Monday, 23 November 2020

TPDC YANG’ARA MASHINDANO YA SHIMUTA TANGA YAILIZA TBS

Katibu wa Michezo kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Elinaike Naburi akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlaly kuhusu namna timu zao zilivyofanya vizuri katika mashindano ya SHIMUTA
TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) ambao waliigaragaza TBS set 2-0 kwenye mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popataly Jijini Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja

TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) ambao waliigaragaza TBS set 2-0 kwenye mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popataly Jijini Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja
TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) ambao waliigaragaza TBS set 2-0 kwenye mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popataly Jijini Tanga walifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza mchezo wao



NA MWANDISHI WETU,TANGA

TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) leo wameibuka na ushindi wa seti 2-0 katika mchezo wa kuvuta kamba dhidi ya timu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika muendelezo wa michuano ya Shimuta inayoendelea Jijini Tanga.

Kwa upande wa wanaume walivuta kamba na chuo cha DIT jana na kupata seti 2-0 na leo wamevuta na chuo cha IAA na kupata mivuto 2-0 na wanaamini mechi zilizobaki wataendelea kushinda na kutinga hatua ya fainali.

Mchezo huo wa uliochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Popatlal Jijini Tanga leo ulionekana kuwa na upinzani lakini TPDC ambao walikuwa wamesheheni wachezaji mahiri na wenye viwango waliweza kuwagaragara wapinzani wao.

Akizungumzia ushindi huo na namna walivyojipanga kuelekea kwenye michezo yao mengine,Kocha wa timu hiyo Joram Ndalalwa alisema timu hiyo imejipanga vizuri kunyakua ubingwa kwenye michuano hiyo.

Joram alisema kila wakati mara baada ya kumalizika kwa mchezo mmoja wanarudi kujitafakari na kujipanga upya kuona namna ya kujiandaa vema .

Alisema baada ya kumalizika mchezo huo na kuweza kuibuka na ushindi wanarudi kujipanga kwa ajili ya mchezo wao unaofuata dhidi ya ATC utakaochezwa Novemba 23 mwaka huu asubuhi na jioni watapambana na UDSM.

Akizungumzia mashindano hayo Katibu wa Michezo kutoka TPDC Elinaike Naburi alisema kwamba walishiriki mashindano hayo ya shimuta mwaka huu ikiwa ni mara yao ya tano mpaka sasa wamekwisha kushiriki michezo wa mpira wa miguu,wavu,pete,kikapu pamoja na michezo ya Jadi,Karata,Table na Draft.

Alisema mchezo wa vishale watamaliza kuanzia Novemba 24 na 25 watafanya mbio mpaka sasa wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 katika mpira wa miguu na Pete waliishia kwenye makundi kwa kuwa mshindi wa tatu huku Wavu wakiishia kwenye makundi lakini walionyesha ushindani mkubwa.

Kikapu waliishia kwenye makundi lakini ushindano wao ulikuwa wa hali ya juu katika michezo ya jadi wameshinda kwa kuwa mabingwa karata upande wa wanawake na mshindi wa pili upande wa wanaume.

Katika mchezo wa drafti alisema waliishia hatua ya robo fainali upande wa wanaume huku wanawake wakiishia hatua za makundi na mchezo wa Pooltable wanawake wamefanikiwa kutetea taji lao kwa kuwa mshindi wa pili mwaka jana mshindi wa kwanza na wanaume waliishia nusu fainali.

Alisema kwamba katika mchezo wa bao wachezaji wao wote wameishia hatua ya nusu fainali huku akieleza malengo ya mashindano hayo kwa TPDC ni kuonyesha ushindani wa hali ya juu.

Alisema pia malengo yao ni kuweza kufahamiana na Taasisi nyengine kujenga mshikamano kama wafanyakazi na kuendelea kutoa morali na motisha kwa wafanyakazi kuendelea kushiriki michezo kwa sababu ni afya.

Hata hivyo alisema wamefurahi kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo na wanaamini wametoa ushindani wa kutosha na wataendelea kufanya hivyo michezo yao iliyobaki.

 

Share:

SERIKALI YA TANZANIA YASEMA IMEONGEZA UWEZO WA KUGUNDUA WAGONJWA WAPYA WA KIFUA KIKUU


Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akigawa cheti cha pongezi kwa Uongozi wa Afya wa Mkoa wa Manyara kupitia Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Damas Kayera mara baada ya kushika nafasi ya kwanza ngazi ya mikoa kwa kufanya vizuri zaidi katika utekelezaji wa afua za kupambana na kifua kikuu na ukoma.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akisema jambo kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi akisema jambo kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe akisema jambo kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma wakisikiliza mada zinazotolewa kwenye mkutano.
Wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma wakiwa katika picha ya pamoja.
***


Na Englibert Kayombo WAMJW - Dodoma
Serikali ya Tanzania imeazimia kutokomeza kabisa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuongeza uwezo wa ugunduzi wa wagonjwa wapya wa kifua kikuu na kuwaweka kwenye matibabu.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi alipokuwa akifungua mkutano wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu an Ukoma uliofanyika Jijini Dodoma.

“Uwezo wa nchi kugundua wagonjwa wapya na kuwaweka kwenye matibabu umeongezeka kutoka wagonjwa 62,908 (33%) mwaka 2015 na kwa sasa kufikia wagonjwa 82,166 (59%)” amesema Prof. Makubi

Kufuatia hatua hiyo Prof. Makubi amesema kuwa maisha ya wananchi takribani 300,000 ikiwemo ya watoto 45,000 yameponywa kwa kupatiwa dawa kwa wakati na kufuatiliwa kwa usahihi kuanzia mwaka 2015 hadi sasa.

Juhudi hizo pia zimeweka kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na kifua kikuu kwa 33%. “Mwaka 2015 kulikuwa na vifo 30,000 hivi sasa vimepungua hadi kufikia vifo 20,000” amesema Prof. Makubi.

Prof. Makubi amesema kuwa mafanikio hayo ya ongezeko la kasi ya ugunduzi wa wagonjwa wapya yametokana na mikakati mbalimbali iliyowekwa na Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma ikiwemo kuboresha huduma za ugunduzi wa TB na kutoa kipaumbele kwa makundi yaliyoathirika zaidi kama vile kaya zenye wagonjwa, wanaoishi kwenye kaya duni, gerezani, wachimbaji wadogo wadogo na kwa waathirika wa madawa ya kulevya.

“Aidha tumewekeza katika afua bunifu mbalimbali za matumizi ya teknolojia mpya za molekyula za kubaini TB kwa usahihi na kwa haraka” amesisitiza Prof. Makubi.

Awali akizungumza, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi amesema Wizara imefanya vizuri kwenye kwa kufikia malengo waliyoyaweka kwenye Mpango mkakati ambao unamalizika mwaka huu 2020.

“Malengo ambayo tulijiwekea ya kupunguza vifo vitokanavyo na kifua kikuu tumeweza kuyafikia pamoja na kupunguza madhaa yanayotokana na ugonjwa huo” amesema Dkt. Subi

Amesema kuwa Serikali imefanikiwa kuongeza vituo vya upimaji wa kifua kikuu sugu kutoka kituo 1 mwaka 2015 hadi kufika vituo 145 hivyo kuongeza wigo wa huduma za matibabu ya ugonjwa huo

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa Dkt. Ntuli Kapologwe amesema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana Wizara ya Afya katika kipindi cha miaka 5 ijayo imejiwekea mikakati ya kuwawezesha watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya ili wawe na ujuzi na uwezo wa kutambua na kutoa huduma kwa wagonjwa wa kifua kikuu.

Share:

TIMU YA WAZIRI MKUU YAKABIDHI MALI ZA SHIRECU ZILIZOPORWA. ..LIMO GHOROFA LA ILALA DAR

 

Mwenyekiti wa timu iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Shinyanga (SHIRECU) Asangy Bangu, (kulia), akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, Hati Saba za viwanja, pamoja na nyumba na ghala, ambazo ni mali tena za SHIRECU zilizokuwa zimeporwa na kuuzwa kinyume na taratibu.

Na Marco Maduhu - Shinyanga. 
Timu ya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, iliyoudwa kwa ajili ya kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliporwa na kuuzwa kinyume na utaratibu, imekabidhi baadhi ya mali na kumilikiwa tena na chama hicho.
Akikabidhi Hati za viwanja, pamoja na nyumba na ghala leo, Mwenyekiti wa timu hiyo Asangy Bangu, amesema wamefanikiwa kurudisha viwanja saba vilivyopo mkoani Shinyanga, nyumba ghorofa tatu ambayo ipo Ilala, pamoja na ghala lililopo Kurasini Jijini Dar es salaam, ambazo ni mali za Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU). 

Amesema zoezi hilo la kufuatili mali hizo za SHIRECU, walilifanya kwa kupitia nyaraka za chama hicho,pamoja na kuhoji watu ambao walikuwa wameuziwa wakiwamo watumishi wa Serikali na watu binafsi, na kufanikiwa kukomboa viwanja hivyo saba, ghala, pamoja na nyumba na kwamba wanaendelea kufuatilia mali zingine. 

"Leo tunakabidhi hati saba za mali za Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na taratibu, kuwa rasmi mali za chama hiki tena, na zoezi hili litakuwa endelevu ili kurudisha mali zote," amesema Bangu. 

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, ameipongeza timu hiyo kwa kufanya kazi kwa uzalendo, ambayo ilikuwa na mizengwe mingi, huku akiutaka uongozi wa SHIRECU, kuzitunza mali hizo na zisiweze kurudi tena mikononi mwa watu binafsi. 

Amesema zoezi hilo la kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), pamoja na vyama vingine ikiwamo Nyanza cha Jijini Mwanza, na KNCU cha Kilimanjaro, lilianza mwaka 2016, ambapo Rais Magufuli aliagiza mali hizo zifuatiliwe, ndipo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akaunda timu ya kufuatilia mali za vyama hivyo.

Ameongeza kuwa Jijini Mwanza tayari jana wameshakabidhi mali za Nyanza, na sasa wanaelekea mkoani Kilimanjaro kukabidhi mali za KNCU.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, ametaka watu ambao waliuza mali hizo za SHIRECU na kuisababishia hasara kubwa wawajibishwe, ili kuwa mfano kwa watumishi wengine ambao siyo waaminifu na kuuza mali za umma. 

Pia amekitaka chama hicho baada ya kupata mali hizo, kijiendeshe kibiashara pamoja na kukuza miradi yao kuinuka kiuchumi, ikiwamo na Shule ya Sekondari Buluba, kurudi kwenye hadhi yake ya kufaulisha wanafunzi kwa kuajiri walimu wazuri. 

Aidha Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU), mkoani Shinyanga Lenis Jishanga, ameishukuru timu hiyo kuwarudishia mali zao, na kuahidi kuzitunza pamoja na kujiendesha kibiashara zaidi. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mwenyekiti wa timu iliyoundwa na Waziri Mkuu kufuatilia mali za SHIRECU Asangy Bangu akitoa taarifa namna walivyofanikiwa kukomboa mali za chama hicho, likiwamo Ghorofa la Ilala Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akizungumza kwenye makabidhiano ya mali za SHIRECU.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, akizungumza kwenye makabidhiano ya mali za SHIRECU.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), Lenis Jishanga, akishukuru kupata mali hizo na kuahidi kuzitunza. 
Mwenyekiti wa timu iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufuatilia mali za Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Shinyanga (SHIRECU) Asangy Bangu, (kulia), akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, hati saba za viwanja, pamoja na nyumba na ghara, ambazo ni mali tena za SHIRECU zilizokuwa zimeporwa na kuuzwa kinyume na taratibu.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wa pili kushoto, akimkabidhi katibu mkuu wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, hati Saba za viwanja, nyumba na ghala, ambazo ni mali rasmi tena za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya, meza kuu akimkabidhi Mwenyekiti wa (SHIRECU) Lenis Jishanga, Hati saba za viwanja, nyumba na ghala, ambazo ni mali tena za chama hicho, wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, kushoto, akishikana mkono na mwenyekiti wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga Lenis Jishanga, mara baada ya kukabidhiwa mali za SHIRECU, ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Zainab Telack, kushoto, akishikana mkono na mwenyekiti wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga Lenis Jishanga, mara baada ya kukabidhiwa mali za SHIRECU, ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Wajumbe wakiwa kwenye makabidhiano ya mali za chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), ambazo ziliuzwa kinyume na utaratibu.
Picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi mali za Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU).

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:

HIACE YAPINDUKA NA KUUA WATU NANE BUKOBA


Watu wapatao nane wamepoteza maisha na wengine sita kujeruhiwa katika ajali ya gari la abiria lenye namba za usajili T.471 DCG linalofanya safari za kubeba abiria kutoka Kemondo kwenda Bukoba Mjini, baada ya gari hilo kufeli breki na kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea Novemba 22 saa 1:45 usiku na gari hilo aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T. DCG lilikuwa likiendeshwa na Ismail Rashid (37) mkazi wa Kemondo.

Via Mwananchi
Share:

RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA AFRIKA AFUNGIWA MIAKA MITANO



Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) Ahmad amepigwa marufuku (amefungiwa) miaka mitano na shirikisho la soka duniani Fifa kwa kukiuka sheria kadhaa za maadili.

Makamu huyo wa rais wa Fifa mwenye umri wa miaka 60 amedaiwa kukiuka sheria ya maadili inayohusisha jukumu lake la utiifu, kwa kutoa na kupokea zawadi hatua ambayo ni kinyume na wadhfa wake mbali na utumizi mbaya wa fedha.

Uchunguzi kuhusu tabia ya Ahmad kutoka mwaka 2017 hadi 2019 ulihusu masuala ya utawala wake katika shirikisho hilo pamoja na kuandaa na kufadhili safari ya kuhiji Mecca ya Umrah, kuhusishwa kwake katika kashfa ya kampuni ya vifaa vya michezo ya Tactical Steel na shughuli nyengine , ilisema taarifa ya Fifa.

Bwana Ahmad ambaye marufuku yake awali ilikuwa imetangazwa na BBCSport Africa , mwezi uliopita pia amepigwa faini ya $200,000.

Hapo awali alikana kufanya makosa yoyote.

Mwezi uliopita makamu huyo wa rais wa Fifa kutoka taifa la Madagascar alitangaza lengo lake kuwania muhula wa pili wakati uchaguzi wa Caf utakapofanyika mwezi Machi mwaka ujao.

Hilo huenda lisifanyike kwasababu atalazimika kupita mtihani wa maadili ili kustahiki kusalia katika baraza la Fifa.

Uwezekano wa yeye kuchaguliwa ka awamu ya pili utategemea iwapo atashinda kesi ya rufaa aliowasilisha katika mahakam ya kutatua mizozo ya michezo CAS , huku kesi hiyo akihakikisha kuwa inasikilizwa mapema ili kumruhusu kuthibitishwa kuwa mgombea.

CHANZO- BBC SWAHILI
Share:

Early Intervention Research Consultant at Sense International (EA)

Job Title:  Early Intervention Research Consultant     Location: Tanzania Terms of reference Identification and addressing barriers of scaling up sensory screening and early intervention services 1. About Sense International Sense International (EA) Tanzania was registered in Tanzania under the NGO Act, 2000 (registration certificate number 00NGO/0390) on 15th February 2008. Sense International Tanzania is part of […]

The post Early Intervention Research Consultant at Sense International (EA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Executive Director at Toa Nafasi Project

Executive Director     ABOUT THE ROLE The Toa Nafasi Project is currently recruiting a new Executive Director to lead the organization into its next phase of existence. We are seeking a passionate, committed, and creative leader who will ensure that programs are running in a timely and impactful manner, that fundraising is maintained to keep […]

The post Executive Director at Toa Nafasi Project appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Online Writer at Scooper News Tanzania

Online Writer Scooper News Job Summary Online English & Swahili content writer for Scooper News Tanzania, home office, must own a computer/laptop. Description/Requirements WE ARE HIRING   Part-time/Intern Online Writer We are fun, we are youthful, we are ambitious. We need self-assured and vibrant individuals who are eager to learn, explore, manage and contribute to […]

The post Online Writer at Scooper News Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Programs Officer at Focus Africa Tanzania

Programs Officer (Reproductive Health and Adolescents)-Tanzania Focus Africa Job Summary The position holder will work closely with diverse teams to formulate and implement specific activities in the annual work plan for the Network in accordance to Focus Africa contractual obligations and internal policies and procedures and provide technical design and management of Sexual Reproductive Health Main […]

The post Programs Officer at Focus Africa Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Centrifugal Operator at Mtibwa Sugar Estates Limited

Centrifugal Operator Mtibwa Sugar Estates Ltd Job Summary Operates centrifugal machines to separate and wash molasses and mother liquor from sugar crystals: Opens gate allowing sugar mass to flow into centrifuge basket and other responsibilities as follows Qualification:   Diploma holder in Mechanical Engineering Diploma holder in Electrical Engineering Diploma holder in Electronic Engineering   […]

The post Centrifugal Operator at Mtibwa Sugar Estates Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MCHEZA MIELEKA MAARUFU UNDERTAKER AJIUZULU WWE



Mchezaji maarufu wa mchezo wa mieleka- Undertaker 

Mchezaji maarufu wa mchezo wa mieleka- Undertaker amethibitisha rasmi kujiuzulu kutoka WWE baada ya miaka 30.

Aliingia ulingoni kwa mchezo wa mwisho katika mchezo wa mwisho wa Survivor Series Jumapili usiku, ambapo aliuhutubia umma wa mashabiki wa WWE Universe kwa mara ya mwisho.

Wakati wa hotuba yake, Undertaker ambaye jina lake halisi ni Mark Calaway –alieleza ni kwanini ameamua kujiuzulu.

"Kwa miaka 30 nimekuwa nikiingia ndani ya ulingo huu taratibu na kuwaangusha watu mara kwa mara," alisema.

"Sasa wangu muda umefika. Muda wangu umefika wa kumuacha Undertaker apumzike... kwa ... amani."

Calaway anajiuzulu akiwa ndiye mchezaji bora wa WWE kuwahi kushuhudiwa katika mashindano hayo na amekuwa ulingoni kwa miongo mitatu na atakumbukwa na mashapiki wake daima.

Chanzo - BBC

Share:

VSO YATOA VIFAA KWA WAHITIMU VETA WAKAJIAJIRI WENYEWE

 

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Shirika la Voluntary Services Overseas (VSO), limetoa vifaa kwa wahitimu wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stadi VETA mkoani Shinyanga, ambao walikuwa wakiwafadhili kupata mafunzo chuoni hapo, kwa ajili ya kwenda kujiajiri wenyewe na siyo kutegemea kuajiriwa.

Zoezi la kukabidhi vifaa hivyo lilifanyika kwenye chuo hicho cha ufundi stadi VETA, ambapo wahitimu hao walikuwa wamesomea fani za mapishi, Saluni, Mapambo, Mabomba, Aluminium, umeme, na ufundi pikipiki. 

Mratibu wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam Katanga, ambao wanajishughulisha na masuala ya kijamii Kanda ya Ziwa, alisema kuwa wamefadhili mafunzo ya ufundi Stadi kwa vijana 200 kutoka mkoani Shinyanga ili kuwapatia ujuzi na kuendesha maisha yao. 

"Shirika letu baada ya kufadhili vijana hawa mafunzo ya ufundi na kuhitimu, tukaona ni vyema kuwaunga kwenye vikundi vya ujasiriamali na kuvisajili, na kuwapatia vifaa ambavyo wataanza navyo kujiajiri wenyewe kulingana na fani zao," alisema Katanga. 

“Vifaa ambavyo tumetoa ni vya Mapishi, Saluni, ushonaji zikiwamo cherehani, ufundi umeme, Aluminium, Mapambo, Mabomba, na pikipiki, ambavyo vijana hawa vitawasaidia kuanzisha shughuli zao na kujipatia kipato, kuliko kurudi nyumbani kukaa kusubiri ajira na hatimaye kupoteza ujuzi wao,”aliongeza. 

Naye Afisa Vijana kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Ruchagula, aliwataka vijana hao licha ya kusajili vikundi vyao, wasisite kwenda kuomba mkopo halmashauri fedha za asilimia 10, ambazo nne kwa vijana zitakazowasaidia kupanua mitaji yao. 

Kwa upande wake Msajili wa wanafunzi Chuo cha Ufundi stadi VETA mkoani Shinyanga Rashid Ntahigiye, aliwataka vijana hao wanapoingia kwenye Soko la kujiajiri wenyewe, wakawe wabunifu kwenye utengenezaji wa bidhaa zao, ili wafanikiwe kupata wateja wengi na kuinuka kiuchumi. 

Nao baadhi ya wahitimu hao akiwamo Magreth Zabron aliyesomea fani ya saluni, walishukuru Shirika hilo kuwafadhili mafunzo hayo pamoja na kuwapatia vifaa vya kuanza kazi, na kuahidi kwenda kujituma kuchapa kazi kwa ajili ya mustakabali wa maisha yao, na hawato waangusha. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 
Mratibu wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam Katanga, akikabidhi vifaa kwa wahitimu wa fani ya ushonaji kwa ajili ya kwenda kujiajiri wenyewe.
Mratibu wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam Katanga, akikabidhi vifaa kwa wahitimu wa fani ya Aluminium, ili kwenda kujiajiri wenyewe.
Mratibu wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam Katanga, akikabidhi vifaa kwa wahitimu wa fani ya mapambo na salooni ili kwenda kujiajiri wenyewe.
Zoezi la kubidhi vifaa likiendelea.
Zoezi la kubidhi vifaa likiendelea , kwa wahitimu wa fani ya mapishi.
Watendaji wa shirika la VSO, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Serikali manispaa ya Shinyanga na chuo cha ufundi stad VETA Mkoani Shinyanga, wakwati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa wahimitu wa fani mbalimbali chuoni hapo. waliofadhiliwa masomo yao na VSO.
Picha ya pamoja wahitimu wa VETA, watendaji wa Shirika la VSO, watumishi wa Serikali na VETA.
Mratibu wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam Katanga, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi vifaa kwa wahitimu wa mafunzo VETA.
Msajili wa wanafunzi chuo cha ufundi stadi VETA mkoani Shinyanga Rashidi Ntahigiye, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi vifaa kwa wahitimu chuoni hapo waliofadhiliwa mafunzo yao na Shirika la VSO.
Afisa vijana kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Ruchagula, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa vifaa wahitimu VETA.
Afisa mtendaji wa Kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga Joshua Masengwa, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Afisa maendeleo Kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga Wema Mashaka, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa vifaa wahitimu wa VETA.
Wahitimu wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stadi VETA Mkoani Shinyanga waliofadhiliwa masomo yao na Shirika la VSO, wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa kwa ajili ya kwenda kujiajiri.
Wahitimu wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stad VETA Mkoani Shinyanga waliofadhiliwa masomo yao na Shirika la VSO, wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa kwa ajili ya kwenda kujiajiri.
Wahitimu wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stadi VETA Mkoani Shinyanga waliofadhiliwa masomo yao na Shirika la VSO, wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa kwa ajili ya kwenda kujiajiri.
Wahitimu wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stad VETA Mkoani Shinyanga waliofadhiliwa masomo yao na Shirika la VSO, wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa kwa ajili ya kwenda kujiajiri.
Wahitimu wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stad VETA Mkoani Shinyanga waliofadhiliwa masomo yao na Shirika la VSO, wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa kwa ajili ya kwenda kujiajiri.
Wahitimu wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stadi VETA Mkoani Shinyanga waliofadhiliwa masomo yao na Shirika la VSO, wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa kwa ajili ya kwenda kujiajiri.
Wahitimu wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stadi VETA Mkoani Shinyanga waliofadhiliwa masomo yao na Shirika la VSO, wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa kwa ajili ya kwenda kujiajiri.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger