Friday 2 October 2020

Picha : TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) YAKUTANA NA WADAU WA UCHAGUZI SHINYANGA… ‘YAONYA UVUNJIVU WA AMANI KWA KISINGIZIO CHA UCHAGUZI’



Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania (NEC) imekutana na wadau wa Uchaguzi mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Oktoba 28,2020.

Mkutano huo uliofanyika leo Ijumaa Oktoba 2,2020 Mjini Shinyanga umefunguliwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini, Baraza la Wazee,wawakilishi wa watu wenye ulemavu,vijana,wanawake,asasi za kiraia na waandishi wa habari.

Akizungumza, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard alivikumbusha vyama vya siasa na wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kampeni zao ikiwemo kuepuka lugha za kashfa,maneno ya uchochezi yanayotishia usalama na amani ya nchi.

“Tume inasisitiza vyama vya siasa na wagombea kuhakikisha wanaepuka kufanya kampeni zinazoashiria ubaguzi katika misingi ya jinsi,ulemavu,ukabila,udini,maumbile au rangi”,alisema Leonard.

Aidha alibainisha kuwa wakati tume inaendelea kuratibu na kusimamia na kuendesha uchaguzi kwa kutumia sheria za uchaguzi ni vyema vyama vya siasa,wagombea na wananchi waelewe kuwa sheria zingine za nchi hazijasimama hivyo wajihadhari na vitendo ama matamshi ambayo yanaweza kusababisha vurugu kwa kisingizio cha uchaguzi.

“Tume inawahakikishia kuwa itasimamia uchaguzi mkuu 2020 kwa kuzingatia Katiba,sheria,kanuni na taratibu zinazosimamia uendeshaji wa uchaguzi.Lengo ni kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru,wa wazi,haki na wa kuaminika kwa kuweka mazingira sawa ya ushindani kwa wagombea na vyama vyote vinavyoshiriki”,alisema Leonard.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa uchaguzi kufikisha ujumbe sahihi kuhusu uchaguzi kwa wananchi ili kila mwenye sifa ya kupiga kura ajitokeze na kadi yake kupiga kura katika kituo alichojiandikisha ili kutimiza haki yake ya msingi ya kikatiba.

“Pamoja na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo kuna jumla ya wapiga kura 29,188,347, tume imefanya maandalizi mengine muhimu kama vile marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020 na Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani za mwaka 2020”,alisema.

Alieleza kuwa Tume ya uchaguzi kwa kushirikiana na serikali na vyama vya siasa waliandaa Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020.

“Maandalizi mengine ni manunuzi ya vifaa na uchapishaji wa nyaraka mbalimbali zikiwemo Fomu,maelekezo kwa watendaji wa uchaguzi na maelekezo kwa vyama vya siasa na wagombea,miongozo ya elimu ya mpiga kura na mwongozo wa watazamaji wa uchaguzi”,aliongeza Leonard.

Alieleza kuwa tayari Tume imekamilisha mafunzo ya watendaji wa uchaguzi wakiwemo waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi,wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi, maafisa uchaguzi wa halmashauri na maafisa Tehama na kwamba mafunzo yaliyobaki ni kwa watendaji wa vituo.

Leonard alisema jumla ya wagombea wa vyama vya siasa 15 wameteuliwa na Tume ya uchaguzi kugombea nafasi ya Urais na imetoa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura kwa asasi za kiraia 245 kwa Tanzania Bara na Asasi za kiraia 7 kwa Tanzania Zanzibar.

“Tume ya uchaguzi pia imeruhusu Watazamaji wa ndani na nje katika uchaguzi mkuu 2020 ambapo imetoa vibali kwa asasi za kiraia na taasisi 97 za ndani na vibali kwa makundi 16 ya watazamaji wa nje”,alisema Leonard.

“Ushirikishwaji mwingine wa wadau ni kupitia mawakala wa vyama vya siasa kwani siku ya uchaguzi vyama vya siasa vimepewa nafasi ya kuweka wakala katika kila kituo cha kupigia kura. Wakala atakuwepo kituoni kwa ajili ya kuangalia taratibu za uchaguzi zinavyoendeshwa kituoni na kama zinazingatia sheria,kanuni,taratibu na maelekezo ya tume. Lengo kubwa ikiwa ni kulinda maslahi ya chama na wagombea”,alifafanua Leonard.

Akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020, Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa alisema tume imekamilisha uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ambapo hivi sasa kuna jumla ya wapiga kura 29,188,347 ambapo wapiga kura 29,059,507 wapo Tanzania Bara na 128,840 wapo Tanzania Zanzibar.

Aliongeza kuwa pia kuna jumla ya wapiga kura 566,352 walioandikishwa na ZEC ambao watashiriki kupiga kura ya kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kati ya wapiga kura 29,188,347 walioandikishwa wanawake ni 14,691,743 ambao ni sawa na 50.33%, wanaume ni 14,496,604 ambao ni sawa na 49.67%. Vijana kati ya umri wa miaka 18-35 ni 15,650,998 (vijana wa kiume ni 7,804,845, wa kike 7,846,153). Aidha kuna jumla ya watu wenye ulemavu 13,211 na kati yao 2,223 wana ulemavu wa macho, 4,911 wana ulemavu wa mikono na 6,077 wana ulemavu wa aina nyingine”,alifafanua Nuru.

Aliongeza kuwa tume itatumia vituo vya kupigia kura 80,155 katika zoezi la kupiga kura Oktoba 28,2020,kati ya vituo hivyo Tanzania Bara itakuwa na vituo 79,670 na Tanzania Zanzibar itakuwa na vituo 485.Vile vile tume itatumia vituo 1,412 vya ZEC kwa upande wa Tanzania Zanzibar.Kila kituo kati ya hivyo,kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500.

Alisema idadi ya majimbo ya uchaguzi mkuu 2020 ni 264 ambapo Tanzania Bara ina majimbo 214 na Tanzania Zanzibar ina majimbo 50 na kata zitakazotumika katika uchaguzi mkuu 2020 ni 3,956.

 Katika hatua nyingine alisema kwa mara ya kwanza katika uchaguzi mkuu 2020 vyama vya siasa vimesimamisha wagombea wengi wa kiti cha Rais hali inayoashiria ukuaji wa demokrasia nchini Tanzania.

"Tume ya uchaguzi imeteua wagombea wa kiti cha Rais/Makamu wa Rais kutoka vyama 15 vya siasa. Katika uteuzi huo wanawake wawili walijitokeza na kuteuliwa kugombea kiti cha Urais na wanawake watano walijitokeza na kuteuliwa kugombea nafasi ya Makamu wa Rais",alifafanua Nuru

Kwa upande wao wadau wa uchaguzi walioshiriki mkutano huo waliipongeza tume ya taifa ya uchaguzi kwa kukutana nao huku wakieleza kukerwa na baadhi ya kauli zinazotolewa na baadhi ya wagombea kwenye mikutano ya kampeni na kuiomba tume ya taifa ya uchaguzi na serikali kuchukua hatua dhidi yao ili kulinda amani ya nchi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Oktoba 2,2020 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna katika Manispaa ya Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga George Bangili akifuatiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi na Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga. Wa kwanza kulia ni Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Reteti Molloimet akifuatiwa na Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Oktoba 2,2020 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga George Bangili akifuatiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi na Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga. Wa kwanza kulia ni Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Reteti Molloimet akifuatiwa na Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard akisisitiza jambo kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga. Alisema wakati tume inaendelea kuratibu na kusimamia na kuendesha uchaguzi kwa kutumia sheria za uchaguzi ni vyema vyama vya siasa,wagombea na wananchi waelewe kuwa sheria zingine za nchi hazijasimama hivyo wajihadhari na vitendo ama matamshi ambayo yanaweza kusababisha vurugu kwa kisingizio cha uchaguzi.
Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020  kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020  kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020  kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020  kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga. kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Kushoto ni Katibu wa Chama cha Watu wenye Ualbino Mkoa wa Shinyanga, Lazaro Anael akitoa msaada wa lugha ya alama kwa watu wenye ulemavu wa kutosikia (Viziwi) waliohudhuria mkutano wa wadau wa Uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga,  Soud Suleiman Kategile akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la KKKT Shinyanga na Simiyu,Trafaina Nkya akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Katibu Mwenza wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga, Khalfan Ally akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Padre Simon Maneno kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Askofu  Raphael Machimu ambaye ni Katibu wa Kamati ya Amani mkoa wa Shinyanga, akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Mdau wa Uchaguzi, Japhet Bulugu kutoka Brotherhood group akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani mkoa wa Shinyanga, Sheikh Balilusa Khamis akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Mdau wa uchaguzi Jonathan Kifunda Manyama kutoa shirika la Thubutu Africa Initiatives akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Mwandishi wa habari wa Channel Ten, John Mponeja akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Mdau wa uchaguzi George Nyanda kutoka shirika la Rafiki SDO akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Mdau wa uchaguzi, John Myola kutoka Shirika la AGAPE ACP akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu mkoa wa Shinyanga, Richard Mpongo akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi mkoa wa Shinyanga, Justine Shindai akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Kushoto ni Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Reteti Molloimet na Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa wakiwa kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa Baraza la Wazee Mkoa wa Shinyanga, Anderson Lyimo akichangia hoja kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano  ulioandaliwa na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kupeana taarifa mbalimbali za mchakato wa uchaguzi na kujadiliana namna bora ya kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga George Bangili,Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi,Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga.,Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Reteti Molloimet  na Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa wakipiga picha ya pamoja na Wawakilishi wa viongozi wa dini baada ya kufunga mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga George Bangili,Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi,Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga.,Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Reteti Molloimet  na Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa wakipiga picha ya pamoja na Wawakilishi wa Baraza la wazee mkoa wa Shinyanga baada ya kufunga mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga George Bangili,Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi,Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga.,Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Reteti Molloimet  na Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa wakipiga picha ya pamoja na Wawakilishi wa wanawake baada ya kufunga mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga George Bangili,Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi,Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga.,Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Reteti Molloimet  na Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa wakipiga picha ya pamoja na Wawakilishi wa vijana baada ya kufunga mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga George Bangili,Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi,Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga.,Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Reteti Molloimet  na Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa wakipiga picha ya pamoja na Wawakilishi wa watu wenye ulemavu baada ya kufunga mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga George Bangili,Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi,Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga.,Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Reteti Molloimet  na Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa wakipiga picha ya pamoja na Wawakilishi wa Asasi za kiraia baada ya kufunga mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga George Bangili,Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi,Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga.,Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Reteti Molloimet  na Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa wakipiga picha ya pamoja na Wawakilishi wa Waandishi wa Habari baada ya kufunga mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Baraka Leonard, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga George Bangili,Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi,Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabian Kamoga.,Afisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Reteti Molloimet  na Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuru Riwa wakipiga picha ya pamoja na Wawakilishi wa Waandishi wa Habari baada ya kufunga mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

MGOMBEA URAIS DR. JOHN POMBE MAGUFULI KESHO KUUNGURUMA ZANZIBAR..WASANII KIBAO WATAKUWEPO


JPM ndani ya Zanzibar. Mgombea Urais Kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli Kesho Jumamosi Oktoba 03, 2020 ataunguruma Visiwani Zanzibar Kwenye Mwendelezo wa Kampeni za Kunadi Sera bora za CCM, Ilani na Kuomba Kura Kwenye Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar. Mitambo imehamia Zanzibar. Diamond Platnumz na Wasanii wengine wengi Watakuwepo. #T2020JPM
Share:

Mradi wa Umeme waPamoja wa Tanzania, Burundi, Rwanda Wafikia Pazuri

 






Share:

AIRO AWASHUKIA WANAODAI HAMUUNGI MKONO CHEGE....ASEMA NI NJAMA ZA WAPINZANI KUWACHONGANISHA WANA CCM


Lameck Airo akiwazawadia watoto waliokuwa wakicheza ngoma ya utamaduni


Na Dinna Maningo,Rorya
Kitendo cha Makada wa CCM wilayani Rorya na waliokuwa wametia nia ya ubunge kuzidi kumwombea kura mgombea Ubunge jimbo la Rorya mkoani Mara Jafari Chege kimezidi kuwaweka njia panda vyama vya upinzani hali ambayo imesababisha baadhi kufanya uchonganishi wenye lengo la kukisambalatisha kikosi kinachoomba kura kwa wananchi.

Imeelezwa kuwa kuna baadhi ya wapinzani wamekuwa wakieneza uvumi kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo wa Rorya Foram na kwa Chege kuwa aliyekuwa mbunge wa Rorya kupitia CCM Lameck Airo na Baadhi ya Watiania akiwemo Francis Olwero hawamuungi mkono Jafari huku wakishawishi Jafari awapige chini baadhi ya wanaomwombea kura akiwemo Airo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni za mgombea Udiwani kata ya Nyamtinga Charles Chacha katika kijiji cha Nyarombo,aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo na mgeni rasmi katika uzinduzi huo Lameck Airo alisema kuwa njama hizo zinasukwa na wapinzani kwa lengo la kuwadhoofisha kisiasa ili wapinzani wapate mwanya kushinda kwenye uchaguzi.

"Wanasema kwamba mimi sizunguki na Chege lakini kuna maeneo tumekuwa tukifanya kampeni tukiwa na Chege na wananchi ni mashahidi na hata maeneo ambayo tunapiga kampeni bila kuwa na Chege bado tukisimama jukwaani tunamwombea kura Chege na wagombea wengine wa CCM tunatumia gharama zetu kuzunguka.

Aliongeza" huo mtandao wa Rorya Foram una wapinzani wengi na ndiyo hao walisema wanataka mgombea msomi,CCM kwakuwa ni chama kinachosikiliza maoni ya watu wakamleta Chege lakini bado watu wanaendelea kutuchonganisha na Chege ili tuchukiane na tukichukia watia nia wakasirike waache kupiga kampeni abaki Jafari mwenyewe, akibaki yeye mwenyewe inakuwa ni njia rahisi kwa wapinzani kupenya."alisema Airo.

Airo alisema kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi yatasemwa mengi lakini hayatamkatisha tamaa nakwamba atapambana kuhakimisha CCM inashinda ambapo alisema atatafuta kura kwa kutumia njia mbalimbali zikiwemo za kupiga kampeni za chini kwa chini.

"Mimi siyo  mtu wa majukwaani hata nisipoongozana na Chege nina mbinu zangu nyingi za kupiga kampeni,mimi napiga kampeni za chini kwa chini,kampeni za usiku,kampeni za vikundi mimi ndiyo Airo CCM tutashinda tuu,maneno ya wapinzani kwenye mitandao ya kijamii hayanisumbui nayasikia nayapuuza sisi tunapambana kutafuta kura na siyo manenomaneo" alisema Airo.

Airo alisema kuwa ataendelea kumuunga mkono Chege" mimi nilikuwa spidi 100 Chege ataenda spidi 500 kwanza ana elimu ana nafasi yakuwa Waziri,mimi ni elimu ya la saba nilikuwa nimebania Rorya nafasi ya uwaziri kwa miaka 10 tuombe Mungu tushinde kwa kishindo ili Rais wetu akiona basi atupe upendeleo Rorya Chege awe Waziri"alisema Airo.

Akimwombea kura mgombea Udiwani kupitia chama hicho Charles Chacha anayetetea kiti hichi aliwaomba wananchi kumchagua Chege  na Chacha bila kumsahau Rais Magufuli kwa kile alichoeleza kuwa Serikali ya awamu ya tano imefanya maendeleo mengi na wananchi ni mashahidi.

Akizungumza na Malunde 1Blog mtiania ya ubunge ambaye kura zake hazikutosha Francis Olwero alisema"Kumekuwa kukienezwa habari za uzushi kuwa mimi namshika miguu Chege nimepewa milioni 15 na wapinzani kumwangusha,ni uongo mtupu mimi tangu kampeni zimeanza tuko na wenzangu tumeacha familia zetu Dar na kazi zetu kwa ajili ya kupambana kumwombea kura Chege.

Aliongeza" hizi ni njama za wapinzani na baadhi ya wana CCM wanaokishika chama miguu kutaka  tukate tamaa kumwombea kura mwenzetu, wanatushonganisha nae,sitakata tamaa maana nilisema nitamwombea kura mwenzangu Dar nitaenda na matokeo ya ushindi wa Chege, kwenye kampeni yanasemwa na yatazushwa mengi wao waendelee kusema kama nilipewa pesa waje  kwenye chama watoe ushahidi"alisema Olwero.

Mgombea Udiwani kata ya Nyamtinga Charles Chacha aliwaomba wananchi kumchagua tena ili aendelee kufanya maendeleo huku akiwaeleza mambo mbalimbali aliyoyafanya akiwa Diwani miaka mitano iliyopita.

"Kata yangu tumefanya maendeleo mengi kwa michango ya harambee tumejenga maboma 4 ya shule ya Sekondari matundu 30 ya vyoo katika shule zetu,tulipokea fedha milioni 175 za maendeleo,tumejenga nyumba za walimu,shule ya Rwang'enyi tumejenga madarasa 3,ofisi ya walimu nakupeleka milioni 7,mradi wa maji Nyarombo wa milioni 847,kijiji cha Manila madarasa 4 mradi wa umeme wa Rea uliogharimu milion 250" alisema Chacha.

Baadhi ya wagombea udiwani kata mbalimbali na wagombea udiwani viti maalumu walimwombea kura Chacha huku wakimwagia sifa kutokana na maendeleo aloyoyafanya akiwa Diwani.

Mwenyekiti wa CCM kata ya Nyamtinga Galus Oyieko alimwomba Airo kuwatengenezea barabara ya kutoka Mwalango hadi Rwang'enyi na alimtaka mgombea udiwani atakaposhinda ahakikishe anatoa hoja halmashauri ili ujenzi wa shule ya Sekondari Rwang'enyi ukamilike kwa wakati.


Walioketi mbele, kulia ni Mgombea Udiwani Kata ya Nyamtinga Charles Chacha katikati ni Lameck Airo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Rorya wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za mgombea udiwani
Kushoto ni Lameck Airo akimnadi mgombea udiwani kata ya Nyamtinga Charles Chacha
Kikundi cha kwaya kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea Udiwani kata ya Nyamtinga
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea udiwani
Wana CCM wakimpongeza mkazi wa Nyamtinga aliyekuwa akiigiza kusoma taarifa ya habari
Share:

Polisi Dar es Salaam wasitisha wito wa kumuita Tundu Lissu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM leo October 2, 2020, limesitisha wito wa kumtaka mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania CHADEMA Tundu Lissu kufika kituo cha polisi na badala yake kuendelea na ratiba za kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
 
Jana Alhamisi tarehe 1 Oktoba 2020, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, lilimuandikia barua ya wito Lissu likimtaka afike katika ofisi zake leo Ijumaa saa 3:00 asubuhi kujibu tuhuma zake. 
 
Leo tarehe 2 Oktoba 2020, SACP Lazaro Mambosasa,  Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, amesema jeshi hilo limesitisha wito wake kwa Lissu likidai, limeona busara Lissu aendelee na ratiba yake.

“Jeshi la Polisi limesitisha wito huo na kumtaka Tundu Lissu kuendelea na kampeni zake za Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.”

“Jeshi la polisi limeona ni vema kutumia busara kumuacha Lissu kuendelea na ratiba zake kipindi hiki cha kampeni na kwa kuwa tayari IGP Sirro alishatoa maelekezi kwa Lissu kuripoti Kituo cha Polisi Moshi Mkoa wa Kilimanjaro. Hivyo Jeshi la Polisi Kanda Maalum limesitisha wito huo,” amesema Kamanda Mambosasa. 

 



Share:

SHIRIKA LA UWO KUTOA FARAJA KWA WAHANGA WA AJALI NCHINI

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo kuwa ya Kiserikali ya Utu Wangu Organization (UWO) Fatuma Mgeni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mjini hapa jana kuhusu kuanzishwa kwa Asasi hiyo yenye makao makuu yake mkoani Singida. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo kuwa ya Kiserikali ya Utu Wangu Organization (UWO) Fatuma Mgeni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) huku akionesha mguu uliojeruhiwa katika ajali aliyoipata Kibaha kwa Mathias mkoani Pwani Desemba 5, 2018.

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo kuwa ya Kiserikali ya Utu Wangu Organization (UWO) Fatuma Mgeni,akifanya mazoezi ya kutembea akiwa nyumbani kwake Singida.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyo kuwa ya Kiserikali ya Utu Wangu Organization (UWO) Fatuma Mgeni, akionesha cheti cha usajili wa Asasi yake ya  Utu Wangu Organization (UWO) kwa waandishi wa habari.



Na Dotto Mwaibale, Singida.


WAHANGA wa ajali hapa nchini ambao wanakosa huduma baada ya kutelekezwa ama kutokuwa na ndugu wataanza kupatiwa msaada wa hali na mali kutoka Asasi isiyo kuwa ya Kiserikali ya Utu Wangu Organization (UWO) yenye makao makuu yake mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo Fatuma Mgeni ambaye ni mhanga wa ajali na Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Mkoa wa Pwani, Mkufunzi, Mwamuzi na Kocha wa Mchezo wa Mpira wa Meza (Table Tennis)  ngazi ya kwanza ya Dunia, alisema jamii bado ipo nyuma kusaidia wahanga wa ajali ambao wanakosa msaada na kuiachia Serikali ambayo ina majukumu mengi.

"Suala la kuwasaidia wahanga wa ajali lipo ndani ya uwezo wa wanajamii wenyewe kikubwa ni jamii kuhamasika na kuwa na moyo wakusaidia wahanga hao" alisema Mgeni.

Alisema lengo la kuanzisha asasi hiyo ni baada ya kupata ajali Kibaha kwa Mathias na kujeruhiwa vibaya mguu wake wa kulia na kukaa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha karibu mwaka mmoja tangu Desemba 5,  2018  hadi leo akipatiwa matibabu ingawa yupo nje ya hospitali.

Mgeni alisema akiwa hospitalini ndipo aliona changamoto ya maisha ya wahanga wa ajali ambao walikuwa hawana msaada baada ya kutelekezwa na jamaa zao na wengine kutokuwa na ndugu kabisa licha ya kupatiwa matibabu.

"Niliguswa na jambo hili nikaona nianzishe asasi hii kwa ajili ya kutoa matumaini kwa wahanga hao kwa kushirikiana na jamii ikiwa ni kumuunga mkono Rais Dkt.John Magufuli za kuboresha huduma katika sekta ya afya na kuhakikisha wahanga hao wanapata haki zao kutokana na majanga walioyapata na kuwa na afya bora ili waweza kurudi katika afya zao za zamani na kuweza kufanya shughuli za maendeleo na kuinua uchumi wao binafsi na Taifa kwa ujumla."  alisema Mgeni.

Mgeni alisema kumekuwa na dhana potofu kuwa wahanga wa ajali ni lazima wasaidiwe mahitaji yote na Serikali wakati kumbe jamii ikielimishwa inaweza kuwa sehemu ya kutoa faraja kwa wahanga hao  kwa kupambana na changamoto zao kuanzia pale wanapopata ajali mpaka kupona kwao wakiwa wazima au  na ulemavu uliotokana na ajali.

Aidha Mgeni alisema changamoto kubwa iliyopo ni kwa jamii kuwa nyuma katika jambo hilo ambapo imefikia baadhi ya watu kuwatelekeza wagonjwa hospitali na majumbani na kuwaacha wakiteseka na kukosa  matumaini ya maisha.

Alisema kupitia Shirika hilo ambalo limesajiliwa na litakuwa likifanya kazi mikoa yote Tanzania Bara litakuwa likijihusisha zaidi kwa ajili ya kuhamasisha jamii kwa ajili ya kuwasaidia wahanga hao wa ajali.

Mgeni alitumia nafasi hiyo kuwa pongeza madaktari na wauuguzi na wafanyakazi wote wa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha kwa jitihada zao kubwa za kitabibu wanazo zitoa kwa jamii hasa kwa watu wanaofikishwa katika hospitali hiyo baada ya kupata ajali kwa kuwapa matibabu kwanza bila ya kuwadai fedha na kuwa ana amini hata hospitali zingine hapa nchini zinafanya utaratibu huo.

Share:

Mgombea ubunge jimbo la Bariadi Mhandisi Andrea Kundo aahidi kumaliza changamoto ya tembo kuvamia makazi.

Samirah Yusuph,Mwananchi
Bariadi, Mgombea ubunge jimbo la Bariadi Mhandisi Andrea Kundo, Ameahidi kumaliza kero ya wanyama( tembo ) kuvamia makazi ya wakazi wa kata ya Gilya na Gibeshi katika wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Mhandisi Kundo aliyasema hayo jana alipo kuwa katika mkutano wa kuomba kura kwa wananchi wa kata hizo na kusema kuwa changamoto ya Tembo kuvamia makazi imakuwa ni ya muda sasa hivyo ni muda muafaka kuweza kuimaliza.

Aliongeza kuwa licha ya uwepo wa juhudi za kuhakikisha tembo hao hawaingii kwenye makazi lakini inabidi kuongeza nguvu ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama muda wote.

"Kumekuwa na tembo ambao wamekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi sababu wanaharibu mazao wakati wa mavuno na hata kusababisha vifo, hivyo nitahakikisha magari ya doria za polisi yanakuwa mengi maeneo haya ili tembo waweze kudhibitiwa kuingia katika makazi," alisema Mhandisi Kundo.

Jambo ambalo wananchi wa kata hizo wamelitaja kuwa ni licha ya uwepo wa changamoto zingine lakini hilo ni tatizo kubwa zaidi kwani uvamizi wa wanyama hao kwenye makazi unawaachia balaa la njaa.

Hali inayopelekea mazao yao wanayo vuna kutoka mashambani kwenda kuyahifadhi vijiji vya nkololo na Ihusi umbali wa zaidi ya kilometa 15 ili kuwakepa wanyama hao kwani wanapoingia vijijini wanavunja nyumba na kula mazao yote wanayoyakuta.

Hivyo njia hiyo ya kuhifadhi vijiji vya jirani inafanya mazao yabaki salama lakini changamoto inakuja pale wanapohitaji chakula kutokana na umbali uliopo kwenda kuvifata vyakula vyao kwa ajili ya familia zao.

"Tembo anapo vamia kwenye kaya anabomoa nyumba na anakula chakula chote anachokikuta wanakula michembe, mahindi hata unga na ni ngumu kwafukuza na wengine ni wabishi akigoma kuondoka inabidi wewe ndiye umkimbie," Alisema Monwa Kilatu mkazi wa kata Ihula.

Kwandu Maluguabili alieleza hali anayokutana nayo wanyama hao wanapofika katika makazi yake "Nyumbani nilipoweka mahindi huwa wanakuja kubomoa nyumba wanakula chakula na kuharibu kila wanachokutana nacho lakini baada ya kuwa hatuna chakula hatupati msaada wowote hivyo tunabaki bila chakula".

Wahanga hao walisema kuwa wanahitaji msaada wa serikali ili kuweza kuwadhibiti wanyama hao kwa sababu juhudi zao zinagonga amwamba kutokana na namna ambavyo wamekuwa wakiwafukuza kienyeji hali inayosababisha mapambano kati yao na kusababisha vifo kwa baadhi ya vijana wao.

Tangu mwaka 2017 tembo walinza kupita katika vijiji vya kata hizi wakiwa wanatafuta njia, na tangu waka 2018 wanyama hawa walianza kuvamia makazi nyakati za usiku na kufanya uharibifu katika makazi.

Mwisho.


Share:

TARURA yatekeleza ahadi za Magufuli


Na. Erick Mwanakulya, Kagera.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), unaendelea kutetekeleza miradi ya Ahadi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kukamilisha ujenzi wa Barabara zenye urefu wa Km 2.76 kwa kiwango cha lami katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, Meneja wa TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Mhandisi Dativa Telesphory alifafanua kuwa utekelezaji wa miradi ya Ahadi za Mhe. Rais umekamilika kwa asilimia 100 baada ya ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami kukamilika na kuanza kutumika.

“Kabla ya TARURA kuanzishwa, Wilaya ya Muleba haikuwa na lami hata Mita 1 lakini hadi sasa kupitia kuanzishwa kwa Wakala na pia utekelezaji wa miradi ya Ahadi za Mhe. Rais tumetekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Km 2.76 ambazo zimekamilika na wananchi wameanza kunufaika na ujenzi wa barabara hizi”, alisema Mhandisi Dativa.

Mkazi wa Muleba Bi. Edvina Jackson ameishukuru Serikali kwa kutengeneza barabara za lami kwenye eneo lao ambalo lilikuwa limesahaulika kwa muda mrefu kwani kwa kiasi kikubwa ujenzi wa barabara hizo umesaidia kupunguza kero ya usafiri na kufanya barabara hizo kupitika muda wote.

‘‘Tunashukuru sana Serikali barabara ni nzuri na pia usimamizi ni mzuri, pale mwanzoni tulikuwa tunapata shida kwenda mashambani na hata masokoni, sasahivi barabara ni nzuri hakuna vumbi wala matope katika kipindi cha mvua na kiangazi”, Bi. Edvina.

Aidha, mbali na utekelezaji wa miradi ya Ahadi za Mhe. Rais, TARURA wilaya ya Muleba imetekeleza ujenzi wa Daraja la Kishara lenye urefu wa Mita 36 katika Mto Ngono linalounganisha Kata za Katoke, Kamachumu na Kata ya Mafumbo ambapo kwa mujibu wa meneja wa TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, amesema wananchi walikua wanazunguka umbali mrefu lakini sasa kero hiyo imeisha.

Naye, Mkazi wa Kitongoji cha Kyamuhaya Bi. Goodselda Liberius alisema kuwa upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo umerahisishwa na uwepo wa daraja hilo kwasababu umewasadia kuvusha mazao yao na bidhaa nyingine za biashara kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

“Tunashukuru kwa kujengewa daraja hili kwasababu limekuwa ni mkombozi kwa sisi wafanyabiashara kusafirisha mazao yetu na tunaishukuru Serikali kwa kutujengea daraja hili,” alisema Goodselda.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijni (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba unaendelea na kazi mbalimbali zikiwemo za matengenezo ya barabara na vivuko katika Wilaya hiyo ili kuwawezesha wananchi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi.



Share:

Trump na Mkewe wakutwa na virusi vya corona


Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba yeye na mke wake Melania Trump wamepatikana na virusi vya corona na wako kwenye karantini. Ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter.

Tangazo hilo linawadia baada ya Trump na wasaidizi wake wawili kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Hope Hicks, 31, mshauri wa rais amekuwa msaidizi wa karibu wa Bwana Trump kupatikana na virusi vya corona hadi hivi sasa.

Bi. Hicks alisafiri na yeye kwa ndege ya kijeshi kwenda kwenye mdahalo wa Televisheni uliofanyika Ohio mapema wiki hii.

Baadae Alhamisi, Bwana Trump alisema yeye na mke wake wanakwenda karantini baada ya Bi. Hicks kuthibitishwa kuwa na corona. 
 
-BBC


Share:

UN YAMUUNGA MKONO RAIS DKT MAGUFULI KUTOKOMEZA UKATILI WA MWANAMKE IKUNGI

 

Mkuu wa  Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi akizungumza baada ya uzinduzi wa mradi kushoto ni  Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania  Zlatan Milisic

Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na wawakilishi wa mashrika ya umoja wa mataifa ,wadau wa maendeleo na kmati ya ulinmzi na usalama ya wilaya ya Ikungi

Na John Mapepele, Ikungi

Mkuu wa  Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi  leo amezindua  miongoni mwa miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa nchini, mradi wa  pamoja  baina ya Mashirika ya Kimataifa ya UN Women na UNFPA kupitia ufadhiri  wa  Shirika la KOICA wa “Tuufikie usawa  wa jinsia kupitia kuwawezesha wanawake na wasichana”.

 

Mradi huo utagharimu takribani bilioni 11.5 za kitanzania  ambao utatekelezwa  katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida na Msalala mkoani  Shinyanga katika kipindi cha  miaka mitatu kuanzia sasa.

 Dk. Nchimbi amesema lengo kuu la mradi huo ni kuchangia  katika kuwawezesha  wanawake na wasichana  kuwakwamua kiuchumi na kijamii katika mikoa ya Singida na Shinyanga  ili kufikia usawa wa kijinsia ambapo amewataka watendaji wote wa Serikali ambao watatekeleza mradi huo kuwa makini katika utekelezaji wa mradi ili  malengo ya mradi huo yaweze kufikiwa.

Amesisitiza kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali watendaji ambao  kwa namna moja au nyingine hawataendana na kasi ya utekelezaji wa miradi chini ya Serikali ya awamu ya Tano  inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ambapo amesema  mrai huo  ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi  ili kuwaletea wananchi  maendeleo ya  kweli.

Kwa mujibu wa  Mkurugenzi wa  KOICA  Tanzania, Bi Jieun Mo,  walengwa wasio wa moja kwa moja takribani  wakazi 40,000 kutoka kwenye wilaya  ya Ikungi na Msalala na walengwa  wa moja  kwa moja 2350 wanawake na wasichana  kutoka katika wilaya hizo watanufaika na mradi huu ambapo pia  wanaume na wanawake 6000 wa Wilaya  ya Ikungi watanufaika kwenye eneo la muingiliano wa  hati za ardhi.

Mo ameainisha kuwa  shughuli za mradi katika kuwaweza wanawake  kwenye eneo la uchumi zitajikiza zaidi kwenye kuimarisha uwezo wa wanawake  na vijana   wakulima ili waweze kutumia  njia nzuri za kilimo na hali ya hewa katika uzalishaji wa alizeti na kilimo cha bustani, kukuza uuzaji wa pamoja, ujuzi wa ujasiriamali na wakala wa uchumi  wa wanawake  na kuimarisha  usalama wa ardhi na umiliki.

Amesisiza kuwa  shughuli hizo zitatekelezeka  kupitia kuunda  vikundi vya uzalishaji wa kilimo cha bustani kwa wanawake, kuunganisha  wanunuzi wa vikundi  vya wakulima vya wanawake,kusaidia ujenzi wa  ghala kubwa  moja la alizeti na kituo cha ukusanyaji kilomo cha bustani ili  kuboresha uuzaji wa pamoja na utunzaji baada ya kuvuna,.

 

Alisema pia watatoa  mafunzo ya ujasiriamali na ufikiaji wa habari za kifedha na kufuatilia ushauri wa usimamizi wa biashara na  fedha na kukuza  umiliki wa ardhi pekee na wa pamoja  wa wanawake kupitia utoaji wa  Hati za Haki za kimila za Makaazi(CCROs).

Mwakilishi wa UN Women  Bi, Hodan Addou ameishukuru Serikali  ya  Tanzania  kuwa ushirikiano wake katika kuhakikisha  kuwa mradi huu  hatimaye umeanza kutekelezwa ambapo amesema Shirika lake  linaunga mkono juhudi za Serikali za kumkomboa mwanamke ili kuondokana na  unyanyasaji wa kijinsia.

Bi Addou amesisitiza kuwa mradi huo utasaidia uwezeshaji kijamii kwa kuwawezesha  wanawake kusimamia haki zao, kujenga ujuzi wa ujasiriamali wa wanawake na wasichana kukabiliana  na unyanyasaji wa kijinsia na kuimarisha mifumo ya kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia kupitia kuanzisha na kuandaa vifaa katika madawati matatu ya  Polisi ya Jinsia na Watoto.

Aidha alisema pia wataaanzisha  vituo vitatu vya  huduma  ya dharura katika  vituo vya wilaya, kuunda nafasi salama ya umma, kujenga uwezo  wa nambari ya msaada ya watoto kitaifa, kuunda na kuimarisha Klabu za Wasichana na kuunda Kamati za ulinzi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania  Zlatan Milisic   ameipongeza Serikali kwa kuwa  na mradi huo na kuongeza kuwa mradi huo unaendana na malengo ya endelevu ya 2030 hususani lengo namba 5 kuhusiana kuwaendeleza wanawake  katika nyanja mbalimbali na kuongeza kuwa mwaka 2020 ni mwaka muhimu sana kwa kuwa tunaelekea  katika kutimiza miaka 25 ya azimio la wanawake la Beijing.

Ameeleza kuwa  malengo endelevu ya 2030 yameeleza kuwa ili kufikia maendeleo ya nchi kumtambua mwanamke ni jitihada muhimu sana  katika kuharakisha na kutimiza malengo yote ya maendeleo ambapo ameihakikishia Serikali ya Tanzania kuendelea kufanya kazi kwa karibu sana  ili kuhakikisha wanawake wanakuwa chachu ya maendeleo katika  nchi ya Tanzania.

Mwakilishi wa UNFPA, Dk. Winfred amesema kuwa uzinduzi wa mradi umelenga kutokomeza aina zote za unyanyasaji wa kijinsia  na kuimarisha usawa katika jamii ikiwa ni pamoja na  kuimarisha maisha ya wanawake ambapo amesisitiza kitovu cha matatizo ya kijinsia  ni wanaume na mila na desturi potofu zinazomtazama mwanamke kwa kumdharirisha hivyo juhudi za makusudi  zinatakiwa  kufanywa za kuwaweka wanaume mbele ili kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.

Naye  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo  amesisitiza kuwa kazi nzuri zinazofanywa na  Rais John Pombe Magufuli katika Nyanja mbalimbali ndiyo zinazoyafanya  jumuiya za kimataifa  kuunga mkono kwa kutoa  misaada  kupitia miradi mbalimbali hapa nchini.

Share:

Tundu Lissu atakiwa kuripoti kituo cha Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro - IGP Sirro

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amemtaka mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Tundu lissu kuripoti kituo cha Polisi Moshi Kilimanjaro kutokana na kitendo chake alichokifanya  akiwa mkoani humo.

IGP Sirro amesema hayo jana ambapo alimtaka Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Freeman Mbowe kukaa na watu wake wazungumze suala la utii wa sheria bila shuruti.

Aidha IGP Sirro ameongeza kuwa Jeshi la Polisi limepewa mamlaka ya kulinda usalama wa raia na mali zao huku akiwaeleza kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kupambana na Jeshi hilo na kwamba wote wanaovunja sheria za nchi watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.


Share:

Mgr: Data Warehousing & Bus Analysis at Vodacom

Joining Vodacom is more than a job, what we do matters. We don’t just carry minutes, texts and data – we carry people’s lives. And that’s a huge responsibility. If you think for a minute about the people you rely on…the likelihood is they rely on us. Customers are at the heart of everything we […]

The post Mgr: Data Warehousing & Bus Analysis at Vodacom appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa October 2



















Share:

TBS YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA MAFUTA YA KULA KANDA YA KATI


Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetekeleza mpango wa mafunzo kwa wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa mafuta ya kula kanda ya kati, yaliyofanyika Mkalama, Kiomboi, Sikonge, Urambo, Shelui, Manispaa ya Tabora,Nzega, Igunga, Manispaa ya Singida, Kondoa Irangi, Kongwa, Mpwapwa, Kibaigwa, Chamwino, Itigi, Manyoni, Dodoma jiji na Bahi. 

Mafunzo haya yamelenga kuwaelimisha wadau hao juu ya uzalishaji bora, uhifadhi sahihi wa bidhaa za mafuta haswa sehemu za kuuzia, ufungashaji sahihi na salama na umuhimu wa kuzingatia na kuweka taarifa sahihi na muhimu katika vifungashio.

TBS imetoa elimu hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya viwanda, SIDO, maafisa biashara, afya na maendeleo wa wilaya ili kuwajulisha wadau wa mafuta ya kula fursa zilizopo ndani ya Serikali ili kuwawezesha kuboresha bidhaa zao ziweze kukidhi matakwa ya viwango na hatimaye kupananua wigo wa soko la ndani na nje ya nchi na kuwafanya kuongeza uzalishaji utakaopelekea kuinua uchumi wao.

Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS),Bw. Lazaro Msasalaga aliwashauri wadau hao kuzingatia kanuni za uzalishaji na uhifadhi bora na salama ili kuepuka kupoteza masoko na kero ya kukutwa na bidhaa hafifu ambayo itawalazimu kuteketeza kwa gharama zao. 

 

Pia aliwashauri kuwasiliana na ofisi ya TBS mara kwa mara pale wanapohitaji msaada wa kitaalamu katika mnyororo mzima wa uzalishaji, uhifadhi na ufungashaji sahihi.

Kwa upande wake Meneja wa Utafiti na Mafunzo (TBS ), Bw. Hamis Sudi Mwanasala alisema mafunzo haya kwa wadau wa sekta ya mafuta ya kula yataendeshwa katika mikoa yote nchini na kwa kuanzia yameendeshwa katika kanda ya kati ikijumuisha mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora. 

"Huu ni mwanzo, kwani Shirika litahakikisha mafunzo kama haya yanamfikia kila mdau na katika ngazi ya chini kabisa, leo tupo kanda ya kati, ila tumeshapita kanda ya kusini, nyanda za juu kusini na kwingineko kwa wadau wa bidhaa nyinginezo"Alisema 

 

Alieleza kwamba mafunzo haoa ni bure na Serikali inagharamia kupitia TBS na tunampango wa kufikia wadau wa mafuta ya kula Nchi nzima" alisema. 

 Pamoja na mada juu ya bidhaa ya mafuta ya kula TBS inatumia mafunzo haya kuelezea majukumu ya Shirika ikiwa pamoja na yale yaliyokua yakifanywa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa ( TFDA).

Kaimu Mkuu wa Kanda ya kati TBS , Bi Salome Emmanuel aliwasisitiza wajasiriamali ambao bado bidhaa zao za mafuta hazijapatiwa nembo ya bora, kuchangamkia fursa ya bure kwa kutuma maombi ya kutumia alama ya ubora kupitia SIDO ili Serikali iwatambue kama wajasiriamali wadogo na kati na waweze kuhudumiwa bure kwa kuwa bidhaa ya mafuta inaangukia katika kiwango cha lazima hivyo kulazimika kukidhi matakwa ya viwango kwa mujibu wa sheria.

Mafunzo haya yalihusisha wadau walioweza kushiriki katika kumbi mbalimbali zilizoandaliwa lakini vilevile utembelewaji wa moja kwa moja wa wadau hao katika maeneo yao ya uuzaji au uzalishaji kama vile maeneo ya Pandambili (Kongwa),soko kuu la Singida, Tarafa ya Pahi ( Kondoa), soko la majengo (jijini Dodoma), Mitundu ( Itigi), soko kuu la Singida, soko kuu la Nzega, soko kuu la Tabora na kwa wauzaji wa barabarani waliopo wilaya ya Shelui

Lengo ni kuwaelimisha madhara yanayotokea pindi mafuta yanapoanikwa juani kwani mwanga,joto na hewa hupelekea mafuta kuharibika kabla ya muda wa mwisho wa matumizi na kusababisha madhara ya kiafya na kuwaelekeza kuboresha mazingira ya utunzaji kwa kuongeza kivuli cha vibanda vyao na kuweka taarifa za vifungashio.

Mzalishaji wa Mafuta ya kula, Bw. Daud Abel Makala na Muuzaji wa Mafuta hayo Bi.Eunice Maneno ambao walibahatika kushiriki mafunzo hayo katika jiji la Dodoma, walipongeza juhudi zinazofanywa na TBS katika kuhakikisha wanawasaidia wadau wa sekta mbalimbali hususani mafuta ya kula kuzingatia viwango ili kuweza kupata masoko ndani na nje ya nchi na kuwa na ushindani huru sokoni.

 

 Hata hivyo waliitaka TBS kuhakikisha huu mpango wa mafunzo sambamba na kaguzi za mara kwa mara masokoni ni endelevu kwa bidhaa zote na haswa maeneo ya vijijini, ili kumlinda mlaji dhidi ya bidhaa hafifu na zile zilizokwisha muda wa matumizi au zisizotakiwa kabisa masokoni.

Nao wauza mafuta ya kula katika soko kuu la Singida na Tabora wameiomba Serikali kurahisisha upatikanaji wa vifungashio na kuhakikisha vinauzwa kwa bei nafuu ili hata wajasiriamali wa chini waweze kupaki mafuta yao kwa vifungashio bora na salama tofauti na sasa ambapo wanatumia zaidi vifungashio vilivyokwishatumiwa awali kwa bidhaaa nyinginezo.

TBS ilianza kutoa mafunzo hayo Septemba 21 hadi Oktoba 01, 2020 na kufikia wadau zaidi ya 1700 katika kanda ya kati.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger