Sunday, 12 April 2020

UTPC,THRDC,MCT NA TEF WATOA MWONGOZO KWA WAANDISHI WA HABARI NA WANANCHI KUJIKINGA NA CORONA


USHAURI KWA WANAHABARI KUHUSU KUCHUKUA TAHADHARI ZAIDI KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA CORONA

Siku ya Ijumaa Aprili 10, 2020 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilitoa taarifa kwa umma juu ya mwenendo wa ugonjwa wa corona nchini. Katika taarifa hiyo Waziri wa afya alieleza idadi ya watu waliothibitishwa kupata maambukizi ya COVID-19 nchini kuwa ni 32. Kati ya hao, wagonjwa 24 wanaendelea na matibabu, watano wamepona na uwepo wa vifo vya wagonjwa watatu tangu ugonjwa huu ulipoingia nchini. 


Tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na familia za waliopoteza ndugu zao kutokana na ugonjwa huu unaosababishwa na virusi vya corona. 
Wito wetu kwa Wanahabari na Wananchi

Kutokana na kuongezeka kwa visa vya corona nchini ambavyo inaonyesha vimeanza kusambaa ndani ya nchi (Local Transmission and not imported). Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa pamoja tunatoa ushauri kwa wanahabari, taasisi mbalimbali na wananchi kama ifuatavyo: 

1. Kuchukua tahadhari zaidi na kutoa taarifa kwa wakati kwenye mamlaka husika endapo wakibaini mtu mwenye dalili za maambukizi ya virusi vya corona. 

2. Tunawasisitiza waandishi wa habari, taasisi mbalimbali na wananchi kutumia teknolojia ya kisasa katika kufanya kazi zao au mikutano, kwa mfano kutumia Skype, Zoom, kupiga simu, WhatsApp N.K. 

3. Tunashauri vituo vya habari nchini kupunguza vipindi vya kawaida na kuanza kutumia vipindi hivyo kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kujikinga na virusi vya corona. Wananchi wapewe nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa kutoka kwa wataalamu. 

4. Waandishi wa habari wanapaswa kuzingatia kwa makini taratibu za kitaaluma, huku wakihakikisha kutumia vyanzo vya habari vya kuaminika kama vile Wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani (WHO).

5. Wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari zaidi za kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa kuzingatia Miongozo iliyotolewa na MCT,(https://ift.tt/2K0u2B4), THRDC (https://ift.tt/34uLcAd), Shirika la Frontline Defenders https://ift.tt/34wsEQ0 pamoja na elimu inayotolewa mara kwa mara na Wizara ya Afya https://ift.tt/3ecouBn.

6. Waandishi wa habari wanapaswa kuchunguza kwa makini aina ya matukio ambayo wanapanga kuhudhuria, kutokana na uwepo wa amri ya Serikali inayokataza mikusanyiko ya idadi fulani ya watu ili kujikinga na hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya corona. 

7. Wamiliki wa vyombo vya habari wanapaswa kuwawezesha waandishi wa habari usafiri binafsi au kutumia uber, gloves ukiwa, mavazi ya kujikinga kiafya kama vile suti ya kitabibu (bodysuit) na barakoa inayofunika uso gubigubi (full face mask). 

8. Tunatoa ushauri kwa waandishi wa habari kufuata sheria na kuomba ruhusu kwa mamlaka husika endapo wanahitaji kukusanya taarifa kutoka maeneo ya karantini, hospitali na maeneo mengine yenye vizuizi vya kuingia. 

9. Tunapenda pia kuishauri serikali kutenga maeneo maalumu ya watoa huduma kwa wagonjwa wa corona ili wasirudi majumbani mwao kuepusha maambukizi kwenye familia zao. 

10. Tunatoa ushauri kwa watu wote mfano viongozi, Asasi za Kiraia, wanasiasa, viongozi wa dini, watu mashuhuli watumie vipaji vyao kuelimisha umma kuhusu namna ya kujikinga na virusi vya corona kwa kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Afya. 

11. Tunawahimiza waandishi wa habari pale wanapokusanya taarifa, kutumia maikrofoni ya kushikilia (directional mic) kwa kuishika kwa mbali iwezekanavyo, badala ya kutumia maikrofoni inayoshikizwa kwenye mavazi (clip mic). 

12. Meza na vifaa vyote vya kufanyia uhariri, kompyuta, vichanganyio (mixers) na vifaa vingine vya kazi lazima vifutwe na vitakasa mikono kila baada ya kipindi au shughuli ya uhariri.

13. Ni muhimu kushirikisha Asasi za Kiraia, vyombo vya habari binafsi na vya serikali katika kamati zinazoundwa kukabiliana na virusi vya corona kwa kuwa AZAKi na vyombo vya habari ni wadau wakubwa katika kutatua changamoto za kijamii. 

Kwa kutambua umuhimu wa kazi za waandishi wa habari, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania utatoa mafunzo kwa waandishi wa habari mikoa yote Tanzania bara na Zanzibar kwa njia ya mtandao ili kuwawezesha namna bora ya kufanya kazi za uandishi salama hasa katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona. 

Imetolewa kwa pamoja na:
THRDC, MCT, TEF na UTPC
Dar es Salaam, Tanzania 
Aprili 12, 2020.
Share:

WHO yafuatilia wagonjwa waliopona kubainika tena kuwa na virusi vya corona

Shirika la Afya Duniani WHO limesema linazitathmini ripoti za baadhi ya wagonjwa wa COVID-19 kugugundulika kuwa na virusi vya corona kwa mara nyingine baada ya vipimo vya awali kubainisha kupona ugonjwa huo. 

Maafisa nchini Korea Kusini waliripoti kwamba wagonjwa 91, ambao walionekana kuwa salama baada ya kupimwa, baadae walipatikana navyo katika vipimo vingine. 

Mkurugenzi wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa na Kinga nchini Korea Jeong Eun-kyeong amesema upo uwezekano wa virusi hivyo kupata nguvu mpya, kuliko maambukizi mapya. 

Shirika la WHO limesema linachukua tahadhari zote juu ya kuwepo kwa taarifa hizo kutoka maeneo tofauti. 

Kwa mujibu wa muongozo wa WHO mgonjwa anaweza kuruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupimwa mara mbili mfululizo katika kipindi cha masaa 24 na kubainika kutokuwa na virusi.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili April 12











Share:

Saturday, 11 April 2020

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO


Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 


⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.

FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

Watu 2,108 Wafariki Kwa Corona Nchini Marekani Ndani ya Masaa 24

Marekani imekua nchi ya kwanza duniani kurekodi zaidi ya vifo 2000 vya virusi vya corona kwa siku moja.

Takwimu kutoka Chuo Kikuu Johns Hopkins zinaonyesha kuwa watu 2,108 wamekufa katika kipindi cha saa 24, huku kukiwa sasa na zaidi ya watu nusu milioni walioambukia virusi hivyo nchini Marekani.

Marekani hivi karibuni inaweza kuipita Italia kwa idadi zaidi ya vifo vinavyotokana na virusi hivyo kote duniani.

Marekani sasa ina takribani vifo 18,693 na idadi ya visa vilivyothibitishwa ni 500,399, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, ambacho ndicho kinachofuatilia takwimu za ugonjwa huo kote duniani.

Italia imeripoti vifo 18,849 huku vifo zaidi ya 102,000 vikiripotiwa kote duniani kutokana na virusi vya corona. 


-BBC


Share:

Mwanafunzi Mbaroni Kwatuhuma Za Kuchapisha Taarifa Za Uongo Mitandaoni Kuhusu Corona

SALVATORY NTANDU
Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linamshikilia Mariamu Jumanne (23) Mkazi wa Mwadui ambaye ni  Mwanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana wa COVID 19 hapa nchini.

Taarifa iliyotolewa leo na  Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Debora Magiligimba kwa vyombo vya habari alisema kuwa Mariamu anatuhumiwa kuchapisha ujumbe wa maandishi kwenye mtandao wa Whatsapp  unaosema Tanzania ina wagonjwa 230 wa COVID 19  na Idadi ya wagonjwa  waliofariki ni wanne.

Alisema kuwa Machi 26 mwaka huu askari wa kikosi kazi cha mtandao kilifanikiwa kuona ujumbe kwenye mtandao huo wa kijamii wenye taarifa za uongo mtandaoni pamoja na kutoa takwimu za uongo.

Kamanda Magiligimba alisema kwa Mariamu alikamatwa  Aprili 9 mwaka huu Majira ya saa mbili Usiku eneo la Mwadui, Mtaa Wa Tabora, Kwenye Machimbo Ya Almasi Wilaya Ya Kishapu Mkoani humo baada ya kumufuatilia kwa njia ya mtandao

“Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii na kuacha kupotosha watu kuhusiana na ugonjwa wa COVID 19,”alisema Magiligimba.

Kamanda Magiligimba alisema kuwa  hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mariamu kuhusiana na makosa aliyoyafanya.

Mwisho.


Share:

Video : NCHAINA MADIRISHA - AGNESS


Hii hapa ngoma mpya ya Msanii Nchaina Madirisha kutoka Kahama inaitwa Agness. itazame hapa mtu wangu

Share:

Mzeewa miaka 75 auawa na kufungwa kamba kuonyesha amejinyonga

Na Amiri kilagalila,Njombe
Mzee Arusha Nziku (75) mkazi wa wilaya ya Wanging’ombe mkaoni Njombe,amekutwa amefariki nyumbani kwake huku akiwa amefungwa kamba ndani ya nyumba yake kuonyesha amejinyonga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema waliotekeleza mauaji hayo walitumia kamba kumfunga na kuonyesha kama amejinyonga.

“Ni mzee ambaye amekufa akiwa nyumbani kwake na hawa wauaji walichokifanya ni kwamba baada ya kumuua wakamfanya kama amejinyonga,ile kamba wameifunga lakini kwa ufupi wa lile jengo na urefu wa ile kamba inaonyesha kifo ni cha mashaka”alisema Hamis Issa

Amesema mpaka sasa jeshi la polisi limeingia kazini kuhakikisha ni kitu gani kilicho sababisha kifo cha mzee huyo.


Share:

Mikopo Yatajwa Kupunguza Ufanisi Wa Kazi Kwa Walimu Kahama

SALVATORY NTANDU
Walimu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutojihusisha na mikopo isiyokuwa na tija kutoka katika taasisi za kifedha hali ambayo imetajwa kupunguza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yao katika vituo vyao vya kazi.

Kauli hiyo imetolewa April 10 mwaka huu na Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama Timoth Ndanya wakati akifungua mkutano wa uchaguzi mkuu wa chama cha walimu wilaya ya Ushetu ambao umefanyika katika Mjini kahama na kujumuisha walimu zaidi ya 126.

Amesema kuna tabia ya baadhi ya walimu wa shule za msingi na Sekondari wamekuwa wakikopa fedha katika taasisi hizo hadi kufikia robo  tatu ya Mishahara yao na kujikuta wakishindwa kumudu gharama za maisha katika vituo vyao vya kazi na kujikuta utendaji kazi wao ukizorota.

“Ofisi yangu inaendelea kufanyia kazi mashauri ya walimu waliokopa fedha katika taasisi hizi ambayo utendaji kazi wao uko chini,hatupendi kuona mwalimu anafukuzwa kazi ama kusimamishwa kutokana na kushindwa kutimiza machukumu yake kutokana na madeni anayodaiwa”,alisema Ndanya.

Ndanya aliongeza kuwa ni bora wakakopa kwa malengo na kuacahana na tabia ya mazoea ya kukopa fedha kwa watu binafsi au benki ambazo zinariba za juu na kujikuta wanakatwa fedha nyingi katika mishahara yao ya kila mwezi na kujikuta wakishindwa kufanya kazi kwa ufanisi katika vituo vyao vya kazi.

“Kuna utaratibu tunauandaa hivi karibuni tutautangaza ambao utawezesha walimu wetu kutojiingiza katika tamaa za kukopa fedha na utawezesha kupata mahitaji ya kujikimu hali ambayo itaongeza ufanisi katika majukumu yao,”alisema Ndanya.

Sambamba na hilo Ndanya aliwataka viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo kuwa daraja la kuwaunganisha walimu na waajiri wao sambamba na kuhakikisha wanasimamia maslahi ya walimu katika vituo vyao vya kazi.

Nae Mwalimu Miraji Jafari alisema kuwa wengi wao wanakopeshwa fedha na taasisi hizo kwa riba kubwa na kujikuta wakishindwa kumaliza madeni yao kwa wakati na kujikuta wakishindwa kutimiza majukumu yao katika vituo vyao vya kazi.

“Serikali iweke utaratibu mzuri wa kuwapa mikopo yenye riba nafuu walimu ili waweze kutimiza malengo yao na kuongeza tija ya kazi katika vituo vyao vya kazi”,alisema Jafari.

Katika Uchaguzi huo Mwalimu Juma Nyakanyenge alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CWT wilaya ya Ushetu,Mwalimu Thomas Athon akichaguliwa kuwa mweka hazina na mwalimu Sanga Maura akichaguliwa kuwa mwakilishi kwa upande wa walimu wa kike.

Mwisho.


Share:

AKAMATWA SHINYANGA KWA KUSAMBAZA TAARIFA NA TAKWIMU ZA UONGO KUHUSU CORONA KUPITIA WHATSAPP


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Mwaka wa Tatu Kitivo cha Kiswahili Mariam Jumanne Sanane (23) kwa kosa la Kuchapisha na kusambaza taarifa na takwimu za uongo kuhusu Corona kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsapp. 

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari leo Jumamosi Aprili 11,2020,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba mtuhumiwa alikamatwa Aprili 9,2020 majira ya saa mbili na dakika saba(2:07) usiku eneo la Mwadui, mtaa wa Tabora, kwenye machimbo ya almasi wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kwa kosa la kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii. 

“Tarehe 26/03/2020 Askari wa kikosi kazi cha mtandao kilifanikiwa kuona ujumbe kwenye whatsapp uliotumwa na mtuhumiwa unaosema ‘mpk ss Tanzania ina wagonjwa wapatao takribani 230 wa Covid 19 na waliofariki ni 04”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

Amesema mtuhumiwa amepekuliwa na kukutwa na simu iliyotumika kutuma ujumbe huo na ameshahojiwa na atafikishwa mahakamani kwa makosa ya kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo mtandaoni pamoja na kutoa takwimu za uongo. 

Kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii na kuacha kupotosha watu kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Share:

Wimbo Mpya : SHY TOWN ARTS - CORONA

Malunde 1 blog inakualika kusikiliza wimbo unaitwa Corona kutoka Kwa Wasanii kutoka Shinyanga 'Shy Town Arts'.
 
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazrti ya Leo Jumamosi April 11





















Share:

Friday, 10 April 2020

Rais Magufuli Ashiriki Ibada Ya Ijumaa Kuu Katika Kanisa La Mtakatifu Yohana....Asema Tanzania Haitafunga Mipaka wala Kuwazuia Watu Kutoka Ndani

Rais Magufuli amesema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa sababu kufanya hivyo kutasababisha madhara ndani na nje ya Tanzania.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Aprili 10, 2020 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mlimani Wilaya ya Chato mkoani Geita alipoungana na waumini kusali ibada ya Ijumaa Kuu iliyoongozwa na Padri Innocent Sanga wa jimbo Kuu Katoliki la Mbeya.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema  Serikali ya Tanzania imeamua kutowazuia watu ndani ya nyumba zao wala kufunga mipaka kwa kutambua madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kutokana na kufanya hivyo ndani ya nchi na kwa nchi nane ambazo zinategemea kupata huduma na bidhaa kupitia Tanzania hususani Bandari ya Dar es Salaam.


Share:

China yakemea ubaguzi wa rangi dhidi ya Waafrika waishio nchini humo kwa kisingizio cha corona

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imekemea vitendo vya unyanyasaji na ubaguzi dhidi ya Waafrika wanaoishi katika jimbo la Guangdong kusini mwa nchi hiyo na kusisitiza kuwa, serikali ya Beijing itaendelea kuhakikisha raia wote wa kigeni wanapatiwa haki sawa nchini humo.

Tamko hilo la Wizara ya Mambo ya Nje ya China limetolewa baada ya video na picha kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha Waafrika wengi wakiwa wamezagaa mitaani katika maeneo mbalimbali nchini China wakiwa na mabegi ya nguo, wakidai wamefukuzwa kwenye nyumba zao na mahotelini.

Taarifa zaidi zimedai kwamba, vitendo hivyo vya ukiukaji haki za binadamu vimekuwa vikifanywa na mamlaka za serikali ya China ambazo zinawashutumu raia wa kigeni hususan Waafrika kwamba wanasambaza ugonjwa wa COVID-19 nchini humo.

Mmoja wa raia wa Kiafrika ambaye kwa sasa anaishi nchini China amesema: "Tunapitia changamoto nyingi, kwani tumejifungia ndani kwa takribani miezi mitatu. Changamoto kubwa ni ubaguzi wa rangi, kwani imefikia wakati sasa haturuhusiwi kupata huduma za afya katika mahospitali."
 
Aidha imeripotiwa kuwa, Waafrika wanaoishi nchini China hawaruhusiwi kununua bidhaa kama chakula katika masoko makubwa na pia wanazuiliwa kula katika migahawa nchini humo.

Akijibu tuhuma hizo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Zhao Lijian, amesema: "Tangu ulipoanza mripuko wa corona, China na nchi za Afrika zimekuwa zikishirikiana kupambana na ugonjwa huu. Hivyo hatuwezi kusahau msaada uliotolewa na nchi za Afrika wakati tulipokuwa tumeathirika zaidi na ugonjwa huu."

Hayo yanajiri wakati hivi karibuni Kikosi Kazi cha waatalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye asili ya Afrika, kimetaka kuwepo na uwiano na usawa wa makundi mbalimbali ya binadamu wakati wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, la sivyo utoaji wa huduma kwa misingi ya rangi unaweza kusababisha vifo zaidi.

Ripoti ya wataalamu hao imetahadharisha kuwa, ubaguzi wa kimfumo katika utoaji  huduma unaleta matokeo ya kibaguzi na vifo zaidi na idadi ya wagonjwa miongoni mwa watu wenye asili ya Afrika.


Share:

Atiwa Mbaroni Kwa Kumuua Mkewe Baada ya Kumfumania na Mwanaume Mwingine Ndani ya Nyumba Yao

Tukio la kwanza
Tarehe 10.04.20202 majira ya 04:00hrs alfajiri, huko kijiji cha Nyamanga, kata ya Ukara, wilayani Ukerewe, Pastory Majura, miaka 52, msukuma, Mkazi wa kijiji cha Nyamanga – Ukerewe, anatuhumiwa na kosa la mauaji baada ya kumuua
Mkewe aitwaye Anusiata James, miaka 52, mzinza, Mkazi wa kijiji cha Nyamanga, kwa kumpiga Kichwani na kitu kizito baada ya kumfumania mke Wake nyumbani kwake akiwa na mwanaume Mwingine ambaye alikimbia baada ya mtuhumiwa Kumkuta nyumbani kwake.

Mume wa marehemu ambaye kwa sasa ni Mtuhumiwa mara baada ya kumshambulia na Kumuua mkewe aliamua kujichoma tumboni na kitu Chenye ncha kali ambapo alipata maumivu makali Na kukimbizwa hospitali ya wilaya ya ukerewe kwa matibabu. Upelelezi wa shauri hili unakamilishwa na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi Na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa Marehemu kwa ajili ya mazishi.

Kuelekea sikukuu ya pasaka.
Jeshi la polisi mkoa wa mwanza kwa kushirikiana Na vyombo vingine vya usalama limejipanga vizuri Kuhakikisha sikukuu ya pasaka inasheherekewa Kwa amani na utulivu.

Linasisitiza wananchi kujiepusha na misongamano isiyo ya lazima kwani adui wetu mkubwa kwa sasa ni virusi vya corona (covid 19), lakini jeshi linatoa onyo juu ya watu wanaopanga kujaribu hata kuwa kwenye nafasi ya kutaka kutekeleza uhalifu kwamba atakaejaribu jeshi halitasita kumkamata kabla na hatua za kisheria zitachukuliwa.

Jeshi la polisi mkoa wa mwanza linaendelea Kuwashukuru wananchi wote wanaoendelea Kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili Wakamatwe kabla ya matukio na linaendelea Kujielekeza katika mfumo wa kimaadili wa Kutotoa siri ya watoa taarifa. Jeshi linawatakia Sikukuu njema ya pasaka.


Share:

Serikali Yasema Licha Ya Mipaka Ya Nchi Kujifunga Wageni Wachache Wanaoingia Nchini Wanahudumiwa Kwa Hadhi Sawa Na Mataifa Mengine

Serikali imesema licha ya mipaka ya nchi kujifunga kutokana na janga la ugonjwa wa COVID 19,wageni wachache wanaoingia nchini wanapokelewa kwa mujibu na taratibu za kuingia nchini na kuhudumiwa kwa hadhi inayoendana na mahitaji ya Kimataifa kama ilivyo katika nchi nyingine yeyote duniani huku tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo ikipewa kipaumbele.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Kanali Wilbert Augustine Ibuge ameyasema hayo alipofanya ziara katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kukagua na kujionea namna wageni kutoka mataifa mbalimbali wanavyopokelewa na hatua wanazopaswa kuzifuata kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini.

Balozi Kanali Ibuge amesema licha ya ukweli kwamba kwa sasa wageni wanaoingia nchini ni wachache sana kutokana na mipaka kujifunga ni muhimu serikali kuhakikisha kuwa wale wachache wanaoingia wanafuata taratibu za nchi na kupewa utaratibu wa namna ya kujikinga na ugnjwa wa COVID 19 bila ya uwepo wa malalamiko kutoka kwa wageni hao.

Ameongeza kuwa ameridhishwa na hali ilivyo katika uwanja huo wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa kuwa hadhi wanayopewa wageni hao haina tofauti na hatua zinazochukuliwa katika mataifa mengine duniani na kwamba ni muhimu kufanya hivyo ili kuhakikisha usalama wa Taifa na raia wake kwa ujumla.

Amewataa watumishi wanaoendelea kutoa huduma katika uwanja huo kuchukua tahadhari ya kujikinga na COVID 19 huku wakitumia kauli nzuri wakati wa kutoa huduma.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Kanali Wilbert Ibuge amekagua jengo la kwanza la uwanja huo na jengo jipya la tatu akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege TAA Mhandisi Julius Ndyamukama.


Share:

Lifahamu Toleo Jipya la Simu ya INFINIX S5pro.....Ina RAM Kubwa na Selfie ya Juu

Teknolojia inaendelea kukua kwa kasi katika uzalishaji wa simu janja na Infinix Imethibitisha hili kupitia toleo jipya la Infinix S5pro iliingia sokoni mapema mwezi huu. Infinix S5pro ni simu ya kwanza kwa kampuni ya Infinix kuwa na teknlojia ya pop up camera. Fahamu mengi zaidi ya Infinix S5pro; 

Simu hizi zina RAM zenye ukubwa tofauti wa 4GB na 6GB hivyo itakuwezesha kufungua programu au kufanya mambo mbalimbali kwa wakati mmoja bila kukwama kwama, na uwezo wake wa kuhifadhi taarifa (video, picha, miziki, faili) ni 64GB na 128GB. Aidha, ina sehemu ya kuweka memory card kwa ajili ya kuiongezea uwezo wa kuhifadhi taarifa. 

Kwa wale wanaopenda simu zenye kioo kikubwa na chenye ubora simu hii yenye uzito wa gramu 195 ni kwa ajili yao kwani kioo chake (IPS LCD) kina ukubwa wa inchi 6.53" chenye ubora wa 1080p.  

Kamera yake ya mbele (selfie camera) yenye 40MP ni ya kipekee zaidi ambapo hutokezea juu ya simu pale unapotaka kupiga picha na ukimaliza inarudi kujificha ndani ya simu, (mechanical pop-up piece) hii inakuwezesha kupata picha zenye ubora zaidi. 

Wale wapiga picha, simu hii ina kamera 3 za nyuma ambapo kamera ya kwanza ina 48MP (f/1.8 lens), kamera nyingine ina 2MP ambayo hii ni sensor kwa ajili ya picha za karibu (potraits) ambazo huonesha hadi sehemu ya mabega. 

Kamera ya mwisho (QVGA) ni maalum kwa ajili ya kuweka sawa mwanga wakati wa upigaji picha. Pia inauwezo wa kurekodi video zenye ubora na muonekano ang'avu wa hadi 1080p. Yote haya ni kuhakikisha wewe mtumiaji unapata kilicho bora zaidi. 

Uwezo wa betri ya simu hii ni 4,000 mAh ambayo inaweza kukaa zaidi ya siku moja bila kuichaji. Simu hii ina mfumo endeshi (OS) Android 10, na utaweza kuuboresha kadiri maboresho yatakavyotoka.  

Katika kuhakikisha kuwa unapata habari mahali popote ulipo, ndani ya simu kuna programu ya redio (FM Radio). Jingine ni kwamba tumeimarisha usalama wa taarifa zako kwani utaweza kuifunga simu yako kwa kutumia alama za kidole. 

Wajanja wanatumia vyenye ubora wa kipekee, tembelea sasa duka letu la Infinix lililopo karibu nawe uwe wa kwanza kujipatia simu hii. Ukikosa utaambia nini watu?


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger