Friday, 18 November 2022

JOHN SIAGI MAGETA MWENYEKITI MPYA WA WAZAZI CCM MKOA WA SHINYANGA...MZEE SIMBA DAH!

John Siagi Mageta 

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Novemba 18,2022 wamechagua John Siagi Mageta kuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambapo amepata kura 332 akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu Salim Abdalah Simba aliyekuwa anatetea kiti hicho ambaye amepata kura 160 na Halima Ismail Juma akipata kura 13. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Msimamizi wa Uchaguzi, Festo Kiswaga akizungumza wakati wa mkutano wa uchaguzi
John Siagi Mageta akiomba kura 
John Siagi Mageta akiomba kura 
Salim Abdalah Simba akiomba kura
John Siagi Mageta na Salim Abdalah Simba 
Halima Ismael Juma akiomba kura
Wagombea wakiomba kura kushoto ni Halima Juma Ismael,John Siagi Mageta na Salim Abdalah Simba.


Share:

MAHAFALI YA KWANZA CHUO CHA VETA 'SHY NET' YAFANA SHINYANGA


Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani pamoja na mgeni rasmi Mhe. Reuben Dotto wakiangalia Nguo zilizoshonwa na wahitimu wa fani ya Ushonaji.

Na Mwandishi Wetu - Malunde 1 blog

CHUO cha Shinyanga Network Training Center (SHY NET) kilichopo katika Kata ya Lubaga Mkoani Shinyanga, kimefanya mahafali ya 1 chuoni hapo, kwa kuwaaga wahitimu wa mwaka wa pili kutoka fani mbalimbali.

Mahafali hayo yamefanyika chuoni hapo Novemba 17,2022, na kuhudhuriwa na viongozi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali ,na Taasisi binafsi huku mgeni rasmi akiwa ni Diwani wakata ya Lubaga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Reuben Dotto.

Akizungumza kwenye Mahafali hayo Mkuu wa chuo cha SHY NET Shinyanga Abubakar Rehani, amesema chuo hicho kilianzishwa mwezi January mwaka 2022,na kuanza kutoa fani 2 ambazo ni fani ya ufundi Umeme ,Ushonaji na ubunifu wa mavazi , lakini mpaka sasa chuo kinatoa kozi za muda mrefu pamoja na kozi zamuda mfupi.


Amesema chuo kilianza kikiwa na mwanafunzi mmoja lakini wamehitimu wanafunzi 12 wa kiume wakiwa 7 na wa kike 5, na kubainisha kuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara hali inayopelekea wanachuo kushindwa kujisomea nyakati za usiku na barabara kushindwa kupitika kipindi cha mvua.

“Mgeni Rasmi chuo chetu kwa sasa tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme pamoja na ubovu wa miundo mbinu ya barabara ya kuja chuoni hivyo wanafunzi wengi kushindwa kujisomea nyakati za usiku na barabara kushindwa kupitika kipindi cha mvua”amesema Abubakari.


Pia, amesema changamoto nyingine ambayo inawakabili chuoni hapo, ni ukosefu wa huduma ya maji ambapo huingia gharama ya kuchimba visima na kutumia sora na jenereta wakati wa kusukuma maji.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wazazi, kuwasaidia watoto wao ambao wanahitimu mafunzo mbalimbali ya ufundi chuoni hapo kwa kuwanunulia vifaa au kuwapatia fedha za mitaji ili wajiajiri wenyewe, kuliko kuwaacha wakilandalanda mitaani na kulalamika hakuna ajira na wakati wana ujuzi wa kutosha.

Aidha Mwanafunzi Catheline Leonard akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake, amesema changamoto kubwa ambayo inawakabili wahitimu wa mafunzo ya ufundi ni ukosefu wa ajira na fedha za mitaji ili wapate kujiajiri wenyewe na ndiyo maana wengi wao huishia mitaani na kukaa bila kazi.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Lubaga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Reuben Dotto , amewatoa wasiwasi wahitimu wa SHY NET hasa wale ambao wanaishi Manispaa ya Shinyanga ,kuwa hakuna ugumu wowote wa kupata fursa zilizopo katika kata hiyo na Manispaa kwa ujumla kwa kuwa wana ujuzi unaweza kuwasaidia kujikwamua kimaisha.


Dotto ametoa ahadi pia kwa wahitimu wa fani ya umeme kuwa ataangalia namna ya kuwasaidia wale wanafunzi wa fani za umeme kwa kuwaombea kazi kwenye miradi mbalimbali ya manispaa hiyo ikiwamo ya ujenzi wa vituo vya afya, zahanati,Sekondari , huku akiwasihi wasione aibu kufungua ofisi yao na kujiajiri wenyewe hali itakayo wewezesha wahitimu kumudu soko la ushindani kwenye ajira, a


Akizungumzia suala la changamoto ya Umeme ,maji ,na barabara Dotto , amesema atafuatilia kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa kwa haraka ikiwemo kuhamasisha jamii kupeleka watoto wao wanao hitimu elimu ya kidato channe katika shule hiyo ili kuongeza idadi ya vijana wenye ujuzi katika kata hiyo na manispaa kwa ujumla.
Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani akitoa taarifa ya chuo hicho.
Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani akitoa taarifa ya chuo hicho.
Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani akimuongoza mgeni rasmi Mhe. Reuben Dotto na kumuonesha mazingira ya chuo.
Wahitimu mwaka wa Pili Chuo cha SHY NET wakimwelezea mgeni rasmi mbinu mpya ya kuunganisha umeme majumbani.
Mgeni rasmi Leuben Dotto pamoja na Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani wakisikiliza maelezo kutoka kwa wahitimu
Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani pamoja na mgeni rasmi Mhe. Reuben Dotto wakiangalia Nguo zilizoshonwa na wahitimu wa fani ya Ushonaji .
Mgeni Rasmi Reuben Dotto akizungumza na wazazi na walezi pamoja na wahitimu kwenye mahafali ya Kwanza ya Chuo cha SHY NET.
Mhitimu Catheline Leonard akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wengine.
Wanachuo wa mwaka wa kwanza wakielezea ujuzi walio pata mpaka sasa katika fani ya umeme.



Wahitimu wa mahafali ya kwanza chuo cha SHY NET SHINYANGA wakiimba wimbo maalum
Wahitimu wakionesha mtindo wa mavazi.
Mhitimu akionesha mtindo wa mavazi.
Wahitimu wakionesha mtindo wa mavazi.
Miundo mbinu ya chuo
Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani akiwaonyesha mazingira ya chuo wageni waalikwa pamoja na wazazi .

Mkuu wa chuo cha SHY NET Abubakar Rehani akiwaonesha mazingira ya chuo wageni waalikwa pamoja na wazazi .
Share:

BENKI YA CRDB YADHAMINI MKUTANO WA MABALOZI

 

 
Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax (kulia) akizungumza na baadhi ya mabalozi walipotembelea banda la Benki ya CRDB katika maonyesho yanayoenda sambamba na Mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mabalozi, unaofanyika kwenye hoteli ya Velde, Unguja Zanzibar. Kupitia mkutano huo wa kimkakati Benki ya CRDB imeendelea kusisitiza utayari wake katika kusaidia utekelezaji wa diplomasia ya kiuchumi na kuiwezesha Tanzania kunufaika na eneo huru la Biashara Afrika (AfCFTA). Benki ya CRDB ni mmoja wa wadhamini wa mkutano huo ulioanza Novemba 14 hadi 21, 2022.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Benki ya CRDB, Jacob Nangi (kushoto) akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Balozi Abdallah Possi, aliyetembelea banda la Benki ya CRDB katika maonyesho yanayoenda sambamba na Mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mabalozi, unaofanyika kwenye hoteli ya Velde, Unguja Zanzibar. Benki ya CRDB ni mmoja wa wadhamini wa mkutano huo ulioanza Novemba 14 hadi 21, 2022. Kulia ni Meneja Mwandamizi Uhusiano wa Biashara wa Benki ya CRDB, Lulu Melo.
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Congo, Balozi Said Mshana, akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Benki ya CRDB, Jacob Nangi wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika maonyesho yanayoenda sambamba na Mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mabalozi, unaofanyika kwenye hoteli ya Velde, Unguja Zanzibar. Benki ya CRDB ni mmoja wa wadhamini wa mkutano huo ulioanza Novemba 14 hadi 21, 2022. Kulia ni Meneja Mwandamizi Uhusiano wa Biashara wa Benki ya CRDB, Lulu Melo.

 
Share:

Thursday, 17 November 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 18,2022
















Share:

SERIKALI YADHAMILIA KUTEKELEZA KWA VITENDO MPANGO WA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kutekeleza kwa vitendo Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) ili kuvutia waweklezaji nchini.

Mhe. Kijaji ameyasema hayo tarehe 17 Novemba, 2022 alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Mhe. Manfredo Fanti aliyeambatana na ujumbe wake.

Mhe. Dkt. Kijaji amemshukuru Mhe. balozi Fanti kwa ushirikiano endelevu uliopo baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kuboresha Mazingira ya Biashara kupitia MKUMBI ambapo sheria na kanuni mbalimbali zimeboreshwa ama kufutwa ili kurahisisha ufanyaji Biashara Nchini Tanzania.

“Mazingira ya kufanya Biashara yameboreka zaidi kwani hivi karibuni tunaenda kuzindua mfumo wa dirisha moja la huduma kwa wawekezaji wa Ndani na Nje ya Nchi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo maombi ya leseni, vibali, hati na kurahisisha malipo ndani ya muda mfupi. Amesema Dkt. Kijaji.

Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Mhe. Manfredo Fanti amesema kuwa Mazingira ya Biashara Nchini Tanzania yamezidi kuboreka siku hadi siku na Nchi za Umoja wa Ulaya zimedhamiria kuja kuwekeza Tanzania katika sekta mbalimbali.

Mhe. Balozi Fanti ameongeza kuwa kutokana na Tanzania kuanzisha na kutekeleza MKUMBI, Mpango huo utaenda kuchapishwa katika tovuti ya Umoja wa Ulaya na kupitia Kongamano la Uwekezaji linaloenda kufanyika Mwezi Februari 2023 litawaunganisha wafanyabiashara wa Nchi za Umoja wa Ulaya na Tanzania na utapelekea kuongezeka kwa uwekezaji baina ya Nchi hizi mbili
Share:

YANGA YAJICHIMBIA KILELENI, YAICHAPA SINGIDA BIG STAR 4-1


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Yanga Sc wamerejea kileleni kwa kuiadhibu Singida Big Star kwa mabao 4-1 kwenye ligi kuu Tanzania Bara, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini dar es Salaam,

Stori kubwa kwenye mchezo huo ni Fiston Kalala Mayele ambaye amefunga mabao matatu, Hat trick baada ya kukaa muda mrefu bila kufakamia nyavu kwenye ligi kuu inayoendelea huku goli lingine likifungwa na Kibwana Shomari.

Singida Big Star bao lao pekee lilifungwa na Meddie Kagere ambaye nae amekaa muda mrefu bila kufunga huku kwenye ligi kifikisha mabao mawili tu na kwa upande wa Fisto Mayele akifikisha mabao sita ndani ya ligi msimu huu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger