Tuesday, 15 February 2022

UCSAF YAKUTANA NA WADAU WA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA...MKUU WA TCRA ATAKA WAPENDANE

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumanne Faberuari 15,2022 katika Ukumbi wa BoT Jijini Mwanza
*****

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) umekutana na Wadau wenye Leseni za huduma za mawasiliano Kanda ya Ziwa kwa lengo la kutoa elimu inayohusu majukumu ya UCSAF pamoja na haki na wajibu wa watoa huduma za maudhui kwa njia ya Televisheni, Redio, Mitandao ya Kijamii na wasambaji wa maudhui kwa njia ya waya (CATV).

Akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumanne Februari 15,2022 Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) amewataka watoa huduma za mawasiliano kupendana na kuacha ubinafsi.

“Mkiacha huu wivu usio na manufaa kwenye hizi Redio zenu mtafika mbali, Mpendane kama kuna shida njoo TCRA tuzungumze,tumieni mnara mmoja ili kupunguza gharama za uendeshaji. Acheni kuchongeana…Hivi Redio ya mwenzako ikizimwa wewe utafaidika nini?”,amesema Mhandisi Mihayo.

Aidha amehamasisha watoa huduma za mawasiliano kwa njia ya redio kuongeza usikivu akibainisha kuwa nafasi za kuongeza usikivu wa Redio kwenye maeneo mbalimbali zipo na TCRA inaendelea kuzitoa.

“TCRA inataka kuwe na Redio kila mahali kwa sababu usikivu wa redio upo chini ya asilimia 50. Nafasi za kuongeza usikivu bado zipo, njooni TCRA tuwapatie lakini pia napenda kuwataarifu kuwa ukianzisha Redio Tozo zimepungua kwani serikali inataka kila mahali kuwe na redio. Nami nataka kuona Kanda ya Ziwa inaongoza kuwa na watoa huduma wengi wa mawasiliano”,amesema Mhandisi Mihayo.

Mwanasheria wa UCSAF, Fredy Kandonga amesema UCSAF inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ukiwemo wa Mawasiliano ya simu ili kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo yasiyo na huduma hiyo na yenye mawasiliano hafifu, kuboresha usikivu wa redio ya Taifa na Redio za Kijamii, Uanzishwaji wa kituo cha miito ya dharura, Tiba Mtandao, Kuunganisha shule kwenye Intaneti na Mafunzo ya TEHAMA kwa walimu.

Amesema wajibu wa mfuko huo ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa uunganishwaji wa kila mtu kwenye mitandao ya mawasiliano ya umma kupitia huduma za mawasiliano ,kuhakikisha huduma za posta na matangazo zinapatikana maeneo ya vijijini na mijini yenye huduma za mawasiliano hafifu na kubainisha na kuainisha maeneo yanayohitaji huduma za mawasiliano kwa wote.

Ameongeza kuwa Wajibu wa watoa huduma ni kushiriki katika upelekaji wa huduma za mawasiliano kwenye maeneo ya vijijini na mijini yasiyo na huduma au yenye huduma hafifu pamoja na kutoa tozo ya huduma kwa wote kila robo mwaka.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumanne Faberuari 15,2022 katika Ukumbi wa BoT Jijini Mwanza. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumanne Faberuari 15,2022 katika Ukumbi wa BoT Jijini Mwanza
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumanne Faberuari 15,2022 katika Ukumbi wa BoT Jijini Mwanza
Mwanasheria wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Fredy Kandonga akizungumza wakati wa Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumanne Faberuari 15,2022 katika Ukumbi wa BoT Jijini Mwanza

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) akisisitza jambo kwenye Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa. Kushoto ni Mwanasheria wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Fredy Kandonga .
Mwanasheria wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Fredy Kandonga akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa. Kulia ni Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) leo Jumanne Faberuari 15,2022 katika Ukumbi wa BoT Jijini Mwanza
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) leo Jumanne Faberuari 15,2022 katika Ukumbi wa BoT Jijini Mwanza
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF)

Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakipiga picha ya kumbukumbu
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakipiga picha ya kumbukumbu

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

NAIBU WAZIRI PINDA AHIMIZA WAMILIKI WA VIWANDA KATAVI KUKATA BIMA KWA AJILI YA KULINDA BIASHARA ZAO

Naibu Waziri Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe. Geofrey Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla alipotembelea viwanda vya kuchakata mazao katika vilivyopo katika kata ya Maji Moto Mkoani Katavi.

Naibu Waziri Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe. Geofrey Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla wakionyesha mchele unaozalishwa na moja ya kiwanda Kinachopatika katika eneo la Maji Moto Mkoani Katavi.

Naibu Waziri Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kavuu Mkoani Katavi Mhe. Geofrey Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni cha Wageni mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha Flamingo Foods Company Limited kujionea ukarabati mkubwa uliofanyika katika kiwanda hicho baada ya maghala ya kuhifandhia mchele kuezuliwa na upepo mkali uliotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Katavi.

Naibu Waziri Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe. Geofrey Mizengo Pinda (kushoto)akiangalia namna mtanbo wa kukamlia mafuta ya alizeti unavyofanya kazi. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla.

..............................................................

Na. Dennis Buyekwa- Katavi.

Wafanya biashara Mkoani Katavi wametakiwa kukata bima kwa ajili ya kulinda biashara zao wakati wanapokabiliwa na majanga mbalimbali yanayotokana na moto, mafuriko pamoja na upepo hatua itakayosaidia kuepuka gharama pale watakapohitaji kuendelea na uzalishaji baada ya majanga hayo kutokea.

Hayo yamezungumzwa mapema leo na Naibu Waziri, Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Geofrey Mizengo Pinda alipowatembelea wafanyabiasha wanaomiliki viwanda vya kuchakata Mchele, Karanga na alizeti ili kijionea ukarabati wa majengo ya kuhifadhia bidhaa yaliyoezuliwa na upepo mkali uliotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika eneo la Maji moto lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi.

Akiwaelezea faida watakazo pata wafanyabiashara hao kwa kukatia bima biashara zao Mhe. Pinda amesema kuwa faida kubwa watakayoipata wafanya biashara hao ni kutosimamisha huduma zao kwa muda mrefu kwa kuwa pindi majanga yatakapotokea kampuni husika zitawalipa fidia na hivyo kuwafanya waendelee kuwahudumia wananchi wao bila kikwazo chochote.

Mhe. Pinda ameendelea kueleza kuwa iwapo wamiliki wa viwanda hivyo watafanikiwa kukata bima kwa ajili ya miradi hiyo itawasaidia kuendesha shughuli zao pasipo na shida yoyote hatua itakayoisaidia Serikali pia kuendelea kupata mapato wakati wote kwa sababu sasa watakuwa na uhakika na huduma wanazotoa kwa wananchi na hivyo kuendelea kuchangia ukuaji wa pato la Taifa.

“nawahimiza kukata bima, kwa sababu ukiwa na bima kwenye mradi wako unakuwa hauna cha kuhofia wakati wa kuendesha shughuli zako hata likitokea la kutokea kampuni za bima zitakulipa ndani ya muda mfupi, hatua itakayosaidia kuendelea na uzalishaji bila wasiwasi. Alisema Mhe. Pinda.

Ameongeza kuwa bima hizo pia zitawasaidia wafanya biashara kuwa na soko la uhakika kwa kuwa sasa wateja wao watakuwa na uhakikika wa kupata huduma zao kwa ufasaha kwa kuwa sasa wafanyabiashara hao watawezakuongeza uzalishaji wa bidhaa na ajira kwa ujumla nchini kwa vile hata majanga yakitokea uzalishaji hautasimama kwa muda mrefu.

Aidha, Mhe. Pinda ametoa wito kwa wamiliki wa bidhaa hizo kuhakikisha wanapata vifungashio vya kisasa kwa ajili ya kufungasha bidhaa zao kwani kwa kufanya hivi itawasaidia kuongeza thamani ya bidhaa zao, kuongeza wigo wa kuamiwa na wateja kujitangaza wao wenyewe pamoja na mkoa wa Katavi kwa ujumla.

“tunataka ulimwengu ujue Maji Moto kuna mchele, karanga na alizeti ili kila atakayetumia bidhaa mnazozalisha ajue kuwa bidhaa hizi zinapatikana Majimoto hapa Katavi”. Alisema Mhe. Pinda.

Akiwa viwandani hapo Mhe. Pinda alipata fursa ya kutembelea na kujione jinsi viwanda vivyo vinavyofanya kazi huku akiahidi kushughulokia changamoto zinazowakabiri wafanyabiashara hao ikiwemo tatizo la umeme ambao umekuwa ukikatika mara kwa mara na kupelekea kukwamisha uzalishaji mkoani humo.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Flamingo Foods Ndg. Leonard Lusaganya, amemshukuru Kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa eneo hilo kwa kufika kujionea halihalisi iliyopo katika viwanda vivyo huku akisema kuwa ziara hiyo imewaongezea ari ya kuendelea kuzalisha bidhaa nyingi na bora Zaidi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaongeza uzalishaji hatua itakayosaidia kupunguza tatizo la upatikanaji wa bidhaa hizo nchini.

Ndg. Lusaganya aliishukuru Serikali ya mkoa wa Katavi kwa kuboreshea mazingira mazuri ya uwekezaji ambapo imewasaidia kuongeza uzalishaji kwa kiwango kikubwa na hivyo kupelekea kuzalisha bidhaa zinazotosheleza mahitaji ya wananchi mpaka kufikia kufanya biashara ndani na nje ya nchi.

Share:

Monday, 14 February 2022

KONTENA LACHOMOKA NA KUUA MWENDESHA BODABODA DAR

MTU mmoja ambaye ni Mwendesha Bodaboda anasadikiwa kufariki dunia baada ya kuangukiwa na kontena lenye nafaka katika eneo la Tabata Bima, jijini Dar es Salaam.

Mtu huyo ambaye jina lake halijatambulika mara moja inaelezwa kuwa aliangukiwa na kontena lililokuwa kwenye lori baada ya lori hilo kukwepa daladala lililosimama ghafla na kontena kuchomoka.

Baadhi ya mashuhuda wamedai abiria aliyekuwa katika bodaboda hiyo alifanikiwa kuruka na kuikwepa ajali.

“Gari ya kontena ilikuwa inakuja kwenye njia yake lakini iliongozana na daladala, wote walikuwa spidi, ghafla daladala akasimama kuchukua abiria, dereva wa lori akalazimika kutanua kukwepa daladala ambapo kontena lilichomoka likaanza kuviringinga.

“Abiria wa bodaboda akaruka, lakini yule dereva akawa anahangaika namna ya kutafuta kukwepa ajali ile tayari kontena likawa limemfunika papo hapo,” wamesema mashuhuda wa tukio hilo.
Share:

BENKI KUU TANZANIA (BoT) YAWATAKA WAANDISHI KUWA SEHEMU YA KUVUTIA UWEKEZAJI KUPITIA KALAMU ZAO

Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mbeya akifungua semina ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa vyombo vya habari nchini inayofanyika kwenye tawi la BoT mkoani Mbeya katikati ni Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo na kulia ni Emmanuel Lengwa wa ITV na mtunza muda wa semina hiyo.

.............................................

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatamani wanahabari wawe sehemu ya kuvutia uwekezaji kupitia kalamu zao kwa kuandika habari zinazoibua fursa mbalimbali za kiuchumi, zinazopatikana nchini ili kuvutia wawekezaji na kuinua uchumi wa wananchi na taifa kupitia fedha za kigeni.

Amesema habari zitakazoandikwa zikiainisha fursa mbalimbali zinazoonyesha fursa zinazopatikana katika kilimo cha Parachichi Nyanda za juu Kusini zitahamasisha wakulima wengi kujiingiza kwenye zao hilo na hatimaye kujikwamua kiuchumi na kuisaidia Taifa kupata fedha za kigeni.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mbeya, Dk. Nicholaus Kessy kwa niaba ya Naibu Gavana wa (BoT) nchini, Bernard Kibesse wakati akifungua semina kwa Wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini inayofanyika katika tawi la (BoT) jijini Mbeya.

"Semina hii imejikita kuwafundisha wanahabari kuwa wabobezi wa habari za Uchumi, fedha na biashara kwa sababu wanahabari wakibobea katika eneo hilo wataweza kuandika kwa weledi habari zinazohusu sera mbalimbali za fedha pamoja na kuchambua kupitia vipindi, na makala zinazoeleza majukumu ya benki kuu Tanzania ,” amesema Dk. Kessy.

Ameongeza kuwa wanahabari wanapaswa kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana hususani Mikoa ya Nyanda za juu kusini ikiwamo vivutio vya uatlii na kilimo ili kuwavutia wawekezaji na watalii kutembelea Hifadhi za Taifa kama vile Kitulo, Ruaha, Katavi , Ziwa Ngosi na maeneo mengine yenye kuvutia.

Naye, Kaimu Meneja wa Mahusiano na Itifaki kutoka Benki ya Tanzania (BoT), Vicky Msina amesema semina inayotolewa kwa waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha inalenga kuwajengea uwezo kuchambua na kuandika habari kwa weledi zinazohusu majukumu ya benki.

Msina amesema miongoni mwa mambo wanayofundishwa wanahabari ni kutambua matumizi ya lugha za kifedha ili kuwasaidia wanahabari kuandika habari zitakazoeleweka kwa jamii.

“Hii ni semina ya tisa tangu kuanza kwa utaratibu huu, tumeona manufaa makubwa baada ya kuwapatia wanahabari mbalimbali nchini kuhusu masuala mbalimbali yanayofanywa na Benki kuu ya Tanzania pamoja na masuala mengine yanayohusu biashara na uchumi,” amesema Msina.
Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania BoT tawi la Mbeya akifungua semina ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa vyombo vya habari nchini inayofanyika kwenye tawi la BoT mkoani Mbeya katikati ni Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo kushoto ni Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki (BoT) Bi. Vick Msina na kulia ni Emmanuel Lengwa wa ITV na mtunza muda wa semina hiyo
Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ili kumkaribisha mgeni rasmi.
Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ili kumkaribisha mgeni rasmi kulia ni mgeni rasmi Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mbeya akimsikiliza.
Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki (BoT) Bi. Vick Msina akitoa neno la utangulizi kabla ya mgeni rasmi kufungua semina hiyo kulia ni Dorcas Mtenga Mwenyekiti wa Semina na katikati ni Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania BoT.
Baadhi ya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania wakiwa na majukumu mbalimbali ili kufanikisha semina hiyo hapa wakijadiliana jambo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika seminahiyo inayofanyika kwenye tawi la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani Mbeya.
Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo akizungumza na washiriki wa semina hiyo kabla ya kuanza rasmi kwa semina hiyo.
Picha ya Pamoja
Share:

Sunday, 13 February 2022

ZAMARADI MKETEMA AZUA GUMZO KUTUNDIKA BANGO BARABARANI KUELEZEA HISIA KWA VALENTINE WAKE

Zikiwa zimebaki saa chache tu kuingia Valentine’s day February 14 2022 Mtangazaji/Mjasiriamali @ZamaradiMketema ameingia kwenye trend mitandaoni baada ya kutundika barabarani bango lenye picha ya Mume wake likiwa na maneno ‘acha dunia ijue nakupenda kiasi gani, YOU ARE MY KING, happy Valentine’s day my love…… from your loving Wife”

Baada ya kusambaa kwa picha hii @ayotv_ ilimpigia simu Zamaradi ili kufahamu mengine ambapo amesema bango hili ambalo alianza kuliandaa kwa wiki mbili zilizopita bila Mume wake kufahamu, limewekwa leo February 13 saa kumi na mbili jioni na amelilipia litakaa hapo kwa muda wa mwezi mzima "hii ni barabara ambayo anapenda sana kupita yani kila siku lazima apite ndio maana nimeliweka pale"

"Baada ya kuliweka nilimchukua mpaka pale amefurahi sana, tulipofika pale alicheka sana alafu akaingia kwenye gari machozi yakawa yanamtoka akaanza kulia akawa ameinama kwenye gari akasema kwahiyo Mke wangu umeamua kuniweka hapa juu…… amefurahi sana kwakweli”

“Sasa hivi tuna miaka mitano ya ndoa lakini sita ya mahusiano, nia yangu kumuweka kwenye bango ni jinsi ninavyompenda, ninampenda sana Mume wangu, Mume wangu amekua ni Mtu flani ambae amenifanyia vitu vingi hakuna Mtu ambaye anaweza akajua” ——— Zamaradi.

“He is a special man in mylife nafikiri siku moja naweza kukupa Interview ambayo sijawahi kuitoa popote.... amekua ni Mtu ambae ananipenda sana hata maneno hayawezi kutosha kumuelezea ni Mwanaume wa namna gani kwenye maisha yangu" amemalizia Zamaradi.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger