Tuesday, 14 January 2020

Katibu Mkuu CCM: Uchaguzi sio Namba, Ni Maamuzi ya Umma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewakumbusha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini maana halisi ya uchaguzi ni maamuzi ya Umma si kama ambavyo wamekuwa wakieleza kwa kupotosha kuwa, uchaguzi ni namba.

Ameyasema hayo tarehe 13 Januari, 2020 alipokuwa akihutubia viongozi wa mashina,matawi, Kata na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya wilaya za Handeni na Kilindi Mkoani Tanga.

“Nimewasikia baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, wanasema uchaguzi ni namba. Uchaguzi sio namba, uchaguzi ni uamuzi wa umma, namba ni kitu cha baadae, waambieni wanaosema uchaguzi ni namba waache kugeuza uchaguzi kama mchezo wa kamari au bingo, uchaguzi ni uamuzi wa wananchi juu ya mustakabali wao.”

Amesisitiza zaidi kuwa, wananchi hufanya hivyo kabla ya siku ya kupiga kura, siku ya kupiga kura ndio siku ya kudhihirisha uamuzi wao, lakini uamuzi wao huanza kufanyika tangu uchaguzi ulipoisha.

Hivyo Katibu Mkuu ameeeleza kuwa, CCM inauona uchaguzi kama zoezi muhimu sana linalohusu uamuzi wa wananchi juu ya mustakabali wa taifa lao, uamuzi wa wananchi juu ya wananchi wenzao wanaofaa kuwaongoza kwa maendeleo yao, uamuzi wa wananchi juu ya chama chenye sifa, kinachoaminika, kinachoweza, chenye rekodi ya kuongoza nchi na sio vinginevyo.

Wakati huo huo Dkt. Bashiru amewahakikishia wananchi msimamo wa CCM kuendelea kuisimamia serikali kutekeleza kila kilichoahidiwa na kisichotekelezwa huelezwa ni kwa nini hakijatekelezwa, hivyo mwaka huu ni mwaka wa wanaCCM wote kuueleza umma yote yalioahidiwa yametekelezwa kwa kiasi gani, yepi yametekelezwa vizuri, yepi yametekelezwa kwa wastani na yepi ambayo Chama kitaongeza nguvu zaidi.

Aidha Katibu Mkuu ametumia mkutano huo wa ndani kuwataka wenyeviti wa Vijiji na Mitaa, watendaji wa mitaa na Halmashauri, kuwa wabunifu na kung’amua fursa za maendeleo, na kwa wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia ubunifu kwa watendaji ili kuwawezesha wananchi kupiga hatua kwa haraka.

Viongozi mbalimbali wakizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu, wameonesha kuridhishwa na kasi kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM licha ya changamoto mbalimbali ambazo wanaendelea kuzishughulikia na kuzitafutia majawabu ikiwa ni pamoja na kasi ya usambazaji wa umeme vijijini.

Mkutano huo umehudhuriwa na wanachama, viongozi wa Chama na Serikali wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndg. Mohamed Salim Ratco (MNEC), Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ndg. Martin Shigela, wajumbe wengine wa Halmashauri Kuu Bi. Mwantumu Zodo, na Bi. Catherine Kitandura na wabunge wa Mkoa wa Tanga.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya siku nne, ambapo ziara hiyo imelenga kuimarisha na kuhuisha uhai wa Chama katika ngazi za Mashina na Matawi.


Share:

Rais Magufuli Awaapisha Mabalozi Wanne

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo amewaapisha Mabalozi Wateule wanne watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi za nje.

Walioapishwa ni;
1. Meja Jenerali (MST) Gaudence Milanzi kuwa Balozi wa Africa Kusini.

2.Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Balozi wa Namibia.

3.Prof. Emmanuel David Mwaluko Mbennah kuwa Balozi wa Zimbabwe.

4.Dkt. Benson Alfred Bana kuwa Balozi wa Nigeria.


Share:

Mo Dwji Aibuka na Jipya Baada ya Kutangaza Kujiuzulu Simba SC

Baada ya jana kupitia ukurasa wake wa twitter kuandika kwamba anaondoka kwenye nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba kutokana na timu hiyo kupoteza mchezo wa fainali kwa kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar, leo Mo amekuja na maamuzi mapya kwamba kilichotokea kwenye Account yake jana ilikuwa ni bahati mbaya. 

 “Kilichotokea kwenye akaunti zangu jana kilikuwa ni bahati mbaya, tuko pamoja, tunarudi kwenye ligi tukiwa na nguvu , tunajipanga kwa ajili ya ligi, nawapongeza Mtibwa kwa kuchukua kombe, mimi ni Simba damudamu, nitabaki kuwa Simba”.Ameandika Mo Dewj 



Share:

TAKUKURU SHINYANGA YAOKOA MIL. 30 KUTOKA KWA VIONGOZI WA AMCOS WALIOFANYA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA WAKULIMA WA PAMBA


Na Josephine Charles - Malunde 1 blog
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga imeokoa kiasi cha Shilingi 30,503,650 kutoka kwa Viongozi wa Vyama vya ushirika (AMCOS) waliofanya ubadhirifu wa Fedha za Wakulima wa Pamba msimu wa Mwaka 2018/2019.



Hayo yameelezwa leo Jumanne Januari 14,2020 na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga ,Hussein Mussa wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za Taasisi hiyo kwa lengo la kutoa taarifa ya kazi zilizofanywa na TAKUKURU Shinyanga katika kipindi cha Robo ya Pili ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 yaani kuanzia Oktoba hadi Desemba 2019.

Mussa amesema pamoja na kazi nyingine za kawaida za TAKUKURU ikiwemo Uchunguzi, Elimu kwa umma,kuzuia Rushwa,ufuatiliaji wa Miradi na kuendesha kesi zilizofunguliwa mahakamani kwa Makosa mbalimbali  ya Rushwa,TAKUKURU Shinyanga ilifuatilia kwa kina madeni ya Wakulima wa Pamba wanaodai fedha zao kutokana na pamba waliyouza kupitia AMCOS mbalimbali katika Mkoa wa Shinyanga. 

Ameeleza kuwa Baada ya uchunguzi TAKUKURU  ilibaini kuwa AMCOS saba kati ya zilizofuatiliwa ambazo ni Lugana, Mwakipoya, Ng'washinong'hela,Nyenze na Kalitu vya wilaya ya Kishapu,Kweli Balimi na Ibadakuli za wilaya ya Shinyanga ndizo zinadaiwa fedha na wakulima wa pamba kiasi cha shilingi 109,497,130/= fedha ambazo walizifanyia ubadhirifu kwa kutumia Fedha nyingi za wakulima zilizotolewa mwanzo na makampuni ya ununuzi wa Pamba kugharamia shughuli za uendeshaji wa chama tofauti na fedha za ushuru wanazodai kutoka kwa makampuni,hivyo kupelekea kuwa na madeni wanayodaiwa na wakulima wa pamba.

Amesema Takukuru ilibaini kuwa mpaka kufikia mwezi Desemba 2019 makampuni yaliyonunua pamba mkoani Shinyanga yalikuwa hayadaiwi Fedha za Wakulima bali walikuwa yanadaiwa ushuru wa AMCOS jumla ya Shilingi 890,105,580/= 

Ameeleza kuwa baada ya kubaini ubadhirifu huo Takukuru iliweza kuwakamata baadhi ya Viongozi wa AMCOS waliofanya ubadhirifu wa fedha za Wakulima na waliweza kurejesha kiasi cha Shilingi 30,503,650/= fedha ambazo zinategemewa kugaiwa kwa Wakulima hivi Karibuni.

Mussa amesema kwa viongozi wa AMCOS  ya Kweli Balimi ya Wilaya ya Shinyanga ambao walirejesha Fedha walizokuwa wanadaiwa kiasi cha Shilingi 6,362,400/= walizokuwa wamezifanyia ubadhirifu na tayari Fedha hizo zimekwisha gawiwa kwa Wakulima,hivyo Wakulima hawana madai wanayodai katika AMCOS hiyo.

Amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa  TAKUKURU kama ambavyo wamekuwa wakifanya ili Kuhakikisha wanaondoa Kero ya Rushwa katika mkoa wa Shinyanga. 
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga , Hussein Mussa wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za Taasisi hiyo. Picha zote na Josephine Charles - Malunde 1 blog
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Hussein Mussa wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za Taasisi hiyo.

 Shilingi 30,503,650 zilizookolewa kutoka kwa Viongozi wa Vyama vya ushirika (AMCOS) waliofanya ubadhirifu wa Fedha za Wakulima wa Pamba msimu wa Mwaka 2018/2019.


Share:

SHEIKH AFUKUZWA KAZI KWA KUMUOA MWANAUME MWENZAKE AKIDHANI NI MWANAMKE

Share:

KILIMO CHA KOROSHO SINGIDA,KUITANGAZA TANZANIA KIDUNIA –DKT NCHIMBI.





Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiangalia  mkorosho uliopandwa katika shamba la pamoja la koshoro la Masigati  Wilayani Manyoni alipotembelea shamba hilo hivi karibuni

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye koti jeusi)  akitoa maelezo ya shamba la pamoja la  Korosho  la Masigati Manyoni  kwa kundi la wanachuo na wakufunzi  wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa waliotembelea shamba hilo. Mwenye shati la kitenge ni Luteni Kanali RG Magemeson, Mshauri wa Jeshi la Akiba  Mkoa wa Singida, anayefuata ni Mkufunzi, Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe. Kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Brigadia Generali Liv Jian Mkufunzi wa chuo hicho



Picha ya pamoja  baina ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mwenye kilemba na kikosi cha wakufunzi na wanachuo cha Ulinzi cha Taifa walipotembelea shamba  la kilimo cha pamoja cha korosho wilayani Manyoni hivi karibuni

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye koti jeusi)  akiwa pamoja  kundi la wanachuo na wakufunzi  wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa  wakikagua shamba la kilimo cha pamoja la  Korosho eneo  la Masigati Manyoni

Mshauri wa Jeshi la Akiba  Mkoa wa Singida,Luteni Kanali RG Magemeson (mwenye shati la kitenge), akipokea  zawadi ya  kiwekeo cha funguo kutoka kwa Mkuu wa msafara na  Mkufunzi wa chuo hicho, Mhe. Balozi Peter Kallaghe baada ya kufanya kazi nzuri ya kuratibu ziara hiyo wakiwa kwenye Mkoa wa Singida.
 
Na John Mapepele

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amesema  uanzishaji wa mpango wa kilimo cha pamoja (block farming) kwenye zaidi ya ekari 12000 wa zao la korosho eneo la Masigati mkoani Singida umefanya eneo hili kuwa miongoni mwa kivutio kikubwa cha utalii wa kilimo duniani utakaochangia katika uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.


Akizungumza wakati wa kuwaaga wanachuo wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa waliotembelea mradi wa shamba la kilimo cha pamoja cha Korosho Masigati wilayani Manyoni leo, Dkt Nchimbi alisema Mkoa wa Singida unaendelea kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii kupitia mkakati wa kuwainua wananchi wote baada ya kubuni kilimo cha pamoja ambapo alisema lengo ni kila mwananchi apate angalau ekari kuanzia tano.


“Katika kipindi hiki cha takribani miaka miwili tunashukuru Mungu kuwa tumeleta mabadiliko makubwa ya kitabia na kifikra kwa wananchi wetu kupitia mradi huu ambao wengi wao wameendelea kujiunga siku hadi siku na kufurahia utajiri ardhi yao” alisitiza Dkt Nchimbi


Alisema licha ya kupata ekari 12000 katika wilaya ya manyoni  pia wamepata ekari 500 katika eneo la Itigi  na Ekari 500  kwenye eneo la Ikungi ambazo zote zinaendelezwa kwa mtindo wa kilimo cha pamoja.

Dkt. Nchimbi aliongeza kuwa mpango wa baadaye ni kuongeza eneo na kuanzisha ushirika wa pamoja wa wakulima wa Korosho ambapo  pia wametenga maeneo kwa ajili ya kujenga viwanda na maghara kwa ajili ya kuchakata na kuhifadhia Korosho.

“Mpango wetu wa baadaye kwenye eneo hili ni kuweka miundombinu ya kisasa na viwanda vikubwa.Tunataka minada yote ifanyike hapahapa”alisisitiza Mkuu wa Mkoa

Aidha alitoa rai kwa wananchi popote nchini kuja kulima zao hilo kwenye  eneo hilo huku akionya kuwa Serikali itamtoa mtu yoyote atakayebainika kutumia eneo hilo kwa lengo lisilokusudiwa.

“Tunaelewa wanakuja ili kupata hati ya eneo hili ili wafanye matumizi mengine.Nawatangazia kuwa wasijidanganye kwa kuwa  hati inayotolewa hapa  ni maalum kwa ajili ya kulima  zao la Korosho na siyo vinginevyo hivyo tupo makini sana katika hilo” alisema


Alisema kutokana na tafiti zilizofanywa na Taasisi ya Kilimo ya Naliandele, imeonyesha kuwa  eneo hilo ni bora ukilinganisha na maeneo mengi hapa nchini na kwa kuwa  korosho za eneo hili zinawahi zaidi kukua na pia zinazaa mara mbili kwa mwaka kutokana na eneo hili kuwa na misimu miwili ya kiangaza hivyo kutoa maua mara mbili kwa mwaka mmoja.


Aidha alisema  kutokana na eneo hili kuwa na umuhimu wa pekee katika kilimo cha Korosho tayari taasisi mbalimbali za kilimo za Serikali zimeanzisha  ofisi za kudumu ili kuwasaidia wananchi kwenye kilimo cha zao hilo. Alizitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni Taasisi ya Utafiti wa kilimo Naliandele na Bodi ya Korosho nchini.


Dkt. Nchimbi alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa  kutoa pikipiki nne kwa ajili ya kusadia kazi hiyo na kwamba aliahidi jumla ya pikipiki kumi.


“Kipekee kabisa nachukua nafasi hii kumpongeza Rais wetu kwa  kweli yupo pamoja na sisi katika  mpango huu ametutia nguvu sana, tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu  aishi miaka  mingi” alisema


Alisema mapindunzi ya kijani ya kilimo cha Korosho yameifanya Singida  kuwa tofauti na ya awali iliyosadikiwa kuwa Singida ya njaa,masikini, kame na isiyokuwa na fursa ambapo hata watumishi wa umma walikuwa anakataa kuhamia.


Alisema  baada  ya kufanikiwa katika mradi huu mkoa unatarajia kuanzisha  mradi mwingine kama huo kwa mazao ya kudumu baada ya kufanya tafiti za kutosha ili kuinua uchumi wa wananchi wa kawaida wa mkoa huo.


Alisema mkakati wa sasa ni kuufanya Singida kuwa mkoa wenye uchumi mkubwa kwa kuwa mbali ya kuwa na rutuba na hali ya hewa nzuri pia una utajiri wa raslimali za kutosha ikiwa ni pamoja na vivutio mbalimbali  vya kihistoria kama kijiji cha kilimatinde ambacho kinahistoria ya kuwa kituo cha njia kuu ya watumwa   toka miaka ya 1885 na ngome ya utawala wa Mjerumani na Mwingireza, mabwawa makubwa ya samaki na kituo kikubwa  duniani cha Hija kilichopo Sukamahela.


Kiongozi wa msafara wa  Chuo Ulinzi cha Taifa, Mhe. Balozi Peter Kallaghe alipongeza juhudi na mapinduzi makubwa yanayofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Singida ambapo alisema  mageuzi haya yanapaswa kuigwa na  mikoa yote hapa nchini ili kuunga mkono jitihada za kuifanya Tanzania kuwa Serikali ya viwanda ifikapo 2025 yanayoongozwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli.


Yajayo yanafurahisha! Tusubiri  tuone. Mungu ibariki Singida, Mungu ibariki Tanzania

                                                                                                                                
Share:

Wimbo Mpya : JUMA MARCO - UMALAYA

Huu hapa wimbo mpya wa Msanii wa Nyimbo za asili Juma Marco unaitwa Umalaya..Usikilize hapa chini mtu wangu

Share:

MTIBWA SUGAR MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI 2020....WAICHAPA SIMBA SC 1-0 ZANZIBAR


Na Saada Akida, ZANZIBAR

MTIBWA Sugar ndio mabingwa wa Kombe la Mapinduzi mwaka 2020, baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa wa Tanzania, Simba SC usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Awadh Salum Juma, mchezaji wa zamani wa timu ya vijana ya Yanga na African Lyon kipindi cha kwanza.

Na hilo linakuwa taji la pili la Kombe la Mapinduzi kwa Mtibwa Sugar baada ya awali kulibeba mwaka 2010 wakiifunga Ocean View katika fainali, lakini pia Wakata Miwa hao wa Manungu wamelipa kisasi cha kufungwa na Simba kwenye fainali mwaka 2015.

Awadh, kijana mwenye nguvu na kasi, alifunga bao hilo dakika ya 38 akimalizia pasi ya kurudishiwa na Jaffar Kibaya baada ya yeye mwenyewe kutoka na mpira nyuma pembeni kushoto akiwapita wachezaji wa Simba. 

Bao hilo halikuonekana kuwavuruga kabisa Simba SC walio chini ya kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck na wakaendelea kucheza kwa kushambulia na kwa kujiamini.

Lakini kipindi cha pili Vandenbroeck aliyejiunga na Simba Desemba tu baada ya kufukuzwa kwa Mbelgiji mwenzake, Patrick Aussems alikianza na mabadiliko ya wachezaji wanne, akiwatoa mabeki Haruna Shamte, Mbrazil Toirone Santos na viungo Said Ndemla na Rashid Juma na kuwaigingiza Nahodha na mshambuliaji John Bocco, beki Muivory Coast Pascal Wawa na viungo Ibrahim Ajibu na Mkenya Francis Kahata.

Hata hivyo, mabadliko hayo hayakuweza kupindua matokeo na zaidi mlinda mlango Beno Kakolanya aliendelea kuwa mtu muhimu kwa kuokoa hatari kadhaa langoni mwake. 

Hii ni mara ya tatu ndani ya miaka minne, Simba SC wanangia fainali ya Kombe la Mapinduzi lakini wanafungwa baada ya 2017 na 2019 kuchapwa na Azam FC mar azote mbili.

Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa: Shaaban Kado, Dickson Job, Jaffary Kibaya, Cassian Ponera, Salum Kihimbwa/Omary Sultan dk68, Ally Makarani, Awadhi Juma, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Abdulhalim Humud, Onesmo Mayaya/Haroun Chanongo dk61 na Kibwana Shomari.

Simba SC: Benno Kakolanya, Haruna Shamte/John Bocco dk75, Gardiel Michael, Toirone Santos/Pascal Wawa dk46, Said Ndemla/Ibrahim Ajibu dk59, Rashid Juma/Francis Kahata dk46, Clatous Chama, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Miraji Athuman/Hassan Dilunga dk37 na Meddie Kagere.

Chanzo- Binzubeiry blog
Share:

Aliyekuwa Kiongozi Wa Brigedi Ya Faru Apongeza Ushirikiano Uliopo Kati Ya Jeshi Na Ofisi Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Tabora

NA TIGANYA VINCENT
Aliyekuwa Kiongozi   wa Brigedi ya Faru amepongeza ushirikiano uliopo baina ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Jeshi la Wananchi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi.


Kauli hiyo imetolewa  na aliyekuwa kiongozi katika Brigedi ya Faru ,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti wakati wa mazungumzo na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alipofika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa tabora kwa ajili ya kuaga mara baada ya kuhama Makao Makuu ya Jeshi mjini Dodoma.

Alisema katika kipindi alipokuwa akisimamia Brigedi ya Faru, Jeshi la Wananchi limeweza kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali ikiwemo utunzaji wa mazingira na upandaji miti katika kutekeleza agizo la Makamu wa Rais.

Brigedia Jenerali Sibuti aliongeza kuwa ana matumaini Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi yake ya kuongoza Brigedi ya Faru ataendelea ushirikiano uliopo na kuchochea maendeleo ya eneo hilo.

Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alimshukuru Brigedia Jenerali Sibuti kwa mchango wake mkubwa wa kukuza ushirikiano kati ya Jeshi la Wananchi na Mkoa wa Tabora na kusaidia katika upandaji miti kwa kutumia wanajeshi.

Naye Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru alisema Jeshi la Wananchi litaendelea kuunga mkono juhudi za uongozi wa Ofisi ya Mkoa wa Tabora ya kuugeuza Mkoa huo kuwa wa kijani kwa ajili ya kukabiliana na uharibifu wa mistu.

Alisema ataendelea kutoa Vijana wa Jeshi la Wananchi ili waweze kushiriki katika upandaji wa miti na shughuli nyingine za maendeleo kwa ustawi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda (kushoto) ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru akifafanua jambo wakati alipomsindikiza  aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru, Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti (katikati) katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuaga mara baada ya kuhamia Makao Makuu ya Jeshi mjini Dodoma. Wengine ni Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (kulia)  na pembeni ni Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Tabora Kanali Mussa Luka Simengwa.

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (aliyesimama) akitoa maelezo mafupi mara baada ya kukutana na aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru ,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti (katikati) ambaye alifika katika  kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuaga mara baada ya kuhamishiwa Makao Makuu ya Jeshi mjini Dodoma. Wengine ni Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda (kushoto) ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru na aliyepembeni ni Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Tabora Kanali Mussa Luka Simengwa. 

Aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru na kuhamia Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi ,Bregedia Jenerali Antony Chacha Sibuti (wa pili kutoka kushoto) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (wa tatu kutoka kushoto) , Brigedia Jenerali Jacob John Mkunda ambaye anachukua nafasi ya kuongoza Brigedi ya Faru(katikati) wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Maafisa wa Jeshi la Wananchi  mara baada ya kumalizika mazungumzo ya aliyekuwa kiongozi wa Brigedi ya Faru Bregedia Jenerali  Sibuti kuagana na uongozi wa Mkoa wa Tabora .


Share:

MO Dewji ajiuzulu Simba SC,Ni baada ya Kupoteza Fainali ya Jana

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba SC MO Dewji amefikia maamuzi mazito ya kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti na kubakia kama muwekezaji wa Simba, 

MO amefikia hatua hiyo kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakitolewa na UD Songo ya Msumbiji hatua ya awali, sare ya 2-2 dhidi ya Yanga inayoonekana kupitia kipindi kigumu kiuchumi na kupoteza fainali ya jana ya Mapinduzi Cup 1-0 dhidi ya Mtibwa.

“Ni aibu Simba kutoshinda, baada ya kulipa mishahara inayokaribia Bilioni 4 kwa mwaka, najiuzulu kama mwenyekiti wa bodi na kubakia muwekezaji, Simba Nguvu Moja, nitatia nguvu kwenye kuendeleza miundombinu na soka la vijana” Ameandika MODewj




Share:

MWANAMKE ANASWA AMEBEBA VIPODOZI HARAMU AKIDAI NI MTOTO


Mwanamke akiwa amebeba vipodozi bandia vyenye muonekano wa mtoto mdogo.

Maafisa wa polisi nchini Uganda, wamemkamata mwanamke mmoja aliyekuwa akivuka mpaka wa nchi hiyo kutokea nchini Congo, akiwa amebeba vipodozi haramu alivyokuwa amevifungasha na kuvivalisha kwenye nguo ya mtoto, ambayo ilileta uhalisia wa mtoto mdogo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Bidhaa nchini Uganda, Dickson Kateshumbwa, amesema kuwa bidhaa hizo zilikuwa zimepakiwa vyema katika nguo za mtoto ili kuonekana kwamba ni mtoto, huku Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA), ikisema kuwa tayari imekwishaitambua mbinu hiyo, hivyo si rahisi kwa msafirishaji yeyote wa vipodozi bandia kupita salama nchini humo. 

"Mtoto ghushi alipandishwa gari la kutoka Congo katika kituo cha mpaka wa Mpondwe, na baadae iligundulika mtoto huyo kuwa ni mwanasesere aliyekuwa amesakamiwa vipodozi haramu, baadhi ya walanguzi huendelea kushangaza" alisema Kateshumbwa. 

Serikali ya Uganda ilipiga marufuku vipodozi hivyo tangu mwaka 2016, kwa sababu ya kuwa na viwango vya madini ya zebaki na hydroquinone, ambapo utafiti kadhaa umefichua kuwa vina madhara kwa afya, ambapo pia Idara ya Ubora wa Bidhaa (KEBS), iliorodhesha baadhi ya mafuta na bidhaa za urembo ambazo zilikosa, kutimiza masharti ya ubora mnamo Novemba 2019.
Share:

KESI YA ERICK KABENDERA YAPIGWA KALENDA HADI JANUARY 27


Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick Kabendera, umeielezea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi katika kesi hiyo umebakia katika maeneo machache kukamilika. 


Wakili wa Serikali, Ester Martin ameileleza Mahakamani hiyo jana  Jumatatu, Januari 13, 2020 wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Martin alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Janeth Mtega upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kwamba wanamalizia vitu vichache ili kukamilisha upelelezi wa shauri hilo.

Hakimu Mtega baada ya kueleza hayo, aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 27, 2020 itakapotajwa.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la kutakatisha fedha kiasi cha Sh173 milioni, katika Mahakama ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.



Share:

MBUNGE WA ROMBO, JOSEPH SELASINI AJIUZULU NAFASI YA MNADHIMU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI

Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini  amejiuzulu wadhifa wa Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni  kutokana na kutotambulishwa rasmi kwa uongozi wa Bunge tangu ateuliwa miaka miwili iliyopita.



Selasini aliteuliwa kukaimu wadhifa huo miaka miwili iliyopita, kufuatia aliyekuwa akishikilia wadhifa huo, Tundu Lissu kuwa katika matibabu nje ya nchi baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 nyumbani kwake Jijini Dodoma.




Share:

Maalim Seif Sharif Hamad Aitwa Polisi

Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba visiwani Zanzibar limemtaka Mshauri mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad kufika kituo cha Polisi Wilaya ya Wete leo Jumanne Januri 14, 2020 saa tatu asubuhi.

Mbali na Maalim Seif, mwingine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa chama hicho, Salim Bimani.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne January 14





















Share:

Monday, 13 January 2020

Basi la Bright Line Lapata ajali Shinyanga na kusababisha vifo na Majeruhi

SALVATORY NTANDU
Watu wawili ambao ni abiria wanadhaniwa kupoteza Maisha huku wengine zaidi ya 50 wakijeruhiwa katika ajali ya basi kampuni ya  Bright Line lenye namba za  za usajili T 437 DFJ lililokuwa kikitokea jijini mwanza kwenda Jijini Dodoma.


Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa tatu asubuhi Katika eneo la Isela kata ya Samuye Manispaa ya Shinyanga ambapo taarifa za awali zinasema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo alikuwa akijaribu kumkwepa dereva boda boda ambaye aligongwa na kukandamizwa na basi hilo

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa baada ya kumgonga mwendesha pikipiki huyo basi hilo pia liligonga gari dogo lingine aina ya Corolla Wagon yenye namba za usajili T 173 ANW.

Endelea kutembelea Mpekuzi Blog taarifa kwa kina itakujia hivi karibuni




Share:

Relationship Manager (Commercial Banking) Job

Relationship Manager – Commercial Banking – (1900031924) Job: Commercial Banking Primary Location: Dar es Salaam Schedule: Full-time Employee Status: Permanent Posting Date: 07/Jan/2020 Unposting Date: 22/Jan/2020 About Standard Chartered We are a leading international bank focused on helping people and companies prosper across Asia, Africa and the Middle East. To us, good performance is about much more than… Read More »

The post Relationship Manager (Commercial Banking) Job appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger