Saturday, 22 July 2023

TOENI ELIMU VIJIJI VINAVYOPANDISHWA HADHI-DKT MABULA


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa tatu kushoto) akifuatilia maelezo ya Mkuu wa wilaya ya Biharamulo Advera Bulimba wakati alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi katika eneo la Lusahunga Wilayani Biharamulo mkoa wa Kagera tarehe 21 Julai 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Biharamulo Advera Bulimba wakifuatilia maelezo yanayotolewa na Razalo Kasigala kuhusina na mgogoro wa ardhi baina ya Kanisa Katoliki na serikali ya kijiji cha Lusahunga tarehe 21 Julai 2023.

****************

Na Munir Shemweta, WANMM BIHARAMULO

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka ofisi za ardhi kuhakikisha zinafuata taratibu na kutoa elimu kwa wananchi hasa katika ardhi za serikali za vijiji zinapopandishwa hadhi na kuwa mamlaka za miji.

Waziri Mabula ametoa kauli hiyo tarehe 21 Julai 2023 katika eneo la Lusahunga wilayani Biharamulo mkoani Kagera alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Rulenge na serikali ya kijiji cha Lusahunga.

Mgogoro huo umeibuka kufuatia serikali ya kijiji cha Lusahunga kutaka sehemu ya eneo lililoombwa na Kanisa Katoliki kwa madai kuwa ndiyo yenye mamlaka. Hata hivyo, Tangazo la Serikali Na 76 la mwaka 1996 lilitangaza eneo hilo kuwa mamlaka ya mji na kulifanya kutoka katika sheria namba 5 ya vijiji na kwenda sheria ya mipango miji.

Sheria namba 8 ya mipango miji ya mwaka 2007 inaipa mamlaka halmamshauri ya wilaya kusimamia mpango wa uendelezaji na hivyo kufanya serikali ya kijiji kutokuwa na mamlaka tena ya kugawa ardhi.

‘’Maeneo ya vijiji yanapopanda hadhi ni lazima taarifa zifike kwa wahusika ili wajue kuwa sasa eneo hili haliko kwetu na liko kwenye mamlaka nyingine’’ alisema Dkt Mabula

Alisema, wilaya ya Biharamulo ina vijiji vingi vilivyopandishwa hadhi na katika kuepuka migogoro ya aina hiyo ameelekeza halmashauri ya wilaya kupita kijiji kwa kijiji kufahamisha wananchi mabadiliko hayo.

‘’Ninaelekeza mkawafahamishe kwa maandishi viongozi wa serikali za vijiji vilivyopandishwa hadhi kuwa hawaruhusiwi kugawa ardhi tena na kama watahitaji kwa ajili ya shughuli za kijiji basi watawasiliana na ofisi ya mkurugenzi kwa kuwa mamlaka ya usimamizi wa utawala wa ardhi hayako kwao tena yapo halmashauri ya wilaya’’ alisema Dkt Mabula

Alisema, watumishi wa sekta ya ardhi wakifuata taratibu sambamba na kuwafahamisha wananchi mabadiliko yanayotokea kwa vijiji vinavyopandishwa hadhi basi hakutakuwa na migogoro na wakati huo shughuli katika maeneo hayo zitakuwa zimewezeshwa.

‘’Eneo lako likipimwa na kupata hati unaweza kuitumia kuchukulia mkopo benki kwa kuwa ardhi yako itakuwa imepanda thamani na hata unapotaka kuuza ni tofauti na yule asiye na hati’’. Alisema Dkt Mabula

Akigeukia mgogoro kati ya Kanisa Katoliki na Serikali ya kijiji cha Lusahanga, Dkt Mabula ametaka makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande hizo mbili ya Kanisa Katoliki kupatiwa ekari 50 yaendelee na kusimamiwa na mkuu wa wilaya na kueleza kuwa ekari 95 zilizobaki zitakuwa chini ya halmashauri ya wilaya ya Biharamulo ambapo kama kijiji kikitaka eneo kinapaswa kuomba huko.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (kulia) akimsikiliza Askofu wa Jimbo Katoliki Rulenge-Ngara Severine Niwemugizi alipowenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya Kanisa Katoliki na serikali ya kijiji cha Lusahunga tarehe 21 Julai 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Lusahunga wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera alipowenda kutatua mgogoro wa ardhi kati ya Kanisa Katoliki na serikali ya kijiji cha Lusahunga tarehe 21 Julai 2023.
Sehemu ya wananchi wa Lusahunga wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya Kanisa Katoliki na serikali ya kijiji cha Lusahunga tarehe 21 Julai 2023.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)


Share:

UKICHEZA SLOTI YA KASINO HII UNAENDA KUWA BINGWA!!

Unaweza kuwa mwenye bahati sana ukiingia nyumba ya mabingwa Meridianbet, michezo ya ubashiri soka, bonasi na kasino ya mtandaoni ni vyumba vya utajiri. Mbali na hilo kuna Sloti ya Weight of the Gun ina mistari 15 ya malipo.

 

Mchezo huu unaangazia Wild West na saluni, benki na ofisi ya sheriff ikiwa nyuma yake. Utaona kivuli cha mti na bastola ambayo mara kwa mara itageuzwa kwa bunduki yake.

 

Sloti ya Weight of the Gun ya kasino ya mtandaoni inaonesha mtu jasiri ananusurika na mapambano. Sheriff yupo hapa kushughulikia mambo, lakini sio rahisi kwake. Mchunga ng’ombe aliye na bastola anapoegemea mti na kuvuta sigara, alama huwashwa kwenye nguzo.

 

Rangi ya mchezo huu wa kasino ya mtandaoni ya Meridianbet ni bluu na inaonesha mandhari ya usiku, alama zina muundo mzuri na zimeundwa kulingana na mada.

 

Alama za Weight of the Gun!

 

Alama ambazo utaziona kwenye safuwima kwenye kasino ya mtandaoni sloti ya Weight of the Gun zimegawanywa katika makundi mawili, kama alama za bei ya chini ya malipo na alama za thamani ya juu ya malipo.

 

Alama ambazo zina thamani ya juu ya malipo huoneshwa kama ndege aina ya tai, dansi yao, salama iliyojaa dhahabu, msichana na sherifu. Alama za thamani ya chini zinaoneshwa na alama za karata.

 

CHEZA HAPA

 

Alama ambazo zitaashiria ushindi kwenye kasino ya mtandaoni zina muundo mzuri na rangi nzuri. Kama alama za thamani ya chini ambapo kuna alama za karata A, K, Q, J, 10.

 

Alama za thamani ya juu ya malipo huoneshwa na matunda yenye sura ya kigeni. Utaona mti wa matunda wa machungwa na ua, moja ya zambarau inayofanana na kitunguu, mti wa matunda mekundu na ya kijani.

 

Ishara ya Wild na ina uwezo wa kuchukua nafasi ya alama nyingine za kawaida, isipokuwa alama za kutawanya.

 

Jokeri anaweza kuonekana kwenye safu yoyote, lakini utahitaji kupokea alama 5 kupitia namba ya malipo ya tuzo ya pesa. Malipo haya yanafaa mara 500 kwa amana yako.

 

Alama ya kutawanya inakuja na uandishi wa Mizunguko ya Bure na itakupa mapato na ziada ya mizunguko ya bila malipo.

 

Bila kusahau mchezo huu wa kasino ya mtandaoni inakupa nafasi ya kupata bonasi kibao na mizunguko mingi ya bure kuendelea kusaka hela.

 

Chini ya sloti hii kuna jopo la kudhibiti na chaguzi zote muhimu kwa ajili ya mchezo. Kubofya kitufe cha Dau +/- hufungua menyu ambapo unaweza kuchagua ukubwa wa mizunguko yako.

 

Kitendaji cha Kucheza Moja kwa Moja kinapatikana pia, ambacho unaweza kukiwezesha wakati wowote. Unaweza kuweka hadi mizunguko 100 kupitia chaguo hili la kukokotoa. Unaweza pia kuweka kikomo kwenye ushindi na hasara zako.

 

Kwa kifungo cha “na” unaweza kuingia kwenye orodha ya habari ambapo unaoneshwa alama na maadili yao. Unaweza pia kusoma sheria za mchezo hapa hapa.

 

CHEZA SASA.

Mizunguko ya Bure

 

Habari njema ni kwamba sloti ya Weight of the Gun ina duru ya bonasi ya mizunguko ya bure ambayo huanza na alama za beji tatu au zaidi za sheriff.

Kulingana na idadi ya alama za kutawanya ambazo mzunguko wa bonasi umekamilishwa nazo, unaweza kushinda idadi ifuatayo ya mizunguko ya bure ya bonasi:

 

  • Alama 3 za kutawanya zitakutuza kwa mizunguko 10 ya bonasi bila malipo
  • Alama 4 za kutawanya zitakutuza kwa mizunguko 12 ya bure
  • Alama 5 za kutawanya zitakutuza kwa mizunguko 15 ya bonasi bila malipo

Ukipata alama tatu zaidi za kutawanya wakati wa duru ya bonasi, mizunguko 5 ya ziada ya bonasi inakungoja.

 

Weight of the Gun sloti ina michezo ya bonasi, na mizunguko ya bure ambayo inaweza kukuletea ushindi wa kuvutia.

Yaani, mwizi anayewezekana wa benki ni ishara ya bonasi inayoonekana katika safuwima za 1, 3 na 5.

 

Ukipata alama zote tatu utawasha Bonasi ya Mexican Standoff. Utakabiliana na bastola tatu, lakini usijali, una faida ya kuwa na kasi zaidi kwenye sare.

 

Kisha utaona targets 12 zimepigwa kwenye skrini. Kazi yako ni kufikia target yoyote mionngoni mwa tatu ili kushinda zawadi za pesa taslimu papo hapo.

 

Sloti ya Weight of the Gun wa kasino ya mtandaoni imejaa vipengele vya bonasi, kwa hivyo mchezo wa kamari unakungoja ambapo unaweza kuongeza ushindi wako mara mbili na mara nne.

 

Katika mchezo wa kamari, unahitaji kukisia rangi ya karata, au ishara, ili kushinda. Rangi zinazopatikana kwa kubahatisha ni nyekundu na nyeusi.

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 22,2023

 









         

          
Share:

Friday, 21 July 2023

Shirika la WOTESAWA latoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wafanyakazi wa nyumbani, vijana

Shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani WOTESAWA limetoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wafanyakazi wa nyumbani pamoja na vijana wanaounda vikundi mbalimbali vya ujasiriamali jijini ili kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa zinazokidhi viwango vya ubora.

Mafunzo hayo ya vitendo yamefanyika kwa muda wa siku tano kuanzia Jumatatu Julai 17 hadi Ijumaa Julai 21, 2023 yakijumuisha washiriki 45 kutoka Kata za Mahina na Buhongwa jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuhamasisha haki za kiuchumi na kijamii kwa wafanyakazi wa nyumbani na vijana unaotekelezwa kwa miaka miwili tangu mwaka 2022 kwa ufadhili wa shirika la Foundation For Civil Society (FCS). 

Msimamizi Msaidizi wa Mradi huo kutoka Shirika la WOTESAWA, Esther Petro alisema mafunzo hayo yatawasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia bidhaa wanazotengeneza hatua itakayowasaidia kuondokana na utegemezi ambao una mahusiano ya karibu na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

"Lengo kuu la shirika la WOTESAWA ni kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani, hata hivyo bila kuwawezesha kiuchumi bado wataendelea kukabiliana na vitendo vya ukatili hivyo tunaamini kupitia mafunzo haya wataweza kujikwamua kiuchumi na kutoendelea kuvumilia vitendo vya ukatili wakiwa kwa waajiri wao" alisema Esther.

Esther aliebainisha kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kutambua umuhimu wa kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo za viungo, chakula na vinywaji ambazo zinakidhi ubora, kusajili biashara zao na kulipa kodi pindi zinapofikia hatua ya ukuaji.

Naye Afisa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa Mwanza, Giliard Abel akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo alisema wajasiriamali wengi hushindwa kurasimisha biashara zao kutokana na ukosefu wa elimu hivyo mamlaka hiyo inaendelea kuelimisha jamii kutambua taratibu za uanzishaji biashara, kupata namba ya mlipa kodi pamoja na sifa za anayepaswa kulipa kodi na anayestahili kupata msamaha wa kodi.

Kwa upande wake Mkaguzi kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mkoa Mwanza, Nelson Mugema alisema ni muhimu wajasiriamali wanaozalisha bidhaa mbalimbali kuthibitisha ubora wa bidhaa zao kupitia TBS kwani hatua hiyo inawasaidia bidhaa zao kushindana sokoni huku akiongeza kuwa kwa sasa wajasiriamali wanaoanza uzalishaji wanayo fursa ya kujisajili kupitia SIDO ambapo wanapata msamaha wa kufanya shughuli zao kwa miaka mitatu bila kutozwa gharama zozote hatua inayolenga kuchochea vijana kukuza mitaji yao.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Martha Benjamini na Khadija Ramadhan walisema awali hawakuwa na uelewa kuhusu namna ya kurasimisha biashara zao hivyo wanatarajia kuyatumia vyema ili kuboresha zaidi shughuli zao.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Msimamizi Msaidizi wa mradi wa kuhamasisha haki za kiuchumi na kijamii kwa wafanyakazi wa nyumbani na vijana kutoka shirika la WoteSawa, Esthe Petro (kushoto) akiwa na mkufunzi wa mafunzo hayo (kulia) kwenye maandalizi ya kuandaa bidhaa ya pilipili ya kupika.
Mkufunzi akitoa ufafanuzi hatua za kufuata wakati wa kuandaa bidhaa mbalimbali ikiwemo viungo vya chakula/ pilipili.
Mafunzo yakiendelea.
Maandalizi ya kuandaa pilipili ya kupika.
Afisa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa Mwanza, Giliard Abel akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Mkaguzi kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mkoa Mwanza, Nelson Mugema akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Afisa Ustawi kutika Shirika la WoteSawa, Demitila Faustine akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA
Share:

RAIS SAMIA ARIDHIA HEKTA 18,031 KUTOLEWA KWA WANANCHI RUTORO


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili kushoto), Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega (wa tatu kushoto) na mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa (Kushoto) wakimsikiliza mmoja wa wawekezaji wa Ranchi ya Kagoma mkoani Kagera wakati wa ziara ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta wilayani Muleba tarehe 20 Julai 2023.

************
Na Munir Shemweta, WANMM MULEBA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameridhia kumegwa eneo la Ranchi ya Kagoma iliyopo wilaya ya Muleba DC na Karagwe mkoani Kagera yenye ukubwa wa hekta 18,031.26 kwenda kwa wananchi kuendelea na shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo makazi.

Hayo yamebainishwa tarehe 20 Julai 2923 katika kijiji cha Rutoro wilayani Muleba mkoa wa Kagera na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa kutoa mrejesho wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 kwa wananchi wa Rutoro.

Kufuatia kumegwa eneo hilo, wananchi wa Rutoro watakuwa wamepata asilimia 44.44 kutoka asilimia 100 ya Ranchi ya Kagoma huku asilimia 55.56 ikibaki katika ranchi hiyo ambapo Waziri wa Ardhi Dkt Mabula alisema kinachokwenda kuwatenganisha wawekezaji na wananchi baada ya maamuzi hayo ya serikali ni mipaka mipya itakayowekwa

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, vijiji ambavyo wananchi wake watanufaika na uamuzi huo ni Rutoro, Kyobuheke, Mishambya pamoja na Byengeregere.

‘’Serikali haijafanya makosa kufanya maamuzi hayo bali ni utaratibu unaolenga kuwapunguzia adha waliyokuwa nayo wawekezaji kwa kugombana na wananchi na mheshimiwa Rais hapendi hayo madhara yanayotokea kwa pande zote ndiyo maana uamuzi umechukuliwa kuwatenganisha’’ alisema Dkt Mabula.

Alisema, utaratibu uliotumika kutoa maeneo kwa wananchi katika kata ya Rutoro utasaidia kumaliza tatizo la Mwisa II kwa kuzingatia mapendekezo ya mkoa wa Kagera.

Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage mbali na kupongeza uamuzi huo wa serikali alionya wananchi wa Rutoro kuepuka kukaribisha watu mara baada ya uamuzi huo na kuwataka kutulia kuisubiri serikali iwapatie vitu walivyovikosa.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewataka wananchi kutovamia maeneo ya watu wengine hasa baada ya uamuzi huo na kueleza kuwa, kufanya hivyo ni kuingia katika hatia na serikali itachukua hatua kwa watakaofanya hivyo.

‘’Msivamie eneo la mtu yeyote hadi utaratibu utakapokuwa umekamilika na yaliyotangazwa hapa hayamfanyi mmoja kati yetu atoke aende kujimilikisha, atakayefanya vitendo visivyokuwa vya kiuungwana kwa kuvamia eneo hatakuwa na mtetezi kutoka upande wowote’’ alisema Ulega

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Khamis Hamza Chilo amewataka wananchi wa Rutoro kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo wanayoenda kuishi ili kutunza mazingira sambamba na kuondokana na athari ya tabia nchi.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Nazir Karamagi alisema, amefurahishwa na ziara ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta katika mkoa wake na kueleza kuwa ujumbe huo umekwenda na mamlaka kamili na kufanya maamuzi waliyokubaliana kuhusiana na utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika eneo hilo.

Naye Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo alieleza kuwa, anaamini baada ya mpango wa matumizi bora ya ardhi kuwekwa kwenye eneo waliopatiwa wananchi na hatimaye wakulima kupangwa vizuri basi utaratibu wa miradi ya umwagiliaji utapelekwa na wakulima watanufaika na miradi hiyo.

Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyohusisha Mwaziri kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mifugo na Uvuvi, Kilimo, Maliasili na Utalii, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo na wale wa Maji, TAMISEMI na Ulinzi imehitimisha ziara yake ya siku moja katika mkoa wa Kagera ikiwa ni muendelezo wa juhudi za kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.
Sehemu ya wananchi wa Rutoro wilayani Muleba mkoa wa Kagera wakifuatilia hotuba za Mawaziri wa Wizara za Kisekta walipokwenda kutoa mrejesho wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na mgogoro wa Matumizi ya ardhi katika eneo hilo tarehe 20 Julai 2023.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Khamis Hamza Chillo akizungumza wakati wa mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta katika eneo la Rutoro Muleba mkoa wa Kagera tarehe 20 Julia 2023.
Abdallah Ulega, Waziri wa Mifugo na Uvuvi akisisitiza jambo katika mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta eneo la Rutoro Muleba mkoa wa Kagera tarehe 20 Julia 2023.
Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akizungumza kwenye mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta katika eneo la Rutoro Muleba mkoa wa Kagera tarehe 20 Julia 2023.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Lucy Kabyemera (wa pili kushoto) akiwa katika mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Kisekta eneo la Rutoro Muleba mkoa wa Kagera tarehe 20 Julia 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger