Sunday, 17 May 2020

Ndugalile Amshukuru Rais Magufuli....Ummy Mwalimu Atoa Neno Baada ya Uteuzi wa Ndugalile Kutenguliwa

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amemshukuru kwa ushirikiano wake aliokuwa akimpa, aliyekuwa Naibu Waziri wake wa Afya, Dkt Faustine Ndugulile ambaye uteuzi wake ulitenguliwa jana na Rais Magufuli.

Hayo ameyabainisha leo Mei 17, 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter, na kumkaribisha kwa moyo wa dhati, Naibu Waziri wa Afya mpya Dkt Godwin Mollel, ambaye ameteuliwa siku ya jana.

"Asante Mh Faustine Ndugulile kwa utumishi wako na ushirikiano mkubwa ulionipatia katika kusimamia Sekta ya Afya nchini, kila la heri katika kuwatumikia wana Kigamboni, hongera Dkt Godwin Mollel karibu Wizara ya Afya, naahidi kukupa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao" ameandika Waziri Ummy.

Mapema leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dr Faustine Ndugalile amemshukuru Rais Magufuli kwa Kumwamini kwa kipindi chote alichodumu kama Naibu Waziri Wizara ya Afya.

"Nimepokea uamuzi wa Mhe Rais kwa unyenyekevu mkubwa. Ninamshukuru sana JPM kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake. Nawashukuru sana @umwalimu  na watendaji wote kwa ushirikiano walionipatia.
Mafanikio ya sekta ni makubwa sana. Namtakia kila la kheri NW ajaye Dkt Mollel. "- Ameandika Ndugalile



Share:

DEOGRATIUS NSOKOLO ACHAGULIWA TENA KUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI KIGOMA..VIONGOZI WENGINE HAWA HAPA

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma (KGPC)Deogratias Nsokolo akishukuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa kumpa fursa ya kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano.
Wajumbe wa mkutano mkuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi mpya wa Kigoma Press Club(KGPC) waliouchagua
Na Editha Karlo,Kigoma
Wanachama wa Chama cha Waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma (Kigoma Press Club - KGPC) wamewachagua viongozi wapya wa chama hicho katika nafasi mbalimbali ambao wataongoza kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka huu 2020 hadi mwaka 2025.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumamosi Mei 16,2020 katika ukumbi wa ofisi za KGPC Mwenyekiti wa uchaguzi huo Richard Katunka ambaye ni Mwandishi wa Star tv Mkoani Kigoma alisema Mwenyekiti mpya wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma ni Deogratius Nsokolo,huku nafasi ya makamu Mwenyekiti ikichukuliwa na Jacob Ruvilo.

Amesema wanachama wamemchagua Deogratis Nsokolo kwa kura wajumbe wote 28 kumpigia kura za ndiyo kuwa mwenyekiti mpya ambayo ni nafasi yake aliyokuwa anaitetea.

Nsokolo ambaye ni mwandishi wa ITV Mkoa wa Kigoma pia Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (UTPC) aligombea nafasi hiyo ya Mwenyekiti akiwa hana mpinzani hivyo wajumbe walimpigia kura za ndiyo na hapana na kufanikiwa kunyakua kura zote za ndiyo.

Nafasi ya makamu mwenyekiti imenyakuliwa na Jacob Ruvilo mwakilishi wa Azam Tv Mkoa wa Kigoma aliyeshinda kwa kura 22 za ndiyo ambapo nafasi hiyo alikuwa anaiwania peke yake.

Nafasi ya katibu Mkuu wa KGPC ilichukuliwa na Mwajabu Hoza mwakilishi wa Channel Ten Mkoa wa Kigoma baada ya kupata kura 15 na kumshinda mpinzani wake Fadhil Abdallah mwandishi wa Magazeti ya TSN aliyekuwa akitetea nafasi yake aliyepata kura 9  huku Rhoda Ezekiel mwandishi wa gazeti la Uhuru alijitoa kwenye nafasi ya kugombea ukatibu na nafasi ya katibu msaidizi ikichukuliwa na Emanuel Senny mtangazaji wa radio Joy aliyepata kura 22.

Nafasi ya Mweka hazina ilichukuliwa na Winne Bwire kwa kupigiwa kura za ndiyo 27 kati ya kura 28.

Kwa upande wa wajumbe wa kamati tendaji waliochaguliwa ni Prosper Kwigize mwakilishi wa DW aliyepata kura 14 Happy Tesha mwandishi wa gazeti la Mwananchi kura 15  na Adrian Eustate mtangazaji wa radio Kwizera aliyepata kura 23 jumla ya wagombea sita walijitokeza kugombea nafasi hizo.

Akizungumza baada ya uchaguzi Mwenyekiti mpya Deogratias Nsokolo aliwapongeza wajumbe kwa kumchagua na kuendelea kuwa na imani naye kuendelea kuongoza KGPC kama mwenyekiti aliahidi ushirikiano ili kuendeleza Klabu hiyo na kuwataka wanachama kutoa ushirikiano kwa uongozi huo mpya.

Aliwataka pia wanahabari kuchukua tahadhari wanapokuwa katika majukumu yao ya kazi kutokana na janga hili lililopo sasa la virusi vya Corona

"Wakati tulionao sasa ni wakati wa hatari kwa sababu ya ugonjwa huu wa virusi vya Corona na kazi zetu hizi kuna kipindi inatulazimu kujitumbukiza kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu tuwe na tahadhari ugonjwa huu hautahangalia eti wewe ni mwandishi tuchukue tahadhari kama tunavyoshauriwa na wataalam wa afya juu ya ugonjwa huu",alisema Nsokolo

Pia aliwataka waandishi kutumia kalamu zao kuelimisha jamii namna ya kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo kwa kufuata maelekezo ya wataalam wa afya.

Naye mwanachama Antony Kayanda amewataka viongozi hao wapya kuendeleza yale mazuri yote yaliyofanywa na uongozi uliopita ili kuendeleza Klabu hiyo ambayo imekuwa mfano kwa Klabu zingine nchini.

Naye mwanachama Magreth Magosso Abdallah amewapongeza viongozi wote waliochaguliwa katika nafasi mbalimbali na kuwataka kuendeleza yale mazuri yote yaliyoanza kufanywa na viongozi waliomaliza muda wao.

"Nina wapongeza nyote mlioshinda na kutangazwa na mlioshinda lakini kura hazikutosha nawapongeza pia tusonge mbele tuijenge KGPC yetu nguvu yetu inatosha kukipeleka chama chetu mbele",alisema
Share:

KANISA LA KKKT LAWAPATIA WAGANGA WA JADI USHETU VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA

Na Salvatory Ntandu - Ushetu
Katika jitihada  za kupambana na Ugonjwa wa homa kali ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona, Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini Mashariki ya ziwa Victoria limetoa Msaada wa vifaa vya kujikinga dhidi ya COVID 19 kwa  waganga wa tiba asili vyenye thamani ya shilingi Milioni 3.5.

Akizungumza katika hafla maalum ya kukabidhi vifaa hivyo Jana na  Askofu wa Dayosisi hiyo Dkt, Emmanuel Joseph Makala kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Michael Matomora alisema kuwa, Kanisa limetoa vifaa hivyo kwa  waganga hao ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa huo katika maeneo yao ya kazi.

Alisema ,Kanisa limebaini kuwa waganga wa tiba asili, wanafanya kazi katika mazingira hatarishi kutokana na kuhudumia wateja wao bila ya kuwa na vifaa maalumu vya kujikinga na ugonjwa wa COVID 19 kama vile  vitakasa mikono, ndoo za maji na barakoa.

“Kundi hili ni Muhimu hivyo,kanisa limeamua kuwajali kwa  kutoa vifaa hivi katika mikoa mbalimbali ya kanda ya ziwa kwa kuanza na Bariadi mkoa wa  Simiyu na Ushetu mkoa wa Shinyanga ili ,kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu”,alisema Dkt Makala.

Awali akipokea vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri hiyo Michael Matomora alilishukuru kanisa la KKKT kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitatumika na waganga wa jadi na vingine vitapelekwa katika  kituo cha afya Ukume ili kuwa kinga wagonjwa wanaokwenda kupata huduma katika maeneo hayo.

Alifafanua kuwa Ofisi yake itahakikisha vifaa hivyo vinawafikia waganga wote wa tiba asili  sambamba na kuyaomba mashirika mengine kuiga mfano wa kanisa la KKKT kwa kuendelea kutoa vifaa vya kujikinga na COVID 19.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa  waganga wa Tiba Asili katika Halmashauri hiyo, Shumileta Charles alisema wanaendelea kuzingatia maelekezo ya serikali katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na wanahakikisha kabla ya kutoa huduma wateja wao wananawa mikono na kuvaa barakoa.

“vifaa hivi vilivyotolewa na kanisa  vitasaidia kuwakinga waganga wa tiba asili dhidi ya janga la Corona na nichukue fursa hii kupitia vyombo vya habari kuwataka wazingatie maelekezo ya serikali ili kujikinga wao na pindi wanapokuwa wanawahudumia wateja wao,”alisema Charles.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MEI 17,2020

















Share:

RADIO FARAJA FM STEREO YAKABIDHI MSAADA KWA KAYA ZENYE KIPATO CHA CHINI KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA.

Share:

Saturday, 16 May 2020

MANISPAA YA SHINYANGA YATOA MICHE YA MITI KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA


Afisa Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga (kulia) akitoa miti ya matunda bure kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ambapo ni mwendelezo kwa manispaa ya Shinyanga kutoa miche ya miti ya kivuli na ya matunda kwa wananchi wanaoishi katika Manispaa ya Shinyanga katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga Shinyanga Press Club - SPC), Shaban Alley ambaye ni mwandishi wa habari wa Star Tv akipokea miti ya miembe,miparachi na mipera kwa niaba ya Waandishi wa Habari (kushoto) ni Mwandishi wa Habari Gazeti la Majira Patrick Mabula. Manispaa ya Shinyanga inaendelea kutekeleza Kampeni ya Kuhifadhi Mazingira kwa kugawa miti ya matunda na kivuli bure.
Mwandishi wa Habari Gazeti la Majira Patrick Mabula akiwa amebeba miche ya miti ya matunda baada ya Afisa Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga kukabidhi miche ya miti kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Mwandishi wa Habari Gazeti la Majira Patrick Mabulaakiwa amebeba miche ya miti ya matunda
Waandishi wa Habari wakichukua miche ya miti. Wa kwanza kushoto Mwandishi wa Habari Gazeti la Mwananchi, Stella Ibengwe ambaye pia ni Mweka Hazina wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga akiwa amebeba miche ya miti. Wa pili kushoto ni Katibu wa Mweka Hazina wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga Ally Lityawi ambaye ni Mwandishi wa habari gazeti la Tanzania Daima akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga Shinyanga Press Club - SPC), Shaban Alley ambaye ni mwandishi wa habari wa Star Tv na Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga Estomine Henry (wa kwanza kulia).
Share:

PROCUREMENT AND SUPPLIES OFFICER II (SUPPLIES OFFICER II) – 1 POST at Tanzania Revenue Authority (TRA)

POST PROCUREMENT AND SUPPLIES OFFICER II (SUPPLIES OFFICER II) – 1 POST POST CATEGORY(S) PROCUREMENT & LOGISTIC MANAGEMENT EMPLOYER Tanzania Revenue Authority (TRA) APPLICATION TIMELINE: 2020-05-15 2020-05-29 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.To identify stock item requirements for placement of orders. ii. To seek approval to purchase the identified requirements. iii.To prepare requests for quotations. iv.To receive… Read More »

The post PROCUREMENT AND SUPPLIES OFFICER II (SUPPLIES OFFICER II) – 1 POST at Tanzania Revenue Authority (TRA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

KIJANA AMUUA MAMA YAKE MZAZI KWA SHOKA KISHA KUNYWA DAMU YAKE ARUSHA

Jeshi la Polisi la Mkoa wa Arusha linamshikilia Daniel Emmanuel (32) Mkazi wa Sakila wilayani Arumeru,  kwa kukutwa akinywa damu ya mama yake Mzazi Eliyamulika Emmanuel Sarakikiya (79) kwenye kikombe, baada ya kumuua kwa shoka na kutenganisha shingo,mkono na mguu na kiwiliwili.




Akizungumza kwa masikitiko, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amesema mtuhumiwa huyo alifanya mauaji hayo Mei 15 mwaka huu, majira ya saa 9:00 mchana katika Kijiji cha Sakila chini,Kata ya Kikatiti,Tarafa ya King'ori wilayani Arumeru.

"Mtuhumiwa alimkata kwa shoka shingoni mama yake na kutenganisha na mwili wale na akaona haitoshi akakata mguu wa kulia na kuutenganisha na akakata mguu wa kushoto  pia akautenganisha wakati anafanya unyama huu alikuwa anakinga damu kwenye kikombe anakunywa,"amesema.

Amesema wakati alifanya tukio hilo majirani walishuhudia akinywa damu hiyo baada ya kumuua.

Kamanda Shana amesema hata hivyo polisi walipofika eneo la tukio mtuhumiwa alitupa kikombe alichokuwa ameshika mkononi kikiwa kimetapaa damu na kujaribu kukimbia.

"Lakini tulifanikiwa kumkamata na tumemweka mahabusu hadi upelelezi utakapokamilika,"amesema

Amesema katika hatua za awali za uchunguzi  inadaiwa mtuhumiwa huyo anamatatizo ya akili.

"Lakini hili sikubaliani sana sababu aliwezaje kuandaa shoka,mazingira tulivu yasio na watu,pia kwanini kama hana akili alikimbia polisi alipowaona na alipokamatwa alikataa kuhojiwa na polisi, hili linanipa shaka,"amesema

Amesema kutokana na hilo amemuagiza askari wa upelelezi wa kesi hiyo kuwasiliana na madaktari ili kumpima kama madai ya matatizo ya akili yana ukweli.

Ametoa wito kwa wananchi kupeleka ndugu zao  wenye matatizo ya akili polisi au hospitalini ili kuepuka madhara kama hayo. 



Share:

Mwanaume atupwa jela miaka 30 kwa kosa la kumwingilia kimapenzi mjukuu wake wa miaka 5

Na,Amiri kilagalila,Njombe
Mwanaume mmoja aliejulikana kwa jina la Charles Mwinami (45) mkazi wa kijiji cha Itunduma wilayani Njombe amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya kukutwa na hatia ya kumwingilia kimapenzi mjukuu wake mwenye umri wa miaka 5 na kutakiwa kulipa fidia ya shilingi Milioni Kumi kwa mwathirika.

Akisoma kesi no 12 ya 2020 hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoani Njombe Hassan Makube amesema mtuhumiwa amekutwa na hatia hiyo baada ya ushahidi wa daktari kuthibitisha mwathirika alifanyiwa kitendo hicho.

Mama mzazi wa mtoto huyo ameiambia mahakama kuwa wakati mtoto wake akifanyiwa ukatili huo alikuwa nje ya mkoa akifanya kazi za vibarua.

Shahidi namba nne ambae ni mtendaji wa kijiji cha Itunduma ameieleza Mahakama kuwa alipopata taarifa za tukio hilo alimwita mtoto ofisini kwake na kumhoji ambapo alikiri kulala na babu yake kitanda kimoja na kufanyiwa ukatili huo.

Mtoto huyo amekiri pia mbele ya mahakama kuwa alikuwa akilala na babu yake kitanda kimoja na kufanyiwa ukatili huo mara zote tangu mama yake kusafiri.

Baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha mahakama imeona mshitakiwa Charles Mwinami anakosa la kujibu ambapo alipopewa nafasi ya kujitetea alikana kufanya kosa hilo huku akisisitiza kuwa wakati huo hakuwa na ndugu wa kumwachia mtoto huyo kulala nae.

Jopo la mawakili wa serikali likiongozwa na  Hendry Mandwa na Happness Makungu wameiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

Akisoma hukumu hiyo hakimu Mkazi Mfawidhi Hassan Makube amesema kwa mujibu wa kifungu cha sheria no 158  kifungu kidogo cha kwanza A sura ya 16 mshitakiwa amekutwa na kosa hivyo amehukumiwa kwenda jela miaka thelathini na kutakiwa kulipa fidia ya shilingi Milioni Kumi kwa mwathirika.

Hata hivyo hakimu Makube amesema mahakama imeona kosa lingine la kubaka lakini hajatoa adhabu yake kwa sababu halikuwa kosa aliloshitakiwa nalo mtuhumiwa huyo.


Share:

ICT OFFICER II-(DATABASE ADMINISTRATOR) – 1 POST at Tanzania Revenue Authority (TRA)

POST ICT OFFICER II-(DATABASE ADMINISTRATOR) – 1 POST POST CATEGORY(S) IT AND TELECOMS EMPLOYER Tanzania Revenue Authority (TRA) APPLICATION TIMELINE: 2020-05-15 2020-05-29 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES     i. Architecture,Designs,develops,implements both logical and physical Database. ii. Develop back and front-end connectivity. iii. Implement security policy and access control. iv. Maintain physical organization of database objects. v.… Read More »

The post ICT OFFICER II-(DATABASE ADMINISTRATOR) – 1 POST at Tanzania Revenue Authority (TRA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Vifo Vya Corona Marekani Vyafika 88,507.....Trump Anadai Anamatumaini Chanjo Itapatikana Mwishoni Mwa Mwaka Huu

Rais Donald Trump wa Marekani amesema serikali yake itawekeza kwa makampuni yote makubwa yanayofanya jitihada za kutafuta chanjo ya virusi vya corona na kwamba imepunguza idadi ya makampuni hayo hadi kufikia 14, huku akitoa ahadi ya kuyapunguza zaidi.

Katika mkutano wake uliofanyikia Ikulu ya Marekani, ambapo ulihudhuriwa na maafisa wengi wa Ikulu hiyo wakiwa wamevaa barakoa, lakini yeye akiwa hajavaa, Trump alionesha matumaini kwamba kinga ya maradhi ya COVID-19  itapatikana kabla ya kumalizika mwaka huu.

Na kuongeza kusema serikali yake itashiriki vyema katika usambazaji wa chanjo hiyo pale tu, itakapopatikana. 

Hayo yanajiri wakati takwimu mpya zilizotolewa na chuo kikuu cha John Hopkins zinaonesha vifo vipya 1,680 ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliopita na kufanya idadi ya vifo kufika 88,507.

Maambukizi nchini Marekani yamefika  1,484,287  na waliopona ni 327,751


Share:

RATING II – 1 POST at Tanzania Revenue Authority (TRA)

POST RATING II – 1 POST POST CATEGORY(S) SECURITY EMPLOYER Tanzania Revenue Authority (TRA) APPLICATION TIMELINE: 2020-05-15 2020-05-29 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES   i. To assist the boat captain on steering the boat. ii. To assist the engineer to carry out the services and repairs. iii. To assist the mooring   and unmooring the boat. iv. To… Read More »

The post RATING II – 1 POST at Tanzania Revenue Authority (TRA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

CUSTOMS OFFICER II (CUSTOMS OFFICER) – 7 POST at Tanzania Revenue Authority (TRA)

POST CUSTOMS OFFICER II (CUSTOMS OFFICER) – 7 POST POST CATEGORY(S) ACCOUNTING AND AUDITING BANKING, ECONOMICS AND FINANCIAL SERVICES HR & ADMINISTRATION LEGAL STATISTICS AND MATHEMATICS TAXATION AND SOCIAL PROTECTION EMPLOYER Tanzania Revenue Authority (TRA) APPLICATION TIMELINE: 2020-05-15 2020-05-29 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES     i. To control imports, export and transit goods. ii. To carry… Read More »

The post CUSTOMS OFFICER II (CUSTOMS OFFICER) – 7 POST at Tanzania Revenue Authority (TRA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wagonjwa Wa Moyo Wapungua Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kwa Hofu ya Corona

Wagonjwa wenye matatizo ya moyo, kisukari, shinikizo la juu la damu, figo na saratani wameshauriwa kuhudhuria kliniki zao bila kukosa ili kuepuka kupata madhara ya kiafya ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha.

Rai hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza kuhusu kupungua kwa idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo tangu virusi vya Corona vilipoingia nchini.

Prof. Janabi alisema hivi sasa idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo imepungua kutoka 300 kwa siku hadi kufikia 50 kwa siku na wagonjwa wanaolazwa idadi yao imepungua kutoka 150 kwa siku hadi kufikia 30.

Kwa upande wa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo idadi yao imepungua kutoka wagonjwa wanne kwa siku na kufikia mgonjwa mmoja .

Wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo wamepungua kutoka kumi kwa siku na kufikia watatu.

Mkurugenzi huyo Mtendaji alisema wao kama madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo hawaelewi hivi sasa wagonjwa hao ambao hawahudhurii kliniki wanatibiwa wapi.

Alisema kama mgonjwa ataogopa kwenda Hospitali kwa kuhofia kupata maambukizi ya ugonjwa wa Corona ambao ukiupata na kupona haukuachi na madhara yoyote wakati kuacha kliniki za magonjwa ambayo kama usipotibiwa yatakusababishia madhara makubwa katika mwili wako.

Alisema wagonjwa wa moyo wanatakiwa kuondoa hofu kutokana na taarifa mbalimbali wanazozipata kuhusiana na ugonjwa wa corona jambo la muhimu wafuate maelekezo ya wataalamu wa afya kwa kufanya hivyo wataweza kuepuka kupata maambikizi ya ugonjwa huo na siyo kuacha kuhudhuria kliniki.

“Wote tunafahamu kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika ulimwenguni zinaonesha wagonjwa wenye matatizo ya moyo, kisukari, shinikizo la juu la damu, figo, saratani na watu wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 60 ndiyo wanaoathirika zaidi na ugonjwa wa Corona ikiwa wagonjwa hawa hawatahudhuria kliniki kama walivyopangiwa na madaktari wao wakipata maambukizi ya virusi vya corona ni rahisi kwao kupoteza maisha,” alisema .

“Wagonjwa wa moyo, kisukari, shinikizo la juu la damu, figo na saratani kama hawatahudhuria kliniki kwa kuhofia kupata maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Corona wanaweza kupata madhara ya kupoteza uhai, kupata kiharusi, kupoteza baadhi ya viungo vya mwili kwa mfano mguu, kupofuka macho na kupoteza nguvu za kiume lakini ukipata maambukizi ya virusi vya corona na ukapona hutaweza kupata madhara yoyote,” alisisitiza Prof.Janabi .

Prof. Janabi alisema ni muhimu wagonjwa hao kwenda Hospitali kutibiwa kwa kuwa mgonjwa akiwa na magonjwa hayo hawezi kujitibia nyumbani.

Alisema jambo la muhimu ni kufuata ushauri wa wataalamu wa afya hii ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni, kukaa umbali wa zaidi ya mita moja kati ya mtu na mtu na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

“Taasisi yetu inatuma ujumbe wa kuwakumbusha wagonjwa wetu kuhudhuria kliniki zao kutokana na tarehe walizopangiwa na madaktari lakini wengi wao hawaji kutibiwa.

“Ninaendelea kuwasisitiza waje kutibiwa kwani tumechukua tahadhari zote za kuhakikisha hawapati maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona wawapo katika eneo la Hospitali”,.

“Wagonjwa wanaofika kutibiwa hapa wanapimwa joto la mwili kabla ya kuanza kupata huduma ya matibabu, tumefunga mabomba ya maji pamoja na kuweka vitakasa mikono katika maeneo mbalimbali ya Taasisi yetu hii inawafanya kupata nafasi ya kunawa mikono mara kwa mara pia wanakaa umbali wa mita moja kati ya mgonjwa mmoja na mwingine,” alisema Prof. Janabi.


Share:

LECTURER – 1 POST at Tanzania Revenue Authority (TRA)

POST LECTURER – 1 POST POST CATEGORY(S) ACCOUNTING AND AUDITING BANKING, ECONOMICS AND FINANCIAL SERVICES IT AND TELECOMS LAND MANAGEMENT LINGUISTICS STATISTICS AND MATHEMATICS TAXATION AND SOCIAL PROTECTION TRADES AND SERVICES TRANSPORT AND LOGISTICS EMPLOYER Tanzania Revenue Authority (TRA) APPLICATION TIMELINE: 2020-05-15 2020-05-29 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.  To teach up to NTA level 8 for… Read More »

The post LECTURER – 1 POST at Tanzania Revenue Authority (TRA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wasamaria Wema Wafanikisha Matibabu Ya Mtoto Aliyezaliwa Na Matatizo Ya Moyo

Mtoto mwenye umri wa miaka minane (jina tunalo) ambaye alizaliwa na tatizo la moyo aliloishi nalo kwa miaka yote hiyo, ametibiwa kwa mafanikio katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Mtoto huyo aliyezaliwa pacha (wawili) alikuwa anakabiliwa na matatizo ya aina mbili ya moyo ikiwamo lile la tundu dogo kwenye vyumba viwili vidogo vya moyo, pamoja na mshipa mkubwa unaopeleka damu kwenye mapafu kwa ajili ya kusafishwa  kuziba  na kusababisha damu kushindwa kusafishwa vizuri.

Akizungumza kuhusu matibabu ya mtoto wake mama  mzazi wa mtoto huyo Stamil Abdallah ambaye ni mkazi wa Mkoani Ruvuma alisema  kwa kipindi cha miaka nane mwanae alikuwa akiteseka na maradhi ya moyo hivyo kupelekea ukuaji wake kuwa wa tofauti ukilinganisha na ule wa pacha wake.

“Nilikata tamaa kama mtoto huyu atakuwa na afya njema kwani kwa hali aliyokua nayo alikuwa anazimia mara kwa mara, moyo kwenda mbio, anachoka na kubadilika rangi katika vidole vya mikono yake na ulimi hali hii ilinipa wasiwasi, lakini sasa namshukuru Mungu mwanangu anaendelea vizuri”, alisema  Stamil.

“Nawashukuru sana wadau mbalimbali waliojitokeza kuokoa maisha ya mwanangu kwani mimi ninatokea katika familia yenye uwezo mdogo kiuchumi. Baada ya mwanangu kufanyiwa vipimo katika Hospitali ya Peramiho  na kugundulika kuwa na matatizo ya moyo nilikata tamaa kwakuwa sikujuwa ni wapi ningepata fedha za matibabu”,.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema  mtoto huyo alizaliwa na matatizo mawili, la kwanza ana tundu kati ya upande wa vyumba vidogo vya kushoto na kulia na tatizo la pili  ni mshipa mkubwa unaopeleka damu kwenye mapafu kwa ajili ya kusafishwa ulikuwa umeziba na kusababisha damu kushindwa kusafishwa vizuri.

Prof. Janabi alisema kutokana na tatizo hilo  damu ilikuwa haiwezi kwenda kwenye mapafu ili  damu chafu iweze kusafishwa kuchukua damu safi iweze kurudi kwenye moyo, ndiyo maana baadhi ya viungo vya mwili wake ikiwemo mikono, kucha, ulimi  na miguu vilikuwa  na rangi ya bluu.

“Baada ya kufanyiwa upasuaji amebadilika kabisa amekuwa wa pinki, ulimi na kucha zimerudi katika hali ya kawaida, tumempa tena nafasi  ya kufurahia maisha, atandelea na masomo yake  na kuweza  kucheza na wenzake kama wanavyofanya watoto wengine,”.

Naye Mkuu wa Idara ya watoto ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto Sulende Kubhoja alisema watoto wenye matatizo kama hayo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo kushindwa kupitisha damu vizuri  wako wengi ambao wanapokelewa na kutibiwa katika Taasisi hiyo.

Dkt. Kubhoja alisema wamefanikiwa kufanya upasuaji wa bila kufungua kifua na kuzibua  mshipa mkubwa unaopeleka damu kwenye mapafu kwa ajili ya kusafishwa  uliokuwa umeziba na kusababisha damu kushindwa kusafishwa vizuri. Baada ya kufanyia upasuaji  kiwango cha oxygen mwilini kimepanda kutoka asilimia 60 hadi kufikia asilimia 100.

“Ninawashauri  wazazi kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito na kuwapeleka watoto kliniki baada ya kujifungua hii itawasaidia kugundulika mapema kama wanamatatizo ya moyo na kuweza kupata matibabu kwa wakati”, alisema Dkt. Kubhoja.

Upasuaji wa bila kufungua kifua huwa unafanyika kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization Laboratory) ambapo mgonjwa anatobolewa tundu dogo katika mshipa wa damu ulioko kwenye paja.


Share:

Uteuzi Wa Wakurugenzi Wa Mamlaka Za Majisafi Na Usafi Wa Mazingira – Arusha Na Sumbawanga

 Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) amefanya uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira za Arusha na Sumbawanga kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia  tarehe 15 Mei, 2020.

Taarifa ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo imewataja walioteuliwa kuwa ni Mhandisi Justine Gordian Rujomba anayekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), na Mhandisi Gibon Nzowa anayekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Sumbawanga (SUWASA).

Uteuzi huo umefanyika chini ya Sheria Namba 5 ya Usambazaji Maji Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019. Aidha,  Wakurugenzi walioteuliwa watakuwa Makatibu wa Bodi za Wakurugenzi katika mamlaka hizo.

Kitengo cha Mawasiliano


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger