Wednesday, 1 April 2020

Viwanja Vikubwa Vinauzwa: Mapinga na Bunju

Viwanja Vikubwa Vinauzwa: Mapinga na Bunju
Mapinga, mpani na Bunju, vipo viwanja vya bei zifuatazo:
Mita 20/20 ni tsh 5 mil,
Mita 20/30 ni tsh 7 mil,
Mita 20/40 ni tsh 10 mil,
Robo eka ni tsh 12 mil,
Nusu eka ni tsh 22 mil,
Eka moja ni tsh 42 mil

Kwa Bunju, viwanja vipo mtaa wa Fanaka (Bunju A) na bei ni milion 30 kwa kiwanja cha sqm 1000.

Viwanja hivi vipo umbali wa km 2 kutoka main road (Dar to Bagamoyo Road) Na huduma zote za umeme na maji zipo.

Ukipata ujumbe huu mjulishe ndugu/jamaa/rafiki.

Hakuna dalali/udalali
Mpigie mhusika: 0758603077,
Whatsap 0757489709


Share:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Yatoa Tahadhari Ya Mvua Kubwa Mikoa 15

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa kwa siku mbili kuanzia kesho katika mikoa 15 ikiwamo Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, katika siku hizo, kutakuwa na mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Njombe, Iringa, Songwe, Mbeya na Rukwa.

Meneja wa Kituo Kikuu cha Utabiri wa Hali ya Hewa (TMA), Samuel Mbuya, alisema kutokana na tahadhari hiyo, athari zinazoweza kutokea kwenye maeneo hayo ni makazi na barabara mbovu kuzungukwa na maji hali itakayosababisha kukosekana kwa makazi na adha ya usafiri.

Kwa siku ya Ijumaa, alisema mvua kubwa inatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, Zanzibar, Pwani, Mafia, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Morogoro na kujirudia tena mikoa ya Njombe na Iringa.

Mbuya alisema kutokana na tahadhari hiyo, wakazi wa mikoa hiyo wanapaswa kuchukua hatua za kujikinga na kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na TMA.


Share:

Burundi yatangaza kuwa na wagonjwa wa corona kwa mara ya kwanza

Waziri wa afya nchini humo Thadée Ndikumana, ametangaza watu wawili ambao ni raia wa Burundi kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Raia hao ambao wote ni wanaume, mmoja ana umri wa miaka 56 huku mwingine ana umri wa miaka 42, na walikuwa wanawasili kutoka Rwanda na Dubai, Waziri alisema.

Taifa la Burundi linatarariwa kuwa na uchaguzi mkuu wa rais tarehe 20 Mei Mwaka huu


Share:

Daktari aliyekutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin wiki iliyopita apatikana na virusi vya Corona

Daktari aliyekutana na rais wa Urusi Vladimir Putin wiki iliyopita alipokuwa akizuru hospitali moja huko Moscow, amepatikana na virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo, Televisheni ya serikali, Rossiya 24, imeripoti leo Jumanne.
 
Rais wa Urusi alizuru hospitali ya Kommunarka Jumanne wiki iliyopita ambapo alikutana na daktari mkuu wa hospitali hiyo Denis Protsenko. 

Wote wawili hawakuwa wamevaa vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona wakati wa mazungumzo yao.

"Hali ni shwari," ofisi ya rais wa Urusi (Kremlin) imesema, ikinukuliwa na shirika la habari la RIA, huku ikikumbusha kwamba Vladimir Putin huwa anafanyiwa vipimo mara kwa mara.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano April 1




Share:

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Aguswa Na Kifo cha Katibu Mkuu CUF...... "Nimepoteza rafiki wa muda mrefu"

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, ameonesha kuguswa na msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Khalifa Suleiman, aliyefariki Dunia usiku wa kuamkia leo na kusema kuwa amepoteza rafiki yake wa muda mrefu.

Dkt Kikwete ameyabainisha hayo leo Machi 31, 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter, na kutoa pole kwa Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wanachama wote na kwamba wamepoteza kada wa kuaminiwa na kutumainiwa.

"Ni kweli tulikuwa pande mbili tofauti, lakini kama wanadamu tulikuwa marafiki tangu wakati tukiwa wote bungeni na hata baada ya mimi kuacha Ubunge, daima nitamkumbuka kwa moyo wake wa upendo, ukarimu, ucheshi na huruma, tuko pamoja katika majonzi na kuomboleza, tunakuombea wewe binafsi, wanachama wote wa CUF na familia ya marehemu moyo wa subira na ustahamilivu. Innalilahi Wainna Ilaihi Rajiun" ameandika Dkt Kikwete.


Share:

Tuesday, 31 March 2020

IGP Sirro Awaonya Watalii Kutojihusisha Na Biashara Ya Dawa Za Kulevya

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa Jeshi la Polisi kamwe halitamvumilia mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo kujihusisha na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya pamoja na uhalifu mwingine.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akifungua kituo cha utalii Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja kisiwani Zanzibar, huku akiwataka watendaji wa Jeshi la Polisi nchini kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa weledi na kwa kufuata misingi ya kisheria na kufuata maelekezo ya Jeshi hilo.

Kuhusu Corona IGP SIRRO ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kufuata maelekezo mbalimbali yanayoendelea kutolewa na viongozi wa kiserikali pamoja na wataalamu wa masuala ya afya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini  Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Khamis, amesema kuwa, mkoa huo unaidadi kubwa za hoteli za kitalii na kwamba ujenzi wa kituo hicho cha Polisi utasaidia zaidi katika kukabiliana na kuzuia uhalifu.

Ujenzi wa kituo hicho ambacho kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 64 zilizotolewa na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa utalii visiwani humo.


Share:

Waziri Mpina Ashtukia Upigaji Wa Bilioni 2.6 Ujenzi Maabara Ya Uvuvi

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesimamisha malipo yote kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Petra Construction co. Limited inayojenga maabara ya kisasa ya Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kituo cha Dar es Salaam hadi uhakiki wa gharama halisi za mradi huo utakapokamilika baada ya kubaini kuwepo matumizi mabaya ya fedha za umma kiasi cha shilingi bilioni 2.6

Hivyo Waziri Mpina ameunda tume ya kiuchunguzi itakayofanya kazi kwa siku saba na kuwahusisha wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kubaini ukweli wa gharama halisi za mradi huo.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) jijini Dar es Salaam, Waziri Mpina alisema amebaini mradi unaojengwa miundombinu yake ni midogo ikilinganishwa na mkataba ulioridhiwa wa sh. bilioni 2.6 na kwamba taarifa ya uhakiki ya mradi huo itawasilishwa wizarani ikiwa na mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya wizi huo wa fedha za umma.

WaziriMpina alisema thamani halisi ya mradi huo hailingani na fedha zilizotolewa na Serikali huku akitolea mfano baadhi ya miradi ya ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo vituo vya afya na hospitali za wilaya zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini.

Hata hivyo wakati wa mjadala ukiendelea wa kuhoji matumizi ya fedha hizo kwenye mradi huo, mmoja wa wakandarasi wanaojenga majengo hayo alimweleza Waziri Mpina kuwa hadi mradi utakapomika kutabaki ‘chenji’ kiasi cha shilingi milioni 500 jambo lililotilia mashaka na kuibua maswali mengi juu ya gharama halisi za mradi huo.

Kufuatia mkanganyiko huo wa maelezo ya mkandarasi na hali halisi iliyoonekana kwenye mradi huo ndipo Waziri Mpina akalazimika kutangaza uamuzi huo wa kuundwa tume hiyo ili iweze kufanya tathmini ya gharama ya mradi iliyofanywa na Mshauri mwelezi wa mradi, namna zabuni ya kumpata mkandarasi ilivyotangazwa na namna mshauri mwelekezi alivyopatikana na hali ya ujenzi unavyoendelea kwa sasa ili kujua dosari ilisababishwa na nani.

Hivyo Waziri Mpina akabainisha kuwa baada ya kazi hiyo ya uhakiki kukamilika ndani ya siku saba ukweli utajulikana na hatua zote zilizopitiwa katika mradi huo ili kubaini kama Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2004 ilikiukwa ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaohusika na ubadhirifu huo wa fedha za umma.

“Sikubaliani na hizi gharama za mradi majengo na miundombinu ni midogo ikilinganishwa na mkataba wa bilioni 2.6, BOQ ilihakikiwa na wahandisi wa wizara, washauri waelekezi walijiridhisha kwamba iko sawa na ujenzi ukaenda hadi bilioni 2.6 mtu yeyote akija anakataa” alihoji Waziri Mpina.

Hivyo Waziri Mpina ameagiza ujenzi wa mradi huo uendelee bila kusimama na ukamilike ifikapo Aprili 20 mwaka huu kama mkataba unavyoeleeza na baada ya jengo litazinduliwa ikiwa ni sehemu ya kuleta mageuzi makubwa ya sekta ya uvuvi kupitia eneo hilo muhimu la utafiti.

“Nitaleta timu ya ukaguzi itakayofanya uhakiki wa thamani ya fedha katika ujenzi wa jengo hili, kuanzia kwenye kutangaza tenda yenyewe, thamani ya mradi, kumpata mkandarasi mwenyewe, cost estimates zilizofanywa na wizara na baadae watafanya uhakiki wa kinachoendelea kujengwa hapa na kujua thamani halisi inayotakiwa na kwanini mradi huu upitishwe hadi kusainiwa”alihoji Waziri Mpina.

Menejawa Mradi wa Swiofish, Flora Luhanga alisema mradi huo wa ujenzi wa Jengo la Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ulianza Juni 10, 2019 kwa gharama ya shilingi bilioni 2, 609,491,754 unajengwa na Mkandarasi Kampuni ya Petra Construction Limited na kusimamiwa na Kampuni ya YP Architect.

Luhangaalisema mradi huo unajumuisha pia ujenzi wa uzio, ofisi ya walinzi, kuchimba kisima cha maji, ujenzi wa tenki la maji ya mvua na kujenga mnara wa maji.

Mkandarasiwa Mradi huo, Nicholaus Mlayi alisema hadi sasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 70 na tayari ameshalipwa shilingi milioni 963 na unatarajia kukamilika mwezi Aprili.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Uvuvi, Magese Bulayi alimhakikishia Waziri Mpina kuwa maagizo yote aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu hasa katika kuangalia thamani ya fedha ‘value for money’ katika mradi huo na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhusika katika mchakato huo.


Share:

Afariki kwa kupigwa na radi akiendesha pikipiki Toka Shambani

Mkazi wa kata ya Kabungu mkoani Katavi, Paulo Chundu (27) amefariki dunia kwa ya kupigwa na radi wakati akitoka shambani.

Tukio hilo lilitokea machi 29 mwaka huu majira ya saa 12: 45 jioni katika mbuga za kalilankulukulu kata ya kabungu wilayani Tanganyika mkoani katavi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoni katavi Benjamin Kuzaga amesema kijana huyo alikutwa na umauti akiwa katika mbuga hiyo akiendesha pikipiki kutokea katika Kijiji cha ikaka akielekea nyumbani kwake.

Kamanda alisema majira ya saa 12:45 alipatiwa taarifa za kijana huyo kufariki kwa kupigwa radi akiwa anatokea shambani kuelekea nyumbani

Baba mdogo wa kijana huyo, John Laurent alisema alimuagiza shambani kumpeka mtu wa kufanya kazi za shambani ikiwemo kutoa majani, hivyo wakati anarudi akafariki kwa kupigwa na radi.

Alisema tukio hilo limemuumiza na kwamba mtoto huyo aliachiwa na kaka yake baada ya kufariki na kupewa jukumu la kumlea.


Share:

Nafasi Mpya Za Kazi 100 Zilizotangazwa Wiki Hii na Makampuni Mbalimbali

Share:

Meya wa Manispaa ya Iringa Aliyeng'olewa kukabidhi ofisi leo

Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe amesema atakabidhi ofisi na gari la meya leo Jumanne asubuhi baada ya kukamilisha taratibu za kiofisi.

Kimbe ametoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari waliofika ofisini kwake kutaka kujua kwanini anaendelea na kazi licha ya kuondolewa madarakani siku chache zilizopita.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Hamid Njovu amesema kanuni zinamtaka meya huyo kuondoka ofisini ndani ya siku 30 na hivyo anatakiwa kukabidhi ofisi na gari mara moja.

Akizungumzia malalamiko ya meya kuwa hakutendewa haki katika mchakato upigaji kura, Njovu amesema uamuzi wa madiwani wa CHADEMA kutoandika chochote kwenye karatasi ya kura ndicho kilichomuangusha.

Aidha, amewaondoa hofu wananchi kuwa kazi za meya zitafanywa na Naibu Meya, Joseph Lyata, na watendaji wake wataendelea kutoa huduma kama kawaida.


Share:

Atiwa Mbaroni Kwa Kumfundisha Mbwa Kuendesha Gari

Mwanaume mmoja kutoka Lakewood Washington nchini Marekani, amekamatwa kwa kosa la kumfundisha Mbwa wake mwenye jinsia ya kike kuendesha gari kwa spidi, hali iliyopelekea kusababisha ajali.

Jamaa huyo alimuweka Mbwa wake katika siti ya dereva, ambapo amesababisha ajali ya gari mbili zilizokuwa mbele yake bahati nzuri hakukuwa na mtu aliyepata majeraha kwenye ajali hiyo.

Ripoti ya msemaji wa Jeshi la Polisi la Washington State Patrol amesema  "Gari la mtuhumiwa lilikuwa linaendeshwa kwa spidi sana tena isiyo ya kawaida, ameendesha maili 109 kwa muda wa saa moja,na alikuwa anajaribu kutukwepa lakini imeshindikana, tunashukuru baada ya ajali hiyo hakukuwa na mtu yeyote aliyepata majeruhi imekuwa kama miujiza".

Pia  ameendelea kusema tayari wanamshikilia mtuhumiwa huyo kama atataka kuachiwa kwa dhamana itabidi alipe fedha za Kitanzania Shilingi milioni 19, na mbwa wake amehifadhiwa kwenye mazingira ya wanyama wengine baada ya mmiliki wake kukamatwa.

Kwa upande wa mtuhumiwa anayemmiliki mbwa huyo amejitetea kwa kusema, alikuwa anamfundisha  mbwa wake jinsi ya  kuendesha gari.


Share:

Spika Ndugai Ataka Tusiwaige Wazungu Katika Kupambana Na Virusi Vya Corona

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa kama nchi haiwezi kuchukua tahadhari kama zilivyochukuliwa na Mataifa mengine duniani ya kupambana na Virusi vya Corona kwa kuwa watu wengi nchini maisha yao ni ya kubangaiza siku kwa siku.

Hayo ameyabainisha leo Machi 31, 2020, Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 Mkutano wa 19.

"Hatuwezi kuchukua measure za wazungu na kuzi copy na ku- paste hapa kwetu kama zilivyo, tutaua watu wetu, lazima tuangalie maisha yetu ya Kitanzania na kujaribu kuchukua hatua kufuatana na mazingira yetu" amesema Spika Ndugai.

Amesema katika maeneo yenye masoko wanatakiwa kuchukua hatua kadhaa kama kuweka maji ya kunawa na sabuni, kutokaa karibu ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

“Kuna nchi polisi wanapiga watu viboko ikilazimika huko Serikali itafanya lakini hatuishauri kwa sasa, tunajaribu kuelimisha zaidi, kutoa wito na kumuomba Mungu atuepushe na janga hili ambalo limezitikisa nchi zenye uchumi mkubwa,” amesema Ndugai 


Share:

Halima Mdee Ashauri Wabunge Wote Wapimwe Virusi Vya Corona

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Mbunge wa jimbo la Kawe jijini  Dar Es  Salaam Mhe.Halima  Mdee ameishauri  Serikali kufanya mchakato wa kupima Corona wabunge wote na watakaobainika wawekwe karantini.

Mhe.Mdee amesema hayo leo Machi 31,2020 bungeni jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa inatakiwa kila mbunge apimwe homa ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona[COVID -19]na akibainika  na maambukizi ya  virusi hivyo atengwe eneo maalum[karantini] na wale watakaobainika kutokuwa na maambukizi waendelee na mkutano ili kujadili bajeti kuu ya serikali ikiwa ni mkutano wa Mwisho kuelekea uchaguzi mkuu.

“Leo wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi wote,kwa nini tusipime wote atakayebainika ana virusi apelekwe karantini na akiwa salama abaki hapa kujadili mambo ya msingi kwa mstakabali wa taifa letu  maana ni mkutano wa mwisho”amesema.

Naye,Mbunge wa   Iringa Mjini  Mch.Peter  Msigwa ameiomba serikali kuja na mpango wa pamoja katika kujadili katika mapambano ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona[COVID-19].

Spika wa bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema katika mkutano wa bunge  la bajeti  ni vyema majadiliano ya pande zote mbili yakazingatiwa huku akitoa wito kwa wabunge kusikilizana na kuelekeza zaidi kwenye bajeti kwani ni mkutano wa Mwisho ambapo bunge litavunjwa kuelekea uchaguzi mkuu  2020.

“Kikao ni chetu kisiwe cha upande mmoja au watu wachache hata kidogo kwa hiyo natoa wito kusikilizana kwa pande zote mbili na ni vyema zaidi mbunge ukajielekeza kwenye bajeti kuliko ukasimama na yako tu ni muhimu sana kuzingatia muda”amesma.

Katika hatua nyingine Mhe.Ndugai ametoa maelekezo kwa serikali kuandaa majibu haraka iwezekanavyo juu ya Hoja Za Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali[CAG] zilizowasilishwa hivi karibuni kwa  Mhe.Rais .


Share:

WAZIRI MPINA ASHTUKIA UPIGAJI WA BILIONI 2.6 UJENZI MAABARA YA UVUVI, AAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA NDANI YA SIKU 7


 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akipata maelezo ya namna ya shughuli ya ujenzi wa mradi wa jengo la Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam  kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Petra Constuction co. Limited, Nicholaus Mlayi alipotembelea mradi huo Kunduchi Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akipata ufafanuzi kutoka kwa Mshauri Mwelekezi wa Kampuni ya Y&P Architect inayosimamia Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam, Anna Shayo alipotembelea mradi huo Kunduchi Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akiangalia ramani ya mradi wa jengo la Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam baada ya kutembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo na kuunda tume kuchunguza mradi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TAFIRI, Dk. Ismael Kimerei . Picha na Mpiga Picha Wetu.

 Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesimamisha malipo yote kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Petra Construction co. Limited inayojenga maabara ya kisasa ya Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kituo cha Dar es Salaam hadi uhakiki wa gharama halisi za mradi huo utakapokamilika baada ya kubaini kuwepo matumizi mabaya ya fedha za umma kiasi cha shilingi bilioni 2.6

Hivyo Waziri Mpina ameunda tume ya kiuchunguzi itakayofanya kazi kwa siku saba na kuwahusisha wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kubaini ukweli wa gharama halisi za mradi huo.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya  Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)  jijini Dar es Salaam, Waziri Mpina alisema amebaini mradi unaojengwa miundombinu yake ni midogo ikilinganishwa na mkataba ulioridhiwa  wa sh. bilioni 2.6 na kwamba taarifa ya uhakiki ya mradi huo itawasilishwa wizarani ikiwa na mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya wizi huo wa fedha za umma.

Waziri Mpina alisema thamani halisi ya mradi huo hailingani na fedha zilizotolewa na Serikali huku akitolea mfano baadhi ya miradi ya ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo vituo vya afya na hospitali za wilaya zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini.

Hata hivyo wakati wa mjadala ukiendelea wa kuhoji matumizi ya fedha hizo kwenye mradi huo, mmoja wa wakandarasi wanaojenga majengo hayo alimweleza Waziri Mpina kuwa hadi mradi utakapomika kutabaki ‘chenji’ kiasi cha shilingi milioni 500 jambo lililotilia mashaka na kuibua maswali mengi juu ya gharama halisi za mradi huo.

Kufuatia mkanganyiko huo wa maelezo ya mkandarasi na hali halisi iliyoonekana kwenye mradi huo ndipo Waziri Mpina akalazimika kutangaza uamuzi huo wa kuundwa tume hiyo ili iweze kufanya tathmini ya gharama ya mradi iliyofanywa na Mshauri mwelezi wa mradi, namna zabuni ya kumpata mkandarasi ilivyotangazwa na namna mshauri mwelekezi alivyopatikana na hali ya ujenzi unavyoendelea kwa sasa ili kujua dosari ilisababishwa na nani.


Hivyo Waziri Mpina akabainisha kuwa baada ya kazi hiyo ya uhakiki kukamilika ndani ya siku saba ukweli utajulikana na hatua zote zilizopitiwa katika mradi huo ili kubaini kama Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2004 ilikiukwa ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaohusika na ubadhirifu huo wa fedha za umma.
 “Sikubaliani na hizi gharama za mradi majengo na miundombinu ni midogo ikilinganishwa na mkataba wa bilioni 2.6, BOQ ilihakikiwa na wahandisi wa wizara, washauri waelekezi walijiridhisha kwamba iko sawa na ujenzi ukaenda hadi bilioni 2.6 mtu yeyote akija anakataa” alihoji Waziri Mpina

Hivyo Waziri Mpina ameagiza ujenzi wa mradi huo uendelee bila kusimama na ukamilike ifikapo Aprili 20 mwaka huu kama mkataba unavyoeleeza na baada ya jengo litazinduliwa ikiwa ni sehemu ya kuleta mageuzi makubwa ya sekta ya uvuvi kupitia eneo hilo muhimu la utafiti.

“Nitaleta timu ya ukaguzi itakayofanya uhakiki wa thamani ya fedha katika ujenzi wa jengo hili, kuanzia kwenye kutangaza tenda yenyewe, thamani ya mradi, kumpata mkandarasi mwenyewe, cost estimates zilizofanywa na wizara na baadae watafanya uhakiki wa kinachoendelea kujengwa hapa na kujua thamani halisi inayotakiwa na kwanini mradi huu upitishwe hadi kusainiwa”alihoji Waziri Mpina.

Meneja wa Mradi wa Swiofish, Flora Luhanga alisema mradi huo wa ujenzi wa Jengo la Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ulianza Juni 10, 2019 kwa gharama ya shilingi bilioni 2, 609,491,754 unajengwa na Mkandarasi Kampuni ya Petra Construction Limited na kusimamiwa na Kampuni ya YP Architect.

Luhanga alisema mradi huo unajumuisha  pia ujenzi wa uzio, ofisi ya walinzi, kuchimba kisima cha maji, ujenzi wa tenki la maji ya mvua na kujenga mnara wa maji.

Mkandarasi wa Mradi huo, Nicholaus Mlayi alisema hadi sasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 70 na tayari ameshalipwa shilingi milioni 963 na unatarajia kukamilika mwezi Aprili.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Uvuvi, Magese Bulayi alimhakikishia Waziri Mpina kuwa maagizo yote aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu hasa katika kuangalia thamani ya fedha ‘value for money’ katika mradi huo na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhusika katika mchakato huo.
Share:

Viongozi wa Dini Rukwa waazimia kupunguza muda wa ibada kujihadhari na Corona

Viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Rukwa wamekubaliana kuwa kila dhehebu kulingana na imani zao kuona namna ya kupunguza muda wa kufanya ibada katika misikiti na makanisa mbalimbali ili kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19).

Wamekubaliana hayo wakati wa kikao kifupi kilichoitishwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura katika kikao hicho kilicholenga kuwaelimisha viongozi hao juu ya Chanzo, usambaaji na namna ya kujikinga na ugonjwa huo ambao unaendelea kuisumbua dunia huku jukumu la kutoa elimu likifanywa na Mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa.

Wakati akielezea namna ya kutekeleza azma hiyo Shekhe wa mkoa wa Rukwa Rashid Akilimali alisema kuwa atazungumza na mashekhe wa wilaya na Maimamu wa miskiti ya mkoa huo kupunguza muda wa ibada ili kukwepa kuwaweka watu wengi katika eneo moja kwa muda mrefu lakini pia kuwafanya waumini hao wasikose ibada hizo.

“Niungane na Askofu wa Monravian, tupunguze nyakati za ibada zetu, na kubwa iwe ni kuongoza dua na maombi kwaajili ya nchi yetu, sisi tumelipunguza hili baada ya kutokea hili, ibada ya nusu saa tumekwenda dakika kumi na tano, dakika kumi inakuwa ni mahubiri na dakika tano ni kuiombea nchi ili Mungu atuepushe na jambo hili,” alisema

Naye Mwakilishi wa Kanisa la Anglikan Mkoani Rukwa Mchungaji Mathias Gwakila alisema kuwa atajitahidi kufikisha ujumbe na elimu aliyoipata kutokana na namna alivyojifunza na kuwasisitiza waumini hao kuendelea kufanya maombi ili kuepukana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa ugonjwa huo ni pepo na hivyo hatunabudi kulikemea na kisha kushauri juu ya kufupisha ibada.

“Hicho ni kitu muhimu mno, ibada ziwe fupi zisiwe ndefu, kwahiyo kwa ushauri wangu kupitia madhehebu mengine yote, viongozi wote wa madhehebu wajitahidi kufupiza, kwa mfano kanisa la Anglican ibada zetu ni masaa mawili, sasa tufupishe, ibada ichukue saa moja katika vipengele vyovyote vile ambavyo wewe utaviona upunguze kipi na kipi ilimradi ibada iwe fupi watu watoke mapema,” Alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Ziwa Tanganyika Mchungaji Haruni Kikiwa alisema kuwa kupitia kikao hicho wamepata elimu ya kutosha ya namna ya kuwaelekeza wananchi ambao ni waumini wao juu ya namna ya kupambana na janga la kirusi cha Corona na kusisitiza kuwa atayafikisha kwa askofu ili kusambazwa kwa makanisa.

“Tunachukua hatua za kunawa kabla ya ibada na baada ya ibada, lakini pia hatua za kupunguza muda wa ibada ili kupunguza muda wa waumini kukaa pamoja katika msongamano lakini pia hatua za kupunguza misongamano kwa makanisa makubwa kwa maana wanaweza wakafanyia hata nje ili kupunguza msongamano watu wakae mbalimbali, haya yote nitayafikisha,” alisema.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu wakati akieleza namna ya kujikinga na ugonjwa huo alitoa msisitizo kwa viongozi hao kutumia maji tiririka pamoja na sabuni ya maji wakati wa kunawa huku akieleza madhara ya kutumia sabuni ya unga na ya kipande kuwa na tabia ya kushikwa na kila mtumiaji.

“Sabuni ya unga ambayo imechanganywa na maji ikawekwa kwenye chombo maalum kama chupa, kwahiyo mtu anaweza kuitumia hii, tunaepuka kuweka sabuni ya unga kama ilivyo kwamba mtu mmoja achukue na mwingine aje achukue na mwingine achukue, tunaepuka kuweka sabuni ya kipande kwasababu lazima mtu aje aishike akishajipaka arudishe mwengine aje aishike, kwahiyo tunasema ni sabuni ya maji na kama ni sabuni ya unga basi ichanganywe na maji,” Alisisitiza.

Wakati akifunga kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura aliwaomba viongozi hao kuzingatia makubaliano ya kikao hicho na kuongeza kuwa anaamini viongozi wa dini wasingependa waumini wao wateketee na kisha kusisitiza juu ya kupunguza muda wa ibada pamoja na mikusanyiko hasa kwa madhehebu ambayo yana waumini wengi.

“Kuna makanisa ambayo ni madogo sana au misikiti midogo watu wanajua lakini kama mikiti naona wameshajipanga wao wanasali muda mfupi lakini kuna makanisa mengine tunatumia masaa mengi, mkishaingia saa 4 mpaka saa 9 kwahiyo huo ni muda mrefu sana mnaweza mkajichanganya sana, hivyo ninaona kwamba hii kumbunguza mud ani muhimu zaidi, vile vipindi vyetu tuvipunguze zaidi tutoe elimu hasa ya kuwa na imani,” Alisistiza
Aidha, alibainisha kuwa kama serikali hawataweza kuwapangia muda wa kufanya inbada hizo huku akiweka msisitizo kuwa imani zinatofautiana na kufafanua kuwa waumini hao wanaweza hata kulala ndani ya makanisa yao kwa kuomba lakini msisitizo ni kuwa wachache ili kuepusha msongamano.


Share:

Elimu juu ya Ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona itolewe katika Maeneo ya Vijijini.

SALVATORY NTANDU
Wakazi wa mkoa wa Shinyanga wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya wananchi wanaokaidi maagizo ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Wazee na Watoto juu ya kujikinga na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya  Corona kwa kutonawa mikono kwa maji yaliyowekewa dawa za kuzuia maabukizi ya ugonjwa huo.

Hayo yalibainishwa Machi 28 na  Kisena Mihambo Mkazi wa Igwamanoni katika Halmashauri ya Ushetu mkoani humo baada ya kutembelewa na shirika lisilo la kiserikali la (REDCROSS) lililokuwa linatoa elimu kwa njia ya vipeperurishi na mabango kuhusina na kuchukua tahadhari juu ugonjwa unaosababishwa na virusi vya  Corona.

Alisema baadhi yao wamekuwa wakikaidi kutii maagizo ya serikali kwa kutonawa mikono hali ambayo inaweza kusababisha wakapatwa na maambukizi ya ugonjwa huo pindi utakapojitokesha na kuiomba serikali kupitia maafisa afya wa ngazi ya kata kuwachukulia hatua kali ili waweze kutii maagizo hayo.

“Katika Maeneo yote ya kutolea huduma za kijamii Serikali imeweka ndoo zenye Maji yaliyokwisha wekewa dawa za kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa Corona lakini baadhi yetu tumekuwa wagumu kunawa mikono na badala yake tunaendelea kushikana mikono pindi tunaposalimiana”,alisema Mihambo.

Zubeda Ramadhani ni Mkazi wa Ntobo katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama alisema endapo wananchi wakihimizwa kwa kupewa elimu sahihi juu ya ugonjwa wa Corona na serikali hususani maeneo ya vijijini itawezakuzuia mlipuko wa virusi vya homa ya Mapafu (Corona).

“Tunaiomba serikali iwashirikishe viongozi wetu wa ngazi za mitaa,vijiji na kata ili kusaidia kuwafikia wakazi wengi hususani wakulima ambao kwa sasa wanaendelea na shughuli za uvunaji wa mazao mashambani ili kuwakinga na maambukizi ya Ugonjwa huo”alisema Ramadhani.

Kwa upande wake Mratibu wa RED CROSS Mkoa wa Shinyanga Samwel Katamba alisema Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la kuwahudumia  watoto Duniani (UNCEF) limewapa jukumu la kusambaza vipeperushi na Mabango nchi nzima kuhusiana na kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Corona.

“Tumeweza kuzifikia Halmashauri Sita  za mkoa wa Shinyanga kwa kuweka Mabango sambamba na kugawa vipeperushi vya ujumbe kuhusiana na ugonjwa huu wa Corona ikiwa ni pamoja na kutumia magari ya Matangazo lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu hii”alisema Katamba.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Ushetu Dk Nichodemas Senguo alisema mpaka sasa wameweza kutembelea kata 20 kwa kuwapatia elimu sahihi ya kujikinga na ugonjwa wa Corona huku mwitikio wa wananchi ukiwa ni mkubwa.

“Niwatake wananchi wa Ushetu waendelee kuzingatia maelekezo ya Wizara ya afya ya kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kutumia vitakasa mikono (Sanitaizer) sambamba na kuepuka kupeana mikono,pamoja na kujizuia kukaa kwenye mikusanyiko isiyokuwa na ulazima”alisema Dk Senguo.

Mwisho


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger