Monday, 24 July 2023

MAKAMU MWENYEKITI CCM BARA APONGEZA USIKIVU , UTULIVU WA RAIS SAMIA KATIKA KULIONGOZA TAIFA


Na Said Mwishehe, Kondoa

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahaman Kinana, ameeleza kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ni msikivu,mtulivu na mwenye kupokea ushauri na kutoa uamuzi kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.

Amesema chini ya uongozi wa Rais Samia Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo na kwa sasa hata ukusanyaji wa mapato umekuwa uko juu kuliko wakati wowote ule katika nchi yetu, hivyo amesema hata wanapompongeza na kumsifu ni kutokana na kazi kubwa na nzuri anayoendelea kuifanya.

Mzee Kinana ameyasema hayo leo Julai 23, mwaka 2023, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ulioandaliwa na Mbunge wa Kondoa Dk.Ashatu Kijaji kwa ajili ya kuelezea utekelezaji wa Ilani katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia.

"Katika kipindi cha miaka miwili Rais Samia amefanya mambo makubwa ya maendeleo na hiyo inatokana na uongozi wake mzuri unatokana utulivu, usikivu, kupokea ushauri na kufanya uamuzi wa busara kwa manufaa ya Watanzania. Kwa hali ilivyo na kwa hatua tuliyopiga tukienda hivi tunavyokwenda mpaka kufika 2025...

"Nina uhakika kila Mtanzania atakuwa na sababu ya kusema tuendelee na CCM, tuendelee na Rais Samia Suluhu Hassan. Hatutokuwa na sababu nyingine yoyote kwanza ni utamaduni wetu Chama Cha Mapinduzi hatubadilishi uongozi katikati ya safari, ukitaka kubadilisha sababu itakuwa nini, hakuna, " amesema Mzee Kinana

Amesisitiza lazima wampe nafasi ili yale aliyokusudia chini ya uongozi wa Chama chetu yatimie."Ikifika 2025 tunakwenda na Rais Samia.Hatusemi haya kwa kujivuna bali kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM lakini tunaangalia na wenzetu wa nchi jirani wanakwendaje.

"Nchi yetu imetulia, inamaani, ina umoja, inamshikamano, nchi ina malengo, na ina mipango ambayo inatekelezwa na kila mtu ni shahidi, CCM itaendelea kuchaguliwa kwa sababu ina sera nzuri ina Ilani nzuri inayotekelezeka,” amesisitiza.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuzungumzia umoja na mshikamano walionao watanzania ambao uko imara na ndio maana kuna watu wamejaribu kuwagawa wananchi kwa misingi ya udini wameshindwa, wamejaribu kuwagawa kwa misingi ya ukabila wameshindwa.

" Kuna watu wamejaribu kutugawa kwa misingi ya ubara na visiwani wameshindwa huku akifafanua katika Bara la Afrika ziko nchi nyingi zimeajaribu kuungana na wanazifahamu ikiwemo Afrika Magharibi na nchi za Uarabuni zote zimesambaratika umoja haupo, lakini Tanzania muungano wao umeendelea kuwa imara na mwakani muungano huo unafikisha miaka 60.

“Sababu ni misingi imara iliyojengwa na wasisi wa taifa letu hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na marehemu Abeid Aman Karume, misingi yenyewe migumu na mnakumbuka katika kipindi mbalimbali muungano wetu umepitia kashikashi lakini tumeendelea kuwa imara,” amesema Kinana.

Ameeleza kwamba anaungana na viongozi wengine pamoja na wananchi kumpongeza Mwenyekiti wa Chama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia kwa uongozi wake madhubuti.

Pia amesema chini ya uongozi wa Rais Samia makusanyo ya fedha yameongezeka na yamekuwa juu kuliko wakati wowote.“Fedha hizo ni mapato ya ndani, mapato ya nje. Mapato ya ndani yaliyokusanywa na serikali katika miaka hii miwili kwa kila mwezi yako juu kuliko kipindi chochote, makusanyo yamefanikiwa bila mtu kusukumwa, bila kutishwa bila mtu kuwekwa mahabusu.

“Hivi karibuni kulikuwa na mashirika mawili duniani ambayo yanafanya tathimini ya hali ya uchumi na namna nchi inavyoweza kukopesheka.Mashirika yote mawili yametoa alama ya juu kwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

"Maana yake ni nini ukitaka kupewa msaada hawa wanaaminika, watatumia misaada vizuri hawataiba, hawatatumia vibaya, hatawapoteza mkitaka kwenda kutafuta mkopo kwa tathimini yao Tanzania tunakopesheka,”amefafanua Kinana.

Kwa upande wake Dk. Kijaji wakati anaelezea utekelezaji wa Ilani Kondoa amempongeza Rais Samia kwa kuitazama kwa karibu Kondoa ambapo katika kipindi cha miaka miwili na nusu miradi ya maendeleo imepelekwa katika sekta mbalimbali na hiyo ni kutekeleza ahadi ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Ilani yake ya Uchaguzi.

Amesisitiza kwamba anatoa shukrani kwa Serikali chini ya uongozi thabiti wa Dk.Samia kwa kutekeleza kwa vitendo na kwa ufanisi mkubwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 .

"Kwa wananchi wetu wa Jimbo la Kondoa kila mmoja wetu anaona kwa macho miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa."


Share:

Sunday, 23 July 2023

MKUTANO WA CHADEMA TEMEKE KUPINGA BANDARI WASUSIWA NA VIONGOZI, WANANCHI

 

* Zitto, Lipumba wakwepa mtego, wautosa mkutano huo

* Wananchi wachache wahudhuria, wengi wachoshwa na siasa za uchonganishi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkutano ulioandaliwa leo na chama cha upinzani cha CHADEMA na kada wake wa zamani, Wilbrod Slaa, kwenye viwanja vya Bulyaga, Temeke, jijini Dar es Salaam, umepooza baada ya kususiwa na viongozi wa vyama vikubwa vya siasa na wananchi.

Ingawa makada wa CHADEMA walisambaza mabango mengi kwenye mitandao ya jamii kuonesha viongozi wakubwa wa vyama vya siasa na makanisa kuwa watahudhuria mkutano huo, hali halisi iliyotokea leo ni kuwa mkutano huo umehudhuriwa na viongozi na wananchi wachache kuliko matarajio ya waandaaji wake.

Viongozi wachache wa makanisa ambao wanaegemea CHADEMA walihudhuria mkutano huo, huku wananchi wengi wakiamua kususia mkutano huo wa hadhara.

Slaa amekuwa akihangaika takribani kwa wiki nzima sasa kuandika barua kwa viongozi kadhaa wa vyama vya siasa, maaskofu wa makanisa na viongozi wastaafu wa serikali kuwaomba wahudhurie mkutano huo.

Lakini vyama vikubwa vya siasa, ikiwemo ACT-Wazalendo na CUF wameamua kutohudhuria mkutano huo baada ya kubaini nia ovu ya Slaa na CHADEMA ya kufanya upotoshaji mkubwa kwenye suala la uwekezaji wa bandari ya Dar es Salaam na kuchochea nyufa za dini kwa kutumia baadhi ya maaskofu.

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, na Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, ni miongoni mwa viongozi wa vyama vikubwa vya siasa ambao walikwepa mtego wa kuhudhuria mkutano huo wa CHADEMA na Slaa.

Video na picha kutoka viwanja vya Bulyaga, Temeke, zimeonesha wananchi wachache kuhudhuria mkutano huo, huku wengi wakiamua kupuuzia hadhara hiyo.

Wahudhuriaji wa mkutano huo waliojitokeza ni makada wa CHADEMA kutoka Temeka na makao makuu, pamoja na viongozi wao, huku wananchi wa kawaida wachache sana wakijitokeza.

"Wananchi tumechoshwa na siasa za udini na ubaguzi wa Zanzibar na Tanganyika zinazoenezwa na viongozi wa CHADEMA kwa kisingizio cha kupinga mkataba wa bandari," Shomari Mzee, mkazi wa Temeke stendi alisema.

"Nawashangaa sana pia hawa maaskofu kuamua kupanda jukwaani na wanasiasa wa CHADEMA kujihusisha na siasa za uchonganishi."

Licha ya kuwa Slaa amejiweka mbele kama muandaaji wa mkutano huo, mkutano huo umetawaliwa na viongozi wa CHADEMA, huku ikiwekwa nembo ya chama hicho na picha kubwa ya Mbowe kwenye bango nyuma ya meza kuu.

Makada wa CHADEMA pia wamekuwa wakiupigia debe mkutano huo kupitia mitandao ya jamii kama mkutano wa chama chao.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ilitoa onyo kwa CHADEMA kabla ya mkutano kuwa kuwahusisha maaskofu kwenye mikutano yao ya siasa siyo sawa kwani ni ukiukwaji wa sheria za nchi ambazo zinakataza vyama vya siasa kutumia udini kufikia malengo yao.

Hata hivyo, CHADEMA wamekaidi onyo la Msajili wa Vyama vya Siasa na kuwapandisha maaskofu kwenye jukwaa katika mkutano wao wa leo wa Temeke, kinyume na sheria za nchi.

Kitendo cha CHADEMA kuwatumia maaskofu kwenye majukwaa yake ya kisiasa kinaweza kusababisha mpasuko mkubwa wa kidini nchini, na kuhatarisha tunu ya umoja na uvumiliaji wa tofauti za dini ambao umeasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume.
Share:

MZEE KINANA AHIMIZA UMOJA, MSHIKAMANO KWA WANA CCM


Na Said Mwishehe, Kondoa

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana, amewahimiza wana CCM kuwa wamoja na kujenga mshikamano ili kwenda katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 pamoja na uchaguzi mkuu wakiwa wamoja na kuibuka washindi pamoja.

Akizungumza leo Julai 23, 2023 kwenye kikao cha ndani cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kondoa mkoabi Dodoma pamoja na mambo mengine Kinana ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wana CCM kuendelea kuwa wamoja katika kila jambo hasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani .

"Nipongeze kazi kubwa inayofanywa na viongozi wa CCM hususan katika ngazi kitongoji, Kijiji, mtaa na Kata kwa kazi nzuri mnayoifanya. Mwakani ni mwaka wa Uchaguzi, hivyo naamini wana CCM tutakwenda kwenye uchaguzi wa Serikali za Mtaa mwaka 2024 tukiwa kitu kimoja," amesema Mzee Kinana.

Ametumia nafasi hiyo kueleza Chama pia kinatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotelewa na viongozi wa CCM katika ngazi za kata, vitongoji, vijiji, wilaya na mkoa kwani wao ndio wanaokutana na wananchi na wakati wa uchaguzi ndio wanaokwenda kuomba kura.

Pia, amewapongeza madiwani wanaotokana na CCM ambao wamekuwa wakisimamia ngazi ya Kata na wamekuwa wakifanya hivyo bila ya kuwa na mshahara lakini wameendelea kujitoa kwa kuwatumikia wananchi.




Share:

WAZIRI AWESO ATAKA WANANCHI VIJIJI PEMBEZONI MWA ZIWA VICTORIA VIPATE HUDUMA YA MAJI




Na Mariam Kagenda _ Kagera

Wataalamu wa Wizara ya Maji wameelekezwa kuweka mpango mkakati wa kuhakikisha vijiji ambavyo vipo pembezoni mwa ziwa Victoria vinanufaika na uwepo wa ziwa hilo ili wananchi wapate suluhisho la kudumu na kupata maji safi na salama.


Maelekezo hayo yametolewa na Waziri wa Maji Jumaaa Aweso wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Nkenge katika halmashauri ya wilaya ya Misenye ambapo kabla ya mkutano wake wa adhara na wananchi hao alizindua mradi wa maji Katolerwa_Ishozi ambao unahudumia wananchi wapatao 7278 uliopo kata ya Ishozi.


Waziri Aweso amesema kuwa mkoa wa Kagera una ziwa Victoria, mto Kagera hivyo maeneo ya vijiji ambavyo vimeambatana na uanda wa ziwa Victoria hivyo lazima mpango mkakati uwekwe kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wananufaika na Ziwa hilo.




Amesema kuwa maelekezo hayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na lazima vijiji hivyo vinufaike kwasababu ni maelekezo pia ya Rais Dkt Samia Suruhu Hassan katika dhana yake ya kumtua mama ndoo kichwani.


Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Nkenge halmashauri ya wilaya ya Misenye Frolent Kyombo amesema kuwa kata ya Ishozi haikuwai kuwa na mradi wa maji huo ni wakwanza ambapo hapo awali wananchi walikuwa wanatumia vyanzo vya maji.


Ameishukuru serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwakumbuka wananchi wa wilaya hiyo hasa kwa kutatua changamoto ya maji.


Naye Meneja wa Ruwasa ambao ni wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijni Injinia Andrew Kilembe wakati akisoma taarifa ya mradi wa maji Katolerwa_Ishozi amesema kuwa ujenzi wa mradi huo ulianza January 25 2022 na kwa sasa mradi huo umekamilika.


Aidha mradi huo unahudumia wananchi wa vijiji vya Nyarugongo 2543,Katano 1365,Luhano 1708 na Katolerwa 1662 ambapo kwa sasa shughuli zinazoendelea ni kuunganisha maji majumbani.



Share:

WATANZANIA MSIWE NA SHAKA NA MAONO YA RAIS KATIKA BANDARI-CHONGOLO


***************

*Asema maono yake kwenye filamu ya Royol Tour utalii umejibu

*Asisitiza CCM haina muda wa kujibu lugha za matusi, wao wanaongoza nchi

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV –Arusha

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amesema kwanini watanzania wawe na shaka na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu uwekezaji unaotaka kufanywa katika bandari ya Dar es Salaam wakati maono kama hayo yamefanya vizuri katika filamu ya Royal Tour na utalii umejibu.

Chongolo ameyasema hay oleo Julai 22,2023 alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara ambapo pamoja na mambo mengine alielezea dhamira ya Serikali katika uwekezaji wa bandari hiyo ukiwa na lengo la kuongeza wigo wa ukusanyaji wa fedha ambazo zitatumika katika kutatua changamoto za wananchi.

“Moja ya kazi ya msingi ya Serikali ni kukusanya fedha na kutafuta fedha za kutekeleza na kutatua changamoto za wananchi, kazi ya serikali sio kupiga makofi , kushangilia, kazi yake ni kutatua changamoto na ili utatue changamoto lazima utengeneze uhakika wa mapato, ili uwe na uhakika wa kutatua changamoto lazima uwe na fungu la kutosha kufanya hivyo.

“Nimesema hapa kwa kutaja barabara zitakazojengwa mkapiga makofi , fedha zinazotakiwa kujenga hizo barabara ni zaidi ya Sh.Trilioni 3.7. Fedha hizi usipokuwa nazo utabaki na ahadi isiyotekelezeka kwa muda mrefu, Serikali makini haikai kushangaa bali inatafuta namna sahihi ya kwenda kutafuta fedha za kutatua changamoto,”amesema.

Amefafanua ndio maana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua bila fedha hawezi kufanya mambo alifikiri na kubuni na kuja na mpango wa kutangaza utalii wa nchi hii kupitia Royal Tour na wakati anapita huko porini kila siku kurekodi ile filamu kwa ajili ya hayo matangazo watu walimbeza wakaona kama anachokifanya hakina maana.

“Leo ninyi wote ni mashahidi , hivi ni wangapi wanapeleka salamu za kumshukuru baada ya filamu ya Royal Tour kujibu? Leo wanaonufaika ni wenye magari ya utalii ni Mama Samia ? Wenye hoteli zinazolaza watalii ni Rais Samia ? Na wale wanaondesha magari wakitoka kule na noti mfukoni wakija wanakuja kununua bidhaa kwenye maduka yetu wanaonufaika ni Rais Samia?

“Ni sisi, tunaona ni jambo la kawaida kwasababu imekaa vizuri, hatukumbuki kama kuna mtu alikesha akabuni,akamua, akachukua hatua ya kutekeleza kufanya matangazo kwa ajili ya kutangaza utalii wa nchi yetu leo tunaonufaika tunakula kiulani hatumkumbuki, hatufikirii , tunamlundukia jambo jipya sisi tunakula starehe, hatutendi haki

“La utalii limetiki sasa tumekwenda kwenye bandari , kelele zao mnazisikia hamzisikii ? kama alikuwa na maono kwenye Royal Tour na utalii umejibu mashaka ya Bandari yanatoka wapi ? Walionitangulia wameeleza kwa kina kuhusu makubaliano ambayo tumeingia na Serikali ya Dubai.Sitaki kurudi huko.”

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuhusu upotoshaji kuhusu bandari ulipoanza mpaka ulipofikia , mwanzo wapotoshaji walikuja wakasema bandari imeuzwa kwa miaka 100 , walipoona jambo hilo lina majibu na limejibiwa wakabadilisha wakasema shida ni uwekezaji hivyo waachane na uwekezaji.

“Walipoona tumewajibu na kuwaambia uwekezaji ni muhimu hakuna anayerudi nyuma tunasonga mbele kama mna kipengele mnachangamoto leteni tujadili tukiweke sawa tusonge mbele tukiwa na mkataba ambao ninyi mtaona unafaa na sisi tutaona unafaa mpaka leo hakuna aliyeleta mapendekezo, wanazunguka tu

“Wameenda mbali wamekosa hoja sasa wameamua kuanza kutukana , sasa mtu akishakosa hoja akaanza kutukana na sisi ni waungwana tunadhamana ya kuwahudumia watanzania tukiingia kuanza kutukana itakuwa kituko, tuna wajibu wa kuongoza nchi, kazi ya kuongoza ya nchi sio lele, mama lazima tukae mguu sawa, lazima tuwe timamu kuhakikisha tunatatua changamoto za watanzania.

“Hatuko kutukanana wala kujibu upuuzi, tupo kutibu changamoto na kutatua changamoto za wananchi.Lakini ukiona hutukanwi ujue hufanyi wewe ukitaka usitukanwe jifungie ndani lala , ukitaka usitukane nenda tu kawe mtu hohe hahe , wewe si asubuhi si mchana upo nani atakutukana…

“Kwasababu huna cha kutukaniwa, sisi tunawajibu wa kufanya matusi, kebehi na maneno yote ya dharau tunayakaribisha ni haki yetu kwasababu tunafanya. Kazi ya kuongoza nchi ni kazi kubwa , kazi ya kutunaka ni rahisi , kazi ya kumfanya mtanzania kuwa na uhakika wa afya, mtoto kusoma, uhakika wa barabara , mlo wake sio kazi ya lele mama ni kazi kubwa ni kazi inayokutaka uwe sawa sawa.

Share:

KATIBU MKUU CCM ASEMA HAWATARUDI NYUMA UWEKEZAJI BANDARI DAR, AKARIBISHA MAONI

-Awaomba wananchi waiamini Serikali ya CCM kwani haina nia mbaya
-Awaonya wanaotoa maneno ya kuchonganisha viongozi, serikali


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV- Arusha


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewaambia maelfu ya wananchi wa Kanda ya Kaskazini kwamba uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam hawatarudi nyuma kwa kuwa lina tija kwa Watanzania.

Akizungumza leo kwenye mkutano wa hadhara uliohusisha wananchi wa Mkoa wa Arusha, Manyara na Kilimanjaro, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid,Chongolo amewaomba wananchi waiamini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).

"Sisi Chama Cha Mapinduzi tutakuwa wa mwisho kutetea jambo ambalo halijakaa sawa kwasababu tunajua ikifika wakati wa kuomba kura sisi ndio tutakuja kwa wananchi, kwanini kujitetea kama tunajua jambo haliko sawa.

" Tunasema haya tukiwa na nguvu tukiwa kifua mbele kwamba jambo hili linatija kwa nchi, lina tija kwa maendeleo ya nchi na tuliahidi wenyewe na kwa hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi na sisi ni sehemu ya Watanzania na ni Watanzania

"Tuna haki ya kusimamia mambo mazuri yatokeee na hili haturudi nyuma , nisisitize watalaam na wajuzi wa sheria ambao wana maoni na ushauri wa namna ya kurekebisha baadhi ya vipengele vikaleta tija zaidi ya ilivyosasa...

" Waje mezani wajadili washauri ili tuboreshe zaidi tutoke tukiwa na kitu ambacho kinaenda kuongeza tija kwa nchi yetu lakini sio vinginevyo,sio kutunga uongo, sio kuchonganisha wananchi na serikali yao ,hatuko tayari, hatutavumilia na hatuko tayari kukaaa kimya kuacha hayo yakitokea."

Akieleza zaidi mbele ya maelfu ya wananchi hao Chongolo amesema uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam lengo kwa ujumla wake linalenga kuongeza tija , kwani kwa sasa kiwango kinachokusanywa kwa asilimia 99 kinatumika pale pale kwenye uendeshaji.

"Maana yake sisi kama nchi hatunufaiki , kuongeza kwenye mfuko wa Serikali kutatua changamoto za wananchi kupitia uzalishaji au mapato yanayotokana na bandari, " amesema Chongolo alipokuwa akizungumzia faida za uwekezaji utakaofanyika bandari ya Dar es Salaam.



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 23,2023

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger