Friday, 24 November 2023

KITANDULA ATOA MSAADA WA VYAKULA NA FEDHA KWA WALIOKUMBWA NA MAFURIKO JIMBONI KWAKE






Na Mwandishi Wetu, MKINGA.

MBUNGE wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula ametoa msaada wa Vyakula na Fedha kwa Kaya 36 zilizopo kwenye Kata ya Manza na Mtimbwani wananchi katika Kijiji cha Msimbazi ambao walikumbwa na kadhia ya mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa nchini

Kitandula ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii aliamua kutoa msaada huo wakati akiwa kwenye ziara ya Jimbo hilo ili kuhakikisha wananchi hao wanaaondokana na changamoto ambazo wamekumbana nazo kutokana na uwepo wa mafuriko hayo

Akizungumza wakati akiwa kwenye ziara hiyo pamoja alipokwenda kushuhudia zoezi la ukoaji wa wananachi katika Kijiji cha Msimbazi Kata ya Manza kutokana na mvua kubwa zinazoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kitandula aliwaeleza wananchi hapo kwamba yupo pamoja nao na kuhaidia kuendelea kuwasaidia kuhakikisha wanaondokana na changamoto mbalimbali ili kuweza kujikwamua kiuchumi

Katika hatua nyengine Mbunge Kitandula alitoa msaada wa Pikipiki kwa kikundi cha wafugaji kwa ajili ya kukusanya maziwa kutoka kwa wafugaji wadogo wilayani humo.

Baada ya kuwakabidhi Pikipiki hiyo alimshukuru Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Maulid Surumbu kwa kumshirikisha kwenye jambo hili ni kazi kubwa na nzuri ambazo zimekuwa zikifanywa kwa ajili ya kuwakwamua kiuchumi wafugaji hao

“Nimeona niwaunge mkono kwa kuwapatia pikipiki hii naamini utakuwa chachu kwenu lakini pia niwaambie kwamba tupo pamoja na tutaendelea kushirikiana “Alisema

Awali akizungumza mmoja wa wanakikundi hao Abdala Mwajasi alimshukuru Mbunge huyo kwa msaada aliowasaidia huku akieleza mbunge huyo ni mahiri sana kuwasaidia wananchi hasa wanapokuwa wamekumbana na changamoto mbalimbali.

“Tunakushuru Mhe Mbunge Wetu kwa kutusaidia jambo hilo la umuhimu mkubwa kwa sababu sisi tauna uwezo wa kununua pikipiki “Alisema
Share:

Thursday, 23 November 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 24,2023





Share:

Breaking : MATOKEO YA DARASA LA SABA ( PSLE 2023 ) YAMETANGAZWA ..TAZAMA MAJINA HAPA

Share:

PROFESA NDALICHAKO AANIKA UMUHIMU WA HIFADHI YA JAMII KWA WATANZANIA

Na MWANDISHI WETU, ARUSHA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amewataka Watanzania kuona umuhimu wa kujiunga na kuchangia katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye.

Profesa Ndalichako alisema hayo tarehe 22 Novemba, 2023, wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yaliyofunguliwa na Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkoani Arusha.

Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu imeshiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo ‘Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo Kiuchumi’.

Profesa Ndalichako alisema Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na mambo mengine inasimamia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo kupitia maadhimisho hayo Mifuko hiyo ni sehemu ya kutoa elimu ya fedha kwa wananchi kwamba wanapopata fedha wanawajibu wa kujiwekea akiba kwa ajili ya kesho yao kupitia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

“Ukitembelea mabanda yetu utakutana na Mifuko yote ya Hifadhi yaJjamii ukiwemo wa NSSF ambao unaendelea kuwahamasisha wananchi kuwa na matumizi sahihi ya fedha kwa kujiunga, kuchangia na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye,” alisema Mhe. Profesa Ndalichako.

Share:

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2023


Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)  litatangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2023 leo Alhamisi Novemba 230,2023 saa tano asubuhi.




Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 23,2023

 


 
Share:

Wednesday, 22 November 2023

WAZAZI WANGU WALIKUWA WANAPIGANA HADI KUUMIZANA

Jina langu ni Sheila, suala la ugomvi lilikuwa limekita mizizi kwenye ndoa ya wazazi wangu, kila mara walipigana makonde nisijue ningeanzia wapi kuwasaidia.

Baba alikuwa ni mtu mpole na mara nyingi hakupenda ugomvi na mtu yeyote, ila mama kwa upande wake alikuwa ni mtu mpenda kelele sana na kila wakati alipokosewa hakutulia au kutaka suluhisho.

Kila wakati ilikuwa ni kugombana na kutupiana makonde mazito mazio, kila mara filamu hii ilitokea muda wa jioni tu baada ya baba kutoka kazini.

Mama yangu hakuwajibika kama mwanamke wa nyumbani na hilo ndilo liliibua ugomvi na mapigano kila mara, hali ile ilipelekea mama kuwa na makovu na alama mingi.

Sikuwa nafurahia vurugumechi ile kwani ilikuwa ni aibu kuitazama, nilijua kuna siku moja kati yao ataumizwa na hata kulazwa hospitali kutokana na majeraha, kwa hivyo nilikuwa najaribu jinsi niwezavyo kuwapatanisha.

Ndungu zangu wote walikuwa mbali kwa ajili ya shughuli za kikazi, hivyo mimi nilikuwa peke yangu pale nyumbani, siku moja sarakasi ilianza na mama akapigwa vibaya jambo lilipelekea kulazwa hospitali kwa muda wa siku tatu.

Alipotoka kwenye matibabu nilidhani kwamba itakuwa mwisho wa ugomvi wao, lakini waliendelea kupigana tena kwa nguvu ajabu, ilikuwa kama ibada lazima kila siku wangepigane hadi mmoja wao amwage damu.

Nilimwelezea rafiki yangu suala hilo na hapo alinielekeza kwa African Doctors kwa ajili ya usaidizi, nilimpigia simu mtaalam huyo wa tiba asilia kwa ajili ya huduma yake kwani hali ilkuwa mbaya sana kwenye familia yetu.

African Doctors alifanya matambiko ya kurejesha amani kwenye ndoa ya wazazi wangu, siku mbili baada ya kutoka kwa African Doctors, mambo kwa hakika yalianza kubadilika, ugomvi iliisha kabisa na kila wakati walikuwa wanaelewana sana.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com




au watumie email; africandoctorheals@gmail.com

Mwisho.


Share:

TMA YATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA ZENYE HATARI YA MAFURIKO


Mvua

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya uwezekano wa kunyesha mvua kubwa kuanzia leo Jumatano Novemba 22 hadi Novemba 25 ambazo huenda zikasababisha mafuriko kwa maeneo machache ambayo yanaweza kusababisha vifo.

Mvua hizo zinatarajiwa kunyesha katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga na visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

Kupitia taarifa ya Mamlaka iliyotolewa jana Jumanne Novemba 21, 2023, imetaja athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya barabara kutopitika kutokana na mafuriko pamoja na vifo kwa siku hizo, hivyo wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari.

Via EATV
Share:

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WANANCHI KUENDELEA KUTUMIA VIPIMO SAHIHI WAKATI WOTE

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara  Mhe. Exaud Kigahe akizungumza
Afisa mtendaji mkuu wa Wakala wa Vipimo Stella Kahwa

Na Mariam Kagenda -  Kagera
Serikali itahakikisha wananchi wanaendelea kutumia vipimo sahihi kwa wakati wote katika sekta zote hasa katika sekta ya kilimo.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara  Mhe. Exaud Kigahe amesema hayo baada ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara,Kilimo na Mifugo kufanya ziara mkoani Kagera na kuzungumza na Taasisi ya Wakala wa Vipimo.

Mhe. Kigahe amesema kuwa yapo maeneo yanayolalamikiwa katika suala la vipimo ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo kwani vipimo katika mazao ya kilimo bado ni changamoto ambapo wafanyabiashara wengi bado hawajawa tayari kufuata taratibu za kununua mazao kwa vipimo.

Ameongeza kuwa kama Wizara moja ya sheria inayosimamiwa na Wakala wa Vipimo inalazimisha kila mmoja awe mnunuzi au muuzaji kutumia vipimo hivyo watahakikisha mazao yote yanauzwa kwa vipimo.

Amesema kuwa tayari kuna kamati maalum ambayo imeshaundwa kutathimini changamoto iliyopo ili kuhakikisha wanakomesha kuuza bidhaa au mazao kwa rumbesa na kamati hiyo itakuja na mkakati maalum.


Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa Wakala wa Vipimo Stella Kahwa amesema kuwa jukumu kubwa la Taasisi hiyo ni kuhakiki vipimo na kuhakikisha vinatumika kwa usahihi na pia kuangalia ni kwa namna gani bidhaa mbalimbali zinafungashwa ili mtumiaji wa mwisho apate kilicho sahihi.

Aidha amesema kuwa watahakikisha wanafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo ili kuhakikisha watanzania wote wanapata haki zao kupitia Taasisi hiyo kutokana na majukumu waliyopewa.
Wajumbe wa kamati wakichangia mada
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger