Wednesday, 2 June 2021

Tangazo La Nafasi Za Masomo shule ya Lake Tanganyika


Uongozi wa shule ya Lake Tanganyika iliyopo Kigoma katika kijiji cha Mkigo inapenda kuwatangazia nafasi za masomo kwa kidato cha tano kwa tahasusi za HGK,HKLna HGK


Pia shule inawatangazia nafasi za kuhamia kidato cha sita kwa tahasusi tajwa hapo juu,kidato cha tatu na kwanza 


Shule inafanya vizuri sana katika mitihani ya kitaifa.Shule ni ya bweni tu na ni mchanganyiko wavulana na wasichana .Shule ina mazingira mazuri na walimu wa kutosha


Ada zetu ni nafuu sana na zinalipwa kwa awamu nne kwa mwaka na ni kama ifuatavyo;
Kidato cha kwanza hadi nne karo ni laki saba na elfu hamsini tu mwaka,na kidato tano na sita karo ni laki nane tu mwaka na na kwa wanafunzi wote wana michango ya shiling laki na hamsini kwa mwaka


Shule inapatikana 40km kutoka kigoma mjini na 50km kutokea kasulu kuelekea manyovu


Kwa mawasiliano zaidi fika shuleni au piga namba zifuatazo
0769697667,0763091810,0745907094,0713221620,

0627557839



Share:

NHIF TANGA YAENDELEA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO HUO

 

MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (MB) wakati alipotembelea Banda lao lililopo kwenye maonyesho ya Biashara ya 8 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akimsikiliza kwa umakini Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (MB) wakati alipotembelea Banda lao lililopo kwenye maonyesho ya Biashara ya 8 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani namna walivyojipanga kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na bima ya Afya

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa mfuko huo kwenye banda lao kulia ni Afisa Matekelezo wa NHIF mkoa wa Tanga Macrina Clemence


NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu amewahamasisha wakazi wa mkoa huo kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfuko huo ili kuweza kujihakikishia kupata huduma za matibabu wanapoungua na hivyo kuwaondolea wasiwasi akiugua itakuwaje.

Mwakababu aliyasema hayo wakati akiwa eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya nane ya Biashara ambapo alisema kuwa na kadi ya bima ni kuwa na daktari hivyo inakusaidia kukuondolea wasiwasi pindi unapougua huku ukiwa hauna fedha.

Alisema hivyo wananchi wanapaswa kutambua umuhimu wa kujiunga na mfuko huo na kuweza kunufaika na huduma mbalimbali za kimatibabu pindi wanapougua

Meneja huyo alisema wameshiriki kwenye maonyesho hayo ya biashara ya TCCIA kwao wanaamini bima ya afya kwa wote serikali ya awamu ya sita inapambana kuhakikisha watu wanajiunga na bima ya afa badala ya kusubiri kupata matibabu kulipia.

“Kwa hiyo ndio maana tupo hapa kutoa elimu kwa wanachama na ushauri wa afya zao kwa kupima uzito,presha,sukari na kushauri mwenendo mzuri wa kula na kuwaeleza umuhumi wa kujiunga na bima”Alisema

Alisema pia ikiwemo Toto Afya Kadi na makundi mbalimbali ambayo serikali imeyaweka kwenye mpango ambao ni wakulima kupitia Amcos zao,waandishi wa habari katika eneo lao walipe laki moja,makundi ya wavuvi,warina asali na watu binafasi wa na vifurushi mbalimbali ikiwemo najali,timiza.

Hata hivyo aliwaomba wananchi wajiunge na wafike na kuchangmkia fursa za kujiunga na mfuko huo kwani kuwa na kadi ya bima inakuhakikishia kupata matibabu .


Share:

CUSTOMS ASSISTANT II – 7 POST at TRA

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST CUSTOMS ASSISTANT II – 7 POST POST CATEGORY(S) ACCOUNTING AND AUDITING HR & ADMINISTRATION LEGAL TAXATION AND SOCIAL PROTECTION EMPLOYER Tanzania Revenue Authority (TRA) APPLICATION TIMELINE: 2021-06-01 2021-06-14 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To receive documents from Wharf, retain copies of the same. ii. To receive requests for scanning from Importer/Clearing Agents. […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

PERSONAL SECRETARY II – 3 POST at TRA

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST PERSONAL SECRETARY II – 3 POST POST CATEGORY(S) HR & ADMINISTRATION IT AND TELECOMS EMPLOYER Tanzania Revenue Authority (TRA) APPLICATION TIMELINE: 2021-06-01 2021-06-14 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To receive, interview and direct visitors accordingly. ii. To prepare letters and various documents. iii. To handle confidential and sensitive information. iv. To ensure […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 2,2021



















Share:

Tuesday, 1 June 2021

NGARIBA NGULI ATUPWA JELA MITANO TENA GEREZANI SERENGETI

Ngariba nguli Mary Onyango Omega (50) maarufu Mkungu Mugesi mkazi wa kijiji cha Kitarungu Kata ya Nyansurura amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara miaka 5 jela kwa kosa la kumfanyia ukatili mtoto (ukeketaji).

Adhabu hiyo ni ya pili kutolewa na Mahakama tofauti ambapo Aprili 28,2021 katika kesi ya Jinai 151/2020 yeye na mzazi wa mtoto aliyefanyiwa ukatili mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Ismael Ngaile walihukumiwa kifungo cha miaka 5 au kulipa faini ya sh500,000 na kumlipa fidia ya sh1,000,000 mtoto aliyefanyiwa ukeketaji,alitoka gerezani baada ya kulipa.

Katika kesi ya Jinai namba 157/2020 mbele ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Serengeti Judith Semkiwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela bila faini kwa kosa la kumfanyia ukatili(ukeketaji)mtoto mwingine tofauti na kesi ya awali ,hata hivyo ngariba huyo hakuwepo mahakamani wakati adhabu hiyo inasomwa.

Mwendesha mashitaka wa Jamhuri Faru Mayengela amesema mshitakiwa alikamatwa aprili 11,2020 katika kijiji cha Kitarungu akikabiliwa na makosa ya kuwafanyia watoto ukatili,ambao katika gwaride maalum la utambuzi walimtambua bila mashaka yoyote.

Chanzo - Serengeti Media Centre

Share:

SINGIDA WAANZA KUKUSANYA MAPATO YA MAEGESHO KWA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI


Mkuu wa Mkoa wa Singida Binilith Mahenge akizungumza  kabla ya kuzindua  Mfumo mpya  wa kielektoniki wa ukusanyaji mapato kupitia maegesho ya vyombo vya moto.

 Na Edina Alex, Singida.

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amezindua  mfumo mpya wa kielektroniki ujulikanao kama "TARURA e-REVENUE MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM" kwa ajili ukusanyaji mapato  ya maegesho ya vyombo vya moto mkoani Singida.

Dkt. Binilith amezindua mfumo huo leo wakati akifungua kikao cha kuwajengea uwezo  viongozi juu ya matumizi ya mfumo huo wa ukusanyaji mapato ya maegesho ya vyombo vya moto, matumizi ya hifadhi za barabara pamoja na tozo za adhabu kutokana na ukiukwaji wa matumizi ya hifadhi za barabara yanayosimamiwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA).

Alisema kuanzishwa mfumo huo utaenda kuleta  ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya serikali  yatakayosaidia  maboresho  na maendeleo ya miundombinu ya barabara,kupunguza kero ya kudaiwa  ushuru kwa kuwa mtumiaji atalipa  kwa kutumia simu ya mkononi ,wakala  ama matawi ya benki ya NMB na CRDB.

"Binafsi naona mfumo huu utaleta tija kubwa  katika ukusanyaji wa mapato ya serikali na utoaji huduma kwa  wananchi", alisema Dkt. Mahenge.

Aidha Dkt. Mahenge  aliutaka wakala huo kuhakikisha  elimu ya mfumo huo inafikishwa kikamilifu kwa wananchi ili wote wawe na uelewa wa pamoja  na kuepusha malalamiko kwa watumiaji.

Alitoa wito pia kwa  wananchi kuyapokea mabadiliko hayo na kulipa wao wenyewe ushuru wa maegesho ili kuepuka tozo ama faini zisizo za lazima.

Akifafanua namna ya ufanyaji  kazi wa mfumo huo  Mhasibu kitengo Cha mapato TARURA makao makuu, Osward Mobily alisema mteja anaweza kulipia ushuru wa maegesho kwa saa ,siku,wiki au mwezi. Pia  mteja anaweza kuomba mwenyewe kumbukumbu namba  ya malipo kwa ajili ya kufanya malipo ya kabla ya ushuru wa maegesho kwa kupiga *152*00#.

Singida ni mkoa wa pili kuzindua mfumo huu ukitanguliwa na Mkoa wa Iringa, ambapo imeelezwa kuwa kama utasimamiwa na kutumika vizuri utaleta tija kwa ustawi wa miundombinu ya barabara zinazozunguka mkoani Singida.
Mtaalamu wa Kitengo cha mapato kutoka TARURA Makao Makuu Osward Mobily akifafanua jinsi ya kufanya malipo kwa mfumowa TeMIS. Picha zote na Edina Alex
Mratibu wa TARURA Mkoa wa Singida William Boniphance akizungumza kwenye uzinduzi huo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kyaratu akichangia hoja ukumbini
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM)Mkoa wa Singida Lucy Shee  akichangia hoja kwa ajili ya maboresho ya mfumo huo.
Mrakibu wa Polisi (SP) Nyangi Choma akichangia.
Mchambuzi wa Mifumo kutoka Makao Makuu ya TARURA, Joseph Chigalula akieleza jinsi ya kufanya malipo ya ushuru wa maegesho kwa kutumia mfumo huo mpya.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida Alhaj Juma Kilimba akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkutano ukiendelea.

Share:

WANAFUNZI 148,127 WAMECHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI, KATI 2021…TAZAMA MAJINA HAPA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu,akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza  majina ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha tano 2021 Vyuo vya Kati na Ufundi leo June 1,2021 jijini Dodoma.

Na Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu,amesema kuwa Jumla  ya Wanafunzi 148,127 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2021,ambapo wasichana 63,878 na wavulana 84249 ya wanafunzi waliofanya mtihani kidato cha nne mwaka 2020.

Hayo ameyasema leo June ,1,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari  pamoja  maafisa  elimu mkoa kwa njia  ya mtandao ,Mhe.Ummy amesema kuwa  hiyo ni baada ya kufanya uchambuzi na kuona kuwa wamekidhi vigezo.

Aidha ameainisha tahasusi za masomo kwa wanafunzi  waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano ambapo wanafunzi   41,504 watajiunga kusoma tahasusi za Hisabati na Sayansi na wanafunzi 46,159 watasoma tahasusi za masomo ya sanaa na biashara.

“Muhula wa kwanza wa masomo utaanza Mwezi Julai 5,2021 na atakayechelewa kuripoti watapangiwa wanafunzi wengine”amesema Mhe.Ummy

Matokeo ya Kidato cha Nne 2020 yanaonesha kuwa Watahiniwa wa Shule waliopata Daraja la I – III walikuwa 153,464 wakiwemo wasichana 67,135 na wavulana 86,329 sawa na asilimia 35.06 ya watahiniwa waliofanya mtihani.

“Watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani wakiwa chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) waliofaulu kwa Daraja la I – III ni 479 wakiwemo wasichana 289 na wavulana 190”amesema 

 Idadi hiyo ya wanafunzi wenye sifa imejumuisha wanafunzi wenye Mahitaji Maalum 288 wakiwemo Wasichana 123 na Wavulana 165.

Aidha, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani wakiwa chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ni 287 wakiwemo wasichana 149 na wavulana 138.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwaka 2021, ni kutoka Shule za Serikali, zisizo za Serikali, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani wakiwa chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na waliosoma nje ya nchi ambao matokeo yao yamefanyiwa ulinganifu wa Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA).

Jumla ya wanafunzi 87,663 wakiwemo wasichana 41,885 na wavulana 45,778 sawa na asilimia 59.18 ya wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule 476 za Serikali zikiwemo shule mpya 42, Kati yao wanafunzi wenye mahitaji maalumu walikuwa 288 wakiwemo wasichana 123 na wavulana 165 sawa na asilimia 100% ya wenye Mahitaji Maalum waliokuwa na sifa za kujiunga na Kidato cha Tano.

Wanafunzi 1,598 wakiwemo wasichana 592 na wavulana 1,006 wamechaguliwa kujiunga na fani mbalimbali katika Vyuo vinne vya Ufundi ambavyo ni Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji (WDMI) na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Jumla ya wanafunzi 55,308 wakiwemo wasichana 21,401 na wavulana 33,907 wamechaguliwa kujiunga kwenye kozi mbalimbali za ngazi ya Astashahada na Stashahada (Certificate and Ordinary Diploma) katika Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo Wanafunzi 2,235 wakiwemo wasichana 1,162 na wavulana 1,073 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Afya ngazi ya Stashahada.

Waziri Ummy amesema  kuwa wanafunzi 5,757 wakiwemo wasichana 2,798 na wavulana 2,959 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Ualimu ngazi ya Astashahada ya Elimu Maalum, Awali, Michezo, Msingi na Ualimu wa Shule zinazofundisha kwa kutumia Lugha ya Kiingereza (English Medium).

“ Wanafunzi 1,709 wakiwemo wasichana 737 na wavulana 972 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Ualimu ngazi ya Stashahada ya Sayansi, Hesabu na TEHAMA. Vilevile, Wanafunzi 45,607 wakiwemo wasichana 16,704 na wavulana 28,903 wamechaguliwa kujiunga naVyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika Kada mbalimbali.

Waziri Ummy alisema Serikali ya Awamu ya Sita ingependa kuona wanafunzi wote waliochaguliwa kwenda Kidato cha Tano wanajiunga kwa pamoja ndani ya muda uliopangwa.

“Serikali inawahimiza Wanafunzi ambao wameshakata shauri kujiunga na shule za Binafsi kuthibhibitisha kujiunga na shule hizo kupitia mfumo wa “Selform” uliotumika wakati wa kubadilisha tahasusi”amesema .

 Aidha Mhe.Ummy amewataka  wakuu wa shule za Binafsi ambazo wanafunzi watadhibitisha kujiunga nazo, watatakiwa kuthibitisha kuwatambua wanafunzi hao kupitia mfumo wa “Selform”.

Nafasi zitakazopatikana kwa njia hii zitajazwa na wanafunzi kwenye “Second Selection” ili nao waweze kujiunga na shule kwa muda sawa na wenzao.

Fomu za maelezo ya mahitaji ya kujiunga na Kidato cha Tano (Joining Instructions)
kwa shule zote za Kidato cha Tano zinapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI
kupitia kiunganishi cha www.tamisemi.go.tz. Vilevile, mfumo wa Selform unaendelea kupatikana kupitia anuani ya selform.tamisemi.go.tz.

Amesema  kuwa kwa wanafunzi waliopangwa kwenye Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wanapaswa kuthibitisha kukubali kujiunga na kozi walizochaguliwa kuanzia tarehe ya leo hadi ifikapo tarehe 8 Agosti, 2021.

Wanafunzi hawa watatakiwa kufanya Uthibitisho kuwa wamekubali Kozi na Vyuo walivyopangiwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ambayo ni www.nacte.go.tz kupitia kiunganishi kinachoitwa Uthibitisho TAMISEMI.

Kwa mwanafunzi atakayetaka kufanya mabadiliko ya kozi na chuo alichopangiwa ataruhusiwa kufanya hivyo kuanzia tarehe 9 – 23 Agosti, 2021 kupitia tovuti ya
NACTE ya www.nacte.go.tz.

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mwaka, 2021 inapatikana kwenye tovuti ya OR- TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ya www.nacte.go.tz.

Kwa upande wake Naibu katibu mkuu TAMISEMI Gerlad Mweli alisema zaidi ya shule mpya 10 zimeongezeka hali  iliyowezesha wasichana wote kuchaguliwa kuendelea na masomo kidato cha tano



Share:

WAKWAPUA POCHI WANASWA MOROGORO



Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu
***
Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia vijana 34 kwa tuhuma za wizi wa kukwapua mali za wananchi kwa kutumia pikipiki ambapo jumla ya pikipiki nane zinashikiliwa na jeshi hilo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu, amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika maeneo ya Mtawala, Kidabaga, Mwembesongo na Mji Mpya Manispaa ya Morogoro, ambapo inadaiwa hutumia njia ya kupakizana vijana wawili kwenye pikipiki hizo na kuvizia watembea kwa miguu wanaoongea na simu au walioshika mikoba na kuikwapua.

Katika hatua nyingine SACP Musilimu, amesema jeshi hilo linawashikilia watu watatu kwa tuhuma ya wizi wa vifaa vya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR ikiwemo vipande vya nyaya za shaba mpya na zilizounguzwa huku nyingine zikiwa zimefumuliwa kwenye 'transfomer' zenye jumla ya uzito wa kilogramu77.9 zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala la mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina moja la Ahmed lililopo mtaa wa Modeco Manispaa ya Morogoro.

Chanzo- EATV
Share:

SMART AFRICA GROUP – KAMPUNI INAYOCHOCHEA MAPINDUZI YA KIDIGITALI, MEDIA NA UBUNIFU

Mkurugenzi Wa SAG Bw. Edwin Bruno (mwenye Suti) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara
Smartcodes imezindua kampuni yake mama, Smart Africa Group (SAG) ambayo itakuwa inasimamia idara zake 5 ambazo kwa sasa zimesajiliwa kama kampuni huru na zinakuwa kampuni tanzu.

 Kwa miaka mingi, Smart Codes imekua kutoka kuwa kampuni inayojihusisha zaidi na masuala ya kiteknolojia mpaka ile inayotoa huduma mbalimbali kwenye masoko, teknolojia na ubunifu.

 Sababu kubwa ya kufanya hivi ni kuwa na mhimili madhubuti utakaowezesha mgawanyo wa huduma kulingana na kampuni hizi tanzu 5.

Smart Codes ilianzishwa mwaka 2010 na Ndg. Edwin Bruno. Kampuni ilisajiliwa mwaka 2014 kama kampuni yenye kikomo na kila siku inazidi kukua. Katika muda wote huu, lengo kubwa la kampuni limekuwa ni kuleta mabadiliko ya kidigitali kwa wateja na washirika wetu.

 Hiki hakitabadilika kwa sababu kampuni ina matarajio ya kufanya makubwa zaidi katika mwongozo huu.

“Kuanzishwa kwa SAG kunawezesha kampuni kusimamia ukuaji na kuongeza Imani kwa wateja wetu. Kazi kubwa ya SAG ni kushauri, kuongoza na kuweka dira. Itasimamia utendaji na kuwa maono ya pamoja miongoni mwa kampuni tanzu ili kusaidia kulinda matarajio ya wateja, na pia kuhakikisha kwamba kila kampuni tanzu inaendelea kukua katika kiwango kilichowekwa na Smart Codes hapo kabla. Kwa kuunda SAG, tunawahakikishia washirika wetu kwamba tuna timu bora, mbinu sahihi na taratibu zenye umakini” alisema Ndg. Edwin Bruno, CEO na CVO wa SAG.

Kampuni hizi tanzu 5 zinajumuisha; Smart Codes ambayo inatoa huduma za matagazo na masoko zilizo kamilifu zinazojumuisha upangaji mbinu,huduma za kidigitali, ubunifu, media,shughuli/hafla, hamasa za hadhara na uhusiano kwa umma; Smart lab itaendelea kuwa maabara ya uvumbuzi na kuchochea ubunifu ikihusiana na programu, ujuzi, vipaji na maabara za kuchochea ubunifu; Smart Foundry inahusiana na uundaji wa bidhaa kuanzia utengenezaji wa mbinu, ubunifu, maendeleo na usimamizi; Smart Nology inahusika zaidi na teknolijia katika huduma zetu wenyewe kwa kutoa nyenzo za kutengenezea tovuti, njia za malipo, aplikesheni za simu mpaka kwenye uundaji wa aplikesheni za bahati nasibu; na Smart Studio inatoa huduma za utengenezaji picha na sauti na pia picha za uhuhishaji (animation).


“Lengo kubwa la SAG ni kutengeneza jukwaa litakalowezesha kushirikiana na kampuni za kiafrika katika kuacha alama kupitia teknolojia, media na ubunifu. Haya yote yatawezeshwa na kampuni zetu tanzu 5 zitakazofanya kazi kubwa ya kuhakikisha washirika wetu wanakabiliana kwa usahihi na changamoto zao. Tunaungana na kampuni na chapa za kiafrika zenye lengo la kuleta mapinduzi ya kidigitali. Kama methali ya kiafrika inayosema, “kama unataka kwenda haraka nenda mwenye, kama unataka kwenda mbali nenda na wenzako” alimalizia Ndg. Edwin Bruno, CEO na CVO wa SAG.
Share:

URUSI NA TANZANIA KUANZISHA MIRADI YA MAZINGIRA



Rais wa Jumuiya ya Urafiki wa Tanzania na Urusi Yuri Korobov (kushoto) akiwa na Rais wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (Diaspora) waishio Urusi Dr. Prof. Zenebe Kinfu Tafesse (Kulia).

Na Mwandishi Wetu

Jumuiya ya Urafiki ya Urusi ambayo iliundwa nchini Urusi na watu maarufu na wajasiriamali, inaungana na Tanzania kuanzisha na kukuza miradi ya mazingira na kufikia kiwango cha kimataifa.

Mkuu wa Shirika, mwanachama wa Jumuiya ya Kijiografia ya Urusi, Yuri Korobov anasema “Kwanza, tumejipanga kufanya kazi katika miradi ya mazingira. Hii ni kati ya Urusi na Tanzania, tatizo la ukataji miti hovyo ni baya. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakikata misitu ya asili iliyoenea kwenye maeneo mbalimbali.

“Tanzania inakabiliwa na matatizo kadhaa ya mazingira, hiyo imekuwa ikiathiri maendeleo ya mazingira kwa kiasi kikubwa.

“Tatizo kubwa linaloikabili Tanzania ni uharibifu wa ardhi, uchafuzi wa mazingira, kukosa maji safi katika baadhi ya maeneo ya mjini na vijijini na upoteaji wa wanyamapori,”.

Jumuiya ya Urafiki ya Urusi inajipanga kufanya kazi na mashirika kama Baraza la Kitaifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambalo lina jukumu la kuishauri serikali juu ya mambo yote yanayohusiana na mazingira.

Korobov alisema pia wataangalia changamoto zingine ambazo zimekuwa kikwazo katika kuathiri mazingira Tanzania.

Kuangalia migodi iliyotelekezwa, ambayo haihifadhiwi vizuri baada ya kuchimba madini, ikitoa gesi hatari za kemikali ambazo husababisha uharibifu wa udongo.

Ukataji miti kwa wingi

“Shida zote hapo juu zinaweza kupunguzwa kwa gharama ya teknolojia zilizopo nchini Urusi. Ndio sababu tumepanga kufanya mafunzo ya pamoja na kubadilishana wataalamu - wanamazingira, wahandisi, wakemia na wanaojitolea,” alisema Korobov.

Jumuiya ya Urafiki ya Urusi na Tanzania zinatarajiwa kutia saini makubaliano yao ya kwanza na Jumuiya ya Urafiki ya Tanzania mwishoni mwa Juni 2021. Kama sehemu ya makubaliano, vyama vitaunda baraza la biashara, ambalo litajumuisha watumishi wa umma na wajasiriamali.

“Kwa pamoja tutafanya kazi na kutekeleza uelewa wa jinsi miradi inapaswa kutekelezwa kila mahali, hata katika miradi ya kibiashara, ambayo tutashiriki kama washauri na kutoa msaada wa habari, kuna mwelekeo wa mazingira,” alisema Korobov.

Aliongeza, shirika limepanga kutekeleza miradi mingine kadhaa, ambapo miongoni mwao ni uundaji wa jukwaa la ushirikiano wa kiuchumi kati ya biashara ya Tanzania na Urusi, kufanyika kwa jukwaa la uchumi lenye kaulimbiu ya kuvutia uwekezaji wa pande zote, utayarishaji wa mipango ya elimu kwa wanafunzi na vijana wa Urusi na Tanzania, ushirikiano katika maendeleo ya sekta ya kilimo ya nchi zote mbili, na pia utekelezaji wa mipango salama ya utalii, ubadilishaji wa kitamaduni.

Jumuiya ya Urafiki na Tanzania ilianzishwa nchini Urusi Aprili 2021 na kikundi cha watu maarufu na wajasiriamali kukuza miradi ya mazingira katika kiwango cha kimataifa.

Mwaka 2019, Sochi iliandaa mkutano wa kwanza wa uchumi wa Urusi na Afrika, ambao ulisababisha tamko lenye malengo ya maendeleo zaidi ya ushirikiano wa Urusi na Afrika katika nyanja za siasa, usalama, uchumi, sayansi, teknolojia na tamaduni.

Mkutano wa pili wa Urusi na Afrika umepangwa kufanyika mwaka 2022.

Tunatarajia urafiki wenye matunda kati ya Urusi na Tanzania kuelekea nchi rafiki ya mazingira na ushirikiano utakaoendelea.

Share:

BARRICK-NORTH MARA YATUNUKIWA TUZO KWA KUFANIKISHA UZINDUZI WA MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI MARA


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (Kulia) akikabidhi cheti kwa Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa mgodi wa Barrick North Mara,Gilbert Mworia, (Kushoto) kutokana na mchango wa kampuni hiyo kufanikisha uzinduzi wa mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa Mara katika hafla iliyofanyika mjini Musoma. Katikati mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, mhandisi Robert Gabriel Luhumbi.
Waziri Mkuu,Mhe. Kassim Majaliwa (Kulia) akikabidhi tuzo kwa Meneja wa Mahusiano ya jamii wa mgodi wa Barrick North Mara, Gilbert Mworia, (Kushoto) kutokana na mchango wa kampuni hiyo kufanikisha uzinduzi wa mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mara, katika hafla iliyofanyika jana mjini Musoma.Katikati mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, mhandisi Robert Gabriel Luhumbi.
Kampuni ya Barrick ilishiriki pia katika maonyesho hayo

***

Kampuni ya Barrick, kupitia mgodi wake wa North Mara, imetunukiwa tuzo kwa  kufanikisha uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji (Investment Guide ) mkoani Mara uliofanyika katika viwanja vya Mwembeni Complex,  mjini Musoma ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhshimiwa Kassim Majaliwa.

Mhe. Kassim Majaliwa, alitumia nafasi hiyo ya kuzindua mwongozo kwa kuwakaribisha wawekezaji kuchangamia fursa mbalimbali za uwekezaji  mkoani humo na kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya 6 itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchi ma kuondoa vikwazo vinavyozorotesha  uwekezaji.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Gabriel ,alishukuru wadau mbalimbali waliofanikisha maandalizi ya uzinduzi huo  ikiwemo kampuni ya Barrick kupitia mgodi wake wa North Mara.

Kwa kutambua mchango huo kampuni Waziri  Mkuu,Mh.Kassim Majaliwa ilkabidhiwa tuzo na cheti   kwa watendaji wa mgodi wa Barrick North Mara.

Mbali na kufanikisha  uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji, Barrick imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kuboresha uchumi wa kijamii ikiwemo kukabiliana na changamoto mbalimmbali za kijamii hususani katika sehemu zinazozunguka maeneo yake ya kazi.

Mchakato wa Serikali kuanzisha mpango wa kila mkoa kuzindua Mwongozi wa uwekezaji umelenga kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo katika maeneo,ili kuvutia wewekezaji wa nje,kukuza biashara katika mikoa hiyo hayo  na kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii.

Uzinduzi huo umekuwa ukifanyika sambamba na maonyesho ya bidhaa ya wajasiriamali na makampuni  kwa ajili ya kutagaza biashara na shughuli zao mbalimbali.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger