Saturday, 9 January 2021
JITIBU TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA KUTUMIA FULL POWER.. UUME MDOGO ZAT 50 NDIYO SULUHISHO
KARIBU GVEN WEAR UPATE MUONEKANO WA PEKEE .....HUDUMA ZA KIPEKEE

Tanzania,china Kuendelea Kushirikiana Kiuchumi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika masuala ya uchumi kwa sababu uhusiano na urafiki wa nchi hizi mbili ni wa muda mrefu.
Hayo yamesemwa jana (Januari 8, 2020), Chato mkoani Geita, wakati Rais Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) wa kipande cha tano kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga, mradi utakaogharimu shilingi trilioni 3.0677.
Rais Magufuli alisema “Natoa wito kwa kampuni ya CCECC inayojenga kipande hiki cha Mwanza hadi Isaka kijengwe kwa haraka zaidi, lakini niombe Serikali ya China katika kipande kilichobaki cha Isaka hadi Makutopora kama wataweza kutukopesha na sisi tutafurahi sana ili kiweze kujengwa kwa sababu kitasaidia sana katika kuleta maendeleo ya nchi yetu na baadae tutaendelea kujenga Tabora, Kigoma na maeneo mengine.”
Vilevile, Rais Magufuli alisema “Nimemuhakikishia Waziri Wang Yi kuwa kufanya biashara na Tanzania kuna faida kwani kupitia nchi yetu watakuwa na uwezo kufanya biashara na nchi zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi zilizo Kusini mwa Afrika kwa sababu Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya hizo”
Alibainisha kuwa China ni nchi tajiri duniani na Tanzania kuna mazao mengi ambayo yanaweza kuuzwa nchini humo hivyo kuwataka watanzania kutumia fursa huyo kwa kuuza mazao na bidhaa nchini China.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alisema kuwa amepokea ujumbe kutoka China, lakini pia ametuma ujumbe kwa Rais wa China, Xi Jinping kumuomba aisaidie Tanzania katika ujenzi wa miradi ya kufua umeme wa maji mkoani Njombe, Lumakali na Luhuji pamoja na ujenzi wa kilometa 148 za barabara kwa kiwango cha lami Zanzibar.
Fauku ya hayo, Rais Magufuli ametaja baadhi ya masuala waliyozungumza na Waziri Wang kuwa ni kuomba Tanzania isamehewe madeni iliyokopa ikiwemo la dola za Marekani milioni 15.7 za ujenzi wa reli ya TAZARA, deni la dola za Marekani milioni 137 la nyumba za askari ambapo Serikali imeshalipa tayari dola za Marekani 164 pamoja na deni la kiwanda cha Urafiki la dola za Marekani milioni 15.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi alisema kuwa uwepo wa Rais Magufuli katika tukio hilo la utiaji saini wa mkataba huo unaonesha umuhimu mkubwa ambao Rais anaupa ushirikiano na urafiki uliopo kati ya nchi hizi mbili na kuzitataka kampuni za kichina kufanyakazi kwa ubora.
“Natumia fursa hii kuyaagiza makampuni ya China yanayotekeleza miradi hapa nchini Tanzania kutekeleza miradi hiyo kwa kuzingatia kwanza maslahi ya Tanzania.” Alisema Waziri Wang
Naye, Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema kuwa zilijitokeza kampuni zaidi ya 18 za kimataifa kwa ajili ya kujenga reli ya kisasa kipande cha Mwanza – Isaka, baada ya kufanya mchakato kampuni za CCECC zilishinda zabuni, gharama ya mradi ni shilingi trilioni 3.0677.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CCECC, Mhandisi Jiang Yigao alisema kampuni yake imekuwa ikifanyakazi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 50 na katika kipindi cha miaka 10 iliyopita imetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo daraja la Busisi- Kigongo, Ubungo interchange na ujenzi wa reli ya TAZARA.
“Kama tulivyofanya ujenzi wa TAZARA tutafanya hivyo hivyo kwa kujenga reli hii ya kisasa tukitumia raslimali zilizopo na kujenga mradi huu kwa wakati na kwa viwango vya kimataifa.” Alisema Mhandisi Yigao
Mwisho
WHATSAPP NA FACEBOOK ZAWALAZIMISHA WATUMIAJI KUTUMA MAELEZO YAO BINAFSI

YANGA YAICHAPA NAMUNGO FC BAO 1-0 MICHUANO YA MAPINDUZI CUP
Friday, 8 January 2021
Trafik akamatwa kwa kuomba rushwa ya ngono akamailieshe uchunguzi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kilimanjaro inamshikilia Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Peter Albert Moshi kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Ngono.
Askari huyo alikuwa akichunguza ajali ya pikipiki ambayo ilimgonga mtoto na kusababisha kuvunjika mkono. Aliomba Rushwa Ngono kwa mama wa mtoto ili aweze kukamilisha Taarifa za Uchunguzi.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro, Frida Wikesi amesema, askari huyo amekamatwa Januari 6 akiwa nyumba ya kulala wageni maeneo ya Soweto Mjini Moshi.
Uchunguzi wa TAKUKURU umebaini kuwa, Peter alimsumbua mama wa mtoto kwa muda mrefu na hivyo kusababisha shauri kuchelewa hali iliyopelekea mama huyo kupeleka malalamiko na wakaweka mtego wa kumkamata.
TAMISEMI KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA AGRI THAMANI
| Madiwani na Viongozi wa UWT wakifuatilia kwa karibu Mafunzo ya Lishe Bora |
NA MWANDISHI WETU,BUKOBA
MRATIBU wa Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dodoma Mwita Waibe amesema watahakikisha wanashirikiana na Shirika la Agri Thamani ambalo limekuwa likitoa elimu ya umuhimu wa lishe bora na athari zake endapo hazitatiliwa mkazo ili kuweza kuibadilisha jamii husika.
Mwita aliyasema hayo wakati wa utoaji wa elimu ya lishe bora wa shirika hilo kwa Viongozi wa makundi mbalimbali kama sehemu ya kuhakikisha malengo ya Lishe yaliyowekwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 yanatekelezwa.
Alisema Ofisi ya Rais TAMISEMI imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Agri Thamani kuhakikisha elimu hiyo inawafikia wananchi huku akiwapongeza sana Agri Thamani kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya kuhakikisha elimu ya Lishe Bora inafika ngazi ya jamii ambapo ndio haswa kazi kubwa ilipo.
Elimu hiyo ambayo imekuwa chachu kubwa imeweza kuwafikia madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mjini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ambao wamenufaika na semina hiyo hususan katika vipengele vya mikataba ya lishe iliyosainiwa kuanzia ngazi ya mkoa hadi kijiji,
“Lakini pia bajeti za lishe na sasa malengo ambayo CCM imejiwekea kwenye Ilani ya Uchaguzi ambayo kimsingi wanajukumu la moja kwa moja kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa na mafanikio makubwa kwa jamiii husika”Alisema
AWALI Afisa Lishe wa Wilaya ya Bukoba Vijijini Desdery Karugaba, amewashukuru Agri Thamani kwa kuandaa Semina hiyo ambayo sasa inakwenda kuongeza kasi ya jitihada za kutokomeza udumavu na utapiamlo kwa ujumla wilayani hapo.
“Kwa kweli niseme kwamba semina hii itakuwa chachu kubwa ya kuweza kuongeza jitihada za kutokomeza udumavu na utapiamlo kwa ujumla kwa wilayani hapo”Alisema
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Murshid Ngeze alisema kwamba wao kama Halmashauri wanaelekeza ajenda ya Lishe Bora iwe ya Vitendo na kuahidi matokeo yataonekana maana ni lazima kama Halmashauri wawe mstari wa mbele kuikoa rasilimali watu.
Hata hivyo Mhe Mbunge Neema Lugangira ambaye pia ni Mkurugenzi wa Agri Thamani amesema kwa kuanzia semina hizi zimeshafanyika Dodoma na hivi sasa zinaendelea mkoani Kagera na zitafanyika Tanga na Kigoma.
"Dhamira yangu binafsi ni kuiona Ajenda ya Lishe inakuwa ajenda ya kila Mtanzania na kila mtu kwa nafasi yake anakuwa sehemu ya kuchangia kutokomeza udumavu kuanzia ngazi ya jamii inayotuzunguka", Mhe Neema Lugangira alimalizia
RAIS MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE YA CHINA WANG YI CHATO GEITA
FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO

Naibu Waziri Bashe Aagiza Takukuru Kuanza Uchunguzi Wa Upotevu Wa Milioni 150 Za AMCOS Ya Chabuma
Naibu Waziri Kilimo Hussein Bashe ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Chamwino kuanza mara moja uchunguzi dhidi ya Viongozi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Zabibu (CHABUMA AMCOS) katika wilaya hiyo; Waliochukua fedha kiasi cha shilingi milioni 150 ambazo zimetumika kinyume cha utaratibu.
Naibu Waziri Bashe amefika katika kijiji cha Buigili na kufanya mazungumzo na Wawakilishi wa Wakulima waliokusanyika katika shamba lao la zabubu katika kijiji cha Mwegamile kata ya Buigili halmashauri ya wilaya ya Chamwino ambapo amemwagiza Mwakilishi wa Kamanda wa TAKUKURU Chamwino kuchukua hatua stahiki baada ya kuelezwa kilio hicho na Wakulima hao.
“Mhe. Mkuu wa wilaya; Naomba uchukue hatua na kwakuwa Mwakilishi wa Kamanda wa TAKUKURU Chamwino yupo hapa. Hawa Viongozi wachunguzwe na hatua stahiki zichukuliwe. Tuziapate fedha za Wakulima wetu kiasi cha shilingi milioni 150.” Amekaririwa Naibu Waziri Bashe.
Wakulima hao wamemwambia Waziri Bashe kuwa CHABUMA AMCOS ilipokea fedha hizo kutoka kwa Kampuni ya ARCO Vintage mwaka 2020 kwa lengo la kuboresha miundombinu ya sehemu ya shamba hilo ili Kampuni hiyo iendelee kununua shehena ya zabibu kutoka katika shamba la Wakulima hao lakini kinyume na utaratibu Viongozi hao walitumia fedha hizo kwa mambo mengine.
CHABUMA AMCOS ni Ushirika wa Wakulima zaidi ya 961 ambapo imeelezwa kuwa kuanzia mwaka 2010 kwa hiari yao walianzisha shamba la zabibu lenye ukubwa wa hekari 296 ambapo walipata mkopo wa bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji pamoja na uwekezaji mwengine ambapo ulichangia shamba hilo kufikia uzalishaji wa juu wa zao la zabibu mwaka 2013 kiasi cha tani 600.
Tangu mwaka 2017 uzalishaji wa zabibu katika shamba hilo uliendelea kushuka na kusababisha Wakulima kutelekeza mashamba yao na kusababisha uzalishaji kusimama kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo adhabu ya riba kutoka Benki ya CRDB kuendelea kuongezeka, kupungua kwa mapato kwa Wakulima pamoja na kukosekana kwa uongozi thabiti pamoja na usimamizi duni.
Katika kukabiliana na hali hiyo Naibu Waziri Bashe ametoa maelekezo kadhaa ili kurejesha hali ya uzalishaji katika shamba hilo.
Naibu Waziri Bashe amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Umwagiliaji kupeleka Wahandisi kuanzia kesho tarehe 8 Januari, 2021 ili washirikiane na Wahandisi wa halmashauri ya Chamwino kufanya tathmini ya gharama ya miundombinu ya umwagiliaji na kuiwasilisha mara moja kwake.
Agizo lingine ni Timu hiyo ya Wahandisi kufanya tathimini kama Mradi huo huo unaweza kutumia nishati ya jua (Solar system) katika kuendesha mashine za kuvuta maji yanayotumika katika kilimo cha umwagiaji katika shamba hilo.
Waziri Bashe ameagiza kila Mkulima ahakikishe anasafisha kipande cha shamba lake ndani ya shamba hilo; Kazi hiyo inatakiwa kukamila ndani ya siku thelathini kuanzia leo (Tarehe 7 Januari, 2021).
Taasisi ya Utafiti wa Mazao ya Kilimo (TARI) imeagizwa kufanya tathmini ya idadi kamili ya miche ambayo itahitaji kwa ajili ya kupandwa baada ya sehemu kubwa ya miche mingi kufa na wakati huohuo TARI inatakiwa kuanzisha kitalu cha miche ya zabibu ambapo miche hiyo itatolewa bure kwa Wakulima wenye uhitaji wa miche hiyo.
Mhe. Bashe amemtaka Mkuu wa wilaya kufanya mawasiliano na Meneja wa Shirika la Ugavi wa Nishati ya Umeme (TANESCO) wilaya ya Chamwino kurejesha huduma umeme katika shamba hilo kwa kuweka ‘transformer’ kama ilivyokuwa awali.
Agizo lingine ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuanda mafunzo ya namna ya kuendesha Ushirika imara na endelevu kwa Wakulima wa CHABUMA AMCOS ndani ya siku thelasini kuanzia(Tarehe 7 Januari, 2021).
Deputy Project Manager at Good Neighbors
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Overview Good Neighbors is an international humanitarian development NGO founded in Korea in 1991. It was granted General Consultative Status from the United Nations Economic and Social Council (UN ECOSOC). The aim is to make the world a place without hunger, where people live together in harmony. In Tanzania it was officially established on 2005 and […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Maternal & Child Health Specialist at UNICEF
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Job no: 535967 Contract type: Temporary Appointment Level: NO-4 Location: Tanzania, Uni. Re Categories: NO-4 UNICEF works in some of the world’s toughest places, to reach the world’s most disadvantaged in order children to save their lives, to defend their right and to help them fulfill their potential. Across 190 countries and territories, we work for every child, everywhere, every […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Fecal Sludge Management Technical Specialist at Tetra Tech International
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Tetra Tech International Development Services (https://ift.tt/1JGwAiR) headquartered in Arlington, VA is currently accepting expressions of interest from qualified candidates for a potential Fecal Sludge Management Technical Specialist position on an anticipated U.S. Agency for International Development (USAID)-funded project in Tanzania. The Activity is anticipated to be a five-year contract to expand the provision and governance […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Youth Officer at Restless Development
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Youth Officer – Tanzania Details Salary: Paid 14,251,668 Location: Tanzania Recommended: About the Programme. The 2021 Generation Equality Forum (GEF) will be a global advocacy gathering in Mexico City and Paris, launching ambitious new commitments on gender equality to galvanize the Beijing+25 Process. Young feminists are at the frontline of shaping gender rights and equality today. With this in […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details







































