Friday, 31 May 2024

MISA TAN YATOA TUZO KWA RAIS SAMIA KULINDA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) , Wakili James Marenga (kulia) akikabidhi tuzo ya kufanikisha  kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) imetoa Tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania ambapo chini. Chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Tanzania imeshika nafasi ya kwanza katika nchi zinazolinda uhuru wa vyombo vya habari Afrika Mashariki . Pia katika upimaji wa uhuru wa habari duniani kuitoa Tanzania nafasi ya 143 mwaka 2023 hadi 97 mwaka 2024 kulingana na utafiti uliotolewa na Reporters Without Borders (RFS) Mei 3,2024.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa MISA TAN, Wakili James Marenga kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Mei 31,2024 wakati wa Kongamano la Siku mbili la Kufanya Tathmini ya Hali ya uhuru wa Kujieleza, Haki ya Kupata Taarifa na Uhuru wa Wana Habari mwaka 2024 linalofanyika Jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi.
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) , Wakili James Marenga (kulia) akikabidhi tuzo ya kufanikisha  kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) , Wakili James Marenga (kulia) akikabidhi tuzo ya kufanikisha  kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi akizungumza wakati wa Kongamano la Siku mbili la Kufanya Tathmini ya Hali ya Kujieleza, Haki ya Kupata Taarifa na Uhuru wa Wana Habari Jijini Dar es salaam

Makamu Mwenyekiti wa MISA TAN, Wakili James Marenga (kulia) akiteta jambo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi wakati wa Kongamano la Siku mbili la Kufanya Tathmini ya Hali ya Kujieleza, Haki ya Kupata Taarifa na Uhuru wa Wana Habari Jijini Dar es salaam
Makamu Mwenyekiti wa MISA TAN, Wakili James Marenga akizungumza wakati wa Kongamano la Siku mbili la Kufanya Tathmini ya Hali ya Kujieleza, Haki ya Kupata Taarifa na Uhuru wa Wana Habari Jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa MISA TAN, Elizabeth Riziki akizungumza wakati wa Kongamano la Siku mbili la Kufanya Tathmini ya Hali ya Kujieleza, Haki ya Kupata Taarifa na Uhuru wa Wana Habari Jijini Dar es salaam

Share:

SWICA YAIINGIZIA SERIKALI DOLA ZA MAREKANI 2,773,000

Na. Beatus Maganja, Bungeni Dodoma 

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Jasmin Kairuki (Mb) amesema katika kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za utalii, Wizara yake imefanikiwa kuanza utekelezaji wa Uwekezaji Mahiri kwenye Maeneo ya Wanyamapori (Special Wildlife Investment Concession Areas - SWICA) ambapo jumla ya Dola za Marekani 2,773,000 sawa na Shillingi bilioni 7.1 zimepatikana ikiwa ni ada ya vitalu zilizokusanywa tangu kusainiwa kwa mkataba tarehe 3 Januari, 2024.

 Ameyasema hayo leo Mei 31, 2024 Bungeni Dodoma akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

Mhe Kairuki amesema kupitia Uwekezaji huo Wizara yake inategemea kuongeza mapato kufikia Dola za Marekani millioni 312 sawa na wastani wa Dola za Marekani millioni 15.5 kwa mwaka.

Akizungumzia suala la uvunaji wa wanyamapori na masharti ya Mkataba wa CITES, Mhe. Kairuki amesema Tanzania imefanikiwa kuingia katika kundi la kwanza (Category I) la nchi wanachama zenye Sheria zinazotekeleza Mkataba wa CITES kikamilifu hatua inayotajwa kuiwezesha Tanzania kufanya biashara ya uwindaji wa kitalii na mataifa ambayo masharti ya kupokea nyara kutoka kwenye nchi ambazo Sheria zake ziko katika kundi la kwanza.

Katika kuhakikisha maeneo ya malikale yanaendelea kukidhi vigezo vya kimataifa na kuvutia watalii, Waziri Angellah Kairuki amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imefanikiwa kupandisha hadhi Eneo la Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, lenye hadhi ya Urithi wa Dunia kuwa miongoni mwa maeneo yenye mahusiano ya kisayansi kati ya binadamu na mazingira (Man and Biosphere Reserve).

Amesema hadhi hiyo imetolewa na UNESCO mwezi Julai, 2023 na hivyo kuongeza idadi ya maeneo yenye sifa hiyo kutoka 5 hadi 6  na hatua inayotajwa kuchochea shughuli za utalii wa malikale kwa kuongeza idadi ya watalii wa Kimataifa katika eneo la Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara hususani kupitia utalii wa meli.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 31,2024

  Magazeti

Share:

DMI YAJIVUNIA KUTOA WATAALAMU WENYE UWEZO MKUBWA

Na Oscar Assenga,Tanga

CHUO cha Bahari cha Jijini Dar es Salaam(DMI) kimeshiriki maonyesho ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu Jijini Tanga huku wakijivunia kutoa wataalamu wenye uwezo mkubwa wa kusanifu na kuzikarabati meli kupitia Temesa na hivyo kuondoa uhaba uliokuwepo awali nchini .

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika Banda lao lililopo eneo la Shule ya Sekondari Popatlaly kunakofanyika maadhimisho ya elimu,ujuzi na ubunifu Captain Mohamed Kauli alisema wameshirika kwa lengo la kueleza wanachokifanya ikiwemo ufanisi wa meli,usafirisha majini,utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi baharini,usanifu ini na ujenzi wa meli na ubaharia.

Alisema awali chuo hicho kilikuwa kinazalisha mabaharia wakati kilipoanzishwa lakini ili kukabiliana na ombwe la ukosefu wa ajira kutokana na vijana wengi kumaliza vyuo na kukosa ajira na wahitimu haoo wanafaida kubwa mbili wanapohitimu chuo kupata ajiri nchini kwenye sekta ya usafirishaji majini na nje ya nchi kwenye meli.

“Kwa kweli tumekuwa tukizalisha idadi kubwa ya mabaharini wanaofanya kazi nje na ndani ya nchi kuna gepu kwenye utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi baharini lakini pia gepu la upatikanaji wa meli awali zimekuwa zikiagizwa kutoka nje kwa gharama kubwa”Alisema

Alisema lakini sasa Serikali imetengeza wataalamu wanaotoka kwenye chuo hicho ambao wanajenga meli,kuzisanifu ,kuzikarabati kwenye eneo hilo serikali kupitia Temesa wanajenga na kukabarati meli hizo hapa hapa nchini.

Awali akizungumza mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho,Masaka Julias alisema kwamba mafunzo ambayo wanayapata kwenye yamewawezesha kubuni vitu mbalimbali a hivyo kuwawezesha wanapomaliza kuweza kujiajiri kupitia ujuzi walioupata.

Alisema kwamba kwa sasa kupitia mafunzo hayo unawasaidia kutengeneza vitu mbalimbali vya ubunifu huku akieleza wamebuni wazo la kutengeneza mashine ya kutengeneza chilsource na ya kufunga vifuniko kwenye chupa ambayo inasahisisha.

Share:

Thursday, 30 May 2024

MWANAFUNZI WA DUCE AIBUKA NA MFUMO WA KUZUIA UPOTEVU WA MAJI NA KULINDÀ UHARIBIFU WA PAMPU

Bw. Kalua Polikarpo, Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu (BSc. Ed) kutoka katika Idara ya Fizikia, Hisabati na Infomatiki ( PMI ) iliyo chini ya Kitivo cha Sayansi ( FoS ) abuni mfumo wa kudhibiti mtiririko wa maji unaotokea pindi maji yanapojaa kwenye matanki na kuzuia uharibifu wa pampu.

Hayo yamedhihirika katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 yanayoendelea hapa jijini Tanga

DUCE tunayo furaha kubwa kuujulisha Umma kuwa Bw. Kalua Polikarpo, Mwanafunzi wetu wa Mwaka wa Tatu anayesoma _Shahada ya Sayansi ( Hisabati na Fizikia) na Elimu_, ameonesha ujuzi wa hali ya juu kwa kubuni mfumo wa kuzuia upotevu wa maji na kupunguza uwezekano wa kuungua kwa pampu kutokana na kuvuta upepo kwa muda mrefu. 

Akifafanua hayo, Bw. Kalua amesema mfumo huo utasaidia kuratibu matumizi bora ya maji. 

Zaidi amesema kuwa mfumo huo mpya utaokoa gharama za matengenezo na ununuzi wa pampu mpya. 

Kimsingi, mradi huu utaleta suluhisho muhimu kutokana na changamoto zinazoikabili jamii yetu. Aidha, ubunifu huu unadhihirisha uwezo wa wanafunzi wetu katika nyanja za elimu, sayansi, na teknolojia.

 Kwa dhati, tunampongeza na tunajivunia ubunifu huu ambao ni chachu kwa maendeleo ya jamii na Taifa. 

Karibuni katika viwanja vya Popatlal jijini Tanga, kushuhudia na kujifunza zaidi kuhusu maonesho ya miradi mbalimbali yenye ubunifu wa hali ya huu kama huu kutoka kwenye Chuo chetu. Hii inadhihirisha kuwa DUCE ni zaidi ya ualimu.

#DUCE #WikiYaElimu2024 #Ubunifu #Ujuzi #ElimuNaSayansi #ProudlyDUCE #Kalua #SaveWater #SustainableLiving #DUCEnizaidiyaualimu

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger