Monday, 13 November 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 13,2023



Share:

Sunday, 12 November 2023

MHE. KATAMBI AZINDUA HARAMBEE YA KUCHANGIA AMANAH SEKONDARI



Na. Mwandishi wetu - Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amezindua harambee ya kuchangia ujenzi wa Shule ya Sekondari Amanah iliyopo Ilongero Mkoani Singida.

Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 11, 2023 Jijini Dodoma ambapo Mhe. Katambi alimwakilisha Waziri wa Fedha Mhe. Lameck Nchemba.

Katambi amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  amekuwa mstari wa mbele katika kujenga miundombinu ya elimu hivyo harambee hiyo ni kuunga mkono jitihada anazozifanya.

Amesema katika harambee hiyo jumla ya shilingi Milioni 25,765,800 zimechangwa, mifuko 100 ya simenti,mabati na ujenzi wa bweni moja ambalo litagharamikiwa na mmoja kati ya wadau waliojitokeza katika harambee hiyo.

Kwa upande wake Mlezi wa Shule hiyo Mhe. Mizengo Pinda ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu, amewataka wadau na viongozi walioshiriki katika uzinduzi wa harambee hiyo kuondoa udini hususani katika kufanya shughuli za maendeleo na badala yake washikamane ili kufikia malengo.

Naye, Mkurugenzi wa Shule hiyo Abdallah Kundya amesema ujenzi wa mabweni hayo utasaidia kuboresha huduma za jamii na uendeshaji  taaluma  shuleni hapo.

Aidha, amewapongeza viongozi na wadau waliojitokeza katika kuchangia ujenzi wa mabweni hapo na kuwaahidi kutumia pesa hizo katika ujenzi wa mabweni hayo. 

Share:

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA KASI YA UJENZI WA BWAWA LA MEMBE, YATEMBELEA NYUMBA ZA VIJANA WA BBT

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mhe. Omari Mohamed Kiguha amesema kuwa kamati imeridhishwa na hatua za ujenzi wa mradi wa bwawa la Membe ziilizofikiwa ikilinganishwa na kiasi cha fedha zilizotolewa kwenye mradi huo.

Mhe. Kiguha ameyasema hayo wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi ikiwa ni sehemu ya mradi inayotembelewa na kamati hiyo ya Bajeti katika ziara yake ya siku nane katika mikoa mbalimbali. 

Aidha katika mkoa wa Dodoma kamati imetembelea shamba la BBT la Chinangali II na kujionea hatua zilizofikiwa za ujenzi wa miundo mbinu ya nyumba za makazi ya vijana kiwanda cha mvinyo wa zabibu maandalizi ya shamba
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde (MB) akiongea na wananchi wa kijiji cha Membe wilayani Chamwino wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya bajeti ya bunge la Tanzania tarehe 11/11/2023





Mradi wa nyumba 46 za makazi kwa ajili ya vijana wa BBT ukiwa katika hatua mbalimbali za ukamilishaji mradi wa Chinangali II. Dodoma
Share:

WAZIRI MAVUNDE AAGIZA KUREKEBISHWA KWA MADUARA NA MIAMBA INAYONING’INIA ENEO LA UCHIMBAJI MWAKITOLYO,SHINYANGA

Kufuatia Taarifa ya ukaguzi uliofanywa na timu ya wataalamu iliyoundwa na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde kuhusu uchambuzi wa mikataba kati ya Vikundi vya wachimbaji wadogo wa madini na wabia(_technical support_) kwenye leseni za uchimbaji mdogo zilizopo katika eneo la Mwakitolyo mkoani Shinyanga kamati imebaini sehemu kubwa ya maduara hayapo katika hali salama ya uchimbaji.


Akiwasilisha taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Timu ya watalaamu Mhandisi Ally Samaje amebainisha kwamba eneo la uchimbaji la mwakitolyo linahitajika kukatwa kwa miamba inayoyoning’inia na kurekekebisha maduara ili wachimbaji wachimbe kwa usalama zaidi na kuongeza uzalishaji kuliko ilivyo hivi sasa.


Sambamba na hapo kamati imebaini kuwa uchimbaji wa pamoja (co-existence) kati ya Wachimbaji wadogo na wabia kupitia muongozo wa uchimbaji utakaosimamiwa na Wizara ya Madini.

Akipokea taarifa hiyo,Waziri Mavunde amemuelekeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Ndg. Msafiri Mbibo kuhakikisha anasimamia kwa ukaribu urekebishaji wa maduara na maeneo yenye miamba inayoning’inia kwa usalama wa wachimbaji wadogo na kuongeza uzalishaji wa madini.


“Suala la usalama katika maeneo ya uchimbaji ni suala muhimu ambalo lazima tulipe uzito mkubwa.

Naelekeza kwamba katika maeneo yote hapo Mwakitolyo yaliyo chini ya ubia wa msaada wa kiufundi(_technical support_) yarekebishwe dosari zote za kiusalama ili kuwaruhusu wachimbaji wadogo wafanye shughuli za uchimbaji katika mazingira ambayo ni rafiki.

Nataka pia niwahakikishie kwamba Hakuna mchimbaji mdogo yoyote atakayeondolewa katika eneo lake kwakuwa eneo hili liligawiwa kwa wachimbaji wadogo kama wanufaika wa kwanza.


Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuelekeza kuhakikisha tunawasimamia na kuwaendeleza wachimbaji wadogo kwa kuwapatia maeneo ya uchimbaji na pia katika upatikanaji wa mikopo na mitaji ili kuongeza tija katika shughuli zenu”, alisema Mavunde


Mkutano huo wa kupokea taarifa ulihudhuriwa na Viongozi wa Mkoa wa Shinyanga,Kamati za Ulinzi na Usalama pamoja na wachimbaji wa eneo la Mwakitolyo
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger