Tuesday, 15 November 2022

ACCESS MICROFINANCE BANK WAANZISHA AKAUNTI YA "BARAKA JUNIOR" KWA AJILI YA WATOTO




Sijaona Saimon Afisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya Access Mcrofinance leo akikabidhi vifaa mbalimbali ikiwemo madaftari, kalamu na Lura kwa Hafsa Athman Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam, vifaa hivyo vimetolewa kwa shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 15 ya huduma zake nchini kutoka kulia ni Mariam Juma Mratibu wa Nyaraka Benkii ya Access na Mwalimu Venancia Kahwemama.


Sijaona Saimon Afisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya Access Mcrofinance leo akikabidhi vifaa mbalimbali ikiwemo madaftari, kalamu na Lura kwa Hafsa Athman Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam, vifaa hivyo vimetolewa kwa shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 15 ya huduma zake nchini kutoka kushoto ni Nicholaus Makunza Afisa Mikopo Benki ya Access.


Picha ikionesha wafanyakazi wa Benki ya Access wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Makumbusho mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo.


Nicholaus Makunza Afisa Mikopo Benki ya Access akigawa vifaa hivyo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho. jijini Dar es Salaam.


Mariam Juma Mratibu wa Nyaraka Access Bank na Hellen Lundalunda Afisa mauzo wakigawa vifaa mbalimbali wa wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho mara baada ya vifaa hivyo kukabidhiwa na benki ya Access.


Picha zikionesha wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam wakionesha vifaa mbalimbali kwa ajili ya kusomea mara baada ya kukabidhiwa na benki ya Access ya jijini Dar es Salaam leo.


Access Microfinance Bank imeanzisha akaunti mpya ambayo wameipa jina la "Baraka Junior Account" ambapo wazazi watakuwa wanawawekea watoto wao akiba kidogo kidogo huku wakieleza kwamba akaunti hiyo inakuwa haina makato wala gharama za mwezi za kuiendeshe.

Hayo yamesemwa na Sijaona Saimon Afisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya Access Mcrofinance Finance leo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari mara baada kutoa msaada wa vifaa mbali mbali katika shule ya msingi Makumbusho ikiwa ni mkakati wa benki hiyo kutoa shukurani kwa jamii ikielekea kufikisha miaka kumi na tano(15) ya kutoa huduma hapa nchini tangu ilipoanzishwa rasmi.

"Leo tumeamua kuja hapa makumbusho shule ya msingi kutoa vifaa vya shule ambapo tumetoa madaftari pisi elfu moja(1000) Rula elfu moja(1000) na kalamu elfu moja(1000) kwa ajili ya kushiriki baraka na kurudisha kwa jamii ambapo tumelenga upande huu wa Elimu mahsusi kwa sababu tunaamini kupitia hawa wanafunzi baadae tutapata wafanyakazi wa maeneo mbalimbali na viongozi wa nchi yetu pamoja na wafanyabiashara," amesema Sijaona Simon

Aidha Sijaona Saimon akizungumza kwa niaba ya benkihiyo amewashukuru Watanzania kwa kuendelea kuwaunga mkono kwa kuendelea kutumia huduma za benki hiyo hapa nchini jambo linalowafanyakuendelea kukua na kuongeza huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini.
Share:

Monday, 14 November 2022

SERIKALI YAJIDHATITI KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA EBOLA


SERIKALI imeendelea kujipanga kuhakikisha inadhibiti kuingia kwa maambukizi ya Virusi vya Ebola nchini kwa kuhakikisha inaanda mipango madhubuti katika maeneo ya uwanja wa ndege pamoja na maeneo ya mipaka ambapo wameweka wataalamu kwaajili ya kuhakikisha wanaoingia nchini wanafatiliwa kwa uangalizi.

Akizungumza leo Novemba 14,2022 Jijini Dar es Salaam Mratibu wa Ufuatiliaji na Udhibiti wa Magonjwa, Dkt.Vida Makundi wakati akifungua Mafunzo kwa Wahudumu ngazi ya jamii ambao kazi yao itakuwa kuwafuatilia wale ambao watakuwa wamekutana na wagonjwa wa Ebola na kutoa taarifa.

Amesema katika harakati za kujiandaa kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa Ebola, wanajiandaa pia katika zoezi la kufuatilia watu waliotangamana na mgonjwa wa Ebola endapo kwa bahati mbaya atakuwa amepatikana.

"Ufuatiliaji wa wasafiri ambao wametoka Uganda na sehemu nyingine ambao wanaweza wakawa wamekutana na wagonjwa tunawafuatilia kwa kuwahoji kila siku kama wanadalili zozote ambazo zinafanana na kuwa na dalili za Ebola". Amesema

Amesema kuwa inaaminika mgonjwa wa Ebola kama amekutana na mtu kati ya siku mbili mpaka siku 21 kama mtu amepatwa na maambukizi ndipo atakapoona dalili hivyo wanafundisha makundi mbalimbali ya wafuatiliaji.

Hata hivyo amesema Wahudumu ngazi ya jamii watakuwa wanatumika endapo ikahitajika kuwafuatilia wale ambao wamekuwa wamekutana na wagonjwa na watakuwa wanatoa taarifa kwa viongozi wao ambao ni Maafisa Afya ndani ya kata ambao watakuwa wanatoa taarifa kwenye halmashauri zao.

Aidha amesema wahudumu ngazi ya jamii pia watakuwa wakifuatilia tetesi za magonjwa ndani ya jamii, wakipata tetesi ya mgonjwa yeyote ambaye yanaonekana yanaambukiza, yanahatari ya kuambukiza wanatoa taarifa kituo chochote cha afya kilichopo karibu au kwa afisa afya ngazi ya kata na taarifa zinakwenda juu kwaajili ya uchunguzi.
Share:

TASAC YATOA ELIMU YA ULINZI,USALAMA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MOROGORO


AFISA Masoko Mwandamizi wa TASAC Martha Kelvin akimuonyesha mmoja wa watumiaji wa vyombo vya majini namna ya kuvaa jaketi la uokozi

Na Mwandishi Wetu,Morogoro


SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa elimu ya Usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira mkoani Morogoro pamoja na kuendesha zoezi la ukaguzi wa Vyombo vya usafiri majini.


Ukaguzi huo ni sehemu mikakati ya Shirika hilo kuhakikisha vyombo vya usafiri majini vinakuwa na ubora unaotakiwa kwa kuzingatia viwango.


Zoezi hilo liliendeshwa na Maafisa Ukaguzi na Udhibiti wa Vyombo vya Majini wa Shirika hilo, Bw. Gabriel Manase na Maulid Nsalamba katika wilaya ya Ifakara mkoani humo. Maafisa hao walitoa elimu ya usalama na ulinzi ikiwemo utunzaji wa mazingira wanapokuwa kwenye shughuli zao


Akizungumza wakati wa zoezi hilo Manase alisema elimu hiyo ina umuhimu mkubwa sana hivyo jamii inapaswa kuitambua na kuweza kuzuzungatia wakati wote wanapotekeleza shughuli zao za kila siku.


Zoezi hili lilianza tarehe 11 Novemba, 2022 ifakara katika maeneo ya Ngalimila, Ngapemba, Utengule, Chita na Mngeta na Mchombe na litaendelea katika mikoa ya iringa na Dodoma lengo ni kuhakikisha jamii inapata elimu.


Zoezi hilo liliendeshwa pia kwa ushirkiano na Afisa Masoko Mwandamizi wa TASAC Martha Kelvin na Afisa Uhusiano Mwandamizi Amina Miruko ambapo waliitaka jamii kuhakikisha inazingatia usalama kwenye vyombo vya maji ili kuweza kuepukana na ajali ambazo zinazaweza kuwakuta wawapo safarini.


Share:

MFUKO WA ELIMU WA TAIFA WATUMIA MILIONI 750 UJENZI WA SHULE YA MTAALA WA KIINGEREZA JIJINI DODOMA.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Prof. Maurice Mbago (mwenye Suti ya Bluu) akipata maelezo kuhusu ujenzi wa Shule ya Msingi Msangalale ya Mtaala wa Kiingereza ya jijini Dodoma inajayojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa TEA kwa thamani ya Sh. milioni 750. Jengo la vyumba vinane vya madarasa katika Shule ya Msingi Msangalale ya Mtaala wa Kiingereza ya jijini Dodoma inajayojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa TEA kwa thamani ya Sh. milioni 750.Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Prof. Maurice Mbago (mwenye Suti ya Bluu) akikagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Msangalale ya Mtaala wa Kiingereza ya jijini Dodoma inajayojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa TEA kwa thamani ya Sh. milioni 750.Jengo la utawala katika Shule ya Msingi Msangalale ya Mtaala wa Kiingereza ya jijini Dodoma inajayojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa TEA kwa thamani ya Sh. milioni 750.

Sehemu ya matundu 32 ya vyoo katika Shule ya Msingi Msangalale ya Mtaala wa Kiingereza ya jijini Dodoma inajayojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa TEA kwa thamani ya Sh. milioni 750.

**************************

Shule ya Msingi Msangalale ya mtaala wa Kiingereza inayojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) inatarajia kuanza rasmi mwezi Januari 2023.

Akitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Prof. Maurice Mbago aliyetembelea mradi huo unaojengwa katika Kata ya Makulu jijini Dodoma, Mkuu wa Divisheni ya Elimu Awali na Elimu Msingi wa jiji la Dodoama, Prisca Myalla amesema shule itaanza na wanafunzi 320 na itaendelea kuongeza wanafunzi hadi watakapofikia 640 idadi ambayo ni uwezo wa shule hiyo.

Bi Myalla ameongeza mradi huo utasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule zenye upungufu wa vyumba vya madarasa, kusogeza karibu na jamii huduma ya elimu na kupandisha ufaulu wa kitaaluma katika Halmashauri ya jiji la Dodoma.

Msanifu Majengo msimamizi wa Mradi huo, Emmanuel Mateo kutoka jiji la Dodoma amesema kwa sasa ujenzi huo unaohusisha jengo la utawala, vyumba vinane vya madarasa na matundu 32 ya vyoo umefikia asiimia 80 ambapo umepangwa kukamilika Novemba 30, 2022.

Mfuko wa Elimu wa Taifa umetoa ufadhili wa Sh. milioni 750 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo itakayotoa elimu kwa lugha ya kiingereza katika mwaka wa fedha wa 2021/ 2022 kwa lengo la kusaidia jitihada za Serikali za kutoa elimu bora.

Share:

MAMLAKA ZA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA ZATAKIWA KUTOA TAARIFA SAHIHI ZA HUDUMA ZA MAJI


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Watendaji kutoka Mamlaka za Maji wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato,(hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato (katikati) akifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.Kulia ni Mhandisi Adam Ishara kutoka Wizara ya Maji na kushoto Meneja Ufundi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA Mhandisi Titus Safari.


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Idara ya Maji na Usafi wa Mazingira mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mamlaka za maji na Miradi ya kitaifa mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma. ............................................

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato, amezitaka Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini kuhakikisha zinatoa taarifa sahihi za huduma ya maji na usafi wa mazingira kwa wananchi ili kushamirisha upatikanaji wa huduma endelevu kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Mhandisi Lumato ametoa maelekezo hayo leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22.

Mhandisi Lumato ameeleza kuwa tathmini iliyofanywa na EWURA imebaini kuwapo mamlaka za maji ambazo zimeendelea kuwasilisha taarifa zenye mapungufu kwenye kukidhi viwango vya huduma, uchakavu, ufanisi wa makusanyo wa maduhuli, muda wa upatikanaji wa huduma, ubora wa maji pamoja na idadi ya wananchi wanaopata huduma, hali hii inakwamisha kufanya tathmini ya hali halisi ya utendaji na upatikanaji huduma.

“Nitoe wito kwa mamlaka zote za maji kuhakikisha zinafanya masahihisho kwenye taarifa zenye mapungufu ili ziweze kutoa hali halisi ambayo mwisho wa siku itasaidia katika kupima utendaji na ufanisi wa huduma wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira” amefafanua Mhandisi Lumato

Kwa upande wake Mwakilishi wa katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Adam Ishara,amezitaka Mamlaka hizo kujitahidi kutekeleza wajibu wake kwa kutoa takwimu sahihi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa huku akisisitiza kuwa, Wizara ipo tayari kutoa miongozo na ushirikiano unaohitajika muda wowote.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira,ambaye ni Meneja Ufundi wa Maji na Usafi wa Mazingaira EWURA, Mhandisi Titus Safari,amesema kuwa mchakato wa maandalizi ya ripoti ya utendaji wa mamlaka za maji ni shirikishi hivyo kila mamlaka itumie kikao hicho kuthibitisha usahihi wa taarifa zake.

WATENDAJI kutoka Mamlaka 25 za Majisafi na Usafi wa Mazingira za miji mikuu ya mikoa na mamlaka 7 za miradi ya kitaifa wamehudhuria kikao kazi hicho kinachofanyika makao makuu ya EWURA jijini Dodoma.
Share:

AJALI YA BASI, LORI YAUA NA KUJERUHI DODOMA

 


Watu Sita wamefariki dunia na wengine 22 wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Arusha Express lenye usajili wa namba T 530 AGG kugongana uso kwa uso na lori Mchanga kampuni ya SINO-HYDRO lenye namba T 939 DZE.

Ajali hiyo imetokea leo Jumapili Novemba 13, 2022 mchana eneo la Veyula Kata ya Makutupora mkoani Dodoma.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema waliofariki wote ni wanaume huku Majeruhi 10 wakiwa ni Wanawake na 12 ni Wanaume.
Share:

Sunday, 13 November 2022

BENKI YA CRDB YATWAA TUZO MBILI CONSUMER CHOICE AWARDS


Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB, Pendason Philemon (watatu kulia) na Moureen Mollel, Meneja Mipango ya Biashara Benki ya CRDB (wapili kushuto) pamoja na viongozi wengine waandamizi wa benki hiyo katika picha ya pamoja wakionyesha tuzo ya Benki Bora katika kipengele cha Huduma kwa Wateja (Most Preferred Domestic Bank at Customer Service) na tuzo ya Huduma Bora za Kidijitali katika Sekta ya Benki (Most Advanced Digital Banking Services) Afrika Mashariki ambazo benki hiyo imetunukiwa katika hafla ya tuzo za Consumer Choice Awards zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jana Novemba 12, 2022. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Benki ya CRDB kushindo tuzo hizo zinazotokana na maoni ya wateja/ watumiaji wa huduma.
Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB, Pendason Philemon (kulia) akipokea tuzo ya Huduma Bora za Kidijitali katika Sekta ya Benki (Most Advanced Digital Banking Services) Afrika Mashariki kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara na Masoko Vodacom, Linda Riwa katika tuzo zako Consumer Choice Awards zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jana Novemba 12, 2022. Katika tuzo hizo Benki ya CRDB pia ilitunukiwa tuzo ya Benki Bora katika kipengele cha Huduma kwa Wateja (Most Preferred Domestic Bank at Customer Service).
Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB, Pendason Philemon (kulia) akipokea tuzo ya Benki Bora katika kipengele cha Huduma kwa Wateja (Most Preferred Domestic Bank at Customer Service) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kilombero Sugar, Guy Williams katika tuzo za Consumer Choice Awards zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jana Novemba 12, 2022. Katika tuzo hizo Benki ya CRDB pia ilitunukiwa tuzo ya Huduma Bora za Kidijitali katika Sekta ya Benki (Most Advanced Digital Banking Services) Afrika Mashariki.


===== ====== ======


Benki ya CRDB imeendelea kudhihirisha kuwa benki bora na kinara nchini kwa kutunikiwa tuzo mbili za umahiri katika sekta ya fedha nchini katika tuzo za Consumer Choice Awards zilizofanyika jana Novemba 12, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.


Tuzo ilizotunukiwa Benki ya CRDB ni ile ya tuzo za Huduma Bora za Kidijitali Afrika Mashariki, pamoja na Huduma Bora kwa Wateja. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Benki ya CRDB kushindo tuzo hizo zinazotokana na maoni ya wateja/ watumiaji wa huduma.


Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hizo, Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB aliwashukuru wa wateja, washirika, wadau wa benki hiyo, pamoja na Watanzania wote kwa kuendelea kuifanya Benki ya CRDB kuwa bora zaidi.


"Tunawashukuru sana kwa kuendelea kutufanya kuwa bora zaidi. Ahadi yetu ni kuendelea kuwa wabunifu katika huduma zetu ili kusaidia kuboresha maisha ya Watanzania," alisema Pendason.


Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Benki ya CRDB imefanya mageuzi makubwa ya kimkakati katika biashara yake ambayo yamepelekea kupata matokeo mazuri kiutendaji, ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa huduma, na ukuaji wa faida.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB amewashukuru wateja, wanahisa na wawekezaji wa Benki hiyo kwa kuifanya benki hiyo kuendelea kuwa bora zaidi.


Mwaka 2022 umekuwa wamafanikio makubwa kwa Benki ya CRDB hivi karibuni benki hiyo inetunukiwa tuzo mbili za ‘Benki Bora Tanzania kwa na majarida maarufu ya fedha na uchumi duniani ya Euromoney na Global Finance kutambua umahiri wake katika kuongeza ujumuishi wa kifedha katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuboresha maisha ya watu.


Pendason ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini akibainisha hiyo pia imekuwa chachu ya Benki ya CRDB kufanya vizuri.
Share:

MASELE ATIA FORA HARAMBEE, ACHANGISHA MILIONI 62 KUNUNUA BASI LA KWAYA YA AIC SHINYANGA, APEWA TUZO


Mhe. Stephen Masele akionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na uongozi wa kwaya kwa lengo la kutambua mchango wake na ushiriki wake katika harambee hiyo.

*****
Aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais Bunge la Afrika na Mbunge mstaafu wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele leo Jumapili Novemba 13,2022 katika Kanisa la AICT KAMBARAGE SHINYANGA ameongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ununuzi wa Basi ambapo amefanikiwa kuchangisha jumla ya shillingi 62,057,300/- (Sh. Milioni 62).


Akizungumza katika hafla hiyo Masele amewashukuru wananchi na waumini wa Kanisa la AICT Shinyanga kwa kuendelea kumkumbuka na kumshirikisha katika shughuli za kijamii hususani za kanisa huku akinukuu kitabu kitakatifu biblia Mithali 8: 17-21, amemshukuru Mungu kwa neema zake na kwa upendo mkubwa kwa taifa letu.


Mhe. Masele amewaomba waumini na wakristo kumuombea mhe Rais Samia Suluhu Hassan, “Tumuombee mama yetu na Rais wetu maisha marefu na afya njema azidi kutuongoza kwa hekima na busara, pia naomba waumini muendelee kuliombea taifa amani, utulivu na upendo".


Mhe. Stephen Masele ametunukiwa Tuzo ya upendo na Kanisa hilo na kumpongeza kwa uaminifu na upendo mkubwa kwa wana Shinyanga.


Akizungumza Mwenyekiti wa kwaya hiyo, Kambira Mtebe amemsifu Masele akisema ni kiongozi mnyenyekevu asiyekuwa na makuu, asiyependa majivuno. “Masele ni msikivu na mpole mwenye upendo sana, anawapenda sana watu”.


Naye Mlezi wa kwaya hiyo Abel Majige ambaye pia ni mmiliki wa Hotel ya Vigmark manispaa ya Shinyanga amemsifu Masele na kusema ni “kiongozi wa watu, Masele ni mtu wa watu” , amesema Majige.
Mhe. Stephen Masele akionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na uongozi wa kwaya kwa lengo la kutambua mchango wake na ushiriki wake katika harambee hiyo
Mh. Stephen Masele akiwashukuru viongozi wa kwaya na kanisa kwa kumualika.
Mhe. Stephen Masele akikata
Mchungaji Magembe akitoa neno la shukrani baada ya zoezi la harambee hiyo kukamilika.
Uongozi wa kanisa ukimkabidhi tuzo mhe. StephenMasele .
Uongozi wa kanisa kwa niaba ya kwaya ukionesha tuzo iliyoandaliwa.
Zoezi la kuhesabu pesa zilizopatikana likiendelea.
Mwenyekiti wa kwaya Kambira Mtebe akimpongeza Mh.Masele.
Mh. Masele akifatilia harambee.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger