Monday, 26 July 2021

Dkt. Mabula Asikitishwa Na Wadaiwa Sugu Wa Kodi Ya Pango La Ardhi, Asema Sheria Itachukua Mkondo Wake.

Na Eliafile Solla-WANMM MTWARA
Dkt. Angeline Mabula Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema amesikitishwa na wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi mkoani Mtwara kutokana na uzito wao katika kutii sheria, kanuni, taratibu na masharti ya umiliki ardhi ambayo sharti mojawapo ni kulipa kodi hiyo kila mwaka.

Hayo yalijitokeza wakati Dkt. Angeline Mabula alipokuwa akizungumza na wadaiwa hao wa kodi ya pango la ardhi katika kikao maalum kilichohusisha watendaji wa sekta ya ardhi mkoani Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mikindani, Bw. Dustan Kyobya, Mkurugenzi wa Halmashauri kanal Emanuel Mwaigobeko pamoja na mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Mhe. Hassan Mtenga.

‘‘Wanamtwara mmekuwa wazito na wagumu sana katika ulipaji wa kodi ya pango la ardhi licha ya jitihada za kuwakumbusha mara kwa mara pamoja na kuwaletea ankara za madai, bado hamuonyeshi ushirikiano, mnaahidi lakini hamtekelezi na hivyo tutaruhusu sheria kuchukua mkondo wake japo siyo lengo la Serikali, alisema Dkt. Angeline Mabula’’

Aidha, katika kusisitiza kuhusu umuhimu wa kodi ya pango la ardhi, Dkt. Angeline Mabula alisema taifa la Tanzania linajengwa na watanzia wenyewe kupitia kodi mbalimbali wanazolipa ikiwemo kodi ya pango la ardhi ambayo mwisho hurudishwa kwao kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.

‘‘Katika ujenzi wa taifa, Serikali inawategemea wananchi na wananchi wanaitegemea Serikali hivyo maendeleo ya nchi ni ushirikiano wetu wananchi na Serikali kwa maana hiyo kodi ya pango la ardhi ina mchango mkubwa sana katika ukuaji wa uchumi, alisema Dkt. Mabula’’

Katika hatua nyingine, Dkt. Angeline mabula alidokeza kwamba, Serikali ilikusudia kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi kupitia vipande vya ardhi wanavyomiliki na hivyo kuanzisha mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha kila kipande cha ardhi kwa lengo la kuiongezea thamani ardhi na kuwanufaisha wamiliki.

‘‘Pamoja na jitihada hizi za Serikali bado wanamtwara mmekuwa wakaidi, hamtaki kuchangia hata zile gharama ndogo za upimaji na mliopimiwa hamuoni haja ya kumilikishwa na kuchukua hati zenu mkazitumie kama vyanzo vya mitaji ili kujiendeleza kiuchumi, alisema Dkt. Mabula’’

Nae mbunge wa Mtwara mjini Mhe. Hassan Mtenga aliwaambia wadaiwa hao kwamba, suala la kodi ya pango la ardhi siyo la hiari, ni sharti la kisheria na ni kodi rafiki endapo italipwa kwa wakati bila kusubiria hadi ijilimbikize na endapo haitalipwa sheria iko wazi imebainisha hatua zitakazochukuliwa kwa watakaokaidi.

Share:

Prof. Manya Atahadharisha Biashara Ya Madini Nje Ya Masoko

 Na Asteria Muhozya, Shinyanga

Wanunuzi wa Madini ya Tanzania wametahadharishwa kutokununua Madini Nje ya Mfumo wa Masoko ili kuepuka kuuziwa madini bandia tofauti na wanapofanyabiashara ndani ya masoko kwani hakuna kificho.

Tahadhari hiyo imetolewa  Julai 25, 2021 na Naibu  Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Biashara na teknolojia kwa Mkoa wa Shinyanga kwa  niaba  ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa .

Prof. Manya amesisitiza kuwa, mfumo wa biashara ya madini uliopo kwenye masoko yote 39 na Vituo vya Ununuzi wa Madini 50 yaliyoanzishwa mikoa yote nchini ni ya uwazi na hauruhusu madini bandia kuuzwa kwenye masoko hayo.

‘’ Mnaotaka kununua madini ya Tanzania msinunue nje ya mfumo wa masoko, nje ya masoko mnauziwa madini feki,’’ amesisitiza Prof. Manya.

Ameongeza kuwa kutokana na Tanzania kuonesha mageuzi makubwa kufuatia kuanzishwa kwa masoko ya madini, ndiyo nchi pekee duniani ambayo inaendesha biashara ya madini kwa uwazi kupitia masoko hayo jambo ambalo limeyafanya mataifa mengine duniani kutaka kujifunza.

 ‘’Wasiotaka kufuata taratibu ndiyo wanaokosoa mfumo wa masoko kwa kudhani Serikali imeyaanzisha ili kukusanya mapato. Wasiojua umuhimu wa masoko hayo waulizeni FEMATA na vyama vya wachimbaji kwenye mikoa watawaeleza,’’amesema Prof. Manya.

Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kuimarisha mifumo, sheria ili wananchi waendelee kunufaika na rasilimali madini na kuongeza kwamba, itaendelea kuimarisha masoko ya madini na kuyaongeza pale itakapohitajika.

Akizungumzia uzalishaji katika Mgodi Almasi Mwadui, Prof. Manya amesema uzalishaji katika mgodi huo uliathiriwa na janga la ugonjwa wa korona na hivyo kupelekea kusitishwa kwa uzalishaji lakini unatarajiwa kuanza tena uzalishaji wake mwezi Agosti, 2021.

Katika hatua nyingine, Prof. Manya amesema kuwa, Mkoa wa Shinyanga uko mbioni kuanzisha kiwanda cha kusafisha dhahabu kama ilivyo kwa mikoa ya Mwanza, Geita na Dodoma ili kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini kufanyika nchini badala ya madini ghafi kusafirishwa katika nchi nyingine jambo ambalo litasaidia kuchochea ajira ikiwemo kuyapatia thamani halisi madini yanayozalishwa nchini.

Aidha, Prof. Manya ametumia fursa hiyo kuwaasa viongozi kuacha alama ya uongozi iliyotukuka kwa kufuata kanuni na misingi ya utawala bora ikiwemo kutoa kipaumbele katika usimamizi wa fedha za maendeleo kwa ajili ya manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Akizungumzia kuhusu kuwaendeleza wachimbaji wadogo amesema kuwa serikali itaendelea kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji   yenye taarifa za msingi za kijiolojia ili kuwawezesha wachimbe kwa tija.

Kuhusu ruzuku kwa wachimbaji wadogo Prof. Manya amesema awali, ruzuku iliyotolewa na Serikali kwa wachimbaji wadogo haikuleta tija iliyokusudiwa na kueleza kuwa, hivi sasa Serikali inaangalia namna bora ambayo itawezesha ruzuku hizo kuwa na tija. Ufafanuzi huo unafuatia ombi lililowasilishwa  na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA) la kuwawezesha wachimbaji kupatiwa ruzuku.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Philemon Sengati amesema kuwa, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 kuna uwezekano wa mkoa huo kukusanya mapato zaidi yanayotokana na rasilimali madini kutokana na kupatikana kwa maeneo mengine matatu kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini.

Ameyataja manufaa ya maonesho hayo kuwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu, kuwakutanisha wazalishaji, wauzaji na walaji na kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo , kuongeza mbinu  bora za kukuza sekta ya madini mkoani humo pamoja na  kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa huo.

Kwa upande wa wakuu wa Mikoa walioshiriki katika maonesho hayo wameleeza kuhusu kuunga juhudi za  mkoa huo,  kujifunza kuhusu namna mkoa unavyosimamia sekta ya madini na kubadilisha uzoefu.

Kwa upande wake, Rais FEMATA John Bina akizungumza katika ufunguzi huo, ameiomba Serikali ione namna ya kuwawezesha mafundi mchundo kupata mafunzo nje ya nchi ili kuwawezesha kujifunza kuhusu teknolojia bora ambazo zitawasaidia wachimbaji wadogo nchini kupata teknolojia rahisi kuendeleza shughuli zao.

Maonesho hayo yamehudhuriwa pia na wakuu wa mikoa kutoka mikoa jirani ikiwemo ya Mara, Tabora, Geita na Simiyu. Aidha, washiriki katika maonesho hayo ni kutoka sekta za umma, sekta binafsi, kampuni za madini, taasisi za kifedha, watoa huduma na wajasiliamali.

Maonesho ya Pili ya Biashara na teknolojia kwa Mkoa wa Shinyanga yanaongozwa na kaulimbiu ‘’Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu’. Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021.

Share:

GRAPHIC DESIGNER and CONTENT WRITER at AA TANCH Holding Company LTD

1. GRAPHIC DESIGNER   2. CONTENT WRITER Location: ARUSHA, Head office P.O.BOX 8024 Reports to: Managing director SUMMARY: AA TANCH holding company ltd is a private limited company established in 2018. It focused on connecting buyers to seller, dedicated in providing easy, reliable and secure trades as well as shipment and delivery of products from […]

This post GRAPHIC DESIGNER and CONTENT WRITER at AA TANCH Holding Company LTD has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Biomedical Technicians at MSD

POST: BIOMEDICAL TECHNICIAN – 6 POST POST CATEGORY(S) HEALTHCARE AND PHARMACEUTICAL EMPLOYER MEDICAL STORES DEPARTMENT (MSD) APPLICATION TIMELINE: 2021-07-22 2021-08-05 DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.To assist higher level technicians in repairing, installing, calibrating, or maintaining a range of general biomedical/ clinical equipment, e.g., replacing components, taking test readings, and wiring circuits in accordance with specific instructions; ii.To perform […]

This post Biomedical Technicians at MSD has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Warehouse Officer at MSD

POST: WAREHOUSE OFFICER – 2 POST POST CATEGORY(S) HEALTHCARE AND PHARMACEUTICAL EMPLOYER MEDICAL STORES DEPARTMENT (MSD) APPLICATION TIMELINE: 2021-07-22 2021-08-05 DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.Records and maintains stocks as per prescribed MSD regulations. ii. Reconciles warehouse stock records with other records in relevant sections. iii. Records and maintains inter-warehouse stock transfers. iv. Facilitates smooth coordination between the receiving, […]

This post Warehouse Officer at MSD has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

PHARMACIST and PHARMACY TECHNICIAN at Reenbook Polyclinic Lab

PHARMACIST – (1 POSITION)   JOB RESPONSIBILITIES   Verify billing, filling and dispensing of drugs to in and out patients are done in the right, orderly and timely manner. Answer drug information queries from doctors, junior staffs and patients.  Identify, intervene and correct medication errors. Train and educate juniors on current good pharmacy practices and hospital […]

This post PHARMACIST and PHARMACY TECHNICIAN at Reenbook Polyclinic Lab has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Office Assistant at Palladium

Office Assistant     Company Overview: About Palladium Palladium is a global group working to create positive impact on the lives and livelihoods of people around the globe; broaden access to health, water, power, and infrastructure; build enduring, sustainable, and transformative institutions and market systems to address global challenges; and conserve the natural world. We operate […]

This post Office Assistant at Palladium has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Drill Master at Sandvik

Drill Master    Sandvik Mining and Rock Technology is seeking a; Location: Mwanza, Tanzania The Role: Get customer satisfaction by installing, repairing, inspecting and commissioning service, considering economical and other aspects. Problem solving by using of approaches, tools, techniques for recognizing, operational or process problems; ability to apply this knowledge appropriately in different kinds of […]

This post Drill Master at Sandvik has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Chief of Party at Abt Associates

Chief of Party – Tanzania RMNCAH   Job Description Opportunity: The anticipated USAID Tanzania C3HP RMNCAH Activity seeks to increase the demand for and use of quality integrated RMNCAH services in target regions, particularly women of reproductive age, youth and children, by improving access to quality RMNCAH services in both facilities and the surrounding communities, promoting […]

This post Chief of Party at Abt Associates has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Sound Engineer at Ubongo

Job Title: Sound Engineer Team Leader: No Department: Production, Studio Location: Dar Es Salaam, Tanzania Work Remotely: No Travel Required: None Position: Full Time Reports To: Studio Coordinator Contract Type: Project Organization: Ubongo Learning Benefits: Applicable Number of Posts: 1 UBONGO is Africa’s leading producer of kids’ edutainment. As a non-profit social enterprise, we create fun, […]

This post Sound Engineer at Ubongo has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

StoryboardArtist at Ubongo

Job Title: Storyboard Artist Team Leader: No Department: Animation Location: Dar-es-salaam,Tanzania Similar Jobs Associate Legal Officer, P-2 (TEMPORARY) at IRMCT July, 2021 Field Processing Supervisor – Tanzania National Hire at Church World Service July, 2021 Chief of Party – Tanzania RMNCAH at Abt Associates July, 2021 Drill Master at Sandvik July, 2021 Work Remotely: No Travel […]

This post StoryboardArtist at Ubongo has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Sunday, 25 July 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 26,2021

Share:

POLISI AUAWA KWA KUKATWA PANGA AKIKAMATA MHALIFU ARUSHA

Picha haihusiani na habari hapa chini

Askari polisi katika kituo kidogo cha polisi Mbughuni mkoani Arusha,PC Damas ameuawa kwa kukatwa na panga kichwani wakati akijaribu kumkamata mtuhumiwa wa wizi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jastine Masejo  amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa tano usiku katika Kijiji cha Makiba wakati askari huyo alipoenda nyumbani kwa mhalifu kwa lengo la kumkamata.

Amesema askari huyo alifariki dunia muda mfupi baada ya kuvuja damu nyingi.

"Askari wetu katika kituo kidogo cha polisi Mbughuni alikatwa panga kichwani na kufariki dunia baada ya kwenda nyumbani kwa mhalifu majira ya saa tano usiku lengo la kumkamata, hivi sasa polisi wanaoendesha operesheni ya kumsaka ili afikishwe kwenye vyombo vya dola", amesema Kamanda Masajo.

Amesema wakati wa harakati za kumkamata ndipo alipotokea mhalifu mwingine nyumba ya jirani ambaye alimkata panga moja kichwani askari huyo na kupoteza naisha.
Share:

PROF. MANYA AFUNGUA MAONESHO YA PILI YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA...AFICHUA SIRI WANAOUZIWA MADINI FEKI

Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akizungumza leo Jumapili Julai 25,2021 wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Na Asteria Muhozya, Shinyanga

Wanunuzi wa Madini wametahadharishwa kununua Madini nje ya Mfumo wa Masoko  ili kuepuka  madini bandia tofauti na wanapofanya biashara  ndani ya masoko kwani hakuna kificho.

 Tahadhari hiyo imetolewa Julai 25, 2021 na Naibu  Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia kwa Mkoa wa Shinyanga kwa  niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa .

Prof. Manya amesisitiza kuwa, mfumo wa biashara ya madini uliopo kwenye masoko yote 39 na Vituo vya Ununuzi wa Madini 50 yaliyoanzishwa mikoa yote nchini ni ya uwazi na hauruhusu madini bandia kuuzwa kwenye masoko hayo.

"Mnaotaka kununua madini ya Tanzania msinunue nje ya mfumo wa masoko, nje ya masoko mnauziwa madini feki,’’ amesisitiza Prof. Manya.

 Ameongeza kuwa kutokana na Tanzania kuonesha mageuzi makubwa kufuatia kuanzishwa kwa masoko ya madini, ndiyo nchi pekee duniani ambayo inaendesha biashara ya madini kwa uwazi kupitia masoko hayo jambo ambalo limeyafanya mataifa mengine duniani kutaka kujifunza.

"Wasiotaka kufuata taratibu ndiyo wanaokosoa mfumo wa masoko kwa kudhani Serikali imeyaanzisha ili kukusanya mapato. Wasiojua umuhimu wa masoko hayo waulizeni FEMATA na vyama vya wachimbaji kwenye mikoa watawaeleza", amesema Prof. Manya.

Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kuimarisha mifumo, sheria ili wananchi waendelee kunufaika na rasilimali madini na kuongeza kwamba, itaendelea kuimarisha masoko ya madini na kuyaongeza pale itakapohitajika.

Akizungumzia suala la uzalishaji wa katika Mgodi Almasi Mwadui, Prof. Manya amesema uzalishaji katika mgodi huo uliathiriwa na janga la ugonjwa wa korona na hivyo kupelekea kusitishwa kwa uzalishaji lakini unatarajiwa kuanza tena uzalishaji wake mwezi Agosti, 2021.

Katika hatua nyingine, Prof. Manya amesema kuwa, Mkoa wa Shinyanga uko mbioni kuanzisha kiwanda cha kusafisha dhahabu kama ilivyo kwa mikoa ya Mwanza, Geita na Dodoma ili kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini kufanyika nchini badala ya madini ghafi kusafirishwa katika nchi nyingine jambo ambalo litasaidia kuchochea ajira ikiwemo kuyapatia thamani halisi madini yanayozalishwa nchini.

Aidha, Prof. Manya ametumia fursa hiyo kuwaasa viongozi kuacha alama ya uongozi iliyotukuka kwa kufuata kanuni na misingi ya utawala bora ikiwemo kutoa kipaumbele katika usimamizi wa fedha za maendeleo kwa ajili ya manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Akizungumzia kuhusu kuwaendeleza wachimbaji wadogo amesema kuwa serikali itaendelea kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji   yenye taarifa za msingi za kijiolojia ili kuwawezesha wachimbe kwa tija.

Kuhusu ruzuku kwa wachimbaji wadogo Prof. Manya amesema awali, ruzuku iliyotolewa na Serikali kwa wachimbaji wadogo haikuleta tija iliyokusudiwa na kueleza kuwa, hivi sasa Serikali inaangalia namna bora ambayo itawezesha ruzuku hizo kuwa na tija. Ufafanuzi huo unafuatia ombi lililowasilishwa  na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA) la kuwawezesha wachimbaji kupatiwa ruzuku.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amesema kuwa, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 kuna uwezekano wa mkoa huo kukusanya mapato zaidi yanayotokana na rasilimali madini kutokana na kupatikana kwa maeneo mengine matatu kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini.

Ameyataja manufaa ya maonesho hayo kuwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu, kuwakutanisha wazalishaji, wauzaji na walaji na kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo , kuongeza mbinu  bora za kukuza sekta ya madini mkoani humo pamoja na  kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa huo.

Kwa upande wa wakuu wa Mikoa walioshiriki katika maonesho hayo wameleeza kuhusu kuunga juhudi za  mkoa huo,  kujifunza kuhusu namna mkoa unavyosimamia sekta ya madini na kubadilisha uzoefu.

Kwa upande wake, Rais FEMATA John Bina akizungumza katika ufunguzi huo, ameiomba Serikali ione namna ya kuwawezesha mafundi mchundo kupata mafunzo nje ya nchi ili kuwawezesha kujifunza kuhusu teknolojia bora ambazo zitawasaidia wachimbaji wadogo nchini kupata teknolojia rahisi kuendeleza shughuli zao.

Maonesho hayo yamehudhuriwa pia na wakuu wa mikoa kutoka mikoa jirani ikiwemo ya Mara, Tabora, Geita na Simiyu. Aidha, washiriki katika maonesho hayo ni kutoka sekta za umma, sekta binafsi, kampuni za madini, taasisi za kifedha, watoa huduma na wajasiliamali.

Maonesho ya Pili ya Biashara na teknolojia kwa Mkoa wa Shinyanga yanaongozwa na kaulimbiu Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu. Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021.

Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akizungumza leo Jumapili Julai 25,2021 wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akizungumza leo Jumapili Julai 25,2021 wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA) , John Bina akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Ally Hapi akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga , Zuwena Omary akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
 Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga, Donald Magesa akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
 Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
 Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Modest akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho, Dkt. Meshack Kulwa ambaye ni Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Burudani ikiendelea kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akitambulisha viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga kwa Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa pili kushoto).
Picha za kumbukumbu baada ya ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:

Share:

WAZALISHAJI WA POMBE KALI MAARUFU 'SHUJAA NA ZHIMWA' WASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA

Wafanyakazi wa Kampuni ya Canon General Supply iliyopo Mjini Shinyanga inayozalisha pombe kali maarufu kwa jina la Shujaa na Zhimwa, Clementina Mkongwa (kulia) na Amina Shamte wakionesha pombe kali wanazozalisha katika kiwanda hicho leo Jumapili Julai 25,2021 kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfanyakazi wa Kampuni ya Canon General Supply iliyopo Mjini Shinyanga inayozalisha pombe kali maarufu kwa jina la Shujaa na Zhimwa, Clementina Mkongwa akionesha pombe kali ya Zhimwa
Wafanyakazi wa Kampuni ya Canon General Supply iliyopo Mjini Shinyanga inayozalisha pombe kali maarufu kwa jina la Shujaa na Zhimwa, Clementina Mkongwa (kulia) na Amina Shamte wakiwa kwenye banda la Kampuni ya Canon General Supply kwenye kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa pombe kali za Shujaa na Zhimwa
Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya akizungumza leo Jumapili Julai 25,2021 wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger