Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Gaspar Kileo maarufu 'GAKI' akirudisha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu (kushoto) leo Ijumaa Julai 17,2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini. Picha na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Friday, 17 July 2020
FRANCIS GILYA KASILI AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI KUPITIA CCM
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Francis Gilya Kasili akirejesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu leo Ijumaa Julai 17,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini. Picha zote na Kadama Malunde -Malunde 1 blog
DKT. EMMANUEL KIBERITI AREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Kiberiti akirejesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Ijumaa Julai 17,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu (kushoto). Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
KADA WA CCM KASHI SALULA GACHA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Kashi Salula Gacha leo Ijumaa Julai 17,2020 amerudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Mjasiriamali Kashi Salula Gacha akichukua fomu ya kuomba ridhaa ya Kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kupitishwa na chama chake kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu Jumatano Julai 15,2020.
Joshua Nassari Ajitosa Tena Kugombea Ubunge Kupitia CCM
Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) kabla ya kuvuliwa Ubunge na baadaye kuamua kuhamia CCM, Joshua Nassari amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge kwa mara nyingine tena katika Jimbo hilohilo la Arumeru Mashariki
Bodi ya mikopo elimu ya juu yafungua dirisha la maombi kwa siku 40, yatoa muongozo
Tunapenda kuwafahamisha wanafunzi wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia HESLB kuwa mfumo wa uombaji wa mkopo kwa njia ya mtandao utakuwa wazi kwa siku 40 kuanzia Jumanne, Julai 21, 2020 hadi Jumatatu, Agosti 31, 2020.
Tunawashauri wanafunzi wahitaji kutumia muda wa sasa hadi mfumo utakapofunguliwa (Julai 16, 2020 hadi Julai 21, 2020) kusoma ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Mwaka 2020/2021’ unaopatikana kuanzia sasa katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) katika lugha za Kiswahili na Kiingereza.
Mwongozo huu unatoa maelekezo ya kina kuhusu sifa, utaratibu na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa upangaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021.
Aidha, baada ya kuusoma, tunasihi waombaji mikopo kuhakikisha wanaandaa nyaraka zote muhimu kama zinavyoelekezwa katika Mwongozo huo.
Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
_________
1. Kupata Mwongozo kwa Kiswahili==> Bonyeza hapa
2.Guidelines and Criteria in English ==>Click here
1. Kupata Mwongozo kwa Kiswahili==> Bonyeza hapa
2.Guidelines and Criteria in English ==>Click here
KADA WA CCM ABEL JOEL KAHOLWE ACHUKUA NA KUREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abel Joel Kaholwe akirejesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu leo Julai 17,2020.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abel Joel Kaholwe amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Abel Joel Kaholwe ambaye ni Afisa Mtendaji kata ya Ntobo halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga amechukua na kurudisha fomu leo Ijumaa Julai 17,2020 asubuhi katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu.
Akizungumza baada ya kurejesha fomu, Kaholwe ambaye aligombea udiwani kata ya Ndala katika jimbo la Shinyanga mwaka 2015 amesema mwaka huu amejitolea kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika nafasi ya Ubunge ili kuendelea kusukuma gurudumu mbele la maendeleo.
“Mimi ni kada mkongwe wa CCM ambaye chama kimekuwa kikiniamini tangu mwaka 2015 ambapo katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kilinipa dhamana ya kupeperusha bendera ya CCM kata ya Ndala. Kwa sasa wote tumeshuhudia kwa miaka hii mitano ya Rais John Pombe Magufuli amekuwa akifanya kazi kubwa sana na ameendelea kuwaamini vijana”,amesema Kaholwe.
“Mimi kama kijana nimejitolea kuja kuwatumikia wananchi wenzangu wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika nafasi ya Ubunge nikiamini kuwa yapo mambo mengi yameshafanywa na walionitangulia lakini zipo kasoro ndogo ndogo za kurekebisha kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo. Shinyanga ni Potential na inahitaji vijana Potential wenye uzalendo wa kuwatumikia wana Shinyanga”,ameongeza Kaholwe.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abel Joel Kaholwe akionesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini baada ya kuchukua katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, leo Julai 17,2020. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abel Joel Kaholwe akirejesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu leo Julai 17,2020.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abel Joel Kaholwe akirejesha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu leo Julai 17,2020.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mafunzo Ya Kilimo Yalenge Kuwa Cha Kibiashara - Katibu Mkuu Kusaya
Wakufunzi wa mafunzo ya Kilimo nchini wameagizwa kufanya kazi kwa weledi kwa lengo la kuwafundisha wanafunzi kuelewa na kuwa mahili katika kilimo kibiashara.
Agizo hilo limetolewa leo Jijini Mbeya na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya alipotembelea na kuzungumza na watumishi na wanafunzi wa chuo cha Mafunzo ya Kilimo (MATI) Uyole.
Kusaya amevitaka vyuo vyote 14 vinavyotoa mafunzo ya Kilimo vya umma na vile 15 vya binafsi kuhakikisha vinawafundisha wanafunzi taaluma ya kufanya Kilimo biashara ili wakihitimu waweze kujiajili na kusaidia wakulima kuzalisha mazao kwa faida
“ Hiki ni chuo cha kilimo lazima tuwafundishe vizuri wanafunzi wetu ili wakitoka hapa wawe wanajua kila kitu katika sekta ya mazao ,hivyo wakufunzi wapeni nafasi wanafunzi wajifunze zaidi kwa vitendo na kutumia teknolojia rahisi” alisisitiza Katibu Mkuu huyo
Aliongeza kusema vyuo vyote hasa vya umma vianzishe shughuli na miradi ya kujiongezea kipato kwa kutumia ardhi na miundombinu iliyopo na kupunguza utegemezi wa bajeti ya serikali.
Katika kufikia malengo hayo ya kufundisha Kilimo cha kibiashara ,Katibu Mkuu huyo ameahidi kukichangia chuo cha MATI Uyole shilingi milioni 30 ili kiongezee katika bajeti yake kununua trekta kwa ajili ya kazi za uzalishaji mazao.
Pia amesema atakisaidia chuo hicho pikipiki tatu kwa ajili ya wakufunzi, kompyuta tano na vifaa vya TEHAMA ili chuo kianzishe maktaba mtandao (e-learning) pamoja na kuwapatia wanafunzi magunia 20 ya mpunga ili wale.
Pia ameahidi kukipatia chuo cha MATI Uyole kitalu nyumba ( Green House) kwa ajili ya wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuzalisha mboga mboga na matunda (horticulture.
Katika kukifanya chuo hicho kinaongeza uzalishaji ameagiza uongozi wa chuo kuwasiliana na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa ajili kuanzisha miundombinu ya umwagiliaji ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza vema kabla ya kuhitimu.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha MATI Uyole Emanuel Mwalukasa alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa jitihada ambazo serikali kupitia wizara ya Kilimo inafanya kuboresha mazingira ya ufundishaji.
Aidha Katibu Mkuu huyo alitembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Uyole ambapo amewapongeza kwa kazi nzuri ya utafiti wa aina nyingi bora za mbegu zenye matokeo mazuri kwa wakulima
Ameitaka taasisi hiyo kuongeza jitihada katika kufanya tafiti zenye lengo la kusaidia wakulima kuzalisha mazao mengi kibiashara na kuchangia katika uchumi wa taifa .
“Ninyi TARI mna deni kubwa kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kufanya utafiti katika Kilimo kionekane chenye tija na kukifanya cha kibiashara na kuwezesha matokeo ya tafiti hizi za mbegu kuwafikia wakulima na maafisa ugani vijijini” alisema Kusaya
Kuhusu maonesho ya Nanenane ameagiza taasisi zote za mafunzo ya Kilimo na utafiti siku zote kuwezesha wakulima na wananchi kujifunza kilimo na teknolojia muda wote ,hivyo elimu itolewe kwa watu wengi zaidi nchini ili kuleta mapinduzi ya kilimo.
Akiwa mkoani Mbeya Katibu Mkuu Kusaya amekagua maandalizi ya maonesho ya Nane nane katika viwanja vya John Mwakangale na kuwataka wadau wajitokeze na kuendelea na maandalizi
Kauli mbiu ya Nanenane mwaka huu inasema “Kwa Maendeleo ya Kilimo,Uvuvi na Mifugo Chagua Viongozi Bora 2020” ambapo kitaifa maonesho hayo yatafanyika mkoani Simiyu .
Katibu Mkuu Kusaya yupo mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi kutembelea taasisi zilizochini ya wizara yake na kuongea na watumishi ikiwa na lengo la kuongeza tija katika utendaji kazi wenye matokeo chanya kwa sekta ya Kilimo.
Imetolewa na ;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
MBEYA
17.07.2020
Membe akubali kuwania Urais wa Tanzania 2020
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje nchini Tanzania amekubali ombi la wanachama wa ACT-Wazalendo la kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020.
Membe ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 17 Julai 2020 ikiwa ni siku moja kupita tangu alipopokelewa rasmi ndani ya ACT-Wazalendo jana Alhamisi katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
Mwanasiasa huyo amejiunga na chama hicho cha upinzani baada ya kufukuzwa ndani ya chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) alichokulia kwa kile kilichoelezwa hakuwa na mienendo inayoridhisha tangu mwaka 2014.
Jana niliombwa na leo nimekubali rasmi kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo. Huu ni wakati muafaka kwangu wa kushiriki katika mazungumzo na vyama vingine kama Chadema ili tusimamishe "KISIKI CHA MPINGO" kimoja!— Bernard K. Membe (@BenMembe) July 17, 2020
PATROBAS KATAMBI AREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI...ASEMA "KUPATA AU KUKOSA UBUNGE NI MIPANGO YA MUNGU"
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akimkabidhi Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu Fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Ijumaa Julai 17,2020 majira ya saa nne asubuhi katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akiwa katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini baada ya kurudisha Fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Ijumaa Julai 17,2020 majira ya saa nne asubuhi.
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini baada ya kurudisha fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Ijumaa Julai 17,2020 majira ya saa nne asubuhi.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amerejesha Fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katambi amerudisha fomu hiyo leo Ijumaa Julai 17,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu.
Akizungumza baada ya kurejesha fomu, Katambi ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumteua kuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma nafasi ambayo ameitumikia kwa kipindi cha miaka miwili tangu mwaka 2018 hadi leo Julai 17,2020 Rais Magufuli alipomteu Josephat Paulo Maganga kuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma.
“Namshukuru sana Rais Magufuli kwa kuniamini na kuniteua kuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma nafasi ambayo nimeitumikia kwa muda wa miaka miwili na matokeo makubwa mmeyaona, Dodoma tumepiga hatua kubwa kimaendeleo”,amesema Katambi.
“Hodi Shinyanga!,baada ya kufanya mambo makubwa Dodoma nimeona nirudi kwetu Shinyanga kuomba kugombea Ubunge kupitia CCM. Muda umefika sasa mimi kuwatumikia Wana Shinyanga. Nimejitoa sadaka kuacha U- DC ili nije niwatumikie wananchi wa Shinyanga, kuleta maendeleo kwa wana Shinyanga.
“Kupata Ubunge au kukosa ubunge ni mipango ya Mungu. Kama kura zitapungua kuniwezesha kugombea ubunge CCM basi nitarudi kufanya majukumu mengine ikiwemo yangu ya Uanasheria”,ameongeza Katambi.
OMEGA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE MAKAMBAKO
Thursday, 16 July 2020
JOHN MLYAMBATE ARUDISHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI
Afisa Habari na Mawasiliano Serikalini, John Mlyambate akikabidhi fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu leo Julai 16,2020.
Akikabidhi fomu hizo, Mlyambate amewakumbusha wajumbe wa Mkutano Mkuu wa wilaya na wagombea wenzake kuzingatia maadili na miiko ya chama katika kuhakikisha zoezi linakuwa huru na haki na hatimaye akapatikane mwakilishi mzuri atakayepeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Shinyanga Mjini.
Afisa Habari na Mawasiliano Serikalini, John Mlyambate akikabidhi fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjinikwa Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu (kushoto) leo Julai 16,2020.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
































