Rais Samia amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya wawili (Moshi na Karatu) kwa kuwahamisha vituo vya kazi huku akiteua mkuu wa wilaya mmoja.
Sunday, 5 December 2021
Saturday, 4 December 2021
RAIS MSTAAFU KIKWETE AONGOZA HARAMBEE UJENZI WA OFISI ZA TAWLA DODOMA
Rais Mstaafu wa wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea Tuzo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa TAWLA Stella Rweikiza (kulia) katika harambee iliyolenga kukusanya fedha kwaajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la Chama hicho Jijini Dodoma. Harambee hiyo ilifanyika Disemba 3, 2021 katika hoteli ya Serena Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa TAWLA Stella Rweikiza (wa pili kulia) akimkabidhi Tuzo Rais Mstaafu Dkt. jakaya Kikwete (wa pili kushoto) katika hafla hiyo, (wa kwanza kushoto), ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Tike Mwambipile.
Rais Mstaafu wa wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Wanachama wa TAWLA na wadau mbalimbali wa Sheria walioudhuria hafla hiyo.
Wakili Mary Richard ambaye pia ni mwanachama wa TAWLA akizungumza kwenye hafla hiyo kuelezea mafanikio ya Chama hicho katika kipindi cha miaka kumi mpaka sasa.
Mmoja wa waanzilishi wa TAWLA Balozi Mwanaidi Maaja akizungumza kwenye hafla hiyo akielezea historia ya Chama hicho, changamoto walizopitia na mafanikio waliyopata.
Wanachama wa TAWLA walioshiriki hafla hiyo wakifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi.
Wageni waalikwa na wadau wa Sheria wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi Dkt. Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Tike Mwambipile akizungumza kwenye harambee hiyo akielezea namna ambavyo walivyoanza ujenzi wa Ofisi za Taasisi hiyo na hatua iliyofikia.
Rais mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akifuatilia maelezo ya Mkurugenzi wa TAWLA Tike Mwambipie (hayumo pichani) wakati wa harambee hiyo.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete (wa tatu kulia) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa TAWLA Stella Rweikiza (wa pili kulia), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Tike Mwambipile (kushoto) katika harambee hiyo iliyofanyika Disemba 3,2021 kwenye hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA HUGHES DUGILO)
********************
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
Imeealezwa kuwa licha ya kuwepo kwa mwamko mkubwa wa wanawake kutafuta msaada wa kisheria wanapopatwa na changamoto mbalimbali katika jamii lakini bado lipo tatizo kubwa la kuchelewa kutoa taarifa zao kwenye vituo vya msaada wa sheria.
Hayo yamebainika Jijini Dar es Salaam wakati wa harambee iliyolenga kukusanya fedha kwaajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania ambapo mgeni rasmi kwenye harambee hiyo alikuwa Rais mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete.
Katika harambee hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Dar es Salaam Serena, Rais Kikwete aliipongeza TAWLA kwa hatua kubwa waliyopiga katika kupanua wigo wa shughuli zake nakwamba Chama hicho kumekuwa msaada mkubwa na kimbilio la wanawake wengi hapa nchini wanapopatwa na changamoto kwenye jamii zao hasa kwenye eneo la mirathi.
Amesema kuwa hatua ya TAWLA kujenga jengo la Ofisi zake Jijini Dodoma kunaonesha kukua kwa Chama hicho nakwamba hilo ni jambo la kuungwa mkono.
“Nawapongeza sana TAWLA kwa kutanua wigo wa shughuli zenu Mimi naamini kukamilika kwa jengo lenu Jijini DODOMA kutawanufaisha pia watu wa mikoa ya jirani hasa waishio vijijini” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wake aliwateua majaji wanawake zaidi ya 30 baada ya kuona jitihada zinazofanywa na TAWLA katika kuwatetea wanawake wanaopitia changamoto mbalimbali katika Jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Tike Mwambipile aĺisema kuwa upo mwamko mkubwa wa wanawake kutafuta msaada wa sheria wanapopatwa changamoto mbalimbali katika jamii lakini wanachelewa kufika kwenye vituo vya kupata msaada nakwamba wapo miongini mwao wanaotumia vishoka na hivyo kujikuta wakiharibikiwa kutokana na upotevu wa muda.
“Tanzania tuna sheria nyingi ambazo ni nzuri zinazomlinda na kumsaidia mwanamke hivyo wanawake wakichukua hatua ya kufika kwenye vyombo vya Sheria wanapata msaada wa haraka” Ameeleza.
Ameongeza kuwa Serikali imejitahidi kwa kiasi kikubwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sheria nakwamba yapo madawati ya msaada wa sheria kwenye vituo vya polisi ambapo wananchi wanapata huduma za awali kabla ya wao kufikiwa.
Akizungumzia harambee hiyo amemshukuru Rais mstaafu Kikwete kwa kushirikiana nao na kuongoza zoezi hilo na kusaidia kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
“Tunamshukuru sana Rais Kikwete kwa kuongoza zoezi zima la harambee yetu tumeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa zaidi ya asilimia 60, kwakweli tumefurahi sana” aliongeza.
Harambee hiyo iliilenga kukusanya fedha kiasi cha Shilingi milioni 100 kwaajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la TAWLA pamoja na Samani zake ambapo jengo hilo lipo eneo la ilazo Jijini Dodoma.
RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MABASI YAENDAYO HARAKA AWAMU YA PILI (BRT II) DAR
KATIKA Kuelekea Miaka 60 ya Uhuru- Mhe. Rais Samia aweka jiwe la msingi Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa -Chang’ombe-Sokoine na Kawawa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa katika sherehe zilizofanyika Mbagala Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Wengine katika picha ni Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbagala hawaonekani pichani mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa zilizofanyika Mbagala mkoani Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Moja ya Kituo Kikubwa cha Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) kilichopo Mbagala mkoani Dar es Salaam.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa zilizofanyika Mbagala mkoani Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila wakati akitoa maelezo ya Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa kabla ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Mradi huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na viongozi Wengine mara baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya pili (BRT II) katika Barabara ya Kilwa-Chang’ombe-Sokoine na Kawawa katika sherehe zilizofanyika Mbagala Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 04 Desemba, 2021.
WATU ZAIDI YA 20 WAFARIKI BAADA YA BASI KUTUMBUKIA MTONI
Katika video iliyoonekana na gazeti la Star siku ya Jumamosi, basi hilo lilijaribu kuliongoza gari hilo kupita daraja lililofurika maji kwa usaidizi wa wakazi.
Baada ya dakika chache, basi hilo lilionekana likihangaika kusogeza magurudumu yake kwa vile mawimbi ya maji yalikuwa makali sana hivyo kulipeleka mtoni.
Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Mashariki Joseph Yakan alithibitisha kisa hicho na kuongeza kuwa waumini wa Kanisa Katoliki la Mwingi walikuwa wakielekea harusini.
The Standard limeripoti kuwa basi hilo lilikuwa na takriban watu 30, ajali hiyo ilipotokea saa 11 asubuhi katika Kijiji cha Ngune, Mwingi ya Kati.
Polisi walisema wanakwaya hao walikuwa wakielekea kwenye harusi ya mwenzao.
Baadhi ya abiria walionekana wakipiga kelele na kuinua mikono yao kupitia madirishani huku basi hilo likizama taratibu.
Chanzo - BBC Swahili
GHANA BINGWA CANAF 2021
Na John Mapepele
Timu ya Ghana wameibuka mabingwa kwenye mashindano ya soka barani Afrika kwa wenye ulemavu (CANAF 2021) baada ya kushinda Liberia magoli 3-2.
Mchezo wa fainali hiyo umechezwa leo Disemba 4, 2021 kwenye uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul akiwa na Katibu Mkuu, Dk. Hassan Abbasi na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi ameongoza watanzania na wadau wa mchezo huo kutoka mataifa mbalimbali kushuhudia mchezo huo.
Kufuatia ushindi huu Ghana inakuwa bingwa wa mashindano ya CANAF 2021 ikifuatiwa na Liberia, Angola inakuwa mshindi wa tatu na Tanzania wenyeji wanakuwa wa washindi wa nne.
Timu zote nne ambazo ni washindi zinakuwa zimefuzu kuwakilisha Bara la Afrika kwenye mashindano ya mchezo huo katika mashindano ya dunia nchini Uturuki Oktoba 2022.
Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka kwa wenye ulemavu (WAF) Mateus Wildack ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi mahiri wa kuiletea Tanzania maendeleo na kuwashirikisha walemavu katika michezo.
WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WAFANYA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA MSIKITI GALAMBA IBADAKULI
KATIBU TAWALA MKOA WA SHINYANGA ZUWENA OMARY AUDHURIA MAULID I AHAIDI USHIRIKIANO
Zaidi ya Shilingi milioni moja zimechangwa na Waumini wa dini ya Kiislam kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa Galamba uliopo katika kata ya Ibadakuli wakati wa Harambee iliyofanyika katika Msikiti wa Safina uliopo katika kata ya Ndembezi halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Harambee hiyo imefanyika leo Jumamosi Desemba 4,2021 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura pamoja na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Ester Makune.
Fedha hizo zimekusanywa katika harambee iliyofanyika katika Msikiti wa Safina Ndembezi ikiwa ni Maadhimisho ya Mazazi ya Mtume Muhammad (Maulid) yaliyoandaliwa na akina mama wa dini ya Kiislamu wilaya ya Shinyanga mjini kata ya Abubakari Swidiq iliyopo katika kata ya Ndembezi.
Katibu wa JUWAKITA Bakwata mkoa wa Shinyanga Mwadawa Hassan ameeleza kuwa wao kama akina mama wa dini ya Kiislamu wilaya ya Shinyanga mjini wameamua kumsifu Mtume Muhammad kwa kuadhimisha na kuzitaja sifa za Mtume Muhammad kwa kuadhimisha Mazazi ya Mtume Muhammad S.A.W (Maulid)
Naye Sheikh Majaliwa Masoud kutoka Ofisi ya BAKWATA mkoa wa Shinyanga ameushukuru uongozi wa akina mama hao na kuwaomba akina mama wengine wa dini ya Kiislamu kuiga mfano uliofanywa na akina mama wa Msikiti wa Safina Ndembezi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa waumini na viongozi wa msikiti huo huku akishauri viongozi kubuni vyanzo vya mapato pamoja na kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na halmashauri za wilaya.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati wa Harambee iliyofanyika katika Msikiti wa Safina uliopo katika kata ya Ndembezi halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga leo Jumamosi Desemba 4,2021. Picha na Amos John
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati wa Harambee iliyofanyika katika Msikiti wa Safina uliopo katika kata ya Ndembezi halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
TCAA YAADHIMISHA WIKI YA USAFIRI WA ANGA KWA KUTOA SEMINA KWA WATOTO NA KUTEMBELEA UWANJA WA NDEGE
Watoto wakiwa kwenye chumba cha kuongozea ndege kilichopo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Watoto wakiwa kwenye picha ya pamoja
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga akizungumza na wanafunzi wa watoto wa watumishi wa TCAA waliofika kwenye semina ili kupata elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga akizungumza na wanafunzi wa watoto wa watumishi wa TCAA waliofika kwenye semina ili kupata elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo
Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Shukuru Nziku akitoa semina kwa watoto wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) waliofika kwenye Mamlaka hiyo ili kupata elimu ya kazi zizofanywa na mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
**
Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani, Mamlaka imeendesha mafunzo Kwa watoto wa watumishi wa TCAA kuhusu Usafiri wa Anga na kufanya ziara katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ili kupata elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa semina hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga amesema Mamlaka hiyo imeamua kuandaa semina ili kuweza kutoa elimu kwa watoto hao ili waweze kujua kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwa nadharia pamoja na vitendo.
Pia amesema watoto ni taifa la kesho hivyo wanapaswa kuandaliwa vyema ili kuweza kufikia malengo pamoja na ndoto zao hivyo wanapaswa kusimamiwa kwa kupewa elimu iliyobora na yenye tija kwa maisha yake ya baadae.
Amesema elimu watakayoipata kwenye semina hiyo isiishie hapo bali iwe chachu kwao na wakawe mabalozi wazuri wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa watoto wenzao wa mtaani pamoja na shuleni.
TRA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA WAKALA WA SERIKALI TUZO ZA NBAA
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata akipokea tuzo ya ushindi wa kwanza katika kundi la Wakala wa Serikali kwenye Shindano la Uandaaji Bora wa Hesabu kwa Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu za Sekta za Umma kwa mwaka 2020. Shindano hilo liliandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) na hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju Dar es Salaam
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata akipokea tuzo ya ushindi wa kwanza katika kundi la Wakala wa Serikali kwenye Shindano la Uandaaji Bora wa Hesabu kwa Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu za Sekta za Umma kwa mwaka 2020. Shindano hilo liliandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) na hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata na Mkurugenzi wa Idara ya Uhasibu Bi. Dina Edward wakiwa wameshikilia tuzo ya ushindi wa kwanza iliyotolewa kwa TRA katika kundi la Wakala wa Serikali kwenye Shindano la Uandaaji Bora wa Hesabu kwa Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu za Sekta za Umma kwa mwaka 2020. Shindano hilo liliandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) na hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju Dar es Salaam.
Watumishi wa Idara ya Uhasibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata tuzo ya ushindi wa kwanza iliyotolewa kwa TRA katika kundi la Wakala wa Serikali kwenye Shindano la Uandaaji Bora wa Hesabu kwa Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu za Sekta za Umma kwa mwaka 2020. Shindano hilo liliandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) na hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju Dar es Salaam
Watumishi wa Idara ya Uhasibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata tuzo ya ushindi wa kwanza iliyotolewa kwa TRA katika kundi la Wakala wa Serikali kwenye Shindano la Uandaaji Bora wa Hesabu kwa Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu za Sekta za Umma kwa mwaka 2020. Shindano hilo liliandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) na hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika mwishoni mwa wiki katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA TRA
MHE. MARY MASANJA AWATAKA WAKUU WA WILAYA KUHIFADHI MAENEO YA URITHI WA UTAMADUNI*
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja (Mb) akikabidhiwa zawadi ijulikanayo kama nyengo katika ufunguzi wa Siku ya Utamaduni wa Mtanzania katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki wa Siku ya Utamaduni wa Mtanzania wakifuatilia matukiao katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Mary Masanja (Mb) akizindua Siku ya Utamaduni wa Mtanzania Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.
******************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amewataka Wakuu wa Wilaya nchini kutathmini na kutafuta maeneo ya utamaduni yenye historia nzuri na kuanzisha makumbusho zitakazoweka kumbukumbu za utamaduni wa eneo husika na kuelezea historia ya jamii hiyo.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowakilishwa na Jamii ya Wanamakete katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.
“Niwaombe sana viongozi wa Serikali hasa wakuu wa wilaya na Halmashauri kwenye maeneo yenye historia nzuri basi tuzitafute ,tuzitunze na kuanzisha makumbusho” Mhe. Masanja amesisitiza.
Ameongeza kuwa endapo Watanzania watadumisha, kuendeleza na kuthamini tamaduni zao utalii utaendelea kukua zaidi.
“Mataifa mengi yamepata mapato kutokana na utalii wa utamaduni sisi pia tukiendeleza maeneo haya na kuyathamini mapato yataongezeka” Mhe. Masanja amesema.
Aidha, Mhe. Masanja ameweka bayana kuwa kupitia matamasha ya utamaduni elimu hutolewa kwa vijanaili wafahamu ni wapi jamii yao imetoka, inaenda na na pia kuzidumisha mila,desturi na tamaduni husaidia kuwaunganisha Watanzania.
Katika hatua nyingine, Mhe. Masanja amewaasa Watanzania kutumia matamasha ya utamaduni kufanya majadiliano ya kimaendeleo ili kuunga mkono jitihada za Serikali zinazohimiza wananchi kujikwamua katika hali ya umaskini, ujinga na maradhi.
Mhe. Masanja pia ameipongeza Bodi ya Makumbusho ya Taifa kwa kubuni mpango huo wa kufanya matamasha ya kiutamaduni lakini amewataka kuhamasisha jamii nyingi zaidi ziweze kushiriki katika matamasha hayo.
Naye, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Christowaja Ntandu ameahidi kuendelea kushirikiana na Jamii ya Wanamakete ili kuhifadhi utamaduni wa jamii hiyo.
MHE.MARY MASANJA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WA KIHISTORIA, UTAMADUNI NA MAMBO YA KALE
***************************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii amefungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa kihistoria,utamaduni na mambo ya kale ili waweze kupata ujuzi wa namna ya kuibua vivutio vipya vya utalii vitakavyoingizwa kwenye urithi wa dunia ili kendelea kuvutia watalii wengi zaidi.
Ameyasema hayo leo mara baada ya kufungua Mafunzo hayo yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Tanzania ni mwenyeji wa Mafunzo hayo na endapo watapata ujuzi sahihi utawawezesha wataalam hao kuweza kuingiza vivutio vyao kwenye orodha ya urithi wa Dunia.
“Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wataalam wanaohusiana na masuala ya kihistoria, utamaduni na mambo ya kale Barani Afrika ili wapeleke ujuzi katika nchi zao na kuweza kuibua maeneo mapya yatakayoweza kuingizwa kwenye urithi wa Dunia na UNESCO” Mhe. Masanja amefafanua.
MHE. GEKUL AKABIDHI BENDERA TIMU YA TAIFA YA KUOGELEA
***************
Na. John Mapepele
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo amekitaka chama cha kuogelea nchini kushirikisha mikoa yote nchini ili kupata waogeleaji wenye vipaji watakaoiwakilisha vema Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa.
Mhe. Gekul ameyasema haya leo Disemba 4, 2021jijini Dar es Salaam allipoambatana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa( BMT) Neema Msitha kuikabidhi bendera na kuiaga timu ya Tanzania inayokwenda kushiriki mashindano ya Afrika ya kuogelea nchini Uganda.
Aidha, amewapongeza wazazi kwa kuwaruhusu watoto kushiriki katika mchezo huu.
"Niwapongeze wazazi kwa mwamko mkubwa wa kuwarushusu watoto kujiunga kwenye mchezo huu, hii itasaidia kupata vipawa na vipaji vingi " amefafanua Mhe. Gekul
Amesema Serikali imeshaandaa Mpango Mkakati wa miaka kumi wa kuinua na kuendeleza michezo ili kuinua michezo.
Naye Msitha amemweleza Mhe. Naibu Waziri kuwa chama cha mchezo wa kuogelea ni miongoni mwa vyama vya michezo inayofanya kazi nzuri ya kuinua mchezo huu hapa nchini.
Kiongozi wa timu hiyo Inviolata Itatilo amesema nchi zaidi ya kumi za Afrika zinashiriki mashindano haya nchini Uganda.