Tuesday, 14 September 2021

VICTOR THOBIAS AONGOZA KURA ZA MAONI CCM UCHAGUZI UDIWANI NDEMBEZI...CHIFU ABDALLAH SUBE APITISHWA KUGOMBEA KUPITIA DEMOKRASIA MAKINI


Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmedi Bwanga

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Uchaguzi wa kura za Maoni kumpata mgombea atakayepeperusha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi mdogo wa nafasi ya udiwani katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga umefanyika leo ambapo ,Victor Thobias  ameongoza dhidi ya wagombea wenzake sita.

Victor amepata kura 41 kati ya kura 78 zilizopigwa akifuatiwa na  Bi. Pendo Sawa  ambaye amepata kura 28.

Akitangaza matokeo hayo katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini , Said Bwanga amesema nafasi ya tatu imeshikwa na Bwana Solomon Najulwa ambaye amepata kura tatu,na kwamba nafasi ya Nne wamegongana watu watatu ambao ni Dotto Joshua, Samwel Jackson na Hamis Hamis ambapo kila mmoja amepata kura mbili, huku nafasi ya tano ikishikwa na  Gelewa Njelo ambaye amepata 0.

Bwanga amesema mchakato wa kumpata mteule atakayepeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi huo mdogo atapatikana kupitia mchujo wa vikao vya ngazi ya Wilaya na Mkoa.

Wakati huo huo Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia Makini Wilaya ya Shinyanga Mjini imemteua Bwana Chifu Abdallah Issa Sube kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya udiwani wa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga

Mteule huyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti na msemaji wa Chama cha Demokrasia Makini Mkoa wa Shinyanga, ameeleza kuwa vikao vinavyohusika na uteuzi vimemthibitisha kuwa ndiye mwakilishi atakayeingia kwenye kinyang’anyiro hicho na wagombea wa vyama vingine vya siasa.

“Nimechukua fomu leo hii ya kugombea nafasi ya udiwani kata ya Ndembezi nimechukua peke yangu sikuwa na mpinzani chama kimeniamini mchakato yatari umefanyika sehemu zote hakuonekana mtu yeyote kusimama basi jina langu likapitishwa”

Mchakato huo wa uchaguzi unafuatia aliyekuwa Diwani wa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga David Nkulila kufariki dunia hivi karibuni ambaye pia alikuwa meya wa Manispaa ya Shinyanga.
Share:

Monday, 13 September 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 14,2021

Share:

NABII EVELYIN JOSHUA AKABIDHIWA MIKOBA YA TB JOSHUA


Kanisa la Sinagogi, SCOAN limemteua mke wa TB Joshua, Nabii Evelyn Joshua kuwa kiongozi mpya wa kanisa hilo.

Kanisa limesema katika taarifa yake kwenye ukurasa wa Facebook kuwa programu nzima ya kanisa itakuwa chini ya uongozi wa Mungu kwa maelekezo ya Evely Joshua.

Kwa mujibu wa chapisho hilo, wakati ulikuwa sahihi, na wafuasi wa kanisa waliombwa wasali kwa ajili ya Utukufu wa Mungu.

Awali kulikuwa na tetesi kuhusu nani atakayeongoza kanisa baada ya mwanzilishi wa kanisa TB Joshua kuaga dunia mwezi Mei 2021.

 Mabishano hayo yalisababisha kufukuzwa hivi karibuni kwa baadhi ya wafuasi wa TB Joshua kanisani.

Huduma ya TB Joshua ilitangaza kuwa mwanzilishi wa kanisa hilo na nabii mkuu wa Nigeria, Temitope Balogun Joshua amejiuzulu kwenye ukurasa wake wa Facebook, Jumamosi Juni 5, 2021.
Share:

JB ATANGAZA KUACHANA NA KAZI YA UIGIZAJI


Msanii wa Bongo Movies, Jacob Steven maarufu kama JB ametangaza kuachana na kazi ya uigizaji na kujikita zaidi katika uongozaji na uandaaji wa filamu.

JB ameandika kupitia akaunti yake ya Instagram;- ‘’Niliwahi kusema napumzika kufanya filamu na nitabaki kwenye tamthilia.. lakini sasa Nafikiria kupumzika pia kuigiza na nitabakia nyuma ya camera kama Producer na Director.

Tamthilia yangu ya #mwanamuzikiseries nafikiri itakuwa ndio ya mwisho..kuigiza.. Ni matumaini yangu kwenye kipindi chote. Tangu 1997 wakati naanza mambo hayo mpaka 2000 wakati naanzisha Jerusalem films umefurahia kazi zangu..lakini nakuahidi huo ni mwanzo tu..mengi mazuri yanakuja nikiwa nyuma ya camera.’’
Share:

JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA - TEF LAMPONGEZA RAIS SAMIA KUIHAMISHA IDARA YA HABARI


 

Share:

SITASAHAU SIKU NILIVYOOPATA SURUALI YA MSICHANA NA KONDOMU KWENYE GARI LA BWANAANGU


Ilikuwa aibu kubwa kwa nyumba yangu siku hiyo. Bwanaangu ni daktari kwenye hospitali moja mtaani kwetu na tulioana naye yapata miaka sita iliyopita kuptia njia ya harusi.

 Tumeishi maisha mazuri na ya amani hadi mwezi jana ndipo alipoanza kubadilisha tabia na mienendo yake.

Kwa wiki nne sasa amekuwa akirejea nyumbani usiku na wakati ninapomuuliza anasema kazi imekuwa nyingi. Nimekuwa nikishangaa imekuaje kazi yao imebadilika na kuwa nyingi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Mwaka juzi aliporudi usiku nilienda kuchungulia gari lake punde tu aliposhuka na niliona maajabu. Kwa kweli niliyoyaona yalinifedhehesha mno. 

Kwenye kiti cha nyuma kulikuwa na suruali nyekundu ya msichana chini ya kiti hicho kulikuwa na mpira ya kufanyia mapenzi. 

Tabia mbaya na ya aibu; sikusema lolote na ilipofika asubuhi nilienda nikachukua vitu hizo zote mbili na nikamuonyesha ndipo ugomvi ulipozuka nyumbani. 

Bwanaangu karibu aniue kwa kisu nikatorokea mlango wa nyuma.

 Nilisafiri hadi nyumbani kwetu kwa mamaangu mzazi nikamuelezea yaliyojiri na hakuamini. Alinikaribisha na kuniambia nisijali. Siku ya pili mama aliniita sebuleni na kuniambia kuwa kuna suluhisho la kudumu. 

Alipigia Daktari mmoja wa miti shamba anayeitwa Kiwanga na kumuelezea kila jambo. Aliponikabidhi simu, Daktari aliniambia kuwa niende jioni kumuona na nilipofika alifanya mambo kadhaa ya kienyeji na kunihakikishia kuwa bwanaangu atajuta alichonifanyia.

 Sikuamani ahadi hiyo. Siku iliyofuata nilisikia simu ikilia na kuichukuwa ni sauti ya bwanaangu aliyekuwa akilia na kusema nimsamehe manaake anaona nyoka wakubwa wakimfuata kila mahali. 

Nilimuambia mimi sijui hayo kisha akasema nimsamehe manaake anahisi nimemfanyia jambo.

Alisema amejuta ya kweli na turudiane. Hata haikuisha siku hiyo mwenyewe alisafiri hadi kwetu na kumuongelesha mamangu kwa heshima kisha kuahaidi kunitunza. Sasa tumerudiana na ameachana na hulka hizo za kuhanya nje. 

Kiwanga vilevile wanatibu magonjwa sugu kama Kisukari na Pressure na magonjwa mengineyo kwa kutumia miti shamba. Wasiliana na Kiwanga Doctors kwa nambari +254 769404965 Kwa WhatsApp ipo pia au tembelea Website yao: www.kiwangadoctors.com. Unaweza kuandika barua pepe yaani Email kwa: Kiwangadoctors @gmail.com.  

Share:

GGML YATOA MAFUNZO YA COVID-19 KWA WAANDISHI WA HABARI 60


Makamu Rais wa GGML, Simon Shayo akifungua mafunzo hayo
Jimmy Mtabwa ambaye ni mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza katika mafunzo hayo ya waandishi wa habari mkoa wa Geita.
Katibu Mtendaji wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita, Novatus Lyaruu akizungumza katika mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo hayo

Na mwandishi wetu
Kampuni ya uchimbaji wa Madini ya Dhahabu mkoani Geita (GGML) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari 60 wa Geita ili kuwajengea uelewa kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona.

Mafunzo hayo yaliyotolewa jana Mjini Geita, pia yamelenga kuwakumbusha waandishi wa habari umuhimu wa chanjo ya Corona.

Akifungua mafunzo hayo, Makamu wa Rais wa GGML anayesimamia miradi endelevu ya kampuni, Simon Shayo amesema GGML mbali na kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuchangia fedha za kudhibiti ugonjwa huo, imeona ni vema kufadhili mafunzo hayo ili kuwajengea uelewa wa kutosha waandishi wa habari.

Alisema moja ya jukumu la kampuni ni kuhakikisha jamii zinazoizunguka zinanufaika kutokana na uwepo wa GGML mahala hapa.

“Kwa hivyo, tumeamua kutumia mikakati tofauti kuendesha kampeni za uhamasishaji namna ya kujikinga na janga la UVIKO-19 na tumeungana na mikakati mbalimbali ya Serikali kuhamasisha watu wengi kuzingatia hatua, vigezo na taratibu zinazotolewa na watalaam wa afya wa Serikali ikiwamo umuhimu wa kupata chanjo.

“Nasema hivi kwa sababu chanjo hizi zina ufanisi mkubwa, na ni muhimu zaidi kwa sababu kinga ni bora kuliko tiba. Kwa kujilinda sisi wenyewe, tunapunguza athari kubwa ya UVIKO-19 kwa wale wanaotuzunguka. Tumeshuhudia mfano bora ukionyeshwa na viongozi wetu wakuu Kitaifa na hata Kimkoa na Kiwilaya kwa kuchanja hadharani ili kuwapa moyo wananchi wengine wachukue hatua ya kuchanja,” alisema.


Aidha, alisema kama sehemu ya ushirki wake kuunga mkono juhudi za Serikali, GGML ilitoa jumla ya Sh bilioni 1.6 kusaidia juhudi za kupunguza kasi ya kuenea kwa UVIKO-19. Lakini pia masharti na taratibu zilizokuwa zinafuatwa na GGML, zilizingatia miongozo iliyotolewa na Serikali ya Tanzania.

“Kati ya fedha zote zilizotolewa, GGML ilitoa takriban Sh bilioni 1.1 kuchangia mfuko wa kitaifa wa dharura katika kupambana na UVIKO-19. Mfuko huu ulioanzishwa na Serikali ulikuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Jumla ya Shilingi milioni 500 zilizobaki zilitumika kusaidia mahitaji mbalimbali ya mkoa na jamii inayotuzunguka hapa Geita hii ikiwa ni pamoja na utoaji wa vifaa tiba na dawa muhimu vikiwemo vya kujikinga kwa watabibu, mitungi ya gesi na kadhalika,” alisema.

Aidha, Jimmy Mtabwa aliyewakilisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wa Geita alitoa wito kwa waandishi wa habari kuungana na serikali katika kuelimisha wananchi kuhusu ugonjwa huo.

Katibu Mtendaji wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani, Geita, Novatus Lyaruu mbali na kuishukuru GGML kwa mafunzo hayo, alisema mafunzo hayo yatawasaidia kupata majawabu ya maswali mengine yaliyokuwa yameibuka kuhusu chanjo ya Johnson &Johnson.
Share:

Chief Executive Officer at Tanzania Centre for Democracy

POSITION: CHIEF EXECUTIVE OFFICER   TANZANIA CENTRE FOR DEMOCRACY Reports to: TCD Summit via TCD Chairperson Country: United Republic of Tanzania (Both Mainland and Zanzibar) About Tanzania Centre for Democracy Tanzania Centre for Democracy is a non-partisan, non-religious and non for profit political parties’ membership organization founded by five political parties with representative from the parliament of the […]

This post Chief Executive Officer at Tanzania Centre for Democracy has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA ATANGAZWA KUWA KINARA WA KUTETEA HAKI ZA WATOTO NJITI

 

Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Ajenga wa Mtoto Njiti iliyofanyika Jijini Dodoma  
Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai (MB) akizungumza mara baada ya kufanya uzinduzi huo
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara  Neema Lugangira akizungumza wakati wa uzinduzi huo

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara  Neema Lugangira ametangazwa kuwa mmoja wa Wabunge Vinara wa Kutetea Haki za Watoto Njiti (National Champions for Rights of Premature Babies).

Hayo yalibainishwa wakati wa Uzinduzi wa Ajenga wa Mtoto Njiti iliyofanyika Jijini Dodoma kwa kuzunduliwa na Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndugai (MB) ambapo katika Uzinduzi huo Taasisi ya Doris Mollel Foundation ilimtagaza Mbunge Lugangira na wengine.

Wabunge wengine waliotangazwa kuwa Vinara wa Haki za Watoto Njiti ni Mhe Stanslaus Nyongo, Mhe Festo Sanga, Mhe Salome Makamba na Mhe Kassim Hassan Haji ambapo kupitia Agenda ya Mtoto Njiti tayari Wabunge hao :inara wameshaainisha maeneo ya kuanza kufanyia kazi.

Maeneo ambayo wataanza kufanyia kazi ni Mama anayejifungua mtoto njiti kuongezewa likizo ya uzazi, bima ya afya itambue huduma zinazohitajika kwa watoto njiti na vifaa tiba (Incubators) vipatikane hospitali zote nchini ikiwemo namna ya kufanya ulezi wa kangaroo.

Aidha pia elimu ya uzazi wa watoto njiti ijumuishwe katika elimu inayotolewa shuleni ikiwemo lishe bora kwa wakina mama wajawazito kama kinga ya kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa wakiwa watoto njiti

Share:

Education Content & Material Development Officer at Plan International

The Organisation   Plan International is an independent development and humanitarian organisation that advances children’s rights and equality for girls. We believe in the power and potential of every child. But this is often suppressed by poverty, violence, exclusion and discrimination. And it’s girls who are most affected. Working together with children, young people, our […]

This post Education Content & Material Development Officer at Plan International has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

RAIS SAMIA : SERIKALI ITAENDESHWA KWA MATENDO MAKALI SIYO MANENO MAKALI 'KUFOKA SIYO HESHIMA'



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema amewataka viongozi kufanya kazi kwa vitendo zaidi badala ya kutoa maneno makali akisema  Serikali itaendeshwa kwa matendo makali siyo maneno makali.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 13,2021 wakati akiwaapisha Mawaziri Watatu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Serikali itaendeshwa kwa matendo makali siyo maneno makali. Kufoka siyo heshima, Sitegemei kuanza kufokea watu wazima wenzangu, nitafoka kwa kalamu", amesema Rais Samia



Share:

MAKADA SABA CCM WAJITOSA KUWANIA UDIWANI KATA YA NDEMBEZI KUBEBA MIKOBA YA NKULILA


Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmedi Bwanga

***
Jumla ya Makada saba wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini wamechukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi ya udiwani wa kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga.

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Saidi Ahmedi Bwanga amesema wanachama 8 wa CCM waliochukua ya kuomba ridhaa kugombea udiwani kata ya Ndembezi kuwa ni Pendo Sawa, Samwel Jackson, Gelewa Njelo, Solomon Najulwa Nalinga, Dotto Joshua, Victor Thobias na Hamis Hamis (ambao pia wamerudisha fomu) na Dkt. Ezekiel Meshaki ambaye hajarudisha fomu.

Bwanga amesema mchakato wa kumpata Diwani wa kata ya Ndembezi unafuatia aliyekuwa diwani wa kata hiyo David Nkulila kufariki dunia hivi karibuni ambaye pia alikuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga.


“Wote waliochukua fomu hizo ni wanachama halisi wa CCM ,wanachama hai na wana sifa zote za kugombea nafasi ya uongozi. Kabla ya tarehe 25 tutakuwa tumeshapendekeza jina la mgombea mmoja ambaye anaweza kuingia moja kwa moja kwenda kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea kupeperusha bendera ya CCM  katika nafasi ya udiwani”,ameongeza.

Share:

WAZIRI AWESO AITUMIA BASHUNGWA CUP KUWAPA MBINU WABUNGE


Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso na mgeni rasmi katika kilele cha mashindano ya Bashungwa CUP 2021 akimkabidhi kombe mwakilishi wa timu ya Bugeni FC baada ya kuibuka washindi kwa mikwaju ya penalti dhidi ya washindani wao FC katika fainali za Bashungwa Cup 2021

Na Projestus Binamungu WHSM

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ametoa rai kwa wabunge hapa nchini kuziomba  mamlaka zinazowazunguka  kuboresh miundombinu ya  michezo ikiwa ni pamoja na viwanja vya michezo katika maeneo yao ili kuwa katika viwango vinavyotakiwa.

 Mhe. Aweso amefafanua kwamba  endapo viwanja vya michezo vitakuwa katika viwango vinavyotakiwa, hali hiyo itawafanya vijana wengi kushawishika  kushiriki michezo mbalimbali.

Rai hizo  amezitoa  jana (Septemba 12,2021) wakati akihitimisha ligi ya Bashungwa Cup iliyokuwa ikizishirikisha timu 23 kutoka kata 23 za Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Kauli ya Waziri Aweso inafutia ombi la wakazi wa wilaya ya Karagwe waliozungumza kwa nyakati tofauti tofauti wakiomba Halmashauri ya wilaya hiyo kuufanyia ukarabati uwanja wa mpira wa Kayanga ili uwe na viwango vya kuruhusu mashindano makubwa ya ngazi ya mkoa na hata taifa kufanyika uwanjani hapo.

Akizungumza katika fainali hizo mwandaaji wa mashindano hayo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Karagwe na Waziri anayesimamia sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono jitihada za kukuza michezo katika safari ya kukuza vipaji vya vijana.

“Wote tunaamini kwenye umoja, ninamaanisha tukiungana tunaweza, Serikali inafanya kila kinachowezekana kukuza sekta ya michezo nchini, lakini si dhambi kwa mdau yeyote kutuunga mkono popote unapoweza katika kutimiza ndoto ya vijana wetu wenye vipaji vya michezo” ,alisema Waziri Bashungwa.

 Fainali hiyo iliyozikutanisha timu mbili ambazo ni Bugeni FC na Nyabiyonza FC zote za wilayani Karagwe. Timu ya Bugeni FC imeibuka mshindi kwa mikwaju ya penaliti na kubeba kombe pamoja na zawadi ya shilingi milioni mbili na laki tano huku timu ya Nyabiyonza ikishika nafasi ya pili na kubeba kitita cha shilingi milioni moja laki mbili na elfu 50, huku mshindi wa tatu ambaye ni Kihanga FC akiibuka na shilingi laki saba na elfu hamsini.

Mashindano ya Bashungwa Cup yalizinduliwa rasmi mwaka 2017 na yamekuwa yakiwakutanisha vijana kila mwaka kushindania zawadi mbalimbali, lengo likiwa ni kuwaunganisha wakazi wa wilaya ya Karagwe na kuibua vipaji vya vijana kupitia mchezo wa soka.
Mlimbwende (Miss) Karagwe mwaka 2021 Regina Kokurama akiingia uwanjani na kombe la ligi ya Bashungwa Cup mapema kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya ligi hiyo uliopigwa Septemba 12 katika uwanja wa Michezo Kayanga Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.
Picha ya pamoja kabla ya Mchezo baina ya timu mbili ambazo ni  Bugeni FC na Nyabiyonza FC zilizocheza mchezo wa fainali katika ligi ya Bashungwa Cup 2021.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso na mgeni rasmi katika kilele cha mashindano ya Bashungwa CUP 2021 akizungumza na wakazi wa Mkoa Kagera mapema kabla ya mchezo wa fainali kuanza.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Karagwe na mwandaaji wa mashindano ya Bashungwa Cup 2021 akizungumza katika kilele cha mashindano hayo.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mchezo wa fainali baina ya timu ya Bugeni FC na Nyabiyonza FC ukiendelea.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mchezo wa fainali baina ya timu ya Bugeni FC na Nyabiyonza FC ukiendelea.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mchezo wa fainali baina ya timu ya Bugeni FC na Nyabiyonza FC ukiendelea.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mchezo wa fainali baina ya timu ya Bugeni FC na Nyabiyonza FC ukiendelea.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mchezo wa fainali baina ya timu ya Bugeni FC na Nyabiyonza FC ukiendelea..
Share:

Programme Finance Associate at UNDP

Location : Dar es Salaam, TANZANIA   Application Deadline : 15-Sep-21 (Midnight New York, USA) Time left : 5d 21h 33m Additional Category : Management Type of Contract : NPSA (Short-Term) Post Level : NPSA-8 Languages Required : English Starting Date : (date when the selected candidate is expected to start) 20-Sep-2021 Duration of Initial Contract : […]

This post Programme Finance Associate at UNDP has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Commercial Relationship Manager- Chinese Desk at Absa

Locations   Absa House – ABT Zanzibar Main Branch – ABT Dodoma Branch – ABT Mikocheni Branch – ABT Morogoro Branch – ABT The Slipway Branch – ABT Dar City Mall – ABT Kilimanjaro Commercial Complex – ABT Tanga Branch – ABT Mbeya Main Branch – ABT Pugu Road Branch – ABT Iringa General Stores […]

This post Commercial Relationship Manager- Chinese Desk at Absa has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Chief of Party – Tanzania RMNCAH at Abt Associates

Job Summary   Manages small to medium program (typically USAID funded). Provides technical and programmatic leadership for program or project. Serves as the formal representative to the donors, alliance partners, host government and private sector stakeholders. Leads and directs the operations and staff. Oversees the project budget and all project financial resources. Manages project communications, […]

This post Chief of Party – Tanzania RMNCAH at Abt Associates has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

MLINZI AUAWA KWA KUCHOMWA KISU AKIMZUIA JAMAA KUFANYA MAPENZI NA MHUDUMU WA GESTI KAHAMA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mlinzi Kampuni ya Ulinzi ya Mast Holding aitwaye Steven Felician Samandari (25) ameuawa kwa kuchomwa kisu tumboni na mtu aliyekuwa amemkamata baada ya kuruka uzio akifuatilia wahudumu wa Bar/Guest house kwa ajili ya mapenzi Mjini Kahama.

Kwa Mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando kwa vyombo vya habari, tukio hilo limetokea Septemba 11,2021 majira ya saa nane usiku katika mtaa wa Nyahanga kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama.

 "Mlinzi huyo aliuawa kwa kuchomwa kisu tumboni na mtu aliyekuwa amemkamata baada ya kuruka uzio akifuatilia wahudumu wa bar/guest kwa ajili ya mapenzi",amesema.

"Chanzo cha tukio hilo ni kufuatilia wahudumu wa bar/guest kwa ajili ya mapenzi. Eneo la tukio kimeokotwa kisu kikiwa tumboni. Mbinu iliyotumika ni kuchoma kisu tumboni",amesema Kamanda Kyando.

Kamanda Kyando amesema Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke aitwaye Fatuma Juma Charles (22), mhudumu wa bar kwa uchunguzi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger