Wednesday, 13 May 2020

UJENZI WA KIWANDA CHA KUCHAKATA DHAHABU MWANZA WASHIKA KASI

 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wapili kulia) akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella  na kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Fredy Mahobe wakimsikiliza  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico Dkt Venance Mwasse akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu kinachojengwa mkoani Mwanza
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa kwanza kulia) na wajumbe alioambatana nao wakimsikiliza  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico Dkt Venance Mwasse akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu kinachojengwa mkoani Mwanza
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico Dkt Venance Mwasse akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu kinachojengwa mkoani Mwanza mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na wajumbe alioambatana nao katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza leo tarehe 12/05/2020.

 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na ujumbe ulioambatana naye wakiendelea na ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu mkoani Mwanza

 Mshauri Mwelekezi na Msimamizi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu kinachojengwa mkoani Mwanza Libaan Yasir akionesha katika ramani namna jengo la kiwanda cha kuchakata dhahabu kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella  na wajumbe walioambatana nao katika ziara hiyo.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella wakihitimisha ziara ya kukagua jengo la kiwanda cha kuchakata madini ya dhahabu mkoani 
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo kushoto akiagana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico Dkt Venance Mwasse mara baada ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho kuhitimishwa

Stamico ,Mkandarasi wamkosha Naibu Waziri Nyongo 

Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata madini ya dhahabu nchini umeshika kasi huku ujenzi wake ukitarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Septemba 2020 na kuifanya dhahabu ya Tanzania kusafirishwa ikiwa tayari imechakatwa na hivyo kuongeza thamani ya madini hayo katika soko la dunia.

Ujenzi wa kiwanda hicho ulianza rasmi mwezi Machi 2020 ambapo ujenzi wake mpaka sasa umefikia asilimia 40, imeelezwa kuwa kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda hicho utapelekea suala la kisheria la kutokusafirisha madini ghafi kutekelezwa ipasavyo.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 12 Mei, 2020 wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa kiwanda hicho na taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho unaoendelea kwa kasi Mkoani Mwanza kutolewa.

Akizungumzia mabadiliko ya sheria ya madini ya mwaka 2017, Naibu Waziri Nyongo alisema kukamilika kwa kiwanda hicho kutakwenda sanjari na sheria inayowataka wafanyabiashara   wa madini kutokusafirisha madini ghafi na badala yake madini yote kusafirishwa yakiwa yamechakatwa na kuongezewa thamani itakayopelekea kuuzwa kwa bei nzuri katika soko la dunia.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika eneo hilo la ujenzi, Naibu Waziri Nyongo alikiri kufurahishwa na usimamizi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na kasi ya mkandarasi anayesimamia ujenzi wa kiwanda hicho na kukiri kuwa Serikali itakuwa ikitembelea eneo hilo mara kwa mara katika  ili kuhakikisha ujenzi wake unakamilika kwa wakati na kiwanda kufunguliwa kwa wakati kama inavyotarajiwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse ameeleza kuwa ukamilishwaji wa mradi huo utakwenda sambamba na mradi wa kuwawezesha wachimbaji wadogo katika suala zima la kusafisha dhahabu waliyochimba katika maeneo yao.

Aidha, Dkt. Mwasse amesema msaada utakaotolewa kwa wachimbaji wadogo kutasaidia kiwanda hicho kupata malighafi zakutosha kwa ajili ya kulisha kiwanda kinachotarajiwa  kuzalisha kg 480 za dhahabu kwa siku yenye purity ya kiasi cha 999.99 ambacho ni kiwango cha juu kabisa cha purity ya dhahabu duniani.

Akielezea usafi wa dhahabu itakayokuwa ikizalishwa katika kiwanda hicho, Dkt. Mwasse amesema dhahabu hiyo itakuwa na thamani ya fedha kwa viwango vyake na hivyo yaweza kuhifadhiwa katika Benki Kuu ya Tanzania kama akiba.

Aidha, Dkt. Mwase amesema yeye na Taasisi anayoisimamia, wanajisikia fahari kubwa kusimamia azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda na wao wakiwa ni miongoni mwa taasisi inayosimamia viwanda mahususi kwa ajili ya kuongeza thamani ya madini nchini na kukiri shirika la madini linatekeleza azma hiyo kwa vitendo.

Pamoja na hayo, Dkt. Mwasse ameahidi kusimamia kikamilifu suala la utoaji wa kodi ya huduma pamoja na Uwajibikaji wa kiwanda hicho kwa jamii inayozunguka mradi huo katika kutatua masuala mbalimbali ya kijamii kama sheria inavyoelekeza.

Kwa upande wake, Mkandarasi wa ujenzi wa kiwanda hicho Libaan Yasir wa kampuni ya Aqe Associates LTD alikiri kuwa mradi huo ulipangwa kukamilika mwezi Desemba mwaka 2020 lakini kwa namna alivyojipanga pamoja na timu yake watakamilisha ujenzi wa kiwanda hicho ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.
Share:

Naibu Waziri Ikupa Atoa Msaada Wa Vifaa Kwa Ajili Ya Kukabiliana Na Ugonjwa Wa Corona Kwa Shirikisho La Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata)

Na.Mwandishi Wetu,Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amekabidhi msaada wa vifaa vya kukabiliana na ugonjwa wa Corona kwa Shirikisho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kwa ajili ya kusaidia kundi hilo maalum katika kujikinga dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19).

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo ikiwemo ndoo za kunawia mikono na mashine maalum ya kunawia pasipo kutumia koki “Free Hand Water Tape” Naibu Waziri, Ikupa alieleza kuwa Serikali inatambua mchango wa Watu wenye Ulemavu na ndio maana viongozi na wadau mbalimbali wamekuwa wakijitokeza katika kusaidia kwenye mapambano dhidi ya janga hili la Corona bila kusahau namna ya kuwasaidia watu wenye ulemavu pia katika kuwawekea mazingira wezeshi ya kukabiliana na ugonjwa huo.

“Nikiwa kama mdau nimeona umuhimu wa kukabidhi ndoo za kunawia mikono 90 na mashine maalum ya kunawia pasipo kutumia koki kwa ajili ya kusaidia watu wenye Ulemavu katika mikoa 10 ikiwemo Dar es salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Tanga, Pwani, Iringa na Morogoro,” alisema Ikupa

“Natambua kuwa uhitaji wa vifaa hivyo pamoja na barakoa (Mask), Vitakasa Mikono na Sabuni vinahitajika kwa wingi kwa ajili ya kusaidia watu wenye ulemavu katika maeneo mengine, nitaendelea kuangalia suala la huu uhitaji ili tuendelee kuwezesha kundi hilo maalum zaidi,” alisema

Aliongeza kuwa Serikali imeandaa miongozo katika kipindi hiki inayotazamia namna watu wenye ulemavu wanaweza kusaidiwa wakati huu ambapo mataifa mengi dunia yanaangalia namna bora ya kukabiliana na ugojwa huo, akitolea mfano wa vifaa vya kunawia ambavyo vimeboreshwa na kuwa jumuishi kwa watu wenye ulemavu pia.

Aidha, Naibu Waziri Ikupa alitoa wito kwa kundi hilo maalum kuendelea kufuata maelekezo yanayotolewa na viongozi na wahudumu wa afya Pamoja na kujenga tabia ya kusoma taarifa kwenye mitandao ya kijamii na meseji wanazopata kupitia simu zao za mkononi juu ya kukabiliana na Ugonjwa wa Corona (Covid-19).

Sambamba na hayo Mheshimiwa Ikupa amewataka wadau mbalimbali wenye nia njema kuendelea kujitokeza na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa Corona nchini.

Naye katibu wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa Dodoma Bw. Justus Ng`wantalima alitoa shukrani kwa Naibu Waziri na Serikali kwa ujumla kwa kutambua watu wenye ulemavu na kuamua kutoa msaada wa vifaa hivyo ambavyo ni rafiki kwa watu wenye ulemavu na alieleza kuwa vitawafikia walemavu wengi nchini na watanufaika kwa kujikinga na ugonjwa wa Corona.

“Haimanishi kama mtu ni mlemavu basi hawezi kupata maambukizi ya ugonjwa huu wa corona, ugonjwa huo unaweza kumpata mtu yoyote hivyo uwepo wa vifaa hivi utasaidia watu wenye ulemavu kujikinga na janga hilo,” alieleza Ng’wantalima.


Share:

Halmashauri Ya Wilaya Misenyi Yakusanya Zaidi Ya Bilioni 2 Mapato Yandani Kwa Mwaka Wa Fedha 2019/2020

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Halmashauri ya wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera imefanikiwa kwa kiwango kikubwa cha  ukusanyaji wa mapato ya ndani wilayani humo kutoka  bilioni 1.2 kwa mwaka wa fedha 2015/16 hadi bilioni 2.5 kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.
 
Ayo yameelezwa Mei 11 na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo (diwani wa kata ya Kyaka) Mh Projestus Tegamaisho wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa mwandishi wa mpekuzi blog mkoani kagera.
 
Akizungumza mh.Tegamaisho amefafanua kuwa kutokana na mafanikio hayo wameweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo  ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu katika sekita ya kilimo ikiwa nikuwapatia elimu juu ya uzalishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo na biashara kama miwa, ndizi, vanira na mazao mengine.
 
“Katika wilaya yetu ya misenyi  kuna uzalishaji wa mazao mbalimbali kama Ndizi, Maharage, Viazi lishe kilimo cha mahindi lakini sasa hivi tumepata zao mbadala watu wanalima Mpunga, Vanira lakini tuna kilimo cha Miwa ambalo ni zao la biashara Misenyi pamoja na kilimo cha Kahawa ”Amesema Tegamaisho
 
Miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo imetekelezwa ikiwa ni pamoja na ukarabati wa barabara zilizopo chini ya wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarura.
 
Kwa upande wa afya amesema vituo mbalimbali vya afya na zahanati zilizopo wilayani humo zimekarabatiwa nahalmashauri hiyo  tayari wamejenga zahanati mpya ya Ngando  katika kata Nsunga na kituo kipya cha afya Kabyaile kata Ishozi.
 
Aidha Tegamaisho ameeleza kuwa Zaidi  ya hekari 50 za aridhi zimetengwa na halmashauri hiyo  kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya hiyo itakayo jengwa katika kijiji Bulembo kata ya Mushasha.
 
Kuhusu sekta ya elimu amesema wakati wakiingia madarakani elimu ya msingi ufaulu ulikuwa 75.5%  lakini hadi sasa ufahulu wilayani humo  ni 84.8% na wanfunzi wote walio fahulu wamefanikiwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na wananchi wa Wilaya ya Missenyi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miundombinu ya elimu kama ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Sanjali na hayo mh Tegamaisho amesema kuwa mpaka sasa takiribani vijiji 68 kati ya vijiji 72 vya wilaya hiyo tayari vina nishati ya umeme na bado vijiji vya Bugango, Kakunyu,  Buchurago na kijiji Katano ambavyo vinatarajiwa kupatiwa umeme katika awamu itakayofuata.


Share:

Serikali yawakabidhi wavuvi injini za boti kuboresha uvuvi nchini

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekabidhi injini nane za boti awamu ya pili kwa wabunge wa majimbo mbalimbali kwa lengo la kuvipatia vikundi vya ushirika vya uvuvi vilivyopo katika majimbo yao ili kusawaidia kuboresha utendaji kazi wao na kufanya shughuli za uvuvi wenye tija. 
 
Awali wizara hiyo ilitoa injini za boti tano na kufanya jumla ya injini zilizotolewa na wizara hiyo kufikia 13 ambazo jumla zimegharimu kiasi cha Sh. milioni 60. 
 
Akikabidhi injini hizo za boti leo jijini Dodoma, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema kuwa Wizara yake inahimiza vyama vingine vya ushirika viboreshe utendaji wao wa kazi ili navyo viweze kupata ruzuku ya Serikali.
 
“Mtakubaliana na mimi kwamba wavuvi wetu wengi wanatumia zana duni sana na wanashindwa kufanya kazi zao za uvuvi kutokana na zana duni wanazotumia katika uvuvi na kutokana na zana zao hizo kuwa duni wanafanya kazi miaka nenda rudi lakini maisha yao hayabadiliki kutokana wanachopata ni kwa ajili ya chakula tu” alisema Waziri Mpina.
 
Ili kujua changamoto za wavuvi nchini, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanya tahmini kwa kuzunguka nchi nzima kujionea wananchi wanavyoendesha shughulizao za uvuvi ikiwemo changamoto wanazokutana nazo ambapo wamefanikiwa kuwaunganisha wavuvi katika vyama na vikundi mbalimbali ambavyo vinasaidia kurahisisha utendaji kazi ikiwemo kupata ruzuku kutoka Serikalini hatua inayowasaidia kufanya shughuli za uvuvi wenye tija kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
 
Akitolea mfano wa vikundi vilivyonufaika na mikopo, Waziri Mpina alisema kuwa Wilaya ya Ukerewe imefanikiwa kuwa na vikundi vya wavuvi ambao wamenufaika na mikopo ya zaidi ya Sh. milioni 500 na kufanya vyama vya ushirika nchini kufanikiwa kukopeshwa na taasisi za fedha zaidi ya sh. milioni 800.
 
Kwa upande wake Mbunge wa Kyela na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa wavuvi nchini wameanza kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano hatua ambayo itawafanya wawe na mafanikio makubwa kiuchumi.
 
Dkt. Mwakyembe alifafanua kuwa wilaya ya Kyelea ina mito mikubwa ya kudumu mine ikiwemo Kiwira, Songwe, Lufilio na Mbaka pamoja na ziwa Nyasa, lakini mazao ya samaki wilayani humo ni duni kutokana na mifaa duni vya uvuvi, hivyo injini ya boti aliyokabidhiwa itawasaidia wavuvi kuwa na uvuvi ambao utawasaidia kupata samaki wengi ambao watakidhi mahitaji ya soko.
 
Amesema injini hiyo itawasaidia wavuvi kuvua kiutaalamu zaidi na kwa usalama ikizingatiwa ziwa Nyasa kuna samaki wakubwa aina ya Mbasa ambao ni wakubwa kupita mitumbwi ya kawaida ambayo inatumiwa na wavuvi hao.
 
“Nina uhakika Wanakyela watahamasika kujiunga kwenye vikundi vya ushirika, wakulima hao hao wa Kyela ni sehemu ya wavuvi, wataunda vikundi imara, tutoke kwenye umasikini, tuongeze zaidi tija na mbinu za kisasa” alisema Dkt. Mwakyembe.
 
Aidha, Dkt. Mwakyembe amemthibitihia Waziri Mpina kuwa injini hiyo itawafikia wananchi na itatunzwa ili iweze kuwa na manufaa zaidi kwa wananchi wa Kyela.
 
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama amesema kuwa wavuvi wadogo wadogo wanachukua asilimia 85 ya wavuvi wote nchini ambapo samaki wote wanovuliwa ni karibu asilimia 90 wanavuliwa na wavuvi wadogo.
 
Katika mwaka 2019/2020, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetambua vyama vya ushirika vya wavuvi vipatavyo 102 katika mikoa yote nchini hatua ambyo imesaidia pia kuhamasisha kuanzishwa vyama vipya 14 na kufanya jumla ya vyama vya ushirika vinavyotambuliwa na wizara hiyo kufuikia 116.
 
Lengo la kuanzishwa vyama hivyo ni kuwawezesha wavuvi na wakuzaji viumbe maji kuwa na sauti ya pamoja ili waweze kupata mikopo na masoko ya bidhaa zao.
 
Vyama vya ushirika vilivyopata injini hizo za boti ni Magawa, Kisiju, Shungubweni vya mkoa wa Pwani, Mwamapuri wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Mbamba Bay wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, kikundi cha wavuvi Kyela mkoani Mbeya, kikundi cha Vita Fishing group Msanga Mkuu na Kikundi cha Jiwezeshe cha Nanyumbu mkoni Mtwara, Wakulima wa mwani Kwaigoma wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Bukasige Finshing Cooperative society cha Ukerewe mkoani Mwanza, kikundi cha wavuvi cha Nyamikoma cha Busega na kikundi cha wavuvi cha Kasanga Kalambo wanaofanya shaghuli zao eneo la ziwa Tanganyika.  





Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano May 13


















Share:

Tuesday, 12 May 2020

PROF.GABRIEL AWATAKA WAFANYAKAZI SEKTA YA MIFUGO KUTEKELEZA WELEDI KWA KUWATETEA WAFUGAJI

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo akizungumza katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katibu wa Baraza hilo Bw.Andrew Ponda akisoma maazimio kwenye kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo Bw.Stuart Mgunya,akizungumza kwenye kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo akieleza jambo katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala, Rasilimali Watu Sekta ya Mifugo Bi. Teddy Njau akizungumza katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mchumi kutoka wizara ya mifugo Bw.Francis Makusaro akitoa taarifa kwenye kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
................................................................................................................ Na.Mwandishi wetu, Dodoma

Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo limeazimia kuwatetea wafugaji ili kutovunja sheria,kanuni na kuwa fanya kutambua haki zao katika kutimiza malengo katika shughuli zao. 

Azimio hilo limetolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo katika kikao kazi cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.

Prof. Gabriel amesema kuwa sekta hiyo imejipanga vema kuchangia katika uchumi wa viwanda kwa kuzalisha malighafi ya kutosha itakayotumika katika viwanda vya hapa nchini katika kusukuma uchumi wa kati. 

"Watumishi wote wa sekta hii mnatakiwa kufanya kazi bila uzembe na kutoleta ubadhilifu katika sekta hii ili kulinda weledi wenu" amesema
 Prof. Gabriel. 

Aidha katika kikao hicho Prof.Gabriel ameeleza kuwa wameazimia kutekeleza majukumu ya wizara katika kiwango bora kinacho hitajika ili kuleta ubora katika kuwahudumia wananchi. 

Prof. Gbriel ameweka wazi kuwa kila mfanyakazi katika sekta hiyo atakatwa kiasi cha shillingi 10,000/= ili kuweza kuchangia katika mfuko wa faraja unaosaidia katika matatizo mbalimbali yanayomkuta mfanyakazi. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo Stuart Mgunya amesema kuwa wafanyakazi wanahaja ya kuwa pamoja katika kuboresha ustawi wa watumishi ili kufikia malengo yao katika kutimiza majukum yao. 

Mgunya ametoa wito kuwa kupatikane siku moja ya kuweza kuwashika mkono wastaafu katika wizara hiyo ikiwa ni ishara ya shukrani na pongezi kwa utumishi wao ulio tukuka katika kutumikia taifa. 

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala, Rasilimali Watu Sekta ya Mifugo  Teddy Njau amesema sasa ni wakati muhimu watumishi kujiunga katika mfuko wa faraja wenye lengo wa kusaidiana katika wizara hiyo.

Katika kikao hicho baraza hilo limemchagua Andrew Ponda kuwa Katibu wa Baraza na Katibu Msaidizi ni Suzanna Silayo ambao watakuwa madarakani kwa miaka mitatu.
Share:

SHIRIKA LA EYP LAUNGANA NA SHIRIKA LA SEMA KUTOA ELIMU YA CORONA

Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali Empower Youth Prosperity (EYP) lenye makao yake makuu Jijini Mbeya na Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoani Singida yameunganisha nguvu katika kutoa elimu ya kujikinga na Maambukizi ya Virusi corona  kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kutoa Elimu hiyo Mei 11,2020 kwenye eneo la Soko Kuu la Manispaa ya Singida Ofisa Mradi kutoka Shirika la SEMA Renard Mwasambili amesema programu wanayoitekeleza ni utoaji Elimu ya namna ya unawaji Mikono, utoaji wa Vifaa sambamba na elimu ya utengenezaji wa vifaa vya kujikinga na Virusi vya Covid 19 vinavyosababisha Ugonjwa wa Corona.

“Lengo la Elimu hii ambayo tunaifanya ni kutembelea maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko ya watu na kutoa elimu kwa mtu mmoja mmoja,makundi na wafanyabiashara namna ya kujikinga dhidi ya Ugonjwa huu”,alisema Mwasambili.

Alisema  programu hiyo imewashirikisha pia maafisa wa Shirika la Empower Youth Prosperity (EYP) kutoka mkoani Mbeya na kuongeza kuwa Kila mtanzania mahali alipo anapaswa kuchukua tahadhari na kamwe asipuuze ushauri wa kitaalamu unaoendelea kutolewa na Serikali pamoja na wataalamu wa afya.

Mkurugenzi wa Shirika la Empower Youth Prosperity (EYP) Mwakyusa amesema wanaendelea kutoa elimu juu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona ambao umekuwa tishio nchini na duniani kote huku akibainisha lengo la Umoja wao ni kupanua mahusiano yao na kuhakikisha ugonjwa Corona unatokomezwa.

Shirika la EYP lilianza mapambano haya mwanzoni mwa mwezi Aprili mkoani Mbeya na mkoa wa Songwe.

Kwa mujibu wa Afisa wa elimu ya afya kwa jamii na mkuu wa kitengo cha tafiti cha Empower Youth Prosperity (EYP) Ndg Amani Twaha amesema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kutoa elimu kwa zaidi ya watanzania 21,520 katika mkoa wa Sngida na Mbeya na kwamba elimu hiyo inatolewa pia katika mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook, Instagram na Whatsapp.

Amani amesema wanatarajia kutoa elimu hiyo katika mikoa mingine ya Tanzania ikiwa ni pamoja na mkoa wa Songwe unaotarajiwa kufikiwa hivi karibuni.


Mwezeshaji wa Mradi kutoka shirika la SEMA, Witness Anderson alisema homa kali ya mapafu inayosababisha Virusi vya Corona ni Ugonjwa unaoambukizwa kwa kuingiwa na maji maji yatokayo kwenye njia ya hewa wakati mtu mwenye Ugonjwa huo anapokohoa ama kupiga chafya.

Alitaja njia nyingine ya maambukizi ni kwa kugusa maji maji yanayotoka puani (kamasi),kugusa kitambaa au nguo zilizotumiwa na mtu mwenye maambukizi ya Ugonjwa huo au maeneo mengine yaliyoguswa na mtu mwenye Virusi vya Corona.

Akielezea jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo alitoa tahadhari ya watu kukaa mbali angalau mita moja au mbili jambo litakalosaidia kujiepusha na maambukizi iwapo mmoja kati ya watu hao atakuwa na maambukizi.

Alisema tahadhari nyingine inayopaswa kuchukuliwa ni kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kutumia kitambaa safi au sehemu ya mbele ya kiwiko cha mkono,kuepuka kugusana na mtu mwenye dalili za ugonjwa huo, kusalimiana kwa kushikana mikono,kukumbatia na kubusiana.

“Safisha mikono yako mara kwa mara kwa maji tiririka kwa kutumia sabuni au dawa ya kutakasa mikono na baada ya kunawa epuka kugusa macho,pua au mdomo na nguo badala yake jifute kwa kutumia tishu ambayo itatupwa sehemu salama baada ya kutumika”,alisema Anderson.

Baadhi ya maeneo ambayo shirika EYP na SEMA walitoa elimu hiyo mkoani Singida ni pamoja na eneo la Soko Kuu la Manispaa ya Singida, Soko Kuu la kimataifa la Vitunguu, Kituo kikuu cha mabasi,vituo vya bajaji, bodaboda, vituo vya kuuza mafuta, mama lishe, barabarani ambapo pia kwa siku ya leo May 12 watakwenda kutoa elimu hiyo katika wilaya za Iramba, Manyoni, Ikungi, Singida DC.
Afisa wa Shirika lisilo la Kiserikali la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoa wa Singida, Witness Andersoon (kushoto) akitoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara wa Soko la Vitunguu la Kimataifa la Manispaa ya Singida namna ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona mkoani Singida
Mmoja wa maafisa wa shirika la EYP Amani Twaha akiendelea kuota elimu kwa wakina mama mkoani Singida
Vita hii dawa yake ni elimu kwa kila kundi
Baadhi ya maafisa wa SEMA na EYP waliojitoa kuoa elimu juu ya ugonjwa wa corona
Elimu ikitolewa kwa madereva barabarani.
Baadhi ya mabango yaliyotumika kufikisha ujumbe
Maafisa wa Shirika hilo, wakitoa elimu kwa njia ya mabango.
Elimu ikitolewa Stendi Kuu ya Mabasi.
Msafiri akitoa maoni yake kwa mwanahabari kuhusu ugonjwa wa Corona.
Elimu ikitolewa kwa Mama Lishe.
Elimu ikitolewa katika vituo vya kuuza mafuta.
Elimu ikitolewa kwa madereva barabarani.
Elimu ikitolewa kwa madereva wa Bajaj.

JUA ZAIDI KUHUSU UGONJWA WA CORONA

Virusi vya Corona (Cov) ni familia ya virusi vinavoysababisha ugonjwa kuanzia mafua ya kawaida hadi magonjwa makali zaidi kama vile matatizo ya kupumua (MERS-CoV) na SARS-CoV.

Virusi vya Corona vya COVID-19 ni mripuko mpya uliogunduliwa mwaka 2019 na havikuwahi kubainika hapo kabla miongoni mwa bindamu. Dalili zake ni pamoja na homa, kikohozi, shida katika kupumua, na katika hali ngumu zaidi, maambukizi yanaweza kusababisha, nimonia, kukosa pumzi, kushindwa kufanyakazi kwa figo na hata kifo.
Share:

Wagonjwa Wa Corona Nchini Kenya Wafika 715 Baada ya Wengine 15 Kuongezeka

Watu waliofariki kutokana na Virusi vya Corona nchini Kenya wamefikia 36, Walioambukizwa 715 huku watu 259 wakiwa wamepona na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini humo imeeleza kuwa Mtoto wa mwaka mmoja na miezi minane ni miongoni mwa waliotambuliwa kuwa na virusi hivyo baada ya sampuli 978 kufanyiwa vipimo katika saa 24 zilizopita.

Naibu Waziri wa Afya Dkt.Rashid Aman ameeleza kuwa raia wawili wa Tanzania ni miongoni mwa waliothibitishwa kuwa na virusi vya Corona katika kituo cha mpakani cha Isebania baada ya kupimwa na hivyo wamerejeshwa Tanzania.

Aidha wizara hiyo ya Afya imefafanua kuwa watu wawili walifariki wakiwa nyumbani na mwingine mmoja akiwa hospitalini ambao wamefikisha idadi ya waliofariki kufikia 36, huku maambukizi mapya 15 ya virusi vya Corona yaliyofanya idadi 715 ya walioambukizwa


Share:

Wawili Mbaroni Kwa Kujaribu Kuingia Mbuga Za Wanyama Kwa Ujangili Huku Wengine Wakimbilia Nchi Jirani Ya Kenya

Na Ahmeid Mahmoud
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha huko kwenye kitongoji cha Oloshoo kata ya Enguserosambu Tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro wamefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya AK 47 yenye namba H 49 ikiwa na risasi 12 iliyokuwa njiani kufanya uhalifu kwenye Mbuga za wanyama.

Aidha kwa muktadha huo Mapambano dhidi ya matukio ya uhalifu na wahalifu ambapo kwa kipindi hichi wahalifu wengi hudhani jeshi la polisi limelala hivyo niwahakikishie hatujalala na tunaendelea kufanya misako na opereseheni mbalimbali iwe wakati wa mvua Jua Tope au Masika Baridi au kiangazi kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi ya kutenda uhalifu.

Akiongea na vyombo vya habari mkoani hapa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana alisema kuwa kikosi hicho kabambe baada ya kupewa taarifa fiche kuwa kuna watu 4 wawili watanzania na wakenya wawili wameonekana maeneo ya Mpakani wakiwa wanajipanga kuwinda wanyama adimu kwenye mbuga zetu muhimu.

Kwa mujibu wa Kamanda Shana baada ya kupata taarifa hizo kikosi kazi chenye askari machachari wazalendo na wenye weledi wa hali ya juu waliendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini juu ya taarifa hiyo na tarehe 10.6.2020 tulifanya msako mkali katika kijiji hicho kuwatafu wahalifu hao.

Alisema kuwa katika msako huo wahalifu wawili walikamatwa wakiwa na silaha moja ya kivita aina ya AK 47na risasi zake 12 ndani ya magazine ambao majina yao tunayahifadhi kwa ajili ya uchunguzi huku jeshi hilo likiendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili waliokimbia nchi jirani ya Kenya.

Aidha jeshi la polisi linawasaka wahalifu hao kujisalimisha mara moja kituo chochote cha polisi kwani wasipofanya hivyo tutalazimika kutumia nguvu kubwa kuwatafuta ili hatua kali za kisheria zichukuliwe.

Kamanda Shana akatumia fursa hiyo kuendelea kuwashukuru wananchi ambao wameendelea kutoa taarifa mbalimbali za uhalifu na wahalifu huku akiwataka kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuwafichua wale wote wenye nia ovu ili kumaliza uhalifu kwenye mkoa wetu.

Amebainisha kuwa Jeshi hilo mkoani hapa linaahidi litatoa donge nono kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazo fanikisha kuwakamata wahalifu wanaojihusisha na Uwindaji haramu ,Ujambazi ,na uhalifu wa aina yeyote.


Share:

Serikali Yaahidi Kuendelea Kutoa Ajira Kwa Wauguzi Nchini

WAMJW - Dar es Salaam
Serikali imesema itaendelea kutoa kipaumbele katika ajira za wauguzi kadri nafasi zitakavyokuwa zikipatikana ili kuboresha huduma za afya nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mwananyamala katika Maadhimisho ya Siku ya Waguzi Duniani  ambayo huadhimishwa tarehe 12 Mei kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Wauguzi; Sauti inayoongoza Uuguzi kwa Dunia yenye Afya.”

Waziri Ummy Mwalimu amesema Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika ajira za wauguzi kwa sababu kuna uhaba wa wauguzi kwenye vituo vya afya licha ya kuwapo zaidi ya wauguzi 30,451 katika vituo vya umma na binafsi nchini.

Amesema asilimia 80 ya huduma  za afya katika vituo vya kutoa huduma za afya zinatolewa na wauguzi hivyo Serikali itaendelea kutambua na kuthamini kazi nzuri zinazofanywa na wauguzi nchini.

 “Wauguzi wamekuwa wapambanaji wakubwa katika kutoa huduma kwa washukiwa wa ugonjwa wa Corona (Covid-19), hivyo hongereni  wauguzi wote nchini Tanzania,” amesema Waziri.

Amesema katika jitihada za Serikali za kuboresha huduma za wauguzi na wakunga, Serikali imekamilisha muongozo wa kutoa huduma kwa kuzingatia utu, heshima na maadili.

Waziri wa Afya amesema jumla ya waguzi 778 katika hospitali 15 za rufaa za mkoa wamepatiwa mafunzo muhimu ili kuwezesha mpango wa kutoa huduma rafiki kwa wananchi na kwa kujali utu wao.

“Mafunzo haya yataendelea kutolewa katika ngazi zote za kutoa huduma na tayari tumetengeneza mfumo wa kupokea taarifa za malalamiko na kero kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Naye Rais wa Chama cha Wauguzi na Wakunga Tanzania (TANNA), Bw. Alexander Baluhya amesema ili kuwapo kwa huduma bora na salama za afya, nchi inapaswa kuwa na wataalamu wenye weledi wa hali ya juu na mazingira bora ya kazi.

“Hivi sasa nchi yetu ina wauguzi 30,451 waliojiriwa katika sekta ya afya ambao ni takribani asilimia 60 ya wataalamu wote wa afya. Wauguzi hawa wanatoa zaidi ya asilimia 80 ya huduma za afya ambazo zimekuwa zikitolewa kwa Watanzania. Hivyo upungufu wa wauguzi na wakunga ni  asilimia 48,” amesema Bw. Baluhya.

Bw. Baluhya amewapongeza wauguzi  nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao hasa katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19).


Share:

Je? Umeachwa na mke/ mume/mchumba na bado unampenda ?

Je? Umeachwa na mke/ mume/mchumba na bado unampenda ? Kuna mtu unamtaka unashindwa kumwambia?

Ipo dawa ya kumvuta  mume, mke ,mchumba na mtu yoyote unaye muhitaji katika mahusiano na kumfanya atimize unachokiitaji kutoka kwakwe na kumfunga asiwe na mtu mwingine zaidi yako hata kama yupo mbali ndani ya masaa .(2) tu na kukutafufuta yeye mwenyewe  .

Unamatatizo ya kushika mimba ? Na ukishishika zinaharibika?dawa zipo .

PIA.TUNAYO DAWA YA ASILI YA NGUVU ZA KIUME YENYE KUTIBU MATATIZO MATATU KWA WAKATI MMOJA (1)nguvu za kiume ,(2) Kuongeza maumbile (3)kuchelewa kufika  kilelen.

Yajue .matatizo yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume .
(1)ngiri ya kupanda na kushuka
(2)korodani moja kuvimba
(3)tumbo kuunguruma,kujaa ges.
(4)kisukari
(5)presha
(6)kiuno kuuma
(7)kutopata choo

 Tunatibu kisukari Suki (14)vidonda vya tumbo siku(30) mmiguu kufa ngazi,kuwaka moto .anapandikiza nyota ya kushinda bahati  na sibu ,kusafisha nyota kukupa mvuto wa ajabu ,kutoa nuksi na mifungo mbalimbali zindiko za nyumba na biashara  Peter za bahati .huzuia chuma ulete kwenye biashara .hurudisha Mali zilizopotea anao uwezo wa kumurudisha alie mbali  :humaliza kesi .(4)PIA TUNATIBU.BUSHA BILA OPARESHEN.

Kwa mawasiliano tupigie No.0747100745( Namba hii pia iko Whatsapp)


Share:

AMUUA MKE WAKE KISHA KUMUUNGUZA MOTO KWA KUNYIMWA TENDO LA NDOA



Jeshi la polisi mkoa wa Mara limamshikilia Mokiri Wambura (46) mkazi wa Kengesi wilaya ya Serengeti mkoani Mara kwa tuhuma za kumuua mke wake Mwise Kyobe(38) kwa kumkata mapanga na kisha kumuunguza kwa moto ndani ya nyumba kwa madai ya kunyimwa tendo la ndoa kwa zaidi ya miaka miwili.

 Bwana huyo pia amemjeruhi kwa kumkata mapanga mtoto wake wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja.
Share:

WANAODAIWA KUWA MAJAMBAZI WAVAMIA NA KUPORA MATAIRI YA GARI LA KAMANDA WA POLISI GEITA


Jeshi la polisi mkoani Geita linawashikilia watu wawili waodaiwa kuwa ni majambazi huku likiendelea kuwasaka watu kadhaa kwa tuhuma za kuvamia usiku wa manane eneo lililokuwa limehifadhiwa gari la kamanda wa polisi mkoa huo na kuiba matairi yake yote manne kisha kutokomea pasipojulikana.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Lotson anasema katika hali isiyo ya kawaida watu hao kwa kushirikiana na walinzi walifanya uporaji huo kwa kufungua matairi hayo kisha kutokomea nayo huku jeshi hilo likiendelea na msako ili wahusika wote wakamatwe na kuchukuliwa hatua. 
Share:

Spika Ndugai Atoa Masharti Ya Kumtimua Bungeni Cecil Mwambe

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, amewataka wale wote wanaotaka amfukuze Ubunge Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe, basi wamshauri amuandikie Spika barua ya kujiuzulu kwake, halafu waone kama ataendelea kukaa bungeni.

Spika Ndugai ameyabainisha hayo leo Mei 12, 2020 na kusema kuwa maamuzi hayo yote ya kumrejesha Mwambe bungeni, yamekuja kutokana na yeye kupata barua ya upande mmoja.

"Nimeeleza Mwambe amewahi kuniandikia barua lini?, hivi wewe ungekuwa Spika ungefanyaje, huna barua ya mtu kujiuzlu ungefanyaje?, unamfukuza tu!, lazima mchunguze na muangalie mzani uko wapi, Mwambe yupo hajafa, mwambieni aandike barua anikabidhi mimi, akishanikabidhi muone kesho yake itakuwaje" amesema Spika Ndugai.

Aidha Spika Ndugai amesema kuwa leo jioni atatolea ufafanuzi kuhusu tamko lililotolewa na CHADEMA, kwamba Wabunge wake waliojiweka karantini kwa sasa hawatorudisha posho kwa sababu wao siyo wezi


Share:

MAMA AUA MTOTO WAKE WA MIAKA MIWILI ILI APATE UTAJIRI KISHIRIKINA ALIVYOELEKEZWA NA SANGOMA WA SUMBAWANGA

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ulrich Matei

Na Esther Macha,Mbeya
WATU wanne wanashikiliwa na Polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mtoto, Tamali Simon (2), ambapo miongoni mwa watuhumiwa ni mama mzazi wa mtoto huyo akidaiwa kushirikiana na watu hao kufanya unyama huo.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ulrich Matei amesema jana kwamba watuhumiwa hao walikamatwa wakati wa msako maalum uliofanywa na Polisi Mei 6, mwaka huu saa 4.00 usiku katika Kijiji cha Iwindi Kata ya Utengule Usongwe Mji Mdogo Mbalizi.

Kamanda Matei amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Rehema Kasela (36) ambaye ni mama mzazi wa mtoto, Riziki Muhema (20) mkazi wa Mtakuja Mbalizi 3, Estar Msongole (52) mganga wa kienyeji mkazi wa Sumbawanga, Mtumwa Haonga (65) mganga wa kienyeji mkazi wa Mtakuja Mbalizi ambao wote wanatuhumiwa kumuua mtoto Tamali mwenye umri wa miaka miwili na miezi mitatu.

Aidha Kamanda Matei amesema chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kupata utajiri kwa njia za ushirikina na baada ya mtuhumiwa ambaye ni mganga wa kienyeji kuwapa masharti yaliyopelekea kifo cha mtoto huyo.

Akielezea zaidi Kamanda Matei amesema Mei 4, mwaka huu saa 2.00 usiku katika Kijiji na Kata ya Iwindi Tarafa ya Usongwe mtoto Tamali alikutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na mtu asiyejulikana na mwili wake kutelekezwa.

Amesema baada ya tukio hilo Polisi walifanya msako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa katika maeneo tofauti na kwamba wakati wa mahojiano watuhumiwa walikiri kuhusika kwenye tukio hilo baada ya kupewa masharti na mganga wa kienyeji.

“Polisi walipofanya upekuzi nyumbani kwa mganga wa kienyeji walikuta vifaa mbali mbali vya uganga na dawa za kienyeji za aina mbali mbali, upelelezi wa tukio hilo unaendelea na mara baada kukamilika watafikishwa mahakamani,”amesema.
Share:

RAIS TRUMP AKATISHA MKUTANO NA WAANDISHI BAADA YA KUKERWA NA SWALI LA MWANDISHI WA HABARI

Rais Trump amekatisha mkutano na waandishi baada ya kukerwa na swali la Mwandishi wa CBS Weijia Jiang aliyemuhoji ni kwanini amekuwa anashindana kwa kujigamba kuwa USA inaongoza kupima corona kuliko wote wakati wana vifo zaidi ya Elfu 81.

Trump alimjibu hapaswi kuulizwa kwanini Wamarekani wengi wanazidi kupoteza maisha wakati sehemu nyingi duniani watu wanapoteza maisha hivyo sio swala la ajabu huku akisisitiza kuwa swali hilo wanapaswa kuulizwa China kwa kuwa wao ndio wameleta Corona na sio Yeye.

Baada ya kuona mwandishi anahitaji kujibiwa swali lake Trump akaona isiwe tabu akaamua kuondoka zake. 

Trump aliulizwa kuwa “Why is this a global competition to you if every day Americans are still losing their lives and we’re still seeing more cases?”
Share:

Kigwangalla: Hatuwezi Kushuhudia Sekta Ya Utalii Ikipigwa na Corona

Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk, Hamis Kingwangalla amesema kuwa hatuwezi kushuhudia  sekta ya utalii ikipigwa na janga la Covid – 19 wakati kunamianya mbalimbali ya kuifungua sekta hiyo kwa kujadili mambo mbalimbali yanayopaswa kuchukuliwa ili watalii waje nchini.

Dk, Kingwangalla aliyasema hayo jana Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii nchini katika maandalizi ya mpango wa kupokea watalii baada ya janga la Covid – 19

Alisema sekta ya utalii itakuwa ni sekta ya kwanza kaamka hivyo kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea na ikumbuke sekta hii ni sekta nyeti inayoingiza fedha nyingi za kigeni.

Alisema ni vyema sasa tujadiliane jinsi ya kuweka mambo mbalimbali ili kuifungua sekta ya utalii ingawa si jambo rahisi maana sekta hii imeathirika sana na ugonjwa huu hivyo lazima tujadili ili kuweka mikakati ya kuweka mbele yetu na baadaye tufungue milango ya kibiashara

“Tunakila sababu ya kujenga imani katika soko hili la utalii ikiwemo upimaji wa Corona kwa wageni wetu na jinsi ya kudhibiti sababu hatutaki tumwambukize virusi mtalii na sisi tusiambukizane”

Lazima tuangalie msingi ya afya iliyotolewa na inayotolewa na sekta za afya tuonaona nchi mbalimbali zimeanza kufungua mipaka yake na sisi lazima tuwe na viwango vibavyitakiwa ili kuwahudumia watalii wataokutwa na virusi tutawahudumiaje

Alisisitiza ugonjwa huu upo hivyo ni lazima sasa kutafuta mbinu zaukuhakikisha  tahadhari  mbalimbali za kudhibiti ugonjwa huu ikiwemo kuhakikisha tunajaribu kufanya utalii kwa tahadhari kubwa na kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na wizara husika.

“Haya tutakqyoyajadili lazima tuweke imani na kufuata muongozo itakayokubaliwa na serikali ikiwemo kuweka viwango vinavyotakiwa hivyo ni lazima tujadili jambo hili kwa kina na kisha kesho (jumanne) nitaongea kwa kina na vyombo vya habari ili kusema yale tuliyokubaliana “

Sekta hii imeathirika sana kwa familia zinazotegemea utalii sekta binafsi, mahoteli na sehemu nyingine hivyo lazima tujadiliane na kuyafikisha katika mamlaka zinazohusika

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Profesa Adolf Mkenda alisema kikao hicho ni muhimu na ni lazima watu wawe wazalendo katika kuhakikisha sekta ya utalii inanyanyuka tena

Kikao hicho kinashirikisha washiriki kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania  (Tanapa) , Mamlaka ya Hifadhi ya Njiro (NCAA) , Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori  Tanzania (Tawa)  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Uhamiaji.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger