Thursday, 14 January 2021

RAIS WA ZANZIBAR DK. MWINYI, MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD WATUA CHATO KUZUNGUMZA NA JPM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 14 Januari 2021. Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya kuzungumza na Wanahabari katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 14 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya kuzungumza na Wanahabari katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 14 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad mara baada ya kuzungumza na Wanahabari katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 14 Januari 2021.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad  akizungumza na Wanahabari mara baada ya kikao chao cha pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya mazungumzo yao ya pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyipamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad. PICHA NA IKULU
Share:

MCHUNGAJI ALIYEBAKA NA KUWAPA MIMBA BINTI ZAKE ATUPWA JELA MIAKA 140...ASEMA ALIPITIWA NA SHETANI



Mahakama nchini Kenya imemfunga kifungo cha miaka 140 jela mchungaji aliyewabaka wasichana wake wawili wa miaka 14 na miaka 16 na kuwapatia mimba.

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa Baricho Anthony Mwicigi, alimuhukumumwanaume huyo kifungo cha miaka 70 kwa kila msichana . Mahakama iliamua kuwa hukumu hizo zitatekelezwa moja baada ya nyingine na hivyo mchungaji huyo ataishi jela miaka 140.

Mchungaji huyo kutoka kaunti ya Kirinyaga kati kati mwa Kenya, mwenye umri wa miaka 51 alikiri kuwabaka watoto wake tarehe 5 Januari na kuwekwa jela tangu tarehe 7 Januari. Alimlaumu shetani kwa ubakaji huo watoto wake na akawaomba msamaha watoto wake na mahakama.

Hakimu mkazi Anthony Mwicigi alisema kuwa mchungaji huyo alipataikana na hatia kwa kukiri mwenyewe kuwabaka watoto wake na akaagiza hukumu dhidi yake itolewe tarehe 14 Januari.

Mchungaji huyo anayefahamika kwa jina la Gichina alikamatwa mahala alipokuwa amejificha baada ya polisi kuanzisha harakati za kumsaka.


Msichana mmoja tayari ana mtoto wa miezi 7 na mwingine ana mtoto wa miezi 5.
Share:

MTWIVILA CITY (IFUENGA UNITED) YAIFUATA IVAMBINUNGU FC FAINALI YA ASAS SUPER LEAGUE


Kikosi cha timu ya Mtwivila city (Ifuenga united) kilichofanikiwa kuingia fainali ya Asas super league

 
Na Fredy Mgunda na Denis Mlowe ,Iringa.
TIMU ya soka ya Mtwivila city (Ifuenga united) imefanikiwa kuingia fainali ya ligi soka daraja la tatu mkoa wa Iringa kwa baada ya kuifunga timu ya soka Irole fc mabao 2 - 1 katika mchezo mkali wa nusu fainali ya pili iliyochezwa kwenye uwanja wa Mkwawa.

Hivyo kutokana matokeo hayo timu ya soka ya Ifuenga United watakutana na  Ivambinungu fc siku ya jumapili katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Samora.

Timu ya Ivambinungu Fc ilikuwa timu ya kwanza kutangulia kwenda fainali baada ya kuwafunga timu ya Kidamali Fc kwa jumla ya magoli 3-1 na kuifanya timu hiyo kufika fainali baada ya kushinda nusu fainali zote mbili zilizopigwa katika viwanja vyote viwili vya nyumbani na ugenini.


Nayo Timu ya Mtwivila city (Ifuenga united) imeingia fainali baada ya kuifunga timu ngumu ya Irole Fc kwa jumla ya goli mbili moja baada ya michezo yote miwili iliyochezwa nyumbani na ugenini.

Akizungunza mara baada ya mchezo wa nusu fainali ya pili  kocha wa timu ya Ifuenga Edger Nzelu alisema kuwa timu hiyo imejipanga vilivyo kuhakikisha wanashinda fainali kwa kuwa mchezo huo muhimu ambao kwa namna yoyote ile lazima washinde kwenda katika ngazi ya kanda.

Nzelu alisema kuwa baada ya kushinda mchezo huo mgumu wa nusu fainali ana uhakika wa kushinda mchezo wa fainali yenyewe kwa kuwa timu hiyo ya Irole Fc ndio ilikuwa kikwazo kwao.

Aliwataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuisapoti timu hiyo ili kuipa nguvu kuhakikisha kwenye fainali na kwenda mbele kwenye mashindano ngazi nyingine

Naye mfadhili wa timu hiyo Joseph Kilienyi alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo wa fainali na kuchukua kombe hilo.

Alisema kuwa timu ya Ivambinungu Fc ni timu nzuri lakini wao wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo muhimu kwao kwa kuwa wanataka kwenda kanda na kuhakikisha timu hiyo inafika katika madaraja ya juu na hatimaye kufika ligi kuu Tanzania Nara.

Timu ya Mtwivila city (Ifuenga) imejipanga kwa kila kitu hivyo wakiwa mabingwa wa mkoa watahakikisha timu hiyo hairudi nyuma tena kwenye ligi ya mkoa wa Iringa tena.

Bingwa wa ligi hiyo iliyojizoelea umaarufu nchini kutokana na udhamini wa kampuni ya maziwa ya Asas ataondoka na sh milioni 2.5 huku mshindi wa pili akichukua milioni 1.5 na mshindi wa tatu ataibuka na laki 750000 baada ya zawadi kuongezwa kwa washindi.
Share:

Bunge Marekani lamshtaki Trump kwa mara ya pili


 Baraza la Wawakilishi katika Bunge la Marekani limepiga kura na kupitisha mashtaka ya kumvua madaraka rais wa nchi hiyo Donald Trump, kufuatia mashtaka ya kuchochea vurugu na uvamizi wa majengo ya bunge wiki iliyopita.

Wabunge 10 wa Chama cha Republic ni miongoni mwa waliopiga kura na Wademocrat dhidi ya Trump. Spika wa bunge, Nancy Pelosi amesema hatua hiyo ya baraza la wawakilishi ni ujumbe kuwa hakuna aliye juu ya sheria, akimrejerea Rais Trump.

Trump amekuwa rais wa kwanza katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya kutokuwa imani naye mara mbili. Hata hivyo baraza la seneti halitaanza mchakato wa kupitisha au kuzuia hatua hiyo ya baraza la wawakilishi kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden Januari 20.

Endapo baraza la seneti litamkuta na hatia hata baada ya kuondoka madarakani, huenda atazuiwa kuwania urais tena katika uchaguzi ujao wa mwaka 2024.




Share:

WATAALAM WA KILIMO SINGIDA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA YA KILIMO CHA UMWAGILIJI KATIKA KAZI ZAO.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu toka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali akiwasilisha mada katika kikao kazi nawataalam wa Kilimo na Ushirika Mkoani Singida
Godwin Mutahangarwa Mwanasheria kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akiwasilisha mada i nayohusu Sheria ya Kilimo cha Umwagiaji ya mwaka 2013 na kanuni zake katika kikao kazi na wataalam wa kilimo Mkoani Singida.


Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Miundo mbinu tokaTume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda, akigawa makablasha kwa wataalam wakilimo wakati wa kikao kazi kilichofanyika Mkoani Singida.
Warishiriki wakifuatilia kikao kazi kilichohusisha wataalam wa Kilimo na Ushirika Mkoani Singida
 

Na Mwandishiwetu - Singida


Maafisa Kilimo Ushirika na Umwagiliaji Mkoani Singida, wametakiwa kuzingatia nakutumia kikamilifu Sheria ya Taifa ya Umwagiiaji ya mwaka 2013 na kanuni zake pamoja na Sheria ya usimamizi na uhifadhi wa Mazingira ya mwaka 2004,ilikuweza kunusuru na kulinda vyanzo vya maji,nakutunza Miundombinu ya kilimo cha Umwagiliaji.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali, alipoikuwa akizungumza katika kikao kazi na maafisa kilimo ushirika na wahadisi wa Umwagilijiaji Mkoani Singida.

Bw. Kaali amewataka wataalam hao wazielewe sheria hizo na kuhakikisha zinafanyakazi na kueleweka kwa umma na bila kupepesa macho kuwe na utii washeria bila shuruti na kuwachulia hatua wale wote wanaofanya uharibifu wa mazingira kwa kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji,ilikulinda miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.

“Ni lazima kuzingatia utunzaji wa mazingira kwa kutokukata miti ovyo,nauchafuzi wa miundombinu ya umwagiliaji, mshirikiane na mamlaka husika ili kuweza kunusuru mazingira na kutunza miundombinu hiyo na mazingira,iko wazi kabisa kuwa, miundombinu mingi iliyoharibika inaonekana kuwa chanzo kikubwa ni uharibifu wa mazingira.” Alibainisha.

Akiongelea suala la Uhabirifu wamazingira litokanalo na mabadiliko ya Tabianchi, Bw. Kaali amesema ili kuhimili na kukabiliana na changamoto hiyo, wamekuwa wakihamasiha matumizi sahihi ya teknolojia nyingine sambamba na kupanga mikakati ya pamoja ya kuelendeleza sekta ya kilimo cha umwagiliaji kwa kushirikiana na sektabinafsi.

Akiongea katika kikao kazi hicho, Bw. Suleiman Musunga Afisa Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji toka Wilaya ya Mkalama ameushukuru Mradi wa kurejesha Ardhi iliyoharibika nakuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame nchini, (Reversing land Degradation trends and increasing food security in degraded ecosystem in semi-arid areas of Tanzania) Unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira ,Kwa kukamilisha hatua ya awali ya kazi ya upembuzi yakinifu na nakuelekea kwenye hatua nyingine ya ujenzi wa mabwawa.


Mradi ambao utawawezesha wakulima katika eneo hilo kuweza kupata maji salama kwa ajili ya kilimo,na wafugaji kwa ajili ya mifugo na matumizi ya jamii iinayoishi maeneo kame.

Kikao kazi hicho cha siku tatu, kilihusisha wataalam wa sekta ya kilimo na umwagiliaji kutoka katika Manispaa ya Singida na wilayaza Manyoni,Ikungi,Itigi,Iramba na Mkalama.

Share:

TAKUKURU YAREJESHA NYUMBA ILIYOPORWA KINYEMELA BAADA YA MMILIKI WAKE KUSHINDWA KULIPA MKOPO WA SHILINGI LAKI TATU KAHAMA


Wananchi wakishuhudia Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akimkabidhi nyaraka za umiliki wa nyumba mtoto wa marehemu Rose Edward ambayo ilikuwa imeuzwa kinyemela.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akimkabidhi nyaraka za umiliki wa nyumba mtoto wa marehemu Rose Edward ambayo ilikuwa imeuzwa kinyemela.

Na Salvatory Ntandu - Kahama
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Kahama imerejeshea nyumba yake Edward Mpolosi mkazi wa Mtaa wa Nyihongo wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambayo ilikuwa imechukuliwa na Masero Nyamhanga mfanyabiashara wa mikopo umiza baada ya kushindwa kulipa mkopo wa shilingi laki tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Mkuu wa Takukuru wilaya ya Kahama Frank Masilamba katika hafla maalumu ya kuikabidhi nyumba hiyo kwa familia ya Mpolosi alisema kuwa utaratibu uliotumika kujimilikisha nyumba hiyo uliofanywa na Masero ulikuwa ni batili na haukuzingatia sheria.

“Marehemu Edward alichukua mkopo wa shilingi laki tatu lakini alipochelewesha kulipa deni hilo liliongezeka riba hadi kufikia shilingi milioni 10 na laki 5 ndipo alilazimika kuingia mkataba batili wa mauziano ya nyumba hiyo huku mkopeshaji akijua wazi kuwa alikuwa anatenda kosa,”alisema Masilamba.

Alifafanua kuwa watoto wa Edward walifika katika ofisi za Takukuru kutoa taarifa kuhusu baba yao kudhulumiwa nyumba iliyopo katika kitalu J 165 mtaa wa Nyihogo walianza uchunguzi na kubaini kuwa makubaliano ya mauziano ya nyumba hiyo yalikuwa ni batili.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha alisema kuwa serikali imeamua kuikabidhi nyumba hiyo watoto wa Marehemu Edward ambao ni Rose na George ili waendelee kuimiliki baada ya Masero kubainika hana uhalali wa mauziano ya nyumba hiyo maelekezo.

“Hatutawavumilia wafanyabiashara wanaotumia fedha zao kunyanyasa wananchi wanyonge kwa kuwakopesha mikopo umiza ambayo imekuwa ikiendelea kupoka haki za watu wengine, tutaendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria watakaobainika kutoa mikopo umiza bila kufuata sheria za nchi,”alisema Macha.

Naye Rose Edward ambaye alikabidhiwa nyumba hiyo aliishukuru taasisi hiyo kwa kufanikiwa kuwarejeshea nyumba yao ambayo ilikuwa imetwaliwa kinyemela na familia ya Masero, mgogoro ambao umewasumbua kwa muda mrefu bila ya kupata mafanikio kutokana na mkopeji huyo kudai kuwa aliuziwa nyumba hiyo na marehemu baba yao.

“Tunaipongeza serikali kwa kutusikiliza sisi wanyonye baada ya baba yetu kufariki tulianza kupokonywa mali zake ikiwemo nyumba,tumeishi maisha ya shida kutokana na mgogoro wa nyumba yetu ambayo leo tumeirejeshewa,”alisema Rose.
Share:

Tigo yaungana na mawakala wa Tigo Pesa kuhitimisha promosheni ya Tigo Pesa Wakala Push, yatoa zawadi kwa mawakala mbalimbali


VUKA LENGO NA USHINDE: “Ili kuwa mshindi, kila wakala alitakiwa kuvuka lengo alilopewa, kulingana na historia ya miamala yake ya kila siku. Zaidi ya mawakala 4,000 walifanikiwa kuvuka malengo yao na kushinda zaidi ya shilingi milioni 400.” Angelica Pesha, Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa #TigoPesaNiZaidiYaPesa #TigoPesaWakalaPush

TIGO PESA BOOST MTAJI!: “Nawashukuru Tigo kwa kuwa kupitia #TigoPesaWakalaPush wameweza kuniboost mtaji wangu” Piason Baruti, Wakala Tigo Pesa na Mshindi wa Milioni 1.5
#TigoPesaNiZaidiYaPesa

Mkuu Kitengo cha Tigo Pesa-Tz akiwa na katika picha ya Pamoja na washindi

WASHINDI KANDA ZOTE! Tumepata washindi kutoka kanda zetu 4,Pwani, kanda ya Ziwa, kanda ya Kusini na kanda ya kaskazini. Na hawa ni washindi waliofanya vizuri zaidi katika kanda ya Pwani.

NIMEONGEZA MTAJI: “Kupitia promosheni hii ya Tigo mtaji wangu umeongezeka hivyo nimeweza kuwahudumia wateja wengi zaidi” Neema Swai-Wakala Tigo Pesa & Mshindi Milioni 1.2
#TigoPesaNiZaidiYaPesa




Wakala



Share:

Kaimu Mkurugenzi Asimamishwa kazi kwa Kusafirisha Maiti Juu ya Gari.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi Joseph Nyamuhanga kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara Jumanne Yassin ili kupisha uchunguzi, kufuatia kitendo cha halmashauri hiyo kusafirisha mwili wa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Emmanuel Sizo juu ya Carrier ya gari.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo baada ya gari iliyobeba mwili wa Mtumishi huyo.kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Amesema amesikitishwa na kitendo hicho ambacho ni kinyume na kanuni za utumishi wa Umma, pamoja na mila na desturi za Mtanzania.

Ameagiza Watumishi wote waliohusika na uzembe huo wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria, kanuni.na taratibu za utumishi wa Umma.

Waziri Jafo amewataka Watumishi wote wa Umma katika tawala za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kujenga tabia ya kuheshimiana, kupendana na kuthaminiana wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.

Sizo alifariki duniani kwa ajali ya gari mkoani Singida Januari 10 mwaka huu.


Share:

Watumishi 23 MOI mikononi mwa TAKUKURU


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), inawachunguza Watumishi 23 wa Taasisi ya Mifupa Muhimboli ( MOI) kitengo cha Famasia, kwa tuhuma ya uchepushaji wa dawa zenye thamani ya shilingi bilioni 1.2.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia JeneraliJohn Mbungo amesema uchunguzi wa kuwabaini Watuhumiwa hao ulianza mwaka 2018 hadi mwaka huu kwa ushirikiano na MOI na TAKUKURU.

Katika hatua nyingine Brigedia Jenerali Mbungo amefanya mabadiliko ya Watendaji ndani ya taasisi hiyo, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi.

Pia amewaambia Waandishi wa habari kuwa, wameanzisha kitengo cha TAKUKURU kinachotembea, kitakachokuwa kikisikiliza na kutatua kero za Wananchi poppte walipo.


Share:

MITANDAO YA KIJAMII YAZIMWA MKESHA WA UCHAGUZI UGANDA

Mamlaka nchini Uganda ilikatiza hudama za intaneti saa kadhaa kabla ya uchaguzi wa urais unaokumbwa na ushindani mkali kati ya nyota wa muziki na mmoja viongozi wa muda mrefu wa Afrika waliohudumu miaka mingi madarakani.

Kundi la ufuatiliaji wa masuala ya Intaneti NetBlocks liliandika kwenye Twitter yake kwamba nchi hiyo ilizima mitandao yote ya intaneti Jumatano saa moja usiku majira ya Afrika Mashariki.

Hatua hiyo ilifuatia agizo la serikali kufungia mitandao yote ya kijamii na programu tumishi za kutuma ujumbe.

Rais Yoweri Museveni alisema alifikia uamuzi huo kwa sababu Facebook ilifunga akaunti kadhaa zinazounga mkono chama tawala.

Mgombea wa urais,mwanamuziki aliyegeuka Bobi Wine aliandika katika Twitter yake kwamba huduma za intaneti zimekatizwa kama sehemu ya njama ya kuiba kura.

"Watu wa Uganda wako imara na hakuna jambo lolote litakatiza azma yao ya kikomesha utawala wa kiimla," aliongeza.

Shughuli za upigaji kura ilianza saa moja asubuhi ya leo Alhamisi, japo matokeo hayatarajiwi kutolewa kabla ya Jumamosi.

Kampeni za uchaguzi zilikumbwa na ghasia ambazo zilisababisha vifo vya makumi ya watu.

Bw. Museveni anagombea muhula wa sita baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.

 CHANZO - BBC SWAHILI

Share:

WAKRISTO WATAKIWA KUPANDA MBEGU BORA WAPATE MAVUNO MENGI


Mtumishi wa Mungu Mwalimu Joyce Mwakalasya  baada ya kutoa mafunzo ya upandaji wa mbegu kwa waumini wa Kanisa la Moravian Usharika wa Kijichi jijini Dar es Salaam Jumapili.

Mchungaji wa Kanisa la Moravian Usharika wa Kijichi jijini Dar es Salaam, Raphael Mwampagatwa (kulia) akiwa na  Mtumishi wa Mungu Mwalimu Joyce Mwakalasya  (katikati) baada ya kutoa mafunzo ya upandaji wa mbegu. Kushoto ni mke wa mchungaji huyo.
Waumini wa kanisa hilo wakifurahi.
Waumini wa kanisa hilo wakibadilishana mawazo baada ya mafunzo hayo. Katikati ni mmoja wa Wazee wa kanisa hilo, Mwalimu Mary Anyitike.


Na Dotto Mwaibale 


WAKRISTO wametakiwa kupanda mbegu bora kwa kumtolea Mungu sadaka ili waje wavune mavuno mengi.

Ombi hilo limetolewa na Mtumishi wa Mungu Mwalimu Joyce Mwakalasya wakati akitoa mafunzo ya upandaji wa mbegu kwa waumini wa kanisa la Moravian Usharika wa Kijichi jijini Dar es Salaam Jumapili.

Mwakalasya alisema suala la upandaji wa mbegu ni la muhimu wakati wa kumtolea Mungu sadaka kwani huwezi ukatoa sadaka ndogo wakati unayo kubwa ukategemea kubarikiwa.

"Hata kabla ya kwenda kutoa sadaka yako Mungu anakuwa anaijua hivyo tunapokwenda kuitoa mbele ya madhabahu tutoe kwa uaminifu ili uje uvune mavuno mengi baada ya kuipanda." alisema Mwakalasya.

Alisema kabla ya kupanda mbegu yako hiyo unapaswa kujua unaipanda eneo gani na kwa wakati upi na si kila eneo utakapo ipanda itastawi.

Mwakalasya alitaja uvivu na uzembe kwa mkristo kuwa ni adui mkubwa wa upandaji mbegu hivyo alitoa rai ya kufanya kazi kwa bidii kwani huwezi kumtolea Mungu sadaka bila ya kuwa cha chanzo cha mapato.

Alitaja vitu vingine ambavyo vinakwamisha kupanda mbegu  ni mtu kuwa na imani haba, wivu usiofaa, uchoyo, ubinafsi, kutosamehe, kufanya kazi isiyo halali na kutolipa kodi ya serikali.

Alitaja changamoto nyingine zinazo changia kuzolotesha upandaji wa mbegu kuwa ubinafsi, hofu, kutokuwa na moyo wa kuthubutu kufanya jambo, kiburi,  ushirikina na kuwaza kinyume cha matokeo.

Alisema mkristo akifanikiwa kuyashinda mambo hayo ni lazima atapata mafanikio Mungu ni zaidi ya yote kwani aliweza kuwa saidia akina Eliya na wengine wengi hivyo ukimtolea sadaka kamilifu kwa kupanda mbegu atakubariki.

Mwakalasya alitumia nafasi hiyo kuwaambia waumini hao kuwa mara baada ya kuvuna mavuno yao yaliyotokana na upandaji mbegu wayatumie kuwa saidia watu wenye uhitaji.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JANUARI 14,2021


















Share:

YANGA BINGWA MAPINDUZI CUP, YAICHAPA SIMBA SC KWENYE MIKWAJU YA PENALTI 4-3


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Michuano ya Mapinduzi Cup Nahodha wa Timu ya Yanga Haruna Nyonzima, baada kuifunga Timu ya Simba katika mchezo wa Fainali uliofanyika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

********************
Na Emmanuel Mbatilo - Zanzibar
Klabu ya Yanga imefanikiwa kunyakua ubingwa wa Mapinduzi Cup baada ya kuinyuka katika mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za mchezo.

Nyota wa mchezo huo ni Farouk Shikalo ambaye aliokoa penalti moja ya Joash Onyango na Meddie Kagere kugongengesha mwamba penalti yake moja.

Saido Ntibanzokiza ambaye alikuwa msumbufu ndani ya dakika zote 90 amesema kuwa wachezaji wenzake walimuomba awape sapoti naye akasema kwamba hana tatizo atafanya kazi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger