Na Sheila Ahmadi, Dar es Salaam
Kongamano la Uchumi wa Bluu linatarajiwa kujadili mikakati ya kuhakikisha Tanzania inazalisha wataalamu wa kutosha katika sekta ya bahari, sambamba na kuangalia fursa za kiuchumi zinazotokana na matumizi endelevu ya rasilimali za bahari.
Akizungumza na Wanahabari jijini Dar esaalam Mkuu wa chuo cha bahari Dar esalaam (DMI) Profesa Tumaini Gurumo amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta mbalimbali zinazohusiana na uchumi wa bluu, hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha nchi inakuwa na wataalamu wenye uwezo wa kukidhi mahitaji yanayotokana na uwekezaji huo.
matumizi ya bahari yanaendelea kuongezeka, hali inayoongeza mahitaji ya wataalamu katika maeneo mbalimbali, ikiwemo ujenzi na uendeshaji wa meli, usafirishaji wa mizigo, shughuli za bandari, uvuvi na sheria za baharini.
Kupitia Chuo cha Bahari Dar es Salaam kimeendelea kuboresha programu zake za elimu na mafunzo ili kukidhi mahitaji ya soko, ikiwa ni pamoja na kuanzisha kozi zinazolenga maeneo mapya yanayohusiana na uchumi wa bluu.
“Tunapoangalia uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta mbalimbali, tunahitaji pia wataalamu wa kutosha watakaoweza kusimamia na kuendeleza uwekezaji huo,” amesema Profesa gurumo"
Aidha, amesema miongoni mwa maeneo yanayofanyiwa kazi ni usafirishaji na usimamizi wa mizigo bandarini, pamoja na biashara ya kimataifa ya baharini, ambayo yanahitaji wataalamu wenye ujuzi maalumu.
kuna umuhimu wa kuwa na wataalamu katika eneo la sheria za baharini, hususani kutokana na kuongezeka kwa shughuli za uvuvi, usafirishaji na matumizi mengine ya rasilimali za bahari.
Vilevile kongamano hilo linatarajiwa kujadili namna ya kuhakikisha rasilimali za bahari zinalindwa na kutumika kwa njia endelevu ili Tanzania iweze kunufaika na uchumi wa bluu kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine profesa gurumo ameongeza kuwa bila kuwepo kwa mikakati madhubuti ya kutunza rasilimali za bahari, nchi inaweza kushindwa kupata manufaa ya muda mrefu kutokana na uchumi huo.
Kongamano hilo litakutanisha washiriki kutoka Tanzania na nje ya nchi, wakiwemo wataalamu, wanazuoni, viongozi wa taasisi za umma na binafsi, pamoja na vijana, kwa lengo la kujadili fursa na changamoto katika maendeleo ya uchumi wa bluu.
Washiriki hao wanatarajiwa kutoka katika nchi mbalimbali, ikiwemo Kenya, Comoro, Seychelles na mataifa mengine, huku wakijadili namna ya kushirikiana katika kutumia fursa zinazotokana na uchumi wa bluu kwa maendeleo ya nchi na ukanda kwa ujumla.




0 comments:
Post a Comment