Tuesday, 10 October 2023
Monday, 9 October 2023
WATENDAJI MADINI KUKUTANA KILA MWEZI KUJADILI MAENDELEO SEKTA YA MADINI
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde ameongoza kikao cha Watendaji wa Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini yake ikiwa ni utaratibu ulioanzishwa wa kukutana kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kujadiliana utekelezaji wa majukumu, miradi pamoja na kufahamishana hatua mbalimbali zilizofikiwa katika Sekta ya Madini na masuala yanayohusu changamoto na maendeleo ya Sekta kwa ujumla.
Kikao hicho cha leo Oktoba 7, 2023, pia kimejadili na kutafakari ikiwemo kuweka mikakati itakayoongeza ushiriki wa Watanzania hususan vijana na wanawake katika Sekta ya Madini pamoja na kuongeza tija na thamani ya Sekta kwenye uchumi wa nchi na hatimaye mchango Pato la Taifa.
Aidha, Mhe. Mavunde amerejea kuhusu uwepo wa mpango mpya unaoitwa Madini kwa kesho bora (Mining for Brighter Tomorrow -MBT) ukiwa na lengo la kuwasaidia vijana, wanawake pamoja na wahitimu wa vyuo vikuu kunufaika kupitia fursa zilizopo katika Sekta ya Madini.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali amesema vikao hivyo vitasaidia kuifungua fursa kwa Watendaji wa Wizara na Wakuu wa Taasisi kutoa mawazo yao kwa kuwa vinajadili masuala muhimu na makubwa kuhusu Sekta ya Madini.
CHONGOLO ATEMBELEA NA KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KATAVI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Ndugu Daniel Godfrey Chongolo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025, aliyoendelea nayo leo mkoani humo kwa kuzuru Jimbo la Mpanda Mjini.
Baada ya kutembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo leo Jumamosi Oktoba 7, 2023, Komredi Chongolo ameahidi kwenda kuweka msukumo kwa serikali kuhakikisha wanapeleka haraka sh. bil. 5 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa mradi huo wa afya pamoja na kujenga jengo la kuhifadhia maiti hospitalini hapo.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Serafini Kisengi Patrice amesema kuwa kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 Serikali imetenga jumla ya shilingi Bilioni 5,000,000,000 kwa ajili ya kuhakikisha ujenzi wa hospitali hiyo unakamilika kwa wakati ili wananchi wapate huduma zilizokusudiwa.
"Tunampongeza na Kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa hospitali hii,” amesema Dkt. Kisengi
.
TBS KANDA YA MASHARIKI YATEKETEZA VIPODOZI TANI NANE VYENYE VIAMBATA SUMU
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Mashariki limeteketeza tani nane ya bidhaa za vipodozi vyenye viambata sumu ambazo zilikamatwa katika Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro
Akizungumza na waandishi wa habari hapo Jana Oktoba 6,2023 Mkuranga mkoani Pwani, Kaimu Meneja wa TBS Kanda ya Mashariki, Bw.Francis Mapunda amesema zoezi la kukamata bidhaa za vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku ni endelevu hivyo amewataka wafanyabiashara kuacha kuuza bidhaa hizo.
Aidha alitoa wito kwa wafanyabiashara wa vipodozi kufanya usajili wa vipodozi na kufuata orodha ya bidhaa za vipodozi ambavyo vimesajiliwa na kuruhusiwa kuuzwa.
Pamoja na hayo amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanajiepusha na biashara ya bidhaa za vipodozi zenye viambata sumu vilivyopigwa marufuku kuepusha usumbufu na gharama zisizo za lazima..jpeg)
.jpeg)
MREMBO AOLEWA NA WANAUME WAWILI......WANALALA KITANDA KIMOJA
Mwanamke mmoja raia wa Congo ambaye ameolewa na waume wawili, amewaduwaza wengi ikizingatiwa kwamba ndoa ya waume wengi ni nadra barani Afrika.
Francine Jisele anaishi na waume wawili, mume wa kwanza Remi Murula na wa pili Albert Jarlace katika nyumba moja pamoja na wanao.
Jisele alifunga ndoa miaka sita iliyopita na Murula na walijaliwa watoto wawili. Murula aliondoka kwenda kutafuta kazi ya kukimu familia yake na kukata mawasiliano na mke wake.
"Kwa sababu maisha hayakuwa rahisi, mwanaume huyo alifunga safari na hakurudi tena. Nilijikuta pekee yangu, nilikaa miaka mitatu na nusu bila mume wangu," aliiambia Afrimax English katika mahojiano.
"Baada ya miaka hiyo yote nilimpoteza na kupendana na mwanaume huyu mwingine. Baada ya mwaka mmoja na mume wa pili, wa kwanza alirudi," alifichua.
Jisele hakutarajia mume wake angerudi baada ya kuwa mbali kwa miaka yote hiyo. Nilikutana na mwanamke huyu nikiwa nafanya kazi kwenye sekta ya madini na akaniambia kuwa ana mume mwingine na jinsi mwanaume huyo alivyomuacha akisema anaenda kutafuta maisha,”
“Nilihisi sina la kufanya kwa sababu tayari tulikuwa pamoja tangu nilipoishi naye bila kujua ana mwanaume mwingine,” alieleza Albert Jarlace.
“Mwanamke huyo aliniomba nisimuache hivyo nikaona ni lazima nibaki naye na kwa sasa tuna mtoto mmoja pamoja,” alisema Jarlace.
Murula aliporudi alipigana na Jarlace akibishana kuwa Jisele ni mke wake.
"Tuko wanaume watatu hapa na tunaelewana, huyu mwanamke ni mke wetu. Tangu niondoke sikuzungumza na mke wangu hata siku moja. Niliporudi nilimkuta mke wangu na mwanaume mwingine," aliongeza Murula.
Murula alikuwa amemwomba mpenzi wake amtimue Jarlace lakini alisisitiza kuwa hana mahali pengine pa kwenda.
"Mwanzoni nilipiga kelele lakini niligundua ikiwa ningezungumza na mke wangu hangefanya jambo kama hilo. Sikuwa na mahali pa kwenda na nilikuwa na makosa," alisema Murula.
“Tunakula meza moja, tunalala chumba kimoja na kitanda kimoja, nawapenda wote wawili, tunaishi kwa amani nyumbani,” alisema Jisele.
Wanaume hao hugawana kazi na kuleta mkate nyumbani huku mwanamke akiwaheshimu wote wawili.
Wasiwasi walio nao ni kutoweza kuwatofautisha watoto wao.
Mwanamke ndiye anayetambua baba wa watoto. Linapokuja suala la kusoma uroda, mmoja wetu humwacha mwingine ili afurahie.
“Familia yangu inafahamu hali yangu na kunishauri nitulie kwa sababu nilimtelekeza mke wangu,” alisema Murula.
Jisele anasema ni ngumu kwake; anatamani kila mwanaume angekuwa na nyumba na angeenda kwao.
Hataki wote wawili waendelee kukutana katika chumba kimoja cha kulala kwa wakati mmoja.
"Nataka kuondoka na kumpa nafasi 'hubby wa mwanamke huyo kwani ni mume wake anajulikana. Ningepata msaada wa tiketi ningeondoka na kumwacha mume mwenzangu abaki nyumbani kwake. Mwanamke asingekubali kuhama mbali," alisema Jarlace.
"Sifurahii kuona sisi wanaume wawili tukigawana mwanamke; ardhi na nyumba ni yangu na mwanamke ni wangu," aliongeza.
HEKARI 807, MAGUNIA 506 YA BANGI, MBEGU NA VIWANDA VYA KUCHAKATA BANGI VYATEKETEZWA MARA
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa, Askari mgambo pamoja na vyombo vingine vya dola, imefanya operesheni maalum mkoani Mara hususani katika kanda maalum ya Tarime Rorya kwenye bonde la mto Mara.
Operesheni hii, iliyofanyika kuanzia tarehe 02 hadi 08 Oktoba, 2023, imefanikisha uteketezaji wa jumla ya hekari 807 za mashamba ya bangi, ukamataji wa gunia 507 za bangi kavu iliyo tayari kusafirishwa, gunia 50 za mbegu za bangi pamoja na kuteketeza viwanda viwili vidogo vilivyokuwa vikitumika kuchakata na kufunga bangi kabla ya kusafirishwa ambapo watuhumiwa 11 wanashikiliwa kuhusika na dawa hizo.
Akizungumzia tukio hilo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, wakazi wa eneo hilo wamelifanya bonde la mto Mara kama eneo maalum kwa ajili ya kilimo cha bangi na kujimilikisha kwa kutoruhusu mtu yeyote asiye mkazi kuingia kwenye bonde kama sehemu ya kuficha uharifu wao na wametishia kumdhuru yoyote atakayeingia ndani ya bonde hilo bila ridhaa yao. Pia, wamediriki kufunga ofisi ya kijiji wakimtuhumu mtendaji wa kijiji cha Nkerege kutounga mkono kilimo cha bangi.
‘‘Kitendo kinachofanywa na wananchi waliopo katika eneo la mto Mara ni kinyume kabisa na sheria, viongozi wa serikali na wananchi ambao sio wakazi wa hapa hawaruhusiwi kabisa kuingia eneo la bonde. Uwepo wa daraja lililopo katika moja wapo ya vijito vinavyopeleka maji mto Mara, linatumika kama kizuizi cha watu kwenda kwenye hifadhi ya bonde la mto maeneo yanayolimwa bangi. Ili mtu avuke anatakiwa kujieleza nia na madhumuni ya kuvuka kuelekea upande wa pili, na wahusika wasiporidhika na maelezo hawakuruhusu kuendelea na safari’’ ,amesema Lyimo.
Ameongeza kuwa, baadhi ya viongozi wasio waaminifu wa vijiji vinavyopakana na bonde hilo pamoja na wananchi waliojimilikisha bonde hilo muhimu kwa uchumi wa taifa, wamekuwa wakikodisha na kuuza mashamba ya kulima bangi ndani ya hifadhi ya bonde hilo.
Aidha, kutokana na mto Mara kuwa muhimu sana katika ikolojia ya mbuga ya Serengeti, Kamishna Jenerali Lyimo ameomba Wizara zinazohusika kushirikiana na Mamlaka kutokomeza kilimo cha bangi katika eneo hilo, kwani mbali na operesheni iliyofanyika bado mashamba ya bangi ni mengi pembezoni mwa mto na wananchi wamekuwa wakitumia maji ya mto kumwagilia.
‘‘Tukiacha kilimo cha bangi kiendelee hivi, na kuwaacha wananchi waendelee kuchepusha maji ya mto kumwagilia bangi mwisho wa siku itaharibu ikolojia katika mbuga ya Serengeti na mto kwa ujumla. Ni vema tukashirikiana kuhakikisha eneo hili linasimamiwa vema ili kufanikisha kusitishwa kwa kilimo cha bangi”, amesisitiza Lyimo.
Sambamba na hilo, amewataka viongozi wa serikali za mitaa waliotoroka kuwa sehemu ya mapambano ya dawa za kulevya kwa kuhakikisha kwamba, wanakomesha kilimo cha bangi watakaporejea.
Pia, Kamishna Lyimo amesema, Mamlaka kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara na uongozi wa wilaya ya Tarime, watafanya mikutano ya hadhara na kufikiria kuwa na mipango kabambe kuona ni namna gani bonde litalindwa dhidi ya kilimo cha bangi na uhalifu mwingine.
‘‘Sisi kama Mamlaka tutafanya operesheni endelevu katika maeneo haya kuhakikisha kilimo cha bangi kinaisha. Bonde hili lina rutuba nyingi na linakubali mazao ya aina zote, hivyo tumekubaliana na mkuu wa mkoa wa Mara kuwa na mikakati ya kusimamia bonde ili kumaliza kilimo cha bangi na kutafutwa kwa shughuli nyingine ambayo itakuwa rafiki’,’ amesema Lyimo.
Naye diwani wa kata ya Tulwa Mheshimiwa Chacha Machugu amesema, viongozi wa serikali za mitaa wanaosaidia kuendelea kwa kilimo cha bangi wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa watu wengine. Aidha, amewaomba viongozi wa dini kusaidia kuwaambia waumini wao kuwa dawa za kulevya hazitakiwi.
‘‘Tutashirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha bangi hailimwi Tarime na yeyote atakaye kiuka miongozo na sheria za nchi atawajibishwa kwani sote tunaongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”.
Magreth Ally mkazi wa Tarime amesema kuwa, vijana wengi wanalima bangi kwa madai ya kupata fedha kwa haraka. Hivyo, ameiomba serikali kutoa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya, kuelekeza na kuwezesha kilimo cha mazao mbadala ili kuepusha kurithishana kilimo cha bangi kama njia pekee ya kujipatia kipato kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Akizungumzia operesheni iliyofanyika, Isaya Banda mkazi wa Tarime, ameiomba serikali kufanya operesheni endelevu katika maeneo yote ili kutokomeza bangi kwani vijana wengi wameathirika na matumizi ya dawa hizo. Pia, amewaomba wananchi kuwafichua wanaojihusisha na kilimo na biashara ya bangi.
Kwa upande mwingine Chacha Michael mkazi wa kijiji cha Nkerege ambako operesheni hii imefanyika, ametoa msimamo wake juu ya kilimo cha bangi kwa kusema; “Hili zao linatuharibia sana vijana wetu, wanaacha kusoma wanaenda kuvuta bangi, vilevile tunauomba uongozi wa mama Samia zoezi hili liwe endelevu kwa sababu hapa mto Mara kilimo cha bangi kimekithiri sana. Kuna mazao mengi ya kulima ukapata hela kila zao linakubali hapa Tarime lakini wengi wamekimbilia bangi, mimi sikubaliani nalo kabisa”, amebainisha Chacha.
Operesheni iliyofanyika mkoani Mara ni mwendelezo wa operesheni zilizofanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini kama moja ya hatua za muhimu katika kupunguza upatikanaji na usambazaji wa dawa za kulevya hapa Nchini.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo
SHEIKH MSAFIRI KITUMBO AMFANANISHA MASELE NA NGAMIA, ATAJA SIFA KUU TANO
Sheikh maarufu Manispaa ya Shinyanga na Kanda ya Ziwa kwa ujumla Sheikh Msafiri Kitumbo ambaye pia ndiye Mratibu wa Maulid za Mtume Mohamed S.A.W Kanda ya ziwa amempongeza na kumfananisha Mhe. Stephen Masele ambaye ni Mbunge mstaafu wa jimbo la Shinyanga mjini na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika mstaafu na mnyama aliyetakaswa Ngamia kwa sifa zake.
Akizungumza wakati wa Maulid, baada ya Masele kutoa ngamia, Sheikh Kitumbo alizitaja sifa kuu tano za ngamia na kuzifananisha na sifa na tabia ya mhe Masele kama ifuatavyo:-
1. UPENDO- Ngamia katika kitabu cha Quran takatifu kuna aya inayomzungumzia upendo wa ngamia, ni kiumbe kilichotakaswa, Mtume Mohamed S.AW alitumia sadaka ya ngamia kueneza upendo, amani na uvumilivu kwa Waislamu na watu wote duniani. Masele ana upendo kama wa ngamia , ana upendo wa dhati kwa watu bila kuwabagua kwa hali zao za kimaisha, ni mtu wa watu, watu wanampenda kwa dhati ndani ya mioyo yao. Masele ni mtu aliyejaa kwenye mioyo ya watu.
2. UVUMILIVU- Ngamia ni mnyama mvumilivu sana, anaweza kuishi katika hali yoyote ya mateso jangwani bila maji kwa muda mrefu na akavumilia, Masele ni mvumilivu sana , amepitia mambo magumu sana lakini ameonesha kiwango kikubwa cha uvumilivu na ukomavu.
3. FURAHA- Ngamia ni mnyama anayeleta furaha kwa watu, kama ilivyo kwa Masele ni mtu wa watu anayependa furaha na kuleta amani na upendo kwa watu wote bila kujali hali zao za kimaisha.
4. UKUBWA: Ngamia ni kiumbe kikubwa- Kumvaa ngamia lazima ujipange, kumvaa Masele lazima mtu ajipange, Masele ni mwanasiasa mkubwa wa kitaifa na kimataifa .
5. UPOLE:- Ngamia ni mnyama mpole sana, ana huruma sana anatembea kwa malingo, anajiamini, hababaishwi na mazingira yoyote. Ndivyo ilivyo kwa Masele ni mtu mpole sana, ana huruma sana, anasaidia sana watu wenye shida mbalimbali iwe ni misiba, harusi, makanisani, misikitini na hata kusaidia wanafunzi wanasoma. Ukiwa na shida ukipeleka kwa masele utapata tu msaada uwe wa mawazo ama pesa. Masele ana moyo wa utajiri wa roho, sio mchoyo ni mtu wa kujitoa kwa watu katika hali na Mali, katika shida na raha.
Naye Sheikh wa mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke amemmwagia sifa nyingi Mhe Masele kwa kusema kuwa hana deni kwa Waislamu, amefanya kitu adimu na kinachoheshimika sana katika dini ya uislamu.
“Kitendo cha mhe masele kutoa sadaka ya Ngamia katika Maulid ya Mtume Mohamed S.AW kimeheshimisha sana uislamu, hakika Masele hana deni kwetu sisi waislamu, tutamuombea duwah Kila siku na Mwenyezi amtimizie haja zake”, aliongeza sheikh Kabeke ambaye ni sheikh wa mkoa wa Mwanza.
Naye sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya alimfananisha Mhe Masele na Mfalme wa Ethiopia aliyekuwa mkristo lakini akajitolea kumpatia “Mahali” ya kuolea Mtume Mohamed S.A.W ili afunge ndoa.
Aliongeza Sheikh Ismail kuwa “Tangu nilipomfahamu mhe Masele miaka zaidi ya 20 iliyopita hajabadilika kitabia awe na cheo ama asiwe na cheo masele ni yule yule mtu wa watu, kijana mwenye heshima, upole, upendo na ni mtu wa msaada. Amekuwa akisaidia jamii Kila kukicha iwe wagonjwa, iwe misiba, iwe harusi, iwe ada za wanafunzi wewe kama una jambo lako mpelekee masele utapata ufumbuzi. Ni kijana mwema sana”.
Viongozi wa kidini walioudhuria Maulid hiyo walimiminia sifa nyingi kwa jinsi wanamfahamu mhe Masele wakiwemo masheikh mkoa wa Simiyu sheikh Kwezi, na wengine wengi. Sheikh Kwezi alisema “Mhe Masele amefanya jambo kubwa sana katika uislamu, ameandika historia kubwa katika mioyo ya Waislamu kwa kufanya jambo alilolipenda Mtume wetu S.A.W, na sisi waislamu tutakuunga mkono katika jambo lako lolote utakalo hitaji msaada wetu”
Mgeni rasmi katika Maulidi hiyo ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Taifa(BAKWATA) Sheikh NUR Mruma amemwagia sifa mhe Masele na kusema ni watu wachache sana wenye moyo wa kujitoa kwa ajili ya wengine kama masele alivyoonesha.
"Tangu nifike shinyanga nimesikia sifa nyingi nzuri za masele kwa jamii, kwamba ni mtu wa msaada sana” endelea na moyo huo na Mwenyezi Mungu atakulipia, atakulipa wema wako kwa jamii yako. Natoa maelekezo na wito kwa masheikh wote wa shinyanga na Kanda ya ziwa kumuombea duwah Masele kila manapokuwa na shughuli zenu ili Mwenyezi Mungu azidi kumlinda dhidi ya mabaya yote, ampe ulinzi na kujalia siha njema” aliongeza sheikh Mruma.
Mh Stephen Masele amewahi kuwa mbunge wa Shinyanga Mjini, Naibu Waziri katika wizara mbali mbali katika serikali ya Rais Kikwete na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika chombo cha Umoja wa Afrika chenye makao makuu nchini Afrika Kusini.

























.jpeg)



.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)



















