiyo nilipoteza fedha zangu kiasi hadi kufikiria kuachana kabisa na kazi hiyo, lakini ndani ya moyo wangu kuna sauti ilikuwa inaniambia kuna siku nitashinda ila sikujua nitashindaje.

Niliamua kuingia kwenye mitandao ya kijamii na kusoma mbinu mbalimbali zinazotumika na watu wengi ili kuweza kushinda bahati nasibu kubwa.

Katika kusoma kwangu nikabaini kuna mtu anaitwa Dr Bokko ambaye amekuwa akiwasaidia watu wengi kuweza kushinda bahati nasibu.

Basi niliwasiliana naye kupitia namba yake +255618536050 na kumuomba msaada wake maana kiu yangu kubwa ilikuwa ni kuondokana na maisha ya umaskini ambayo nilikuwa nimeyaishi tangu utoto wangu.

Nashukuru Dr Bokko alinifanyia dawa yake ya maajabu ambayo iliniwezesha kushinda mamilioni ya fedha baada ya kubashiriki kwa ufasaha kabisa Jackpoti ya mamilioni ya fedha.

Hadi napata dawa ya Dr Bokko tayari nilikuwa nimejaribu kushiriki Jackpoti zaidi 10 bila mafanikio lakini baada tu ya usaidizi wa  Kiwanga, basi nilipata ushindi wa kishindo.

Ndipo nikachukua fedha zangu na kwenda kuanza ujenzi mara moja wa nyumba mbili ambapo moja naishi mimi na nyingine nimepangisha. Asante sana Dr Bokko.

Mwisho.


Share:

DOTTO MAGARI : CHADEMA MKIKAA KWENYE VIKAO VYENU KUWENI WAKWELI MAMA SAMIA NDIYO KILA KITU


Na Mwandishi wetu

Mfanyabiashara mashuhuri wa magari nchini Tanzania, Dotto Keto maarufu kama 'Dotto Magari', ameonyesha kuridhika na juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kudumisha amani nchini. 

Ameeleza kuwa, ni muhimu kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuachana na siasa za upotoshaji na kumpongeza Rais Samia kwa juhudi kubwa anazozifanya kwa maslahi ya taifa.

Magari amesema "Nyinyi majirani zetu mlikuwa hamna ofisi kwa takribani miaka 30, leo Mama kajitahidi katoa fungu kawahamishieni ofisi na kupelekwa Mikocheni mnataka nini majirani?"

Aidha Magari amewataka CHADEMA kumuunga mkono Rais Samia kwa kutengeneza mazingira bora ya kuvutia wawekezaji na ya kufanyia biashara nchini.

“Mnasema nchi haina amani, ni amani gani mnayoitaka? Wawekezaji wamerudi, watu wanafanya wanachotaka,hata nyie mnaongea mnachojisikia,  hiyo siyo amani? . Mama anafanya kazi kubwa, ameshughulikia umeme, maji, treni ya umeme, barabara kujengwa kwa viwango na viwanda, mpeni Rais Samia maua yake kwani anafanya mengi kwenye hii nchi”

“Mkikaa kwenye vikao vyenu kuweni wakweli kwamba mama Samia ndiyo kila kitu, apewe mitano yake na akija tena apewe mitano mingine jumla 10, huyu mama ndiyo aliyeweza kuiongoza hii nchi” ,amesisitiza

Share:

Sunday 15 September 2024

WAZIRI MAVUNDE AIPONGEZA TUME YA MADINI KWA KUVUNJA REKODI YA UKUSANYAJI WA MAPATO

 

Waziri wa Madini Anthony Mavunde akizungumza leo wakati akifungua kikao kazi na Menejimenti ya Tume ya Madini Jijini Tanga 

Naibu Waziri wa Madini Dkt Steven Kiruswa akizungumza wakati wa kikao hiho
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Mhandisi Yahaya Samamba akizungumza wakati wa kikao kazi hicho
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza



Na Oscar Assenga,TANGA

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde ameipongeza Tume ya Madini kwa kuvunja rekodi kukusanya kiasi cha Sh Bilioni 196 kwa kipindi cha siku 75 huku akieleza jambo hilo ni kubwa na inaonyesha wamedhamiria kuifanya sekta ya madini inachangia kwenye uchumi wa nchini.

Mavunde aliyasema hayo leo Jijini Tanga wakati akifungua kikao kazi na Menejimenti ya Tume ya Madini Jijini Tanga ambapo alisema kiwango hicho kimepokelewa mpaka leo 15 Septemba ndani ya miezi miwili ya mwaka huu na hilo linatokana na .

Alisema kiwango hicho kimeifanya kuvunja rekodi ya makusanyo ilihali mwaka 2015/2016 ilichukua mwaka mzima kukusanya Bilioni 161 lakini leo ndani ya siku 75 tume hiyo imeshakusanya kiasi hicho na hivyo kuvunja rekodi kwani waliojiwekea makusanyo ya Bilioni 60 mpaka Bilioni 65 kwa kila miezi na mwili iliyopita mmekusanya Bilioni 83 kila mwezi mmevuka malengo yao.

“Niwatie moyo na wakikaza buti na kuendelea na usimamizi huo mzuri na makusanyo wakifika mwakani mwezi wa saba watakuwa mmeandika historia kubwa”Alisema

Katika hatua nyengine Waziri Mavunde amewataka maafisa madini wakazi wa mikoa kuhakikisha wanashughulikia migogoro kwenye maeneo yao kwa haraka inapojitokeza badala ya kusubiri mpaka wafike viongozi wakubwa ikiwemo Waziri.

Alisema haiwezekani wao wapo kwenye mikoa na wanashindwa kutatua migogoro iliyopo hivyo wabadilike wahakikishe wanaishughulia na utatuzi wake unapatikana haraka bila kumuonea mtu.

Alisema anajisikia vibaya kuona mgogoro inapotokea mpaka aende waziri au Naibu Waziri wakati wapo maafisa madini wakazi mpaka umshinde ndio uvuke uende ngazi lakini kazi yenu hya kwanza ni utatuzi wa migogoro labda mniembie nyie ni sehemu ya migogoro lakini kama sio sehemu ya migogoro tatueni migogoro,

“Niwaambieni kipimo chenu cha kazi kitakuwa ni namna mnavyotatua migogoro tatueni na sio mpaka msubiri ufike hatua ya juu anzeni nao lakini mtatue migogoro katika haki asionewe mtu simamieni haki ndugu zangu”Alisema Waziri Mavunde

Udhibiti wa Utoroshwaji wa Madini

WAZIRI Mavunde aliwataka maafisa hao kuhakikisha wanadhibiti utoroshwaji wa madini katika maeneo yao hususani ile ya mipakani

“Mmeona hivi karibuni kuna kesi nyingi sana zinapelekwa mahakamani na juzi tumewakamata watu Bandari Dar na kilo 15 za dhahabu na tumezitaifisha ela dhahabu na wanakwenda mahakamani,huko kwenye maeneo yenu hakikisheni mnashirikiana kwenye task force kudhibiti hili lisitokee”Alisema Waziri Mavunde

Aidha Waziri Mavunde aliutaja Mkoa wa Madini wa Kahama ndio unaongoza kwa shughuli za za utoroshaji wa madini na mbinu hivi sasa zimebadilika wanasikie wale ambao wanakwenda kuuziana kwenye mashine za Mpunga ambapo alimtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo kuhakikisha anaimarisha eneo hilo.

Katika hatua nyengine Waziri Mavunde amewataka maafisa madini wakazi wa mikoa kuhakikisha wanashughulikia migogoro kwenye maeneo yao kwa haraka inapojitokeza badala ya kusubiri mpaka wafike viongozi wakubwa ikiwemo Waziri.

Mavunde alitoa agizo hilo leo Jijini Tanga ambapo alisema haiwezekani wao wapo kwenye mikoa na wanashindwa kutatua migogoro iliyopo hivyo wabadilike wahakikishe wanaishughulia na utatuzi wake unapatikana haraka bila kumuonea mtu.

Alisema anajisikia vibaya kuona mgogoro inapotokea mpaka aende waziri au Naibu Waziri wakati wapo maafisa madini wakazi mpaka umshinde ndio uvuke uende ngazi lakini kazi yenu hya kwanza ni utatuzi wa migogoro labda mniembie nyie ni sehemu ya migogoro lakini kama sio sehemu ya migogoro tatueni migogoro,

“Niwaambieni kipimo chenu cha kazi kitakuwa ni namna mnavyotatua migogoro tatueni na sio mpaka msubiri ufike hatua ya juu anzeni nao lakini mtatue migogoro katika haki asionewe mtu simamieni haki ndugu zangu”Alisema Waziri Mavunde

Udhibiti wa Utoroshwaji wa Madini

WAZIRI Mavunde aliwataka maafisa hao kuhakikisha wanadhibiti utoroshwaji wa madini katika maeneo yao hususani ile ya mipakani

“Mmeona hivi karibuni kuna kesi nyingi sana zinapelekwa mahakamani na juzi tumewakamata watu Bandari Dar na kilo 15 za dhahabu na tumezitaifisha ela dhahabu na wanakwenda mahakamani,huko kwenye maeneo yenu hakikisheni mnashirikiana kwenye task force kudhibiti hili lisitokee”Alisema Waziri Mavunde

Aidha Waziri Mavunde aliutaja Mkoa wa Madini wa Kahama ndio unaongoza kwa shughuli za za utoroshaji wa madini na mbinu hivi sasa zimebadilika wanasikie wale ambao wanakwenda kuuziana kwenye mashine za Mpunga ambapo alimtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo kuhakikisha anaimarisha eneo hilo.



“Lakini pia nimemwambia Katibu Mkuu waifanye Kahama kama Kanda Maalumu kwa maana dhahabu nyingi inatoroshewa kupitia Kahama nimekuona RMO mara mbili mara tatu mnatoka mnakamata endeleee na mikoa mingine hasa mikoa ya Mipakani”Alisema Waziri huyo.

Waziri huyo aliwataka maafisa hao kila mmoja katika eneo lake ahakikishe anakuwa sehemu ya udhibti wa utoroshaji wa madini kwa maana utoroshwaji huo unasababisha kupoteza mapato mengi.

Hata hivyo Waziri huyo aliitaka Ofisi ya Kamishna wa Madini kushirikiana na RMO kuwalea wachimbaji wadogo na kuwaendeleza katibu mkuu pale wizara wawekezaji wakubwa wana meneja wake ndani ya wizara wa kuyasimamia katibu mkuu kupitia Ofisi ya Kamishna natoa maelekezo tengenezeni utaratibu kushirikiana na RMO kuwaibua watanzania wawekezaji wa sekta ya madini kupitia ofisi ya Kamishna wawelee nao wagraduate kutokana na kwamba hivi sasa wenyewe hawana muangalizi.

Alisema ili siku moja waweze kutengeneza mabilioni wengi kupitia wachimbaji wadogo hivyo wakikaa nao na kuwasaidia kama wanavikwazo waone namna ya kuyatatua ili kuweza kuongeza mapato.

Katika hatua nyengine Waziri Mavunde aliwataka kuhakikisha wanadhibiti upotevu wa mapato waende wakazibe mianya na makusanyo yaweze kuongezeke huku akieleza hiyo ni sehemu ya kazi yako ya msingi.

“RMOs kila mtu amewekewa malengo ya kuwafikia kwa mwaka wa fedha huu kama unahisi kwako unashindwa kufikia malengo kwa jambo ambalo halihusiani na wewe ni tatizo la kimfumo,kimundo lipo nje ya uwezo
Share:

MSIGWA AIPONGEZA TBS KWA KUHAMASISHA MICHEZO MAENEO YA KAZI



NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amezitaka taasisi mbalimbali za serikali kushiriki na kufanya mabonanza ya michezo ambapo itasaidia kuimarisha afya za wafanyakazi na kuleta manufaa kwa taifa kwa kuongeza idadi ya wachezaji na wawakilishi katika mashindano ya kimataifa.

Rai hiyo imetolewa  Septemba14,2024 Jijini Dar es salaam alipokuwa katika Bonanza la michezo la watumishi lililoandaliwa na Shirika la viwango Tanzania (TBS).

Msigwa ameipongeza TBS kwa kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya sita kwa kuhamasisha michezo maeneo ya kazi kwa kutengeneza bajeti na kuruhusu wafanya kazi kushiriki katika michezo ili kuimarisha afya na kujenga mahusiano mazuri kazini jambo ambalo huoongeza ubunifu na ufanisi maeneo ya kazi.

Ameongeza kwa kuiasa Menejimenti ya TBS kutenga bajeti ya kujenga viwanja bora maeneo ya kazi ili kuwawekea wafanyakazi mazingira bora wakati wa kushiriki michezo mbali mbali.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi TBS Prof. Othman Chande amesema walianzisha Bonanza hilo miaka mitano iliyopita ambapo limelenga kuimarisha afya za wafanyakazi  pamoja na kujenga umoja. 

"Wachezaji wanacheza kama timu mbili tofauti lakini ni walewale wakishamaliza mchezo wanaenda pamoja inaongeza urafiki". Amesema 

Aidha Prof.Chande ameeleza kuwa mashindano hayo ya mabonanza yatachangia kuwa na machaguo mengi ya wachezaji watakao wakilisha katika mashindano ya kimataifa.

Nae Mwenyekiti wa Michezo Shirika la viwango Tanzania (TBS) Nyabutwenza Methusela ameeleza faida za bonanza hilo ambapo amesema kuwa linasaidia watumishi kuondokana na changamoto ya afya ya akili kwa kujikita zaidi katika michezo ambayo inawaondolea msongo wa mawazo na  kuongeza ufanisi wanaporudi  kufanya kazi.

"Kupitia michezo afya ya akili na mwili inaboreshwa, wafanyakazi wanakuwa wachapakazi kwasababu wameboresha afya zao za akili pamoja na mwili". Nyabutwenza ameeleza.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger