Monday, 17 January 2022

MBUNGE SANTIEL KIRUMBA AZINDUA SACCOS YA UWT KAHAMA...ATOA BIMA ZA AFYA, MIL 5 KUWAPIGA TAFU


Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akijiandaa kumkabidhi shilingi Milioni 5 Mwenyekiti wa SACCOS ya UWT Kahama,  Ashura Ally (katikati) wakati akizindua SACCOS ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM (UWT) wilaya ya Kahama. 

Na Mwandishi wetu - Kahama
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba amezindua SACCOS ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM (UWT) wilaya ya Kahama huku akikabidhi shilingi Milioni 5 kwenye SACCOS hiyo ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kuwaunga mkono kwenye SACCOS hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mhe. Santiel Kirumba amezindua SACCOS hiyo ya UWT wilaya ya Kahama yenye jumla ya wanachama 133 kutoka kata 58 za wilaya ya Kahama, Jumamosi Januari 15,2022 wilayani Kahama.

Mhe. Santiel Kirumba pia ametoa bima za afya na kuzindua bima kwa wanawake wa kata 58 za wilaya ya Kahama kwa wanachama 133 wa SACCOS ya UWT wilaya ya Kahama.
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa SACCOS ya Kahama, Ashura Ally Hati ya Usajili wa SACCOS ya UWT Kahama ‘SACCOS ya Wanawake Wilaya ya Kahama wakati akizindua SACCOS ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM (UWT) wilaya ya Kahama.
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza wakati akizindua SACCOS ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM (UWT) wilaya ya Kahama. Mhe. Santiel alichangia shilingi Milioni 5 ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kuwaunga mkono kwenye SACCOS hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza wakati akizindua SACCOS ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM (UWT) wilaya ya Kahama. Mhe. Santiel alichangia shilingi Milioni 5 ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kuwaunga mkono kwenye SACCOS hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akimkabidhi shilingi Milioni 5 Mwenyekiti wa SACCOS ya UWT Kahama  Ashura Ally wakati akizindua SACCOS ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM (UWT) wilaya ya Kahama. 
Mwenyekiti wa SACCOS ya UWT Kahama  Ashura Ally akionesha shilingi Milioni 5 zilizotolewa na Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba  ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kuwaunga mkono kwenye SACCOS hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kushoto) akikabidhi kadi za bima ya afya kwa mmoja wa wanawake wa UWT Kahama
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kushoto) akikabidhi kadi za bima ya afya kwa mmoja wa wanawake wa UWT Kahama
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kushoto) akikabidhi kadi za bima ya afya kwa mmoja wa wanawake wa UWT Kahama
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kushoto) akikabidhi kanga za Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya wanawake wa UWT Kahama
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza na wanachama wa UWT Kahama




Share:

RAIS KEITA AFARIKI DUNIA



Rais wa Mali aliyeondolea madarakani Ibrahim Boubacar Keita amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Januari 17, 2022 akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki zake wamethibitisha kifo hicho na kusema Keita amefariki majira ya saa 600 usiku kwa saa za Afrika Mashariki nyumbani kwake mjini Bamako.

Itakumbukwa kuwa, Miaka miwili iliopita, Keita aliugua kiharusi lakini chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi mpaka sasa.

Keita aliiongoza Mali kwa miaka saba kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2020, wakati alipopinduliwa kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali kutokana na jinsi alivyolishughulikia suala la Wanajihad.

Mgogoro wa kiuchumi na uchaguzi ulio huru pia ulisababisha maandamano hayo dhidi ya utawala wake. Keita alihusika katika siasa kwa zaidi ya miongo mitatu, akihudumu kama waziri mkuu wa nchi hiyo tangu mwaka 1994 hadi mwaka 2000.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 17,2022

Magazetini leo Jumatatu January 17 2022


Share:

Sunday, 16 January 2022

WASIOMWAMINI MUNGU WATOA ONYO KANISA LA PEFA KUWAPIGIA KELELE

Chama cha Wasioamini Uwepo wa Mungu Kenya (AIK) kimetishia kulishtaki Kanisa la Pentecostal Evangelistic Fellowship of Africa (PEFA), Nairobi kwa kile kilitaja kama uchafuzi wa kelele.

Chama hicho kimesema kimekuwa kikipokea malalamishi kuwa Kanisa la PEFA mtaani Saika hupiga kelele nyingi wakati wa kesha Ijumaa na siku ya Jumapili. Katika barua iliyoandikwa Jumamosi, Januari 15, rais wa chama hicho, Harrison Mumia aliipa kanisa hilo makataa ya siku 14 kupunguza kelele ama lichukuliwe hatua za kisheria.

"Kelele kutoka kwa kanisa la PEFA haiwezi kuvumilika kwa wakazi wengi wanaoishi karibu nalo," ilisoma barua iliyotumwa kwa Askofu John Okinda na Mchungaji Alex Wanyonyi.

Mumia aliongeza kuwa malalamishi hayo si ya wanachama wa AIK bali Wananchi Wakenya ambao wanahisi kanisa hilo linawaharibia starehe zao. 

Waandikia NEMA barua 

Awali, chama hicho kiliandikia Mamlaka ya Kuhifadhi Mazingira (NEMA), barua kikiitaka ifunge maabudu yenye kelele.

Mumia alisema maabudu hayo yanakiuka sheria zilizowekwa za kuzuia uchafuzi wa kelele. 

Kulingana na taarifa iliyotolea siku ya Jumanne, Januari 19, 2021, wasiomwamini Mungu walisema walipokea malalamishi kutoka kwa Wakenya wakidai makanisa hayo yaliwakosesha amani. 

Kwa mfano, Mumia alisema kuna misikiti ambayo huendesha ibada zao kila baada ya saa tano huku wakiwekwa vipasa sauti nje ya majengo yao. 

Share:

UJENZI WA IKULU YA CHAMWINO KUKAMILIKA MWEZI MEI 2022


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Januari 16, 2022 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ikulu inayojengwa katika eneo la Chamwino, Jijini Dodoma na kusema ameridhishwa na kasi ya ujenzi na ubora wa majengo hayo na amemtaka mkandarasi ahakikishe mradi huo unakamilika mwezi mei mwaka huu.

Waziri Mkuu amewasisitiza wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa wakati na kuwapongeza wote wanaohusika na ujenzi. “Tunataka kumuwezesha Mheshimiwa Rais kufanya kazi katika eneo lake maalum na afanye kazi katika mazingira mazuri na kwa ufanisi.”
“Nimefurahishwa na taarifa kwamba ujenzi huu umefikia asilimia 91 na hatua iliyobaki hizi asilimia 9 ni kazi ndogondogo kama uwekaji wa milango, njia za mifumo ya hewa na umeme na zote zinaenda vizuri.” Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan pia anatarajia kuona ujenzi huo unakamilika kwa wakati.
Waziri Mkuu amelipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kutekeleza ujenzi huo kwa ufanisi. “Ramani iliyoko hapa iko sawasawa na jengo la Ikulu lililoko Dar es Salaam, Wakandarasi wetu mmefanya kazi kubwa sana, Hii imedhihirisha kuwa nchi yetu ina wataalam wa kutosha kujenga aina yoyote ya majengo.”

Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mhandisi Daudi Kondoro amemhakikishia Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamba mradi huo utakamilika na kukabidhiwa mwezi Mei kama inavyotarajiwa kwani sasa uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji.
Share:

WATAALAM SEKTA YA UVUVI WATAKIWA KUTIMIZA LENGO LA UKUSANYAJI MADUHULI YA SERIKALI


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza katika kikao cha wataalam wa Sekta ya Uvuvi (hawapo pichani) kilichojadili hali ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali ambapo amewaeleza wataalam hao kuwa katika kipindi kilichobaki cha mwaka wa fedha 2021/2022 ni lazima lengo la kukusanya bilioni 40 litimizwe. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Bw. Emmanuel Bulayi na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Nazael Madala. Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Morena Hotel Jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Bw. Emmanuel Bulayi akizungumza wakati wa kikao cha wataalam wa sekta ya uvuvi kilichojadili kuhusu ukusanyaji wa maduhuli ya serikali. Kulia kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Nazael Madala. Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Morena Hotel Jijini Dodoma.


Mhasibu Mkuu wa Sekta ya Uvuvi, Bw. Lupakisyo Mwakitalima (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu hali ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kwenye sekta ya uvuvi kwenye kikao cha Waziri wa Mifugo na Uvuvi na wataalam wa sekta hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Morena Hotel Jijini Dodoma.


Baadhi ya Viongozi na Wataalam wa Sekta ya Uvuvi wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa kuhusu ukusanyaji wa maduhuli kwenye sekta hiyo.


Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Mashimba Ndaki (Mb) na Wataalam wa Sekta ya Uvuvi waliofanya vizuri katika ukusanyaji wa maduhuli ya serikali ambapo wote wamekusanya zaidi ya asilimia 70 ya lengo walilopangiwa. Kulia waliokaa ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Bw. Emmanuel Bulayi na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji, Dkt. Nazael Madala.

...............................................................

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amewataka wataalam wa sekta ya Uvuvi kuhakikisha wanakusanya maduhuli ya serikali ili kutimiza lengo la kukusanya bilioni 40 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Waziri Ndaki ameyasema hayo leo (15.01.2022) kwenye kikao cha wataalam wa sekta ya uvuvi kilichojadili hali ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kupitia sekta ya uvuvi ambapo mpaka sasa sekta hiyo imekusanya bilioni 10 kati ya bilioni 40 zilizolengwa.

Katika kikao hicho taarifa za ukusanyaji wa maduhuli ya serikali ziliwasilishwa kwa kila kituo ambapo pia changamoto ziliwasilishwa na kujadiliwa namna gani ya kuweza kukabiliana nazo ili kuhakikisha ukusanyaji wa maduhili unafikia malengo yaliyowekwa.

Akizungumza na wataalam hao Waziri Ndaki amesema kuwa ni lazima wataalam kuhakikisha wanaongeza usimamizi kwenye maeneo yao ili malengo ya ukusanyaji wa maduhuli yatimie. Ili kuhakikisha malengo ya ukusanyaji maduhuli yanafikiwa Waziri Ndaki amesema vituo vitatakiwa kutoa taarifa ya ukusanyaji wa maduhuli kila wiki ili kama kunakuwepo na changamoto iweze kutatuliwa kwa wakati.

Lakini pia wataalam wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na kwa kujitolea ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali yanatimizwa. Waziri Ndaki amewaeleza wataalam hao kuwa katika muda wao wa utumishi ndani ya sekta ya uvuvi ni lazima waache alama ikiwemo ya ukusanyaji mzuri wa maduhuli.

Wataalam hao wametakiwa kuwa wabunifu katika ukusanyaji wa maduhuli ya serikali na kuhakikisha wanasimamia sheria, kanuni, miongozo na taatibu zilizowekwa. Pia wametakiwa kuhakikisha kuwa wanalinda na kuzisimamia rasilimali za uvuvi. Vilevile amewaonya wataalam hao kutojihusisha na uvuvi haramu kwani wakibainika hatua zitachukuliwa dhidi yao.

Waziri Ndaki amesema kuwa wizara ina malengo makubwa ya kuwawezesha wavuvi ili wakue kimapato na hivyo waweze kuchangia kwenye pato la taifa kupitia sekta ya uvuvi. Aidha, amesema kuwa wizara itafanya mapitio ya tozo mbalimbali za uvuvi na kuzifanyia marekebisho endapo yatahitajika.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Bw. Emmanuel Bulayi amesema kuwa lengo la kuitisha kikao hicho ni kufanya tathmini ya hatua iliyofikiwa katika ukusanyaji maduhuli ya serikali pamoja na hali ya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi.

Pia amemshukuru Waziri kwa uamuzi wake wa kuitisha kikao hicho kwani kimesaidia kwa kuwawezesha wakuu wa vituo vyote Tanzania kukaa kwa pamoja kujadili changamoto walizonazo na kutoka na mkakati wa pamoja ili kuhakikisha ukusanyaji wa maduhuli unakwenda vizuri.

Getrude Migodela kutoka Kitengo cha Udhibiti wa Rasilimali za Uvuvi Mwanza amesema kuwa watakwenda kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Waziri ili kuhakikisha wanakusanya maduhuli kulingana na malengo yaliyowekwa. Pia ameishikuru Wizara kwa maelekezo yake ya kuwataka wafanyabiashara wa samaki na mazao ya uvuvi waanze kulipia kwenye eneo mzigo unapotoka kwa kuwa hiyo itawasaidia kuongeza mapato kwenye vituo vyao.

Kikao hicho cha wataalam kimefanyika kwa lengo la kuwakutanisha wataalam wa uvuvi wanaohusika na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali ili waweze kujadili changamoto na mikakati itakayowezesha sekta ya uvuvi kutimiza malengo ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali lakini pia kuhakikisha uvuvi haramu unadhibitiwa.
Share:

YANGA YAZIDI KUJICHIMBIA KILELENI, YAICHAPA COASTAL UNION 2-0


***************


EMMANUEL MBATILO



Klabu ya Yanga Sc imefanikiwa kuondoka na alama tatu mara baada ya kufanikiwa kuichapa Coastal Union ya Tanga kwa mabao 2-0 katika dimba la Mkwakwani Tanga.

Yanga Sc ilianza kupata bao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa DR Congo Fiston Mayele ambaye alimalizia krosi iliyopigwa na beki Djuma Shabani dakika ya 40 ya mchezo.

Goli la pili la Yanga liliwekwa kimyani na Said Ntibazokiza dakika ya 90 ya mchezo akipokea pasi murua kutoka kwa Farid Mussa.
Share:

AJALI YA TRENI YAJERUHI NA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO TANGA



Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kuwa Treni ya abiria yenye injini namba 9022 imepata ajali majira ya saa 10 Alfajiri kati ya Mkalamo na Mvave Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga January 16,2022 ikiwa inatokea Arusha kuelekea Dar es salaam ikiwa na behewa 14 zenye abiria 700 ambapo behewa 5 zilipinduka na nyingine 4 ziliacha njia na kupelekea majeruhi watano na kifo cha Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka saba.

Shirika la Reli limesema linaendelea kufuatilia kwa ukaribu kufahamu chanzo cha ajali hiyo ili kuchukua hatua.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger