Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb), ametembelea kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Viwango House eneo la Mateves, Mkoani Arusha.
Ziara hiyo imelenga kujionea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hizo, pamoja na kufahamu hatua zinazofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo.
Ujenzi wa Ofisi za TBS Mateves unatarajiwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za viwango na uhakiki wa ubora kwa wananchi, wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa katika Mkoa wa Arusha na maeneo jirani.
Aidha, uwepo wa ofisi katika eneo hilo utasaidia kusogeza huduma za TBS karibu zaidi na wadau, kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma na kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Shirika katika kuhakikisha bidhaa na huduma zinazotumika nchini zinakidhi matakwa ya viwango.



0 comments:
Post a Comment