Wednesday, 9 June 2021

CVAC Client Service Assistant at International Organization for Migration

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST DESCRIPTION   I. POSITION INFORMATION Vacancy Notice IOM/DAR/010/2021 Position title CVAC Client Service Assistant (Canada Visa Application Centre) Position grade G4-Graded Duty station Dar es Salaam Durations Six (6) Months Special Short-Term with possibility of extension Position number N/A Job family Core Migration/Administrative Organizational unit Operations Reporting Directly to VAC Team Leader 2nd Manager Operations Manager Overall […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Primary Health System Expansion Consultant at D-tree International

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Terms of Reference for Consultancy to Create Blueprints for a Digitalized Primary Health System with a Strengthened Connection to the Community Health Program A.    Summary These terms of reference provide the background to the recruitment of a consultant to provide technical leadership for developing a situational analysis and system blueprint for the expansion of client-centered, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

TASAC KUNUNUA BOTI KUZUIA VITENDO VYA UCHAFUZI WA MAZINGIRA BAHARINI

MENEJA wa Huduma za Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nelson Mlali akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga hivi karibuni wakati wa maonyesho ya biashara

MENEJA wa Huduma za Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nelson Mlali amesema shirika hilo lipo kwenye utaratibu wa manunuzi ya boti ambayo itapita maeneo mbalimbali kuelimisha jamii ikiwa ni mkakati wa kuzuia vitendo vya uchafuzi wa mazingira kwenye bahari.

Mlali aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kwenye maonyesho ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini hapa ambapo alisema kabla ya mwaka huu kwisha itapatikana ili waweze kushirikiana na taasisi nyengine.

Alisema taasisi ambazo watashirikiana nazo ni zile ambazo zinaangalia maeneo hayo kiusalama wa mazingira na pia kiusalama wa nchi kwa sababu bandari ni mipaka ya kimataifa.

Alisema kwa Tanzania uchafuzi wa mazingira kwenye pwani yao sio mkubwa kama zilivyo nchi nyengine huku akibaini changamoto zinazowakabili ni wananchi kutokufahamu shirika hilo na shughuli wanazofanya kwa sababu bado ni changa hivyo wapo kwenye utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi.

“Elimu hiyo itakuwa ni kuhusu biashara za kimataifa kupitia njia za maji zinazofanyika kwa hivyo tumekuwa tukifanya mikutano mbalimbali ya kuwapa uelewa mkubwa”Alisema

Hata hivyo alisema uingiaji wa meli nchini umeongezeka hasa kwa sababu ya madhara yaliyotokana na COVID 19 kwa nchi nyengine ambazo walikuwa wameweka vizuizi lakini kwa hapa nchini hatukujaweka na hivyo kuruhdu meli kuja kuleta shehena na kubadilisha mabaharia.

“Meli kutoka Dunia nzima zimekuwa zikiingia kwa mfano za mafuta zinazotoka ukanda wa Huba zinaleta mafuta ikiwemo Kuiwati,Saudi Arabia na nchi nyengine nyingi..,Meli za ngano kutoka Ulaya Mashariki na nyengine dunia nzima”Alisema Hata hivyo alitoa wito kwa wafanyabiashara wazingatia masuala ya usalama wanapotumia njia za usafiri wa majini na wanapopanda vyombo na wanaposafirisha mizigo huku akiwataka wamiliki wa vyombo wafuate utaratibu.
Share:

OFA! Viwanja vilivyopimwa vinauzwa Mbezi- Kwembe Kwa Bei Nzuri Kabisa


Ofa! Ofa! Viwanja vilivyopimwa vinauza Mbezi- Kwembe- Nyuma ya ofisi za halmashauri ya Ubungo, kituo cha Luguruni. Ukubwa ni kuanzia Sqm 400 Bei sqm 1 =17,500/= (7,000,000/=). Malipo ndani ya miezi sita. Kianzio 25% ya bei ya kiwanja. Eneo ni zuri lina Umeme, maji na kuna watu wa kutosha
0659 972868
0759 461893


Share:

Finance Manager at FHI 360

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

FHI 360 is a nonprofit human development organization dedicated to improving lives in lasting ways by advancing integrated, locally driven solutions. Our staff include experts in Health, Education, Nutrition, Environment, Economic Development, Civil Society, Gender, Youth, Research and Technology; creating a unique mix of capabilities to address today’s interrelated development challenges. FHI 360 serves more […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Program Manager at EngenderHealth

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Title:                       Program Manager Program                 EngenderHealth, Tanzania/ FCDO Program Reports to:             Project Director Duty Station:          Dar es Salaam   Company Summary: EngenderHealth envisions a gender-equal world where all people achieve their sexual and reproductive health and rights. We believe this is essential for ensuring all people can achieve their full potentials. To achieve this […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Resources Management Officer (P2) at IOM

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Position Title Resources Management Officer Duty Station : Kasulu, Tanzania, United Republic of Classification :Professional Staff, Grade P2 Type of Appointment : Fixed term, one year with possibility of extension Estimated Start Date : As soon as possible Closing Date : 20 June 2021 Established in 1951, IOM is a Related Organization of the United […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

MAMA AJIFUNGUA WATOTO 10 KWA MPIGO..AVUNJA REKODI YA DUNIA


Gosiame Thamara Sithole akiwa na mme wake
**
Mwanamke aitwayr Gosiame Thamara wa Afrika Kusini amejifungua watoto 10 kwa mpigo na kuvunja rekodi ya ulimwengu ambayo ilikuwa imewekwa na mwanamke kutoka Mali aliyepata watoto tisa miezi kadhaa iliyopita.

Gosiame Thamara Sithole mwenye umri wa miaka thelathini na saba alijifungua watoto hao kumi usiku wa Jumatatu, Juni 7,2021.

 Mama huyo alikuwa akitarajia kujifungua watoto wanane kutokana na uchunguzi wa ujauzito uliofanyika awali, lakini watoto wengine wawili walipatikana wakati wa kujifungua. Kulingana na ripoti ya Pretoria News na vituo vingine vya habari, Thamara alijifungua wavulana saba na wasichana watatu kupitia upasuaji katika hospitali ya Pretoria.

Sasa ni mama wa watoto 12 kwani tayari ana pacha wa miaka sita. Mumewe, Teboho Tsotetsi, alisema ujauzito wa Thamara ulikuwa wa asili kabisa kwani hakuwa kwenye matibabu yoyote ya uzazi. "Sasa tuna wavulana saba na wasichana watatu. 

Alizaa baada ya miezi saba na siku saba," baba huyo aliyejawa furaha alisema. 

Katika mahojiano mwezi mmoja uliopita kabla ya kujifungua, mama huyo ambaye sasa ana watoto 12 alisema kuwa alishtuka kubaini kuwa huenda akajaliwa watoto wengi kwa wakati mmoja.

Awali alikuwa akitarajia kujaliwa watoto wanane lakini wawili zaidi walipatikana wakati akijifungua.

Mumewe, ambaye kwa sasa hana ajira, alisema alikuwa na furaha ya kuwakaribisha watoto wake ulimwenguni. 

"Nilihisi kana kwamba nilikuwa mmoja wa watoto wa Mungu lakini bado sikuamini. 

Nina hamu sana kuwashika watoto wangu mikononi mwangu," alisema.

 Awali, iliripotiwa kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 25 nchini Mali alijifungua watoto tisa kwa mpigo ambapo anaingia katika vitabu vya historia kwahi kujifungua idadi ya watoto kama hiyo.

Wizara ya Afya katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilisema mwanamke huyo, Halima Cisse alitarajia kujifungua watoto saba, lakini uchunguzi wa ultrasound haukugundua watoto wengine wawili ndani ya tumbo lake.

Wizara ilifichua kuwa Cisse alijaliwa wasichana watano na wavulana wanne kwa njia ya upasuaji.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 9,2021



 












Share:

FAMILIA YA MUME WANGU MAREHEMU INANIFUATILIA KUNIPOKONYA URITHI WANGU WA MAMILIONI YA FEDHA

Share:

Tuesday, 8 June 2021

IGP Sirro atangaza operesheni ya mwezi mmoja kusaka wahalifu nchini.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro , ametangaza operesheni ya mwezi mmoja ya kusaka wahalifu nchini.

IGP Sirro ametangaza operesheni hiyo, akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polisi wa Mikoa ya Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo Jumanne, tarehe 8 Juni 2021, jijini humo.

IGP Sirro amesema, operesheni hiyo itaanza kesho Jumatano tarehe 8 Juni 2021.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi Tanzania, amewaonya watu wanaopanga kufanya uhalifu, waache mara moja, kwa kuwa jeshi hilo limejipanga kukabiliana nao kwa mujibu wa sheria.

“Kesho tunaanza operesheni ya mwezi mzima na hii operesheni ni ya nchi nzima. Jambo la msingi wale wahalifu waliotoka na kuanza uhalifu mbaya mbaya wasije kulalamika na sie tukiwafanyia mambo mabaya mabaya. Sisi tutafanya mambo mabaya kwa mujibu wa sheria,” amesema IGP Sirro.

Sirro ameongeza “suala la msingi waache uhalifu na kufanya kazi za uhalali, wakienda kinyume wasilaumu jeshi, wasilaumu Serikali.”

IGP Sirro amesema, operesheni hiyo itaenda sambamba na msako wa makosa ya usalama barabarani, ambapo ameagiza Makamanda wa Polisi wa Usalama Barabarani (Traffic) wa Mikoa, kusaka magari mabovu.

“Pia , nimeelekeza operesheni ya usalama barabarani, kuna makosa ya usalama barabarani yameanza kujitokeza kama mnaona, ajali zimetokea ajali. Operesheni dhidi ya magari mabovu itaanza kesho,” amesema IGP Sirro na kuongeza:

“Nawaambia makamanda na wakuu wa Traffic mikoa yote kufanya operesheni, dhidi ya magari mabovu ambayo hayatakiwi kuwa barabarani na wahakikishe wanakua wakali kusimamia sheria za usalama barabarani.”



Share:

Wasanii Wa Kizazi Kipya Kupamba UMISSETA, UMITASHUMTA


Na John Mapepele, Mtwara
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, taarabu na singeli ni miongoni mwa makundi ya wasanii watakaopamba Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA) yanayofunguliwa leo Juni 08, 2021 na Waziri Mkuu, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, amebainisha hayo alipofanya mahojiano na Vituo vya Redio mjini Mtwara leo ambapo amewataja wasanii wa kizazi kipya watakaopamba mashindano hayo kuwa ni pamoja na Ibrah kutoka Konde Gang, Beka Flavour, Peter Msechu na Linah Sanga, pia msanii maarufu wa Singeli Dulla Makabila na Mfalme wa taarabu Mzee Yusuf.

Amesema mashindano ya mwaka huu yanaanza leo na kumalizika Julai 3, mwaka huu, ambapo amesisitiza kuwa lengo la Serikali kwa sasa ni kuendelea kuboresha na kuongeza baadhi ya michezo ambayo itawasaidia kuweza wanafunzi wanapomaliza masomo yao kupata ajira.

“Tunakusudia kuangalia michezo inayoweza kumwandaa kijana kupata ajira baada ya kumaliza shule. Michezo ya maigizo ni miongoni mwa tasnia inakua kwa kasi kubwa hapa nchini ambayo kama mtoto akiandaliwa  vizuri anaweza kujiajiri” ameongeza Dkt. Abbasi

Amewataka wazazi kuondokana na fikra potofu ya kwamba michezo haina maana kwa kuwa kwa sasa michezo ni uchumi na ajira kubwa duniani.

Pia Dkt. Abbasi amesema katika mashindano ya sasa wamevialika vilabu, vyama, na mashirisho mbalimbali kuja kuona vipawa na vipaji vya wanamichezo hawa chipukizi

Mashindano hayo yatafanyika katika Viwanja vya Nangwanda Sijaona, Chuo cha Walimu Mtwara (TTC kawaida), Chuo cha Walimu ufundi Mtwara Ufundi Mtwara na katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara maarufu Mwasandube.


Share:

Alichokisema Rais Samia maiti kuzuiwa mochwari kisa deni la matibabu


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri wa Afya,  Dk Dorothy Gwajima kuweka mpango mzuri wa ndugu kulipa deni la hospitali ili ikitokea  mgonjwa wao amefariki dunia wakati akitibiwa, maiti isizuiwe.

Amesema utaratibu wa sasa ambao umekuwa ukizuia kutoa maiti hospitalini kwa kigezo cha kulipa gharama za matibabu kabla ya kifo si mzuri.

Rais Samià Suluhu Hassan ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati wa mkutamo wake na Wanawake wa Tanzania kupitia Wanawake wa mkoa wa Dodoma.

Amesema ni vema wakati wa matibabu ndugu wa mgonjwa ama mgonjwa mwenyewe akawa anapatiwa gharama za matibabu za kila siku, badala ya kusubiri hadi kifo kinapotokea, na hivyo kuleta usumbufu.



Share:

Watanzania wawe waangalifu na Dawa za Antibiotiki- TMDA


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Nchini (TMDA), Bw. Adam Fimbo ameitaka Jamii kuwa watambuzi kwenye kuzingatia dawa halisi ama bandia kwa dawa za Antibiotiki hasa matokeo ya dawa hizo wanazotumia kuwa na viashiria ikiwemo harufu kwa mkojo.

Fimbo amesema hayo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku Nne (4) kwa Wakaguzi 59 wapya kutoka Kanda Nane (8) za Mamlaka hiyo yanayofanyika mjini hapa, Kibaha Mkoani Pwani alisema

Ambapo alibainisha kuwa TMDA wanakuwa na utaratibu wa mafunzo hayo mara kwa mara ilikuwajengea uwezo wakaguzi ilikuzuia mianya ya kuingiza dawq bandia ama zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu.

Ametoa rai kwa jamii kutambua dawa zote za Antibiotic endapo watazitumia lazima ile harufu ya dawa hiyo baada ya kutumia itatoa harufu katika mkojo wa mtumiaji.

“Kama hutasikia harufu katika dawa hiyo ujue hakuna dawa humo.” Alisema Fimbo kwa kusisitiza jamii kutambua hilo.

Pia ameongeza kuwa, kwa upande wa dawa za wajawazito za kuongeza damu za Iron (foric acid) , lazima baada ya kutumia dawa hizo kinyesi chake kiwe cheusi kuashiria ni dawa sahihi.

“Kinyesi kisipokuwa cheusi ujue hamna dawa humo ndani ya hiyo dawa. Kila dawa inamatokeo yake baada ya kutumia lakini isipotoa matokeo husika ujue dawa hiyo ni bandia hivyo inatakiwa hatua kuchukuliwa haraka”. Alisema Fimbo.

Aidha aliongeza kuwa, dawa zote zilizosajiliwa ama zilizokaguliwa na TMDA zinatakiwa kuwa na namba za TMDA za usajiri ili kuwahakikishia watumiaji ubora na viwango vilivyokusudiwa katika matumizi hata hivyo mtumiaji lazima achukue taadhari ya dawa anayotumia kama ni sahihi au ni bandia.

Fimbo alisema mwananchi akague nembo maalumu ya usajiri kutoka TMDA katika kila dawa anayonunua ilikujiridhisha kama ni salama ili kuepuka kutumia dawa bandia na kupata madhara.

“Dawa zilizosajiliwa na TMDA zina nembo inayoanzia na TZ na nembo ya dawa inayoanzia na TZA ambapo kila unapoangalia lebo ya dawa utaona namba hizo ambazo zitakuhakikishia kwamba dawa hiyo imesajiliwa na TMDA”. Alisema Fimbo.

Aliongeza kuwa: Dawa inapaswa ikuponye na iwapo unatumia dawa kwa muda ulioandikiwa lakini hukupona hiyo ni dawa bandia.

Katika mafunzo hayo, pia amewataka Wakaguzi hao wapya kujiadhari na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa kwani mamlaka hiyo imekuwa ikisimamia haki katika kulinda afya za jamii hivyo hakuna kupokea wala kutoa rushwa.

“Sekta ya dawa inavishawishi vikubwa kwa wadau wake ikiwemo vitendo vya rushwa kwakuwa nyinyi ni Wakaguzi wapya muende mkazingatie maadili ya utumishi ikiwemo kuepuka vitendo vya rushwa.

“Mkiruhusu dawa kwa vitendo vya rushwa tutabaini tu kwani matumizi ya dawa yanachukua muda mrefu na bahati nzuri wafanyabiashara ukiwabana wanataja, sasa mzingatie maadili ya nchi nyinyi ni muhimu sana kulikokupitisha dawa bandia itasababisha madhara makubwa kwa jamii na kutia aibu kwa taifa”. Alimalizia Fimbo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TMDA, anayeshughulikia dawa na vifaa tiba Dkt. Yonah Mwalwisi amesema mamlaka hiyo inatumia mbinu na mifumo mbali mbali inayosaidia ya kudhibiti ubora katika soko la nchi kwa kuhakikisha linapata vitendanishi na vifaa vyenye ubora, salama na vyenye ufanisi unaotakiwa.

“TMDA tunatumia mifumo ya kisasa ya kielectroniki ambayo hutumika kuthibiti wakati wa kuingiza vifaa tiba au vitendanishi nchini kwa mteja wa bidhaa husika kutoka taifa analotaka kisha hukaguliwa kwa lengo la kujiridhisha ubora wa kifaa husika.” Alisema Mwalwisi.

Mafunzo hayo ya siku Nne, yameanza leo ambapo wakaguzi hao watapatiwa mafunzo ya nadharia na kwa vitendo na yanatarajiwa kufungwa 10 Juni mwaka huu.

TMDA imeandaa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani [WHO] amabapo mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na kila mwaka kwa wakaguzi na maafisa wa TMDA.


Share:

Serikali Kutangaza Zabuni Ya Kupeleka Mawasiliano Maeneo Ya Mipakani


Na Faraja Mpina, Dodoma
Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatarajia kutangaza zabuni ya awamu ya sita yenye lengo la kupeleka mawasiliano katika kata 179 zenye vijiji 358 mradi unaolenga kupunguza changamoto ya mawasiliano kwa wananchi waishio mipakani.

Akizungumza katika kikao chake na watendaji wakuu wa makampuni ya simu kilichofanyika  jijini Dodoma tarehe 07/6/2021 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema Mfuko huo utatangaza zabuni hizo mwezi huu kwa lengo la kuendelea kuboresha huduma za mawasiliano nchini

“Kama Serikali tumejielekeza katika kuboresha mawasiliano ya mipakani ambayo yanakuwa na mwingiliano na nchi za jirani, makampuni ya simu mkiwa kama wadau wa Sekta hii tunaomba mtoe ushirikiano kwa Serikali ili wananchi waishio mipakani wapate mawasiliano ya uhakika ya ndani ya nchi”, alisema Dkt. Ndugulile

Katika hatua nyingine Dkt. Ndugulile ametoa rai kwa watendaji hao kufanya maboresho ya utoaji wa huduma za mawasiliano kwa kufanyia kazi maeneo ambayo wananchi wanayalalamikia ikiwa ni pamoja na kuhakiki namba zilizosajiliwa kwa alama za vidole na kuimarisha mifumo ya usajili wa laini za simu pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa umma ili kupunguza utapeli kwa njia ya simu za mkononi.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mhandisi Kundo Mathew amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na watoa huduma pamoja na watumiaji wa huduma za mawasiliano ili kuweza kutambua mahitaji halisi na changamoto zilizopo katika sekta hiyo na kuzitatua kwa lengo la kuendelea kuboresha Sekta hiyo muhimu nchini kwa kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za mawasiliano popote alipo.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba  amesema kuwa lengo la Mfuko huo ni kupeleka mawasiliano kwa wote na zabuni zitakazotangazwa mwezi huu ni kwa ajili ya kupeleka mawasiliano katika maeneo ya mipakani na kuyaomba makampuni ya simu kuchukulia zabuni hizo kwa uzito stahiki pindi zitakapotangazwa.


Share:

Serikali Yasisitiza Miongozo Ya Ya Kujikinga Na Corona Izingatiwe


Na.Catherine Sungura,Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesisitiza miongozo yote iliyotolewa kwa umma kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya CORONA (COVID – 19), izingatiwe.

Mkurugenzi wa Idara ya Kinga wa Wizara hiyo, Dkt. Leonard Subi amesema Tanzania ni salama hata hivyo kwa kuwa bado kuna tishio la maambukizi ya Virusi hivyo duniani, ni muhimu kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga.

Dkt. Subi amesema hayo leo alipohojiwa na moja ya chombo Cha habari jijini Dodoma ni hatua gani Tanzania inaendelea kuzichukua kuhakikisha jamii inakingwa dhidi ya wimbi jipya la maambukizi ya COVID – 19.

“Tanzania tupo salama lakini tunatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi hayo ambayo kwa takriban mwaka na nusu sasa bado yanaikabili dunia.

“Wizara kazi yetu ni kuendelea kihimiza wananchi kujikinga dhidi ya COVID – 19, tuendelee kuchukua tahadhari, tuliona katika wimbi la kwanza 2020 wananchi waliitika wito wa kunawa mikono, kuvaa barakoa, kukaa umbali, kufanya mazoezi, lishe bora na masuala mengineyo,” amesema.

Ameongeza “Tunataka kusisitiza kinachotokea Afrika maambukizi yanaongezeka na baadhi ya Wakuu wa Nchi wanatoa matamko kama tulivyomsikia Rais wa Uganda na sisi Tanzania tumekuwa na mwingiliano na uhusiano mwema na nchi jirani.

“Watanzania kinga ni bora kuliko tiba tusije tukasubiri kuingia kwenye mitungi ya oksijeni, tuendelee kujikinga. Hali ni shwari hata Rais Samia Suluhu Hassan anachukua tahadhari kujikinga na maambukizi akikutana na watu mbalimbali,” amesema.

Amesisitiza “Mashuleni, vituo vya afya tuliweka vifaa kwa kunawa kwa maji safi tiririka, tunawe mikono.

Akitolea mfano wa Ma-benki kwenye ‘ATM’ waliweka vipukusi ‘sanitizers’, Ila Kwenye ATMs sasa hivi havipo na watu wanashika wanabonyeza bonyeza pale inaweza kuwa chanzo cha maambukizi.Alizitaka benki zote wahakikishe wanarejesha vitakasa mikono na kuwapa siku tatu.

“Hatua tulizopiga tusije tukarudi tulipotoka, sisi Serikali tunaendelea kufuatilia kwenye mikusanyiko, mabasi, ndege wachukue tahadhari.

Amesema Serikali imeimarisha hatua za ufuatiliaji kwenye maeneo ya mipaka, viwanja vya ndege watu wanapimwa hali zao za afya.

“Tunafahamu kuna tishio kubwa la anuwai mpya (aina mpya ya kirusi cha CORONA) duniani, kuna cha India, Uingereza, Afrika Kusini na Brazil ambavyo vimeendelea kugharimu maisha ya watu.

“Tunashirikiana na Mamlaka za mikoa, Serikali za Mitaa kuhakikisha tunaendelea kuwafikia wananchi,” amesema.

Dk. Subi pia ametoa rai kwa vyombo vya habari kuendelea kuelimisha jamii na kuihamaisha kujikinga dhidi ya maradhi hayo.

“Tunaomba vyombo vya habari mtumie muda wenu kidogo hata mara moja au mbili kwa siku kuwakumbusha wananchi kuchukua tahadhari juu ya COVID – 19.

“Suala la mapambano dhidi ya magonjwa si la hiyari, tuna maafisa afya pia, Watanzania suala la afya ni la muhimu na la msingi kwa Maendeleo ya Taifa tukicheza tutarudi nyuma, kila mmoja atimize wajibu wake.

“Kwenye familia ndoo za kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni ziwepo, bebeni vipukusi na katika maeneo ya mikusanyiko tunashauri barakoa zivaliwe kwa kuzingatia mwongozo tuliotoa na kwenye nyumba, magari kuwe na mzunguko wa hewa, tujikinge,” ametoa rai Dk. Subi.


Share:

Wizara Ya Ardhi,TAA,TCAA Na Mipango Miji Dodoma Kuondoa Kero Za Ardhi


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), na Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, imekubaliana kuja na mwarubaini wa kuondoa kero za matumizi ya ardhi kwa wakazi na wawekezaji wanaojenga maeneo karibu na viwanja vya ndege nchini.

Kauli hizo zimezungumzwa hivi karibuni na wadau mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma walioshiriki kwenye warsha ya siku moja ya mipango endelevu ya matumizi bora ya ardhi yanayoenda sambamba na uendeshaji wa viwanja vya ndege nchini, iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Mazingira cha TAA, Maxmilian Mahangila amesema warsha hiyo inalengo la kuweka sheria sawa kati ya sheria za ardhi, mipango miji pamoja na sheria za masuala ya usalama wa anga, ambapo zimekuwa zikitofautiana kutoka kwenye taasisi moja na kwenda nyingine.

“Ukiangalia hizi sheria zimekuwa zikisigana bila kujua, ambapo ukiangalia sheria zilizowekwa za masuala ya anga zinakataza ujenzi wa majengo marefu, minara na makazi karibu na viwanja vya ndege, lakini sheria za ardhi na hata mipango jiji zinaruhusu ujenzi wa aina yeyote katika maeneo hayo, ambapo hutoa kibali kwa wazawa au wawekezaji kujenga bila tatizo,” amesema.

Hatahivyo, amesema wadau mbalimbali wametoa ushauri juu ya matumizi ya sheria hizo ili ziwe na mtazamo mmoja, ukizingatia sheria na kanuni za masuala ya anga ili kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa kwa kutokuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi.   

Warsha hiyo ilikuwa na mada tatu, ambazo ni “Mipango ya Matumizi ya ardhi yanayoenda sambamba na uchafuzi wa mazingira” iliyowasilishwa na Joyce Kasebele, Afisa Mazingira wa TAA, ambapo amezungumzia mazao yanayoweza kulimwa maeneo yanayozunguka viwanja vya ndege, ambayo hayavutii ndege hai.

Pia amezungumzia  jinsi wananchi wanaoishi maeneo ya kuzunguka viwanja hivyo kuhakikisha wanayaweka katika hali ya usafi, ili kuepusha wanyama na ndege hai kuingia na kufanya madhara kwenye ndege za abiria na mali nyingine.

Naye Meneja wa TCAA wa mkoa wa Dodoma, Ludovic Ndumbaro aliyewasilisha mada ya “Sheria na kanuni za masuala ya anga kuhusiana na matumizi ya ardhi yanayozunguka viwanja vya ndege nchini”.

“Majengo marefu ni hatarishi karibu na viwanja vya ndege, na kila anayejenga maeneo hayo lazima apate kibali maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, baada ya kujiridhisha kama halina madhara ataruhusiwa lakini yale yenye madhara hayawezi kuruhusiwa kwani yanaweza kuzuia ndege wakati wa kupaa na kutua,” amesema Ndumbaro.

Halikadhalika Afisa Mipango Miji Mwandamizi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Edward Mpanda aliyewasilisha mada ya “Mpango wa matumizi ya Ardhi” amesema ndani ya wizara na katika ngazi za wilaya mipango ya matumizi ya ardhi yamezingatia maeneo ya viwanja vya ndege.

“Pamoja na kwamba hizi sheria na mipango ipo wazi kuanzia ngazi ya wilaya na wizarani, lakini imeshughudiwa baadhi ya viwanja vya ndege vimekuwa sio salama kutokana na matumizi mabaya ya ardhi kutoka kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo kuhakikisha majengo yao yanakuwa na urefu wa kawaida ili kuondoa vizuizi vya wakati wa kutua na kuruka kwa ndege,” amesema Mpanda.

Naye Mpima Ardhi Jiji la Dodoma, Hudson Magomba amesema kwa upande wa mpango jiji kumekuwa na mpango wa muda mrefu kuhusuana na  viwanja vya ndege wa mwaka 2010 na baadae kufanyiwa maboresho mwaka 2019-2039.

Hatahivyo, amewataka wananchi kufuata taratibu za ujenzi na kujenga maeneo yaliyopimwa na serikali, na wasivamie maeneo ya viwanja vya ndege kwani ni hatarishi kwa maisha yao.

MWISHO


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger