Monday, 11 April 2022

ASKOFU SANGU AKEMEA NGO's ZINAZOTUMIA SHIDA NA MAHANGAIKO YA WATU KUPIGA 'MICHONGO'


Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akiwa katika Picha ya pamoja na Bw. Richard John anayetarajia kufunga ndoa hivi karibuni mara baada ya Misa ya Dominika ya Matawi iliyofanyika katika kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo.
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akizungumza katika Misa ya Dominika ya Matawi katika kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo.
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akiwa katika ibada fupi ya kubariki matawi katika uwanja wa shule ya msingi Bugoyi(A)kushoto ni katibu wake Pd.Deusdedith Kisumo.
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akibariki matawi ya waamini kupitia ibada maalum iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Bugoyi (A)
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akibariki matawi ya waamini kupitia ibada maalum iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Bugoyi (A)
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akitoa baraka za mwisho kwa waamini mara baada ya Misa ya Dominika ya Matawi katika kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo.

************

Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu ameendelea kukemea tabia ya baadhi ya watu kutumia shida na matatizo ya wengine kama fursa ya kujinufaisha badala ya kuwasaidia.

Akizungumza kupitia Misa ya Dominika ya Matawi ambayo imefanyika leo Jumapili April 10, 2022 katika kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga,askofu Sangu amewataka wanaofanya vitendo hivyo kuacha kuwaongezea maumivu watu walioko katika mahangaiko ya namna mbalimbali na badala yake waongozwe na moyo wa utu, huruma na upendo na kuwasaidia kadri ya mahitaji yao .

"Na kamwe tusitumie shida na mahangaiko ya wengine kwa lengo la kujinufaisha,mfano zipo NGO’S nyingi sana ndani ya nchi yetu lakini ukiangalia kwa undani kabisa si kwa ajili ya watu wenye mateso na wenye mahangaiko na badala yake kinachowafikia walengwa ni asilimia ndogo ya raslimali zinazotolewa na wahisani,kiasi kikubwa kinatumika kwa ajili ya watu kujinufaisha kupitia shida zao”,amesema.

Askofu Sangu pia ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza Wakristo wote kuepuka dhuluma na kutokuwa chimbuko la mateso kwa wengine na badala yake wahakikishe wanakuwa chimbuko la matumaini na faraja kwa watu wenye shida.

Leo,Kanisa Katoliki kote ulimwenguni linaadhimisha Dominika ya Matawi ambayo ni kumbukumbu ya kupokelewa kwa Shangwe kwa Yesu Kristo mjini Yelusalemu,tukio lililofanyika siku chache kabla ya kukamatwa kwake,kuteswa na kufa msalabani na baadaye kufufuka siku ya tatu.
Share:

Sunday, 10 April 2022

AL BARAKAH YA BENKI YA CRDB YAWAGUSA RC NA SHEIKH MKUU TANGA


Mkuu wa Idara ya Hazina ya Benki ya CRDB, Bw. Alex Ngusaru akizungumza na wateja na wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tanga wakati wa futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Wateja na wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tanga wakishiriki futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Hashim Mgandilwa akizungumza na wateja na wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tanga wakati wa futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Hashim Mgandilwa akishiriki futari na wateja na wadau wa Benki ya CRDB wa Mkoa wa Tanga.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Sheikh Juma Luwuchu akizungumza na wateja na wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tanga wakati wa futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Wateja na wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tanga waliojitokeza kushiriki futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Hashim Mgandilwa akiwa na Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Benki ya CRDB, Bi. Chiku Issa (wa pili kushoto) wakikabidhi vyakula kwa kituo cha wenye uhitaji cha Imani Chumbageni ikiwa ni sehemu ya mchango wa Benki ya CRDB kwa kituo hicho katika mfungo wa mwezi Ramadhani.
Wateja na wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tanga waliojitokeza kushiriki futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Wateja na wadau wa Benki ya CRDB Mkoa wa Tanga waliojitokeza kushiriki futari ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
Wafanyakazi wanawake wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushiriki futari na wateja na wadau wa benki wa Mkoa wa Tanga.


Tanga 9 Aprili 2022 – Huduma ya Al Barakah ya Benki ya CRDB inayozingatia misingi ya kutotoza au kupokea riba imewafurahisha wananchi, wadu na viongozi wa mkoa wa Tanga.

 Hilo limebainika katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wateja, wadau na wenye uhitaji katika Mkoa wa Tanga ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Benki hiyo kufuturisha kipindi cha mfungo wa Ramadhani. 

Hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Hashim Mgandilwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Sheikh Juma Luwuchu.

 Akizungumza katika futari hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Hazina na Masoko ya Mitaji wa Benki ya CRDB, Bw. Alex Ngusaru alisema kuwa Benki ya CRDB imeendelea kusikiliza maoni ya wateja na kuendelea kuleta sokoni bidhaa na huduma bunifu zinazoendana na mahitaji ya soko.

 “Uanzishwaji wa huduma ya Al Barakah unadhihirisha ni kwa kiasi gani ambavyo Benki yetu inaishi kauli mbiu yake ya “Benki Inayomsikiliza Mteja” kwani kupitia kusikiliza maoni ya wateja wetu ndipo tulipoweza kuja na huduma hii makhususi kwa ajili ya wenzetu ambao wanaamini katika misingi ya kutopokea wala kutozwa riba”, alisema Ngusaru. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Hashim Mgandilwa ambae alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika hafla hiyo aliipongeza na kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuandaa futari hiyo kwa wakazi wa Tanga pamoja na kuandaa vyakula kwa ajili ya wenye uhitaji ili kuwasaidia katika kipindi cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

 Mkuu wa Wilaya aliongeza kuwa ujio wa huduma ya Al Barakah utakua chachu ya kuongeza wigo kwa kufikisha huduma za fedha kwa Watanzania kwani wapo ambao walikua hawawezi kutumia huduma za benki kwa kuwa tu haziendani na misingi ya imani yao.

 “Nawapongeza sana Benki ya CRDB kwa hili la futari na kugusa wenye uhitaji lakini zaidi niwapongeze kwa kuja na huduma hii makhusi ya Al Barakah ambayo inaendana na imani ya wenzetu wasioamini katika kutozwa au kupokea riba” alisema Mh. Mgandilwa. 

Kwa upande wake Sheikhe wa mkoa wa Tanga Juma Luwuchu ambae aliambatana na masheikh wengine wa Mkoa alitoa shukrani na pongezi kwa Benki ya CRDB kwa kuipa heshima Tanga kwa kuamua kuifanya kuwa moja kati ya mikoa ambayo benki itaandaa futari kwa mwaka huu lakini zaidi akifurahishwa na huduma ya Al Barakah inayofata misingi ya Sharia. 

Sambamba na hilo Sheikh Luwuchu aliwaasa Waislamu pamoja na taasisi nyingine kuiga mfano wa Benki ya CRDB cha kukumbuka wenye uhitaji katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan huku akiwataka Waislamu kuhakikisha wanadumisha yale mema na mazuri yaliyoelekezwa katika Quran tukufu.

 “Benki ya CRDB wametuonyesha mfano mzuri kwa kuwakumbuka wateja na wadau wao lakini hawakuishia hapo wamekumbuka pia watoto wetu wenye uhitaji kutoka kituo cha Imani Chumbageni,” alisema Sheikh Luwuchu.

 Kituo cha Imani Chumbageni ambao pamoja na kualikwa katika futari hiyo pia walikabidhiwa vyakula mbalimbali ikiwemo ngano, sukari, tambi, tende na mafuta ya kupikia ili kuwasaidia kupata futari kipindi cha mfungo wa mwezi Ramadhani.
Share:

Picha : MAPOKEZI YA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM KINANA JIJINI DAR ES SALAAM

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakishangilia katika hafla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg. Abdulrahman Omar Kinana Mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee .
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg. Abdulrahman Omar Kinana akisalimiana na wazee wa CCM katika hafla ya kumkaribisha Makamu mwenyekiti huyo leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini wa Dar Es Salaam muda huu
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg. Abdulrahman Omar Kinana akifurahi jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe.Daniel Chongolo katika hafla ya kumkaribisha Makamu mwenyekiti huyo leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini wa Dar es Salaam muda huu

Share:

MWENYEKITI MPYA WA BODI YA BANK OF AFRICA ATEMBELEA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA BENKI


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bank of Africa Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikaribishwa na Mkurugenzi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Adam Mihayo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo juzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bank of Africa Bw.Nehemia Kyando Mchechu akiongea na viongozi wa benki hiyo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es alaam juzi,(wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Adam Mihayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bank of Africa Bw.Nehemia Kyando Mchechu (Kushoto) akipokea nyaraka za kazi kutoka kwa Mkurugenzi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Adam Mihayo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es alaam juzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bank of Africa Bw.Nehemia Kyando Mchechu akibadilishana mawazo na Mkurugenzi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Adam Mihayo, wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es alaam juzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bank of Africa Bw.Nehemia Kyando Mchechu (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa benki wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es alaam juzi.
Share:

DKT. BITEKO ATATUA MGOGORO WA WACHIMBAJI WADOGO CHAMWINO


Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko

Na. Tito Mselem, Dodoma

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ametatua mgogoro wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika kijiji cha Nayu Kata ya Dabalo wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma.

Mgogoro huo ulio dumu kwa zaidi ya mwaka mmoja ulitokea baada ya wachimbaji wadogo kugundua madini ya dhahabu katika Mlima wa Nayu uliopo ndani ya Hifadhi za Misitu ambapo Mwekezaji Sarehe Mohamed alitangulia kukata leseni ya uchimbaji mdogo wa madini katika eneo hilo kabla ya wagunduzi.

Inaelezwa kuwa, kijiji cha Nayu kina jumla ya leseni 16 ambazo Mwekezaji ana leseni 8 na wanakijiji wana leseni 8 ambazo zinamilikiwa kihalali kwa kufuata Sheria na Taratibu zilizowekwa na Serikali.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo wa madini, Dkt. Biteko amesema Wizara ya Madini inatoa leseni za uchimbaji madini katika maeneo mbalimbali, pale inapotokea leseni ipo ndani ya Hifadhi za Misitu ni lazima mmliki apate Kibali kutoka Mamlaka ya Uhifadhi wa Misitu Tanzania (TSF).

“Sisi Wizara ya Madini tunatoa leseni kwenye maeneo yenye madini lakini ukitaka kuchimba kwenye Hifadhi za Misitu lazima upate Kibali kutoka TSF ili uchimbe kwa utaratibu ambapo Wataalam wa Misitu watakagua eneo na watakupa Kibali cha Tathimini ya Athari za Mazingira ili kuhakikisha mazingira yanabaki salama,” amesema Dkt. Biteko.

Aidha, Dkt. Biteko amemtaka Mwekezaji wa madini ya dhahabu katika kijiji hicho Sarehe Mohamed kujenga mahusiano mazuri na wanakijiji aliowakuta katika eneo hilo ili afanye kazi kwa ushirikiano.

Dkt. Biteko amesema, Rais wa Nchi hii Mhe. Samia Suluhu Hassan anataka kuona wachimbaji wadogo wa madini wananufaika na rasilimali zilizopo nchini, anataka kuwaona wachimbaji wadogo wanatoka kwenye uchimbaji mdogo kwenda wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa.

“Mwenyezi Mungu amewapa bahati ya kuwa na madini katika eneo lenu, niwaombe mchimbe madini haya kwa kupendana na kushirikiana, madini yawaunganishe acheni mambo ya kufitianiana na kuleteana majungu chimbeni kwa ushirikiano,” amesisitiza Dkt. Biteko.

Sambamba na hayo, Dkt. Biteko amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya pamoja na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma Chagwa Marwa kufungua Soko la Madini katika kijiji cha Nayu ili kuwarahisishia wachimbaji wadogo mahali pa kuuzia madini yao na kusaidia kijiji kupata tozo kutoka kwenye madini yaliyopo kwene eneo lao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya amesema migogoro mingi inayotokea katika eneo hilo inasababishwa na ukosefu wa elimu kwa wachimbaji wadogo, ambapo mara nyingi wakigundua madini wanaanza kuyachimba bila kufuata Sheria na Taratibu ikiwemo kukata leseni.

Naye, Mbunge wa Chamwino ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Deogratius Ndejembi amempongeza Waziri wa Madini kwa kukubali kuongozana naye ili kutatua mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu.

Madini ya dhahabu katika kijiji cha Nayu yaligunduwa na wachimbaji wadogo ndani ya Hifadhi ya Misitu Mwaka 2020 hali iyopelekea wananchi zaidi ya mia saba kuingia katika eneo hilo kutafuta madini.
Share:

MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI SISTER OSINACHI AFARIKI DUNIA


Sista Osinachi alitamba na nyimbo ya Okwueme akishirikishwa na Mchungaji Prospa Ochimana
Sista Osinachi akiimba nyimbo za Dini wakati wa uhai wake

MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za Injili kutoka nchini Nigeria, Sister Osinachi Nwachukwu maarufu kupitia wimbo wake wa “Ekwueme” amefariki dunia katika Hospitali moja iliyoko Abuja nchini humo.

Taarifa kutoka vyombo vya habari nchini Nigeria zinasema Osinachi alifariki dunia jioni ya jana Ijumaa (April 8, 2022) baada ya kupambana na maradhi ambayo hayajawekwa wazi kwa takriban miezi miwili huku vyanzo vingine ambavyo havijathibitisha vikidai ni kansa ya koo.

Kifo cha Osinachi kinakuja ikiwa ni wiki mbili tu tangu kifo cha mwimbaji mwenzake Chinedu Nwadike.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 39 alidaiwa kuwa anaendelea vizuri kutokana na maradhi ya figo na alikuwa amepangiwa kusafirishwa kwenda nchini India kwa matibabu zaidi ambapo kifo chake kilimkuta Machi 27, 2022 kabla hajaondoka kwenda India kutibiwa.

Baadhi yake nyimbo za Osinachi pamoja na “Nara Ekele” akiwa na Mchungaji Paul Enenche (Dunamis, Abuja), “Ekwueme” akiwa na Prospa Ochimana na nyinginezo nyingi zinazopendwa na kusikiliza/kutazamwa na mamilioni ya watu duniani kote.


Wimbo wa Ekwueme umejipatia umaarufu sana kutokana maudhui yake huku ukitasambaa na kuimbwa na jamii kubwa duniani.


Osinachi ameacha mume na watoto wanne.
Share:

WAZIRI MABULA AONYA WANAOTUMIA HISANI YA RAIS KUVAMIA MAENEO YA HIFADHI


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao na viongozi wa mkoa wa Mara kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 wakati timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta ilipotembelea mkoa huo tarehe 9 April 2022.

Sehemu ya washiriki wa kikao cha viongozi wa mkoa wa Mara na timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati timu ya mawaziri hao ilipotembelea mkoa huo kupeleka mrejesho wa utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 9 April 2022.

Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akizungumza katika kikao na viongozi wa mkoa wa Mara kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 wakati timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta ilipotembelea mkoa huo tarehe 9 April 2022.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Khamis Chillo akisisitiza jambo wakati wa kikao na viongozi wa mkoa wa Mara kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 pale timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta ilipotembelea mkoa huo tarehe 9 April 2022.

Naibu Waziri wa Malisili na Utalii Mary Masanja akizungumza katika kikao na viongozi wa mkoa wa Mara kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 wakati timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta ilipotembelea mkoa huo tarehe 9 April 2022.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Mara kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 9 April 2022.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Mara kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 9 April 2022.

********************************

Na Munir Shemweta, WANMM MUSOMA

Waziri wa ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametoa onyo kwa wananchi wanaotumia hisani ya Rais Samia Suluhu Hassan kuvamia maeneo ya hifadhi yaliyomegwa na kurejeshwa kwa wananchi kutokana na kuwa na migogoro ya matumizi ya ardhi.

"Na nitoe tahadhari kumekuwa na tabia leo serikali inakumegea halafu kesho unategemea tena utamegewa, hapatakuwa na kubadilisha mipaka au kumega tena maeneo yaliyotolewa, kilichofanyika ni hisani ya mhe Rais Samia kuweza kuridhia lifafanyike jambo hilo lakini siyo ada kila watu wakihitaji wanamegewa" alisema Dkt Mabula.

Timu ya Mawaziri wa Wizara za kisekta ikiongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi iko katika awamu ya pili ya ziara kwenye mikoa mbalimbali nchini kupeleka mrejesho wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi kwenye vijiji 975.

Alisema, kinachohitajika kwa maeneo yote yaliyomegwa kwa ajili ya shughuli za wananchi ni kuandaliwa mpango wa matumizi mazuri na jukumu la mikoa ni kuhakikisha mipango ya matumizi bora ya ardhi inaandaliwa kwa maeneo yote yaliyomegwa.

Akizungumza na uongozi wa mkoa wa Mara tarehe 9 April 2022 wilyani Musoma Dkt Mabula ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta alisema, mkoa wa Mara pekee ulikuwa na vijiji 19 na mtaa mmoja vyenye migogoro ya matumizi ya ardhi na kubainisha kuwa vijiji 19 katika mkoa huo vitaendelea kubaki na kufanyiwa marejeo huku mtaa mmoja ukifanyiwa tathmini.

Sehemu kubwa ya migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 ni uvamizi wa maeneo ya hifadhi, mashamba, ranchi, vyombo vya usalama, mapori ya akiba na vyanzo vya maji ambapo uvamizi huo umeleta changamoto kubwa inayofanyiwa kazi na Mawaziri wa Wizara za Kisekta.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, kazi inayofanyika katika kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi ni pamoja na kubadilisha maeneo ya hifadhi yaliyopoteza sifa, kurekebisha mipaka kati ya hifadhi za misitu, wananchi na wanyama ambako kuna muingiliano ili kuweka alama zitakazoonekana ambazo kila mmoja ataheshimu.

Kwa upande wao, Mawaziri wa Wizara za kisekta walisisitiza umuhimu wa uongozi wa mkoa kuanzia ngazi za chini hadi juu kuhakikisha unasimamia vyema sheria ili maeneo ya hifadhi yasivamiwe tena sambamba na kutilia mkazo uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji sambamba na kuwepo mipango ya matumizi bora ya ardhi.

‘’ Elimu ya utunzaji vyanzo vya maji itolewe kwa wananchi kwa kuwa wananchi wamekuwa wakifanya shughuli kwenye vyanzo maji na hivyo kuathiri vyanzo hivyo na wakati mwingine kuvikausha hasa nyakati za kiangazi’’ alisema Mhandisi Marypricsa Mahundi.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Khamis Chillo alitaka wananchi kupewa taaluma ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira ili kuepuka uharibifu wa mazingira.

‘’Wananchi waelimishwa namna bora na sahihi ya matumizi ya ardhi kwa kuwa kuna shughuli nyingi za kibinadamu zinazofanywa katika ardhi na inawezekana zinafanyika kutokana na watu kutofahamu matumizi sahihi ya ardhi lengo letu ni kupunguza migogoro ya ardhi’’ alisema Chillo.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde alisema, utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi utasababisha baadhi ya maeneo kutengwa kuwekewa mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kusaidia kupunguza changamoto za ardhi.

Mary Masanja aliwaambia viongozi wa mkoa na wilaya wa mkoa wa Mara kuwa, maeneo yanayomegwa kwa ajili ya wananchi yalikuwa sehemu ya maeneo yaliyohifadhiwa na kusema kuwa, wananchi wajiandae kukutana na changamoto za wanyama na kuwataka viongozi kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuishi maeneo hayo.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 10,2022



















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger