Tuesday, 9 June 2020

PICHA: Naibu Spika Dkt Tulia Ackson Akiwasili Hospitali Kumjulia Hali Freeman Mbowe Aliyevamiwa na Kuvunjwa Mguu Dodoma

Naibu Spika, Dkt Tulia Ackson akiwasili katika Hospitali ya DCMC Ntyuka kumjulia hali M/Kiti wa Chadema na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliyelazwa katika hospitali hiyo akipatiwa matibabu baada ya kuvamiwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana.

*****

Naibu Spika, Dk.Tulia Ackson  amemjulia hali Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe katika Hospitali ya Ntyuka, Dodoma anakopatiwa matibabu  baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kisha kujeruhiwa na kuvunjwa mguu mmoja na kusema kuwa amemuona akiwa na majeraha mguuni na kwamba wanasubiri taarifa ya daktari ili kujua ameumia kwa kiasi gani.

"Ana maumivu ya mguu, mimi nimemuona ila bado wanaendelea kufanya uchunguzi na vipimo vingine, niwatoe hofu watanzania kwamba yupo anaendelea kupata huduma"- Amesema Naibu Spika Baada ya kumtembelea Mbowe 


Share:

PICHA: Freeman Mbowe Akiwa Amelazwa Baada Ya Kushambuliwa na Kuvunjwa Mguu Dodoma Leo

Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwa amelazwa katika hospitali ya DCMCT Ntyuka mkoani Dodoma kwa matibabu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana na kuvunjwa mguu.




Share:

Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Wapungua Hadi Asilimia 3.2% Kutoka Asilimia 3.3%

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Mei  umepungua hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili 2020.
 
 Hayo yamesemwa jijini  Dodoma  Juni 8,2020 na , kaimu mkurugenzi wa sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bi Ruth Minja wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa.
 
Amesema kuwa mfumuko wa Taifa umeshukua kufuatia kushuka kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwezi Mei 2020.

Akizungumzia hali ya Mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa nchini Kenya mfumuko wa bei ulioishia mwezi Mei umepungua hadi kufikia asilimia 5.47 kutoka asilimia 5.62 kwa mwezi ulioishia April  2020 huku  Nchini Uganda, mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Mei mwaka huu, umepungua hadi asilimia 2.8  kutoka asilimia 3.2 kwa mwaka ulioishia mwezi April  2020.

Ikumbukwe kuwa Ofisi ya taifa ya takwimu (nbs) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa sheria ya takwimu ya mwaka 2015 iliyopewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji wa wa taarifa za kitakwimu nchini.


Share:

Taarifa za Awali za Jeshi La Polisi Kuhusu Kuvamiwa na Kujeruhiwa Freeman Mbowe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amevamiwa na watu watatu waliomkanyaga na kumvunja mguu wake wa kulia.

Hayo ameyabainisha mapema leo Juni 9, 2020, na kusema kuwa taarifa kamili wataitoa hapo baadaye.

"Zipo taarifa kwamba Mh Mbowe amevamiwa na watu watatu, wakamkanyaga kanyaga na kumvunja mguu wake wa kulia, lakini tunafuatilia tutatoa taarifa kamili baadaye na yuko Hospitali ya Ntyuka wodi namba 4" amesema Kamanda Muroto.

Taarifa zinaarifu kuwa Mbowe ameshambuliwa majira ya saa 7:00 usiku wa kuamkia leo.


Share:

Operation Manager at at Coast Mart Supermarket

About Us Coast Mart Supermarket is located in the heart of Kibaha, in a new modern building with its 1,200 square meters meets the different needs of customers with entire departments dedicated to fresh, healthy and all other products. A store that represents a real concentrate of quality, freshness and above all enhancement of all products to meet… Read More »

The post Operation Manager at at Coast Mart Supermarket appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Human Resource Officer at International Rescue Committee

Job Title: Human Resource Officer Requisition ID: req9221 Job Title: Human Resource Officer Sector: Human Resources Employment Category: Regular Employment Type: Full-Time Open to Expatriates: No Location: Dar es Salaam, Tanzania Job Description Specific duties:  Ensure the implementation of the HR Policies and Procedures and provide day-to-day HR support to IRC Dar office and staff. Act as a focal… Read More »

The post Human Resource Officer at International Rescue Committee appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Korea Kaskazini kusitisha mawasiliano yote na Korea Kusini

Korea Kaskazini imesema itasitisha njia zote za mawasiliano na Korea Kusini wakati ikiendeleza shinikizo dhidi ya jirani yake kwa kushindwa kuwazuia wanaharakati kusambaza mpakani vipeperushi vya kuipinga Korea Kaskazini. 

Shirika la habari la Korea Kaskazini limesema leo kuwa njia zote za mawasiliano ya pande mbili za mpakani zitasitishwa leo mchana. 

Onyo hilo la Korea Kaskazini limekuja wakati mahusiano kati ya Korea hizo mbili yakiwa katika hali tete kutokana na mkwamo wa muda mrefu wa diplomasia ya nyuklia kati ya Korea Kaskazini na Marekani.


Share:

Breaking News : MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE AVAMIWA NA KUSHAMBULIWA



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa na Kiongozi wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni  Freeman Mbowe ameshambuliwa na kujeruhiwa na Watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake jijini Dodoma usiku wa kuamkia leo Jumanne Juni 9,2020.


Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha kuwa Mbowe amevamiwa na kushambuliwa na watu wasiojulikana.

"Ni kweli ameshambuliwa na ameumizwa,amepelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu. Tutatoa taarifa zaidi baaadae",amesema Makene.

Taarifa zaidi zinakuja hivi punde...
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 9,2020


Magazetini leo Jumanne Juni 9,2020














Share:

Monday, 8 June 2020

Tundu Lissu atangaza nia ya kugombea Urais 2020

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu leo amezungumza kwa Mubashara kupitia ukurasa wake wa Facebook akiwa ughaibuni na kutangaza nia ya kugombea Urais nchini Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa October 2020.


Lissu amechukua hatua hiyo siku kadhaa tangu John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema, kuwataka wanachama wenye nia ya kugombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, kuwasilisha taarifa zao katika ofisi yake, kuanzia tarehe 3 hadi 15 Juni 2020 

Lissu amesema, endapo atafanikiwa kuwa Rais, ataboresha uchumi wa nchi, mahusiano na jumuiya za kimataifa na nchi marafiki, utawala bora, misingi ya haki za binadamu, demokrasia na mfumo wa vyama vingi.

Amesema uchaguzi wa mwaka huu, utaamua kama Chama cha Mapinduzi (CCM), kitapata fursa ya miaka mitano mingine ya kuendelea kuharibu uchumi wa nchi na kufukarisha wananchi, au mwanzo mpya kwa Tanzania, kujiimarisha kiuchumi.

Lissu amesema, akifanikiwa kuwa Rais wa Tanzania, atahakikisha mihimili ya nchi, ikiwemo Bunge na Mahakama, inakuwa huru na kujitegemea kwenye maamuzi yake.

Amesema katika uongozi wake kama atafanikiwa kuwa Rais wa Tanzania, atavitumia vyombo vya ulinzi na usalama kulinda haki za binadamu, na si katika kukandamiza wapinzani wake, vyombo vya habari na asasi za kiraia.


Amesisitiza kuwa  endapo atafanikiwa kuwa Rais, Serikali yake itaendeshwa kwa kufuata misingi ya utawala bora na sheria, inayoendana na Katiba ya nchi pamoja na mikataba ya kimataifa, ambayo Tanzania iliikubali.

Lissu amesema, akifanikiwa kuwa Rais wa Tanzania, ataponya majeraha ya wananchi pamoja na kurejesha umoja wa kitaifa, huku akisisitiza kwamba hatalipa kisasi kwa maadui zake.


Share:

Ngoma Mpya : NYANDA MAJABALA ' KISIMA' - AMANI....NGOMA MATATA KUELEKEA UCHAGUZI TZ



Mwaka 2020 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu Tanzania... Msanii Nyanda Majabala 'Kisima' kutoka Bariadi mkoani Simiyu anakualika kutazama video yake mpya inaitwa Amani!!.. Imetengenezwa Makula Studio...Kisima Kazungumzia mambo kadhaa kuhusu masuala ya uchaguzi!!

Itazame ngoma ya Nyanda Majabala 'Kisima'  - Amani hapa chini

Share:

SERIKALI IMEFANIKIWA KUDHIBITI CORONA -WAZIRI UMMY




Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akikata utepe wakati wa uzinduzi wa makabidhiano ya vifaa vya Kunawia Mikono kudhibiti ugonjwa wa Covid 19 Mkoa wa Tanga kulia ni Country Director Water Mission Benjamini Filskov    


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwa Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Ngamiani Angelina Mashaka

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya makabidhiano ya vifaa vya kunawia mikono kudhibiti ugonjwa wa Covid 19 hayo kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Msaidizi wa Afya Mazingira Wizara ya Afya Salvata Silayo na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwa kwenye kituo cha Afya Ngamiani Jijini Tanga wakati aliopokwenda kukabidhi vifaa hivyo kulia ni
Mwakilishi wa Mkurugenzi Msaidizi wa Afya Mazingira Wizara ya Afya Salvata Silayo

Country Director Water Mission Benjamini Filskov kushoto akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Jonathan Budenu



Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Country Director Water Mission Benjamini Filskov


Sehemu ya vifaa ambavyo vimetolewa

SERIKALI imesema kuwa imefanikiwa kudhibiti na kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya virusi vya corona huku ikiwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ili kuutokomeza kabisa.

Hayo yalisemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake ya kushtukiza kwenye kwenye Kituo cha Afya cha Ngamiani Jijini Tanga ambapo aliweza kuzungumza pia na wahudumu wa Afya na kupokea msaada wa vifaa vya kunawia maji kudhibiti Ugonjwa wa Covid 19 vilivyotolewa na Shirika la Water Mission Tanzania

Mwalimu alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na wananchi wake na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa imeweza kuudhibiti ugonjwa huo huku ikiendelea na juhudi za kuumaliza kabisa.

"Kwa kiasi kikubwa tumeweza kuidhibiti corona na sasa tunaelekea kuumaliza kabisa, tuachane na kusikiliza baadhi ya vyombo vya habari vya wenzetu wanaotaka kututisha kuhusu ugonjwa huu" Alisema.

"Lakini pia ndugu zangu waandishi wa habari mnaona hali halisi hapa tumefika hakuna mgonjwa hata mmoja wa corona, hivyo muwajulishe wananchi habari hizi kwamba ugonjwa tumeudhibiti na hatuna kituo chenye wagonjwa wa corona ndani ya mkoa wetu" Alisisitiza Mwalimu.

Aidha alifafanua kwamba wananchi wote wanaokwenda kupata huduma za kijamii ni lazima waendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya corona kwa kufuata maagizo ya serikali na wataalamu wa afya.

Awali alipofika katika kituo hicho cha afya alikuta hali ya msongamano wa wagonjwa katika eneo la kusubiria huduma ya kuonana na daktari.

Mwalimu alisema kuwa kutokana na msongamano huo kuna asilimia kubwa ya kupatikana maambukizi ya corona kwa wagonjwa hao ambao pamoja na kuvaa barakowa lakini walikaa kwa kubanana sana jambo ambalo limempa wasiwasi.

"Wagonjwa wamefuata tiba hapa lakini kuna wasiwasi watu wakaondoka na corona, mnatakiwa muendelee kujikinga, nimeona pale nje mnanawa kwa maji tiririka na sabuni, barakowa mmevaa lakini kwa mlivyokaa kwa msongamano mnaweza kuambukizana" alisema.

Hata hivyo waziri alimuagiza Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Ngamiani Angelina Mashaka pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kupata eneo la kuongeza sehemu ya kukaa wagonjwa wanaofuata tiba ili kuepusha msongamano.

Vile vile alimtaka Mashaka kuendelea kuwakumbusha wagonjwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya corona wanapofika kupata tiba kwa kuzingatia tahadhari zote zinazotakiwa.
Share:

TUNDU LISSU ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS TANZANIA 2020

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu leo Juni 8 ametangaza nia ya kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu 2020.

Amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook alipokuwa akizungumza na wananchi, ambapo ametoa ahadi kadhaa endapo atachaguliwa nafasi hiyo.

''Napenda kuwataarifu kuwa nimetangaza rasmi nia yangu ya kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi ujao mwezi Oktoba na nimeshawasilisha kila kitu kwa katibu mkuu wa chama chetu'', amesema Lissu. 

''Endapo nitachaguliwa kwenye uchaguzi ujao, nitahakikisha serikali yangu inaandaa sera nzuri ya kiuchumi, udhibiti wa mfumo wa bei ya vitu kwa maslahi ya wananchi na mfumo mzuri wa ukusanyaji mapato usiokandamiza wenye kipato cha chini'', amesema.

"Endapo nitachaguliwa, nitarudisha mamlaka ya Bunge kama zamani, nitaondoa vifungo na mateka yaliyowekwa kwenye mahakama zetu na nitaheshimu uhuru wa Mahakama katika wajibu wao wa kutenda haki''.

''Nimezunguka karibu dunia nzima kasoro bara la Australia ndio sijafika hivyo nina uzoefu wa kutosha na mahusiano mazuri na nchi tofauti tofauti, endapo nitachaguliwa katika uchaguzi ujao, nitatumia vizuri mahusiano hayo kwa manufaa ya taifa'' ,amesema.

''Nafahamu ubora wa Watanzania haswa kwenye ubunifu hivyo nikiwa Rais nitaweka mfumo rahisi kwa wananchi kunufaika na kazi zao tofauti na sasa ambapo wengi hawawezi kuonesha uwezo wao kutokana na kujaa hofu'', amesema

Kuhusiana na uhalali wake wa kugonmbea nafasi hiyo, Lissu amesema, ''mimi nina sifa zote za kuwania nafasi yoyote katika nchi hii na wala sijapoteza sifa hizo kutokana na Spika Job Ndugai kunifutia ubunge. Sijawahi kutuhumiwa wala kuthibitika kuwa na makosa mbele ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma''.

Waliojitokeza kuwasilisha fomu za kugombea Urais katika chama hicho mpaka sasa ni yeye Tundu Lissu pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa.
Share:

Monitoring and Evaluation Coordinator at WeForest/GRA

Job Description Job Title: Monitoring and Evaluation Coordinator Location:  Musoma, Tanzania Reporting to: GRA-Tanzania Tree Program Manager and WeForest Global Resource Alliance, Inc. Global Resource Alliance, Inc. (GRA) is a non-profit organization headquartered in Ojai, California. It was founded in April 2002 to provide financial and technical support to community organizations in the world’s least developed regions working for… Read More »

The post Monitoring and Evaluation Coordinator at WeForest/GRA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya 14

Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA   
Kelele za furaha zinazo sikika sebuleni zikamfaya mrs Sanga kukurupuka ndani kwake na kukimbilia sebeeni. Mapigo ya moyo yakamstuka mara baada ya kukutanisha macho yake uso kwa uso na mume wake ambaye hajaonyesha sura yoyote ya kumchangamkia. RCP akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa pingu huku akimtazama mrs Sanga anaye shuka kwenye ngazi huku akilazimisha tabasamu la kinafki kwani shida zote zilizo tokea katika siku mbili hizi yeye ndio chanzo.

ENDELEA   
“Ohooo pole sana mume wangu”
Mrs Sanga alizungumza huku akimkumbatia mume wake. Nabii Sanga hakuonyesha kitu chochote kibaya kwa mke wake.
“Nashukuru mke wangu. Pole sana kwa kukuweka katika kipindi kigumu sana wewe na watoto”
Maneno hayo ya nabii Sanga yakamfanya RPC kurudisha pingu zake mfukoni huku akiwatazama.
“Pole sana na wewe mume wangu. Vipi hawajakuumiza?”
Mrs Sanga alizungumza kwa mahaba mazito ambayo kwa namna moja ama nyingine ni uigizaji.
“Nipo salama kabi.”
“Mzee nina weza kupata muda wa kuzungumza na wewe kwa dakika chache?”
RPC alizungumza na kumfanya nabii Sanga kumuachia mke wake. Wakatoka nje na kuingia kwenye gari la RPC.
“Ahaa natambua kwamba hili jambo nitakalo kwenda kukueleza kidogo linaweza kukustua mzee wangu. Ila sina namna zaidi ya kukuambia, ili kama nitaamua kwenda mbele zaidi ya hapa basi uwe umesha jiandaa kisaikolojia.”
“Niambie tu usiwe na hofu”
“Ili kukupata wewe, tulifanikiwa kumkamata kijana mmoja anaitwa Tomas, ni dalali na pia niligundua ni kijana wako wa karibu sana?”
“Yaa Tomas ni kijana wangu nina muamini sana. Kwa nini mume mkamata?”
Nabii Sanga aliuliza kana kwamba hajui ni kitu gani kinacho endelea.
“Ahaa…ngoja kwanza”
RPC alizungumza huku akitoa simu yake mfukoni. Akaweka sauti ya mahojiano yake na Tomas. Nabii Sanga akajifanya akistushwa sana na kukiri kwa Tomas, ila ukweli ni kwamba ana fahamu kila kitu kinacho endelea kati ya Tomas na mke wake.
“Ohoo Mungu wangu nimpe nini huyu mwanamke?”
“Ndio hivyo, sasa yule kijana yupo mahabusu. Ila mke wako yupo uraiani, endapo tukimpeleka mahakamani kijana huyo na aka zungumza jambo juu ya mke wako, basi tambua mke wako ata tiwa nguvuni na atastakiwa kutokana na makosa yake na pia atatumikia kifungo jela na akitumikia kifungo jela, huduma yako ina mambo mawili, ina weza kuyumba au kutoweka kabisa. Kwani itakuwani kashfa kubwa sana kwako na familia yako kwa ujumla na unavyo tambua Watu kwakukuza mambo, basi utapotea kinamna hiyo.”
Nabii Sanga akaka kimya huku akitafakari juu ya adhabu gani ambayo ana weza kumpatia Tomas kwani kazi aliyo wapo Rama D na wezake hawato weza kuifanya kutokana na Tomas kukamatwa na polisi na hadi sasa nabii Sanga hatambui kwamba Rama D na ndugu zake wamesha uwawa na askari.
“Una weza kunisaidia kazi moja RPC?”
“Kazi gani?”
“Nahitaji kijana huyo afe kabla ya kupelekewa mahakamani, je itawezekana”
“Kuwezekana ina wezekana mzee. Ila sikuzote vitu kama hivi vina kwenda kwa pesa maalumu ambayo itatufanya kujilinda hata pale likitokea la kutokea, ikiwemo kusimamishwa kazi au kushushwa vyeo”
“Una hitaji kiasi gani?”
“Acha nikajitafakari kisha nitakuambia kabla ya saa mbili asubuhi”
“Sawa, ila hakikisha kwamba mke wangu haguswi kabisa na tuhuma hizi. Pia nitumie audio hiyo kwenye email yangu”
Nabii Sanga akamtajia RPC email yake na akatumiwa sauti hiyo.
“Nashukuru sana”
“Ila ushauri ni mmoja sasa kuwa makini sana na mke wako. Hakikisha kwamba mke wako una muweka mikononi mwako vizuri la sivyo ata kuja kukudhuru ukiwa humo ndani kwako. Kama alifanikiwa nje, basi ndani ni rahisi zaidi ya nje.”
“Nimekuelewa RPC”
“Nashukuru kwa kunielewa mzee”
Nabii Sanga na RPC wakashuka kwenye gari na kuingia ndani. RPC akamuaga mrs Sanga na wanaye, kisha akaondoka huku nyumbani hapo wakiwaacha askari wawili, watakao linda hadi asubuhi kisha kuanzia hapo nabii Sanga ata endelea na maisha yake na familia yake kama kawaida na swala la ulinzi litakuwa juu yake mwenyewe.
“Vipi mume wangu ume kula?”
“Ndio nipo vizuri. Naombeni niende kupumzika”
“Sawa baba”
Nabii Sanga akapandisha gorofani huku mke wake akimfwata kwa nyuma.
“Simu yako ina salio?”
“Ndio”
“Wasiliana na sekretari. Muambie kesho saa nne asubuhi nahitaji kuzungumza na waandishi wa habari. Nahitaji kuwafahamisha waumini wangu kote duniani kwamba nipo salama”
“Kwa nini usisubiri subiri siku ya kesho ipite, ili urudi katika hali yako ya kawaida”
“Hali ipi ya kawaida?”
“Uzoee mazingira ya nyumbani na ujipange tena upya kisaikolojia kisha ndio uzungumze na waandishi wa habari”
“Sikiliza mama Juliethi. Kuna watu wamefunga na wana sali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba nina kuwa salama. Watu hao kitu cha pekee cha kuwalipa na waamini kwamba Mungu amejibu maombi ya vile wanavyo viomba ni mimi kesho kusimama mbele ya waandishi wa habari na kuwaleza nini kilinikumba ni nani aliniteka huku huyo aliye niteka akisaidiana na nani kwenye kuniteka. Na aliye toa wazo la mimi kutekwa pia nita muanika hadharani ili dunia nzima ijue adui yangu ni nani hata siku ikitokea siku nime pata madhara basi adui yangu ana kuwa wakwanza kukamatwa”
Fumbo la nabii Sanga likamfanya mrs Sanga kustuka sana. Mwili ukaanza kumtemeka kwa maana yeye ndio mtu aliye toa wazo la mume wake kutekwa. Tomas yeye ndio aliye tekeleza wazo hilo.
“Mpigie una nitolea nini macho?”
Mrs Sanga akachukua simu yake na kupigia sekretari wa kanisa lao.
“Ehee zungumza naye”
Mrs Sanga alizungumza hukua akimkabidhi mume wake simu hiyo na akaiweka sikioni mwake.
“Baba mchungaji”
“Naam”
“Ohoo asante Mungu upo hai. Hapa mama alipo niambia kwamba niandae kikao kesho, nilikuwa na kigugumizi huku nikijiuliza naandaa kikao na waandishi wa habari je usipo tokea nini nitajibu nini. Ila nina furahi sana kusikia sauti yako baba”
“Usijali kijana wangu. Watesi wangu walijiinua ila Mungu ambaye hashindwi na jambo aliweza kusimama kwangu na kunipigania na kama sikufa katika kutekwa huku. Basi siku ni kifa nitakufa kwa amani tena baada ya kupitisha ule umri wa miaka themanini ambao Mungu aliupanga juu ya wana damu wake”
“Amen amen”
“Basi fanya hivyo na kesho tatu asubuhi njoo nyumbani kwangu”
“Sawa baba”
Nabii Sanga akakata simu na kumrudishia mke wake.
“Kuna wakati wa kuliaaaaa…..wakati wa kuombolezaaaaa, ila adui yako ni mtu wa karibu….”
Nabii Sanga aliimba wimbo huo huku akivua nguo zake na kuelekea bafuni huku akimuacha mrs Sanga akiwa katika wakati mgumu sana wa kujitafakari kama hicho anacho kizungumza mume wake kipo kweli kichwani mwake au ana hisi tu.
                                    ***
    Magreth akaamka asubuhi na mapema. Akapanga nguo zake zote ambazo ana hisi zina umuhimu kuingia kwenye ulimwengu wa maisha yake mapya ya utajiri. Alipo hakikisha kwamba ame chukua vitu vyake muhimu, akwaamsha mama Boka na wezake. Wakingia chumbani kwake huku kila mmoja akiwa na shahuku ya kujua ame itiwa nini.
“Jamani mimi nina hama. Kuna kitanda godoro, jiko hii meza na sofa hapo, muna weza kugawan kwa kuchukua au mkaviuza vitu hivyo na mukapata pesa mutakayo gawana”
“Ehee shosti bora kuviuza, itakuwa ni jambo zuri”
Mama Boka aliwahi kuzungumza na kuwafanya wezake wamtazame.
“Basi ngoja nitoe wazo. Viuzeni, kisha pesa itakayo patikana nyinyi mugawane sawa kwa sawa. Asitokee hata mmoja kuwazidi wezake”
“Hapo Mage umesema. Ila shosti kweli una taka kutuambia kwamba leo hii una hama na kutuacha huku uswahilini?”
“Ndio mbona hamuamini?”
“Yaani nina ona kama ni ndoto vile”
“Kwa nini?”
“Yaani una tuacha hivi hivi, sisi tuna zidi kufubaa tu hapa na huyu bibi Ngedere”
“Wala musijali. Nikiweka mambo safi nita waalika muje kupaona kwangu. Tena niandikieni namba zenu”
Magreth alizungumza na kumpatia mama Boka simu yake. Wakaanza kuandika namba zao za simu.
“Yaani kweli Mage mambo yamekubadilikia. Sijawahi kukuona ukimiliki smart phone. Nilisha kizoea kile kisumu chako cha nokia ya tochi”
“Hahaa kiobama?”
“Ndio, mwenyewe kile hata ukikiacha huko uwani hakuna ambaye alikuwa ana shughulika nacho kukaiba”
“Hahaa ndio hivyo Mungu ninaye muomba sio wa mchezo mchezo. Siku akiamua kukufungulia manoti ya pesa, hakuna ambaye ana weza kuyazuia”
“Ila rafiki yetu tuambie siri ya kufanikiwa”
“Kuokoka tu, ndio siri ya kufanikiwa. Sasa nyinyi kaeni hapa kwa huyu mama mukichambana na kuzungumza mambo mabaya mwishowe. Mutaishia hapa hapa”
“Jamani kweli anacho kizungumza Mage. Tuache kukaa vibarazani na kuwachamba watu”
Magreth akampigia Sheby na kumuomba afike nyumbani kwake. Hazikupita hata dakika tano Sheby akafika nyumbani hapo. Mama Boka, akamsaidia Magreth kubeba begi hilo la nguo huku moyoni mwake akiwa ametawaliwa na wivu mkubwa sana. Magreth akagonga kwa nguvu mlango wa bi Ngedere.
“Nani huyo mja lanaaaa?”
Bi Ngedere alizungumza kwa kufoka na kuwafanya Magreth na wezake kucheka kichini chini. Magreth akagonga kwa nguvu hadi bi Ngedere akafungua huku akiwa amevimba kwa hasira. Bi Ngedere akatoa msunyo mzito huku akimpandisha na kumshusha Magreth.
“Nini na wewe?”
“Chukua funguo za chumba chako. Funguo nyingine utaichukua kwa mama Bakari pale, kuna vitu ndani ya chumba wakitoa basi watakupatia”
“Kisa funguo ndio una nigongea kama nime vamiwa?”
“Aha…jamani mbona hivyo. Una chukua au huchukui? Nakuachia banda lako la kuku nakwenda kuishi wanapo ishi watu sio hapa kwenye banda lako hili”
Magreth alizungumza kwa kejeli huku akimtazama mwana mama huyo.
“Koma wewe nyumba yangu si banda la kuku?”
“Basi kama si la kuku, ni banda la njiwa. Hahaaa ulininyanyasa sana wewe mama, ukihisi kwamba sinto fanikiwa. Ila Mungu amenifanikisha. , sasa uwe na kinywa kizuri kwa hawa wapangaji wengine, siku ukiwakejeli haki ya Mungu, Tanroad watakuja kupitisha bararaba ya lami hapa mtaani na hili banda lako litavunjwa na hapo ndipo utakapo rudi kwenye maisha ya chini kabisa. Utajua shida ambazo tunapitia sisi wapangaji”
Magreth mara baada ya kuzungumza hivyo, akafungu pochi yake na kutoa noti tano za shilingi elfu kumi na kumpiga nazo bi Ngedere usoni.
“Tutaonana huko barabarani kwa maana sitaki siku nikiwa na gari langu nishindwe kukupa lifti”
Magreth akawafwata nje wapangaji wezake. Akaagana nao na kuingia kwenye gari.
“Sheby”
“Naam boss”
“Leo tuna mizunguko mingi. Nipeleke kwenye duka lenye hadhi ya kuuza furniture za ndani”
“Sawa hapa kwa haraka haraka ni Danube pale Mlimani City”
“Haya twende ila kabla ya hapo twende hospitali nikamuone mgonjwa wangu”
 Magreth akafika hospitali ya Mwananyamala. Akaelekea kwenye chumba alicho lazwa Evans Shika. Wakasalimiana kwa furaha.
“Samahani juzi nilipata dharura na siku ya jana sikuweza kuonekana, kuna mambo kidogo yalitokea. Vipi una endeleaje?”
“Nina endelea vizuri sana. Dokta leo ameniambia kwamba wiki inayo fwata, nitapewa ruhusa”
“Habari nzuri sana Evans. Vipi wana kushughulikia vizuri swala la chakula?”
“Yaa wameniletea chakula kizuri na nina kula kwa wakati kabisa”
“Nafurahi kusikia hivyo. Leo ratiba yangu ni ngumu kuna sehemu nina zunguka zunguka baadae nitapita kukuona”
“Sawa Mage. Leo ume pendeza sana”
“Kweli?”
“Ndio”
Magreth akajiona mwanamke mwenye bahati sana mara baada ya kusifiwa na Evans. Akatamani kumbusu ila akajikuta akishindwa kwani hakuna kitu chochote walicho weza kukubaliana kwenye mapenzi.
“Evans nina swali moja”
“Swali gani?”
“Una mchumba?”
“Hapana sina kwa kweli”
“SAWA”
Magreth alijibu huku akiwa na furaha sana. Akamuaga Evans na kurudi kwenye gari. Wakaelekea katika duka kubwa linalo uza vifaa vya ndani. Magreth aka nunu kila kitu anacho kihitaji katika duka hilo, kisha akapatiwa lori la usafiri la kubebea vitu hivyo kwani ni vingi sana. Akaongozana na watu wa lori hilo huku yeye na Sheby wakiwa mbele. Wakafika nyumbani kwake maeneo ya Kigamboni. Akawasimamia watu wa kampuni hiyo ya Danube, kumpangia kila kitu alicho kinunu dukani kwao. Ndani ya muda mfupi nyumba hiyo tayari ikawa imebadilika, huku kila mmoja akisifia kwamba imepangwa vizuri.
“Sheby hapa ni kwangu”
“Aisee ina maana huto uza tena maandazi?”
“Ndio, nitakuwa nina rudi kitaani kuwasalimia kama kawaida”
“Aisee kweli nina haki ya kukuita boss”
Kabla Mage hajazungumza kitu chochote simu yake ikaanza kuita. Akaitazama namba hiyo ngeni, akaipokea na kupewa maelekezo na mwanaume aliye jitambulisha kwa jina la Clayton ni ofisi zipi aende akachague gari, huku akidai ni agizo kutoka kwa nabii Sanga.
                                    ***
    Mrs Sanga hadi kuna pambazuka hakuweza kupata usingizi kabisa. Mapigo yake ya moyo yamebadilisha muelekeo wake kabisa na amekuwa ni mtu aliye tawaliwa na mawazo kiasi kwamba ana tamani ardhi ipasuke ili immeze. Saa kumi na mbili asubuhi akaamka kitandani na kuelekea jikoni, akaandaa kifungua kinywa kizuri, kisha akarudi chumbani na kumuandalia mume wake suti anayo ipenda.
“Baba Julieth sasa hivi ni saa tatu kasoro amka ujiandae”
Nabii Sanga akamtazama mke wake kwa macho yaliyo jaa maswali. Akanyanyuka na kuingia bafuni, akaoga na kusafisha kinywa chake. Akafungua kabati la nguo na kutazama ni suti gani ambayo ata ivaa kwa siku hiyo.
“Baba Julieth nimesha kuandalia nguo hizo hapo”
Mrs Sanga alizugumza huku akujitahidi kutengeneza tabasamu la bandia. Nabii Sanga akazitazama nguo hizo alizo andaliwana mke wake, ila hakudhubutu kuzigusa. Akachukua suti nyingine na kutoka nazo hadi sebleni. Akambidhi mfanyakazi wake na kumuomba ampigie pasi. Akaingia jikoni, aka kaanga mayai mawili na soseji mbili.
“Dady leo ume amua kuingia jikoni?”
“Yaa mwanangu vipi chuo umekwenda siku mbili hizi?”
“Hapana sija enda. Askari walinizuia kwenda wakihofia usalama wangu”
“Ahaa..basi hakikisha leo una kwenda. Ulinzi wa malaika kutoka mbinguni utasimama juu yako”
“Sawa baba, ila mbona mama amesha andaa brakefast?”
“Ahaa nimependa leo nile chakula nitakacho pika kwa mkono wangu”
“Sawa dady I love you”
“I love you too daughter”
Julieth akambusu baba yake shavuni na kuelekea mezani. Mrs Sanga mambo yote yanayo endelea jikoni aliweza kuyashuhudia. Hali aliyo kuwa nayo mume wake hakika ikazidi kumuweka katika wakati mgumu sana. Wakati ambao hajui ni wapi ana anza kumuuliza mume wake, ikiwa ana tambua hali halisi iliyo mpata Tomas. Nabii Sanga akapata kifungua kinywa hicho. Akakabidhiwa suti yake na mfanyakazi wake na kuelekea chumbani, akavaa haraka haraka na kujiweka sawa.
“Baba Julitethi tuna weza kuzungumza”
“Kuhusiana na nini?”
“Mbona umerudi ila una onekana kuwa tofauti sana na awali?”
“Mkuu wa majambazi walio niteka aliniambia kwamba bosi wao ana hitaji nishikiliwe hadi wiki ijayo ndio wataniachia ili niende zangu Nigeria kwenye kikao cha wa wachungaji.”
Maneno hayo ya nabii Sanga yakamnyong’onyeza mrs Sanga. Hadi hapo akatambua kwamba mume wake ana tambua ni nini kinacho endelea na siri aliyo ihisi kwamba Tomas hato izungumza basi ipo wazi kwa mume wake.
“Ila sijui kwa nini aliye wapa kazi hakuhitaji kuniua kwa kutumia watekaji wake. Ila nina hisi ana hitaji siku moja aje kuitoa roho yangu kwa mikono yake mwenyewe. Ila kabla ya yeye kufanya hivyo basi nita hakikisha kwamba nina itoa roho ya kibaraka wake aliye mpatia pesa za kwenda kuwalipa majambazi kisha nitaitoa roho yake. Au una semaje mke wangu hilo si wazo zuri eheee?”
Nabii Sanga alizungumza huku akimkazia macho mke wake. Taratibu mrs Sanga akakaa kitandani huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga kwani kila kitu kinacho zungumwa na mume wake kina muhusu yeye.
                                                                                                ITAENDELEA
Haya sasa, Nabii Sanga ameamua kutumia njia ya mafumbo kumfikishia ujumbe mke wake. Mrs Sanga sasa yupo kwenye wakati mgumu wa mawazo je ata kiri kwa mumewe kwa makosa aliyo yafanya? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 15.
 


Share:

Digital Marketing Manager at Bongo Live

Digital Marketing Manager   Bongo Live is a cloud communications service provider based in Dar es Salaam with a presence across 18+ African markets (www.bongolive.africa). Our unique service provides enterprises the ability to reach and transact with customers across Africa via SMS, USSD, Airtime and Mobile Payments. Bongo Live has been named a Forbes Africa top 20 technology startup… Read More »

The post Digital Marketing Manager at Bongo Live appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Zonal Manager KCB Bank

Job Title: ZONAL MANAGER – CHANNELS Location TANZANIA Organization Name DIGITAL FINANCIAL SERVICES Department Description KCBT Digital financial services play a key role of enabling customers access various banking services through digital channels without them necessarily visiting the banking halls. It also plays a key role on driving the banks digital strategy that focuses on becoming digital first and digital… Read More »

The post Zonal Manager KCB Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger