Thursday, 2 June 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 2,2022

Share:

Wednesday, 1 June 2022

MADEREVA WAKATAA KULIPIA TOZO WANAPOTUMIA BARABARA YA JUU


Nairobi Expressway

Katibu Mkuu wa Uchukuzi nchini Kenya, Paul Mwangi Maringa, amesema kwamba madereva nchini humo wamekuwa wakikataa kulipia tozo mara wanapotumia barabara ya juu (Nairobi Expressway) kwa madai ya kwamba hawana pesa za kutosha na wengine wakidai hawana kabisa.


Madereva hao wamekuwa wakikataa kufanya malipo hasa wanapofika mahali pa kutokea, na kusema ipo haja kwa wizara kutoa elimu juu ya matumizi ya barabara hiyo kwa wananchi wake.

Katibu Mkuu Maringa amesema, kuna aina tatu za ulipaji wa ushuru huo, ikiwemo kwa njia ya fedha taslimu ama kwa njia ya mtandao na kwa kutumia kadi ya malipo.

Ujenzi wa barabara hiyo ya juu nchini Kenya ulianza mwaka 2019 na ilifunguliwa wiki mbili zilizopita kwa ajili ya majaribio.
Share:

WABUNGE WATOA SOMO KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUJIUNGA NA NSSF, WENYEWE WAHAMASIKA WACHANGAMKIA FURSA


Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Mbeya, Mhe. Suma Fyandomo, akizungumza katika semina ya wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) ambapo aliwasihi kujiunga na kujiwekea akiba na NSSF.

Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Mtwara, Mhe. Agnes Hokororo, akiwahimiza vijana kuelekeza fikra zao katika kujiajiri baada ya kuhitimu masomo kwa kuwa wamepata elimu ya kujiwekea akiba kutoka NSSF.
Mbunge wa Jimbo la Mwanga, Mhe. Joseph Tadayo akizungumza na wanafunzi wa Chuo IAA, ambapo aliwahimiza kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwa kujiunga na NSSF.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Festo Fute, akizungumza wakati wa semina ya wanachuo wa IAA.
Meneja wa NSSF wa Sekta Isiyo Rasmi, Rehema Chuma, akitoa elimu ya Hifadhi ya Jamii na kuweka akiba kupitia mpango wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi kwa wanachuo wa IAA.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Arusha, Josephat Komba, akizungumza wakati wa semina ya hifadhi ya jamii kwa wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).
Wanachuo cha Uhasibu Arusha (IAA) wakiendelea na zoezi la kujaza fomu kwa ajili ya kujiunga na NSSF baada ya kupata elimu ya hifadhi ya jamii.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Dkt. Mwaitete Cairo akizungumza wakati wa semina na wanafunzi wa Chuo hicho
Mwakilishi wa TAHLISO, Katibu wa Rais TAHLISO Louisa Liheta akizungumza wakati wa semina hiyo.
Wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) wakisikiliza kwa makini mada kuhusu umuhimu wa kujiwekea akiba iliyotolewa na NSSF pamoja na baadhi ya wabunge.

**


Baadhi ya wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Katiba na Sheria wamewahamasisha wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kujiunga na kujiwekea akiba na NSSF kupitia Mpango wa Kitaifa wa Sekta Isiyo Rasmi chini ya kampeni ya “Boom Vibes na NSSF” iliyotua katika Mkoa wa Arusha.


Kampeni hiyo ya “Boom Vibes na NSSF” inalenga kufikisha elimu ya hifadhi ya jamii pamoja na kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini na vyuo vya kati kuhusu umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba na NSSF kwa ajili ya kuandaa maisha bora ya sasa na baadaye.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti na wanachuo hao baadhi ya wabunge hao ambao ni Mhe. Suma Fyandomo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya. Mhe. Agness Hokororo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mtwara na Mhe. Joseph Tadayo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mwanga walisema kuna faida kubwa kwa wanafunzi wa elimu ya juu kujiunga na kujiwekea akiba NSSF kwamba itawasaidia katika kutafuta mitaji mbalimbali ya kibiashara.


“Niwasihi sana fedha mnayopata kila mwezi iwe ni kutoka kwenye mkopo au kwa wazazi, msiitumie yote kwenye matumizi yenu, mnaweza kuanza kuweka akiba kupitia NSSF na mkianza kuweka akiba sasa basi itakapofika muda wa kumaliza elimu yenu, akiba mliyoweka inaweza kuwasaidia katika maisha yenu ya baadaye na hamtajutia uamuzi wenu,” alisema Mhe. Suma Fyandomo.


Kauli yake hiyo iliungwa mkono na Mhe. Joseph Tadayo: “Nilijiunga na NSSF na kuanza kuchangia kabla sijawa mbunge, miaka hiyo ya nyuma ya umri wangu huduma nyingi zilikuwa bure na hata ajira pia zilikuwa tele lakini kwa sasa hali haiko hivyo mtu anakuwa nacho sio kwa kile anachoingiza bali kile anachoweka, tunahitaji kuwa na utamaduni wa kuweka akiba tena kutokana na kile ulichovuna kutokana na jasho lako.”

Lakini Mhe. Agnes Hokororo alisema: “Vijana mnapaswa kuelekeza fikra zenu katika kujiajiri baada ya kuhitimu elimu yenu, ninyi mmepata bahati ya kuelimishwa kujiwekea akiba chini ya kampeni ya Boom Vibes na NSSF, changamkieni fursa hii kwani hamtajutia uamuzi wenu.”


Kampeni hiyo ambayo ni mkakati wa Mfuko wa NSSF wa kutembelea taasisi mbalimbali za elimu ya juu na kati nchini, ili kuhamasisha wanachuo kujenga tabia ya kujiwekea akiba kwa kujiunga na kuchangia kila mwezi ili hatimaye wanufaike na mpango wenyewe.


Akizungumza na wanafunzi hao, Meneja wa Sekta Isiyo Rasmi, Rehema Chuma, alisema wanachuo ni wanufaika wakubwa wa mpango huo kutokana na kipato wanachokipata wanaweza kutenga ziada na kujiwekea akiba NSSF kwa manufaa ya sasa na baadaye.


Kuhusu namna ya kuchangia, Rehema alifafanua kuwa mwanachama wa NSSF anatakiwa kuhakikisha anachangia kiasi kisichopungua shilingi 20,000 kila mwezi au zaidi na kwamba anaweza kuchangia kidogokidogo kulingana na kipato chake ambapo hata akiwa na shilingi 1,000 kwa siku anaweza kujichangia.


Naye, Meneja wa NSSF Mkoa wa Arusha, Josephat Komba alisema lengo la Mfuko ni kuhakikisha inafikisha elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi wote waliopo katika sekta rasmi na sekta isiyo rasmi wakiwemo wanafunzi wa elimu ya juu ili waweze kujiunga na kujiwekea akiba.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 1,2022


Magazetini leo Jumatano June 1 2022






Share:

RAIS SAMIA AZINDUA KITABU CHA MSANII WA HIP HOP JOSEPH MBILINYI SUGU 'MUZIKI NA MAISHA' AMPA TUZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimpa Tuzo Msanii wa Muziki wa Hiphop nchini Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ya kuthamini mchango wake katika Sanaa na kuzalisha ajira kabla ya kuzindua kitabu cha msanii huyo chenye jina la Muziki na Maisha from the Street katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Mei 31,2022 Serena Hotel Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa Muziki wa Hiphop Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ mara baada ya kuwasili Serena kwa ajili ya kuhudhuria tamasha la maadhimisho ya miaka 30 ya msanii huyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitabu cha Msanii Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ chenye jina la Muziki na Maisha from the Street katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Sasha Joseph Mbilinyi mtoto wa Msanii wa Hiphop Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan leo Mei 31, 2022 amezindua kitabu cha mwanamuziki nguli wa Hip Hop, Mr 2 Proud au maarufu kama Sugu kiitwacho muziki na maisha kwenye tamasha la kutimiza miaka 30 katika tasnia hiyo.


Katika tamasha hilo lililoitwa The dream concert, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu, watendaji wa Wizara na wadau mbalimbali wamehudhuria.


Tamasha hili limepambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sugu mwenyewe ambaye ametumbuiza na kukonga nyoyo za mamia ya watu waliohudhuria.




Mhe. Rais amemtunukia tuzo, Sugu huku akimpongeza kuwa miongoni wasanii wenye nyimbo zenye maadili.
Share:

KWANINI NI VIGUMU KWA WANAWAKE WASOMI KUOLEWA?

Share:

Tuesday, 31 May 2022

VIJANA 200 WAPATIWA MAFUNZO YA KILIMO KIDIJITALI


Wadau mbalimbali wa Westerwelle Startup Haus Arusha wakijadili jambo wiki iliyopita kwenye uzinduzi wa kituo hicho Jijini Arusha, (picha na Queen Lema).

Na Queen Lema, Arusha.

Westerwelle Foundation kutoka Ujerumani imeungana na Obuntu Hub kutoka Tanzania kufungua kituo kipya kwa ajili ya kuwainua vijana wajasiriamali (Innovation Hub).


Mbali na kufungua kituo hicho Jijini Arusha, pia mpaka sasa vijana zaidi ya 200 wameshanufaika na mafunzo kwenye kituo hicho.


Akiongea mwishoni mwa wiki na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kituo hicho, Meneja mkuu wa Westerwelle Startup Haus Arusha Bw. Collins Kimaro amesema kuwa uwepo wa kituo hicho ni msaada mkubwa sana kwa vijana


Kimaro amesema kuwa vijana hao 200 walipatiwa ujuzi wa kidigitali kutoka katika sekta ya kilimo.


Kimaro amesema kuwa vijana hao kutoka Arusha na Iringa walipewa ujuzi wa kidigitali.


"Ni fursa kubwa sasa kwa vijana kunufaika na kituo hiki maana hata hao vijana 200 ambao tumewafikia toka mwezi Juni tayari matokeo yameshaonekana kwaiyo tuseme kuwa kila kijana mjasiriamali sasa atumie kituo hiki" ameongeza


Akiongea kituo hicho amesema kuwa ni muungano wa Obuntu Hub na Westerwelle Foundation,ambapo sasa kwa umoja huo wamefungua Westerwelle Startup Haus Arusha(WSHA) ambapo kituo hicho kitatoa nafasi za kisasa za kufanyia kazi yaani co working space,


Ameongeza kuwa programu ya mafunzo mbalimbali na kuwakutanisha wajasiriamali wa kitanzania na mtandao kimataifa.


Kimaro amebainisha kuwa anawashukuru wafadhili mbalimbali ambao wamejitolea kuwasaidia vijana ambapo mpaka sasa matunda yameshaonekana


Akahitimisha kwa kusema kuwa kwa sasa vijana wanakabiliwa na changamoto Kama vile ukosefu wa mitaji,na masoko lakini sasa wanatakiwa kujiunga na kituo hicho,lakini pia wanatakiwa kuchangamkia fursa pamoja na mashindano ya kimataifa ambayo yanatangazwa.


Naye mkurugenzi wa Westerwelle foundation Bw Oliver Reisner amesema kuwa wamefurahi sana kufika Tanzania na wameona muamko wa vijana na wataungana na jitiada za Serikali ya Tanzania kuchochea maendeleo kupitia ubunifu na ujasiriamali.


George Akilimali ni mmoja wa wanufaika, amesema kuwa umoja huo umekuwa msaada kwa vijana wengi sana hapa nchini ambapo kwa yeye aliweza kupata msaada mbalimbali ikiwemo elimu,na mtaji


Amedai kuwa hapo awali hakuwa na uwezo wa kupata masoko ya kimataifa ila kwa sasa amekutanishwa na wadau wa kimataifa hivyo vijana wanatakiwa kutumia kituo hicho.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger