Tuesday, 25 July 2023
DC SAMIZI AWATAKA WATANZANIA KUWAENZI MASHUJAA KWA KULIPIGANIA TAIFA NA KUDUMISHA AMANI
JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA TANGA YAHIMIZA JAMII KUTUNZA MAZINGIRA
Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika zoezi la kupanda miti wa pili kutoka kulia ni Mjumbe wa Wazazi wilaya ya Tanga Pamela Chaula
Na Oscar Assenga,TANGA.
KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga Urassa Nanyaro ameshiriki kwenye kampeni ya upandaji wa miti katika kituo cha Afya Mwakidila Jijiji Tanga huku akiitaka jamii kuendelea kutunza mazingira.
Nanyaro aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati Jumuiya hiyo iliposhiriki kwenye kampeni inayoendeshwa na Taasisi ya Tea inayojishughulisha na mazingira ikiwemo upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali kwenye Jiji hilo.
Alisema kwamba wananchi na jamii kwa ujumla wanapaswa kutunza mazingira kwa mustakabvali wa kuimarisha vyanzo vya maji na uchumi wa Taifa letu kwa sababu maji ndio chanzo kikubwa cha nishati ya umeme.
Aidha alisema na nishati ya umeme inapatikana kutokana na utunzaji mazingira na unapandwaji wa miti na hivyo kupatikana mvua za kutosha zinazopelekea mitambo ya kuzalisha umeme kutokana na uwepo wa mvua za kutosha.
“Niipongeze taasisi ya Tea kwa kuendesha kampeni hii kwani miti inapopandwa inasaidia kupata lishe,kivuli na matunda na kuwasaidia kuwezesha kupata mvua ya kutosha itakayowezesha kuendesha mitambo na kuzalisha nishati ya umeme inayotumika hospital viwanda na kuinua uchumi wa Taifa letu”Alisema Nanyaro.
Akiwa katika shule ya Msingi Mwakidila Katibu huyo aliwapongeza walimu wa shule hiyo kutokana na utunzaji wa mazingira na wana hifadhi ya mazingira ambayo ndio chanzo za utunzaji huo
“Sisi Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga majukumu yetu ni kushrikiana na shule za msingi ,awali,sekondari vyuo Lengo kuhamasisha vijana wapate malezi bora kulingana na tamaduni ya kitanzania tupo hapo leo wanapoanda miti ya matunda na kwa hali hiyo tuliokuta tunaamini miti itakuwa kwa muslakabali wa viumbe hali na kutunza vyanzo vyetu na vya maji “Alisema
Hata hivyo alisema licha ya utunzaji wa vyanzo vya maji lakini pia mwisho wa siku kupitia mazingira mazuri Taifa liweze kusonga mbele kiuchumi likiwa na watu wenye afya na siha njema.
MSITOE DAWA KWA WAGONJWA KAMA HANA CHETI CHA DAKTARI-DKT SHEKALAGHE
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Shekalaghe akizungumza wakati akifungua kongamano la mrejesho wa Tafiti za Kukinga na kudhibiti Maambukizi na Usugu wa dawa za Antibiotic lililofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Prof. Said Shehe Aboud na kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Shehe Aboud akizungumza wakati wa kongamano la mrejesho wa Tafiti za Kukinga na kudhibiti Maambukizi na Usugu wa dawa za Antibiotic lililofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo
| Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Naima Yusuf akizungumza wakati wa kongamano hilo |
| Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Naima Yusuf akizungumza wakati wa kongamano hilo |
Na Oscar Assenga,TANGA
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Shekalage amewataka wenye maduka ya dawa nchini wafuate taratibu zilizowekwa na Serikali wasitoe dawa kwa wagonjwa kama hawajakwenda na cheti kilichoandikwa na daktari.
Dkt Seif aliyasema hayo Jijini Tanga wakati akifungua kongamano la mrejesho wa Tafiti za Kukinga na kudhibiti Maambukizi na Usugu wa dawa za Antibiotic lililofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.
Alisema jambo hilo ni la msingi na Serikali wameweka sheria kali mtu akimakatwa anachukuliwa hatua lakini sasa wanazungumza wanaofanya kwa njia za siri ambao hawajagundulika wanasababisha tatizo linakuwa kubwa.
“Katika hili napenda kusisitiza hili kwa wenye maduka ya dawa nchini wafuate taratibu zilizowekwa na Serikali wasitoe dawa kwa wagonjwa kama hawajakwenda na karatasi iliyoandikwa daktari”Alisema
Alisema jambo jingine ni wenzao wanaoshirikiana nao wanaouza dawa za mifugo mtu anakwenda anasema kuku wake anatatizo fulani anatoa dawa lakini ushauri unatolewa kwa wahusika kwamba huyo kuku anaumwa nini na anapaswa kutibiwa vipi.
Katibu Mkuu huyo alisema wanahitaji waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuweza kutoa elimu kwao waandihi wa habari kila mkoa kuewaeleza athari za dawa na mambo mengine na kuifikisha jamii na hivyo kuweza kuondosha kasumbua hiyo kwa jamii.
Alisema zipo dawa ambazo mtu anajisikia anaumwa na kichwa kununua panado kwa sababu ya kutuliza kichwa iili uende kwa daktari akakupe dawa hilo ndio jambo la msingi sana
Alisema waanajua zipo dawa muhimu zilizowekwa kwenye maduka lakini dawa za antibayotiki wananchi wasitumie tu kwa sababu wanapotumia dawa bila kupata ushauri kwa daktari dawa za aina gani kwa sababu kufanya hivyo wanatengeneza mwili wao kuwa na usugu vimelea vinavyokupata kuweza ku kutibiwa na zile dawa ambazo ni sahihi kwa sababu umeshatengeneza usugu wa kuweza kutrumia tu dawa,
Awali akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Shehe Aboud alitoa wito kwa wananchi wasiende kwenye duka la dawa kununua bila cheti cha daktari kwani kumekuwa na mazoezi wananchi kwenda kujinunulia dawa bila kujua kama kweli wanahitaji kutumia hizo au la.
Alisema pia vilevile wanapoandikiwa dawa za daktari wahakikishe wanatumia dozi kamili na wanatumia kwa mujibu ilivyoandikwa na Daktari.
Aidha aliwataka pia kuhakikisha kwamba pale wanapokwenda kununua kwenye duka la dawa na mambo ya kujitibu wenyewe wanapopata tatizo la kiafya waende hospitalini waonwe madaktari wapimwe wapate vipimo vya maabara na vikapaporudi kwa daktari ndio wanaweza kujua wanapaswa kutumia dawa ya aina gani.
Naye kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Dkt Naima Yusuf alisisitiza wananchi kuacha kutumia dawa bila kujua wanaumwa na nini kwani kufanya hivyo zinaweza kuwasababishia madhara mbalimbali.
Alisema katika utafiti huo walichofanya walichukua sampuli kutoka kwa mama na mtoto aliyezaliwa na kama amezaliwa kwa njia ya kawaida au upasuaji na vifaa vilivyotumika.
“Tupo hapa kwa ajili ya kusisitiza wananchi wasitumie dawa bila kujua wanaumwa na nini kwani kuna tabia unaumwa kidogo unakwenda duka la dawa unachukua dawa mwishowe zile dawa zinaacha kufanya kazi”Alisema
Dkt Naima alisema kwa sababu utakwenda kununua kwa hela ulionayo anunua dozi ambayo haijakamilika na unanunua dawa hujui unaumwa na nini ni vijidudu gani vimesababisha hali hiyo”Alisema
VIFAA VYA MAWASILIANO 108,395 VYAFUNGWA

CRDB WAKALA : MUONGO MMOJA WA KUWEZESHA JAMII NA KUBORESHA MAISHA NCHINI
Monday, 24 July 2023
BABA KAIKIMBIA FAMILIA NA KWENDA KUOLEWA!

Mwaka 2014 mama yetu aliondoka nyumbani na kurudi kwao Iringa kutokana na tabia ya baba yetu ya ulevi na kuwa na wanawake wengine nje ndoa bila kujali yake inahitaji matunzo.
Baada ya mama kuondoka maisha ya nyumbani yalibadilika sana, baba akawa anakunywa pombe hadi anamaliza siku bila mbili kurejea nyumbani.
Hatimaye tulipata habari kuwa baba kaolewa na mwanamke mwenye Baa alipokuwa anakunywa pombe mara kwa mara, basi nilibeba jukumu la kuwalea wadogo wangu.
Maisha ambayo tulikuwa tunapitia tulitambua kuwa chaguo baya zaidi maishani ni kuchagua mume au mke asiye kuwa na sifa nzuri na ndicho kilichomgharimu mama yetu hadi kuja kutufikia sisi.
Kutokana na hilo, nilikuwa makini sana na wanaume ambao walikuwa wanaomba kunioa ila mimi nilikuwa nimeandaa sifa tatu muhimu ambazo mwanaume yoyote atakayetaka kunioa lazima awe nazo kuepuka kuwapatia tabu na shida watoto wangu.
Nilipofikisha miaka 24 shangazi yangu akaniambia kuwa natakiwa kuolewa kwa sababu umri unaenda, mimi sikujali kwa sababu niliona bora nisiolewe kuliko kuolewa kisha nikaanza kujutia.
Siku moja nikiwa nyumbani rafiki yangu Rita alikuja kunijulia hali na wadogo zangu, Rita ni rafiki yangu tangu tukiwa shule ya msingi hivyo alikuwa anajua mengi sana kunihusu.
Katika stori zetu aliweza niambia kuwa alimfunga Boyfriend wake asiweze kumpenda msichana mwingine zaidi yake hadi wakimaliza Chuo na kufunga pingu za maisha. Nilipomuuliza alimfunga kivipi ndio akanipatia namba hizi +254 769 404965 na kuniambia ni za African Doctors.
Akanieleza kuwa African Doctors anaweza nisaidia kumpata mwanaume mwenye sifa nizitakazo kwa muda mfupi tu, siku kadhaa zilizipita nikaamuua kutembelea tovuti yao www.african-doctors.com na kuona kweli wana huduma hiyo.
Nikiwa bado katika tovuti yao niliona namba ile niliyopewa na Rita kisha nikatuma ujumbe WhatsApp kwa ajili ya kuomba msaada, African Doctors alinijibu vizuri kisha akaniambia kuwa nimtumie sifa za mume ambaye namhitaji.
Nilituma kisha akaniomba nisubiri kwa masaa 48 tu nitaweza mtambua mtu sahihi kwangu, masaa 48 kabla ya kuisha aliweza kujitokeza kijana kutoka Kondoa mjini kisha kuniomba kuwa mke wake. Nilipotazama kila sifa niliyotaka alikuwa nayo, hatimaye tulifunga ndoa na kwa sasa tunaishi wote kwa amani na furaha.
Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.
Mwisho.




.jpeg)

.jpeg)











